Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

Shilole na wadau kutoka Golden State California

$
0
0
Shilole katika picha ya pamoja na wadau kutoka Golden State California alipokutana nao hivi karibuni mjini Washington DC. Kutoka kushoto ni Prof Mrisho, Yassin Kapuya , Shilole na Walter Minja.

MIAKA 10 YA MAFANIKIO YA MFUKO WA UWEKEZAJI TANZANIA UTT

$
0
0
Dhamana ya Uwekezaji Tanzania ilianzishwa tarehe 19 juni, 2003. Tangu kuanzishwa kwake, Dhamana ya Uwekezaji Tanzania imeendelea kutekeleza madhumuni yake. Mojwapo ya madhumuni ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania ni kuanzisha na kuendesha mifuko ya uwekezaji wa pamoja hapa nchini. Katika kufanikisha madhumuni yake, Dhamana ya Uwekezaji Tanzania imeweza kupata mafanikio ya kuanzisha mifuko mitano ya uwekezaji wa pamoja, ambayo hadi kufikia tarehe 08/07/2013 imekuwa na jumla ya wawekezaji hai wapatao 91,516.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), Hamis Kibola akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu shughuli za mfuko huo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2003 ambapo unatimiza miaka 10. Kushoto ni Kaimu Ofisa Uendeshaji Mkuu Uwekezaji, Rashid Mchatta. 
 CEO, Hamis Kibola akifafanua jambo.
 Ofisa Uendeshaji Mkuu, Asset Management & Investor Services akifafanua jambo.
 Dk. Gration Kamugisha Acting CEO, Project
 James Washima akifafanua jambo.


Article 0

$
0
0
ANKAL PAMOJA NA TIMU NZIMA YA GLOBU YA JAMII INAKUTAKIA MFUNGO MWEMA WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI UNAOANZA RASMI LEO BAADA YA KUANDAMA KWA MWEZI. INSHAALLAH TUNATARAJIA KILA MUUMINI WA KIISLAMU ATAHITIMISHA NGUZO HII MUHIMU KWA SWALA NA MAAMRISHO YAKE.

VIKUNDI VYA POLISI JAMII HANDENI VYAPATIWA MISAADA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu akishiriki kufyatua matofali katika kijiji cha Kwedikabu kata ya Kwamsisi wilayani humo. Tofali hizo zitatumika katika ujenzi wa ofisi za Serikali za Vijiji na Shule za Sekondari wilayani Handeni.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu, akipata maelezo ya mbuzi wa kienyeji anayezaa mapacha kila mwaka kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Mazingara Wilayani humo Mwl. Matei wakati wa ziara zake za kukagua shule za sekondari wilayani humo.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga SP. Zuberi Chembera, akikabidhi tochi, betri na filimbi kwa vikundi vya Polisi Jamii na Uluinzi Shirikishi wilayani Handeni ili ziwasaidie katika shughuli za ulinzi.Tochi hizo ni msaada kutoka kwa wafanyabiasha mbalimbali wilayani humo.

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi-Handeni

Juhudi zinazochukuliwa na mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, za kutoa elimu juu ya Sera ya Polisi Jamii na Ulinzi Shikishi nchini kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali zinazaa matunda karibu kila pembe ya nchi yetu.

Hayo yamedhihirika baada ya Wafanyabiashara wilayani Handeni katika mkoa wa Tanga, kuamua kwa hiari yao kuwachangia Polisi kwa vifaa ambavyo navyo vinatolewa kwa vikundi vya Polisi Jamii wilayani humo.

Wafanyabiashara hao wametoa vitendea kazi kama vile, tochi na betrii ili ziwasaidie Polisi lakini pia Mkuu wa polisi wilayani Handeni SP Zuberi Chembera, kwa kujua umuhimu wa Polisi Jamii naye ameamua kutoa msaada huo kwa vikundi mbalimbali vinavyojishughulisha na ulinzi mitaani.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo, Mkuu huyo wa Polisi wilayani handeni amesema kuwa ameamua kukabidhi sehemu ya misaada hiyo kwa kutambua kuwa Vikundi vya Ulinzi ni msaada mkubwa kwa Jeshi la Polisi katika kukomesha uhalifu nchini.

Amesema ofisi yake itajitahidi kutoa kila aina ya msaada kwa vikundi hivyo vya Polisi Jamii ili navyo viweze kuimarisha na kudumisha usalama katika maeneo yao.

Aidha SP Chembera ametoa wito kwa wananchi mbalimbali wilayani humo pia kuwaunga mkono katika kuvisaidia vikundi hivyo ambavyo amesema ni muhimu kuwepo ndani ya Jamii zetu katika kulinda usalama wa watu na mali zao kama ilivyo kwa jeshi la Polisi.

ZIARA YA WAZIRI WA UJENZI DKT, JOHN MAGUFULI KUKAGUA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA JIJINI DAR

$
0
0
Muoenekano wa ujenzi wa mradi wa daraja la Kigamboni katika awamu ya kwanza ambalo umekamilika kwa asilimia 47, katika mradi huo ujenzi huo utagharimu sh.Bilioni 214,kati ya fedha hizo asilimia 60 zimetolewa na Shirika la Hifadhi ya Mfuko wa Jamii (NSSF). Picha hii imepigwa jana wakati Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli hayupo pichani wakati alipofanya ziara ya siku moja ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya Dar es Salaam ikiwemo ya ujenzi wa daraji hili.
Waziri wa Ujenzi Dkt, John Magufuli, (mwenye kofia ya pama) akiongea na Diwani wa kata ya Mwenge Dkt. Julian Bujugo(aliemshika begani) wakati ya ziara yake .
Picha ya Pamoja kati ya Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na viongozi waliokuwa katika ziara yake.
Muonekano wa ujenzi unaoendelea wa ujenzi wa barabara ya Davis Corner- Vituka - Jet Corner.
Baadhi ya ujenzi wa vituo vya mradi wa Mabasi ya mwendo kasi (DART) barabara ya eneo la Ubungo,Mwembechai , Jangwani na Kivukoni vikiendelea.
Sehemu ya muonekano wa kituo cha mabasi ya mwendo kasi eneo la Kigamboni.
Ujenzi wa Daraja katika maeneo ya Tegeta wilaya ya Kinondoni ukiendelea. Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.

mbunge viti maalum ccm,Mh.Ritta Kabati apongezwa mkoani iringa kwa kuisaidia jamii.

$
0
0
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mh.Ritta Kabati akizungumza jambo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa,Bwa. Athumani Mungi,mara Mbunge huyo alipokwenda kutazama maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha polisi kinachojengwa na Mbunge huyo,kilichopo maeneo ya Tumaini.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa,Bwa. Athumani Mungi akipata maalezo mafupi kuhusiana na ujenzi wa kituo hicho kidogo cha polisi,pichani kati anaeshuhudia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mh.Ritta Kabati. 
 Baadhi ya Mafundi wakiendelaea na ujenzi wa kituo hicho kidogo cha polisi
Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa,Bwa. Athumani Mungi akimuelekeza jambo Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mh.Ritta Kabati. 
======  =======  =======

Viongozi mbalimbali mkoani Iringa wamekutana kujadili suala la uboreshaji wa miundombinu (barabara) katika kikao cha bodi ya barabara kwa kushirikiana na mamlaka ya barabara TANROADS mkoa wa Iringa akiwemo mkuu wa mkoa Dr.Christine Ishengoma ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao hicho.

Viongozi hao wamefikia maadhimio kadhaa ili kuongeza ufanisi na ukarabati wa barabara katika mkoa wa iringa ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira na usafi,ikiwemo na kupitisha sheria ya kukaguliwa kwa magari yasiyokuwa na vyombo maalum kwa ajili ya utupaji taka na gari yoyote itakayokamatwa ikiwa haina kifaa hicho itachukuliwa hatua ili kuwa fundisho kwa wengine,.

Sambamba na hilo vingozi hao wamempongeza Mh.Ritta Kabati kwa kuwawakilisha vyema wanawake na wananchi wa mkoa wa Iringa hasa katika kupigania maendeleo ya mkoa,miongoni mwa mambo ambayo amekuwa akiyapigania ni pamoja na Ukarabati wa miundombinu,elimu pamoja na Benki ya akina mama iliyoko Dar es Salam pekee ikiwa ni benki ya akina mama wote nchini, hivyo amewataka viongozi wanaohusika na benki hiyo kuifikisha katika mkoa wa Iringa ili hata akina mama wa mkoa huo waweze kunufaika,



 kutokana na kilio cha wanachi wa maeneo ya Tumaini,Semtema na maeneo jirani kudai kituo kidogo cha Polisi ,Mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Iringa Mh.Ritta Kabati amejitolea kujenga kituo cha Polisi katika maeneo hayo ili kuwasaidia wananchi wa maeneo hayo waliokuwa wakionelewa na watu wasio wema, hivyo amesema kituo hicho kitaweza kusaidia kupunguza idadi ya uharifu katika maeneo hayo kwani kituo hicho ni moja kati ya vituo vingi vinavyohitajika mkoani ha Iringa.



Akimuonesha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Bw.Athumani Mungi Mh.Kabati amemhakikishia kamanda kuwa ujenzi huo utakamilika mapema iwezekanavyo ili kuepusha adha kwa wananchi wa maeneo hayo.
Kwa upande wake kamanda wa Polisi mkoani Iringa,amempongeza Mbunge huyo kwa moyo wake wa kujitolea katika mambo ya jamii ambapo amesema Jeshi la Polisi linapenda kushirikiana na wadau wanaounga mikono jitihada za jeshi hilo katika kuboresha amani nchini huku akitoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo kwa umoja ni nguvu utengano ni Udhaifi.

CHAMA CHA WAFANYAKAZI WILAYA YA KILOLO KUFANYA MAANDAMANO YA KUMUONDOA MKUU WA WILAYA HIYO.!

$
0
0
Mwenyekiti wa TALGWU,Bwa, Andrea Mwandimbile pichani akifafanua jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani} zaidi kuhusiana na maandamano hayo kumuondoa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo.

Chama cha wafanyakazi wilaya ya kilolo wamepanga kufanya mandamano ya kumuondoa mkuu wa wilaya ya kilolo,Mh. Gerald Guninita kwa madai kuwa anawanyanyasa na kuwadhalilisha watumishi wa umma.


Wakizungumza na wandishi wa habari mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wilaya ya kilolo TALGWU,Bwa, Andrea Mwandimbile, wamesema kuwa hawamwitaji mkuu huyo wa wilaya kutokana na utendaji wake wa kazi kwa wafanyakazi wa umma, kuwa wa vitisho.


Wamesema kuwa kutokana na kutoa kauli za vitisho kwa watumishi hao wa umma, zimekuwa zikiathiri utendaji na uhusiano makazini kutokana na wengi wao kufanya kazi kwa hofu.


Kwa upande wake katibu wa chama cha wafanyakazi wilaya ya kilolo TALGWU ,John Mbingi ,wamewataja watu ambao tayari wamefanyiwa udhalilishaji na mkuu huyo kuwa ni Thomas Nyambage, ambaye ni afisa mifugo na kaimu wao kata ya Mlafu pamoja na Beatus Nyato,Afisa usafirishaji kilolo ambao walipigwa pingu hadharani na kuwekwa ndani na kisha kuachiwa huru bila kufunguliwa mashitaka.


Aidha amesema tayari uongozi umeshafanya taratibu za kutoa taarifa kwa viongozi wa ngazi za juu akiwemo mkuu wa mkoa.kutokana na malalamiko hayo mkuu wa wilaya hiyo GERARD GUNINITA ambaye ndiye mlalamikiwa amekanusha mashitaka hayo na kusema kuwa hajapata malalamiko hayo. 

KIA, JNIA win Africa Airport Marketing Awards 2013

$
0
0
The Kilimanjaro Airport Development Company (KADCO) Business  
Development Manager Christine Mwakatobe (third left) poses for a group photo with other Tanzanian delegates during the 8  in Kampala this week. Looking on at the left is Mkunde Senyagwa from the Arusha International Conference Centre (AICC) and right is John Weatherill from  intervistas. 
========  ======  ========
KIA, JNIA win Africa Airport Marketing Awards 2013

By Correspondent, Kampala
TANZANIA’S two international airports, Kilimanjaro International Airport (KIA) and Julius Nyerere International Airports (JNIA) have scooped the top awards during the 8th Routes Africa event held in Kampala between 7th to 8th of July, 2013.

The event hosted by Civil Aviation Authority of Uganda and Entebbe International Airport brought together Over 300 aviation professionals from across the world.
During the event, KIA emerged winner for the under 4 million passengers per annum category while JNIA was highly recommended in under 4 million passengers per annum category.

Speaking shortly after award ceremony, the Tanzanian delegation head Bakari Murusuri from Kilimanjaro Airport Development Company (KADCO) said the awards won is a land mark to in the country’s aviation sector.
 “The awards are not only an inspiration to the two airports but Tanzania’s aviation sector as a whole. Our focus should now ensure that the two airports meet international standards,”.

He added that as the overall winner of the Africa Heat, KIA will automatically be shortlisted for world routes marketing awards taking place in Las Vegas, Nevada, USA in October, 2013. The KADCO Business Development Manager Christine Mwakatobe said “This has been one of the most amazing evenings for us at Kilimanjaro International Airport to win this award. 

“We would like to thank all of the airlines that serve the airport for voting for us in this process and we are pledging our commitment that we will keep working hand-in-hand with all of our partners,” she added.

Other Tanzanian delegates present at the occasion included Scholastica Mukajanga from TAA, Efatha Lyimo from JNIA and Elisilia Kaaya from AICC, Mkunde Senyagwa from AICC and John Weatherill from  intervistas. Meanwhile, Zimbabwe is set to host next year’s 2014 Routes Africa event betweenand will be hosted by the Civil Aviation Authority of Zimbabwe.

Nigel Mayes, VP Commercial – Routes, UBM Live said of the announcement:  “We are thrilled at the decision to take Routes Africa to the stunning destination of Victoria Falls which is a World Heritage Site.  Hosting Routes Africa will deliver the route development community to Victoria Falls providing the opportunity to market this destination extensively whilst also showcasing the potential of the airport once it has undergone the major infrastructure changes which began earlier this year.”

American People sponsor Agricultural and Nutritional Studies for 29 Tanzanians

$
0
0
A group photo of representatives from the United States Agency for International Development (USAID) Feed the Future Initiative; Ministry of Agriculture and students, when the USAID hosted a farewell program for 29 Tanzanian students receiving grants to study agriculture and nutrition at universities in Tanzania and abroad. The scholarships are sponsored by the American People through USAID under the Feed the Future Initiative. Over a five-year period, Feed the Future is sponsoring 95 Tanzanians for postgraduate studies in agricultural and nutrition sciences. The first cohorts of six Tanzanian students pursuing Master’s degrees are scheduled to complete their studies by September 2013. A second cohort of 58 trainees began Master’s degree and PhD studies in 2012, and they are now in mid-course at universities in the United States and throughout Africa. The third cohort of 29 trainees, who were commissioned on July 10, will pursue Master’s degrees: 13 in the United States, four in Tanzania, ten in other African countries, and two in India. The farewell program held at the United States Embassy Dar es Salaam yesterday. (Photo United States Embassy Courtesy).

RC ISHENGOMA AAGIZA HALMASHAURI KUSIMAMIA FEDHA ZA MIRADI

$
0
0
 Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma  akifungua  kikao cha RCC mkoa wa Iringa kulia ni mstahiki meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi na kushoto ni katibu  tawala  mkoa wa Iringa Wamoja  Ayub.
 Wajumbe wa  kikao cha kamati  ya ushauri mkoa (RCC)  wakiwa wamesimama kwa kumkumbuka aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya  Kilolo marehemu Mohamed Gwalima aliyefariki ghafla  hivi karibuni ,kutoka  kushoto ni mkuu wa wilaya ya  Kilolo Gerald Guninita, mbunge  wa jimbo la Kilolo Prof Peter Msolla,mwenyekiti  wa Halmashauri ya  wilaya ya  Kilolo Joseph Muhumba na kaimu mkurugenzi wa wilaya ya Kilolo.
 Wajumbe wa kikao cha RCC Iringa  wakimkumbuka aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo Mohamed Gwalima aliyefariki dunia hivi karibuni ,kutoka kulia ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati, mbunge wa viti maalum mkoa  wa Iringa Lediana Mafulu Mng'ong'o ,mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini Mendlad Kigolla ,mku wa wilaya ya Mufindi, Evarita kalalu na mwenyekiti wa Halmashauri ya  Mufindi Peter Tweve .

Na FrancisGodwin blog -mzee wa matukiodaima

Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma ameziagiza Halmashauri mkoa wa Iringa kuhakikisha wanasimamia vema fedha za miradi zinazotolewa na serikali katika maeneo yao.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa agizo hilo leo katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo wakati akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC).

Amesema kuwa lengo la serikali kutuma fedha za miradi katika Halmashauri husika ni kuwezesha kusukuma mbele kasi ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri.

Hivyo alisema haitapendeza kuona fedha za miradi katika Halmashauri zinakosa usimamizi mzuri na kupelekea miradi kukwama kumalizika kwa wakati.

Aidha alitaka viongozi wa Halmashauri kubuni miradi ya kuziwezesha Halmashauri zao kuongeza mapato zaidi. Kwani alisema bila ya Halmashauri kubuni miradi ya kiuchumi uwezekano wa Halmashauri kujiendesha utakuwa mdogo zaidi. Kuhusu watumishi wasiojituma katika kazi mkuu wa mkoa ametoa onyo kwa watumishi hao na kuwa kamwe hata wavumilia.

Katika hatua nyingine mkuu huyu wa mkoa ametoa agizo kwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa kupitia askari wake wa usalama barabarani kuwakamata na kuyakamata na kuyatoza fani magari yote ya abiria ambayo yatapita katika mkoa wa Iringa bila kuwa na vifaa vya kuhifadhia taka na yale yatakayobainika yakichafua mazingira ovyo.

Tahadhari ya taarifa kwa umma kuhusu mafuta ya ubuyu.

Mteja wa Airtel tumia AIRTEL YATOSHA kushinda Jumba Hilooo

$
0
0
Huu ndo mjumba wa kifahari utakaoshinda kupitia droo ya mwisho wa mwezi Hii ni sehemu ya mbele ya Nyumba mojawapo ya AIRTEL YATOSHA Nyumba hizi zimejengwa kwa mpangilio maalum na wataalam kutoka shirika makini la nyumba Tanzania (National Housing Corporation) Mahali iliko ni Kigamboni Kibada wilaya ya Temeke General View ukiwa maeneo ya nyumba iliko Vitu vizuri unavyoweza kuviona ukiwa nyumbani kwako endapo utaibuka mshindi ni pamoja na Uwanja wa Taifa, uwanja wa ndege na utaweza kujione vizuri vikwangua anga vya jijini dar es salaam kama vile PPF Tower, Uhuru height, Jubilee Tower, Serena Hotel n.k Jiunge na kifurishi cha Airtel Yatosha SIKU, WIKI au MWEZI kwa kupiga *149*99# na chagua kifurushi kitakachokufaa ili uwe mmoja wa washindi watakaofaidika na nyumba hizi.
Nyumba zote Tatu zinavyumba vitatu vyakulala, Sebule, Jiko na Public toilet na Garden nzuriiiii/ kaliiiiii...... Mwishoni mwa waki wadau wa vyombo vya habari na baadhi ya Blog watatemebelea eneo hili kukujulisaha mambo mazuri zaidi

MIMI NA TANZANIA- NINI KIFANYIKE ILI KUTOKOMEZA USHOGA?? - Patr 2

kumbumbuku

$
0
0
Sekoutoure Khalifa Mndeme (24 Julai 1965 – 10 Julai, 2011)

Tarehe 10 Julai, 2011 Sekoutoure ‘Toure’ Khalifa mzawa wa Usangi, Wilaya ya Mwanga, mkazi wa Kunduchi-Mtongani, Dar es Salaam, aliaga dunia katika Hospitali ya Apollo, nchini India.

Jamii ilitoa msaada mkubwa tangu pale Toure alipolazwa Hospitali ya Aga Khan mwishoni mwa Juni, baadaye akahamishiwa Taasisi ya MOI (Muhimbili) na kisha kupelekwa India kwa uchunguzi zaidi na matibabu, hadi alipofariki. Tuliendelea kupata ushirikiano wenu hadi mwili wa Toure ukarejeshwa Dar toka India tarehe 13 Julai na hatimaye kusafirishwa kwenda Usangi–Ngujini kwa mazishi, Ijumaa, trh 15 Julai, 2011.


Familia ya Sultani na Omari Muyanza ya Usangi Mwanga, ya Hemedi Mwamtemi ya Lushoto na ile ya Toure (mjane Halima H. Mwamtemi, wanawe Khalifa (18), Hemedi (15) na Bi Hafsa “Doctor” (8) walifarijika mno kwa upendo na ushirikiano wa ninyi ndugu, jamaa, majirani na marafiki.


Leo tarehe 10.07.2013, Bw. Sekoutoure ‘Toure’ Khalifa ametimiza miaka miwili (2) tangu alipofariki.


Familia inafarijika sana kwa upendo na ushirikiano unaoonyeshwa na ndugu, jamaa na marafiki tangu mpendwa wetu alipotutoka hadi leo. Tunawashukuru sana na tunawaomba muendelee na upendo mlionao kwetu. Pia, tunawaomba muendelee kumuombea ndugu yetu kwa Allah.


Toure; ni kweli kwamba umetutoka kimwili, lakini utabaki ndani ya mioyo yetu daima. Upendo, ucheshi, hekima na busara zako zitabaki kama dira na changamoto ya kuwania ubora kwa sote ulotuacha nyuma.

“INNA LILLAH wa Ina ILLAYH RAJ’UNN – Kwa Mola tumetoka na Kwake tutarejea.” - Al Quran, Sura 6:128


MOLA AILAZE ROHO YA SEKOUTOURE MAHALI PEMA PEPONI - AMINA.




Shukran

KAULI YA POLISI KUHUSU CHADEMA KUANZISHA KIKUNDI CHA KUJIHAMI

$
0
0

Mnamo tarehe 09/07/2013, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Freeman Mbowe alitoa kauli kwamba wanaunda kikundi chao cha kuwalinda ambacho watakipatia mafunzo ya ukakamavu.

Kitendo cha chama chochote cha siasa ikiwemo CHADEMA kuanzisha kikundi cha kujihami ni kinyume cha sheria za nchi na endapo watafanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Kufuatia kauli hiyo, Jeshi la Polisi nchini limeanza uchunguzi na litachukua hatua kulingana na ushahidi utakaopatikana. Aidha, Jeshi la Polisi litamshughulikia mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha sheria bila kujali wadhifa wake.



Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Rais Kikwete afunga Kongamano la Kujadili Amani ya Taifa leo

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya kufunga Kongamano la Kitaifa Kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salam leo jioni.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Centre for Democracy(TCD) ambaye pia ni kiongozi wa chama cha NCCR Mageuzi Mhe. James Mbatia akimkabidhi Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete maazimio ya Kongamano la Kitaifa kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam na kufungwa leo jioni.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wa vyama vya siasa vilivyoshiriki katika Kongamano  la kitaifa Kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.Kushoto ni kiongozi wa Chama cha NCCR Mageuzi Mhe.James Mbatia (MB), Mwenyekiti wa TLP Mhe.Augustine Lyatonga Mrema(watatu kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mhe.John Momose Cheyo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(aliyekaa katikati) Akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na washiriki wa Kongamano la Kitaifa Kujadili Amani ya Taifa lililofanyika katika Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Taswira katika msiba wa mke wa katibu Mkuu wa Temeke Jogging club

$
0
0
Juma lililopita limekuwa ni la huzuni kwa wanabiafra na tasnia ya mchezo wa mbio za pole pole (jogging) mkoa wa Dar es Salaam kwa ujumla. mwanzo mwa juma tulipokea taarifa ya msiba wa mke wa katibu Mkuu wa Temeke Jogging (Rasmi) ndugu Togocho ambapo mazishi yalifanyika maeneo ya kurasini Mivinjeni. Vilabu kadhaa vya jogging viliendelea kuonesha umoja kwa kushiriki kwenye msiba huo na mingine.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Biafra Henry Maseko (mwenye shati jeupe) akitoa nasaha kwenye msiba wa mke wa ndugu Togocho

Siku ya Jumatano wanachama wa Biafra kundi la watoto Mtoro Elvis na kaka yake Jimmy Elvis (pichani chini)  nao walifiwa ni bibi yao mlezi ambapo mazishi yalifanyika huko Mlandizi mkoa wa Pwani. 

masanja mkandamizaji na shilole katika vekesheni jijini New york

$
0
0
Msanii Shilole akipata kitu inaitwa Mbwa wa moto "Hot Dog" wakati alipokua New York City akisubili boti kuelekea kuliko statue of Liberty akiwa ameambatana na msanii mwenzake Masanja (hayupo pichani) Jumanne July 9, 2013,
Kutoka kushoto ni Ebra NY, Libe, Masanja na Shilole wakiangalia Statue of Liberty kwenye mto wa Hudson unaotenganisha New Jersey na New York.
Libe, Masanja na Shilole wakinyanyua mikono yao juu kwa mfano wa Statue of Liberty.
Ebra Vijimambo vya NY (kushoto) akiwa na wageni wake Libe, Shilole na Masanja wakati alipokua akiwadhurulisha New York City Jumanne July 9, 2013.
Masanja akipata picha nje ya mahali panapoumiwa kupandia boti kwa wasafili wanaoelekea kwenye astatue of Liberty.
Masanja akipata picha kwenye gari la Polisi wa New York.
Juu na chini ni Shilole na Masanja wakipiga picha na Polisi kikosi cha farasi Manhattan New York.
Shilole akipata picha na jamaa aliyejichora na baada ya picha hua analipwa $1.00.
Masanja, Shilole na Libe wakiwa na mwenyeji wao Ebra wakipata chakula kwenye mgahawa mmoja wapo Manhattan, New York.
Shilole akiongea na mtayarishaji wa Video ili amshutie Video ya wimbo wake mpya ambayo anatarajiwa kuifanyia New York City.
kutoka kushoto ni Ankal Miraji, Ebra, Shilole na Bagdela wakitafakali jambo maeneo ya Times Square.

JK katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya JKT leo

$
0
0
 Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea saluti mara baada ya kuwasili Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo tayari kuongoza kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
 Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride katika  Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)

  Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa meza kuu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamsi Vuai Nahoda (kulia) na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Samweli Albert Ndomba (kulia kwake)  katika  Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Baadhi ya askari wa JKT na JWTZ katika sherehe hizo
 Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea saluti akiwa  na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamsi Vuai Nahoda, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Luteni Jenerali Samweli Albert Ndomba  (kulia) na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhuga (kulia kwa Rais )  katika  Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
 Gwaride likipita mbele ya  Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete
 Ukakamavu
 Nidhamu
Utii

MALIASILI: ASANTENI KWA KUTUFANYA KUWA NAMBA MOJA

$
0
0
WIZARA ya Maliasili na Utalii inawashukuru watu wote waliotembelea Banda la Maliasili na Utalii katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salam na kutuwezesha kuibuka mshindi wa Kwanza wa Banda Bora katika kundi la Taasisi za Serikali zilizoshiriki katika maonyesho ya Kimataifa ya 37 ya Saba Saba 2013. 
Ushindi huu unaama kubwa sana kwetu kwani haikuwa rahisi kuhakikisha wananchi waliokuwa wakiingia kwa wengi bandani kwetu wanapata elimu yakutosha kutoka kwa wataalamu na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii, wanyamapori na mambo ya kale waliokuwa wakitoa elimu mbalimbali zikiwemo za uhifadhi endelevu wa wanyamapori, ufugaji nyuki na utalii. 
Aidha wale ambao hawakujaaliwa kwa sababu moja ama nyingine kufika kwenye banda letu wasiwe na wasiwasi wanaweza kuungana nasi kwenye Maonyesho ya Nanenane Dodoma ambapo tutahakikisha tunafanya vema zaidi. 
 Sambamba na hilo Wizara inachukua fursa hii kuomba radhi kwa wale wote wailiokwazika kwa namna yoyote ile katika kipindi chote cha Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara 37 kwani tunatambua wananchi wengi mlikuwa na kiu ya kutembelea banda la wanyama hai hata muda ambao tulilazimika kulifunga (saa kumi na mbili jioni) kutoa fursa kwa wanyama kupumzika na kupata mlo wao wa usiku. Mwisho kabisa Wizara inawatakia Ramadhani Kareeem wale wote waliofunga na Mwenyezi Mungu awajaalie kila la heri katika mwezi huu mtukufu Amin.
 BAADHI YA WATENDAJI WAKUU NA MAAFISA WAANDAMIZI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAKIWASHUKURU WANANCHI MBALIMBALI WALIOKUWA WANAPITA NJE YA BANDA LA MALIASILI NA UTALII KWENYE MAONYESHO YA 37 YA KIMATAIFA YA BIASHARA MWAKA HUU KWA KUWAPUNGIA MIKONO NA KUWAONYESHA MOJA KATI YA TUNZO WALIZOZIPATA.

Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images