Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

UBALOZI WASHINGTON, DC WAMUAGA RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI

$
0
0
Juu na chini ni Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiongea machache katika chakula cha jioni alichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani katika kumuaga baada ya kumaliza ziara ya siku tano aliyofanya Washington, DC na kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa Kiswahili Marekani lililofanyika Jumamosi July 6, 2013 Capitol Heights, Maryland.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiingia Ubalozini kwenye chakula cha jioni alichoandaliwa na Ubalozi huo kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano.
Juu na chini ni Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Washington, DC wakiwemo wanakamati wa miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa Kiswahili Marekani.
Afisa Ubalozi Suleiman Saleh akitambulisha wakati mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa kwenye chakula hicho na kumtakia safari njema .

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Katiba: Ufafanuzi Kuhusu Toleo la Kiingereza la Rasimu ya Katiba

$
0
0
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetoa ufafanuzi kuhusu Rasimu ya Katiba iliyotolewa hivi karibuni katika lugha Kiingereza na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na kusema rasimu hiyo haitoi tafsiri sahihi ya maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal Juni 3 mwaka huu (2013).

Rasimu hiyo iliyotolewa na LHRC ambayo inasambazwa kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, pia inatumika katika mikutano na warsha mbalimbali zinazojadili kwa lengo la kutoa maoni kuhusu Rasimu iliyotolewa na Tume.

“Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine kuwa Rasimu hiyo ya Katiba katika lugha ya kiingereza iliyoandaliwa na LHRC haitoi tafsiri sahihi ya maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume katika lugha ya Kiswahili na hivyo kupotosha umma kuhusu maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa hivi karibuni,” amesema Katibu wa Tume hiyo, Bw. Assaa Rashid katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habari leo (Julai 9, 2013).

Bw. Asaa amewataka wananchi kuendelea kusoma na kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika lugha ya Kiswahili ambayo amesema imesambazwa kwa wananchi, taasisi, jumuiya na taasisi mbalimbali. Rasimu hiyo pia inapatikana katika tovuti ya Tume (www.katiba.go.tz) na kutolewa bure katika Ofisi za Tume zilizopo Dar es Salaam na Zanzibar.

Aidha, Tume hiyo imesema iliandaa Rasimu ya Katiba katika lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi ambao wengi wao wanajua kusoma na kuandika kwa lugha ya Kiswahili kuelewa maudhui ya Rasimu hiyo.

Katika taarifa yake, Tume imewataka wadau wote wanaotaka kutafsiri Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume kuwasiliana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ina Wataalamu wa Uandishi wa Sheria (Legislative Drafters).

SIMBA NA YANGA ZAKABIDHIWA VIFAA VIPYA KWA AJILI YA MSIMU WA 2013/14

$
0
0
Ikiwa ni sehemu ya udhamini wake, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi vifaa vya michezo kwa klabu maarufu za Simba SC na Young Africans SC kwa ajili ya msimu wa 2013/14 wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema “Tunawapatia vifaa mapema kabla ya ligi kuanza ili wapate muda wa kutosha kujiandaa kwa ajili ya msimu wa 2013/14 ambayo bila shaka itakuwa na changamoto kubwa kwa timu hizi mbili na pia tunaamini kuwa siri ya mafanikio katika michezo ni maandalizi mazuri. Ni matumaini yetu kuwa wachezaji wapya waliosajiliwa Simba na Yanga wataiwakilisha Kili vizuri na kufurahia kuzichezea klabu hizi kongwe.”



Kavishe aliongeza kuwa Vifaa ambavyo leo tunatoa ni pamoja na mipira, viatu, soksi, shin guards, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vitu vingine vingi ambavyo vitawezesha timu hizi za Simba na Yanga kucheza wakifurahia kuvaa vifaa vyenye ubora wa hali ya juu.

Kilimanjaro Premium Lager kama mdhamini mkuu wa Simba na Yanga, na kinywaji kinachoongoza katika udhamini wa soka hapa nchini tunadhani kwamba uhusiano wetu na klabu hizi ni kiungo muhimu sana katika kuendeleza mpira wa miguu hapa Tanzania. Tutaendelea kutimiza wajibu wetu kwa klabu hizi na kama ilvyo kawaida yetu, tutahakikisha tunalifikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.


Kavishe alisema kuwa udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Simba na Yanga umelenga kukuza soka la Tanzania, kuleta msisimko, na kuvutia mashabiki wengi wa mpira wakati na vilevile kuwaweka wachezaji wa Tanzania katika nafasi nzuri ya kimataifa.


Tunawashukuru viongozi wa Simba na Yanga, mashabiki wote, vyombo vya habari na wadau wote wa mpira kwa ushirikiano mzuri tunaoendelea kupata kwenye udhamini wetu na hiyo ndio siri ya mafanikio ya uhusiano wetu na klabu hizi mbili maarufu.

“Tunawaomba mashabiki wa Simba na Yanga waendelee kuiunga mkono bia yao ya Kilimanjaro Premium Lager kwani tunafanya kila jitihada kuwapa burudani na kufikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.”

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD WAZEE WA KAZI; GOOD NEWS TO ALL!

$
0
0
FROM NOW ALL OUR CARGO WILL GO  WITH KENYA AIRWAYS!
THIS MEANS A DIRECT FLIGHT TO NAIROBI/DAR EVERY WEEK 
THIS MEANS NO MORE DELAYS OR EXCUSES!
THIS MEANS BETTER SERVICE THAN BEFORE!
AIR CARGO TO DAR  
£3.50 per KILO! INCLUSIVE CLEARANCE
ONCE YOU PAY HERE IN UK YOU DONT PAY ANYTHING IN TANZANIA
UKIISHA LIPA UK UNAKWENDA KUCHUKUA
ILALA MTAA WA ARUSHA 
KAMA UKO DAR TUNAKUFIKISHIA MZIGO MLANGONI KWAKO
FLIGHTS EVERY WEEK
WE APOLOGISE FOR DELAYS CAUSED ON OUR FISRT AND SECOND CARGO, 
THOSE WHO HAVE SUFFERED DELAYS BEFORE WILL GET CREDIT OF £100 ON THEIR NEXT CARGO
NOW WE OUR CARGO GOES WITH KQ WCHICH MEANS THERE SHALL BE NO MORE DELAYS!
TO COLLECT CARGO FROM LONDON £25 
TO COLLECT CARGO FROM OUTSIDE LONDON £50
KWA WALE WANAOTAKA KUNUNUA VITU UK 
TUTUMIE EMAIL AU TUPIGIE TUTAKUFIKISHIA SEBULENI DAR
MINIMUM WEIGHT IS 40K
40' CONTAINER TO DAR/MOMBASA NOW £1,800
CHRIS LUKOSI +44 07903828119  & 07404279633 
SIMON LOUIS (MOHSIN) +44 07950689243

HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477

taswira za njiani Mkoani Tanga

$
0
0
 Kona ya Segera kuelekea Mkoani Tanga.
 Taswira za Kona ya Milima ya Korogwe Mkoani Tanga.

introducing jumbo sms services

NEWS ALERT: HATIMAYE MOTO WADHIBITIWA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
Moto mkubwa ulioanza katika Mlima Kilimanjaro tangu siku ya Jumapili tarehe 7.7.2013 umeendelea kudhibitiwa kwa kiwango kikubwa bila kuathiri shughuli za utalii katika Hifadhi ya Kilimanjaro.
Hadi kufikia leo tarehe 9.7.2013 moto umedhibitiwa kwa kiwango cha asilimia 75 na dalili zinaonyesha kuwa katika kipindi kifupi kijacho utaweza kudhibitiwa wote.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas Gama ametoa agizo kwa wilaya zote za Mkoa wa Kilimanjaro kushiriki operesheni maalum ya kuzima moto huo kwa kutoa askari mgambo watakaoshirikiana na TANAPA katika kuzima moto.
Hifadhi ya Kilimanjaro imeweka kambi mbili maalum kwa ajili ya kuhudumia wanaoshiriki zoezi la kuzima moto moja ikiwa katika eneo la Nanjara wilayani Rombo ambako ndipo ulipo sehemu kubwa ya moto na kambi ya pili ipo katika eneo la Marangu kwa ajili ya kuhudumia 
eneo la Kilema Juu.
Shughuli za Utalii katika Mlima Kilimanjaro zinaendelea kama kawaida na hakuna watalii wowote walioathirika na moto huu hasa kwa kuwa njia zote muhimu za Marangu, Mweka, Machame, Umbwe, Lemosho na Rongai zinazotumika kwa ajili ya kupandisha watalii mlimani na zile za kushukia hazijaathiriwa na moto. 
TANAPA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wanaendelea na juhudi za kutafuta waliohusika na uharibifu huu na mara zoezi la kuzima moto litakapokamilika taarifa ya tathmini ya madhara ya moto itaweza kufanywa.

Imetolewa na Idara ya Uhusiano
Hifadhi za Taifa Tanzania
09.07.2013

yale yale.....

$
0
0
  TUTAZZZ! Cheki alama ya tahadhari ili kupunguza mwendo kabla ya kukwea tutazzz barabara ya Korogwe, labda uwe na bodaboda utaiona!!  Maana haina kiakisi mwanga waka nini hivyo usiku kazi ipo. Ujenzi wa barabara maeneo ya Korogwe ukiendelea. Picha na mdau Florence Lawrence 


SERIKALI YAOMBWA KUWAWEZESHA VIJANA WANAOHITIMU VYUO VYA UFUNDI

$
0
0
Na Mohammed Mhina

Serikali imeombwa kuwasaidia wajasiriamali wadogowadogo kwa kuwapa vifaa na uwezo wa kujiendeleza ili waweze kudumisha ajira isiyo rasmi na kujikwamua kimaisha.

Ombi hilo limetolewa na wanafunzi wa chuo cha ufundi cha Saweruo kilichopo Handeni mkoani Tanga wakati wa mahafali yao chuoni hapo.

Wahitimu hao walisema kama Serikali itasaidia kutoa vifaa vya ufundi na ruzuku kwa vijana waliojiajiri katika sekta hiyo ni wazi kuwa wataweza kujikwamua katika dimbwi la umaskini na kuondokana na utegemezi wa ajira zinazotangazwa na serikali ambazo mara nyingi zinakuwa na ushindani mkubwa na hazitoshi kwa wote.

Wamesema vyuo vya ufundi vimekuwa vikiwasadia vijana kuelekea kujitegemea kimaisha lakini mara nyingi wahitimu wamekuwa wakikwamishwa na kutokuwa na mitaji ya ununuzi wa vifaa vinavyowazesha kujiajiiri wenyewe katika sekta ya ufundi mijini na vijijini na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Naye Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo Bi. Sharifa Abebe, ambae ni Diwani ya kata ya Kwamgwe wilayani Handeni, aliwaasa vijana kutochagua kazi na badala yake wajiunge katika vikundi na kubuni miradi itakayowakwamua kiuchumi kikiwemo kilimo na biashara mbalimbali.

Bi. Sharifa pia ametoa wito kwa walezi na wazazi wenye vijana waliomaliza vyuo vya ufundi kuwahimiza kutobweteka lakini pia kuwawezesha kwa vifaa vya kiufundi badala ya kuisubiri Serikali ambayo amesema ina mzigo mkubwa kitaifa.

"Niwaombe wazazi wenzangu, tuwashawishi vijana wetu wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari, kujiunga na vyuo vya ufundi ambavyo vipo katika maeneo mengi hapa nchini na wamalizapo wataweza kujiajiri wenyewe". Aalisema Bi Abebe.

Wahitimu hao wamejifunza ufundi mbalimbali ukiwemo wa utengenezaji wa samani za majumbani na maofisini, ushoni na shughuli za mapambo katika kumbi za mikutano ama sherehe mbalimbali.

Kamati ya Uongozi EALA yatembelea Ukumbi mpya wa Bunge

$
0
0
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Margareth Zziwa, akiwa na Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo, walipotembelea ukumbi mpya wa Bunge la EALA uliopo kwenye jengo la Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha Tanzania, tayari kwa kikao cha Bunge kinachotarajiwa kuanza tarehe 18/08/2013.
Spika ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi - EALA pamoja na Wabunge wanaounda Kamati ya Uongozi, wakionyesha nyuso za furaha walipokuwa katika ziara hiyo.
Sehemu ya ukumbi wa Bunge la EALA.

Waziri Fatma Abdull Habib Fereji apongeza ushirikiano kati ya Bodi ya madawa na vipodozi Zanzibar na Baraza la mazingira la Tanzania Bara

$
0
0
Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwaza wa Rais Fatma Abdull Habib Fereji amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Ofisi hiyo, Bodi ya madawa na vipodozi Zanzibar na Baraza la mazingira la Tanzania Bara kwa mashirikiano ya kufanikisha zoezi la kuangamiza unga mbovu uliokuwepo bandarini Zanzibar kuazia mwezi wa April mwaka uliopita hadi Julai mosi mwaka huu.

Pongezi hizo alizitoa leo huko Baraza la wakilishi wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya hali halisi ya unga huo ambao haufai kwa matumizi ya binaadamu.

Amesema unga huo ulioharibika umeanza kuangamizwa kwa ushirikiano wa pande mbili za Muungano baaada ya Zanzibar kukosa eneo ambalo litaweza kuhifadhi afya za wananchi wakati wa kuuangamiza.

Amesema Serikali ya Muungano ilikubali ombi lao na kuanzia tarehe 14 Mei hadi tarehe 15 Juni kontena 15 za unga mbovu ulisafirishwa kupelekwa Tanzania Bara kwenda kuangamizwa.

“Tulizungumza na wezetu Tanzania Bara kutupatia eneo la kuteketeza unga huu tuna shukuru wezetu hawakutuvunja moyo walikubali na sasa umeshateketezwa chini ya usimamizi wa Baraza la Mazingiara ”, alisema Waziri huyo.

Aidha alifahamisha kuwa unga huo unateketezwa na kiwanda cha saruji cha Twiga simenti kilioko Tanga kwa makubaliano ya Wizara yake , Bodi ya madawa na vipodozi na msimamizi baraza la mazingira la Tanzania Bara.

Amesema kuanzia sasa hakutakuwa na muhali na vyakula vibovu vinavyo letwa na wafanya biashara na amewaomba wananchi washirikiane kufichua maovu hayo ili kulinda afya zao .

Unga huo unaofikia tani 780 uliingizwa nchini Aprili mwaka jana na Kampuni ya Bopary Inteprise kutoka nchini uturuki.

RAIS KIKWETE AAGANA NA MABALOZI WAPYA LEO IKULU, DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi saba walioteuliwa hivi karibuni na kuagana nao kabla hawajaripoti kwenye vituo vyao katika nchi mbali mbali leo Ikulu jijini Dar es salaam. Mabalozi hao toka kushoto ni Mhe Modest Melo anayekwenda Umoja wa Mataifa, Geneva, Uswisi, Mhe Mabrouk n. Mabrouk (Abu Dhabi – Umoja wa Falme za Kiarabu – UAE), Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (Beijing, China), Mhe Anthony Cheche (Kinshasa - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC), Mhe Chabaka Kilumanga (Visiwa vya Comoro), Mhe Wilson Masilingi (The Hague, Uholanzi) na Mhe Liberata Mulamula (Washington DC, Marekani). PICHA NA IKULU.

Article 10

AOTTL Buying Season Starts

$
0
0
AOTTL MD, Mark Mason taking the Hon. Christopher Chiza (MP) Minister for Agriculture, Food and Cooperatives around the AOTTL Unprocessed tobacco Storage. In between the Minister and Mason is Elizabeth Chuma - Receiving and Green Storage Manager.

Kali TV Online: This week's Around Town


WAZIRI WA UCHUKUZI AZINDUA MPANGO WA UFATILIAJI UFANISI WA UCHUKUZI KATIKA UKANDA WA KATI NA NCHI JIRANI ZA RWANDA, BURUNDI, UGANDA, TANZANIA NA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO

$
0
0
 Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe akihutubia katika uzinduzi wa mpango wa ufatiliaji ufanisi wa uchukuzikanda ya kati na nchi jirani za Burundi, Rwanda, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Uganda, leo katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam. Mpango huu utakuwa wa miaka minne na umefadhiliwa na Shirika la Trade Mark East Africa (TMEA).
 Wajumbe walioshiriki katika uzinduzi wa mpango wa ufatiliaji ufanisi wa uchukuzi ambao umejumuisha Mawaziri wanaoshughulika na Uchukuzi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Rwanda, Burundi na wenyeji Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania, Dkt . Harrison Mwakyembe (hayupo pichani). Uzinduzi huo umefanyika katika hotel ya Serena, jijini Dar es Salaam leo mchana.

 Waziri wa Uchukuzi Tanzania, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mpango wa ufatiliaji ufanisi wa uchukuzikatika kanda ya kati na nchi jirani za Burundi, Rwanda, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo , Uganda na wenyeji Tanzania. Uzinduzi huo umefanywa leo katika hotel ya Serena,jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Waziri wa wa Nchi Uchukuzi kutoka nchini Uganda,  Bw. Steven Chemoiko Chebroto, na wa pili  kutoka kulia ni Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mitambo wa Burundi, Mhandisi Deogratius Rurimunzu. Wa kwanza kushoto ni Bw. Scott Allen kutoka Trade Mark East Africa (TMEA)Nairobi.
 Waziri wa ya Uchukuzi wa Tanzania, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto), Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mitambo wa Burundi, Mhandisi Deogratius Rurimunzu (mwenye tai nyekundu) na Waziri wa Nchi Uchukuzi wa Uganda, Bw. Steven Chemoiko Chebroto, wakiweka sahihi kwenye vitabu kuashiria uzinduzi wa mpango  maalum ufatiliaji ufanisi wa uchukuzi katika ukanda wa kati na nchi jirani, uzinduzi huo umefanyika katika hotel ya Serena,jijini dare s
Salaam leo.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo, akiweka sahihi katika kitabu cha mpango muhimu wa ufatiliaji ufanisi wa uchukuzi katika kanda ya kati na nchi jirani za Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania, Uzinduzi wa Mpango huo  umefanywa leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo(kulia), akibadilishana mawazo na Muwakilishi Mkazi wa Benki ya Mendeleo ya Afrika (AfDB) , Bi Tonia Kandiero, wakati wa uzinduzi wa mpango ufatiliaji ufanisi wa uchukuzi katika kanda ya kati na nchi jirani za Rwanda, Burundi,Uganda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, uliozinduliwa leo katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam. Mwenye suti ya kaki ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. John Mngodo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi

Inflation drops to 7.6 per cent, on slow food prices

$
0
0
INFLATION continued to fall in the year to June due to slower rises in the prices of food and energy, the National Bureau of Statistics (NBS) said yesterday.
The year-on-year rate of inflation fell to 7.6 per cent from 8.3 per cent in May, the lowest level in two years.
20130709-195901.jpg
NBS report released yesterday says: “The decrease of inflation rate explains that, the speed of price increase for commodities in June has decreased compared to the speed recorded in May.”
The rate shows that the authorities in the country are ahead of International Monetary Fund (IMF) projection of lowering inflation to 7.0 per cent by the end of December 2013.
Given the speed of declining, the IMF projection goal may be reached before the third quarter (September) ends, even to reach the projected policy goal of 5.0 per cent before the year end.
Mzumbe University Dar es Salaam Business School Senior Lecturer (economics), Dr Honest Ngowi, said the decline was the continuation of the downward trend experienced for several months now.
“The rate and trend are good. And we may soon reach our policy goal of 5.0 per cent in the very near future,” Dr Ngowi said, adding “it reflects a good effort made by central bank for controlling money supply (in the economy).”
The senior economics lecturer said the worries are on taxes adopted for this fiscal year because some are inflationary in nature and might derail the achievements. “We cannot reach the 5.0 per cent goal unconditionally.
The way forward is to safeguard the achievements by addressing structural issues that erode the desires to achieve the policy rate,” Dr Ngowi said.
The initiatives, to address structural issues, like President Barack Obama’s Power Africa are commendable as would lower the cost of electricity and ultimately production

KIFO CHA MTANZANIA: MSAKO MKALI WAENDELEA, BABA WA MAREHEMU KUWASILI LEO MAREKANI

$
0
0
Omar Sykes enzi za Uhai wake.

Na Swahili TV
Familia ya  mwanafunzi mtanzania aliyeuwa mjini washington DC, marehemu Omary Sykes inatarajiwa kuingia nchini Marekani leo hii, swahili TV inaripoti. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu familia hiyo itaongozwa na baba wa marehemu bwana Adamu Sykes na baba mkubwa  wake bwana Ilyasa Sykes.

Marehemu ambaye alikuwa na  miaka 22,  ni mjukuu wa mpigania uhuru maarufu wa Tanzania mzee Kleist Abdulwakili sykes na  pia ni ndugu wa  msanii star wa bongo Flava Dully Sykes.

Omar  aliuawa kwa shambulio la risasi karibu na maeneo ya chuo anachosoma cha Howard University usiku wa alhamisi julai 4, 2013 akiwa na mwenziwe katika mtaa wa Fairmont North West, kwa mujibu wa Polisi Washington DC (MPDC)  na Polisi wa chuo hicho (HPD), watu wawili ndio wanaoshukiwa kuhusika na mauaji hayo.Wahusika bado hawajatiwa mbaroni.

Kwa mujibu wa habari za ndani za jeshi hilo la Polisi, kitengo maalum cha uchunguzi wa mauaji kilishaanza upelelezi mkali ukiongozwa na Bwana Gabriel Truby wa MPDC na wameieleza Swahili TV kuwa  licha ya upelelezi wanaoendelea nao wanaomba ushirikiano wa wananchi kwa ajili ya kufanikisha uchunguzi wao. Zawadi ya dola za Kimarekani 25,000 itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wauaji hao. 

Maripota wa Swahili TV wamefanikiwa kufanya mawasiliano na kitengo cha mauaji cha MPDC, Howard University Police  pamoja na familia ya marehemu Omar Sykes. Kwa mujibu wa maelezo yao  mwili wa marehemu bado upo hospitalini kwa ajili ya uchunguzi na swahili TV inaahidi kuwaletea habari zote zinazohusiana na upelelezi huu. 
Stay tuned kwa exclusive story.
Tembelea http://swahilitv.blogspot.com/

UKISHANGAA YA MUSA....

$
0
0
Baada ya safu za video zenye mafanikio makubwa za NGOMA AZIPENDAZO ANKAL, MIONDOKO YA KUMEREMETA KWENYE MNUSO na MKATAA KWAO MTUMWA, Globu ya Jamii inakuongezea safu ingine ya video ya UKISHANGAA YA MUSA...katika kunogesha Libeneke. Tunaanza na mdau anayecheza Salsa na mbwa huko Columbia. Shukran kwa Chef Issa aliyeleta video hii na wazo hilo la kuanzisha safu hii mpya. RAMADHAN KARIM Chef!

DAWASCO YAJA NA MFUMO WA KIELEKRONIKI WA MALIPO YA ANKARA ZA MAJI

$
0
0
Dawasco imezindua rasmi Mfumo wa Malipo ya ankara za Maji ulioanza rasmi kutumika Tarehe 01.07.2013 Katika vituo vyake vyote 13. Mabadiliko haya yanalenga kuboresha huduma kwa Mteja. 
Pia mfumo utasaidia kupunguza msongamano wa muda mrefu uliokuwepo wa kulipia Madirishani na utampa mteja njia mbalimbali za kulipia Bili yake na kwa wakati wowote. 
Mfumo huu pia utamsaidia Mteja kufanya malipo sehemu yoyote nje ya Jiji la Dar es salaam na hata nje ya Nchi Malipo kwa njia ya Benki yatafanyika kwenye tawi lolote katika Benki zifuatazo: CRDB – A/C No. 01J1021921900, BARCLAYS- A/C No. 0014003711, BANK OF ( BOA) –A/C No. 02022460009 na NMB No. 20103300047 
Mteja atakwenda Benki anayotaka kufanya Malipo na kujaza Fomu ya fedha (deposit Slip). Mteja ahakikishe ameandika namba ya account ya Dawasco kwa usahihi ikifuatiwa na kiasi cha fedha anacholipia, kisha kurudisha fomu kwa karani wa Benki kwa Malipo. 
Huduma za kibenki kwa kutumia simu za kiganjani ni kwa Wateja Wenye Akaunti Katika Benki za; CRDB, NMB, BENKI YA POSTA, AKIBA COMMERCIAL BANK (ACB) Na EXIM BANK. Malipo kwa kutumia Simu ya kiganjani yatafanyika Kupitia M-PESA, AIRTEL MONEY, TIGO PESA, Na ZANTEL EZY PESA. 
 Pia malipo kwa ankara za Maji zinafanyika kupitia ATM ZA UMOJA SWITCH, huduma ya SELCOM na MAXMALIPO inayopatikana kwa Mawakala waliopo kila kona ya Jiji La Dar Es Salaam. Aidha kuna matawi ya Benki yako karibu na vituo vya Dawasco hivyo wateja wa maeneo husika watapata urahisi wa kufanya Malipo yao ya kila mwezi na kuondoa usumbufu wa kwenda mbali zaidi. 
Matawi hayo ya Benki yaliyo karibu na Vituo vya Dawasco ni haya yafuatayo: Kituo cha Dawasco Temeke kilichopo Temeke Usalama kipo karibu na Matawi ya Benki ya NMB- Temeke Hospital, CRDB – Quality Centre Kituo cha Dawasco Kawe kilichopo njia panda ya Kawe kipo karibu na Matawi ya Benki ya CRDB yaliyopo Mbezi Beach, Kijitonyama, Mikocheni na Mlimani City na matawi ya NMB yaliyopo Mlimani City, Mbezi Beach na Mwenge na Tawi la BOA Bank iliyopo Sinza Kituo cha Dawasco Tabata kilichopo Dar West kipo karibu na Matawi ya Benki ya CRDB Tabata Magengeni. 
 Kituo cha Dawasco Kimara kilichopo kimara mwisho (Matankini) kipo karibu na Matawi ya Benki ya CRDB-Ubungo Mwisho, CRDB-Mbezi Stand Mpya, CRDB-Mlimani City, NMB, BANK OF AFRICA (BOA) zilizoko Ubungo Plaza, CRDB Ubungo Stand, ATM ZA UMOJA SWITCH-zilizopo Mbezi Suka Kituo cha Dawasco Kinondoni kilichopo nyuma ya jengo la Airtel kipo karibu na Matawi ya Benki ya NMB- Namanga/Msasani, ATM ZA UMOJA SWITCH- Mwanamboka, AKIBA COMMERCIAL na CRDB zilizopo Millenium Tower Makumbusho Kituo cha Dawasco Magomeni kilichopo Magomeni Mapipa kipo karibu na Matawi ya Benki ya BARCLAYS- Magomeni Mapipa na NMB-Magomeni Mikumi. 
 Kituo cha Dawasco City Centre kilichopo Kisutu kipo karibu na matawi ya Benki ya EXIM BANK-Morogoro Road eneo la Fire na CRDB-Lumumba. Kituo cha Dawasco Ilala kilichopo Boma jirani na Mwalimu House kipo karibu na Matawi ya Benki ya BOA-Amana, NMB-Boma, Barclays-Buguruni Malapa, AKIBA COMMERCIAL BANK-Mtaa wa Uhuru na Likoma, CRDB-Lumumba, Mnazi Mmoja na Mtaa wa Uhuru. 
 Kituo cha Dawasco Kibaha kilichopo karibu na Ofisi za TRA kipo karibu na Matawi ya Benki ya NMB-Kibaha na CRDB-Kibaha Kituo cha Dawasco Mlandizi kipo karibu na Matawi ya CRDB na NMB Kituo cha Dawasco Bagamoyo kilichopo karibu na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kipo karibu na Matawi ya Benki ya CRDB-Bagamoyo na NMB-Bagamoyo Kituo cha Dawasco Gerezani (Makao Makuu) kilichopo karibu na jengo la Water Front kipo karibu na Matawi ya Benki ya CRDB-Water Front, NMB-Samora. 
Kituo cha Dawasco Boko kipo karibu na Matawi ya Benki ya NMB na CRDB jengo la Kibo Complex, ATM ZA UMOJA SWITCH zilizoko eneo la Africana. 
 LIPA BILI YAKO YA MAJI UKIWA MAHALI POPOTE NA WAKATI WOWOTE IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO DAWASCO MAKAO MAKUU
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng. Jackson Midala (Kulia) na Meneja Uhusiano Bi. Irene Mkene akionyesha mita mpya ya malipo ya kabla katika uzinduzi wa Mfumo mpya wa ulipaji bill wa kieletroniki (e-Bill payment) makao makuu Dar es salaam
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng. Jackson Midala akionyesha mita mpya ya malipo ya kabla wakati wa uzinduzi wa Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji wa kieletroniki (e-Bill payment) makao makuu Dar es salaam
 Wawakilishi wa mabenki katika uzinduzi wa Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji kwa kieletroniki (e-Bill payment), DAWASCO makao makuu- Dar es salaam.
Wawakilishi wa mitandao ya mawasiliano katika uzinduzi wa Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji kwa kieletroniki (e-Bill payment), DAWASCO makao makuu- Dar es salaam
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images