Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 189 | 190 | (Page 191) | 192 | 193 | .... | 3278 | newer

  0 0
 • 07/08/13--03:46: Antony na Gema Wameremeta.
 •  Harusi:Ndugu Antony David Mtavangu na Gema Nicholaus Temba wakila kiapo cha kuishi pamoja katika kanisa la Mtakatifu Peter ,siku ya Jumamosi tarehe 6 Julai 2013.
   Antony na mkewe Gema wakiwa wamependeza sana katika siku yao ya harusi.
   Antony Mtavangu na Bi. harusi Gema wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasimamizi wao.
  Saleh Saphy akizungumza kwa niaba ya wanafunzi waliosoma na Antony, chuo kikuu cha Mysore India, pamoja na kumtaka Antony maarufu kama 'Tony Yayo' kumtunza mkewe , vijana hao walimtakia maisha mema na kamwe kutomlisha mkewe 'Egg Puf '.

  0 0

  Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva,Nassib Abdul a.k.a Diamond akiwapagawisha mashabiki wake wakati Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Moshi na mikoa ya Jirani waliokataa kupitwa na Onyesho hilo.
  Wanamuziki wakongwe katika medani ya muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydee na Joseph Haule au ukipenda waweza muita Profesa Jay wakiburudisha maelfu ya mashabiki wa muziki waliofurika katika Uiwanja wa Ushirika mjini Moshi mwishoni mwa wiki katika muendelezo wa Maonyesho ya Tamasha la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.
  Kundi bora la muziki wa Reggae Tanzania kwa mujibu wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013.  Warriors from the East, wakionesha uwezo wao katika kulimiliki jukwaa kwenye onyesho la tatu la Tamasha la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mwishoni mwa wiki.
  Kundi bora la muziki kwa mujibu wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013,Jambo Squard, wakionesha ubora wao katika jukwaa la tatu la ziara Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013 zinazoendelea nchi nzima.
  Mwamba wa Kaskazini, John Makini akifanya vitu yake jukwaani.
  Mwanamuziki bora wa Hip Hop 2013, Kala Jeremiah akiwarusha mashabiki wake juzi katika viwanja vya Ushirika jijini Moshi.
  nyomii la hatari

  kwa picha zaidi
  TEMBELEA WWW.OTHMANMICHUZI.BLOGSPOT.COM

  0 0

  Kaka Michuzi habari ya kazi,

  naomba nirushie hii kwa jamii.kundi la Bodaboda Kampen ambalo linajihusisha ya kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madeleva wa bodaboda wakishirikiana na jeshi la polisi ambapo mwaka huu wamejitolea kutoa mkono wa pole kwa wagonjwa waliopata ajali za pikipiki,ambapo tulianzia na hospitali ya Taifa Muhimbili na tunatarajia kufanya kila mkoa.

  kwa hiyo tunaomba wadau wajitokeze kutupa sapoti katika kutoa elimu kwa waendesha Boda Boda na kuwatembelea mahospitalini pindi wapatapo matatizo kwani mahospitalini wamesahaulika sana wengi wao ndugu zao wapo mbali,kwahiyo wanatakiwa kupata misaada midogomidogo kama nguo, sabuni, mafuta, maji, miswaki, juice, matunda, hiyo ndio misaada tuliotoa jana tarehe 07/07/2013 katika hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Mifupa (Moi).

  tunaomba wadau wajitokeze kutusapoti tuweze kutembelea katika hospitali za mkoa wa Dar es salaam baada ya hapo mikoani na vijijini.

  tunatumai ombi letu litakubaliwa kwa wadau mbalimbali.
   Msafara ukielekea Muhimbili.
   Tulipokelewa na Uongozi na kutoa tulichofika nacho.
   Mmoja wa wahanga wa Boda Boda akizungumza na wanahabari.

  0 0


  0 0

  By Correspondent, Dar es Salaam

  The African Union (AU) programme for governance assessment-the Peer Review Mechanism (APRM) Tanzania chapter has urged for views of the people to prevail on the final document of the Constitution.

  The APRM has also hinted that it is reviewing the just released document to see whether there are some issues that need to be enhanced so that the country finally get its final document that would lead Tanzania into a more prosperous and peaceful country in the future.

  That was said in Dar es Salaam yesterday at the Dar Salaam International Trade Fair by APRM Tanzania Head of Media and Communications, Mr. Hassan Abbas when he was responding to a query from a section of the press.

  “While our findings in the APRM report are clear that most Tanzanians wanted the new constitution process to start, now the wish has been granted. In my opinion I think it is the people who will have to dictate on crucial matters in each item that has been proposed in the released draft constitution,” he said.

  Asked on the controversial Union structure proposed by the Constitution Review Commission, Mr. Abbas who is also a trained lawyer said APRM as governance monitoring Mechanism is conducting its own review of the released draft to take stock of the main issues that were recommended in its report and what has been included in the Commission’s document.

  “The constitution review is a mandate of the Commission; APRM cannot interfere with any of the activities of the Commission. But as an advisory Mechanism on governance issues in the country, we always consult relevant institutions when there are APRM issues that need to be given attention.

  “Regarding the structure of the Union, the views of the people in the APRM report were also so diverse. On this basis APRM cannot have its own opinion or stance on the matter but when we met the Constitution Review Commission our submission was that people’s views should prevail. This remains our position even now that the first draft is out,” he said.

  He said that APRM Tanzania hopes the formed constitutional councils will help to refine the document including the issue of Union structure. He urged few Tanzanians appointed or elected to participate in the forums to do their job with a view of making a a better Tanzania.

  Tanzania joined the APRM since 2004 and is scheduled to present its final report in Addis Ababa, Ethiopia at the end of January, 2013 for consideration before an AU/APRM Forum of Heads of State and Government.

  33 out of 54 African countries have acceded to the Mechanism and are at different stages of implementation. The APRM review process is conducted every after four years.

  0 0

  Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akiongea wakati wa kufunga michuano ya Fainali ya mashindano ya Airtel Rising Stars katika viwanja vya karume jijini Dar es saalam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso akiongea wakati wa kufunga michuano ya Fainali ya mashindano ya Airtel Rising Stars katika viwanja vya karume jijini Dar es saalam.
  Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos akiongea na wachezaji kabla ya kuanza mechi za fainali.
  Mlinzi wa Mwanza Ally Mnasi (kushoto) akipambana na Evance Robert wa Morogoro wakati wa fainali kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar mwishoni mwa wiki. Mwanza walishinda 1-0.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika kuwataarifu wananchi na wakazi wa jiji kwa jumla kuwa huduma ya treni ya jiji haitokuwepo kwa muda wa siku 2 kuanzia leo Julai 8, 2013 kutokana na hitilafu kubwa katika  kichwa kimojawapo cha treni hiyo.

  Uamuzi huo unatokana na sababu za kiufundi unaosimamia uendeshaji wa huduma hiyo jijini.
  Kwa utaratibu huduma hii huendeshwa kwa kutumia vichwa vya treni vitatu ambapo viwili uhudumia moja kwa moja na cha tatu huwa cha akiba . Kuanzia siku ya Jumamosi ambapo huduma haikuwepo, kichwa cha tatu kiligundlika kuhitaji matengenezo makubwa na kupelekwa katika karakana yetu ya Morogoro.

  Kutokana na utaratibu tulioainisha hapo awali kukosekana kichwa cha dharura ’standby’ kunalazimisha tusitishe huduma kwa muda. Hata hivyo Wahandisi na Mafundi wa Karakana yetu Kuu Morogoro wanatarajia kukamilisha kazi hiyo kabla ya siku ya Jumatano na hivyo kutoa fursa huduma hiyo kuanza tena siku ya  Jumatano Julai 10, 2013.

  Uongozi wa TRL unawaomba radhi wakazi wa Jiji na kuwataka kuwa na uvumilivu wakati huu wa ukarabati  kichwa cha treni unaoendelea na kwamba muda sio mrefu Wanareli wa TRL  watafanya kila linalowezekana kuirejesha huduma hii walioizoeya.

  Tamati
  Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya
  Mkurugenzi Mtendaji ,
  Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
  Dar es Salaam,
  Julai 08, 2013.

  0 0

  Rais mpya wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es Salaam, Rotarian Ambrose Nshala, akihutubia katika hafla ya kumsimika rais mpya wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Rais huyo amechaguliwa kwa mwaka wa pili kushika uongozi huo. Wengine kutoka kushoto ni Gavana Mstaafu, Amu Shah, Theodosia Muhulo ambaye ni mke wa rais huo na Gavana Msaidizi wa Rotary, Irene Kamau.
  Rais wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam, Rotarian Ambrose Nshala(kulia), akimvisha pini rotarian mpya, Mhandisi Dennis katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Rais wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es Salaam, Rotarian Ambrose Nshala (kulia), akimpa nyaraka rotarian mpya wa klabu hiyo, Paul Mashauri katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Rotary klabu ya Mzizima, Rotarian Ambrose Nshala (kushoto) akiwaongoza wanachama wengine wa klabu hiyo kuselebuka katika hafla ya kmsimika rais na viongozi wengine wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  MKUU wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi amewasisitiza wadau mbali mbali kuwekeza katika mpira wa miguu kwani hutoa ajira nyingi kwa vijana na kuwafanya wajipatie kipato.

  Akiongea na waandishi wa habari baada ya kufunga mashindano ya Bonnah Cup yaliyoandaliwa na diwani wa kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa, Mkuu wa wilaya alisema kuwa kwa miaka ya sasa mpira umekuwa kimbilo kubwa la ajira kwa vijana kwani huweza kuwasaidia kujiingizia kipato.

  Mushi alisema kuwa pamoja na wadau kuwekeza katika mpira wa miguu, Tanzania itaweza vile vile kukuza vipaji ambavyo huwa vinapotea.

  “Tanzania tuna vipaji vingi sana vya mpira wa miguu, tatizo ni vipaji hivyo kuvumbuliwa hivyo nawaombeni wadau mbali mbali kutoka sekta zote kujitokeza kuweza kuwekeza katika tasnia hii, ambapo tutawezesha vijana wetu kujipatia ajira,” alisema

  Timu ya Stakishari kutoka Mogo iliifunga timu ya Vipaji Halisi kutoka eneo la airport katika fainili na kukabidiwa kombe pamoja na kiasi cha shilingi laki tano, ambapo mshindi wa pili alipata kiasi cha shilingi laki tatu na mpira moja na mshindi wa tatu alipata shilingi laki moja na mpia.

  Jumla ya timu 20 kutoka katika kata ya kipawa zilishiriki katika mashindano hayo.

  Muandaaji wa mashindano hayo diwani wa kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa alisema “Lengo kubwa ya kuandaa mashindano haya ni kuwaleta vijana pamoja iliwaweze kufahamiana na kushirikiana lakini pia kuinua vipaji vya vijana katika mchezo wa mpira wa miguu. Vijana wengi wanaocheze katika ligi hapa nchini wamechipukia katika kata ya Kipawa. “ Napenda kuendeleza na kukuza vipaji wa vijana iliwaweze kufikia kiwango cha juu zaidi katika mchezo huu”, alisema.

  Said Mkuwa, Mwenyekiti wa mashindano hayo aliongezea: “Tunamshukuru sana diwani kuandaa mashindano haya kwa ajili ya vijana, alisema “Nimefurahi kwamba mashindano yamekwenda vizuri tangu mechi za mwanzo hadi fainali na vijana wameshirikiana vizuri katika michezo yote”

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Bandari mpya ya Abiria katika bandari ya Malindi Zanzibar leo.mchana (kushoto) Sheikh Said Salum Bakhresa.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alitembelea sehemu mbali mbali katika ikiwemo IMMIGRATION DEPARTURES pamoja na Viongozi aliofuatana nao baada ya kugungua Bandari ya Abiria katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Injinia Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamad,(katikati) wakati alipotembelea sehumu ya Kuegeshea Meli ya Mizigo katika sherehe za ufunguzi wa Bandari mpya ya Abiria katika bandari ya Malindi Zanzibar leo.mchana.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi zawadi mfadhili wa Kampuni ya ujenzi wa Bandari mpya ya Abiria,Sheikh Said Salum Bakhresa,katika sherehe za ufunguzi wa Bandari mpya ya Abiria katika bandari ya Malindi Zanzibar leo mchana.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi na waalikwa katika sherehe za ufunguzi wa Bandari mpya ya Abiria katika bandari ya Malindi Zanzibar leo.mchana,(kushoto) Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundimbinu Issa Haji Ussi (Gavu) Harison Mwakiembe Waziri wa Miundombinu Bara,na Sheikh Said Salum Bakhresa (kulia).[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]

  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha 

  Wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mererani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wameiomba Serikali kuipatia leseni kampuni ya kizalendo ya Tan Youth Mining Ltd,ili wauziwe zana za milipuko kwa bei nafuu.

  Wakizungumza leo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini chini ya Kaimu Mwenyekiti wake Anne Kilango Malecela,wachimbaji hao walisema kampuni hiyo ikipatiwa kibali na kufutiwa kodi watachimba madini kwa urahisi.

  Mmoja kati ya wachimbaji hao,Sokota Mbuya alisema kampuni hiyo chini ya Mkurugenzi wake,Mohamed Karia ingepatiwa kibali cha kuwasambazia wachimbaji wadogo zana za milipuko wangekuwa na unafuu mkubwa.

  “Kwanini mzalendo asipewe kibali cha kutusambazia zana,apewa mtu wa South Africa,ambaye hatusaidii chochote yaani inatusababisha twende hadi Nairobi Kenya kufuata zana za milipuko ya migodi,” alisema Mbuya.

  Hata hivyo,Kamishna Msaidizi wa madini kanda ya kaskazini,Benjamin Mchwampaka aliieleza Kamati hiyo kuwa kwa alishaidhinisha kampuni hiyo ipatiwe kibali hicho,ila kinachokwamisha ni makao makuu wizarani.

  “Kampuni hiyo ingeweza kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa suala la milipuko na nilishasaini yote yanayonihusu,ila wizarani bado hawajasaini na alishahojiwa mpaka na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ,” alisema Mchwampaka.

  Akizungumzia kuhusu hilo,Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo,Anne Kilango Malecela aliwataka wachimbaji hao kuandika barua kwenye kamati hiyo wakutane na wizara mwezi ujao ili kampuni hiyo ipatiwe kibali hicho.

  0 0

   Ujenzi wa soko jipya na la kisasa Afrika Mashariki ,lililopo kando kando ya barabara iendayo Air Port ukiendelea ndani ya jijini la Mwanza,kama lionekanvyo mara baada ya kunaswa na kamera ya Globu ya jamii iliyokuwa ikijivinjari hapa na pale jijini humo.


  0 0

  On behalf of all the Smart Partners in the Movement, including HE Jakaya Mrisho Kikwete, President of Tanzania and CPTM Fellow, Global 2013 Host Patron & Adviser and His Colleagues, CPTM Chairman, Dialogue Resource Group, Joint Executive Group, Project Management Group, Joint Secretariat Teams, including CPTM Smart Partners' Hub, Global 2013 Joint Dialogue Conveners, Ambassador Sefue, Chief Cabinet Secretary of Tanzania and myself personally, we should like to express our shock, sympathy and compassion to Amos's family, NECF Patron, NECF Council Members and staff, as well as all Zimbabwean Smart Partners.

  The last message on my mobile from Amos says, "Mihaela, I am here in Dar es Salaam.  When and where is the JEG meeting to organise the briefings for the Dialogue sessions?"  This was on Thursday morning, 27th June.  Then he reported to the Joint Dialogue Resource Group briefing and, as usual, made exceptional contributions.  We will save that message to remind us what a Smart Partner is and what is a Smart Partners' Hub.

  Since I met Amos, who took the joint leadership of NECF forward, all the Smart Partners, including me, have always been able to refer to Amos as the main successful example and point of reference in the Smart Partnership Movement of how to maintain and develop a National Smart Partnership Hub.  He always openly shared the NECF's activities with the Smart Partnership Movement.

  Amos, as Head of NECF, became an honest broker of policy options, a Smart Partnership network builder, a super-node, which made him extraordinarily effective in influencing and delivering what was going on.  He had an open mind, he was always informed and able to facilitate deliberative, purposeful and impartial dialogues.  He was always seeking to create limitless opportunities the Smart Partnership way in Zimbabwe as well as in the Smart Partnership Movement more generally.

  Amos will always be remembered for being the Smart Anchor of all the Smart Partners' Hubs, in particular throughout Southern Africa, and a leading example of Smart Values, Ideas and Delivery in the Commonwealth and beyond.  The evolving Smart Partnership Movement Spiral of Dialogues and achievements since 1995 owes a great deal to Amos's emotional and intellectual driving force.  We owe him the debt of continuing in the same spirit.

  We dedicate the most successful outcome and way forward of the 21st Smart Partnership International Dialogue in Dar Es Salaam to Amos and his colleagues in NECF, Zimbabwe, on whom we rely for taking forward the Smart Partnership Movement in 2014 in South Africa and beyond.Additionally on behalf of the Smart Partnership Movement we would like to thank the Tanzanians, especially HE Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania and all of the medical team who treated him.

  We would like also to thank all Smart Partners/Members who willingly gave their urgent assistance as well as Zimbabwe's Ambassador to the Republic of Tanzania,  Major-General Edzai Chimonyo.  We thank the Lesotho Smart Partners' Hub for representing Southern Africa and the Smart Partnership Movement as a whole at the funeral service.
     
  If you would like to send a message of condolence to Amos's wife Barbra and family, please write either to her at bmushaninga@hotmail.com or to the Smart Partners' Hub at smart.partnership@cptm.org and we will forward any messages.
  Warm Regards,
  2012 with MYS 

  0 0

  DSCF1512
  Mwandishi wa habari wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa, Joseph Msami akifanya mahojiano na Rais mstaafu wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

  Hivi karibuni Mwandishi wa Habari wa Idhaa Ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa,Joseph Msami, alipata nafasi ya kukutana na kufanya mahojiano na Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi ambapo waliongelea mambo kadhaa na hususani umuhimu wa lugha ya Kiswahili. Mahojiano hayo yalifanyika kandoni mwa tamasha la Utamaduni wa Lugha hiyo lililofanyika jijini Washington,DC mwishoni mwa wiki. 

  Kusikiliza mahojiano hayo tembelea 
  Blog dada ya Globu ya Jamii, BongoCelebrity 

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akifungua rasmi Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission-JPC) kati ya Tanzania na India unaofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency-Kilimanjaro kuanzia tarehe 08 hadi 09 2013. Mkutano huo unaowashirikisha Wadau kutoka sekta mbalimbali za hapa nchini na India utajadili pamoja na mambo mengine masuala ya ushirikiano katika sekta za Uchumi, Ufundi, Sayansi na Teknolojia, Elimu, Afya, Utalii, Kilimo na Nishati na Madini. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Uholanzi Mhe.Dkt.Ad Koekkoek anayemaliza muda wake wa uakilishi nchini. Balozi huyo baadaye alifanya mazungumzo na Rais Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Spika wa bunge la Korea ya Kusini Mhe.Hee Chang wakati spika huyo na ujumbe wake walipomtembelea Rais ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Spika wa bunge la Korea Mhe.Hee Chang (kulia) akimfurahia Simba aliyekaushwa na kupamba lango la ikulu leo asubuhi. Kushoto ni mwenyeji wake,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na na Waziri wa Mambo ya nje wa India Mhe.Preneet Kaur ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya nje wa India Mhe.Preneet Kaur(wapili kushoto) na ujumbe wake ikulu jijini Dar es Salaam leo.kulia ni Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard Membe(picha na Freddy Maro)

  0 0


  0 0

   Mke  wa  waziri  mkuu Mama  Tunu Pinda ( wa tatu  kushoto) akiwasikiliza  viongozi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya TARWOC DROP-IN iliyopo Mkimbizi mjini Iringa pindi alipotembelea  taasisi  hiyo. Wengine  pichani ni viongozi wa taasisi hiyo akiwemo mkurugenzi wake Mhe. Lediana Mng'ong'o ambae ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa  wa tatu  kushoto na wapili  kushoto ni mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  Terresia Mahongo
  Siku ambayo  shirika lilionyesha mfano kwa  kutoa Baiskeli kwa Mbalozi wa Kata 20 wakisubiri kukabidhiwa usafiri wa Baiskeli nje ya kituo cha shirika la TARWOC DROP IN.    


  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko akifafanua jambo kwa waandishi wahabari alipokutana na Wageni kutoka Taasisi ya Right To Play leo jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Right To Play International ambaye pia ni mwanzilishi wa Taasisi hiyo Johenn Olav Koss akisisitiza jambo katika mkutano baina yake na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa Right To Play Tanzania Bibi Josephine Mukakalisa (Kulia) akifafanua jambo katika mkutano wa Taasisi yao na uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Right To Play International Johenn Olav Koss.
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo akifafanua jambo kwa waandishi wahabari alipokutana na Wageni kutoka Taasisi ya Right To Play leo jijini Dar es Salaam,Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Michezo Bibi Juliana Yassoda.


older | 1 | .... | 189 | 190 | (Page 191) | 192 | 193 | .... | 3278 | newer