Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110180 articles
Browse latest View live

UWT MKOA WA RUVUMA KUJENGA KIWANDA CHA SABUNI

$
0
0
Hayo yamesemwa na mwenyekiti mpya wa jumuiya wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT bi scholla manyasa wakati akizungumza na baadhi ya viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni.

VIWANDA MOROGORO VYA PONGEZWA KWA KUNUSURU UHARIBIFU WA MAZINGIRA

$
0
0
 Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mhe. Luhaga Mpina, Mbele yake ni Bw. George Mratibu wa Kiwanda cha Ngozi Morogoro , cha ACE LATHER TANZANIA LTD, wakiwa katika ukaguzi wa mtambo wa kisasa wa kutibu majitaka kiwandani hapo ambapo Mpina yupo Mkoani Morogoro katika ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa Sheria ya Mazingira na kanuni zake, kufuatia maagizo aliyoatoa awali katika ziara ya viwanda hivyo.

 Kushoto kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji Taka mjini Mororgoro, inginia Halima Mbiru, akimuonyesha Naibu Waziri Mpina Mpaka wa mabwawa ya maji taka mali ya mamlaka hiyo, hayapo katika picha. Mhe. Mpina alifanya ziara ya ukaguzi wa mabwawa hayo mapema leo.

 Katika picha ni washiriki katika ziara ya Naibu Waziri Mpina alipokagua Mabwawa ya majitaka kama yanavyoonekana katika picha.

Kushoto, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina kulia ni Mwenyeji wake  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Steven Kebwe katika kikao kabla ya kuanza ziara ya ukaguzi wa viwanda Mkoani hum oleo. (Picha na Evelyn Mkokoi)

Magonjwa ya moyo huua watu milioni 17 duniani – Dk. Sanga

$
0
0
Na.Paschal Dotto-MAELEZO

SERIKALI ya Awamu ya Tano kupitia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), imewashauri wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kuweza kugundulika mapema iwapo wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi hiyo, Tulizo Sanga alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Dk Sanga alisema tafiti zinaonesha zaidi ya watu milioni 17 hupoteza maisha kutokana na kuugua magonjwa ya moyo kila mwaka duniani.“Ni magonjwa ambayo husababisha vifo vya watu wengi duniani huku hali ikionekana kuwa mbaya zaidi katika nchi zinazoendelea,” alisema Dk Sanga.

Alisema tafiti zinaonesha pia zaidi ya watu milioni 75 huugua magonjwa hayo kila mwaka duniani.“Tanzania bado hatujafanya utafiti wa kina lakini tangu Taasisi hii imeanza kufanya kazi tunaona zaidi ya wagonjwa 300 kwa siku na wengi huja wakiwa katika hatua mbaya ya ugonjwa,” alisema.

Alisema tangu Septemba 25 hadi 29, mwaka huu madaktari wa JKCI wamewafanyia upasuaji wagonjwa 28 kwa kushirikiana wenzao wa Taasisi ya Madaktari Afrika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.Kwa upande wake, Mtaalamu wa lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Louiza Shem alisema mfumo mbovu wa maisha hasa ulaji usiofaa na kutokufanya mazoezi kunachangia wengi kupata magonjwa ya moyo.

“Kwa bahati nzuri hamna chakula ambacho mtu hatakiwi kutumia ili kujiepusha na magonjwa ya moyo, huwa tunashauri jinsi gani na kwa kiasi gani uvitumie ili kuepuka kupata magonjwa haya,” alisema.

Mtaalamu huyo alitoa mfano “Kuna vyakula vya wanga kama vile wali, ugali na vinginevyo, unakuta mtu anakula… amejaza sahani.“Unapaswa kula kulingana na aina ya kazi unayofanya, kwa mfano wengi ambao tunafanya kazi ofisini hatutumii nguvu nyingi kulinganisha na wale wanaobeba mizigo, wengi tunakula nyama kwa kiwango kikubwa, ni vema kupunguza kiasi.

“Mafuta yanayopatikana kwenye nyama zinaongeza uzito kupita kiasi na huenda kuziba mishipa ya damu, ikiwa ni ya kichwani utapooza mwili na ikiwa ni kwenye moyo utapata ‘heart attack’,” alibainisha.Alishauri pia jamii kupunguza kiwango cha chumvi kwani inapotumika kwa kiwango kikubwa huathiri afya ya moyo.

“Kundi kubwa tunaloona linaathirika na magonjwa haya ni wale waliopo kwenye umri wa uzalishaji na umri unavyozidi kuongezeka ndivyo uwezekano wa mtu kupata ugonjwa huu unavyoongezeka,” alisema.

MANISPAA YA DODOMA YAANZA KUANDAA HATI MILIKI ZA ARDHI ZA MIAKA 99 KWA KASI, BARAZA LA MADIWANI LAPONGEZA

$
0
0


NA Ramadhani Juma,OFISI YA MKURUGENZI 

HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma imekamilisha uandaaji wa hati 912 za umiliki wa ardhi za miaka 99 kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli Mei 15 mwaka huu wakati akitoa tamko la kuivunja iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) na shughuli zote kuhamishiwa katika Manispaa ya Dodoma.

Akizungumza katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichopokea taarifa rasmi ya makabidhiano ya majukumu ya iliyokuwa CDA kuhamia Manispaa ya Dodoma jana, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Godwin Kunambi aliwaambia Madiwani na wananchi kwa ujumla waliohudhuria Baraza hilo kuwa, hatua hiyo imefikiwa katika kipindi cha miezi miwili ya Julai na Agosti, huku akiahidi kuwa,Manispaa hiyo itaendelea kutoa huduma hiyo na nyingine kwa kasi inayoendana na matarajio ya wananchi.

Alisema kati ya hati hizo, hati 674 zilizowasilishwa kwa Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Wizara ya Ardhi zimeshasajiliwa na zipo tayari kwa ajili ya kukabidhiwa kwa wananchi husika, huku hati 238 zikiwa katika hatua ya kukaguliwa ili zisainiwe.

Alifafaua zaidi kuwa, uandaaji huo wa hati unaenda sambamba na utoaji wa vibali vya ujenzi kwa haraka, ambapo mchakato wa kutoa kibali cha ujenzi unakamilishwa ndani ya siku saba tu baada ya maombi kupokelewa mpaka muombaji anakabidhiwa kibali chake.

Kufuatia taarifa hiyo, wajumbe wa Baraza la Madiwani wakiongozwa na Meya wa Manispaa ya Dodoma Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe wameipongeza Menejimenti ya Halmashauri na watumishi wote na kuwataka waendelee na juhudi hizo ili pamoja na mambo mengine kuufanya mji wa Dodoma ukue kwa kasi kwa kuwawezesha wananchi na wadau wengine kujenga. 
Mkurugenzi wa wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (kulia) ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akizungumza wakati wa Baraza la Madiwani la Mnispaa hiyo.

Tanzania yakabidhiwa mashine ya kutoa dawa ya usingizi wakati wa upasuaji.

$
0
0
Na.Paschal Dotto-MAELEZO. 

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekabidhiwa mashine maalumu ya kutoa dawa za usingizi kwa mama wajawazito wenye uzazi pingamizi wakati wa upasuaji kwaajili ya kuokoa maisha yao.

Akizungumza katika makabidhiano hayo leo Jijini Dar es Salaam Waziri mwenye dhamana ya Afya Mh.Ummy Mwalimu alisema kuwa, hiyo ni hatua kubwa katika kupambana na vifo vya wakina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga.

Waziri Ummy alitoa pongezi kwa watu waliojitolea kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya kuokoa maisha ya mama na mtoto wakiongozwa na Dkt.Ahmed Mohamed Makuwani, ambapo alisema kuwa waliopanda mlima Kilimanjaro wamewezesha kupatikana kwa msaada wa mashine hiyo, hivyo akawashukuru na kuomba wadau wengine kuiga mfano huo.

“Tunawashukuru Utepe Mweupe wa Uzazi Salama kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kushirikiana na serikali ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo kwa watoto wachanga, hatua hii inatufariji sana na naomba watanzania na wasio watanzania wenye mapenzi mema na afya ya mama na mtoto kuendelea kusaidia juhudi hizi ”, alisema Waziri Ummy.

Akieleza mafanikio katika sekta ya Afya waziri Ummy alisema kuwa kuna zaidi ya vituo vya afya 480 nchi nzima na kati ya hivyo vituo 109 vinavyumba vya upasuaji ambayo ni sawa na asilimia 20 huku akibainisha kuwa kufikia Juni, 2018 serikali inatarajia kujenga vyumba vya upasuaji 170 vitakavyosaidia upasuaji wa mama wenye uzazi pingamizi na idadi hiyo itaongezeka na kufikia vituo 279. 
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kupokea msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi zilizotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ). Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Idara kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya na  Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ) Rose  Mlay. 

Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ) Rose  Mlay akielezea jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi iliyotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ). Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Afya, Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kas Medics Limited Nishitha Kulshreshtha  mara baada ya kukabidhiwa kukabidhiwa msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi iliyotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ) kufuatia udhamini wa kampuni hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Idara kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipata maelezo kuhusu namna mashine ya kutolea dawa za usingizi inavyofanya kazi wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa mashine hiyo iliyotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ) leo Jijini Dar es Salaam. Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. 

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 30,2017

DC WA KAKONKO KANALI NDAGALA APIGA MARUFUKU UNYANYASAJI KWA WAZEE,KUWATUHUMU WANAZUIA MVUA

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewaagiza Wananchi wa Wilaya ya Kakonko kuacha tabia ya kuwatuhumu baadhi ya wazee kuwa Wanazuia Mvua na kutaka kuwaondoa ikiwa ni pamoja na kuwauwa kwa kwa imani za kishirikina , na vikundi vitakavyo gundulika vinawatuhumu watachukuliwa hatua ili kukomesha vitendo hivyo.

Akizungumza na Wananchi jana katika maadhimisho ya siku yaWazee Wilayani humo katika kijiji cha Kasanda ,Ndagala alisema kumekuwa na tabia ya Wananchi wengi kuwatuhumu baadhi ya wazee kuwa wanazuia mvua, jambo ambalo ni imani za kizamani na zilizopitwa na wakati.
 
 "Kwa hiyo mimi nawaomba tuendelee kushirikiana na wazee wetu hawa kwa kuwa pia wana mchango wao mkubwa katika jamii,ni vyema tukawafanya wazee wetu waishi kwa amani na kuachana na imani hizo zinazoweza kuleta chuki na uhasama mkubwa baina yetu",alisema Ndagala.

Alisema vitendo kama hivyo vilijitokeza mwaka jana, baadhi ya wazee walitaka kuuwawa kwa tuhuma hizo,alisema na kuongeza kuwa imani hizo zinapaswa kupuuzwa kwani zinaweza kuchochea uvunjifu wa amani Kwa Wazee hao ambao ni hadhina kubwa kwa jamii. 
 
"Niwaombe wananchi mshirikiane na Wazee waliopo katika maeneo yenu, tumeona mchango wao ni mkubwa sana katika jamii na Taifa kwa ujumla Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni thamini mchango wa wazee kwa maendeleo ya Nchi yetu, na serikali inalitambua hilo ndio maana inatoa kipaumbele kwa Wazee kwa kuhakikisha wanakuwa na Afya njema kwa kupatiwa matibabu bure kutokana na mchango wao", alisema Ndagala.

 Baadhi ya Wazee wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye maadhimisho hayo
 Mkuu Wawilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa timu ya wazee wa kijiji cha Kasanda iliyofanya vizuri katika michezo wakati wa maadhimisho hayo ya Wazee.
  MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabizi vitambulisho vya matibabu kwa baadhi ya wazee wilayani Kakonko.
  MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabizi vitambulisho vya matibabu kwa baadhi ya wazee wilayani Kakonko.
 Baadhi ya wazee wakicheza ngoma katika maadhimisho ya siku ya wazee..





WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO YAKUTANA NA WADAU MJINI DODOMA KUJADILI MABORESHO YA MKAKATI DHIDI YA MAUAJI YA WAZEE NCHINI.


ISANJABADUGU WAKABIDHI VITENDEA KAZI KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOGWE.

$
0
0
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Mh Vicent Busiga.amepokea vinakilishi vitatu vyenye thamani ya Tsh 3,000,000 kutoka kwenye kikundi cha wachimbaji wadogo wadogo kinachoitwa Isanjabadugu kilichopo kwenye kata Nyakafulu wilayani Mbogwe.

Akiongea wakati wa makabidhiano, Mwenyekiti wa halmashauri amemshukuru Mungu kwa Neema ya machimbo mapya ya dhahabu yaliyogundulika hivi karibuni katika kata ya nyakafulu kwa kuwa ni neema ya pekee na kuwataka wachimbaji hao kusimamia vizuri eneo hilo na wahakikishe wanalipa kodi ya serikali kama inavyotakiwa,vilevile mwenyekiti amewataka waendelee kuihudumia jamii inayowazunguka na kuendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo ya wilaya hii kwani Wilaya bado ni changa na inakabiliwa na changamoto nyingi.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw Joseph Katemi Watwa, amesema wametoa msaada huo wa vinakilishi baada ya kutembelea ofisi za halmashauri na kugundua kuwa ofisi hizo zinakabiliwa na changamoto kubwa ya vitendea kazi vikiwemo vinakilishi hivyo wakaamua kuchuka hatua ya kutoa msaada wa vifaa hivyo ili kupunguza changamoto hiyo. Bw Joseph ameendelea kusema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwenye shughuli zote za maendeleo ya wilaya pamoja na kulipa kodi zote za serika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Elias Kayandabila ametoa shukrani kwa wachimbaji hao na kuwaomba waendelee kuunga mkono shughuli za maendeleo kwenye wilaya hii kwani wilaya bado ni changa na inakabiliwa na changamoto nyingi. 


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Elias Kayandabila Akipokea Computer kutoka kwa Katibu wa Wachimbaji wadogo wadogo (Isanjabadugu).
Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe mhe Vicent Busiga Akipokea computer kutoka kwa Mwenyekiti wa Isanjabadugu ndg Joseph Katemi watwa.
Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe wakiwa na Uongozi wa wachimbaji Wadogo Wadogo

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es salaam atembelea vituo vya daladala

$
0
0
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es salaam (ZTO) Kamishna Msaidizi wa Polizi ACP Awadhi Haji akitoa maelekezo kwa afande Doria 72 Sgt John wa doria 26 alipotembelea kituo cha Daladala kilichopo Gerezani jijini Dar es salaam. Afande Haji alielekeza wakamate magari yote yanayodaiwa.
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es salaam (ZTO) Kamishna Msaidizi wa Polizi ACP Awadhi Haji akiongea na baadhi ya madereva wa Daladala ambao magari yao yalikamatwa kwa kutokulipa madeni alipotembelea kituo cha Daladala kilichopo Gerezani jijini Dar es salaam. 
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es salaam (ZTO) Kamishna Msaidizi wa Polizi ACP Awadhi Haji akiongea na baadhi ya madereva wa Daladala ambao magari yao yalikamatwa kwa kutokulipa madeni alipotembelea kituo cha Daladala kilichopo Gerezani jijini Dar es salaam. 
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es salaam (ZTO) Kamishna Msaidizi wa Polizi ACP Awadhi Haji akiongea na baadhi ya madereva wa Daladala ambao magari yao yalikamatwa kwa kutokulipa madeni alipotembelea kituo cha Daladala kilichopo Gerezani jijini Dar es salaam. 

Introducing "SEMA" by Madee ft. Nandy

BETTER HEALTH, WATER AND FOOD FOR TANZANIA WITH THE HELP OF NUCLEAR TECHNOLOGIES AND INTERNATIONAL PARTNERS

$
0
0
Science and technological innovations play a fundamental role in assisting African leaders to root causes of poverty, hunger and climate change. 

It is therefore no surprise that nuclear science and innovative nuclear technologies are playing a major role in providing viable solutions to help achieve these targets.

It is well known globally that nuclear technologies have much to offer in the fight against poverty, hunger, dread diseases, and water shortages, not to mention its ability to provide sustainable and environmentally friendly electricity. 


Let’s take a closer look these various applications.

Nuclear medicine helps millions of people across the globe to successfully fight cancer and has reducedthe mortality rate of non-communicable diseases by one third. Moreover, nuclear science centers and research facilities are indispensable in the production of radioisotopes which are used in complex medical treatments. African countries have already made significant steps in nuclear science development under the guidance of the United Nation’s International Atomic Energy Authority (IAEA) and its key member states.

For example, in Zambia “people can access treatment locally for a fraction of the cost they would pay by travelling outside the country. More than 17,000 new cases of cancer have been diagnosed and treated over the last 10 years,” said MulapeKanduza, Chief medical physicist of the Cancer Diseases Hospital (CDH) in Lusaka.“Without the assistance of the IAEA, it would have been very difficult for us to set up a highly technical centre like this one and care for so many patients,” said Dr Lewis Banda, the CDH’s Senior Medical Superintendent.

Tamko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, Oktoba 1, 2017

$
0
0
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na wadau wote duniani katika kuadhimisha siku ya wazee duniani. Wakati dunia inaadhimisha siku hii, Tume inatoa wito kwa jamii ya Watanzania kuondoa vitendo vyote vya unyanyasaji dhidi ya wazee ili kuhakikisha kuwa wanaishi katika kutekeleza kauli mbiu ya taifa inayosema: “Kuelekea uchumi wa viwanda: Tuthamini mchango, uzoefu na ushiriki wa wazee kwa maendeleo ya taifa.” 

Uzee na kuzeeka havikwepeki; hivyo ustaarabu wa jamii au nchi yoyote duniani si wingi wa raslimali na mazingira mazuri bali katika uwekaji wa mifumo madhubuti ya kulinda na kutetea haki za makundi maalum yanayohitaji ulinzi wa jamii husika. Kwa kulitambua hilo Desemba 14, 1990, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Azimio lake Na. 45/106 ulipitisha tarehe 01 Oktoba, ya kila mwaka kuwa siku ya wazee Duniani. Vipaumbele katika Azimio hilo ni pamoja na suala la uhuru wa wazee, wazee kushiriki na kushirikishwa katika shughuli za maendeleo, kutunzwa na kuheshimiwa. 

Hivyo siku hii ya tarehe 01 Oktoba, dunia inawapa nafasi wazee kukutana pamoja na kubadilishana mawazo juu ya nini cha kufanya kuhusiana na mustakabali wa haki zao kwa ujumla, katika kuleta maendeleo ya Taifa tunapoelekea Tanzania ya viwanda. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTALII DUNIANI MKOANI IRINGA

$
0
0
Na Hamza Temba-WMU

Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe jana tarehe 30 Septemba, 2017 amefungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Iringa na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na Serikali katika kupambana na Ujangili kwa kutoa taarifa za siri zitakazoweza kuwaibaini na kuchukuliwa hatua.

“Ili kulinda uwepo wa rasilimali za utalii zilizopo kwa vizazi vya sasa na vijavyo, ni lazima wananchi kushirikiana pamoja na Serikali katika mapambano dhidi ya ujangili, mkiona mtu ananyemeleanyemelea huko porini tuambieni tutamshukia kama mwewe” alisisitiza Prof. Maghembe.

Ufunguzi huo wa Siku ya Utalii Kitaifa umeenda sambamba na ufunguzi wa Maonesho ya Karibu Kusini pamoja na maonesho ya wajasiariamali wa viwanda vidogo SIDO yaliyoshirikisha wajasirimali kutoka mikoa ya nyanda zajuu kusini kwa lengo la kuonesha bidhaa zao zitakazoweza kutumiwa na watalii pamoja na watoa huduma hiyo. 

Alisema, kaulimbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu kwa upande wa Siku ya Utalii Duniani ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo wakati ile ya Maonesho ya Karibu Kusini ikiwa ni “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.

Alisema sekta ya utalii imechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi kwa kuchangia asilimia kubwa ya mapato ya Serikali, kuongeza ajira, kipato cha jamii na kuchochea ukuaji wa sekta zingine. 

"Utalii ndio ndio sekta pekee inayoongoza kwa kuliingizia taifa fedha za kigeni kwa asilimia 25, Aidha, inachangia asilimia 17.5 ya pato la taifa na asilimia 11 ya ajira zote nchini" alisema prof. Maghembe. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mkakati wa Utalii wa Mkoa wa Iringa ambao umeandaliwa kwa lengo kuunga mkono azma ya Serikali wa kufungua utalii wa Nyanda za Juu Kusini katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Amina Masenza na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto), Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wa Serikali wakionesha Mkakati wa Utalii na Jarida la Iringa baada ya uzinduzi rasmi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip Chitaunga akiwa na baadhi ya washiriki wengine kwenye ufunguzi wa maadhimisho hayo.
Sehemu ya washiriki wa maadhimisho hayo ya Wiki ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini. Nyuma yao ni mabanda ya maonesho hayo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

IGP SIMON SIRRO AFANYA MAZOEZI NA MAOFISA NA ASKARI WA MAKAO MAKUU YA POLISI

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akiongoza maofisa na askari wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam katika mazoezi ya pamoja ambayo hufanyika kila mwisho wa mwezi. IGP amewahimiza Makamanda wa Polisi wa Mikoa yote kuhakikisha wanafanya mazoezi ya pamoja ili kuendelea kuboresha afya za maofisa na askari. 

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akiongoza maofisa na askari wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam katika mazoezi ya pamoja ambayo hufanyika kila mwisho wa mwezi. IGP amewahimiza Makamanda wa Polisi wa Mikoa yote kuhakikisha wanafanya mazoezi ya pamoja ili kuendelea kuboresha afya za maofisa na askari. 


MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM- Taifa) RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM-TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) kabla ya kufungua mkutano huo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) kabla ya kufungua mkutano huo jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli akipiga makofi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano wa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) wakipiga makofi mara baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli kuwasili ukumbini hapo jijini Dar es Salaam. 
Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakiendelea na Kikao jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU. 

CRDB BANK YAKUTANA NA WATEJA WAKE WAKUBWA JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akizungumza katika hafla fupi iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa wateja wake wakubwa, yenye lengo la kuwafahamisha fursa mpya na kukusanya maoni yao juu ya njia za kuwapa huduma bora, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Septemba 29, 2017. Hafla hiyo pia iliambatana na uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dkt. Charles Kimei, kuzungumza katika hafla fupi iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa wateja wake wakubwa, yenye lengo la kuwafahamisha fursa mpya na kukusanya maoni yao juu ya njia za kuwapa huduma bora, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Septemba 29, 2017.
Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Goodluck Nkini akizungumzia mikakati mbalimbali ya Benki hiyo kwa wateja wake, wakati hafla fupi iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa wateja wake wakubwa, yenye lengo la kuwafahamisha fursa mpya na kukusanya maoni yao juu ya njia za kuwapa huduma bora, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Septemba 29, 2017.
Mkurugenzi wa Hazina wa Benki ya CRDB, Alex Ngusaru akisisitiza jambo katika hafla fupi iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa wateja wake wakubwa, yenye lengo la kuwafahamisha fursa mpya na kukusanya maoni yao juu ya njia za kuwapa huduma bora, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Septemba 29, 2017. 
Sehemu ya wateja wakubwa wa Benki ya CRDB waliohudhuria hafla hiyo.

BARAZA TAIFA LA TAFES LAZINDUA SIKU 40 ZA MAOMBI KUOMBE AMANI NA WANAFUNZI WATAKAOANZA MASOMO VYUONI.

$
0
0
BARAZA la taifa la TAFES hapa nchini limezindua siku 40 za maombi kwaajili ya kuombe amani hapa nchini pamoja na wanafunzi watakaoanza mwaka mpya wa masomo katika vyuo vikuu vyote hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa baraza la taifa la TAFES, Profesa Lazaro Busagala wakati akizungumza na wanafes waliohudhulia mkutano wa chama hicho jijini Dar es Salaam leo.

Nae Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, amesema kuwa ili kuwa na taifa lenye maadili lazima kuwe na taasisi za kidini na za kiroho zitakazokuwa zikiwalea watoto na vijana katika vyuo hapa nchini, pia amesema kuwa Baraza la taifa la Tafes ambalo linawalea wanafunzi wa vyuo vikuu wa madhehebu ya kiprotestandi yanafanya kazi kubwa sana kwa kuwalea wanafunzi hao wawapo vyuoni na kuwa na maadili yanayokubalika katika jamii.

Amesema kuwa ili kuwa na jamii yenye maadili lazima kuwepo na watu wenye karama ya kuwafunza wengine maadili ya kiroho.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akizungumza na wanachama wa Taasisi ya wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini wakati wa kuzindua siku 40 za maombi kuombea Nchi pamoja na wanafunzi watakao jiunga na vyuo vikuu wa dini za kiprostandi hapa nchini.Taasisi hiyo ambayo inasaidia kuwaandaa kiroho na kijamii wanafunzi ili kuwe na jamii adilifu pamoja na viongozi waadilifu.
Taasisi hiyo inamchango mkubwa katika kuitengeneza jamii kuondokana na jamii yenye watu wenye roho mbaya.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba akizungumza na wanaTAFES walikusanyika katika ukumbi wa mikutano wa benki kuu jijini Dar es salaam.

Mtoa maada Dk. Joshua Wathang'a akizungumza kuhusiana na kwanini huduma ya kiroho itolewe vyuoni kwa wanafunzi hii kwasababu elimu hii humwandaa mwanafunzi kukubalika katika jamii pamoja na kuwa na watu wenye hufu ya Mungu na wenye maadili mazuri.Wathang'a ameyasema hayo mbele ya wanachama wa TAFES waliohudulia katika mkutano huo jijini Dar es salaam.
Mnyekiti wa baraza la taifa la TAFES, Profesa Lazaro Busagala akizungumza na wanafes waliohudhulia mkutano wa chama hicho jijini Dar es Salaam Uliofanyika kwaajili ya Kuombea Taifa pamoja na wanafunzi watakaoanza mwaka mpya wa masoko katika vyuo vikuu hapa nchini.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba Akiwa katika mkutano wa wanatafes uliofanyika jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuliombea taifa amani pamoja na kuwaombe wanafunzi watakaoanza mwaka mpya wa masomo mwaka huu. 
Baadhi ya wageni waliohudhulia katika mkutano wa wanaTAFES wakimsikiliza Mgeni rasmi jijini Dar es Salaam. 
Picha zote na Avila Kakingo,Globu ya jamii.

ELIMU SOLUTION WASAFIRISHA WANAFUNZI 50 KWENDA KUSOMA NCHINI CHINA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Elimu Solution, Neithan Swed akizungumza na  waandishi kuhusu kampuni ya Elimu Solution ilivyoweza kusafirisha wanafunzi hamsini(50) kwenda kusoma nchini China kwa miaka minne kwa ufadhili leo katika uwanja wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mwanadunzi anayekwenda kusoma nchini China, Osmund Mbilinyi akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kuhusu namna alivyoweza kufanikisha kuomba ufadhili wa kusoma nchini china kuputia kampuni ya Elimu Solution.
 Mmoja wa wazazi wa wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini China, Marysponser Nhwan akizungumza na waandishi wa habari kuhusu furaha aliyonayo baada ya mtoto wake kupata nafasi ya kwenda kusoma nchini Chini akiwa na ufadhiri kwa takribani miaka minne(4).
  Mmoja wa wazazi wa wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini China, Saimoni Mapunda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna walivyoweza kuomba ufadhili wa mwanae kwenda kusoma nchini China kupitia kampuni ya Elimu Sotion leo katika uwanja wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wanaokwenda kusoma China pamoja na wazao wao wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye uwanja wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo

TCCIA YAZINDUA MALIPO KWA NJIA YA MTANDAO

$
0
0

Rais wa TCIA akifafanua jambo mbele wa wafabiashara walioshirika katika mkutano mkuu wa mwaka.Chama cha wafanyakazi, kilimo na viwanda Tanzania kimefanya mkutano wake mkuu wa mwaka pamoja na kuzindua mfumo mpya wa ulipiaji bidhaa kwa njia ya mtandao ‘LIPA FASTA’ lengo kubwa likiwa ni kusaidia wafanyabiashara ambao wamekuwa wakisafirisha bidhaa zao nje ya nchi. Mfanyabiashara na mwanachama wa TCCIA ndugu mustafa hassanal akisalimiana na mgeni rasmi ndugu Raymond Mbilinyi katika mkutano mkuu wa mwaka, pembeni ni makamu Rais wa TCCIA ndugu Octavian Mshiu

Huduma hii imezinduliwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa TCCIA ambapo wanachama wote wa TCCIA pamoja na wafanyabiashara mbalimbali walihudhuria mkutano huo kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa huduma hii ambayo itakuwa mkombozi kwa wafanyabiashara wengi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Gotfrid Muganda akiongea na wafanyabishara waliohudhuria katika mkutano mkuu wa mwaka

Akizungumza kwenye mkutano huo Mkurungezi Mtendaji ndugu Gotrid Muganda alisema ‘LIPA FASTA ni mkombozi kwa wafanyabiashara wote katika kurahisisha njia zao za kufanya malipo. Kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakisafirisha bidhaa zao nje ya nchi, sasa hawana haja ya kuwa na wasiwasi katika kufanya malipo kwani mfanyabiashara anaweza kufanya malipo akiwa ofisini kwake.Mfumo huu utasaidia wafanyabiashara kupata cheti cha uwasili kwa muda mfupi.Rais wa TCCIA ndugu John Mayanja akifafanua jambo katika mkutano hu0
Nae makamu wa Rais wa chama Ndugu Octavian Mshiu amesema’ mpango huo utaendeshwa na TCCIA kuanzia ngazi ya wilaya ili kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa zao nje ya nchi’
LIPA FASTA ni zaidi ya njia ya malipo kwani hapa hata watanzania waishio nchi za nje ya nchi watapata nafasi ya kupata taarifa sahihi za soko, kuhifadhi taarifa sahihi za soko na bidhaa zilizopelekwa kwenye maitaifa mbalimbali pamoja na kumwezesha mfanyabiashara kufanya malipo popote alipo.Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano mkuu wa mwaka wakifwatila mkutano
Viewing all 110180 articles
Browse latest View live




Latest Images