Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live

TSN,TBC ZA TWAA TUZO ZA DSE 2017 PIA ZIPO NMB, TBL NA STANDARD CHARTERED BANK

0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara yaFedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  ya Chombo bora cha habari mwaka 2017 (Magazeti), Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dk. Jim Yonazi (kulia) baada ya Kampuni hiyo kuibuka mshindi katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Moremi Marwa. (Picha:Mroki Mroki/TSN Digital).
 Naibu Katibu Mkuu Wizara yaFedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  ya Chombo bora cha habari mwaka 2017 (Digital), Kaimu Mkurugenzi wa habari na Matukio wa TBC, Prudence Costantine (kulia) baada ya Kampuni hiyo kuibuka mshindi katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Moremi Marwa.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara yaFedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  kwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani (kulia) baada ya Benki hiyo kuibuka mshindi katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Moremi Marwa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara yaFedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania,(TBL), Bruno Zambrano (kulia) baada ya Kampuni hiyo kuibuka mshindi katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Moremi Marwa.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara yaFedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  kwa Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB anaeshughulika na Mikakati na mahusiano ya wawekezaji, Anna Mwasha (kulia) baada ya Benki hiyo kuibuka mshindi wa pili katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Moremi Marwa.


IGP SIRRO AWAKABIDHI BENDERA ASKARI WANAOKWENDA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA ULINZI WA AMANI DARFUL NCHINI SUDAN

0
0
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Andrew Sattaa akiwakabidhi bendera ya Taifa kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo (IGP) Simon Sirro, askari wa Jeshi hilo wanaokwenda Darful, nchini Sudani kushiriki shughuli za Ulinzi wa amani ambapo amewataka askari hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kufuata taratibu kwa kipindi chote watakachokuwemo nchini  humo. Picha na Jeshi la Polisi
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Adrew Satta, akimuwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiwaaga askari wanaokwenda kushiriki shughuli za Ulinzi wa Amani Darful Nchini Sudan, ambapo amewataka askari hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kufuata taratibu kwa kipindi chote watakachokuwemo nchini  humo. Picha na Jeshi la Polisi.

SEKTA BINAFSI ZAONGEZA NGUVU KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA SINGIDA.

0
0
Wadau mbalimbali wa sekta binafsi wameweza kuongeza nguvu katika kuboresha sekta ya Afya Mkoani Singida kutokana na ushirikiano mzuri ulipo baina yao na serikali.

Hayo yamebainishwa katika mkutano maalumu wa siku mbili uliohitimishwa jana Mjini Singida, ambapo viongozi wa serikali, taasisi na mashirika 15 yanayotoa huduma za Afya na Ustawi wa jamii Mkoani hapa wamejadiliana namna ya kuboresha ushirikiano baina yao.

Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Singida Dkt Mohamed Mbalazi amesema katika mapambano dhidi ya Ukimwi na Virusi vya Ukimwi (VVU) Mkoani hapa, Sekta binafsi zimekuwa na mchango mkubwa.

Dkt Mbalazi amesema wadau hao wameweza kutoa dawa za kupunguza makali ya VVU, tiba lishe, mafunzo kwa watoa huduma wa afya, ufuatiliaji wa watumia wa dawa za VVU pamoja na kuandaa takwimu jambo ambalo limeboresha mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.

“Sisi kama watendaji wa serikali tunathamini na kutambua mchango wa wadau wa sekta afya kwakuwa ni nguzo muhimu sana, mfano wadau wetu shirika la EGPAF, wametenga bilioni 1.6 kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi na maambukizi ya VVU” Mkoani Singida”, amesema na kuongeza kuwa,
Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Singida Dkt Mohamed Mbalazi akitoa mada katika mkutano ulijadili uboreshaji wa ushirikiano baina ya serikali na wadau wa sekta binafsi zinazotoa huduma ya Afya Mkoani Singida.
Afisa Lishe Mkoa wa Singia Teda Sinde akifafanua jambo katika mkutano ulijadili uboreshaji wa ushirikiano baina ya serikali na wadau wa sekta binafsi zinazotoa huduma ya Afya Mkoani Singida.
Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma Mkoa wa Singida Dkt Evans Mlay (wa kwanza kushoto) akipitia dondoo, kabla ya kuwasilisha mada iliyoonyesha mchango mkubwa wa wadau Sekta ya Afya katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu Singida, Kulia kwake ni Afisa Mradi wa AMREF Mkoa wa Singida Donathapeace Kayoza.

PROF. KABUDI ATEMBELA UBALOZI WA TANZANIA UBELIGIJI

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Prof. Palamagamba John Kabudi, ametembelea ubalozi wa Tanzania Brusels, Ubeligiji tarehe 29 Septemba, 2017. Prof. Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania Nchini Ubeligiji Mheshimiwa Joseph Edward Sokoine. 

Prof. Kabudi yuko Mjini Brussels, Ubeligiji akiambatana na Mhe. Rais Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Uganda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi.

 Wakati akiwa Brussels, Prof. Kabudi ameshiriki mazungumzo baina ya Rais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Rais wa Kamisheni ya Jumuiya ya Ulaya kuhusu Mkataba wa Ubia wa Kiuchumi baina ya Jumuiya ya Ulaya na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe Prof. Palamagamba Kabudi,Waziri wa Katiba na Sheria akiwa kwenye picha ya pamoja Bw. Geoffrey Kabakaki, Mwambata Maalum (Minister Plenipotentiary) wakati alipotembea makazi ya Balozi.
Mhe. Prof Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria akisalimiana na Mhe. Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi za Ubalozi zilizoko Mjini Brussels, Ubeligiji
Mhe. Prof Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria akiwa kwenye picha ya Pamoja na Mhe. Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi za Ubalozi zilizoko Mjini Brussels, Ubeligiji
Picha ya pamoja

HOTUBA YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA, RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOFUNGUA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCM

SEMINA KWA MAFUNDI UMEME WA MIKOA YA TANGA, ARUSHA, MANYARA NA KILIMANJARO KUHUSU KANUNI MPYA ZA EWURA

DC SHINYANGA AWEKA JIWE LA MSINGI NA KUENDESHA HARAMBEE UJENZI WA BWALO LA CHAKULA SHULE YA LITTLE TREASURES

0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Jumamosi Septemba 30,2017 ameweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.

Mbali ya kuweka jiwe la msingi pia ameendesha harambee kwa ajili ya kupata shilingi milioni 200 kwa ajili kukamilisha ujenzi huo,ambapo wazazi na walezi wameshiriki katika harambee hiyo. 

Akizungumza katika shule hiyo,Matiro aliwapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi kwa kujitoa kwa hali na mali kusaidia shule hiyo ambayo imejizolea sifa lukuki kwa utoaji wa elimu bora. 

“Shule hii imejizolea sifa nzuri,hii ni miongoni mwa shule bora kabisa nchini,kila mzazi anapenda mtoto wake asome kwenye shule nzuri,ukifika Shinyanga ukauliza shule gani nzuri,utatajiwa shule hii,nimeambiwa siri ya mafanikio haya inatokana na maono na utayari wa wazazi na marafiki kuisaidia shule hii”,alifafanua Matiro. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (wa pili kulia) akiwasili katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School”.-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School”. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisoma maandishi baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures. 
Maandishi yakisomeka kwa lugha ya Kiingereza yakiwa na maana ya 'Jiwe la Msingi limewekwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro leo Septemba 30,2017'. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures. 

KATIBU MKUU MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO BIBI SIHABA NKINGA AFUNGUA KONGAMANO LA WAZEE MJINI DODOMA


NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, RAMO MAKANI AFUNGUA KONGAMANO LA MAONESHO YA UTALII YA KARIBU KUSINI.

0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani, amefungua kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa.

Kongamano hilo limefanyika kwa muda wa siku moja katika Ukumbi wa Chuo cha Walimu wa Kleruu likiwakutanisha wasomi na wahadhiri kutoka vyuo vikuu nchini, wanafunzi pamoja na wadau wa utalii wanaofanya shughuli za kiutalii likiwa na lengo la kutathmini na kuangalia namna mikoa ya Nyanda za Juu Kusini inavyoweza kunufaika kutokana na utajiri wa vivutio vya utalii vilivyopo.

Sambamba na kongamano hilo, maonesho hayo yanaendelea kufanyika hadi Oktoba 2 katika viwanja katika viwanja vya Kichangani yakiwa yamewakutanisha Wajasiriamali wadogo 350 kutoka kona zote za mikoa hiyo.Akizindua Kongamano hilo Naibu Waziri Makani amewataka wananchi kuanza kuutupia macho utalii wa nje ya hifadhi kwa kuwa watalii wengi kwa sasa hawaji kuangalii wanyamapori pekee.
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Walimu cha Kleruu wakifuatilia maada inayowasilishwa kuhusiana na Mradi wa SPANEST jinsi inavyoshirikisha wananchi katika masuala ya uhifadhi mara baada ya kufunguliwa kwa kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani, (katikati) wa pili kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Jamhuri David, wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mara baada ya kufungua kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa. (Picha na Lusungu Helela- MNRT)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani, (katikati) wa pili kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Jamhuri David, wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiwa kwenye picha ya pamoja na Sekretarieti ya Waandaji wa kongamano mara baada ya kufungua kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa (Picha na Lusungu Helela- MNRT).


RATIBA YA MAZISHI YA MTANGAZAJI WA E-FM RADIO DENNIS RUPIA

TANZIA:MTANGAZAJI WA E-FM AFARIKI DUNIA

0
0

"Uongozi na Wafanyakazi wa E-FM,TV-E kwa majonzi na masikitiko makubwa tunatangaza kuondokewa na Mwanafamilia Mwenzetu Dennis Rupia (Chogo),aliyefarika Dunia baada ya kuugua kwa kipindi cha muda mfupi.

Aidha kwa taarifa zaidi tataendelea kufahamishana taratibu za kumpumzisha mpendwa wetu kupitia vyanzo mbalimbali vya mawasiliano.

Hakika ni kipingi Kigumu kwetu,Wasikilizaji wa Redio na familia kwa ujumla tuendelee kuombea Mpendwa wetu" ,E-FM.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OCTOBA 1,2017

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI YALIVYOFANA MKOANI SHINYANGA

0
0
.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee mkoa wa Shinyanga, Faustine Masale Sengerema,kushoto ni Katibu mkuu wa Baraza la Ushauri la Wazee mkoa wa Shinyanga,Underson Lyimo. 
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee mkoa wa Shinyanga, Faustine Masale Sengerema akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wazee ambapo alisema wazee wanaunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Wazee wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea....
Katibu mkuu wa Baraza la Ushauri la Wazee mkoa wa Shinyanga,Underson Lyimo akisoma risala ambapo alizipongeza halmashauri zilizofanikisha zoezi la kutoa kadi za matibabu bila malipo kwa wazee zikiongozwa na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Aliyeshikilia kipaza sauti ni Afisa Maendeleo ya Jamii Sekretarieti ya mkoa wa Shinyanga Glory Mbia.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi kadi ya matibabu bila malipo kwa mzee Philipo Njabuga.

DC HAPI ATEMBELEA KITUO CHA MABASI MAKUMBUSHO NA KUKUTANA NA MAMBO HAYA.....

Taasisi ya Trademark East Africa, imepongezwa kwa kuiwezesha Tanzania yapongezwa

0
0
Taasisi ya Trademark East Africa, imepongezwa kwa kuiwezesha Tanzania, kuwa ndio nchi inayoongoza nchi zote za Afrika ya Mashariki, kwa matumizi ya mifumo ya malipo kwa njia ya Mtandao, kulipia huduma mbalimbali za kibiashara, hivyo kupunguza gharama za kufanya biashara na wakati huo, kuifanya Tanzania kuwa ni nchi ya mfano wa kuingwa na nchi nyingine za Afrika ya Mashariki, katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara. 
 Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Mhandisi Raymond Mbilinyi, ambaye amesema kupitia ufadhili wa TradeMark East Africa (TMEA), kwa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Tanzania, TCCIA, na kile cha Zanzibar, (ZNCCIA) kumeifanya Tanzania kuwa ndio nchi ya kwanza kunufaika na kufaidika na mfumo madhubuti na wa kisasa wa usajili vyeti vya uhalisia (certificate of orgin) na kuripoti vikwazo vya kibiashara kwa kutumia simu za mkononi, wakati wa halfa ya uzinduzi wa Mfumo wa Malipo, kwa njia ya Mtandao kwa TCCAI ujulikanao kwa jina la LIPA FASTA, uliofanyika jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanya biashara zaidi ya 200. 
 Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa TMEA, Tawi la Tanzania, John Ulanga amesema, "Sisi kama TMEA tuna furaha kubwa kusaidia mfumo huu wa LIPA FASTA kufanya kazi kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania, hivyo kukuza biashara na kuleta ufanisi wa biashara kwa Tanzania. Ulanga amesema TMEA imetumia zaidi ya Dola za Marekani, $ 600,000 katika kufanikisha mradi huu kwa kwa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Tanzania, TCCIA, lakini pia unahusisha Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Zanzibar, (ZNCCIA), F
fedha za kugharimia mpango huu, zimetolewa na Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo la kimataifa, (DFID) kupitia TradeMark, East Africa, (TMEA) inayosimamia utekelezaji wa mradi huo. Ulanga amesema maboresha ya biashara, yanafungua zaidi fursa za Watanzania kufanya biashara, kilichobaki ni kwa Watanzania kuchangamkia fursa hizo, kwa hoja kuwa fursa hazingoji mtu, tukishindwa kuzichangamkia fursa hizi, zitachangamkiwa na wengine. 
Kwa upande wake, Rais wa TCCIA Ndibalema Mayanja amesema "Tunaishukuru sana TMEA kwa misaada wa kugharimia mfumo huu, muhimu ambao utaokoa muda na kupunguza gharama, kwani muda ni mali muhimu sana kwa mfanyabiashara yoyote, ukiokoa muda, umeokoa fedha na umeongeza faida”, hivyo LIPA FASTA itaongeza kasi ya usajili wa vyetu vya uasili kuongeza kasi ya kufanya biashara.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la  Biashara (TNBC) Mhandisi Raymond Mbilinyi, (wa tatu kulia) akibonyeza kitufe kuzindua Mfumo wa malipo kwa mtandao, kutumia simu za mkononi Kulipia huduma za TCCIA  ujulikanao kwa jina la LIPA FASTA, katika hafla ya uzinduzi mfumo huo iliyofanyika jiji Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mfumo huo umefadhili wa na  TradeMark East Africa (TMEA), kwa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Tanzania, TCCIA. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa TMEA, Tawi la Tanzania, John Ulanga (wa pili kulia) na Makamo rais wa TCCAI, Joseph Kahungwa (kulia)
Mkurugenzi wa TMEA, Tawi la Tanzania, John Ulanga (katikati) akiteta jambo na Rais wa TCCIA Ndibalema Mayanja  (kushoto), wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa malipo kwa mtandao, kutumia simu za mkononi kulipia huduma za vyeti vya uhalisia, vinavyotolewa na TCCIA  ujulikanao kwa jina la LIPA FASTA, katika hafla ya uzinduzi mfumo huo iliyofanyika jiji Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mfumo huo umefadhili wa na  TradeMark East Africa (TMEA),  kulia ni Makamo rais wa TCCAI, Joseph Kahungwa (kulia).
Mkurugenzi wa TMEA, Tawi la Tanzania, John Ulanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa malipo kwa mtandao, kutumia simu za mkononi kulipia huduma za vyeti vya uhalisia, vinavyotolewa na TCCIA  ujulikanao kwa jina la LIPA FASTA, katika hafla ya uzinduzi mfumo huo iliyofanyika jiji Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mfumo huo umefadhili wa na  TradeMark East Africa
Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki  uzinduzi wa Mfumo wa malipo kwa mtandao, kutumia simu za mkononi kulipia huduma za vyeti vya uhalisia, vinavyotolewa na TCCIA  ujulikanao kwa jina la LIPA FASTA, katika hafla ya uzinduzi mfumo huo iliyofanyika jiji Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mfumo huo umefadhili wa na  TradeMark East Africa 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la  Biashara (TNBC) Mhandisi Raymond Mbilinyi, (katikati) kwenye picha ya pamoja na viongozi wa wafanyabiashara, baada ya  kuzindua Mfumo wa malipo kwa mtandao, kutumia simu za mkononi Kulipia huduma za TCCIA  ujulikanao kwa jina la LIPA FASTA, katika hafla ya uzinduzi mfumo huo iliyofanyika jiji Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mfumo huo umefadhili wa na  TradeMark East Africa (TMEA), kwa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Tanzania, TCCIA. 

Majaliwa afungua mkutano mkuu wa 48 wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba Viongozi wa Jumuiya na Taasisi zote za kidini nchini wahakikishe wanawapiga vita watu wote wanaopanga na kutaka kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini kwa sababu watakwamisha maenendeleo. 
Amesema Serikali inaelewa kwamba dini ni miongoni mwa vyanzo muhimu vya maendeleo ya ustaarabu wa mwanadamu kwani inatoa elimu ya maadili mema yenye kuwafanya waumini waepukane na maovu mbalimbali. 
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumapili Oktoka 01, 2017) wakati akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa 48 wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya uliofanyika katika eneo la Kitonga kata ya Msongola wilayani Ilala, Dar es Salaam. 
Amesema kila Mtanzania anatakiwa ahakikishe anadhibiti matukio yote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani kwa kutoa taarifa katika mamlaka husika.”Tanzania ni nchi salama na yenye utulivu, hivyo ni lazima wote tushirikiane kuitunza.” 
 “Napenda niwahakikishieni kuwa Serikali inaunga mkono juhudi za Jumuiya za kidini katika kupiga vita maovu ya kila aina; mathalan utumiaji wa dawa za kulevya, wizi, rushwa, uzinzi ambao husababisha madhara mengi ukiwemo ugonjwa wa UKIMWI.”  
Amesema iwapo dini zetu zitatumika vizuri tutaweza kwa haraka sana kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli  la 'Hapa kazi tu' kwani kila mtu ataepuka uzembe na kuwajibika ipasavyo. 
Waziri Mkuu amesema ana imani kwamba jumuiya hiyo kama zilivyo taasisi zingine za kidini itaendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii yetu kwa kuwapatia waumini wao na wananchi kwa ujumla elimu na maarifa ya kuboresha tabia zao na maadili yao kiroho. 
Amesema amani na utulivu uliopo nchini unatokana na mambo mengi ikiwemo na wananchi kupata ustawi, kuweza kufanya shughuli zao vizuri na kuwa na imani na Serikali yao, ambayo imejiwekea mikakati ya kuhakikisha wananchi hususan wanyonge wanapata faraja ndani ya nchi yao.  
Waziri Mkuu amesema mambo yameweza kupatikana baada ya Serikali kupambana na rushwa na ufisadi pamoja na kuimarisha maadili ya watumishi wa umma, ambayo vimekuwa ni vyanzo vya kupotea kwa amani na utulivu katika baadhi ya nchi.“Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kupambana na ufisadi, kupitia mikataba mibovu na kuimarisha maadili ili kujenga imani kwa wananchi, kuondoa migongano na tofauti ya kipato, kuwa na matumizi mazuri ya rasilimali za umma, kuleta tija kwa kuongeza thamani ya huduma na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.”Awali, Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry  amesema Jumuiya hiyo imekuwa ikifanya mikutano kila mwaka kwa lengo la kukumbushana misingi sahihi ya dini tukufu ya kiislam pamoja na kukuza undugu wao.Sheikh Chaudhry amesema mkutano wa mwaka huu umejumisha watu zaidi ya 4,000 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wageni kutoka nchi za Uingereza, Canada, Rwanda, Uganda, Ujerumani, Kenya, Burundi, Malawi na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).Amesema Jumuiya hiyo mbali na masuala ya kidini pia inatoa huduma mbalimbali za kijamii kama elimu, maji na afya kwenye mikoa tofauti tofauti nchini.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na kiongozi na mbashiri mkuu wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania,Tahir Mahmood, kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa jumuiya hiyo Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam leo Oktoba 1, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waumini wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania, kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa Jumuiya hiyo huko Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam leo Oktoba 1, 2017 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waumini wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania, kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa Jumuiya hiyo huko Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam leo Oktoba 1, 2017 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kitabu kutoka kwa Katibu wa Malezi Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania, Mahmood Hamsin, baada ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa jumuiya hiyo Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017. Kulia ni kiongozi na mbashiri mkuu wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania,Tahir Mahmood. (Habari na Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TANZANIA HAINA BUDI KUTUMIA MIFUMO YA KIDIGTALI KUJITANGAZA KIMATAIFA

0
0
Wakati dunia ikisherehekea siku ya Utalii Duniani, Jumia Travel imebainisha kwamba matumizi ya tekinolojia za kisasa hususani mtandao wa intaneti una manufaa makubwa katika kuvitangaza vivutio vya kitalii kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea nchini Tanzania, Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Umma wa Jumia Travel Kimataifa, Bw. Abdesslam Benzitouni ameweka wazi kwamba Tanzania haina budi kutumia ipasavyo njia zote za kidigitali ikiwemo mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Youtube na Instagram kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watumiaji. 

“Intaneti imekuwa na mchango mkubwa kwenye sekta ya utalii na ukarimu hususani kwenye kutoa taarifa. Tofauti na kipindi cha nyuma hivi sasa watu wanaweza kupata taarifa muda wowote na mahali popote walipo bila ya kutembelea moja kwa moja eneo husika.

 Jumia Travel inazitumia njia zote za mtandaoni kuzionyesha na kuzitangaza hoteli pamoja na vivutio vya kitalii nchini. Tovuti na kurasa za mitandao yetu ya kijamii tuzipatia hoteli tunazoshirikiana nazo fursa kubwa ya kujitangaza na kuonekana mtandaoni ambapo kwa kiasi kikubwa huongeza idadi ya wateja,” alisema Benzitouni. 
“Wakati dunia ikisherehekea siku ya Utalii Duniani, bara la Afrika limeshuhudia idadi ya watalii kufikia milioni 58 mwaka 2016. Na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka maradufu ndani ya miaka 15 ijayo na kufikia milioni 130. Mafanikio hayo yamechangiwa na ukuaji wa kasi wa sekta ya usafiri wa anga, ambapo mashirika ya ndani na kimataifa yana mchango mkubwa kwenye kuwasafirisha watalii ndani na nje ya nchi, ” aliongezea Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Umma wa Jumia Travel Kimataifa.
Aliendelea na kufafanua zaidi kwamba kwa Tanzania kutajwa kuwa ni miongoni mwa nchi ambazo zinatembelewa zaidi barani Afrika, sawa na nchi zingine kama vile Morocco, South Africa, Rwanda na Namibia, ni dalili nzuri kwamba utalii unaleta tija kubwa na inaweza kunufaika nao kwa kutumia mbinu tofauti ili kuvutia wageni wa kimataifa zaidi.

“Kupitia ripoti ya Utalii na Ukarimu ambayo Jumia Travel tuliiwasilisha mapema mwaka huu, tuligundua kwamba idadi ya watalii kwa mwaka 2016 iliongezeka kwa 16%. Pia kuongezeka kwa idadi ya watanzania wanaotumia mtandao wa intaneti kunaashiria matumizi ya mifumo mipya ya kidigitali. 
Tunaweza kuitumia katika kuvitangaza vivutio vyetu, kutoa taarifa za kutosha zaidi, pamoja na bei nzuri na zenye ushindani kwenye soko ili kurahisisha shughuli za kitalii. Tafiti zinaonyesha idadi kubwa ya watalii wanaotembelea Afrika wanatokea nchi za bara la Asia zaidi. Kwa mfano, 10% ya Wachina wanaosafiri duniani hutembelea zaidi nchi za Afrika,” alihitimisha Benzitouni.

Kati ya mambo ya msingi ambayo Jumia Travel inajitahidi kuyaangazia kwenye sekta ya utalii na ukarimu nchini Tanzania pamoja na kwingineko ilipo Afrika ni gharama za juu za malazi. Kwa waafrika wengi, malazi yamekuwa ni kati ya changamoto kuu inayokwamisha shughuli za kitalii kwa miaka kadhaa sasa. 
Kulipatia ufumbuzi hilo kampuni hiyo imejizatiti kuhakikisha kwamba inaweka aina zote za malazi kwenye mtandao wao ili yafikiwa kwa urahisi na wateja. Lengo kuu ni kumuwezesha kila mtu aweze kupata huduma ya malazi kwa gharama nafuu licha ya uwezo alionao.

MAHAKAMA YAAMURU MSHITAKIWA HARBINDER SETHI AKATIBIWE HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI NDANI YA SIKU 14

0
0
Harbinder Sethi
Na Dotto Mwaibale

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kwa mara nyingine mshtakiwa Harbinder Sethi akatibiwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ndani ya siku 14.

Korti imesema iwapo hilo halitatekelezwa, mkuu wa gereza afike mahakamani kujieleza. Sethi yupo mahabusu katika Gereza la Segerea.

Amri hiyo ya mahakama imetolewa baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kudai kesi ilipangwa leo Ijumaa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika, hivyo aliomba shauri lipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa.

Baada ya maelezo hayo, wakili Joseph Makandege anayemwakilisha Sethi alieleza kuwa kumekuwepo mfululizo wa amri za Mahakama zikiagiza mteja wake akapatiwe matibabu na kufanyiwa uchunguzi Muhimbili.

“Hadi leo asubuhi tuliwasiliana na mteja wetu na kubaini hajapelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kama amri za Mahakama zilivyoagiza, hivyo ni rai yetu kwamba kitendo hicho cha kutotekelezwa amri za Mahakama ni ukaidi wa amri halali za Mahakama yako tukufu,” amesema Makandege.

Alisema kwa kuwa upande wa mashtaka umekaidi amri za Mahakama, anaomba itoe adhabu inayostahili.Makandege alisema kitendo cha upande wa mashtaka cha kutotekeleza amri za Mahakama kinasigana na kukiuka mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Mashtaka .

Rais Nkurunziza avutiwa na ubora wa bidhaa za Tanzania

0
0
RAIS wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza ametembelea maonyesho ya kwanza ya biashara ya Tanzania nchini hapa yanayolenga kuangalia soko pana la bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali kutoka Tanzania na kusifu ubora wa bidhaa hizo. 
Maonyesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Tempete vilivyopo jijini Bujumbura, yalianza Septemba 28 mwaka huu na yamekamilika leo Oktoba 1, mwaka huu yameandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa lengo la kuongeza fursa za kibiashara katika nchi za ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati. 
“Hii ni ishara ya kukomaa kwa udugu kati ya Tanzania na Burundi, wananchi wa Burundi walikuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata bidhaa hadi Dar es Salaam, lakini sasa wameletewa mlangoni. 
"Kwa muda mrefu tumekuwa tukifurahia bidhaa aina hii lakini bei zilikua kubwa kutokana na gharama za usafiri, kwa sasa mambo yamekua mazuri,” alisema Rais Nkurunziza. 
Rais Nkurunziza aliongeza kuwa: “Uhusiano wetu unazidi kuimarika, naaminiile dhana ya utangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inatekelezwa kivitendo. Naahidi kuunga mkono juhudi zote za kuimarika kiuchumi kati ya nchi mbili hizi.” 
Aidha, ubalozi wa Tanzania nchini Burundi kwa kiasi kikubwa umeshiriki kufanikisha maonyesho haya chini ya Balozi Rajabu Gamaha ambaye ndiye aliyewashawishi maofisa wa TanTrade kuwa na maonyesho aina hii kutokana na maombi ya kupata bidhaa kutoka Tanzania kuwa mengi ofisini kwake. 
Awali katika hotuba yake ya ufunguzi Septemba 27 mwaka huu, Makamu wa Pili wa Rais nchini hapa, Dkt. Joseph Bitore alisema biashara ni kitu kinachounganisha mataifa mawili kiuchumi hivyo watachukulia maonyesho hayo kujifunza lakini pia kutanua wigo wa mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na Burundi. 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TanTrade, Mhandisi Christopher Chiza alisema, uamuzi wa kupeleka bidhaa Burundi ulipofika mezani kwake hakutaka kusita kwa sababu alijua hiyo ni njia pekee ya kufikisha mbali bidhaa za kitanzania. 
“Tunapofanikiwa kufika Burundi maana yake tunalenga soko pana la ukanda huu, tunatarajia kufikia soko la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa sababu hata wao tumearifiwa kuwa wananunua bidhaa kutoka Burundi. “Kwa muda mrefu kama alivyoeleza mheshimiwa Rais Nkurunziza, wajasiriamali kutoka Burundi wamekuwa wakifuata bidhaa za vyakula hasa nafaka na mavazi kutoka pembezoni mwa mikoa ya Tanzania, lakini na wao walikuwa wakipeleka bidhaa hizo Mashariki ya Kongo. Hivyo tunalenga soko pana la takriban watu milioni 20, si jambo dogo.” 
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bwana Edwin Rutageruka aliahidi kuendeleza biashara kati ya Tanzania na Burundi hata baada ya kumalizika kwa maonyesho hayo ya siku nne: “Huu ni mwanzo, tayari wafanyabiashara tulioongozana nao wamechukua mawasiliano ya wateja wao na watawauliza wanahitaji nini ili baadaye walete.” Kwa muda mrefu sasa TanTrade wamekuwa katika harakati za kuondoa dhana kuwa maonyesho ya biashara yanafanyika jijini Dar es Salaam tu, hivyo wametanua mipaka ambapo wiki kadhaa zilizopita yalifanyika maoneyesho makubwa ya kibiashara mkoani Kigoma na bado maonyesho mengine yanaandaliwa katika mikoa ya pembezoni ili kuwafikia watanzania wengi zaidi.
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi akiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Mhandisi Chistopher Chiza, Balozi wa Tanzania nchini Burundi Rajabu Gamaha pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TanTrade, Edwin Rutageruka kuelekea kwenye banda la Tanzania katika maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Tempete jijini Bujumbura mwisho mwa wiki.
 Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi akipatiwa maelezo kuhusu bidhaa za Tanzania kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu TanTrade, Edwin Rutageruka alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Tempete jijini Bujumbura mwisho mwa wiki.
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi akifurahia jambo kuhusu bidhaa za Tanzania alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Tempete jijini Bujumbura mwisho mwa wiki.

Vodacom yatoa mafunzo ya upatikanaji wa masomo kwenye simu za kinganjani na kompyuta mlandizi

0
0
 Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, Sozi Ngate,(Wapili kulia) akipokea msaada wa kompyuta kati ya 20 toka kwa Mkurugenzi wa Bridge for change,Ocheck Msuva na Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea shule za sekondari ya Kilangala na Miembe Saba,kwaajili ya kuwashauri  juu ya  mafunzo ya upatikanaji wa masomo kwenye simu za kinganjani na kompyuta(Free Digital Learning) na kutoa msaada wa komyuta kwa kushirikiana na Taasisi ya Bridge for change katika shule hizo mwishoni mwa wiki,Anaeshuhudia kulia ni Mkuu wa shule ya Kilangalanga,Albert Mabiki.
Ofisa Mtambo Tanakilishi wa Vodacom Tanzania PLC, Robert German akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Sekondari ya Kilangalanga iliyopo Mlandizi mkoa wa Pwani wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea shule za sekondari ya Kilangalanga na Miembe Saba,kwa ajili ya kuwashauri  kwa  juu ya mafunzo ya upatikanaji wa masomo kwenye simu za kinganjani na kompyuta(Free Digital Learning) na kutoa msaada wa kompyuta 20  kwa kushirikiana na Taasisi ya Bridge for change katika shule hizo mwishoni mwa wiki.
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live




Latest Images