Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1935 | 1936 | (Page 1937) | 1938 | 1939 | .... | 3284 | newer

  0 0

  These are: Schneider Electric East Africa, the Schneider Electric Foundation, ADEI, EDF Help and the Foundation for Technical Education (FTE). Speaking during the event, KIITEC Director of studies, Mr. Daniel Mtana, said the opening of this solar power plant speaks to the accomplishment of institute’s vision to become the centre of training excellence for renewable energy, particularly solar photovoltaic systems in East Africa. 

  “Committed to true hands-on experience, KIITEC has now invested heavily in photovoltaic solutions and strives to be recognized as the premier provider of quality technical education in a student-centered community.” General manager at Schneider Electric East Africa, Mr. Mr. Edouard Heripret, said in most sub-Saharan countries, the rate of enrolment in formal secondary technical and vocational training and education (TVET) does not exceed 5%. 

  “Vocational training has always been at the heart of Schneider Electric’s DNA. In East Africa, we have been committed to support technical training since 2009. Kiitec was one of our first training partners and I am pleased today to participate in the inauguration of the solar plant and laboratory, as these new components will allow students to have a full set of competencies to enter the labour market and will support access to energy for everyone.” Mr. 
  Excellency Malika Berak, Ambassador of France in Tanzania (C) cuts a ribbon to officiate the launch of Solar Power plant and laboratory at KIITEC in Arusha, others in photo are senior officials from the partners institutions supporting the Institute. 
  FTE President Fransis Bronchon,(R) briefing invited guests on Solar Project at KITEEK during the launch event at Arusha. 
  Excellency Malika Berak, Ambassador of France in Tanzania(C) got briefing on project from, Albert Mtana, (R)-Teacher of Electrical and Solar Photovoltaic System (L) is Michel Ramser-VP Strategic Marketing and Sponsorship (ADEI). 
  Solar panel installed at the centre. The Kilimanjaro International Institute for Telecommunications, Electronics and Computers (KIITEC) has launched 30KW solar power plant and solar laboratory at its training centre in Arusha recently. The Guest of Honour at launch event was Her Excellency Malika Berak, Ambassador of France in Tanzania, also the event brought together the partners that have supported KIITEC for many years.   0 0

  Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya imekamilisha ujenzi wa Makumbusho mapya ya Olduvai ambayo yanaonesha Chimbuko la Binadamu (The Cradle of Humankind) katika Bara la Afrika.

  Makumbusho hayo mapya pamoja na Onesho la Chimbuko la Binadamu, yatafunguliwa rasmi na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tarehe 03 Oktoba, 2017 katika eneo la Olduvai, ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

  Onesho hilo ni matokeo ya utafiti wa muda mrefu uliofanyika katika Bonde la Olduvai na Laetoli katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. Wananchi, viongozi mbalimbali wa kitaifa na Mabalozi wanatarajiwa kuhudhuria kwenye hafla hiyo.

  Idadi kubwa ya vioneshwa katika Makumbusho hiyo, vilipatikana katika bonde la Olduvai na Laetoli nchini Tanzania kupitia utafiti wa kisayansi wa muda mrefu na vilikuwa vimehifadhiwa katika Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam. Vioneshwa hivi ni pamoja na masalia ya zamadamu, zana za mawe na masalia ya wanyama walioishi takribani miaka milioni 4 iliyopita.

  Makumbusho hayo yamepangwa kuonesha sehemu kuu nne zinazowiana.  Sehemu ya kwanza inahusu ushahidi wa nyayo za zamadamu zilizongunduliwa huko Laetoli mwaka 1978 na mtafiti Dr. Mary D. Leakey.  Nyayo hizi ziliachwa na zamadamu anayeiitwa Australopithecus afarensis na ndio ushaidi usiopingika wa zamadamu kutembea wima kwa miguu miwili takribani miaka milioni 3.6 iliyopita.
  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani Morogoro kuhusu uzinduzi wa Makumbusho Mapya ya Olduvai na Onesho la Chimbuko la Mwanadamu ambayo yatazinduliwa tarehe 03 Oktoba, 2017 na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Olduvai wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. 


   Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani Morogoro kuhusu uzinduzi wa Makumbusho Mapya ya Olduvai na Onesho la Chimbuko la Mwanadamu ambayo yatazinduliwa tarehe 03 Oktoba, 2017 na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Olduvai wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. (Picha na Hamza Temba - WMU)

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wapili kulia), akimkabidhi Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro (katikati), mchoro wa ramani ya nyumba za Polisi za kisasa zitakazojengwa kufuatia za awali kuteketea kwa moto. Hatua ya ujenzi imeanza mara moja kufuatia Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, kutoa kiasi cha shilingi milioni 260 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Hanspaul, Kamaljit Singh, na kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (DCP) Charles Mkumbo na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Wakala ya Majengo Arusha Bw. Victor
  Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akiagana na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, alipomtembelea ofisini leo tayari kwa safari ya kurejea Dar es salaam, baada ya kuwapapole na kukagua eneo la nyumba za Polisi zilizoteketea kwa moto. Picha na Jeshi la Polisi.

  0 0


  Mshtakiwa  Harbinder Singh Sethi (mbele)akitoka katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabiri na mahakama kuamuru kuwa akatibiwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ndani ya siku 14 .
    Mshitakiwa James Rugemarila akitoka mahakamani mara baada ya kusomewa mastaka yanayomkabiri na mahakama hiyo kuauru mwenzake Seth kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
  Washtakiwa Harbinder Singh Sethi (Mbele) na James Rugemarila wakitoka mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada yamahaka hiyo kuamuru Seth akatibiwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ndani ya siku 14 na Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 13, 2017.
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii.
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kwa mara nyingine tena  mshtakiwa  Harbinder Singh Sethi akatibiwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ndani ya siku 14 ikishindikana Mkuu wa gereza la keko ambako mshtakiwa ndiko anapatikana afike mahakamani kujieleza.

  Amri hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi mkuu, Huruma Shahidi wakati kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kusisitiza kuwa amri za mahakama lazima zifuatwe.

  Hatua hiyo imekuja baada Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi kudai kuwa kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika

  Baada ya taarifa hiyo, wakili wa utetezi wa Sethi, Joseph Makandege ameieleza mahakama kuwa “licha ya kuwepo kwa amri mfululizo zilizotolewa na mahakama juu ya kutibiwa kwa mshtakiwa Seth katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, mpaka leo  asubuhi tumewasiliana na Sethina ametueleza kuwa, hajapelekwa Muhimbili.

  Amedai , kitendo hicho cha kutokutekelezwa kwa amri za mahakama ni ukaidi na kuiomba mahakama itoe adhabu inayostahili kwani wanasigina sheria na kukiuka mamlaka aliyopewa DPP kwani yeye ndio anatakiwa kuongozwa na haja ya kutenda Haki kwani lengo ni kutogeuza mashtaka ya jinai na mahakama kwa nini vyombo vya utesaji.

  Alidai kuwa, mashtaka yaliyopo ni mashtaka ya hila ambayo yana lengo la kuupa upande wa mashtaka fursa ya kuwaadhibu washtakiwa hasa mshtakiwa wa kwanza Sethi kabla hawajahukumiwa.

  Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kumzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),Leonard Swai amedai magereza wamekuwa wakiwatibu wafungwa na mahabusu hata pasipokuwa  na amri ya Mahakama, magereza wapo katika hatua za mwisho, kukamilisha utaratibu wa kumpeleka Sethi Muhimbili.

  Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 13, mwaka huu(2017)
  Katika kesi hiyo, Sethi na James Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka  mbali mbali ya uhujumu uchumi na utakatishaji USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

  0 0

   Mkurugenzi wa Tathmini, Archard Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50) wakitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
  Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

  UPANDE wa Mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni mbili, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Tathmini, Archard Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50) umeieleza mahakama kuwa, sehemu kubwa ya upeleleIezi dhidi ya kesi hiyo umekamilika.

  Aidha wamedai kuwa wako kwenye majadiliano kuona kama wataongeza washtakiwa wengine au la.

  Wakili wa serikali, Paul Kadushi ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage. Wakati shauri hilo lilipokuja kwa kutajwa na kudai kuwa upelelezi  bado bado haujakamilika.

  Aidha upande wa utetzi umeiomba mahakama tarehe itakayofuata upande wa mashtaka uje ueleze hatua ya upelelezi ilipofikia.

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Octoba 12 mwaka huu.
  Katika kesi hiyo, Kalugendo ambaye ni Mkazi wa Kinyerezi na Rweyemamu anayeishi Mwananyamala ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na  Madini wanadaiwa  kati ya Agosti 25 na ,31, mwaka huu, katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga washtakiwa

  wakiwa wathamini walioajiliwa na Wizara ya Nishati na Madini waliisababishia serikali ya hasara ya USD 1,118,291.43 Ambayo no sawa na 2,486,396,982.54.

  0 0


  0 0

  Wadau wa habari nchini wameomba kupata taarifa iwe ni haki ya kila mtu ambayo inapaswa kulindwa kwa nguvu  zote na ni kiashiria kimoja wapo cha serikali yenye uwazi na inayothamini mchango na ushiriki wa wananchi wake katika ujenzi wa taifa.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti, katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upatikanaji wa habari yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, wamesema kila mtu ana haki ya kupokea na kutoa taarifa ili mradi tu asiende nje ya swala husika.
  Wamesema kuwa, lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya haki ya kila mtu na kupata taarifa muhimu kwa Maisha yao ikiwa ndani ya hifadhi ya Serikali na kwingineko, namna viongozi waliyochaguliwa na wanavyotekeleza majukumu yao.

  Katika maadhimisho hayo MISA-TAN walikabidhi tuzo kwa taasisi mbali mbali za umma zinazotoa taarifa kwa uwazi na zile zinazobana taarifa. Kwa mwaka 2017, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeibuka mshindi wa kwanza kwa utoaji na upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma na taasisi iliyokuwa mshindi wa mwisho ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) baada ya kubainika kuwa inabana taarifa.  Kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Kila Mtanzania Anayo Haki Ya Kupewa Taarifa."
  Kaimu Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania. Bi. Lianne Houben akizungumzia jinsi ubalozi unavyofanya kazi na taasisi za habari hapa nchini ili kuweza kufanikisha upatikanaji wa habari kwa wananchi nchini Tanzania.
  Wageni waalikwa wakisimama kwa kuwakumbuka waandishi waliyopoteza maisha katika maadhimisho ya kwanza Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa yaliyofanyika leo Dar es Salaam, Tanzania.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI), Kajubi Mukajanga akiakitoa utangulizi kuhusu upatikanaji wa taarifa kwa wananchi nchini Tanzania kwenye siku ya maadhimisho ya kimataifa ya upatikanaji wa taarifa leo jijini Dar es Salaam. 
  Baadhi ya wadau mbalimbali wachangia mada kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upatikanaji wa habari.
  KWA PICHA ZAIDI BODYA HAPA.

  0 0

  NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

  MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na ugeni kutoka Jiji la Shanghai nchini China na kujadili mambo mbalimbali yamaendeleo jijini hapa ikiwemo suala la uboreshaji wa kituo cha Mabasi Ubungo.

  Ugeni huo uliambatana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Linghang Cathy Wang ambayo ndiyo imeingia mkataba na Halmashauri ya jiji kwa ujenzi wa kituo hicho.Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo, Meya Mwita alisema kuwa ugeni huo umeridhia kuwekeza katika nyanja mbalimbali ikiwemo kituo cha mabasi ubungo.

  Alifafanua kuwa jiji la Dar es Salaam linakaribia kunza kwa ujenzi wa mradi mkubwa wa kubadilisha kituo cha mabasi ubungo na kwamba hatua mbalimbli zimeshakamilika ili kupisha mradai huo.Alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa mradi huo jumla ya watanzania 20,000 watapata ajira jambo ambalo litawezesha kuongeza kipato kwa wananchi na hivyo pia kuwezesha vijana kuondokana kwenye makundi ambayo sio salama.

  Alisema kufanikisha kwa mradi huo, utasaidia pia kuongeza mzunguko wa fedha jijini hapa kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za kibiashara.“ Leo nimekutana na ugeni ambapo kwa kiasi kikubwa mnafahamu ndugu zetu hawa wamekuwa na urafiki mkubwa katika nchini yetu, tumejadiliana mambo mengi ambayo yote ni yakuleta maendeleo katika jiji letu.

  “ Lakini kubwa zaidi ni kuhusu ujenzi wa kituo cha mabasi Ubungo, ambapo hivi karibuni tunatarajia kuanza kwa mradi huo, na wananchi pia watajulisha, nitumie fursa hii kuwaeleza wananchi kuwa jiji linafuata utaratibu katika kutekeleza mradi huo” alisema Meya Mwita.


  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa BBC, Idhaa ya Kiswahili kwa upande wa Tanzania, Bw. John Solombi leo katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje. Timu ya BBC imeanza ziara kuwatembelea wadau wake wakubwa katika masuala ya kupashana habari na wameanza kwa kuitembelea Wizara ya Mambo ya Nje na baadaye walielekea kwa msemaji wa Jeshi la Polisi nchini. Katika mazungumzo hayo, wawili hao walikubaliana kufanya kazi kwa karibu kwa maslahi ya kuuelimisha na kuuhabarisha umma. 
  Bw. Solombi akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo. 
  Mazungumzo yanaendelea. Katika picha anaonekana Bw. Aboubkar Famau, Mtangazaji wa BBC na Mkuu wa Kitengo cha Uratibu wa Vipindi, akichangia jambo katika mazungumzo hayo. Kulia kwake ni Bw. Ally Kondo, Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya Nje na aliyekaa peke yake ni Bi. Halima Nyanza, Mtangazaji wa BBC. 
  Picha ya pamoja 
  Timu ya BBC baada ya kukutana na Kitengo cha Mawasiliano ilipata fursa ya kusalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba (Mb). Pichani anaoenekana Mhe. Naibu Waziri akiwapa neno la shukrani Team ya BBC kwa uamuzi wao wa kuichagua Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuwa mdau wa kwanza kutembelewa.
  Mhe. Naibu Waziri akiwa katika picha ya pamoja na Team ya BBC na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali cha Wizara ya Mambo ya Nje 

  0 0

  Mpenzi wa kabumbu ni lini mara ya mwisho umeangalia mpira mubashara kupitia simu yako ya mkononi? Angalia usipitwe na uhondo huo! Furahia maisha ya bila kugongea kwa jirani ukiwa na kifurushi cha #VodacomREDRLX kinachokupatia MB za kutosha. Kujiunga piga *149*01# chagua RED.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
  Serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania leo imezindua kituo kipya cha kimarekani kitakachokuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia kakinacholenga kukuza fikra yakinifu na mijadala ya kina kuhusu masuala mbali mbali ya kuwapa wananchi haki ya kupata elimu na kupata taarifa bila kikwazo.

  Kituo hicho kitakuwa ni daraja la kuzifikia taasisi za elimu ya juu za Kimarekani, taasisi za utafiti, za kimarekani, na hata ufadhili wa masomo na kushirikisha hulka ya ubunifu na ujasiriamali kwa watanzania watakaobuni mustakabali mpya.” Tunawekeza

  Akizungumza kwenye uzinduzi wa kituo hicho, Kaimu balozi wa  Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson amesema, kituo hicho kipya kitakuwa kiunganishi cha kidijitali kati ya Tanzania na eneo la Silicon Valley (kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia)Tehama na ubunifu.

  Dk.Patterson amesema Vituo vya Kimarekani ni maeneo yaliyotengwa maalumu katika taasisi mbalimbali za nchini Tanzania “kituo hiki cha lugha ya kiingereza tunachofungua leo kitatoa uwezo wa moja kwa moja wa kujifunza lugha ya Kiingerezaa, ushauri wa elimu, na habari kuhusu fursa za elimu Marekani.

  Amesema, kituo hiko kilichopo maktaba kuu jijini hapa kitakuwa wazi kutumiwa na wananchi wote bila malipo oyote na kitakuwa wazi kwa umma kwa siku za Jumatatu hadi Ijumaa na jumamosi asubuhi hadi mchana.

  Akifungua kituo hicho, Naibu Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia mhandisi Stella Manyanya amesema, kituo hicho kitakuwa daraja la kuzifikia taasisi za elimu ya juu za kimarekani, taasisi za utafiti na ufadhili wa masomo.

  Aidha aliumba ubalozi wa marekani kusaidia kujenga vituo vingine katika mikoa mingi nchini ili kusaidia elimu kwa umma.
   Naibu waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya pamoja na Kaimu balozi wa  Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson wakikata utepe kuashiria kufunguliwa kwa kituo cha Kimarekani  kilichoanzishwa kwa kushirikiana na Ubalozi wa  Marekani nchini Tanzania pamoja na serikali ya Tanzania.
   Naibu waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya akihutuba katika uzinduzi wa kituo cha Kimarekani kilichoanzishwa kwa kushirikiana na Ubalozi wa  Marekani nchini Tanzania pamoja na serikali ya Tanzania. Kituo hicho kitakuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia kitakachowawezesha wananchi kupata elimu na taarifa bila vikwazo. 
   Kaimu balozi wa  Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson akizungumza kuhusu uzinduzi wa kituo cha Kimarekani kilichozinduliwa leo kuwa kitakuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia kitakachowawezesha wananchi kupata elimu na taarifa bila vikwazo.


  0 0

  Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
  Vijana wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wajitokeza kujiunga  na mradi wa sauti ya vijana MYICD iliyo sajiriwa  mwaka 2009, ikiwa kijana ni nguvu kazi ya Taifa ambapo  wanalenga zaidi umri kuanzia 15-35  na kauli mbiu ni kijana paza sauti.

  Katika semina hiyo ya mafunzo yaliyofanyika ofisi ya mtendaji kata ya Kilakala  kwenye halmashari ya Temeke Jijini Dar es Salaam ikiwa  dhumuni la  mafunzo hayo ni  kujua  namna ya kuunda majukwaa ya vijana kuhamasisha, ushirikiano, muongozo wa vijana katika kisiasa, kiuchumi, kijamii pamoja na kidini.

  Pia vijana hao wametakiwa kujitambua katika kupata sauti zao pamoja juu  ya haki na mahitaji yao, kwa kujikusanya na kutoa taarifa shirikishi  juu  ya fursa za kimaendeleo.

  Afisa maendeleo kata ya Kilakala, Mwajuma Msafiri amesema kuwa vijana hao wameupokea wito  huo vizuri kwa kuchangamkia fursa  hiyo na wapo bege kwa bega katika kushirikiana na vijana wenzao waishio katika mitaa mitano (5) ya kata hiyo ambayo ni Barabara ya Mwinyi, Igunga, Kilakala, Kiaembe Samaki na Yombo Dovya.

  Nae Mkurugenzi Taasisi  ya MYIDC, Ismail Mnikite amesema kuwa katika mradi huo unaohusisha kata nne  za Halmashauri ya Temeke ambazo ni Buza, Makangarawe, Tandika na Kilakala ambapo vijana wa vikundi vya  mbio za pole pole ndio waliojitokeza  kujiunga na mradi ili   kupata mafunzo yanayowajenga katika kuleta maendeleo hapa Nchini, vile vile ametoa shukrani za dhati Kwa wiongozi wa Halmashauri hiyo Kwa kuonyesha ushirikiano juu ya Swala hilo.
   Mkurugenzi Taasisi MYICD, Ismail Mnikite akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo ulisajiriwa mwaka 2009 ikiwa ni dhumuni  la  kuinua vijana katika kuwanchinimafunzo na fursa mbalimbali katika kuleta   maendeleo katika ofisi ya mtendaji kata ya kilakala  Halmashauri ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
   Afisa maendeleo kata ya Kilakala, Mwajuma Msafiri akizungumza na waandishi wa habari   kuhusu muamko wa vijana kujitokeza kujiunga na kupata mafunzo yanayotolewa mradi wa MYICD Kwa lengo la  kutaka kuleta mapinduzi  na maendeleo hapa nchini katika ofisi ya mtendaji kata ya Kilakala halmashauri ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
   Mratibu wa mradi, Kassonga Mario akitoa mafunzo kwa vijana hao katika ukumbi wa ofisi ya mtendaji kata ya Kilakala Halmashauri ya Temeke Jijini Dar es Salaam. 
  Vijana wa kata ya kilakala waliojitokeza kwenye mafunzo katika Ukumbi wa ofisi ya mtendaji kata ya Kilakala halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam yalioandaliwa na mradi wa MYICD ikiwa lengo ni kutaka kupaza sauti za vijana. Picha na Agness Francis, Blogu ya Jamii

  0 0

  Katika mechi hiyo, mgeni rasmi alikuwa ni Balozi wa Vijana Usalama Barabarani, James Mwakibinga ambapo akizungumza kabla ya mchezo huo, aliwasifia wachezaji wa Bongo Fleva na wa Kampuni ya Mawasiliano Airtel kwa kuungana pamoja na kucheza mchezo wao wa kirafiki.
  “Nawapongeza wote mliofika na kushiriki mchezo huu, ni jambo la busara kwenu kuwa wamoja na kudumisha amani ya nchi yetu.
  “Katika kuhakikisha tunaunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, katika kuendeleza umoja baina ya mtu mmojammoja na hata makampuni kama ilivyotokea leo kwa Airtel na Bongo Fleva,” alisema Mwakibinga.

   Balozi wa Vijana Usalama Barabarani, James Mwakibinga ambapo akikagua timu ya Bongo Fleva kabla ya mpambano wao na wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano Airtel katika mchezo wao wa kilafiki uliomalizika kwa sare ya 0-0 katika uwanja wa Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam
    Balozi wa Vijana Usalama Barabarani, James Mwakibinga ambapo akikagua timu ya Bongo Fleva kabla ya mpambano wao na wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano Airtel katika mchezo wao wa kilafiki uliomalizika kwa sare ya 0-0 katika uwanja wa Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam
    Balozi wa Vijana Usalama Barabarani, James Mwakibinga ambapo akikagua timu ya Kampuni ya Mawasiliano Airtel katika mchezo wao wa kilafiki uliomalizika kwa sare ya 0-0 katika uwanja wa Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam
     Balozi wa Vijana Usalama Barabarani, James Mwakibinga ambapo akikagua timu ya Kampuni ya Mawasiliano Airtel katika mchezo wao wa kilafiki uliomalizika kwa sare ya 0-0 katika uwanja wa Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam
    Balozi wa Vijana Usalama Barabarani, James Mwakibinga akifuatilia mchezo huo katika uwanja wa Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam.

  0 0


   Chama Cha Mapinduzi, kimefafanua kuhusu Katibu Mkuu wa Chama hicho, ABDULRAHMAN KINANA, kutohudhuria Kikao cha Kamati Kuu, kikisema kwamba hakuhudhuria Kikao hicho kutokana na kupata Dharura ya Kihali ya Ki-Utu. 

  Hata hivyo, kimesema kazi yote ya Maandalizi ya Kikao cha Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa-NEC, kinachoanza kesho imefanywa na KINANA. 

  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, HUMPHREY POLEPOLE, amesema Kamati Kuu katika kikao chake ilipata taarifa rasmi kupitia kwa Mwenyekiti Rais JOHN MAGUFULI kwamba Katibu Mkuu ameomba udhuru wa kihali. 

  Katika hatua nyingine, Wajumbe wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa-NEC, wameanza kuwasili jijini Dar es salaam, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba kwa ajili ya kukamilisha taratibu muhimu kabla ya kuanza kwa Vikao hivyo muhimu vya Chama.

  Kuanza kwa kikao hicho kesho kunatokana na kumalizika kwa Kikao cha Kamati Kuu ambacho kilikuwa chini ya Mwenyekiti wake, Rais JOHN MAGUFULI. 

  Pamoja na mambo mengine, POLEPOLE, amesema vikao hivyo vya maamuzi vina kazi ya kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho wa wana-CCM-wanaoomba ridhaa ya nafasi ya Uenyekiti wa CCM ngazi ya Wilaya. 

  Kikao cha NEC kitafanyika kwa siku Mbili, Jumamosi na Jumapili.


  0 0  0 0

  Serikali imepongeza juhudi zinazofanywa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) za kuboresha huduma sanjari na kuwawezesha watalaam kusoma ili wapate ujuzi zaidi na kutoa huduma bora na za kibingwa.

  Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulusubisya wakati akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo kupitia Idara ya Usingizi.

  Dk. Mpoki amesema serikali inatambua juhudi zinazofanywa na uongozi wa hospitali na kwamba hatua hiyo inaleta faraja kwa Watanzania kwani sasa wana uhakika wa kupata huduma bora .

  “Naona mabadiliko makubwa hapa Muhimbili, mmeongeza vyumba vya upasuaji, Vyumba vya wagonjwa mahutuni (ICU) na pia mnaendelea kuboresha huduma zingine kwakweli hatua hii ni ya kupongezwa na ninaomba muendelee kujituma kwani hospitali hii inategemewa kwa sababu mna watalaam wengi waliobobea hapa,’’ amesema Dk. Mpoki.

  Kuhusu kusomesha wataalam, Katibu Mkuu amesema hatua hiyo ni nzuri kwani watalaam hao watapata fursa ya kuwatawafundisha wengine ili nao wapate ujuzi .

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru amesema MNH inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa wataalam katika Idara ya Usingizi na kwamba hospitali inaendelea kutatua changamoto hizo.

  Dk. Mpoki ambaye ameambatana na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dk. Doroth Gwajima pamoja na mambo mengine wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwemo vyumba vya upasuaji, wodi ya wagonjwa mahututi na wodi ya watoto.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulusubisya (kulia) akitembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo ili kuona maeneo mbalimbali yaliokarabatiwa vikiwamo vyumba vya upasuaji na vyumba vya kulaza wagonjwa wa figo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulusubisya akizungumza na wafanyakazi wa Idara ya Uzingizi leo pamoja na watumishi wengine wa hospitali hiyo
  Baadhi ya wafanyakazi wa idara hiyo pamoja na watumishi wengine mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Ulusubisya leo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Ulusubisya kuzungumza na wafanyakazi wa idara hiyo leo.
  Wafanyakazi wa Muhimbili wakiwamo wa Idara ya Usingizi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Museru.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili

  0 0

  A few days after addressing more than 80,000 people at the Place de la Concorde in central Paris as part of the Primtemps Solidaire global event, Zuriel headed to Morocco where he current film - "Follow The Ball" is making its second country premiering. 
   Before showing the film in her premier, she addressed a gathering of delegates from more than 15 countries, including Spain, Gabon, Senegal, the UK, Nigeria, France, Cameroun, Guyana, South Africa, Ghana, Kenya and Benin at the annual WIA [Women In Action] at the Beldi Country club, in Marrakech http://beldicountryclub.com/en/

  0 0

  Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam 
  SERIKALI ya China imeipatia Tanzania msaada wa Shilingi bilioni 29.4 kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu ya ufundi stadi, utalii wa kijiolojia na kukarabati wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 
  Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Gou Haodong. 
  Bw. Doto James alisema kuwa kiasi cha Shilingi bilioni 22.4 cha msaada huo kitatumika kujenga Chuo cha Ufundi Stadi-VETA wilayani Ngara mkoani Kagera, ambacho kitakapo kamilika kitadahili zaidi ya wanafunzi 400. 
  “Fedha hizo zitatumika kujenga vyumba 19 vya madarasa, ujenzi wa karakana 9 za kutolea mafunzo ya elektroniki, ufundi bomba, useremala, ufundi uashi na upakaji rangi” alisema Bw. James. 
  Alieleza kuwa kiasi hicho pia kitatumika kujenga majengo ya utawala, mabweni, nyumba za walimu na miundombinu mingine itakayosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwenye chuo hicho. 
  “Tunaamini kwamba msaada huo utakuwa sehemu ya kusaidia jitihada za Serikali za kujenga uwezo wa wataalamu wake watakaochangia kukuza sekta ya uzalishaji na hatimaye kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana nchini” alisema Bw. James
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong (wa tatu kushoto) wakisaini makubaliano ya msaada wa Sh. bilioni 29.4 kwa ajili ya miradi ya Ujenzi wa Chuo cha VETA Mkoani Kagera, Utalii wa Kijilojia na Ukarabati wa Uwanja wa Taifa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya msaada wa Sh. bilioni 29.4 kwa ajili ya miradi ya Ujenzi wa Chuo cha Ufundi (VETA), Mkoani Kagera, Utalii wa Kijiolojia na Ukarabati wa Uwanja wa Taifa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) wakiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) hati ya makubaliano ya msaada wa Sh. bilioni 29.4 uliotolewa na Serikali ya China kwa ajili ya miradi ya Ujenzi wa Chuo cha Ufundi (VETA) Mkoani Kagera, Utalii wa Kijiolojia na Ukarabati wa Uwanja wa Taifa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Amina Khamis Shaaban (kushoto) na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bw. John Rubuga (kulia) wakishuhudia utiliwaji saini makubaliano ya msaada wa Sh. bilioni 29.4 uliotolewa na China kwa ajili ya miradi ya Ujenzi wa Chuo cha Ufundi (VETA) Mkoani Kagera, Utalii wa Miamba na Ukarabati wa Uwanja wa Taifa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati), Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong (wa pili kulia) na Maafisa waandamizi kutoka Tanzania na China wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kusainiwa makubaliano ya msaada wa Sh. bilioni 29.4 uliotolewa na Serikali ya China kwa ajili ya miradi mbalimbali katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.  
  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano 
  Serikali Wizara ya Fedha na Mipango)

  0 0

    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa (kulia) na pamoja na Mjumbe wa Bodi  kutoka Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakisaini Mkataba wa ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.

    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa (kulia) na pamoja na Mjumbe wa Bodi  kutoka Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakibadilishana Mkataba wa ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.

     Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa (kulia) na pamoja na Mjumbe wa Bodi  kutoka Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakionyesha kwa waandishi wa habari  Mkataba wa ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.

       Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.
     Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hawa Ghasia akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.


  0 0


older | 1 | .... | 1935 | 1936 | (Page 1937) | 1938 | 1939 | .... | 3284 | newer