Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1933 | 1934 | (Page 1935) | 1936 | 1937 | .... | 3270 | newer

  0 0

  NA VICTOR MASANGU, KIBAHA PWANI 

  JUMUIYA  za  umoja wa vijana (UVCCM)   zimetakiwa kumuunga mkono Rais wa  serikali ya awamu ya tano Dk. John Magufuli katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na kuwa wazalendo na nchi yao   ili kuweza  kutimiza azma ya kuwa na Tanzania yenye uchumi wa viwanda na kuwaasa  kuachana kabisa na masuala ya kuwa tegemezi kila kukicha. Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa (UVCCM) Mkoa wa Pwani  Ramadhani Kapeto wakati wa mkutano maalumu wa uchaguzi wa jumuiya ya umoja wa vijana katika Wilaya ya Kibaha vijijini ambao umefanyika katika ukumbi wa JKT Ruvu mlandizi.

  Katibu huyo alisema kwa sasa vijana hususn wa UVCCM wanatakiwa kubadilika na kuwa na mtazamo chanya wa kujikita zaidi katika kutafuta  fursa zilizopo za  kuanzisha miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo itaweza kuwasaidia kuwapatia kipato ambacho kitaweza kuwasaidia katika kujikimu kimaisha na kupambanana wimbi la umasikini kuliko kukitegemea chama pekee kiwasaidie.

  “Vijana hasa wa UVCCM mimi napenda kuwaambia kuwa inabidi kujituma kwa hali na mali kwa lengo la kuweza kukipogania chama chenu, pamoja na kuhakikisha mnakuwa na kazi yoyote ambayo inakuingizia kipato na sio kuwa omba omba hivyo ni vema mkawa na miradi yenu mbali mbali ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa kuliko kukitegemea chama, kazi za chama ni kujitolea hakuna ajira hivyo ni vema mkalifahamu hilo,”alisema Katibu huyo.

  Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini Amoud Juma amewataka vijana  hao wa UVCCM kuhakikisha wanashikamana kwa hali  na mali kwa lengo la kuweza kushinda katika chaguzi mbali mbali na kuweka mipango madhubuti katika kukiimarsiha chama cha mapinduzi kiweze kushinda katika chaguzi  za ngazi  mbali mbali zinazokuja. Aidha Mbunge huyo ambaye pia ni mlezi wa UVCCM Kibaha vijijini alibainisha kuwa katika kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuwa na uchumi wa viwanda atahakikisha anaweka mipango madhubuti na kuandaa program maalumu  ya kuviwezesha vikundi mbali mbali vya  vijana kwa lengo la kuweza kujikwamua na wimbi la umasikini pamoja na kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

  “Kwa upande wangu mimi kama wa jimbo hili la Kibaha vijijini lengo langu kubwa ni kuwasaidia vijana waweze kutimiza malengo yao na kwa sasa nipo katika mipango ya kuendelea kuwawezesha katika vikundi nia na madhumuni ni kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini,”alifafanua Jumaa. Aidha Mbunge huyo aliongeza kuwa katika kuunga juhudi za Rais wa awamu ya tano atahakikisha kwamba anawapatia mafunzo mbali mbali ya ujasiliamari pamoja na kuwapatia mitaji  vijana hao ili waweze kuingia katika kufanya biashara pamoja na kuwa na viwanda vidogovidogo ambavyo vitaweza kuwawezesha kujiajiri wao wenyewe.

  KATIKA kinyang’anyoro cha uchaguzi  huo wa jumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM) katika Wilaya ya Kibaha vijijini imeweza kupata safu mpya ya uongozi ambao utaongoza kwa kipindi cha miaka mitano, huku Jumanne Mbonde akichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya baada ya kupata kura 230 kati ya kura 253 ambazo zilipigwa na wajumbe wa mkutano huo kutoka kata 14.

  0 0


  0 0


  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewapa fursa mashabiki wengi kuingia uwanjani kuishangilia timu ya taifa ya wanawake wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ itakayocheza na Falconets ya Nigeria, Jumapili Oktoba mosi, mwaka huu. 
   TFF imetoa ofa katika kiingilio. Kiingilio kitakuwa ni Sh. 500 tu kwa mashabiki watakaoketi eneo la mzunguko huku kwa wale watakaokaa Jukwaa Kuu (VIP) watalipia Sh. 1,000 tu katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam. 
   “Lengo ni kuvutia mashabiki wengi wakaangalie soka la wanawake. Wakaingalie timu yetu. Wakaangalie uwezo wa timu yetu, waishangilie kwa nguvu zote,” amesema Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred. 
   Kocha wa Tanzanite, Sebastian Nkoma, amesema kwa namna alivyokiandaa kikosi chake ana imani kitaweza kupindua matokeo ya awali ambayo Tanzania kwa bahati mbaya ililala mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Samuel Ogbemudian, ulioko Jimbo la Benin nchini Nigeria, wiki mbili zilizopita.

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiangalia eneo lililoathiriwa na ajali ya moto iliyoteketeza makazi ya askari  tukio lililotokea jana majira ya jioni, IGP Sirro yupo mkoani Arusha, kwa ajili ya kuwapa pole askari na familia zao pamoja na salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, na kutoa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 260 kwa ajili ya kujenga upya makazi yao kulia ni kamanda wa Polisi mkoani humo (DCP) Charles Mkumbo.
   MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akisalimiana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro (ACP) Hamisi Issah, na anayeshuhudia katikati ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (DCP) Charles Mkumbo, alipowasili mkoani Arusha, kuwapa pole askari wa jeshi hilo kufuatia ajali ya moto iliyoteketeza makazi yao waliyokuwa wakiishi.

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na askari ambao ni waathiriwa wa tukio la ajali ya moto iliyotokea mkoani Arusha, na kuteketeza nyumba na mali zilizokuwemo, alipowasili mkoani humo kwa lengo la kuwapa pole pamoja na salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, na kutoa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 260 kwa ajili ya kujenga upya makazi yao. 
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kulia), akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, alipowasili mkoani humo kwa ajili ya kuwapa pole askari na familia zao kufuatia ajali ya moto iliyoteketeza makazi yao waliyokuwa wakiishi pamoja na kuwapa salamu za pole kutoka kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, na kutoa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 260 kwa ajili ya kujenga upya makazi yao. 
  Picha na Jeshi la Polisi.

  0 0

  Uongozi mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ukiongozwa na Rais wake, Wallace Karia, umetembelea Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ambayo ni wadhamini wakuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars. Ziara hii imefanywa na uongozi mpya wa TFF ikiwa ni wiki moja kabla ya mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayozikutanisha Taifa Stars na Malawi, mchezo utakaofanyika  kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

  Tangu imepata udhamini wa SBL mwezi Mei mwaka huu, Taifa Stars imecheza mechi nane kati ya 12 ikiwa ni mechi za kimataifa na kufanikiwa kuweka rekodi nzuri kwenye mechi zote ilizocheza. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Rais wa mpya wa TFF aliishukuru SBL kwa udhamini wake kwa timu ya taifa na aliihakikishia SBL kuwa uongozi wake umeunda  menejimenti ya Taifa Stars ili kuhakikisha kuwa timu ya taifa inapata ushindi kwenye kila mechi. 

  “Tunaishukuru SBL kwa kutoa msaada uliokuwa unahitajika sana na ambao umeiwezesha timu yetu ya taifa kujiandaa vyema na mechi na kufanya vizuri kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa,” alisema Karia

  Karia alisisitiza kuwa fedha zilizotolewa kwa ajili ya udhamini wa timu ya taifa, zitatumika vizuri na kuongeza kuwa uongozi wa TFF unalenga kuongeza imani kwa wadhamini wa Taifa Stars na wadau wa soka kwa ujumla wake.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie alimpongeza Rais mpya wa TFF pamoja na timu yake kwa kuchaguliwa na kueleza kuwa SBL itaendelea kutoa misaada inayolenga kuendeleza michezo hapa nchini.

  “SBL inatambua mchango muhimu ambao michezo inatoa kwenye maendeleo ya kiuchumi na kijamii na ndiyo maana tunaamini kuwa tunapoidhamini Taifa Stars, tunachangia katika kuwaburudisha na kuwaunganisha Watanzania wakiwa na bia yao bora ya Serengeti ikwa na ujumbe wake wa sifa yetu, bia yetu, nchi yetu,” alisema 

  Mwezi Mei mwaka huu, TFF iliingia mkataba wa ufadhili kwa Taifa Stars utakaodumu kwa kipindi cha miaka 3 utagharimu shilingi blioni 2.1na kuifanya SBL kuwa mdhamini mkuu wa timu ya taifa. Ikizalishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1996, bia ya Serengeti imetengenezwa na kimea kwa asilimia 100 huku ikiweza kushinda tuzo zaidi ya 10 kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa kutokana na ubora wake wa kimataifa.

  0 0


  0 0


  0 0
 • 09/28/17--08:32: Article 6
 • Jovina Bujulu-MAELEZO

  Hivi karibuni, Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea (TFRA) imeingiza nchini mbolea yenye uzito wa tani 55,000 kwa mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja bila kuwepo malipo ya ziada bandarini. 

  Mfumo huo utasaidia kupunguza bei na kuhamasisha matumizi ya mbolea kwa wakulima wengi nchini.

  Uingizwaji wa mbolea hiyo ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2017/18, mjini Dodoma.

  DKt. Tizeba alisema kuwa kuanzia msimu wa 2017/18  Serikali itaanza kuagiza mbolea kwa mfumo wa pamoja kwa kuanza kuagiza aina mbili za mbolea ambazo ni mbolea ya kupandia (DAP) na ya kukuzia (UREA), kwa kuwa ndizo  zinatumika sana nchini.

  Alitaja sababu za kutumia mfumo huo kuwa ni pamoja na kuongeza matumizi ya mbolea nchini kwa kuhakikisha kuwa wadau wote wanapata uhakika wa upatikanaji wa mbolea kwa bei ya ushindani. 

  Aidha, mfumo huo unawawezesha wafanyabiashara wadogo wanapata nafasi ya kuagiza mbolea na kuimarisha mtandao wa usambazaji hadi ngazi ya mkulima.

  Vilevile utaratibu huo unawawezesha waagizaji kununua mbolea wakati bei ikiwa ndogo na TFRA  kufuatilia bei hiyo ili kuepuka mwanya wa waagizaji kuongeza bei zaidi ya ile iliyonunuliwa kwa bei ndogo

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack A. Kamwelwe amezitaka halmashauri za Mkoa wa Singida kuongeza ujenzi wa mabwawa, utakaosaidia kilimo cha umwagiliaji ili kuzalisha chakula cha kutosha na kwa ajili ya makao makuu ya nchi, Dodoma.

  Mhandisi Kamwelwe ametoa maelekezo hayo wakati wa mkutano uliojumuisha wakuu wa idara zote pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida ili kujadili hali ya Sekta ya Maji kabla ya hajaendelea na ziara yake katika halmashauri za Mkoani hapa.

  Amesema ardhi ya Singida pamoja na kiwango cha mvua cha milimita 500 mpaka 800 kwa mwaka vinatosha kuzalisha chakula kwa ajili ya matumizi ya mkoa lakini ujenzi wa mabwawa utaongeza uzalishaji wa chakula hasa kwa lengo la kulisha mkoa wa Dodoma.
  Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack A. Kamwelwe na Mkuu wa Mkoa wa Singida wakisoma kwa umakini taarifa ya Sekta ya maji Mkoa wa Singida wakati wa kikao na wakuu wa idara mbalimbali.

  “Mkuu wa Mkoa wa Singida una malengo makubwa na mazuri kwa mkoa huu, mpango wako wa kuifanya Singida iilishe Dodoma ni mzuri na utafanikiwa hasa mkiongeza bidii katika uzalishaji na kuweka kipaumbele katika kilimo cha umwagiliaji”, amesema Mhandisi Kamwelwe.

  Ameongeza kuwa Singida inapata mvua za wastani lakini imekuwa ikizalisha kwa wingi mazao ambayo yamekuwa yakitumika katika mikoa yote nchini kwa mfano alizeti, viazi vitamu, vitunguu na asali ambapo mazao hayo yamekuwa yakipendwa kutokana na ubora wake. Mhandisi Kamwelwe ameongeza kuwa hali ya upatikanaji wa maji kwa Mkoa wa Singida bado inatakiwa kuboreshwa zaidi kutokana na kuwa kila mwaka serikali imekuwa ikitenga fedha nyingi lakini asilimia ya upatikanaji wa maji haiongezeki kwa kasi inayotakiwa.

  Aidha amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Singida kusimamia matumizi ya fedha za serikali zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maji ili ziweze kufanya kazi iliyokusudiwa na kwa ubora mkubwa.
  Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack A. Kamwelwe akisikiliza taarifa ya mradi wa maji wa Ughandi kutoka kwa Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Edward Kisalu.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amesema kuwa Singida sio kame kwakuwa hakuna mazao yanayoweza kumea katika ukame isipokuwa Singida imejikita katika mazao yanayotumia maji kwa ufanisi.

  Dkt Nchimbi amesema Singida inazalisha mazao ya mahindi, alizeti, vitunguu, viazi vitamu na mazao mengine kwa wingi kutokanana na kuwa mvua zinazonyesha zinatosheleza kustawisha mazao hayo. Ameongeza kwa kuwataka wakuu wa idara zote kusimamia matumizi bora ya fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya maji kwakuwa suala la maji ni la kila mmoja na sio kuwategemea watumishi wa idara hiyo pekee katika kusimamia fedha na miundominu ya maji.

  Dkt Nchimbi amesema Mkoa unahamasisha uchimbaji wa mabwawa kwa halmashauri, taasisi na hata makundi mengine kwakuwa mabwawa hayo yatasaidia kuinua kilimo cha umwagiliaji Mkoani Singida pamoja na kukuza uchumi.
  Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack A. Kamwelwe akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ughandi A halmashauri ya Wilaya ya Singida alipotembelea eneo la mradi wa maji kijijini hapo.

  Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida Buhacha Kichinda amesema hali ya upatikanaji wa maji kwa Mjini ni asilimia 50.6 huku vijijini ikiwa ni asilimia 44 na kuongeza kuwa wastani huo ni mdogo kwakuwa unarudisha nyuma jitihada za kuinua uchumi.

  Kichinda amesema Mkoa umejipanga kushirikisha wadau zaidi ili kuongeza kasi ya ujenzi wa miradi ya maji ya visima virefu pamoja na ujenzi wa mabwawa pamoja na kusimamia fedha zote za serikali zinazotolewa kwa ajili ya sekta ya maji zinatumika ipasavyo. Amesema ili kuhakikisha mvua zinaendelea kunyesha vizuri pamoja na kutunza vyanzo vya maji, mkoa umeweka mkakati wa “ Achia shoka Kamata Mzinga” ili kuwahamasisha wachoma mikaa waache kukata miti bali wajikite katika kutundika mizinga itakayotunza mazingira.

  0 0

  Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wamefanya ziara ya siku moja katika Mitambo ya Uzalishaji Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini  iliyopo Mlandizi na Bagamoyo mkoani Pwani ,ziara iliyoandaliwa na Shirika la Maji safi na Maji taka Dar es Salamaa (DAWASCO) kwa lengo la kujifunza namna matibabu ya maji yanavyofanyika kuanzia yanapotoka mto Ruvu.
  Mbali na kutembelea Mitambo ya uzalishaji maji pia Wanahabari hao wametembelea ofisi za Dawasco mkoa wa Tabata kujionea utendaji kazi kwa watendaji wa Shirika hilo ,kituo cha Tabata. 

  Meneja wa Dawasco Tabata, Victoria Masele akiwakaribisha wanahabari ofisi kwake mara baada ya kumtembelea.

  Meneja Biashara wa Dawasco Tabata, Jamal Chuma kifafanua jambo kwa wanahabari.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0  0 0  0 0  0 0


  0 0


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mheshimiwa Pierre Nkurunziza, leo tarehe 28.9.2017 ametembelea Maonesho ya Kwanza ya Biashara ya Tanzania yanayofanyika katika Viwanja vya Maonesho vya Tempete vilivyopo Mjini Bujumbura.
   
   Maonesho haya yaliandaliwa na TANTRADE kwa ushirikiano na Ubalozi wa Tanzania Burundi pamoja na Mamlaka ya Bandari Tanzania ( TPA ) yamefunguliwa rasmi tarehe 27.9.2017 na Dr Joseph Bitore, Makamu wa Pili wa Rais wa Burundi yanatarajia kumalizika tarehe 1.10.2017. 
   
  Baada ya kutembelea Maonesho haya, Mh. Rais Nkurunziza alisifu uhusiano uliopo baina ya Burundi na Tanzania na aliahidi kuunga mkono juhudi zote za kuimarisha uchumi baina ya Nchi hizi mbili. 
   
  Picha chini zinamuonesha Rais Nkurunzinza akiongozwa na Mh. Christopher Chiza, Mwenyekiti wa Bodi TanTrade, Balozi Rajabu Gamaha, Balozi wa Tanzania Burundi pamoja na Bw. Edwin Rutageruka, Kaimu Mkurugenzi Mkuu TanTrade ambao wapo Mjini Bujumbula kwa sasa kubudhuria Maonesho haya.

    Rais Nkurunzinza akipata maelezo mafupi kuhusu bidhaa mbalimbali zinazouzwa kwenye maonesho hayo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu TanTrade Bw. Edwin Rutageruka,ambao wapo Mjini Bujumbula kwa sasa kubudhuria Maonesho hayo.
   Rais Nkurunzinza akiongozwa na Mh. Christopher Chiza, Mwenyekiti wa Bodi TanTrade, Balozi Rajabu Gamaha, Balozi wa Tanzania Burundi pamoja na Bw. Edwin Rutageruka, Kaimu Mkurugenzi Mkuu TanTrade ambao wapo Mjini Bujumbula kwa sasa kuhudhuria Maonesho hayo.
   Mheshimiwa Pierre Nkurunziza, Rais wa Jamhuri ya Burundi, leo tarehe 28.9.2017 ametembelea Maonesho ya Kwanza ya Biashara ya Tanzania yanayofanyika katika Viwanja vya Maonesho vya Tempete vilivyopo Mjini Bujumbura.
   
   Rais Nkurunzinza akihojiwa na baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani),kwenye maonesho hayo, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi TanTrade, Christopher Chiza pamoja na  Kaimu Mkurugenzi Mkuu TanTrade Bw. Edwin Rutageruka,ambao wapo Mjini Bujumbula kwa sasa kubudhuria Maonesho hayo.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya MGen Insurance Tanzania ya jijini Dar es salaam Bw. Charles Sumbwe akikabidhi msaada wa mashine mbili za Kupima Kiwango cha Hewa na Mapingo ya Moyo kwa Watoto wachanga (Pulse Oxmeter) kwa Daktari Bingwa wa Watoto katika hospitali ya Mwananyamala Dkt. Elnestina Mwipopo leo jijini Dar es salaam, Kampuni hiyo imetoa mashine hizo zenye thamani ya shilingi milioni 2.8 na vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto katika hospitali hiyo jumla ya msada wote ni shilingi milioni 3.8.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya MGen Insurance Tanzania ya jijini Dar es salaam Bw. Charles Sumbwe akikabidhi msaada wa Vifaa mbalimbali vya kuwahudumia watoto kwa Daktari Bingwa wa Watoto katika hospitali ya Mwananyamala Dkt. Elnestina Mwipopo leo jijini Dar es salaam, Kampuni hiyo imetoa mashine hizo zenye thamani ya shilingi milioni 2.8 na vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto katika hospitali hiyo
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya MGen Insurance Tanzania ya jijini Dar es salaam Bw. Charles Sumbwe na Daktari Bingwa wa Watoto katika hospitali ya Mwananyamala Dkt. Elnestina Mwipopo mara baada ya kukabidhiana msaada wa mashine mbili za Kupima Kiwango cha Hewa na Mapingo ya Moyo kwa Watoto wachanga (Pulse Oxmeter) kwa leo jijini Dar es salaam.


  0 0

  Na Pascal Dotto, MAELEZO

  Serikali imesema kasi kubwa ya maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo imeikumba sekta ya habari inalazimu jamii kufanya maboresho ya mara kwa mara ya Sera na Kanuni ili kuepusha matumizi mabaya ya vyombo vya habari.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kuwa katika kufanya hivyo ni wajibu wa wadau wote kushirikiana kutumia vyema maendeleo hayo ya tekinolojia kwa ajili ya ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa.

  Profesa Elisante alisema hayo leo wakati akifungua mkutano wa siku moja wa mashauriano miongoni mwa wadau wa sekta ya habari kuhusu mapendekezo ya Kanuni za maudhui yanayorushwa na vituo vya Utangazaji vya Redio na Televisheni na Kanuni za Maudhui Mtandaoni.

  “Ni wajibu wetu kama taifa linalosimamia maadili na ambalo lingependa kudumisha amani na mshikamano, kutunga kanuni ambazo zitahakikisha kuwa kunakuwa na matumizi mazuri, sahihi na salama ya maudhui ya mtandaoni”Profesa Elisante alisisitiza.

  Aliwaambia washiriki wa mkutano huo kuwa kuweka kanuni ni suala muhimu na kuwakumbusha matumizi ya mfumo wa habari mtandaoni wakati mwingine umetumika kupotosha jamii, kujenga chuki, kutoa habari za faragha za watu binafsi au habari zilizoleta sintofahamu miongoni mwa jamii.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta habari ili kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta habari ili kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka TCRA, Fred Ntobi, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Rodney Thadeus akielezea jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya habari ili kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni leo Jijini Dar es Salaam.
  Mjumbe wa Kamati ya Maudhui kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka akiwasilisha mada kuhusu kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya habari ili kujadili kanuni hizo leo Jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Marie Stopes Tanzania (MST) leo imeizindua upya hospitali yake iliyopo Mwenge inayopatikana kwenye kitalu namba 421 na 422 Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Hebogard Jensen ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliipongeza MST kwa kuonyesha juhudi za dhati za kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba wananchi wengi zaidi wanapata huduma za afya zilizo bora na bei nafuu.

  “Nchini Tanzania, Marie Stopes inatambulika kwa utoaji wa huduma bora za afya ambazo wananchi wengi wanaweza kuzimudu, lakini kubwa zaidi ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za afya,” alisema Jensen.Kuzinduliwa upya kwa hospitali hiyo ni matunda ya ushirikiano kati ya MST na DANIDA/ Ubalozi wa Denmark ambapo wameifanya hospitali hiyo kuwa miongoni mwa vituo bora vya afya kwa ajili ya uzazi wa mpango na huduma ya elimu ya afya ya uzazi.

  Alisema ushirikiano wa DANIDA na Marie Stopes Tanzania utakuwa endelevu kwa manufaa ya Watanzania wote.“Tutaendelea kuwekeza kwenye jamii ambayo tunafanya kazi ili kusaidia kutekeleza miradi yetu mbalimbali ya afya, elimu na pamoja na vita ya kutokomeza umaskini,” alisema.

  Jensen pia alizindua kituo cha mawasiliano cha ‘MST Contact Centre’ ambacho kitakuwa ni kitovu cha huduma ya kupiga simu bure kutoka kwa wateja na umma kiujumla ili kuimarisha mawasiliano na watoa huduma wa MST. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay alisema hospitali hiyo iliyozinduliwa upya itatoa huduma nzuri kwa wateja ikiwa pamoja na mazingira mazuri zaidi kwa wagonjwa.

  Aliongeza kuwa huduma mbalimbali zinapatikana na kwenye vituo vya MST ikiwa ni pamoja na huduma ya afya ya uzazi inayotolewa mikoa yote ya Tanzania kupitia njia ya simu ya mkononi.MST inafanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya Tanzania kwa hatua zote ikiwa ni pamoja na kusaidia awamu ya nne ya Mpango Mkakati wa Afya wa HSSP-IV wa mwaka (2015-2020) ikiwa kama mshirika wa sekta binafsi (PPP).
  Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Hebogard Jensen (katikati) akikata utepe wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospitali iliyoboreshwa ya Marie Stopes Mwenge leo jijini Dar es salaam. Hospitali hiyo pia imezindua kituo cha kupokea simu na pia kuanzisha huduma ya bure ya siku tatu kwa watakaopenda kupima magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, Ukimwi, ushauri wa masuala ya uzazi wa mpango, Kansa ya mlango wa kizazi huku huduma nyingine za kitabibu zikitolewa kwa gharama.
  Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Hebogård Jensen akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa hospitali iliyoboreshwa ya Marie Stopes Mwenge leo jijini Dar es salaam. Hospitali hiyo pia imezindua kituo cha kupokea simu na kuanzisha huduma ya bure ya siku tatu kwa watakaopenda kupima magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, Ukimwi, ushauri wa masuala ya uzazi wa mpango, Kansa ya mlango wa kizazi huku huduma nyingine za kitabibu zikitolewa kwa gharama. Anayeshuhudia (kulia) ni Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay.
  Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospitali iliyoboreshwa ya Marie Stopes Mwenge leo jijini Dar es salaam. Hospitali hiyo pia imezindua kituo cha kupokea simu na kuanzisha huduma ya bure ya siku tatu kwa watakaopenda kupima magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, Ukimwi, ushauri wa masuala ya uzazi wa mpango, Kansa ya mlango wa kizazi huku huduma nyingine za kitabibu zikitolewa kwa gharama. 
  Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Hebogard Jensen (katikati) akikata utepe wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha kupokea simu cha Marie Stopes Mwenge leo jijini Dar es salaam.Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa marie Stopes Tanzania Anil Tambay na Mratibu wa huduma ya Afya ya Mzazi na Mtoto Edith Manase Mboga.


older | 1 | .... | 1933 | 1934 | (Page 1935) | 1936 | 1937 | .... | 3270 | newer