Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1932 | 1933 | (Page 1934) | 1935 | 1936 | .... | 3272 | newer

  0 0


  NA VICTOR MASANGU, KIBAHA 

  NAIBU Waziri wa Tamisemi Seleman Jafo amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa Tumbi na kutoa muda wa wiki moja kwa mtendaji mkuu wa Shirika la elimu Kibaha kuanza mara moja ujenzi kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa majengo baada ya kubaini umekwama kwa kipindi cha miaka saba bila ya kuendelezwa kitu chochote hali ambayo imesababisha kwa sasa eneo hilo kuota nyasi na kugeuka kuwa vichaka.

  Jafo akizungumza kwa masikitiko makubwa na baadhi ya watumishi wa hospitali ya Tumbi,pamoja na viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani amechukizwa kuona mradi huo kutelekezwa na kusababisha miundombinu yake ya majengo kuchakaa kabla hata ya kuanza kutumika kitendo ambacho amekilaani vikali na kusema suala hilo hawezi kulifumbia macho hata kidogo.

  Jafo alibainisha kuwa serikali tayari imeshatoa kiasi cha shilingi milioni 600 na fedha hiyo imeshaingizwa katika Ofisi ya Ras Pwani tangu mwaka jana kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo lakini anashangazwa kuona mradi huo kusimama, hivyo amewaagiza watendaji wa mamlaka zinazohusika kukutana na kuliweka sawa jambo hilo kwa lengo la kuweza kuboresha sekta ya afya.

  “Kwa kweli natoa wiki moja kwa mtendaji mkuu kufanya haraka iwezeknavyo mradi huu wa upanuzi ambao ulikuwa umesimama kwa kipindi kirefu kukaa chini na watendaji wenzake wakubaliane na kuweza kuanza mara moja ujenzi huo maana fedha zipo tu na kwamba tayari tumeshazitoa shilingi milioni 600 sasa sijui nini tatizo kwa hiyo wiki ijayao nataka kuona ujenzi huo unaanza kuendelea,”alisema Jafo.
  Naibu Waziri wa Tamisemi Seleman Jafo akisalimiana kwa kumpa mkono mmoja wa wagonjwa mara alipofanya ziara yake ya kushtukiza katika hospitali ya tumbi kwaa ajili ya kuweza kufanya ukaguzi katika mradi wa upanuzi wa hospitali hiyo.PICHA NA VICTOR MASANGU.  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amepiga marufuku Shule zote Mkoani Singida kuagiza chaki nje ya Mkoa kwakuwa kuna viwanda vinavyozalisha chaki bora mkoani hapa.

  Dkt Nchimbi ametoa katazo hilo mara baara ya kufanya ziara katika viwanda viwili vinavyozalisha chaki katika halmashauri ya Itigi na kushuhudia chaki yenye ubora ikiwa imezalishwa kwa wingi na ikiwa haijapata soko.

  “Hawa wenye viwanda wamejitahidi kuzalisha chaki bora haina vumbi na inauzwa kwa bei sahihi lakini shule zetu badala ya kuja kununua hapa ambapo ni karibu wanaagiza Dar es salaam na mikoa mingine”, amesema na kuongeza kuwa,

  “Yani mnasubiri chaki hii hii iende Dar es Salaam halafu mnainunulia kutoka huko, hii haikubaliki, kuanzia leo shule zote zinunue chaki hapa hapa ili tupunguze gharama pamoja na kuinua viwanda vyetu”.Dkt Nchimbi ameongeza kuwa Mikoa ya Jirani itakayonunua chaki katika Viwanda vya Singida, vitasafirishiwa chaki hiyo bure kama motisha kwa kuunga mkono viwanda hivyo.

  Amezitaka halmashauri kushirikiana katika kuboresha mazingira ya utendaji wa viwanda hivyo hasa kwa kuangalia namna ya kuboresha barabara zinazoenda katika machimbo ya jasi yanayotumika kutengeneza chaki kwakuwa wenye viwanda wamekuwa wakilalamikia ubovu wa barabara hizo.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akishiriki zoezi la kutengeneza chaki katika kiwanda cha Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
  Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Miraji Jumanne Mtaturu akiwa amebeba ili kuzianika chaki alizotengeneza Mkoa Singida Dkt Rehema Nchimbi katika kiwanda cha Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akikagua kiwanda cha kutengeneza jasi cha Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
  Wafanyakazi wa kiwanda cha Dober Color wakifungasha chaki, Meneja wa Kiwanda hicho amesema sehemu ya kufungasha chaki hiyo inafanywa na wanawake kwakuwa wako makini na haraka.


  0 0
 • 09/27/17--22:47: KUMBUKUMBU
 • HAYATI JOHN MGEJA
   BABA ni miaka 17 tangu ulipotuacha ghafla Mpendwa wetu....Unakumbuka kwa upendo wako wa dhati na Mke Wako RUTH NKIYA MGEJA, Wanao LOUIS MANGALA MGEJA, MUSSA MWANDU MGEJA, FRANK JOHN MGEJA, MARC MIPAWA MGEJA pamoja na EDGER NKONOKI MGEJA. Kaka, Dada pamoja na Ndugu na jamaa zako wote uliopata kuwa karibu nao ktk uhai wako. Upumzike kwa Aman Baba Yetu. Bado unaishi ndani ya mioyo yetu hata sasa.

  0 0

   

   

  Balozi wa Nordic Foundation Tanzania, Najma Abdallah akiwasiliana na Mwalimu wa Shule ya Msingi iliyopo Songwe Mkoani Mbeya, Hassan Mwamburi baada ya kuibuka mmoja wa washindi 10 katika droo ya Pili ya kampeni ya Afyabando iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Washindi watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya zenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya matibabu pamoja na familia.

   Balozi wa Nordic Foundation Tanzania Najma Abdallah akiwasiliana na Diana Peter Mkazi wa Morogoro baada ya kuibuka mmoja wa washindi 10 watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya zenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya matibabu pamoja na familia, katika droo ya ya pili ya Afyabando.

   Mabalozi wa Nordic Foundation Tanzania Hilary Daudi' Zembwela' na Najma Abdallah wakiendesha kampeni ya Afyabando kuwapata washindi 10 watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya zenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya matibabu pamoja na familia. Mchezo huo umechezeshwa jijini Dar es Salaam hivi karibuni. 

  Mabalozi wa Nordic Foundation Tanzania Hilary Daudi' Zembwela' na Najma Abdallah wakiwa na Mkaguzi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha, Bakari Maggid aliyesimamia zoezi la kuendesha kampeni ya Afyabando kuwapata washindi 10 watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya zenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya matibabu pamoja na familia. 


  0 0
  0 0

  Hatimaye Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba iliyokuwa ikiendeshwa kwa zaidi ya miezi 6 na Kampuni ya Global Publishers ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa wasomaji wake, imefikia mwisho ambapo mshindi kutoka Dodoma amepatikana.
  Katika droo ya fainali hiyo, ambayo imefanyika kweNye Viwanja vya Las Vegas, Mabibo jijini Dar huku mgeni rasmi akiwa Diwani wa Kata ya Mabibo, Kassim Lema, mshindi aliyejishindia nyumba hiyo iliyopo Bunju B, nje kidogo ya Jiji la Dar, ni George Majaba mkazi wa Mkoa wa Dodoma.
  Akizungumza na Gazeti hili, mapema baada ya kumaliza shughuli ya kumtangaza mshindi wa nyumba hiyo, Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho aliwashukuru wasomaji wa Magazeti ya Global kwa kuwa waaminifu katika kipindi chote ambacho wameshiriki kimamilifu kwenye kinyang’anyiro cha kumpata mshindi. Mbali na mshindi huyo wa nyumba, pia kulikuwa na washindi wengine walioibuka na zawadi za dinner set, ambao ni Kahabi Suleiman wa Vingunguti, Dar, Melania Swai wa Mbezi, Dar na Philemon Faustine wa Dar. Diwani ya Kata ya Mabibo (aliyefungwa kitambaa machoni), akipelekwa na MC wa shughuli hiyo, Chaku kwenda kuchagua kuponi ya ushindi.Kazi ya kuchanganya kuponi ikiendelea.[/caption] [caption id="attachment_174254" align="aligncenter" width="640"]Mheshimiwa diwani akiwa ameshika kuponi ya ushindi, iliyotoka Gazeti la Championi.Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akizungumza kwenye droo hiyo kubwa ya Shinda Nyumba.
   


  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya 87 ya Taifa la Kifalme la Saudi Arabia yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Prof. Maghembe alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Kulia ni Balozi wa taifa hilo nchini Tanzania, Balozi Mohammed Bin Mansour Al Malik.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mohammed Bin Mansour Al Malik (wa pili kulia) na viongozi wengine wa ubalozi huo wakijiandaa kukata keki ya maadhimisho hayo.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mohammed Bin Mansour Al Malik (katikati) na viongozi wengine wa ubalozi huo wakikata keki ya maadhimisho hayo.

  Baadhi ya watoto wa Taifa la Kifalme la Saudi Arabia wakiinua bendera ya nchi hiyo kuashiria maadhimisho ya siku ya 87 ya Taifa hilo yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  NA: ANDREA NGOBOLE, PMT

  Jumla ya Kampuni 126 zinazodaiwa kiasi cha shilingi bilioni moja pointi tano zinatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo na shirika la Taifa la hifadhi ya jamii NSSF mkoani Arusha kwa kosa la kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mapema jana meneja kiongozi wa NSSF mkoani Arusha Dr. Frank Maduga amesema kuwa makampuni hayo yamegawanyika kati ya waajiri wakubwa 14 wanaolipia kiasi cha shilingi milioni 50 na kuendelea, wajiri wa kati 69 wanaolipia milioni 5 hadi 49.9 na wale waajiri wadogo 53 wanaolipia kiasi cha shilingi elfu ishirini hadi milioni 4.9 kwa mwezi ambapo jumla ya michango yao inafikia Zaidi ya bilioni moja nukta tano mpaka sasa.

  “Waajiri wakubwa wote wamekwisha pelekewa onyo la Mwisho na sasa taratibu za kimahakama zinaendelea hivyo kuanzia jumatatu ya tarehe 2 october 2017 mtawajua ni waajiri gani wameshindwa kutekeleza wajibu wao na kwa kiasi gani wanadaiwa kila mmoja wao” alisema dokta Maduga

  Amesema kuwa Mashitaka yatakayokuwa yakiwakabali waajiri hao ni kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati na kwa muda unaozidi miezi sita, kitendo hicho kimekuwa na madhara makubwa kwa wafanyakazi na wategemezi wao kwa kukosa huduma za matibabu , fao la uzazi na pia kuna baadhi ya wanachama taarifa zao za kumbukumbu hazioneshi fedha yoyote katika muda ule ambao michango haijawasilishwa na kusababisha taharuki na msongo wa mawazo kwa wafanyakazi husika.
   Meneja kiongozi wa NSSF mkoa wa Arusha katikati Dr. Frank Maduga akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuwapeleka waajiri 126 mahakamani kwa kosa la kutowasilisha michango ya waajiriwa inayofikia kiasi cha shilingi bilioni moja nukta tano kwa kipindi cha miezi sita sasa. 

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa kwanza kutoka kushoto akikagua vichochoro vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini katika kijiji cha Mugulika Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera. Kamishna Jenerali yuko mkoa wa Kagera kujionea shughuli zinazotekelezwa na Idara yake mkoani humo.
  Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa kwanza kutoka kushoto akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera Godfrey Mheluka watatu kutoka kulia katika kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera.Kamishna Jenerali huyo amefanya ziara katika Vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kutoka nchini nyingine kuingia Tanzania.
  Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa nne kutoka kulia akiwa katika Mkutano wa Hadhara na baadhi ya Wananchi (hawapo pichani) wa Kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera.Kamishna Jenerali huyo amefanya ziara katika Vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kutoka nchini nyingine kuingia Tanzania.
  Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala katika Mkutano wa Hadhara baina ya wanakijiji hao na Ujumbe huo wa Idara ya Uhamiaji kutoka Makao Makuu ambapo katika Mkutano huo Dk. Makakala alitoa wito kwa wanakijiji hao kutowahifadhi wahamiaji haramu kwenye makazi yao sambamba na kuwataka kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola pale wanapogundua kuna mgeni asiyeeleweka na wanamtilia mashaka kwenye makazi yao.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

  0 0

   Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa kwanza kutoka kushoto  akikagua vichochoro  vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini katika kijiji cha  Mugulika  Kata ya Bwerenyange  wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera. Kamishna Jenerali yuko mkoa wa Kagera kujionea shughuli zinazotekelezwa na Idara yake mkoani humo.
   Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa kwanza kutoka kushoto  akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera  Godfrey Mheluka watatu kutoka kulia  katika kijiji cha Muguluka  Kata ya  Bwerenyange  wilaya ya Karagwe  Mkoa wa  Kagera.Kamishna Jenerali huyo amefanya ziara katika Vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kutoka nchini nyingine kuingia Tanzania.

   Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa nne kutoka kulia akiwa katika Mkutano wa Hadhara na baadhi ya Wananchi (hawapo pichani) wa Kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe  Mkoa wa  Kagera.Kamishna Jenerali huyo amefanya ziara katika Vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kutoka nchini nyingine kuingia Tanzania.

  Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe  Mkoa wa  Kagera wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala katika Mkutano wa Hadhara baina ya wanakijiji hao na Ujumbe huo wa Idara ya Uhamiaji kutoka Makao Makuu ambapo katika Mkutano huo Dk. Makakala  alitoa wito  kwa  wanakijiji hao  kutowahifadhi wahamiaji haramu  kwenye makazi yao sambamba na kuwataka kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola pale wanapogundua kuna mgeni asiyeeleweka na wanamtilia mashaka kwenye makazi yao.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)


  0 0

   MTWARA, 26th September, 2017 – Mtwara and Lindi regions launched the roll out of the decentralized births registration system that is expected to benefit more than 290,000 under-five children in the two regions. 

  The launch, held at Tandahimba, was graced by Hon. Dr. Harrison Mwakembye, the Minister of Information, Culture, Artists and Sports on behalf of Hon. Minister for Constitutional and Legal Affairs Professor Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi and other distinguished guests. The goal of the programme is to establish a system for registering all new births and reduce the backlog of unregistered under-five children in the two regions.
  The programme moves the points of registration closer to the community. It establishes registration points at health facilities, which provide reproductive and child health services, and at the community ward executive offices in line with the government policy of decentralization through devolution.

  This will enable parents in these two regions to easily access more than 780 registration points set up compared to 10 registration points at present. Moreover, there will be more than 1,500 trained Registration Assistants to support the registration process.

  The government has waived fee for registration under this programme and the first copy of the certificate is given free of charge. The programme introduces a ‘one step, one visit’ process adapts an innovative way of data collection. Through the use of mobile phone technology data will be instantly transferred and uploaded through SMS, facilitating a real-time tracking of progress.

  The decentralized system significantly accelerates birth registration in Tanzania Mainland, after years of stagnation. “We are transforming the system to make it easier for children and their families to access the entitlement of a birth certificate,” said Emmy Hudson Acting Chief Executive Officer of the Registration, Insolvency and Trusteeship Agency (RITA), responsible for the programme.  She added that; “Now parents can receive birth certificates from the designated health facilities or through the ward executive offices.
  The system has helped thousands of children in the regions where the decentralized system is in operation and we have a plan to replicate this throughout Tanzania Mainland in the shortest possible time.” She further added that, “ the government duly recognizes the contribution of UNICEF, the Government of Canada and TIGO for their commitments to this cause”.


  0 0

  NI ukweli usiopingika utekelezaji wa sekta ya viwanda inahitaji
  nishati ya umeme katika shughuli zake mbalimbali ikiwemo za uzalishaji mali ili kuweza kupata mafaniko yanayoweza kusaidia kuinua uchumi wao.

  Kwani bila kuwepo kwa nishati hiyo kwa baadhi ya maeneo hasa vijijini kuna pelekea kushindwa kufikia malengo yao kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa kuhofia iwapo zitakaa muda mrefu zitaharibika.Licha ya hivyo lakini pia kukosekana kwa nishati hiyo kuna sababisha watanzania wenye nia ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo kukwama kufikia malengo yao waliojiwekea kwa kuvianzisha.

  Kufuatia kuwepo kwa changamoto hiyo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (The United Nations Capital Development Fund –UNCDF) kwa kushirikiana na kampuni ya Ensol Tanzania Limited waliamua kuanzisha mradi wa umeme wa jua (sola) kwenye kijiji cha Mpale Kata ya Mpale wilayani Korogwe Mkoani Tanga.

  Mradi huo ambao umekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Kijiji hicho umefadhiliwa na Shirika hilo ambao umelenga kuwasaidia kuondokana na changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili ikiwemo kutumia vibatari wakati wakienda kujifungua kwenye zahanati ya Kata hiyo.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo akizundua mradi huo 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo kushoto akipata maelezo ya mradi huo mara baada ya kutembelea kwenye eneo la mtambo huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi,Robert Gabriel.


  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo akishiriki kucheza ngoma ya wananchi wa Kijiji hicho mara baada ya kuzinduaa mradi huo .

  0 0


  MKUU WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTERI TANZANIA KKKT, ASKOFU DKT. FREDRICK SHOO ANAWAALIKA WASHARIKA WOTE NA WAPENDA MAENDELEO KUNUNUA "APP" YA KITABU CHA "TUMWABUDU MUNGU WETU" KUCHANGIA KAZI ZA UMOJA WA KANISA KWA SH. 3,000 TU, APPLICATION HII INAPATIKANA KWENYE GOOGLE PLAY KWA WATUMIAJI WA SMARTPHONE NA TABLET.

  TAREHE 29 SEPTEMBA 2017 MKUU WA KANISA ANAWAALIKA KWENYE HARAMBEE ITAKAYOFANYIKA MBEZI GARDEN DAR ES SALAAM KUANZIA SAA 9 ALASIRI NA KURUSHWA MUBASHARA NA  VITUO MBALIMBALI VYA TV NA REDIO ILI KUWEZESHA WAPENDA MAENDELEO KUCHANGIA MOJA KWA MOJA KWA NJIA YA MTANDAO.


  TIGOPESA, PIGA * 150 *01#

  KISHA BOFYA NAMBA 4
  HALAFU CHAGUA NAMBA 3
  INGIZA NAMBA YA KAMPUNI 00200
  WEKA KUMBUKUMBU NAMBA 201323
  INGIZA KIASI UNACHOCHANGIA
  KISHA NAMBA YA SIRI NA
  THIBITISHA KUTUMA
  KWA M-PESA, PIGA * 150 *00#


  BOFYA NAMBA 4

  KISHA CHAGUA TENA NAMBA 4 KUINGIZA NAMBA YA KAMPUNI 001963
  WEKA KUMBUKUMBU NAMBA KWA KUBOFYA 1
  INGIZA KIASI UNACHOTAKA KUCHANGIA
  INGIZA NAMBA YA SIRI
  BOFYA 1 KUTHIBITISHA KUTUMA.  Kwa maelezo piga
  0764 931 035
  WOTE MNAKARIBISHWA

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Hapi akizungumza na baadhi ya wakazi wa Bunju A mapema leo asubuhi,waliokuwa Wakimsubiri Kumueleza Changamoto zao Mbalimbali zinazowakabili ikiwemo changamoto ya soko la wa Wafanyabishara wa soko la Bunju A ambalo inaelezwa kuwa limechukuliwa na Muwekezaji.

  DC Hapi akitoa ufafanuzi wa changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na Wananchi hao,ikiwemo changamoto ya eneo la Soko Bunju A,Mh Hapi amesema ametoa siku kumi 14  kwa ofisi ya Mkurugenzi kumletea nyaraka za soko la Bunju A ili ajiridhishe na kutoa maamuzi ya umiliki wa soko hilo kwa wananchi, huku kwa mmiliki anayetajwa kuhodhi eneo hilo  amepewa siku  tatu kuwasilisha nyaraka zake za umiliki.
   DC Hapi akitoa ufafanuzi wa changamoto mbalimbali,ambapo pia ametoa siku kumi 14  kwa ofisi ya Mkurugenzi kumletea nyaraka za soko la Bunju A ili ajiridhishe na kutoa maamuzi ya umiliki wa soko hilo kwa wananchi huku kwa mmiliki anayetajwa kuhodhi eneo hilo  ametoa siku  tatu ampelekee nyaraka zake za umiliki
  Baadhi ya Wakazi wa Bunju A wakimsikiliza DC Hapi alipokuwa akizungumza nao mapema leo na kusikiliza matatizo ya wananchi hao ikiwemo pia kuyapatia majibu.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Hapi akisoma baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na wakazi hao wa Bunju A mapema leo asubuhi,yakiwa na jumbe za changamoto zao wakihitaji kutatuliwa  0 0


  0 0

   Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imezindua muongozo utakaosaidia kuwahudumia watoto wachanga ( Neonatal Guideline) wenye umri kuanzia siku 0 hadi siku 28 ili kuhakikisha wanapata huduma inayostahiki.

  Muongozo huo umeandaliwa na madaktari wa MNH na kupitiwa na wadau mbalimbali wakiwemo wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) pamoja na Chuo Kikuu cha Kwazulu Natal kilichopo Afrika Kusini.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru amesema muongozo huo si tu unamanufaa kwa MNH bali pia una manufaa kwa hospitali zingine kwani utawezesha mtoto kupata tiba inayotakiwa hata sehemu ambazo hakuna watalaam.

  Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Watoto Edna Majaliwa ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Watoto Wachanga wa hospitali hiyo amesema kuwepo kwa muongozo huo kutasaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga sanjari na kupunguza rufaa za watoto hao kuletwa Muhimbili .
   Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza katika uzinduzi wa kitabu chenye mwongozo jinsi ya kutoa huduma ya afya kwa watoto wachanga wenye umri sufuri hadi siku 28. Uzinduzi huo umefanyika leo katika hospitali hiyo.
   Madaktari na wauguzi wakiwa kwenye mkutano wa kuzindua kitabu kinachoelezea jinsi ya kuwahudumia watoto wachanga baada ya kuzaliwa.
    Daktari wa watoto wa hospitali hiyo, Dk. Judith Cosmas ambaye ameshiriki kuaanda kitabu hicho akizungumza kwenye mkutano huo.
   Baadhi ya wataalamu wa afya wakiwa kwenye mkutano huo leo.
   Mkuu wa Idara ya Watoto, Dk. Merry Charles akisisitiza jambo huku akionesha kitabu hicho ambacho kitakuwa kikitumika wakati wa kuwahudumia watoto hao.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida amewataka watumishi wa umma wote mkoani hapa kulima ekari moja ya korosho ili kutunza mazingira, kujiongezea kipato pamoja na kuonyesha mfano kwa wananchi wengine ili waweze kulima zao hilo kwa ufanisi.

  Dkt Rehema Nchimbi ametoa agizo hilo mapema wiki hii mara baada ya kutembelea na kukagua shamba la mkulima wa zao hilo Juma Patrick katika kijiji cha Sanjaranda halmashauri ya wilaya ya Itigi.

  Dkt Nchimbi amesema kuongoza ni kuonyesha njia hivyo watumishi wa umma wanatakiwa kuonyesha njia kwa kulima vizuri hasa katika mazao ya biashara yanayopewa kipaumbele kitaifa ambapo kwa mkoa wa Singida ni korosho, pamba na tumbaku.

  “Watumishi hamuwezi kuwaambia wakulima walime korosho au pamba wakati wewe haujalima wala haufahamu changamoto na faida za kilimo hicho, naagiza kila mtumishi alime ekari moja ya korosho ili muwe mabalozi wazuri wa zao hilo mkoani hapa”, amesisitiza Dkt Nchimbi.
   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akisisitiza jambo wakati akikagua shamba la korosho la mkulima Juma Patrick wa Kijiji cha Sanjaranda halmashauri ya Wilaya ya Itigi.

   Mkulima Juma Patrick wa Kijiji cha Sanjaranda halmashauri ya Wilaya ya Itigi akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Singida mikorosho iliyostawi katika shamba lake.
   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Miraji Jumanne Mtaturu wakiwa katika shamba la korosho la mkulima Juma Patrick wa Kijiji cha Sanjaranda halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
  Shamba la mikorosho lenye ukubwa wa ekari 11 la mkulima Juma Patrick lililoko halmashauri ya Wilaya ya Itigi likiwa limestawi.


  0 0

  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, FortunatusMuslim akizungumza na waandishi habari hawapo pichani juu hatua ambazo wanazichukua kwa madereva wanakiuka sheria za usalama barabarani, leo jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
    MADEREVA saba (7) wa Mabasi yaendayo  mkoani wamefutiwa leseni zao pamoja na kufutiwa madaraja ya leseni hizo kutokana na kukiuka sheria za usalama barabarani.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, FortUnatus Muslim amesesema kuwa madereva saba hao wamekiuka sheria za usalama na kwa mamlaka yake amefuta leseni zao kwa kipindi cha miezi sita na wanatakiwa kurudi darasani kwa kipindi cha miezi hiyo na kuhakikiwa upya kupewa leseni hizo.

  Amesema kuwa madereva hao walikuwa wakiendesha mabasi kilomita 90 kwa saa ambapo kikosi cha usalama barabarani kiliweka  mahabusu  na kulipa faini kati ya sh. 100,000 hadi sh. 300,000 na kupoteza sifa za kuwa madereva.

  Muslim amasema kwa mamlaka aliyopewa kwa anafuta leseni hizo kwa madaraja ya C na E kwa madereva ili warudi kusoma juu ya jinsi ya kujihami wanavyoendesha vyombo vya moto vva abiria na mizigo kibiashara kwa miezi sita hiyo.

  Madereva hao Hamad Salum,  Kija Mayenga, Isack Mbijina, Hassan Semazua, Stanley Mosha, Abdallah Hussein yuko mahabusu kwa kokosa kulipa faini pamoja na Sempunda Yusufu.

  Aidha madereva watatu wamefungiwa leseni zao za kubeba abiria kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kusababisha ajali.

  Madereva hao Ismail Nyami alisababisha ajali iliyoua watu wawili na kujeruhi 42 iliyotokea Septemba 23 mkoani Ruvuma mkoani Ruvuma ,, Mseka Salum alisababisha ajali iliyoua  Mtu mmoja  na kujeruhi 25 Kishapu mkoani Shinyanga, Malick Hassan alisababisha ajali kwa kugonga Ng’ombe  na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi Sita.

  Muslim amesema kuwa operesheni zitaendelea kuendesha hadi majira ya usiku hivyo madereva wazingatie sheria za usalama barabarani.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Glogu ya  jamii  
   MAFUNZO ya elimu ya ufundi yananafasi kubwa ya kuongeza, kusaidia  na kukuza ajira kwa vijana wanaosoma masomo hayo kwenye vyuo vya ufundi  kwa kuajiriwa au kujitengenezea ajira wao wenyewe.

  Kaimu katibu mtendaji wa baraza la taifa elimu ya ufundi (Nacte), Dkt, Adolph Rutayuga amesema hayo leo jijini dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya mradi wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO.

  Akizungumza kwa niaba ya Katibu mkuu wizara ya elimu,sayansi na teknolojia,Dkt,Rutayuga amesema nia kubwa ya mradi huo ni kuangalia ufundi unaumuhimu gani kwenye sekta ya uchumi hasa unapozungumzia sekta ya uchumi wa viwanda.

  Aidha tunaangalia ubora wa mafunzo yanayotolewa kwenye elimu ya ufundi sababu kukiwa na vyuo vingi ambavyo vinaendeshwa katika ubora usiotakiwa, wanafunzi wanaotoka kwenye vyuo hivi hawatakuwa wazuri.

  “Tunalenga kujenga mazingira ya kutoa mafunzo bora kwenye elimu ya ufundi, elimu iliyobora kwa kusapoti walimu wanaofundisha,miundombinu ya kujifunza na kufundishia na pia kujaribu kuangalia mahusiano yaliyopo kati ya viwanda na soko la ajira kwa kile kinachotolewa kwenye vyuo vya ufundi.

  Ameongeza,kama suala zima la mambo ya mitaala, linaweza kuboreshwa, na ile dhana potufu ya kizamani iliyokuwepo kwamba kwamba Tivet ni kwa wale walioshindwa,inapaswa iondoke, watu wajue kwamba mchango mkubwa kwenye uchumi unafanywa na hawa watu kwenye sekta ya kati

  “Malengo makubwa ni kujaribu kuinua ubora wa mafunzo yanayotolewa na vyuo vya ufundi, kuinua umuhimu  mafunzo ya ufundi na Jinsi inavyoweza kisaidia kwenye maendeleo ya kukuza uchumi”,amesema.

  Naye, Afisa kiongozi wa Unesco nchini Axel Plathe amesema warsha hiyo itajadili kwa undani vitendo vya ufanisi, utekelezaji na jukumu la uwezo ambao kila wadau watafanya katika mradi uliopendekezwa chini ya maeneo matatu umuhimu, ubora na mtazamo wa elimu na ujuzi wa kiufundi.

  “Elimu bora kwa Afrika itatekelezwa kuanzia mwaka huu hadi 2021 kwa lengo la kukuza elimu na ujuzi wa kitaaluma na mafunzo ambayo ni muhimu kwa mahitaji ya soko la ajira na mahitaji ya watu binafsi na jamii”amesema Plathe.

  Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Lutayuga akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wakati wa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Unesco ya kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam leo.
   Afisa  Kiongozi wa UNESCO Dar es Salaam, Alex Plante akizungumza washiriki wa warsha ya kuzindua Mradi wa mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. 

   Baadhi ya washririki wa Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam leo.
   Mwakilishi wa UNESCO Dar es Salaam, Alex Plante,na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Lutayuga wakiwa katika picha ya pamoja na  washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa  kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  0 0

  Afisa wa NIDA Wilaya ya Ikungi Agness Mtei akimpa maelekezo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ya namna vitambulisho vya Taifa vinavyotengenezwa mara baada ya kuzinduzi zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa.

  Na Mathias Canal, Singida.

  Zoezi linalotekelezwa na serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi la usajili na utambuzi wa watu wanaoishi katika Wilaya ya Ikungi wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea limezinduliwa rasmi huku wananchi wakihamasishwa kutoa ushirikiano katika zoezi Hilo. 

  Zoezi Hilo litatekelezwa katika awamu nne ambapo katika awamu ya kwanza utekelezaji wake utakuwa katika Tarafa ya Ikungi yenye Kata sita kwa wananchi wapatao 45,599, Awamu ya Pili itakuwa Ni Tarafa ya Sepuka yenye Kata Saba na wananchi wakiwa Ni 49,035, Awamu ya Tatu Ni Tarafa ya Ihanja yenye Kata nne huku wananchi wakiwa 54,887 na awamu ya nne itakuwa katika Tarafa ya Mungaa yenye Kata Saba na jumla ya wananchi wapatao 35,311. 
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi.

  Akizungumza Katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi kwenye uzinduzi wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa zoezi Hilo linalenga kupata taarifa sahihi za watu zitakazotumiwa na mifumo Yote ya serikali na binafsi kubadilishana taarifa kwa lengo la kuboresha Huduma na kuinua hali za watu kutoka kipato Cha chini kwenda Cha Kati. 

  Alisema umuhimu wa zoezi Hilo Ni Kuimarisha ulinzi na usalama wa Nchi hususani maeneo ya mipakani, Wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji Mali hususani Biashara, usalama katika miamala ya kibenki pamoja na kuwezesha wananchi kukopeshana kirahisi, Upatikanaji kirahisi wa pembejeo na zana za Kilimo, na Wananchi katika Kaya maskini kutambulika haraka na kupata misaada kupitia TASAF. 
  Maafisa wa NIDA Wilaya ya Ikungi wakiwasalimu wakazi wa kijiji na Kata ya Dung'unyiwakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika. Kulia ni Agness Mtei, Doris Niyukuri na Mary Maputa.

  Umuhimu mwingine Ni Upatikanaji wa mikopo ya elimu ya just, Kupunguza ukiritimba katika upatikanaji wa Huduma za Jamii na Kupunguza serikali gharama za kusafirisha daftari la wapinga kura na kuwa na daftari lenye taarifa sahihi za watu na mahali walipo. 

  BOFYA HAPA HABARI NA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 1932 | 1933 | (Page 1934) | 1935 | 1936 | .... | 3272 | newer