Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

BODI YA WADHAMINI YA TANAPA IKIONGOZWA NA MWENYEKITI WAKE JENERALI (MSTAAFU) WAITARA YATEMBELEA HIFADHI YA KATAVI

$
0
0
BODI ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa bodi, Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara, leo Septemba 28, 2017 imetembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa ajili ya kukagua utendaji kazi ambapo ilipata fursa ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Hifadhi Izumbe Msindai.

Bodi imepongeza utendaji kazi katika Hifadhi ya Katavi hususani suala zima la kupambana na ujangili na juhudi zinazofanywa katika kuongeza idadi ya watalii hifadhini.Aidha, Jenerali Waitara aliutaka uongozi wa hifadhi kuongeza jitihada katika kukabiliana na changamoto za mifugo ambayo ni kubwa kwa Katavi na pia alipongeza uongozi wa mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali mstaafu Raphael Muhuga kwa ushirikiano mkubwa anaotoa kwa hifadhi katika kupambana na mifugo hifadhini.

Mapema kabla, bodi iliweza kutembelea kituo cha mafunzo cha Mlele na kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Kituo Mhifadhi Genes Shayo na kupata nafasi ya kuongea na askari wapya wanaoendelea na mafunzo katika kituo hicho.

Jenerali Waitara aliwataka askari hao kuwa na nidhamu, uwajibikaji, bidii na uzalendo katika mafunzo yao na kuwa ni lazima waonyeshe kuiva ili waweze kupambana vilivyo na changamoto ya ujangili katika Hifadhi za Taifa nchini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), na wajumbe wa bodi hiyo, wakikaribishwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Katavi, Mhifadhi Izumbe Msindai, walipowasili kwenye hifadhi hiyo leo Septemba 28, 2017. 

Jenerali Waitara, akionyesha kitu wakati yeye na wajumbe wa bodi walipotembelea enelo wanakohifadhiwa Viboko

Jenerali Waitara akizungumza na askari wanaopatiwa mafunzo kwenye kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi


Baadhi ya wajumbe wa bodi waliofiatana na Jenerali Waitara
Baadhi ya askari wanaopatiwa mafunzo ya ulinzi wa wanayamapori kwenye kituo cha mafunzo cha Mlele wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi za Taifa, (TANAPA), Jenerali mstaafu George Marwa Waitara (hayupo pichani), alipowatembelea leo Septemba 28, 2017


ASILIMIA 75% YA NCHI WANACHAMA WA INTERPOL, YAKUBALI KUJIUNGA KWA PALESTINA KATIKA TAASISI HIYO

$
0
0
Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Polisi wa kimataifa wa kuzuia uhalifu wa kijinai “Interpol”, umekubali kujiunga kwa Palestina katika taasisi hiyo,baada ya nchi wanachama 75 kulipigia kura ya ndio azimio hilo. Interpol imethibitisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa, Palestina na visiwa vya Solomon kuanzia sasa ni miongoni mwa wanachama wake.

Interpol ni taasisi kubwa zaidi ya kipolisi wa kimataifa iliyoasisiwa mwaka 1923, inajumuisha masuala ya nchi wanachama 190,huku makao makuu yake yakiwa mjini Lyon nchini Ufaransa.Aidha Interpol imekubali uanachama wa Palestina mnamo siku ya jumatatu iliyopita jioni kufuatia ombi la nchi hiyo, kabla ya kulijumuisha katika ajenda zake zitakazopigiwa kura katika Mkutano wake Mkuu,ambao uliketi nchini China Jumatano iliyopita na kuikubalia Palestina ombi lake hilo.

Kwa upande mwingine,Israeli na Marekani zilijaribu kukwamisha hatua hiyo ya kukubaliwa uanachama wa Palestina katika Interpol, kwa kutumia mashinikizo kadhaa juu ya taasisi hiyo ili isikubali ombi la Palestina kuwa mwanachama.

Wakati huo huo, Dr.Riyad Al-Maliki ambae ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina, amepongeza hatua ya kuipigia kura ya ndio nchi yake na hatimae kukubaliwa uanachama wa Interpol,kupitia mkutano wake mkuu uliofanyika mjini Beijing nchini China. Amesisitiza kuwa hatua hiyo inathibitisha kuaminika uwezo wa Palestina katika kutekeleza sheria,dhamira halisi na maadili muhimu ya Interpol.

Waziri pia ameashiria kupatikana kwa ushindi huo,kumetokana na msimamo wa awali wa idadi kubwa ya nchi wanachama wa Interpol, iliyotetea sababu ya kuwepo kwa taasisi hiyo na kanuni zake za msingi,pale zilipokataa waziwazi kuupa nafasi ubabe wa kisiasa utawale. Huku waziri akiongeza kusema:"Leo haki na kanuni zimeshinda mambo mengine yote"."Leo, ukweli na kanuni zimeshinda mambo mengine yote.

Dr.Riyad Al-Maliki kwa niaba ya taifa la Palestina,amezishukuru nchi wanachama zilizoiunga mkono Palestina katika jitihada zake,huku akitilia mkazo kuendelea kwa nchi yake katika jitihada za kujiongezea hadhi na nafasi mbalimbali kimataifa,ikiwa ni pamoja na kutetea haki za Wapalestina,uhuru na amani yao kwa njia ya kidiplomasia na kisheria, ikiwa ni pamoja na kujiunga na taasisi husika za kimataifa.

Kwa mnasaba huu pia, Waziri Al-Maliki amesisitiza ahadi ya nchi yake ya Palestina katika kutimiza majukumu yake ya kuchangia kupambana na uhalifu na kuimarisha utawala wa sheria katika ngazi ya kimataifa. Huku ikishirikiana na nchi wanachama wa Interpol katika kukuza hadhi na nafasi ya taasisi hiyo, ushiriki wa kidhati kabisa wa kimataifa dhidi ya uhalifu unaohatarisha maisha wananchi na mustakabali wao duniani.

Aidha ameongeza kusema: "Nchi ya Palestina inauchukulia uanachama huu na majukumu yake kama ni sehemu ya wajibu wake kwa Wapalestina,pia ni wajibu wa kimaadili kwa walimwengu wote. Palestina ipo tayari na inaweza kubeba majukumu na wajibu huu kama mshirika wa dhati katika jamii ya kimataifa,itachangia hasa kuendeleza maadili yetu ya msingi ya pamoja kama mataifa. " 
Mwakilishi wa Palestina akipokea bendera kutoka kwa Rais wa Interpol Bw. Meng Hongwei kuashiria uanachama kamili wa Palestina ndani ya Taasisi ya Polisi ya Kimataifa ya kuzuia uhalifu wa kijinai duniani.

Article 9

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 29,2017

MAADHIMISHO YA SIKU YA MOYO DUNIANI TAASISI YA MOYO (JKCI) KUFANYA UPIMAJI KWA WANANCHI BILA MALIPO

$
0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) katika kuadhimisha siku ya Moyo Duniani watafanya upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa jirani. Upimaji huo utaenda sambamba na utoaji wa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.

Upimaji huu utafanyika katika viwanja vya Taasisi ya Moyo ambapo wananchi watapimwa urefu, uzito, shinikizo la damu (BP), sukari na kupewa ushauri. Kwa wale watakaokutwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu. Kauli mbiu ya siku hii ni: “Moyo wenye Afya”.

Katika wiki hii ya maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani tuna kambi maalum ya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua ambayo imeanza tarehe 25/09/2017 hadi tarehe 29/09/2017. Kambi hii tunaifanya kwa kushirikiana na Taasisi ya Madaktari Afrika ya nchini Marekani.

Hadi sasa tayari tumewafanyia upasuaji wa bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa Cathlab (kwa jila la kitaalam Cathertarization) wagonjwa 23, siku ya kesho tutamalizia kuwafanyia upasuaji wagonjwa watano ili kufiokia idadi ya wagonjwa 28 tuliyolenga. Nia ya kambi hii ni kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa na kubadilishana uzoefu wa kazi.

Wafanyakazi wa Taasisi hii tunahakikisha tunatoa huduma bora zaidi za magonjwa ya moyo kwa wananchi wenye matatizo hayo. Mpango wetu ni kutoa tiba ya moyo, upasuaji wa moyo na elimu kwa jamii ambayo itawasaidia wananchi kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusiana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na mtu anaweza kuyaepuka kwa kufuata ushauri wa kitaalam.

Tangu mwaka 2015 tumewafanyia upasuaji wa kupasua kifua, kuziba mishipa ya moyo, upasuaji wa mishipa ya moyo, upasuaji wa mishipa ya damu, kuweka vyuma ndani ya moyo, na kuweka kifaa maalum cha kuusaidia moyo ili uweze kufanya kazi vizuri (Pacemaker) zaidi ya wagonjwa 1500.

Hatua hiyo imewezesha Serikali kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 45 fedha ambazo zingetumika kuwatibia wagonjwa wa moyo iwapo wangepelekwa njje ya nchi, hii ni sawa na asilimioa 85.Taasisi pia inatoa huduma ya uchunguzi wa kipimo cha magonjwa ya moyo kwa watoto wachanga waliopo tumboni mwa mama zao (FETAL ECHOCARDIOGRAPHY) ili kujuwa kama wanamatatizo ya moyo au la.

Tangu kuanza kutolewa kwa huduma hii mwezi wan ne mwaka huu jumla ya kinamama wajawazito 37 wameshafanyiwa uchunguzi wa kipimo hicho kati ya hao watoto watano walikutwa na matatizo ya moyo jambo ambalo litawawezesha kupata matibabu mapema pindi watakapozaliwa.

Tunawaomba wananchi waadhimishe siku hii kwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao hii itawasaidia kujuwa kama wanamatatizo ya moyo au la na hivyo kuanza matibabu mapema kwani asilimia kubwa ya wagonjwa tunaowapokea mioyo yao huo haiku katika hali nzuri.


Imetolewa na :

Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

MTENDAJI MKUU WA TFS, PROF. DOS SANTOS SILAYO AFANYA ZIARA WILAYANI MKURANGA KWA AJILI YA KUIMARISHA UHIFADHI NA KUJADILI MIKAKATI YA KUZUIA WAVAMIZI KWENYE MISITU WA HIFADHI

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo alimpomtembelea jana Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga ofisini kwake akimuonesha baadhi ya maeneo kwenye ramani jinsi vyanzo vya maji vilivyoharibika kutokana na tabia ya baadhi ya wananchi kuvamia kwa kuanzisha shughuli za kibinadamu katika Hifadhi za Misitu. Mwingine ni Meneja Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wa Wilaya ya Mkuranga Christina Mohamed
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo akiteta neno na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga wakati wa ziara ya kujionea jinsi wananchi walivyovamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu katika Hifadhi za Msitu wa Vikindu.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo kuu akisaini jana kitabu cha wageni mara alipotembelea ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga ikiwa lengo la ziara hiyo ni kujadili mikakati ya kuzuia wavamizi kwenye msitu wa hifadhi
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akimuonesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo baadhi ya maeneo ya Hifadhi yaliyovamiwa na kuanzishwa shughuli za kibinadamu katika Hifadhi ya Msitu wa Vikindu. Lengo la ziara Mtendaji Mkuu wa TFS hiyo ilikuwa ni kuimarisha uhifadhi kwa kujadili mikakati ya kuzuia wavamizi kwenye msitu wa hifadhi

"Mafunzo ya Elimu ya ufundi yana nafasi ya kukuza ajira"- Rutayuga

$
0
0

 Kaimu katibu mtendaji wa baraza la taifa elimu ya ufundi (Nacte), Dkt, Adolph Rutayuga amesema hayo jana  jijini dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya mradi wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO.
 
Akizungumza kwa niaba ya Katibu mkuu wizara ya elimu,sayansi na teknolojia, Dkt, Rutayuga amesema nia kubwa ya mradi huo ni kuangalia ufundi unaumuhimu gani kwenye sekta ya uchumi hasa unapozungumzia sekta ya uchumi wa viwanda. Aidha tunaangalia ubora wa mafunzo yanayotolewa kwenye elimu ya ufundi sababu kukiwa na vyuo vingi ambavyo vinaendeshwa katika ubora usiotakiwa, wanafunzi wanaotoka kwenye vyuo hivi hawatakuwa wazuri. 
 
“Tunalenga kujenga mazingira ya kutoa mafunzo bora kwenye elimu ya ufundi, elimu iliyobora kwa kusapoti walimu wanaofundisha,miundombinu ya kujifunza na kufundishia na pia kujaribu kuangalia mahusiano yaliyopo kati ya viwanda na soko la ajira kwa kile kinachotolewa kwenye vyuo vya ufundi.
 
 Ameongeza,kama suala zima la mambo ya mitaala, linaweza kuboreshwa, na ile dhana potufu ya kizamani iliyokuwepo kwamba kwamba Tivet ni kwa wale walioshindwa,inapaswa iondoke, watu wajue kwamba mchango mkubwa kwenye uchumi unafanywa na hawa watu kwenye sekta ya kati “Malengo makubwa ni kujaribu kuinua ubora wa mafunzo yanayotolewa na vyuo vya ufundi, kuinua umuhimu mafunzo ya ufundi na Jinsi inavyoweza kisaidia kwenye maendeleo ya kukuza uchumi,” amesema. 
 
Naye, Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe amesema warsha hiyo itajadili kwa undani vitendo vya ufanisi, utekelezaji na jukumu la uwezo  ambao kila wadau watafanya katika mradi uliopendekezwa chini ya maeneo matatu umuhimu, ubora na mtazamo wa elimu na ujuzi wa kiufundi. “Elimu bora kwa Afrika itatekelezwa kuanzia mwaka huu hadi 2021 kwa lengo la kukuza elimu na ujuzi wa kitaaluma na mafunzo ambayo ni muhimu kwa mahitaji ya soko la ajira na mahitaji ya watu binafsi na jamii”amesema Plathe. Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii .
Mafunzo ya elimu ya ufundi yananafasi kubwa ya kuongeza, kusaidia na kukuza ajira kwa vijana wanaosoma masomo hayo kwenye vyuo vya ufundi kwa kuajiriwa au kujitengenezea ajira wao wenyewe.
Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe akizungumza washiriki wa warsha ya kuzindua Mradi wa mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam jana . Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Rutayuga akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wakati wa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Unesco ya kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washririki na Meza kuu wakiwa katika warsha ya uzinduzi wa Mpangowa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

WATANZANIA WANG'ARA SHINDANO LA MWANDISHI BORA WA SAYANSI NA KILIMO AFRIKA

$
0
0
Mwandishi wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu ameshinda tuzo ya umahiri wa habari za sayansi katika eneo la magazeti huku akiwaashinda waandishi wengine kutoka nchi zingine saba za Afrika.

Kitabu alikuwa anachuana na waandishi kutoka nchi za Nigeria, Burkina Faso, Ghana, Ethiopia, Kenya, Tanzania na Uganda. Shindano hilo lilifanyika jana katika Hoteli ya Speke Resort Munyonyo iliyoko nje kidogo ya jiji la Kampala.

Kwa ushindi huo, Kitabu ambaye ni mshindi wa jumla wa shindano la Tanzania, alijinyakulia kitita cha dola za marekani 1,500 pamoja na simu aina ya iPhone 7+ yenye thamani za dola za Marekani 1,200. 

Mwandishi mwingine wa Tanzania aliyepata tuzo ni Koleta Makulwa kutoka Radio Free Afrika ambaye aliwashinda waandishi wengine ambao walikuwa wanashindana katika eneo la Radio. ambapo Tanzania ilizidi kung'ara baada ya Mwandishi wa Star Tv Dino Mgunda kuwa mshindi wa pili katika waandishi wa televisheni. 

Koleta aliondoka na kitita cha dola za Marekani 1,500, simu aina ya iPhone 7+ ya thamani ya dola za marekani 1,200 wakati Dino Mgunda alipata zawadi ya dola za marekani 1,000 na simu ya iPhone7+ ya thamani ya dola za marekani 1,000.

Katika shindano hilo jumla ya waandishi 20 waliwakilisha nchi hizo. waandishi hao ni wale ambao walikuwa washindi katika shindano la nchi mahalia, shindano ambalo lilifanyika mwanzoni mwa wiki hii katika nchi hizo ikiwemo tanzania. 

Shindano hilo liliandaliwa na Jukwaa la wazi la Bioteknolojia za Kilimo (OFAB) ambalo linahamasisha matumizi ya bioteknolojia katika kilimo ili kuwezesha nchi za Afrika ziweze kujitosheleza kwa chakula.Mshindi wa jumla katika shindano hilo la jana ni mtangazaji wa kituo cha TVC, Omolara Afolayan kutoka Nigeria. Washindi waliteuliwa na jopo la majai watano.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona (kushoto), akimkabidhi cheti Mwandishi wa Star Tv Dino Mgunda kuwa mshindi wa pili kwa waandishi wa Televisheni kwenye shindano hilo lililofanyika jana nchini Uganda.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona, akimkabidhi cheti Mwandishi wa Tanzania Koleta Makulwa kutoka Radio Free Afrika ambaye alipata tuzo na kuwashinda wenzake ambao walikuwa wanashindana katika eneo la Radio.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona, akimkabidhi cheti Mwandishi wa Tanzania wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu ambae alishinda tuzo ya umahiri wa habari za sayansi katika eneo la magazeti huku akiwaashinda waandishi wengine kutoka nchi zingine saba za Afrika. 
Keki ikikatwa katika hafla hiyo


PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA NCHI 21 DUNIANI KWA AJILI YA KUJADILI UKUKUZAJI WA SEKTA YA UPANDAJI WA MITI KIBIASHARA

$
0
0
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. Aliwataka wajumbe hao kujadili namna ya kuwawezesha wakulima wa miti wakati wanasubiri kuvuna mazao yao waweze kujishuulisha na kilimo cha mazao ya muda mfupi kwa kutumia mbinu bora za kisayansi ili waweze kujikimu kimapato.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. 
Baadhi ya wajumbe kutoka nchi 21 duniani wakifuatilia mkutano huo. Nchi hizo ni Burkina Faso, Chad, Ethiopia, Gambia,Ghana, Italy, Mali, Niger, Nigeria, Senegal, Sudan, Liberia, Cameroon, Swaziland, Finland, Zambia, Canada,Mozambique, Zimbabwe, Kenya na Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Steven Kebwe akizungumza katika mkutano huo. Aliwataka wajumbe wa mkutano huo kujadili na kuishauri dunia namna bora ya kutunza na kuendeleza misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho ikiwemo utekelezaji wa sheria za usimamizi wa misitu.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wajumbe kujadili kwa uwazi kuhusu mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto za sekta ya misitu na kwamba Serikali kupitia Wizara itapokea maoni na mapendekezo yao kwa ajili ya kuyafanyia kazi ili kuimarisha ustawi wa sekta hiyo. 

MBUNGE AZZA HILAL AWAPIGA JEKI WANAFUNZI WENYE ULEMAVU SHULE YA MSINGI ALIYOSOMA SHINYANGA

$
0
0
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) ametembelea shule ya msingi aliyosoma Tinde iliyopo katika kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga kisha kutoa msaada kwa wanafunzi nane wenye ulemavu wa viungo akiwemo kijana ambaye hawezi kuongea wala kutembea. Mbunge huyo ametembelea shule hiyo jana Jumatano Septemba 27,2017. 

Mheshimiwa Hilal ametoa msaada wa baiskeli kwa kijana ambaye hawezi kutembea wala kuongea anayesoma katika shule hiyo huku akijitolea kuwanunulia wanafunzi hao nane mahitaji yao yote ya shule mpaka watakapomaliza masomo yao ya shule ya msingi. 

“Hii shule nimesoma,baada ya kufika hapa nimeambiwa kuna watoto wenye ulemavu,baada kumuona kijana huyu nimempatia baiskeli lakini pia nimejitolea kuwahudumia wanafunzi hawa wanane ambao wana ulemavu wa viungo,nitawanunulia mahitaji yao ya shule na watakuwa wanakunywa uji kila siku kwa gharama zangu”,ameeleza Mbunge huyo. 

Mbali na kutoa msaada huo Mheshimiwa Azza Hilal ameshiriki zoezi la Upandaji miti katika wilaya ya Shinyanga lililoanzishwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro lenye kauli mbiu ya "Shinyanga Mpya, Mti Kwanza". 

Akiwa katika kata ya Tinde,mbunge huyo aliungana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kupanda miti katika shule ya msingi Tinde,pia katika barabara kuu ya kutoka Tinde kwenda Kahama na barabara ya kutoka Tinde kwenda Nzega mkoani Tabora.
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi mwenye ulemavu (hatembei wala haongei) katika shule ya msingi Tinde-Picha na Said Nassor-Malunde1 blog Tinde
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi mwenye ulemavu wa viungo katika shule ya msingi Tinde,aliyeshikilia kipaza sauti ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro.

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAKAZI DUNIANI

$
0
0
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itajumuika na Ulimwengu wote kuadhimisha Siku ya Makazi Duniani, tarehe 02 Oktoba, 2017 – Karimjee Hall, ambapo Wadau mbalimbali wanategemewa kujumuika katika hafla hiyo, itakayoambatana na Maonyesho. 

Siku ya Makazi Duniani huadhimishwa duniani kote kila Jumatatu ya kwanza ya mwezi Oktoba. Lengo kuu la maadhimisho haya ni kutoa mwongozo kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutafakari kwa pamoja masuala yanayohusu makazi ulimwenguni kwa kuangalia changamoto mbalimbali zilizopo na kushirikishana mbinu na mikakati ya kupambana nazo. 

Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Makazi Duniani – UN-HABITAT hutoa mwongozo kupitia kauli mbiu ambayo huongoza tafakari hiyo duniani kote. Mwaka huu maadhimisho hayo, ambayo ni ya 32 yanafanyika kwa kuongozwa na Kauli Mbiu isemayo “Housing Policies”: Affordable Homes: Tafsiri ya kauli mbiu hiyo ni “Sera za Nyumba: Nyumba za Gharama Nafuu: Kauli mbiu hii inaelekeza kutafakari namna tunavyoweza kutunga Sera za Nyumba katika nchi zetu zinazojielekeza kutatua changamoto ya upatikanaji wa nyumba, hususan za gharama nafuu ili kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini waweze kumudu kujenga, kununua ama kupanga. 

Madhumuni ya Maadhimisho ya Siku ya Makazi kufuatana na kauli mbiu ya mwaka huu Oktoba, 2017 ni kuhakikisha kuwa Sera zetu za Nyumba na Makazi zinazingatia yafuatayo: 

· Kuwa na Nyumba na Makazi bora yenye huduma za msingi za jamii toshelezi (Inclusive housing and social services),

· Kuwa na mazingira salama ya kuishi kwa wananchi wote, hususan wenye mahitaji maalum wakiwemo watoto, vijana, wanawake, wazee na wenye ulemavu (A safe and healthy living environment for all — with particular consideration for children, youth, women, elderly and disabled),

· Upatikanaji wa usafiri na nishati endelevu zenye gharama nafuu (Affordable and sustainable transport and energy),

· Kukuza, kulinda na kuhifadhi maeneo ya wazi mijini (Promotion, protection, and restoration of green urban spaces),

· Upatikanaji wa maji safi na salama ya kunywa na mfumo thabiti wa uondoshaji majitaka (Safe and clean drinking water and sanitation),

· Uwepo wa hewa safi na ya kutosha (Healthy air quality),

· Kuwepo fursa za ajira (Job creation) ,

· Kuimarisha upangaji miji na kuboresha makazi duni (Improved urban planning and slum upgrading),

· Kuwepo na mfumo thabiti wa usimamizi wa taka (Better waste management)

Kaulimbiu iliyotolewa kwa mwaka huu, pia inahimiza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutumia ngazi zote za Serikali pamoja na wadau wote muhimu kutafakari nanma ya kuibua mikakati ya kuwezesha uwepo wa nyumba bora na za gharama nafuu katika nchi zao ikiwa ni utekelezaji wa mojawapo ya Agenda Mpya ya Makazi Duniani iliyoidhinishwa Quito, Oktoba, 2016 na Malengo Endelevu ya Milenia. 

Chimbuko la maadhimisho hayo ni Azimio Namba 40/202 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwezi Desemba mwaka 1985 na kuanza kuadhimishwa rasmi mwaka 1986. 

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI


Airtel yatoa mafunzo ya TEHAMA kwa Walimu Dar

$
0
0
Kampuni yasimu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) imeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa waalimu katika maabara ya kompyuta iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama Manispaa ya Kinondoni.

Mafunzo hayo kwa waalimu yameanza kufuatia Airtel na DTBi kutangaza kuanza kwa mafunzo hayo na kuwaalika vijana kuanzia ngazi ya shule za msingi,sekondari, vyuo vikuu na wafanya biashara kujiandikisha na kufaidika na mafunzo haya yatakayowasaidia kuvumbua application mbalimbali, kuwapatia vijana ujuzi katika mswala ya Tehama na pia kuwawezesha vijana wajasiriamali kuendesha shughuli zao za kibiashara kwa kutumia technologia za kisasa

Akiongea kuhusu kuanza kwa mafunzo hayo, Meneja Mradi wa Airtel Bi Jane Matinde alisema,‘Hapo awali tulikuwa tumeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa wanafunzi lakini tumeona ni bora na waalimu wa hapa shule hii Kijitonyama nao waanze kupata mafunzo. Hii itasaidia kwani kwa baadae ndio watakaokuwa wakitoa mafunzo kwa wanafunzi na hii itatupa nafasi ya kuendelea kuwezesha shule zingine.

Waalimu wamepokea hatua hii kwa furaha na wanao hamasa kubwa kwenye mafunzo. Hii inathibitisha nia ya kampuni ya Airtel ya kutoa fursa kwa kila Mtanzania, aliongeza Matinde.

Hata hivyo, Matinde alisema kuwa mafunzo kwa wanafunzo ambao walikuwa washaanza yataendelea vile vile. ‘Utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wale wanafunzi ambao walikuwa washaanza utaendelea vile vile. Kilichofanyika ni chukua hatua ya ziada ya kuwapa walimu mafunzo ya Tehama ili nao waweze kuwa kwenye nafasi ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi hawa’ alisema Matinde.

Matinde aliongeza kuwa bado tunapokea maombi ya kujiunga hivyo tunatoa wito kwa vijana wa sekondari , wale waliomaliza darasa la saba , wafanyabiashara kutumia vyema maabara hii yenye lengo la kuwezesha jamii hususani vijana kuongeza ujuzi na ueledi kwenye maswala ya technologia na Tehama kwa ujumla.

Kwa upande wake Meneja wa maabara ya Airtel Fursa, Agape Jengela alisema “ Tayari tumejipanga kutoa mafunzo kwa walimu wa shule ya Kijitonyama. Tuhahakisha kuwa walimu wamepata mafunzo na kuelewa kabisa ili nao waanze kutoa mafunzo na elimu kwa wanafunzi.

Jengela alisema mafunzo hayo ni pamoja na lego Robotics, program za uhuishaji kwa watoto(ziitwazo scratch) na ubunifu na uchapishaji wa“3D objects” msingi wa kompyuta, uelewa wa kompyuta, kutengeneza program mbali mbali

Bado tunapokea maombi, Tunato wito kwa wazazi na walezi kuwaandikisha vijana wao kwa kupitia www.teknohama.or.tz na www.airtelfursa.com au kwa kutembelea maabara iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama.
Meneja Matukio wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kushoto) akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” Dar es Salaam jana. 
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” Dar es Salaam jana.

Alihassan with Greenbird Highschool Inter-classes Three times back-to-back Champions

$
0
0

The Greenbird Highschool Inter-classes Three times back-to-back Champions at Mwanga in Kilimanjaro region. The guy in yellow socks is Alihassan you can see below collecting his Best Standard two Student Award at St. Patric's Primary school in Arusha in October 2005.

KIDZ WORLD PARTY ACCESSORIES

$
0
0



We are located at Dar free market mall, 1st floor Oyster Bay, Ally Hassan Mwinyi Road, Dar es salaam near the embassies of Kenya and France. 
Call or  whatsapp ☎📞📱+255 714 660 559, Or +447737823787.     
 Opening hours (Muda wa kazi): Mon-Sat:10am-8pm.  Sunday: 10am-6pm. 
Tunapokea order na kutuma mikoani. #putsmileonkidswithus     
 #giftsolutionitsherenow @kidzworld6 #productfromuk @kidzworld6 @rm_kidzworld

ZOGO BUNGENI UGANDA


IGP SIRRO AKABIDHIWA RAMANI YA NYUMBA ZA POLISI ZITAKAZOJENGWA ARUSHA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wapili kulia), akimkabidhi Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro (katikati), mchoro wa ramani ya nyumba za Polisi za kisasa zitakazojengwa kufuatia za awali kuteketea kwa moto. Hatua ya ujenzi imeanza mara moja kufuatia Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, kutoa kiasi cha shilingi milioni 260 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Hanspaul, Kamaljit Singh, na kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (DCP) Charles Mkumbo na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Wakala ya Majengo Arusha Bw. Victor,. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akiagana na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, alipomtembelea ofisini leo tayari kwa safari ya kurejea Dar es salaam, baada ya kuwapapole na kukagua eneo la nyumba za Polisi zilizoteketea kwa moto. Picha na Jeshi la Polisi.

Airtel yatoa mafunzo ya TEHAMA kwa Walimu Dar

$
0
0
Kampuni yasimu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi)  imeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa waalimu katika maabara ya kompyuta iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama Manispaa ya Kinondoni. 
Mafunzo hayo kwa waalimu yameanza kufuatia Airtel na DTBi kutangaza kuanza kwa mafunzo hayo na kuwaalika vijana kuanzia ngazi ya shule za msingi,sekondari, vyuo vikuu na wafanya biashara kujiandikisha na kufaidika na mafunzo haya yatakayowasaidia kuvumbua application mbalimbali, kuwapatia vijana ujuzi katika mswala ya Tehama na pia kuwawezesha vijana wajasiriamali kuendesha shughuli zao za kibiashara kwa kutumia technologia za kisasa. 
Akiongea kuhusu kuanza kwa mafunzo hayo, Meneja Mradi wa Airtel Bi Jane Matinde alisema,
‘Hapo awali tulikuwa tumeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa wanafunzi lakini tumeona ni bora na waalimu wa hapa shule hii Kijitonyama nao waanze kupata mafunzo. Hii itasaidia kwani kwa baadae ndio watakaokuwa wakitoa mafunzo kwa wanafunzi na hii itatupa nafasi ya kuendelea kuwezesha shule zingine.
Waalimu wamepokea hatua hii kwa furaha na wanao hamasa kubwa kwenye mafunzo. Hii inathibitisha nia ya kampuni ya Airtel ya kutoa fursa kwa kila Mtanzania, aliongeza Matinde.
 Meneja Matukio wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kushoto) akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” Dar es Salaam leo.
 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” Dar es Salaam leo.

 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” Dar es Salaam leo/

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” Dar es Salaam leo.

MAADHIMISHO YA SIKU YA MOYO DUNIANI YAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Muakilishi wa Jimbo la Mpendae Said Mohd Dimwa wapili kushoto akifuatana na Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi katika Maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani yaliofanyika katika Ofisi ya Jumuiya ya watu wenye maradhi yasioambukiza (ZNCDA)Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja
Maandamano yalioongozwa na Bend ya Chipukizi yakielekea katika Ofisi ya Jumuia ya watu wenye maradhi yasioambukiza katika maadhimisho ya Siku ya moyo Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja
Vikundi mbalimbali vya mazoezi vikishajiisha suala zima la ufanyaji mazoezi ili kulinda afya na maradhi mbalimbali, katika siku ya maadhimisho ya Siku ya moyo Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.
Makamo mwenyekiti wa ZNCDA Ali Zubeir Juma akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya moyo Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.
Mgeni rasmi katika maadimisho ya siku ya Moyo Duniani Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Said Mohd Dimwa akitoa hotuba kuhusiana na kujikinga na maradhi mbalimbali yanayotokana na Ulaji,Unywaji wa Pombe na Uvutaji wa Tumbaku katika maadhimisho hayo yliofanyika katika Ofisi ya Jumuiya ya watu wenye maradhi yasioambukiza (ZNCDA)Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kupimwa afya zao katika maadhimisho ya Siku ya moyo Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Serikali Kuzichukulia Hatua Taasisi Zilizokiuka Taratibu za Manunuzi 2016/2017

$
0
0

Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

Serikali imesema itazichukulia hatua Taasisi zote zilizokiuka sheria na kanuni za manunuzi ya Umma pamoja na zile zenye viashiria vya rushwa ambazo zimebainika katika ripoti ya tathmini ya utendaji iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa mwaka wa Fedha 2016/17.

Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipokuwa akipokea ripoti ya tathimini ya utendaji wa Taasisi za Serikali katika sekta ya Manunuzi iliyofanywa na PPRA kwa mwaka wa Fedha 2016/17.

“Tutazichukulia hatua na kuziwajibisha taasisi zote ambazo zimebainika katika ripoti hii kuwa na viashiria vya rushwa au kufanya malipo yenye utata katika manunuzi yao,” alisema Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango amesema kuwa, zaidi ya 70% ya fedha za Umma zinatumika kununua vifaa na huduma mbalimbali hivyo Serikali haitavumilia kuona fedha hizo zinatumika bila kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PPRA Balozi Dkt. Matern Lumbanga amezitaja taasisi ambazo zimekiuka sheria na taratibu za manunuzi kwa mwaka 2016/2017 kuwa ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Taasisi ya Mifupa (MOI) pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.

 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akikata utembe baada ya kupokea Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akionesha kwa wanahabari na wajumbe wengine wa Bodi(hawapo pichani) kitabu cha Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, , Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga. 
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wajumbe wa Bodi ya ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) baada ya kupokea Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma ambapo ameahidi kuzichukulia hatua taasisi zote zilizokiuka taratibu za manunuzi zilizoainishwa kwenye Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MWILI WA MSANII MAREHEMU MOHAMEDI IDDI MTURUMA KUWASILI DAR JUMAMOSI 30-09-2017 USIKU KUTOKEA NCHINI SPAIN

$
0
0
Marehemu Mohamedi Idi Mturuma (Muddy)

Umoja wa Tanzania Ujerumani(UTU) ukishirikiana na watanzania wanaoishi Ujerumani na Spain ,unawajulisha ndugu,jamaa,marafiki ,wapenzi na watanzania wote kuwa mwili wa msanii marehemu Muhamedi Iddi Mturuma aka MUDDY utasafirishwa siku ya ijumaa 29-09-2017 na utafika siku ya jumamosi 30-09-2017 saa 8.30(saa nane na nusu) Usiku wa kuamkia Jumapili katika uwanja wa ndege wa JKN Dar-es-salaam,mazishi yatafanyika nyumbani kwa marehemu huko Mbezi ya Kimara,na taratibu za maziko mnaweza kupiga simu namba 0653319069 au 0656210725 ili kujua lini mazishi yatafanyika,mwili a marehemu utafuatana na rafiki yake kipenzi msanii Mussa Selemani aka MOSES FAB anayeishi Uingereza .

Marehemu Mohamedi Iddi Mturuma "MUDDY" alikuwa anaishi nchini ujerumani na umauti ulimfika siku ya 18.09.2017 nchini Spain ambako alikwenda kufanya shughuli zake za usanii wa sarakasi.
Allah amlaze mahala pema peponi- AMIIN
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live


Latest Images