Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

Benki ya KCB Tanzania yadhamini ligi ya soka TFF Vodacom 2017/18

$
0
0

Benki ya KCB Tanzania leo imetangaza rasmi udhamini mwenza wa ligi ya soka ya TFF Vodacom 2017/18 wenye thamani ya shilingi za kitanzania 325,000,000. Mkataba wa makubaliano hayo ulisainiwa rasmi leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario na Raisi WA TFF Wallace Karia.

Hafla hiyo ya makubaliano ilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Benki ya KCB Tanzania, Bi, Zuhura Muro, Mwenyekiti wa bodi  ya Udhamini TFF, Mhe, Mohammed Abdulaziz, Wakurugenzi wa Bodi ya KCB Tanzania, Wafanyakazi Benki ya KCB Tanzania, wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya soka na waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario alisema kuwa udhamini huo upo ndani ya vipaumbele vya benki kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo. “Sekta ya michezo ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na pia ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi nchini, hivyo benki ya KCB imechukua uamuzi huu kujiunga na TFF kukuza mchezo wa mpira wa miguu” alisema Kimario.

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania Zuhuru Muro alisema kuwa “Benki ya KCB Tanzania tunajivunia kuwa sehemu ya ligi hii na tunaamini kuwa udhamini wetu utachangia kuleta hamasa kubwa kwa wapenzi wa mpira wa miguu na kukuza vipaji vya vijana.” Alieleza kuwa udhamini huo utakuwa chachu ya maendeleo kwa benki, wateja wake, TFF, wachezaji, mashabiki na wananchi kwa ujumla.



Rais wa TFF aliishukuru benki ya KCB kwa kuidhamini Ligi kuu Vodacom jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu 2017/18. Pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.


Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario (aliyekaa Kulia) na Raisi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia (aliyekaa kushoto) wakisaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya soka ya Vodacom 2017/18 wenye thamani ya shilingi 325,000,000 uliotolewa na benki ya KCB Tanzania kwa TFF. Pamoja nao wakishuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Zuhura Muro (aliyesimama kulia), Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura (aliyesimama katikati) na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao (aliyesimama kushoto). 

 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario (Katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Zuhura Muro (wapili kulia) wakikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 325,000,000 kwa Raisi wa Shirikiso la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia (wapili kushoto), ikiwa ni udhamini kwa ajili ya ligi kuu ya soka ya Vodacom 2017/18. Pamoja nao kwenye picha ni Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura (wakwanza Kulia) na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao (wakwanza kushoto).



Vice President Advocates Accountability, Effectivenes and Indepence of the Judiciary

$
0
0
Jonas Kamaleki- MAELEZO

The Vice President of the United Republic of Tanzania, H.E. Samia Suluhu Hassan has urged the Judiciary to be independent, accountable and effective in order to come up with a foundation of a democratic system.

She made this remark while officiating at the opening of the Commonwealth Magistrates and Judges Association Conference held in Dar es Salaam today.

H.E. Samia said that the expectations of the people to the judiciary may at times be overwhelming given the capability challenges

“Regardless of these challenges and independent, effective and accountable judiciary needs to be in place to ensure the adherence of the rule of law, equal access to justice, security of livelihoods of all and peoples’ participation in peaceful governance of their countries,” said Samia.

Vice President said that she was glad that Magistrates and Judges had taken upon themselves the leading role to ensure effective judiciary was in place by including such topics perennial complaints of our people on issues regarding to delays, financial and procedural constraints on access to justice which threaten loss of trust and confidence in Judiciary, in the program.

She further said the Government of Tanzania has played its safeguarding role by enacting the Judiciary Administration Act, 2011 which established Judiciary Fund, designed to fund the disposal of cases. Despite all those efforts, in developing countries like Tanzania, funding was not always sufficient to cover all requirements of the Judiciary, she added.

TUMEKUSOGEZEA MATUKIO MAKUBWA YALIYOJILI MKOANI RUVUMA NA NJE YA MKOA WA RUVUMA WIKI HII.

$
0
0
Kama ulipitwa na matukio ya wiki nzima yaliyojili mkoani Ruvuma na nje ya mkoa wa Ruvuma kuanzia Sep 18 hadi Sep 24, 2017 basi usipate tabu tumekusogezea , Matukio ni haya hapa kazi yako ni kubonyeza hii video uweze kuyafahamu na kuyatazama.

WAANDISHI WA HABARI ZA BIOTEKNOLOJIA WAPEWA TUZO ZA UANDISHI BORA.

$
0
0
 Mshindi wa kwanza katika mashindano ya  uandishi bora  wa habari za sayansi na kilimo (Biotchnolojia) katika kuendeleza Kilimo, Gerald Kitabu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Elimu , Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako mara baada ya kumkabidhi cheki ya Dola 1500 kwa kuwa mshindi wa mashindano ya uandishi bora wa habari za Sayansi makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Tume ya Sayansi (Costech) jijini Dar es Salaam leo.

Katika tuzo hizo Mshindi wa Kwanza amezawadiwa cheki ya Dola 1500, wapili dola 1200 na watatu Dola 100o na wengine Dola 750, 375 na 250 pia baadhi ya Vyombo vya habari wamezawadiwa cheti cha Shukrani kwa kuchapisha kazi za Sayansi na Kilimo.

Ukiacha Gerald Kitabu wengine ni Kelvin Gwabara, Innocent Mugune, Coletha Makurwa, Shadrack Sagati, Elias  Msuya, Fatma Abdul, Lucy Ngowi, Restuta Damian, Heren Kwavava, Daniel Sembelya na Zakaria Gabriel. 
Baadhi ya washindi wa Tuzo za uandishi mahiri wa habari za Sayansi  na Kilimo(Bioteknolojia) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Elimu ,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Prof.Joyce Ndalichako na  Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Hassan Mshinda katika hafla ya kuwazawadia washindi wa habari waliofanya vizuri zaidi kwenye kuandika na kuelimisha umma kuhusu matumizi ya Sayansi, Teknologia na ubunifu hususani Bioteknologia katika kuendeleza kilimo.
Waziri wa Elimu , Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akimkabidhi Kelvin Gwabara tuzo yake wakati aliposhinda tuzo ya uandishi bora wa habari za Sayansi na kilimo kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Hassan Mshinda katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Costech jijini Dar es salaam leo. Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Hassan Mshinda

Waziri wa Elimu , Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akimkabidhi hundi ya Dola 750 wakati aliposhinda tuzo ya uandishi bora wa habari za Sayansi na kilimo kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Hassan Mshinda katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Costech jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Elimu , Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako, Mkuu Mkuu wa Tume ya Sayansi na Technologia, (COSTECH)Hassan Mshinda na Mkurugenzi wa TBC wakiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa tuzo za umahili bora wa habari za Sayansi na Kilimo jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamaii
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

HOME GYM WAFIKISHA MIAKA 19 KWA KISHINDO,WAWAASA WAKAZI WA DAR ES SALAAM KUPENDA KUFANYA MAZOEZI

$
0
0
Home Gym Mwenge yafikisha miaka 19 kwa kishindo. Weekend iliyopita ilishuhudia Home Gym Mwenge moja ya Gym maarufu ya mazoezi ya viungo jijini Dar es salaam ikitimiza miaka 19 yangu ianzishwe. 
Sherehe hizo zilifanyika kwenye viwanja vya Shule ya wanasheria jijini na kuhudhuriwa na Mamia ya watu. Akiongea wakati wa sherehe hizo mwanzilishi na mmiliki wa Gym hiyo Andrew Mango alishukuru wanachama wa Gym hiyo na Wadhamini. 
Pia aliwataka wakazi wa Dar es salaam kupenda kufanya mazoezi ili kujenga afya bora.

JAFO AWAPONGEZA WATAALAM WA AFYA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA DODOMA NA KUTAKA UBORESHAJI MIUNDOMBINU

$
0
0
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara ya kukagua miundombinu katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na kuahidi kuwa serikali itafanya ukarabati wa baadhi ya majengo haraka iwezekanavyo.

Akizungumza mara baada ya kukagua miundombinu ya hospitali leo mjini Dodoma, Jafo amesema hospitali hiyo ndio kimbilio la watu wengi na kwamba baadhi ya majengo yake yanahitaji kufanyiwa maboresho ili yaendane na hadhi ya Makao makuu ya Nchi.

Amesema majengo hayo yamejengwa tangu enzi za Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ni ya zamani hivyo yanatakiwa kufanyiwa maboresho ili yawe ya kisasa na kwamba serikali inajipanga kufanya maboresho hayo na kwa kuanzia itapeleka Sh.milioni 500 kuanza ukarabati katika jengo la upasuaji.

Ameeleza jengo la upasuaji ni la muda mrefu na miundombinu yake kwa ndani haiendani na hali ya sasa na kwamba inatakiwa kukarabatiwa ili iwe ya kisasa.“Serikali tutaleta fedha ili tukarabati jengo hili liendane na hali halisi ya mahitaji hasa ikizingatiwa Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi hivyo ni kimbilio la watu wengi,”amesema Jafo

Aidha amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa Dk.Charles Kiologwe na uongozi wa hospitali hiyo kuanza mchakato wa kuwasilisha maombi serikalini kwa ajili ya kuboresha majengo ya hospitali hiyo ambayo asilimia kubwa yalijengwa wakati Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Kadhalika, amepongeza ujenzi wa jengo jipya la kisasa la akina mama na watoto na kuagiza ujenzi wake ukamilishwe kabla ya mwisho wa mwezi wa oktoba mwaka huu kwa kuwa serikali imeshapeleka fedha za ukamilishaji.

Aidha amepongeza ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Bima ya Afya na kwamba linapokea wagonjwa wengi kwa siku kutokana na ubora wa miundombinu yake.Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Caroline Damian amesema jengo hilo limekuwa likitumika kufanya upasuaji kwa wastani wa watu 500 kwa wiki.

Naye, Mganga Mkuu Dk. Kiologwe amesema miundombinu ya hospitali hiyo ilijengwa mwaka 1929 na kwamba licha ya changamoto ya miundombinu lakini huduma za afya zimekuwa zikitolewa kwa ufanisi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali wa serikali katika ukaguzi wa jengo la Akinamama na watoto katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua miundombinu ndani ya jengo la upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.Charles Kiologwe akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipokuwa akikagua chumba cha kufulia nguo za Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa wakandarasi wa ujenzi wa jengo la Akinamama na watoto alipofanya ziara ya kukagua miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Serikali Yasisitiza Umuhimu wa Mafunzo Zaidi Kwa Wakaguzi wa Dawa

$
0
0
Serikali imesisitiza umuhimu wa mafunzo zaidi kwa wataalamu wa ukaguzi na udhibiti ili kuhakikisha dawa zinazoingizwa na kutengenezwa nchini zina ubora kwa kuzingatia viwango na vigezo vilivyowekwa.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Ulisubisya Mpoki amesema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazozikabili nchi nyingi barani Afrika katika kuwapatia wananchi wake huduma bora za afya ni ukosefu wa wataalamu wa kutosha wa ukaguzi wa dawa hivyo mafunzo ya wataalamu hao hayana budi kupewa kipaumbele.

“Tanzania tunaagiza asilimia themanini ya mahitaji yetu ya dawa na kutengeneza kiasi kilichobaki hivyo suala la weledi katika ukaguzi na udhibiti wa dawa ni jambo linalopaswa kupewa umuhimu mkubwa” Dk. Mpoki alisema.

Katibu Mkuu huyo amesema hayo leo wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku tisa ya ulinganishaji wa viwango vya dawa kwa wakaguzi na wataalamu wa udhibiti wa dawa kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika kituo Mahsusi cha Kanda cha Ukaguzi na Udhibiti wa Dawa kwa Afrika Mashariki kilichopo Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi ya Afya, Muhimbili.


Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania, Bw. Hiiti Sillo akitoa maelezo ya utangulizi kwa washiriki.
Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto , Dkt. Ulisubisya Mpoki akisisitiza jambo katika hotuba yake ya ufunguzi.


Picha ya pamoja baina ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto , Dkt. Ulisubisya Mpoki (wa tatu kushoto, msitari wa mbele), akiwa na waratibu, na washiriki wa mafunzo ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Afya Duniani (WHO) na Sekeretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wameshiriki katika uratibu wa mafunzo hayo na kutoa misaada ya hali na mali.

DK. MPOKI AFUNGUA MAFUNZO YA KUTATHIMINI KWA ULINGANIFU UFANISI , UBORA NA USALAMA WA DAWA KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii

CHUO Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili kupitia Shule ya Famasi kwa kushirikiana kwa Kituo cha cha Mafunzo ya Kutathimini Dawa cha Afrika Mashariki wameendesha mafunzo ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi , Ubora na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Afya Duniani (WHO) na Sekeretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wameshiriki katika uratibu wa mafunzo hayo na kutoa misaada ya hali na mal.i

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto , Dk. Ulisubisya Mpoki amesema mfumo kutathimini dawa za Afrika Mashariki ni muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi wa ukanda huo wanapata dawa bora, salama na zenye ufanisi mkubwa.

Dk. Mpoki amesema mafunzo hayo ya nadharia na vitendo kwa wataalam wa dawa wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki yanalenga kuhakikisha kuwa dawa zote zilizokidhi vigezo zinasajiliwa kwa mfumo wa ulinganifu unaotumika baada wataalam hao kujiridhisha kisayansi.

Nae Mkuruenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bw. Hiiti Sillo amesema kuwa kumekuwa na ushirikiano wa karibu na wananchi katika utoaji wa taarifa pale wanapoona kuna dawa zenye mashaka ziko mtaani, hivyo kusaidia katika dhima ya kulinda afya ya jamii.

Amesema kuwa kuanzishwa kituo cha kutathimini Dawa cha Afrika Mashariki kitakuwa ni msaada mkubwa katika kuhakikisha kuwa kila dawa zilizo katika nchi za Afrika Mashariki ni zilizosajiliwa na usajili kwa matumizi ya wananchi wote wa ukanda husika.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo  ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi , Ubora na usalama wa  dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki yalifanyika leo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA , Hiiti Sillo , Kulia ni Mkurugenzi wa Shahada za awali  wa MUHAS, Profesa Mainen Moshi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafunzo  ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi , Ubora na usalama wa  dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam
 Mratibu wa Mafunzo  wa MUHAS –TFDA , Profesa Eliangiriya  Kaale akitoa neno la shukrani baada ufunguzi wa mafunzo  ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi , Ubora na usalama wa  dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akiwa katika pamoja na Maprofesa wa Chuo cha Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi pamoja na Watalaam leo jijini Dar es Salaam.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

WAKURUGENZI MKOANI SINGIDA WAAGIZWA KUNUNUA CHAKI ZINAZOZALISHWA MKOANI HUMO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akishiriki kazi ya uzalishaji chaki wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea Kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji chaki cha Dober Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akikagua kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji chaki cha Dober Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi wakati wa ziara ya kikazi 
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimkabidhi boksi tano za chaki Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi mara baada ya kutembelea na kukagua kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji chaki
cha Dober Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi wakati wa ziara ya kikazi

WAZIRI DKT. HARRISON MWAKYEMBE ATEMBELEA ENEO LA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA NALIENDELE (FARM 17)

WANANCHI ILINDENI MIUNDOMBINU YA MAWASILIANO VIJIJINI INATUMIA KODI ZENU: KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU

$
0
0
Kamati ya Miundombinu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania inaendelea na ziara ya kukagua ujenzi wa minara ya simu, ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini na kwenye maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata na kutumia huduma za mawasiliano kwenye maeneo mbali mbali nchini. Kamti hiyo imeendelea na ziara yake kwenye mikoa ya Dodoma na Tabora ili kujiridhisha na utendaji kazi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wa kufikisha mawasiliano kwa wananchi.

Katika ziara hiyo, Mtendaji Mkuu wa UCSAF Eng. Peter Ulanga amesema kuwa Mfuko umetoa ruzuku kwa Kampuni ya simu ya TIGO kujenga mnara ili kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi. Mfuko umetumia zaidi ya dola za marekani elfu arobaini na moja na mia tano (41,500) ambapo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 85 kuipatia kampuni ya TIGO kujenga mnara ambao sasa unahudumia zaidi wa wakazi 4,000 wa kijiji cha Mayamaya na vijiji vingine vya kata ya Zanka wilaya ya Bahi mkoani Dodoma ambapo walikuwa hawana huduma za mawasiliano na sasa wananufaika na uwepo wa huu mnara na wanapata huduma za mawasiliano. Mnara huu ulikamilika mwezi Machi mwaka jana na kuanza kutoa huduma ya mawasiiano kwa wananchi.

Naye mwakilishi wa kampuni ya simu ya TIGO mkoa wa Dodoma mhandisi Hassan Said Gimbo wa kampuni hiyo amewaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu waliofanya ziara ya kukagua ujenzi wa minara, ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano kuwa kampuni yao imekamilisha ujenzi wa mnara na sasa unatoa mawasiliano kwa wananchi. Pia ameongeza kuwa kampuni ya TIGO inafuatilia mara kwa mara kwenye eneo hilo na kuhakikisha kuwa mawasiliano yanapatikana. “Tunajitahidi kwa kiasi kikubwa kukarabati na kuhakikisha kuwa pale mawasiliano yanapopotea au kuwa hafifu tunafanya haraka kuyarudisha”, amesema mhandisi Gimbo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigallla King (aliyesimama) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kizengi (hawapo pichani) kilichopo kata ya Kizengi wilaya ya Uyui mkoani Tabora baada ya kukagua ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini wakati wa ziara ya Kamati hiyo. 
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Eng. Peter Ulanga(aliyesimama mbele) akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini kwenye kijiji cha Mayamaya kilichopo Kata ya Zanka wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
Meneja wa Kampuni ya Simu ya TTCL Mkoa wa Tabora Bwana James Mlaguzi (wa kwanza kulia) akitoa taarifa kwa wajumbe wa Kamati hiyo wakati wa ziara yao ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano viijini kwenye kijiji cha Kizengi kilichopo kata ya Kizengi wilaya ya Uyui mkoani Tabora.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Mussa Ntimizi akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Kizengi kilichopo kata ya Kizengi wilaya ya Uyui mkoani Tabora wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UFAFANUZI KUHUSU MASHINDANO YA UREMBO NA TUZO ZA MUZIKI KUTOKA BASATA

MARUFUKU UPIGWAJI WA VIGODORO TANGA-R.P.C TANGA

NAIBU WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR ATEMBELEA BOHARI KUU YA DAWA NA KUKUTA DAWA ZA KUTOSHA

$
0
0

Na Mwashumgi Tahir     Maelezo Zanzibar 
SERIKALI ya  Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya Zanzibar imewahakikishia wananchi kuwa Bohari kuu ya Dawa inadawa za kutosha za kuhudumia wagonjwa wanaofika kupata matibabu katika Mahospitali na vituo vya Afya.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman wakati alipofanya ziara katika Bohari kuu ya Dawa na kuangalia namna ya upatikanaj i wa dawa.
Amesema uwepo wa Dawa katika Bohari kuu ya dawa nikuonesha kuwa Serikali   ina imani na wananchi wake kwa kuongeza Bajeti ya ununuzi wa dawa kwa asilimia mia moja ambapo upungufu upo kidogo kwenye dawa za wagonjwa wa akili ambap o Wizara iko mbioni kutatua tatizo hilo.
”‘Wananchi msininuwe dawa katika mahospitali na vituo vya Afya zipo za kutosha  kwani Serikali imefanya jitihada kubwa ya kueneza dawa na kuzisambaza mahosptalini    mote na vituo vya afya ambapo kama kutakuwa na upungufu wa  dawa  Wizara tutatoa taarifa maalum kwa wananchi wake”. Naibu Waziri huyo Alisisitiza.
Amewataka wafanyakazi wa Mahospitalini na Vituo vya Afya kuagiza dawa kwa wakati kwani kufanya hivyo kutasaidia kuondosha urasimu kwa wagonjwa ambao wanaokwenda kupata huduma ya matibabu na kuwambiwa dawa hakuna ambapo kuna dawa za kutosha katika Bohari ya dawa.
Kwa upande wa Mkurugenzi Bohari kuu ya Dawa Zahran  Ali  Hamad amesema kwa mujibu wa mahitaji ya dawa muhimu zinazotumika katika visiwa vya Unguja na Pemba dawa zipo za kutosha kwa kuwahudumia wananchi.
Amezitaja dawa hizo ni pamoja na za akinamama wanofika kujifungua,dawa za mpango wa uzazi, dawa ya kisukari na pressure na maradhi mengine na kuwasisitiza wahudumu wa afya kuagiza dawa  kwa wakati.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harusi Said Suleiman akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa Zahran Ali Hamad alipotembea kuona dawa katika bohari hiyo, iliyopo Maruhubi Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.

DAKTARI WA HOSPITALI YA AGA KHAN ASHANGAA MANJI KUUGUA MOYO KATIKA UMRI MDOGO

$
0
0

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Daktari bingwa Wa magonjwa ya moyo wa Hospital ya Aga Khan, Prof. Mustapha Bapunia (62), ameileza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, inashangaza, Manji katika umri mdogo alionao anamatatizo sugu ya moyo ambayo yanampasa kujilinda sana.

Dkt, huyo ambaye ni shahidi Wa tatu upande wa utetezi katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya Heroin inayomkabili mfanyabiashara Yusufu Manji amedai hayo leo wakati àkitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha.Akiongozwà na Wakili wa utetezi, Hajra Mungula, shahidi Hugo amedai, Manji ana vyuma vinne kwenye moyo ni hatari na kwamba ni lazima ajiangalie sana kwasababu anaweza kufa muda wowote.

Amedai katika umri mdogo alionao Manji kuwa na vyuma vinne kwenye moyo inashangaza sana na kitaalamy anapaswa kujiangalia sana.Amedai Februari mwaka huu Manji alipelekwa hospitalini hapo akiwa anasumbuliwa na maumivu kwenye moyo ambapo kutokana na historia ya ugonjwa iliyotolewa na manji mwenyewe na kwamba aliwahi kuzibuliwa mishipa ya moyo mitatu ilizibuliwa India, Dubai na Marekani lakini pia bado alikuwa akipata maumivu inaonyesha kuwa anatatizo sugu la moyo.

Alidai kuwa hata baada ya kumfanyiwa uchunguzi ilionekana kuna mshipa mwingine ulioziba licha ya ile iliyozibuliwa kuwa wazi lakini walipotaka kumzibua alikataa na kuomba apewe dawa kwasababu familia yake na matibabu yake yapo marekani.

Baada ya vipimo walimshauriwa kutumia dawa za aina nne ambazo ni muhimu sana kwasababu ya umri wake mdogo ili ya kupunguza maumivu makali. Kwani vipimo vinaonyesha Manji ana maumivu sugu ya mgongo na kukosa usingizi ambapo alipewa dawa za kupunguza maumivu (Benzodiazepines)ambazo zinatotewa kwa cheti cha daktari lakini baadae tatizo lilijirudia na kurudishwa tena february 24,2017 saa mbili usiku ambapo majibu ya vipimo vilionyesha kapata mshtuko, wakarekebisha na kumuwekea chuma na kuruhusiwa Machi 14,2017.
Mshtakiwa Yusuph Manji anayekabiliwa na shtaka la matumizi ya dawa za kulevya, akijadili jambo na Wakili wake Hajra Mungula kabla ya kupanda kizimbani kwa ajili ya kuanza kujitetea.

WAZIRI DKT MWAKYEMBE ATOA AGIZO KWA WANAOSIMAMIA UWANJA WA TAIFA

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewaagiza wanaosimamia Uwanja wa Taifa Kuhakikisha wanaitisha Zabuni ya Kimataifa Ili kuweza kumpata Mkandarasi atakayeweza kutoa Tiketi za Kielektroniki zitakazokuwa na number ya Siti za Kukaa kwa kila Mtazamaji wa Mpira.  

MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBA 26,2017

Dkt. Harrison Mwakyembe: “Nataka Mkandarasi Mpya wa Kutoa Tiketi Uwanja wa Taifa Utakapofunguliwa”

$
0
0

Na Benedict Liwenga-WHUSM.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kwamba pindi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam utakapokamilia kufanyiwa ukarabati atahakikisha anapatikana Mkandarasi Mpya mwenye vigezo na ambaye ataleta mabadiliko hususani katika utoaji tiketi kulingana na namba za viti vilivyopo ndani ya Uwanja huo.

Kauli hiyo ameitoa jana Mkoani Mtwara wakati alipotembelea Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Nangwanda ili kujionea miundombinu ya uwanja huo ikiwemo baadhi ya changamoto zinazoikabili kiwanja hicho.

Dkt. Mwakyembe ameeleza kwamba, kumekuwa na changamoto ya kutofahamika idadi kamili ya watu wanaoingia ndani ya uwanja hali inayopelekea watu kukaa ovyo katika sehemu zisizo rasmi na wengine kulundikana nje ya uwanja wakati pesa za viingilio wamelipia ambapo ameweka wazi kuwa hali hiyo inasababishwa na urataibu mbovu wa utoaji tiketi.

Akiongea na Uongozi wa Uwanja huo wa Nangwanda Mkoani hapo alisema kwamba, kwakuwa sasa Uwanja wa Taifa uko katika ukarabati, pindi utakapokamilika Mkandarasi mpya lazima apatikane ili pindi mtu anunuapo tiketi yake iendane na kiti chake atakachokaa na sio vinginevyo kwakuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kuboresha sura za viwanja nchini.

“Napenda kusisitiza suala hili kuwa, ntahitaji apatikane Mkandarasi atakaetoa tiketi kulingana na siti atakayokaa mtazamaji wa mpira, kwasababu kumekuwa na kero kubwa katika utoaji tiketi hapo mwanzo jambo ambalo halileti sura nzuri kwa jamii”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Aliongeza kuwa Watanzania hawanabudi kuiga mifano ya nchi nyingine ambazo zimejidhatiti katika masuala ya utoaji tiketi wakati wa michezo.

Sambamba na hayo, Waziri Mwakyembe ameupongeza uongozi wa uwanja huo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuutunza uwanja wa Nangwanda huku akiaihidi kuzifikisha changamoto za uwanja huo katika Viongozi wa Juu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ili waweze kushirikiana kwa pamoja kuona namna ya kuzitatua.

Uwanja wa Nagwanda ulianzishwa miaka ya 1980 ambapo awali ulikuwa ukiitwa jina la Uwanja wa Umoja Mtwara na baadaye kupewa jina la Uwanja wa Nagwanda lililotokana na jina la mtu maarufu wakati huo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akisalimiana na baadhi ya Viongozi wanaosimamia Uwanja wa Nangwanda Mtwara wakati alipofanya ziara kujionea changamoto katika uwanja huo 25 Septemba, 2017 Mkoani Mtwara.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akiongea na baadhi ya Viongozi wanaosimamia Uwanja wa Nangwanda Mtwara wakati alipofanya ziara kujionea changamoto katika uwanja huo 25 Septemba, 2017 Mkoani Mtwara.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akiangalia eneo la uwanja wa mpira wa miguu akiwa na baadhi ya Viongozi wanaosimamia Uwanja wa Nangwanda Mtwara wakati alipofanya ziara kujionea changamoto katika uwanja huo 25 Septemba, 2017 Mkoani Mtwara.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM

KUPATA ZUIO LA MAHAKAMA.

$
0
0

Na  Bashir  Yakub.


1.ZUIO  LA  MAHAKAMA  NININI.


Ni  amri  inayotolewa  na  mahakama  kumzuia  mtu  kutofanya  jambo  fulani  kwa  muda. Kampuni  nayo  ni  mtu  ambapo  yaweza  kuomba  zuio  au  kuzuiwa. Aidha yeyote  ana  haki ya  kuomba  amri  hii  ikiwa  anaona  kuna  jambo  fulani  linafanyika  na  ikiwa  litaendelea  kufanyika  basi  litaharibu  au  kupoteza  kabisa  kitu  fulani.


Kwahiyo  zuio   ni  amri inayobeba  maagizo  maalum  kwa  mtu  au  watu  maalum  kuwaamrisha  kutoendelea  na  kitu  fulani  kama  tulivyoona  hapo  juu.

Sheria  ya  Mwenendo  wa Madai,  Sura  ya  33 na  Sheria  nyingine  mtambuka  zimeongelea  kuhusu  zuio.


2.   KATIKA   MATUKIO   GANI  UNAWEZA  KUOMBA  ZUIO.


( a ) Kwa  mfano, umeshindwa  kulipa  mkopo  na  tayari  una  taarifa  kuwa  benki au  taasisi  yoyote  ya  fedha  inataka kwenda  kuuza  na  unahisi  kuna  pahala   hapaendi  sawa katika  mikataba yenu. Basi  unaomba  zuio  ili  hiyo  mali  yako  uliyoweka  rehani  isiuzwe  mpaka  hapo  hilo eneo  ambalo  mmeshindwa  kuelewana  litakapopatiwa  majibu.

( b ) Kwa mfano, umemuuzia  mtu  gari, pikipiki,  au  mashine  yoyote.  Mtu  huyo  hajalipa  kiasi  cha  pesa  iliyobaki kama  mlivyokubaliana. Lakini  anaendelea  kutumia  kifaa  hicho. Unaweza  kuomba   kumzuia  kuendelea  kutumia  mpaka  atakapolipa  kiasi  kilichobaki  ili  asiendelee  kuharibu  au  kuzeesha  kifaa  hicho.


( c ) Kwa  mfano, we  ni  mpangaji  katika nyumba ya kuishi  au  biashara.  Mwenye  nyumba,eneo anataka  kukutoa  kwenye  pango  hilo  bila  kufuata  utaratibu  au  kwa  kukiuka baadhi  ya  makubaliano  kwenye  mkataba  wenu. Unaweza  kuomba  zuio asiendelee  kukutoa.


Pia  mazingira  mengine  yoyote  ambayo  unahisi  kuna  kitu, jambo  linataka  kuharibiwa  au  kuingiliwa, kuuzwa, kupotezwa,kufichwa  kinyume  na  utaratibu  unaweza  kuomba  zuio  hilo.


KUSOMA   ZAIDI   sheriayakub.blogspot.com


                                        

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>