Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1928 | 1929 | (Page 1930) | 1931 | 1932 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Mbulu

  Halmashauri zote nchini zimetakiwa kutenga maeneo ya michezo wakati wa kupanga mipango miji kwa matumizi bora ya ardhi katika maeneo yao.

  Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura alipokuwa akifunga fainali ya mashindano ya Jimbo Cup inayodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay iliyochezwa katika eneo la kata ya Dongobesh Wilaya ya Mbulu Mkoani wa Manyara.

  “Natoa wito kwa Halmashauri zote ikiwemo halmashauri yenu ya wilaya ya Mbulu wakati wa kupanga matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya mipango miji mkumbuke kutenga maeneo ya michezo, Baraza la Michezo la Taifa litatoa mafunzo ya michezo na utaalam” alisema Naibu Waziri Wambura.

  Akikabidhi zawadi za washindi katika mashindano hayo ambao ni timu ya Qatajiring kutoka kijiji cha tumati ambao ni mshindi wa kwanza na timu ya Zahanati kutoka kijiji cha Diomati mshindi wa pili, Naibu Waziri Wambura amewahimiza wachezaji na wananchi kuthamini michezo kwa kuwa ni ajira, inaleta umoja na mshikamano miongoni mwa jamii.

  Dakika 90 za fainali hizo ziliisha kwa timu zote kufungana bao 2-2 na hatimaye timu ya Qatajiring iliibuka kidedea kwa ifunga timu ya Zahanati kwa penati 4-1.Akionesha umuhimu na umahiri wa wilaya ya Mbulu katika michezo, Naibu Waziri Wambura amesema wilaya hiyo imekuwa kitovu cha wanamichezo bora hasa mchezo wa riadha ambao wameiletea sifa Tanzania ndani na nje ya nchi.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akiongea na Wananchi wakati wa kuhitimisha fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (kulia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Qatajiring zawadi mbalimbali mara baada ya kuibuka kidedea baada ya kuifunga timu ya Zahanati wakati wa fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu. Katikati ni mdhamini wa mashindano hayo Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay.
  Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay akiongea na Wananchi wakati wa kuhitimisha fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (aliyevaa miwani) akikagua timu za Qatajiring na timu ya Zahanati wakati wa fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu. Katikati ni mdhamini wa mashindano hayo Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay.


  0 0

  Ujumbe kutoka Ofisi yaMakamu wa Rais ukiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji wakimsikiliza Mmiliki wa Mgodi wa Sambaru uliopo wilayani Ikungi Mkoani Singida, Bwana Yusuf Mwandami walipofanya ziara ya kutembelea mgodi huo.
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,Bi Magdalena Mtenga akiuliza swali kwa mmiliki wa mgodi wa sambaru uliopo Ikungi Mkoani Singida mara baada ya ujumbe toka Ofisi ya Makamu wa Rais kutembelea mgodi huo wa mwisho katika picha ni Afisa madini kanda ya Singida aliyeongozana na ujumbe huo Bi. Sofia Omary.
  Mmiliki wa Mgodi mdogo wa dhahabu wa Sambaru uliopo Ikungi Bwana Yusuf Mwandami akitoa maelekezo kwa ujumbe huo juu ya mashine mbalimbalimbali zilizofungwa mgodini hapo zitakavyokua zinafanya kazi. Wa kwanza kulia ni Afisa madini kanda ya Singida aliyeongozana na ujumbe huo Bi. Sofia Omary.
  Ujumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa rais ukiongozwa na Mkurugenzi wa sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi-Mazingira Bi. Magdalena Mtenga wakipata maelezo juu ya uendeshaji wa mgodi mdogo wa dhahabu ulioko Ikungi Bwana Ahmed Magoma

  0 0

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya Kituo cha Uwekezaji (TIC )na tovuti ya jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza katika uzinduzi wa Bodi hiyo mapema hii leo, Mwijage amesema kuwa "Tunapambana kuondoa urasimu,tayari tumeanzisha kamati ya kitaifa ya kuhudumia wawekezaji na wajumbe ni taasisi zote zinazotoa huduma kwa wawekezaji, Mpaka sasa matokeo ni mazuri na tumeanza kupata ripoti za kutupongeza katika juhudi zetu za kuondoa urasimu kwenye utoaji wa vibali na leseni mbalimbalihapa nchini"
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji (TIC),Profesa Longinus Rutasitara Bodi akizungumza mapema hii leo wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya na tovuti ya TIC jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Bodi yetu itatoa ushirikiano kuhakikisha majukumu ya TIC yanatimizwa ipasavyo.

  Tunapambana kuondoa urasimu, tayari tumeanzisha kamati ya kitaifa ya kuhudumia wawekezaji na wajumbe ni taasisi zote zinazotoa huduma kwa wawekezaji. Mpaka sasa matokeo ni mazuri na tumeanza kupata ripoti za kutupongeza katika juhudi zetu za kuondoa urasimu kwenye utoaji wa vibali na leseni mbalimbali.
  Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Geoffrey Idelphonce akizungumza katika uzinduzi wa Bodi ya wakurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) jijini Dar es Salaam.

  0 0


  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde kulia  akipokea
   sehemu ya Msaada wa mabati 500 kwa ajili ya kuezeka kwenye majengo ya shule hiyo baada ya kuezuliwa na upepo kutoka kwa meneja wa ALAF tawi la Dodoma  Grayson Mwakasege.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Shule ya msingi Huzi, Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde akiwa na ujumbe wake pamoja na walimu wakikagua eneo la majengo ya shule hiyo lililoezuliwa mapaa na upepo hivi karibuni.
  Muenekano wa Majengo ya shule ya Msingi Huzi yakiwa hayana mapaa kutokana baada ya kuezuliwa na upepo.
  Kibao cha shule ya msingi Huzi.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuja Juma Homera kushoto akipokea Cheki ya Shilingi Milioni moja kutoka kwa mkurugezi wa kampuni ya kuuza mafuta ya OIL COM mjini hapa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Nakayaya mjini hapa. 

   Na Steven Augustino wa Ruvuma TV Tunduru

   SERIIKALI imewataka wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza kusaidia ujenzi wa Kituo cha Afya cha Afya Nakayaya Mjini hapa na Kwamba baada ya kukamirika kwa ujenzi huo kituo hicho kitasaidia kupunguza msongamano katika Hospitali ya Serikali ya wilaya ya Tunduru. 

   Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Juma Homera wakati akipokea msaada wa Shilingi Milioni 1,400,000 kutoka kwa mkurugenzi wa Kituo cha kuuza mafuta cha OIL COM Mjini hapa na kutolewa kwa kwamba msaada huo kutasaidia kukamirika kwa baadhi ya shughuli za ujenzi huo. Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera akionyesha Zahanati ya Kata ya Nakayaya ambayo inaendelea kujengwa. Aidha katika taarifa hiyo pia dc Homera ametumia nafasi hiyo kuwapongeza baadhi ya wadau wa maendeleo wa ndani la nje ya wilaya hiyo kwa kujitokeza na kumuunga mkono juhudi za Serikali katika ujenzi wa Kituo hicho kwa lengo la kuwasogezea huduma wananchi.

   Alisema pamoja na michango hiyo kutoka kwa wadau pia serikali inatengeneza utaratibu wa kuwashirikisha wananchi katika ujenzi huo ili nguvu kazi watakayo itoa iweze kusaidia kupunguza gharamaa za ujenzi.

   Tayali ujenzi Zahanati hiyo umekwisha anza na kukamilisha jengo la Utawala katika kituo hicho na kwamba hadi kukamilika kwa ujenzi wa majengo yote 8 yaliyopangwa kughalimu zaidi ya shilingi 419. Akizungumzia tukio hilo Mkurugenzi wa Kituo cha mafuta Cha OIL COM Bw. Ghulam Kalamal alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya kampuni yake kurudisha faida iliyopata kutokana na biashara hiyo ili iweze kuhudumia jamii katika eneo hilo. 

   Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Goerge Chiwangu amesema kuwa zaidi ya Wagonjwa wanje 100 hufikana kupatiwa matibabu kwa siku huku kukiwa na kundi la kaati ya akina mama 15 na 20 ambao hufika hospitalini hapo kwa lengo la kijifungua. Hii hapa Video yake .

  0 0


  Naibu Waziri Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiagana na wananchi baada ya kumaliza mkutano wa hadhara,wakati waziara ya kikazi ikiwa lengo ni kukagua masuala ya Ulinzi na Usalama na kusikiliza maoni na kero za wananchi. Mkutano huo ulifanyika katika Viwanja vya Ikwiriri, wilayaniRufiji,MkoaniPwani .
   Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akizungumza katika mkutano wahadhara wakati waziara ya kikazi ikiwa lengo ni kukagua masualaya Ulinzina Usalama na kusikiliza maoni na keroza wananchi. Mkutano huo ulifanyika katika Viwanja vya Ikwiriri, wilayani Rufiji,mkoani Pwani.
   WananchiwakifurahiajambokwenyemkutanowahadharawakatiwaziarayakikaziyaNaibu Waziri Wizaraya Mambo ya NdaniyaNchi,Mhandisi Hamad Masauni(hayupopichani),ikiwalengonikukaguamasualayaUlinzinaUsalamanakusikilizamaoninakerozawananchi. MkutanohuoulifanyikakatikaViwanjavyaIkwiriri, wilayani Rufiji,mkoaniPwani.
  PichanaWizaraya Mambo yaNdaniyaNchi
  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

  0 0

  Na Muhidin Amri, Songea.
  MFUKO wa taifa wa Bima ya Afya(NHIF) umewahimiza wana michezo nchini kuchangamkia fursa ya kujiunga na mpango wa matibabu kupitia mfuko wa afya ya jamii(CHF) na mfuko wa taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kwa ajili ya kupata huduma bora za matibabu pindi wanapoumia wakiwa michezoni.

  Rai hiyo imetolewa  mwishoni mwa wiki na meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)mkoani Ruvuma Abdiel Mkaro wakati wa Bonanza maalum la kuhamasisha jamii hususana wana michezo kujiunga na mfuko huo na kushiriki mazoea mara kwa mara ili kuepuka uwezekano wa kupata magonjwa yasiokuwa ya lazima.

  Aliwataka wana michezo na jamii ya watanzania wakiwemo waandishi wa habari,kuona umuhimu wa kijunga na mpango huo  kwa lengo la kuwa na uhakika wa matibabu  pale  inapotokea kupata ajali na magonjwa ya kawaida.

  Bonanza hilo liliandaliwa na NHIF lilishirikisha michezo mbalimbali kama vile kukimbia,mazoezi ya viungo,kukimbiza kuku pamoja na mpira wa miguu ambap timu ya soka ya Mkambi FC ilifanikiwa kuibuka mshindi baada ya kuifunga timu ya NHIF 4-2 kwa njia ya Penalti kufuatia matokeo ya kufungana 1-1 ndani ya Dkt 90 za mchezo huo.

  Hata hivyo Bonanza hilo lililoonekana kuvutia watu wengi kutoka maeneo mbalimbali ya manispaa ya Songea, baadhi ya washiriki  wameiomba Nhif kuendelea kuandaa bonanza kama hilo kila mwiso wa mwezi ili kutoa fursa kwa wananchi kushiriki na kufanya mazoezi ili kuepusha uwezekano wa kupata magonjwa.

  0 0

  Na Mwandishi wetu
  RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.

  Nchi hizo mbili zinaungana na nchi nyingine sita zilizothibitisha kufanya hivyo awali kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Chama Cha kuogelea nchini (TSA), Leena Kapadia.

  Kapadia amezitaja nchi hizo kuwa ni Afrika Kusini, Zambia, Kenya, Uganda, Djibouti na wenyeji Tanzania.

  Kapadia amesema kuwa bado wametoa nafasi kwa nchi nyingine kuthibitisha kushiriki hadi wiki moja kabla ya mashindano ili kuleta mvuto na ushindani zaidi. 

  “Tumezipa nafasi zaidi kutafuta fedha ili kushiriki, tutafunga mlango wa kuthibitisha wiki moja kabla ya mashindano,” alisema Kapadia.
  Alisema kuwa  TSA bado inatafuta wadhamini kwa ajili ya kufanisha mashindano hayo na mpaka sasa kampuni za simu ya Vodacom Tanzania imethibitisha kudhamini mashindao hayo kama wadhamini wakuu.
  Kampuni hiyo itagharimia medali na vikombe.

   Wadhamini wengine ni JCDecaux (billboards), Label Promotions (billboards), Print Galore na Slipway Hotel.
  Pia kampuni ya ndege ya Swissair imejithibitisha kudhamini tiketi za ndege za waogeleaji wa Tanzania ambao wanasoma nchini Uingereza ambao wapo kwenye timu ya Taifa. Waogeleaji hao ni Sonia Tumiotto, Smriti Gokarn, Anjani Taylor, Collins Saliboko, Natalie Sanford na Marin De Villard. 
  Alisema kuwa Tanzania itashirikisha waogeleaji 60 wakigawanywa kwa timu mbili (Tanzania A na B) chini ya makocha wao, Alex Mwaipasi na Michael Livingstone.

  Nchi ambazo zimeongezewa muda wa kuthibitisha kushiriki katika mashindano ni Ethiopia, Eritrea, Somalia, Sudani Kusini ambazi zipo kanda ya tatu na za kanda ya nne ni Angola, Botswana, Comoro, Madagascar, Lesotho, Malawi, Mauritius, Seychelles, Msumbiji, Namibia, Zimbabwe na Swaziland.

  Alisema kuwa kwa kamati yao inatafuta wadhamini kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo. Wanahitaji kiasi cha Sh 100 milioni ili kufanya mashindano hayo kwa hadhi inayostahili.
  Alisema kuwa wanatarajia waogeleaji zaidi ya 200 kushiriki katika mashindano hayo ambayo Tanzania ni mabingwa watetezi.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu.
  STARTIMES Tanzania kupitia chaneli yake ya Star Swahili kufungua pazia jipya la shindano la kusaka vipaji vya sauti litakalofanyika jijini la Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Meneja Masoko na Mahusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Sharobaro amesema  mashindano hayo ni fursa tosha kwa washiriki pamoja na ajira kwa washiki pamoja na washindi hao. 

  Amesema kuwa shindano la kusaka vipaji vya sauti litakalofanyika katika maeneo matatu hapa nchini ambayo ni jiji la Dar es Salaam watachukua washindi kumi, jijini Mwanza  watachukua washindi watano na Zanzibar watachukua washindi watano hao wote wataingia fainali itakayohusisha washiriki 20. 

  Washindi wa Shindano la kusaka vipaji vya sauti watapata fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu ya Startimes yaliyopo jijini Beijing nchini China.

  Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Seleman Sewangi amesema kuwa Startimes Tanzania wanasaidia kukuza vipaji vya vijana pamoja na kukuza kiswahili ndani na nje ya Tanzania. 

  Amewaasa Startimes kuangalia namna ya wasanii hao kunufaika na kazi zao mara baada ya kumaliza mikataba. Pia alisisitiza kuwepo namna ya kunufaika kati ya nchi mbili ambazo ni Tanzania na Chini katika kazi hizo za sanaa.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Seleman Sewangi akizungumza kwenye mkutano wa kwanza kati ya Startimes Tanzania pamoja na waandishi wa habari unaohusu shindano la kusaka vipaji vya sauti linaloandaliwa na kampuni ya Startimes kwa kushirikiana na ubalozi wa Chini nchini Tanzania.
  Meneja Masoko na Mahusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Sharobaro akizungumza na waandishi wa habari na wageni mbalimbali kwenye awamu ya kwanza ya kuandaa shindano la kusaka vipaji vya sauti linaloandaliwa na kampuni ya StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa Chini nchini Tanzania litakalofanyika Dar Es Salaam, Mwanza na Zanzibar.
  Mhadhiri kutoka Taasisi ta Taaluma za Kiswahili(UDSM), George Mrikaria akizungumza kuhusu  chuo hicho kitavyoweza kwenda sambamba na Startimes ili kuweza kuwapata washindi wazuri watakaoitangaza pamoja na kukitangaza kiswahili katika nchi mbalimbali hasa nchini China.

  0 0

  Kupitia onyesho hili la Coke Studio linaloandaliwa na kampuni ya Coca Cola muziki wa Tanzania unazidi kutangazwa ikiwemo vipaji vya wanamuziki kutoka hapa nchini ambao wanashirikiana na wenzao kutoka Afrika na linarushwa kwenye luninga kwenye nchi zaidi ya 50 Onyesho la Coca Studio msimu huu barani Afrika linajumuisha wasanii kutoka katika nchi za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Afrika Kusini, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius, Mozambique, DRC na Cameroon. Wasanii wa Tanzania waliopo katika onyesho la Coke Studio msimu huu ni Ali Kiba, Rayvanny, Izzo Bizness, na Nandy.

  Wengine kutoka nchi nyingine ni Khaligraph Jones na Band Becca (Kenya),Sami Dan (Ethiopia),Bebe Cool, Eddy Kenzo, Sheebah, Ykee Benda ( Uganda). 

  Wengine ni Nasty C, Busiswa, Mashayabhuqe kutoka Afrika ya Kusini, Youssoupha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Runtown na Yemi kutoka Nigeria, Dji Tafinha kutoka Angola, Laura Beg kutoka Mauritius,Jah Prayzah na Slapdee kutoka Central Africa Republic, Bisa Kdei na Worlasi kutoka Ghana. 

  Tangia onyesho hili lianzishwe limekuwa kiungo kikubwa cha kuwakutanisha wanamuziki wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na kupiga muziki wenye vionjo kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo kuleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki.
  Baada ya onyesho la pili la Coke studio msimu wa tano kupitia luninga ya Clouds kuacha gumzo kwa washabiki wengi wa muziki,mwishoni mwa wiki katika onyesho la tatu walipagaishwa tena na kolabo za wasanii mbalimbali zenye midundo ya kiafrika na zilizosukwa kwa ustadi mkubwa na magwiji wa kutengeneza muziki.

  Wasanii waliotoa burudani kwenye onyesho la tatu ni mwanamuziki Nandy kutoka Tanzania ambaye amefanya kolabo na mwanamuziki Betty G kutoka Ethiopia ambapo wameimba kwa pamoja vibao vya Don’t break my heart na Mane Fistum, vilivyotengenezwa studio kwa umahiri mkubwa na mtengenezaji wa muziki nguli nchini Nahreel. Wasanii wengine ambao wamefanya kolabo ya kuvutia katika onyesho hilo ni Khaligraph Jones kutoka nchini Kenya akishirikiana na mwanamuziki Bruce Melodie kutoka nchini Rwanda. 

  Kwenye onyesho la pili, Ali Kiba kutoka Tanzania, Patoranking kutoka Nigeria, Ozane kutoka Togo, Sami Dan kutoka Ethiopia, Laura Beg kutoka Mauritus, Sauti Sol kutoka Kenya na Chidinma kutoka Nigeria walionyesha umahiri wao katika tasnia ya muziki na kutawala jukwaa katika onyesho lao lililotengenezwa na nguli wa kutengeneza muziki wa studio barani Afrika kutoka nchini Nigeria, MasterCraft. 

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akizungumza wakati akifungua semina ya siku moja kwa vikundi vya kijamii na wajasiriamali, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Sunrise, Kigamboni jijini Dar es salaa.
  Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, akizungumza katika semina ya siku moja kwa vikundi vya kijamii na wajasiriamali, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Sunrise, Kigamboni jijini Dar es salaam
  Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Rahel Muhando akizungumza wakati alipokuwa akitambulisha sehemu ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa Wilaya hiyo, katika semina ya siku moja kwa vikundi vya kijamii na wajasiliamali, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Sunrise, Kigamboni jijini Dar es salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa (watatu kushoto), Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Rahel Muhando (kulia), Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa pamoja na Meneja wa CRDB Tawi la Mbagala, Midlaster Nsanzugwanko wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina ya siku moja kwa vikundi vya kijamii na wajasiriamali, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Sunrise, Kigamboni jijini Dar es salaam.

  0 0

  MFUKO wa taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umewahimiza wana michezo nchini kuchangamkia fursa ya kujiunga na mpango wa matibabu kupitia  mfuko wa afya ya jamii (CHF) na mfuko wa taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kupata huduma bora za matibabu pindi wanapoumia wakiwa michezoni.

  Rai hiyo imetolewa  mwishoni mwa wiki na meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Ruvuma Abdiel Mkaro wakati wa Bonanza maalum la kuhamasisha jamii hususana wana michezo kujiunga na mfuko huo na kushiriki mazoea mara kwa mara ili kuepuka uwezekano wa kupata magonjwa yasiokuwa ya lazima.

  Aliwataka wana michezo na jamii ya watanzania wakiwemo waandishi wa habari,kuona umuhimu wa kijunga na mpango huo  kwa lengo la kuwa na uhakika wa matibabu  pale  inapotokea kupata ajali na magonjwa ya kawaida.

  Bonanza hilo liliandaliwa na NHIF lilishirikisha michezo mbalimbali kama vile kukimbia,mazoezi ya viungo,kukimbiza kuku pamoja na mpira wa miguu ambap timu ya soka ya Mkambi FC ilifanikiwa kuibuka mshindi  baada ya kuifunga timu ya NHIF 4-2 kwa njia ya Penalti kufuatia matokeo ya kufungana 1-1 ndani ya Dkt 90 za mchezo huo.

  Hata hivyo Bonanza hilo lililoonekana kuvutia watu wengi kutoka maeneo mbalimbali ya manispaa ya Songea, baadhi ya washiriki  wameiomba Nhif kuendelea kuandaa bonanza kama hilo kila mwiso wa mwezi ili kutoa fursa kwa wananchi kushiriki na kufanya mazoezi ili kuepusha uwezekano wa kupata magonjwa.
  Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF mkoa wa Ruvuma Abdiel Mkaro akikagua timu ya Soko ya NHIF wakati wa Bonanza maalum la kuhaamsisha wana michezo mkoa wa Ruvuma kuchangamkia fursa ya kujiunga na mfuko huo kwa ajili ya kupata huduma bora za matibabu pindi wanapoumia.
  Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Ruvuma Abdiel Mkaro kulia akikagua timu ya soka ya Makambi FC kabla ya kuanza mchezo kati ya timu hiyo na timu ya NHIF katika Bonanza la kuhamasisha wana michezo kujiunga na mfuko huo.
  Baadhi ya wafanyakzi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)mkoa wa Ruvuma wakizunguka uwanja wa shule ya msingi Mkambi katika manispaa ya Songea wakati wa Bonanza maalum la kuhamasisha wana michezo kujiunga na mfuko huo ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu pale wanapougua.
  Wafanyakazi wa NHIF mkoa wa Ruvuma Wakifanya mazoezi ya viungo wakati wa Bonanza la kuhamasisha wanamichezo na jamii kuchangamkia fursa ya kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na mfuko wa afya ya Jamii CHF.
  Wafanyakazi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)mkoa wa Ruvuma Salah Kalolo kulia na Edwina Bilungi wakishindana kukimbiza kuku katika Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Makambi Songea mwishoni mwa wiki.

  0 0

  Uwanja wa Majimaji Songea.

  Na. Honorius Mpangala.

  BADO sijafanikiwa kupata majibu na kujua ni nini wanachopewa kamati ya ukaguzi wa viwanja vinavyotumika ligi kuu. Yawezekana kuna mazingira ambayo yanafanyika ili kuweza kuruhusu viwanja kama wa Majimaji Songea kutumika ligi kuu. Januari 2017 katika moja ya makala zangu iliyohusu Viwanja niliandika mengi kuhusu viwanja visivyowatendea haki wachezaji wetu. Na katika hilo moja kwa moja huwezi kupindisha kulielekeza TFF kama wadau namba moja ndipo baadae liende kwa Wamiliki wa Uwanja.

  Nashukuru makala ile nilipata ujumbe mwingi wa simu kutoka maeneo mbalimbali. Hatimaye Uwanja wa Namfua uliokuwa kama picha katika makala ile unarekebishwa. Niliandika kuhusu Namfua ikiwa daraja la kwanza na inapambana kupanda ligi kuu. Watu wa Singida kwa namna moja au nyingine naweza kusema walinisoma na walinielewa kwa sababu Uwanja wao ilikuwa sehemu ya kufungia mifugo kama mbuzi na ng'ombe.

   Shirikisho kuendelea kuwaheshimu watazamaji na kuwanyima raha wale wanaotazamwa uwanjani ni jambo linalosikitisha. Hata ikitokea kama tuna malengo makubwa ya kulifanya soka letu lichezwe maeno mengi  ya nchi basi tuna kazi ya kubadili mitazamo ya viongozi wetu kwa kiasi kikubwa. 

  Uchaguzi mkuu wa TFF umefanya lile rungu la kufungia viwanja baada ya kukaguliwa lisifanye kazi kwasababu ya hofu ya kupunguza kura. Ikiwa tunaelekea kwenye uchaguzi wa shirikisho vifungo kadhaa vilifunguliwa kwa wale waliofungiwa. Hapo ndipo hali ya kiutendaji kwa wakati ule ilipokuwa ya kusaka kura zaidi kuliko kusimamia kwa weledi mambo ya yanayohusu soka.

  Ni aibu kuona uwanja kama wa Majimaji ambao msimu wa tatu mfululizo Tangu timu ilipopanda Mara ya mwisho 2015 kuwa na nyasi zile. Kila msimu kamera za Azam TV zinapokuwa katika uwanja wa huo unasikitika mtazamaji. Viko vibanda umiza ambavyo wamiliki hufikia hatua ya kusema mechi ya Majimaji msilipe kiingilio maana inachezwa Kwenye jaruba lililotoka kuvunwa mpunga hivi punde. Kiuhalisia huwezi kutofautisha kati ya majaruba ya shamba la Nafco Kapunga kule Mbarali Mbeya na eneo la kuchezea la uwanja wa Majimaji. Halafu unakuta chama cha soka eneo hilo kinajinasibu kufanya vyema katika utawala wao. Unaweza kujiukiza maswali mengi kuwa mgawanyo wa mapato kwa wamiliki na chama cha soka yanatumika ipasavyo au ni kama shamba la miwa karibu na shule msingi.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Rwanda na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.

  Nchi hizo mbili zinaungana na nchi nyingine sita zilizothibitisha kufanya hivyo awali kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Chama Cha kuogelea nchini (TSA), Leena Kapadia.
  Kapadia amezitaja nchi hizo kuwa ni Afrika Kusini, Zambia, Kenya, Uganda, Djibouti na wenyeji Tanzania. Kapadia amesema kuwa bado wametoa nafasi kwa nchi nyingine kuthibitisha kushiriki hadi wiki moja kabla ya mashindano ili kuleta mvuto na ushindani zaidi.

  “Tumezipa nafasi zaidi kutafuta fedha ili kushiriki, tutafunga mlango wa kuthibitisha wiki moja kabla ya mashindano,” alisema Kapadia.

  Alisema kuwa TSA bado inatafuta wadhamini kwa ajili ya kufanisha mashindano hayo na mpaka sasa kampuni za simu ya Vodacom Tanzania imethibitisha kudhamini mashindao hayo kama wadhamini wakuu.
  Kampuni hiyo itagharimia medali na vikombe. Wadhamini wengine ni JCDecaux (billboards), Label Promotions (billboards), Print Galore na Slipway Hotel.

  Pia kampuni ya ndege ya Swissair imejithibitisha kudhamini tiketi za ndege za waogeleaji wa Tanzania ambao wanasoma nchini Uingereza ambao wapo kwenye timu ya Taifa. Waogeleaji hao ni Sonia Tumiotto, Smriti Gokarn, Anjani Taylor, Collins Saliboko, Natalie Sanford na Marin De Villard.
  Alisema kuwa Tanzania itashirikisha waogeleaji 60 wakigawanywa kwa timu mbili (Tanzania A na B) chini ya makocha wao, Alex Mwaipasi na Michael Livingstone.

  Nchi ambazo zimeongezewa muda wa kuthibitisha kushiriki katika mashindano ni Ethiopia, Eritrea, Somalia, Sudani Kusini ambazi zipo kanda ya tatu na za kanda ya nne ni Angola, Botswana, Comoro, Madagascar, Lesotho, Malawi, Mauritius, Seychelles, Msumbiji, Namibia, Zimbabwe na Swaziland.
  Alisema kuwa kwa kamati yao inatafuta wadhamini kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo. Wanahitaji kiasi cha Sh 100 milioni ili kufanya mashindano hayo kwa hadhi inayostahili.

  Alisema kuwa wanatarajia waogeleaji zaidi ya 200 kushiriki katika mashindano hayo ambayo Tanzania ni mabingwa watetezi.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii.
  CHUO  Kikuu cha Tiba na Sayansi  Shirikishi  Muhimbili  kupitia Shule ya Famasi  kwa kushirikiana  kwa Kituo cha cha Mafunzo ya kutathimini Dawa cha Afrika Mashariki wameendesha mafunzo ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi. Ubora na usalama wa  dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Afya Duniani (WHO) na Sekeretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wameshiriki katika uratibu wa mafunzo hayo na kutoa misaada ya hali na mali.

  Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mgeni Rasmi,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki amesema mfumo wa kutathimini dawa za Afrika Mashariki ni muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi wa ukanda huo wanapata dawa bora, salama na zenye ufanisi mkubwa.

  Dk. Mpoki amesema mafunzo hayo ya nadharia na vitendo kwa wataalam wa dawa wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki yanalenga  kuhakikisha kuwa dawa zote zilizokidhi vigezo zinasajiliwa kwa mfumo wa ulinganifu unaotumika  baada wataalam hao kujiridhisha kisayansi.

  Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bw. Hiiti Sillo amesema kuwa kumekuwa na ushirikiano wa karibu na wananchi katika utoaji wa taarifa pale wanapoona kuna dawa zenye mashaka ziko mtaani, hivyo kusaidia katika dhima ya kulinda afya ya jamii.

  Amesema kuwa kuanzishwa kituo cha kutathimini Dawa cha Afrika Mashariki kitakuwa ni msaada mkubwa katika kuhakikisha kuwa kila dawa zilizo katika nchi za Afrika Mashariki ni zile zilizosajiliwa na usajili huo ni kwa matumizi ya wananchi wote wa ukanda husika.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi , Ubora na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki yalifanyika jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, Kulia ni Mkurugenzi wa Shahada za awali wa MUHAS, Profesa Mainen Moshi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi, Ubora na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki yalifanyika jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akiwa katika pamoja na Maprofesa wa Chuo cha Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi pamoja na Watalaam jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Agness Francis, Blogu ya jamii
   SSERIKALI ya Tanzania wakishirikiana na serikali ya Korea Kusini  wamezindua utekeleza mradi utakaosaidia kuboresha  upatiikanaji wa  huduma bora  za ardhi  katika mkoa  wa Mwanza  na mradi huo  utanzia Manispaa ya Ilemela na Nyamagana.

  Ambapo  hafla hiyo ya mradi huo umezinduliwa leo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Dkt Angeline Mabula  katika ukumbi wa  Hyatt Regency hoteli Jijini  Dar es Salaam.   

  Katika ushirikiano huo wa kuimarisha utawala wa ardhi nchini ambapo makubaliano rasmi  ya ushirikiano huo yalianza mwaka 2015, ikiwa ni msada wa vifaa vya upimaji na mafunzo yanayohusu  matumizi ya vifaa vya kisasa vya upimaji, nayo yalianza mwaka 2016.

  Naibu waziri Angeline Mabula ametamabaisha kuwa kuleta teknolojia hiyo mpya na nafuu  itarahisishia serikali  upimaji ardhi kwa kupanga na kupima kila kipande, pamoja na kusaidia wananchi kupata kumbukumbu na taarifa za ardhi kwa urahisi.

  Mbali na hayo Dkt Angeline Mabula  ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Korea Kusini kwa kuona umuhimu wa utekelezaji wa mradi  huo ambao utaleta mapinduzi makubwa  katika sekta ya ardhi hapa nchini.
   Balozi wa Korea Kusini Tanzania, Song Geum-Young  akizungumza na mkurugenzi halmashauri ya Manispaa Ilemela pamoja na wakuu wa idara na taasisi wizara ya ardhi kuhusu ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Korea Kusini kuimarisha mfumo bora wa upimaji ardhi kwa urahisi.leo katika uzinduzi uliofanyika kwenye ukumbi Hayyat Regency Hotel Jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa biashara  wa Kampuni ya LX, Cho Man-Seung akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kuwa mradi huo unatarajia kuanza kutekeleza  hivi karibuni na  utakuwa ni wa kisasa zaidi hapa Nchini.
   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dkt Angeline Mabula akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa maradi wa uboreshaji wa huduma za ardhi leo  uliofanyika kwenye ukumbi wa Hayyat Regency Hotel Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na wakuu wa idara na taasisi wizara ya ardhi waliohudhuria uzinduzi huo leo katika ukumbi Hayyat Regency Hotel Jijini Dar es Salaam. (Picha na Agness Francis, Blogu ya Jamii)

  0 0

  Basi la Tashriff lililokuwa likitokea Tanga - Dar es Salaam limewaka moto majira ya saa 8 mchana eneo la Pongwe, Tanga. Kwa mujibu wa taarifa za awali chanzo cha moto huo hakijafahamika japo hakuna mtu aliyezurika japo mizigo yote imeungua.
  Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji Mkoani Tanga wakiendelea na zoezi la uokoaji na kuzima moto kwenye basi hilo. 


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Ian Ferrao (katikati) na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakionyesha mabango yanayoelekeza jinsi yakupata vifurushi vya bando la”Pinduapindua” kwa ajili ya wateja wao hususani vijana wakati wa uzinduzi wa bando hilo ambapo mteja anatakiwa kupiga namba *149*01# kisha kuchagua kifurushi cha siku, cha wiki au cha mwezi,Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Jaquiline Materu, Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Nandi Mwiyombela ,Mkurugenzi wa Masoko, Hisham Hendi na Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma kwa Wateja, Linda Riwa.

  Vijana wakitanzania na wateja wote kwa ujumla wa Vodacom Tanzania PLC,wameletewa Uhuru na wepesi zaidi wa kutumia bando jipya la”Pinduapindua” lililozinduliwa jana na kampuni hiyo likiwa mahususi kwaajili ya wateja wa mtandao huo.

  Akiongea wakati wa Uzinduzi wa huduma hiyo,Mkurugenzi wa biashara na Masoko wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Hisham Hendi alisema huduma ya bando hili jipya la “Pinduapindua” ni ya kwanza na yakihistoria katika kampuni zote za mawasiliano nchini,Hii ni moja ya mikakati ya kampuni yetu kutaka kuleta mabadiliko kwenye jamii hususani vijana kwa kuwarahisishia maisha yao ikiwemo kuongeza vipato na dhamira kubwa yakuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.

  “Utafiti wetu unaonyesha kwamba vijana ni moja ya kiungo kikubwa sana kwa mapinduzi yakiuchumi nchini pia ni tabaka linalokuwa kwa kasi ya kuridhisha na wana mahitaji maalum yakipekee yakiteknolojia tunapenda vijana watambue kwamba Vodacom Tanzania PLC imesikia kilio chao ndiyo maana leo hii tumewaletea Pinduapindua ”, alisema Hendi.

  Pinduapindua ni kifurushi huru na chakipekee zaidi kuliko vifurushi vingine vinavyowapangia wateja wa kampuni zingine za mawasiliano nchini,Bando hili litawapatia vijana na wateja uhuru wao wa kuchagua kiasi cha kupangia kwenye data, kupiga simu (voice) au ujumbe mfupi (SMS) kulingana na mahitaji ya wakati huo. “Pinduapindua” pia itamwezesha mteja kutumia Facebook (ikiwa pamoja na picha), Whatsapp (maandishi na picha) na SMS hadi 200 bure.

  Mkurugenzi huyo alifafanua zaidi kwamba kampuni inaelewa kwamba mahitaji ya wateja wao ya utumiaji hubadilika siku hadi siku kuna siku unaweza kuhitaji matumizi ya mtandao (data) zaidi ya muda wa maongezi, kwa hiyo unakuwa huru kupangilia matumizi ya kifurushi chako kuendana na mahitaji yako na jinsi yakupata vifurushi vya bando

  hili ni rahisi mteja atahitaji kupiga namba *149*01# kisha kuchagua kifurushi cha siku, cha wiki au cha mwezi. Vifurushi hivi vinaweza kulipiwa kupitia muda wa maongezi au Mpesa na mara baada ya kununua, mteja atapatiwa kifurushi chake, Facebook BURE, Whatsapp BURE na SMS, vyote ambavyo vitatumika kwa muda wote wa kifurushi alichochagua” alisema Hendi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Ian Ferrao (katikati) akicheza na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa bando jipya la Pinduapindua kwa ajili ya wateja haswa vijana,Jinsi yakupata vifurushi vya bando hili mteja anatakiwa kupiga namba *149*01# kisha kuchagua kifurushi cha siku, cha wiki au cha mwezi.
  Wacheza shoo wa promosheni ya bando la Pinduapindua la Kampuni ya Vodacom Tanzania wakicheza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Dar es Salaam jana. Jinsi yakupata vifurushi vya bando hili mteja anatakiwa kupiga namba *149*01# kisha kuchagua kifurushi cha siku, cha wiki au cha mwezi.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (kushoto) akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhiwa tablets kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kufanyia Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Kulia ni Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Nadia Belhaj Hassine Belghith.

  Na Emmanuel Ghula.

  OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imepokea Tablets 500 zenye thamani ya Shillingi milioni 400 kutoka Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18.

  Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya tablets hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema kupatikana kwa tablets hizo kutasaidia kurahisisha zoezi la ukusanyaji wa taarifa muhimu za Mapato na Matumizi ya Kaya pamoja na kupunguza gharama ambazo zingetumika kuchapisha madodoso ya karatasi.

  “Ofisi ya Taifa ya Takwimu leo tumepokea tablets 500 kutoka Benki ya Dunia ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Tablets hizi zitasaidia kurahisisha kazi na kupunguza gharama ambazo tungetumia kuchapisha madodoso ya karatasi,” amesema Dkt. Chuwa.

  Dkt. Chuwa amesema utafiti huu utahusisha maeneo wakilishi 796 na kaya wakilishi 9,552 zilizochaguliwa kitaalamu kuweza kutoa matokeo ya viashiria vya umaskini na viashiria vingine. Amesema utafiti huu utatoa takwimu za msingi kwa viashiria vya kiuchumi na kijamii ambavyo vitasaidia kusimamia na kutathmini mwelekeo wa serikali katika harakati zake za kupunguza umasikini. Taarifa za utafiti huu pia zitasaidia kupima utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Awamu ya Pili (FYDP-II) 2016/17 – 20/21 na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs 2030), pamoja na kuwezesha kufanyika kwa tafiti mbalimbali zinazohusu mwenendo wa hali ya umaskini katika ngazi ya Mikoa na Wilaya.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird amesema Benki ya Dunia imetoa tablets hizo kwa NBS ili kurahisisha ukusanyaji wa taarifa kwa kutumia teknolojia ya kisasa badala ya kutumia njia ya madodoso ya karatasi ambayo ni gharama kubwa. Amesema Benki hiyo kwa muda mrefu imekuwa ikishirikiana na NBS katika tafiti mbalimbali na hivyo vifaa hivi ni mwendelezo wa ushirikiano huo katika upatikanaji wa takwimu rasmi nchini ambazo pia hutumika kimataifa katika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

  Kukamilika kwa utafiti huu kutasaidia kupatikana kwa takwimu rasmi zinazohusu Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi zitakazotumika kwa ajili ya kusimamia na kutathmini program mbalimbali za Kitaifa, Kikanda na Kimataifa. Utafiti huu unafanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na idara mbalimbali pamoja na Wadau wa Maendeleo.
  Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Nadia Belhaj Hassine Belghith (kulia) akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi tablets katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kufanyia Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Kulia ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mayasa M. Mwinyi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (kushoto) akipokea tablet kutoka kwa Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Nadia Belhaj Hassine Belghith (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Ofisi ya Taifa ya Takwimu imekabidhiwa tablets hizo kwa ajili ya kufanyia Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18.

older | 1 | .... | 1928 | 1929 | (Page 1930) | 1931 | 1932 | .... | 3272 | newer