Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109921 articles
Browse latest View live

INTRODUCING BANEMBE JEREMIE-MOON (Official Music)


MIGOGORO YA ARDHI ISIZUIE MAWASILIANO VIJIJINI

$
0
0
Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote imeendelea na kazi ya kuhakikisha kuwa wanachi wote waishio vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara wanapata huduma za mawasiliano kwa wakati ili kuweza kuchangia ukuaji wa uchumi na upatikanaji wa huduma za kijamii na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Hayo yameelezwa na Mtendajii Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua ujenzi wa minara ya simu za mkononi na upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwenye maeneo mbalimbali vijijini ya mkoa wa Arusha na Manyara. Eng. Ulanga amesema kuwa migogoro ya ardhi kwenye baadhi ya vijiji mbalimbali nchini inachangia ucheleweshaji wa ujenzi wa minara na ufikishaji wa huduma za mawasiliano vijijini.

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Mfuko huu uliweka lengo la kufikisha mawasiliano kwenye vijiji 4,000 nchi nzima ifikapo mwezi Novemba mwaka huu. Uwepo wa migogoro ya ardhi unachangia kuchelewesha kampuni za simu zilizopatiwa ruzuku na Serikali kujenga minara, “mgogoro wa ardhi kwenye kijiji cha Timbolo kata ya Sambasha Wilayani Arumeru umeichelewesha kampuni ya Halotel kujenga mnara na hivyo wananchi wa kata hii kukosa mawasiliano kwa kuwa mgogoro huo umechukua zaidi ya miaka miwili kukamilika mahakamani,”amesema Eng. Ulanga.

Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya simu ya Halotel wa Mkoa wa Arusha Bwana Philemon Joel amesema kuwa mahakama iliweka zuio la ujenzi wa mnara kwenye eneo la kijiji cha Timbolo kata ya Sambasha ambapo kesi ya mgogoro huo umechukua miaka miwili kufanyiwa maamuzi kwenye ngazi ya mahakama. “Tumekuwa tukienda mahakamani mara kwa mara na kupigwa tarehe kuambiwa Hakimu hayupo na mara nyingine inapita miezi minne bila ya kesi kusikilizwa hivyo imetuchelewesha kuanza ujenzi,”amesema Bwana Joel.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Timbolo, kata ya Sambasha Bwana Samwel Saning’o amesema kuwa Serikali ya kijiji ilisimama na kusema kuwa wanataka mawasiliano na sio utalii kwa kuwa kulikuwa na mgogoro baina ya mmiliki wa eneo la jirani na eneo la mwingine ambapo mnara unatakiwa kujengwa. 

Bwana Saning’o amemshukuru sana Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bwana Alexandra Mnyeti kwa kuingilia kati mgogoro huu, kusimamia na kuhakikisha kuwa unakamilika ili wananchi waweze kupata mawasiliano. Eng. Ulanga amesema ujenzi wa mnara wa Halotel kwenye eneo hili hauwezi kukamilika mwezi Novemba mwaka huu, hivyo sisi kama Mfuko wa UCSAF tutawapatia muda wa ziada ili waweze kukamilisha ujenzi wa mnara na wananchi waweze kupata mawasiliano. Pia Eng. Ulanga amewataka wanachi wa vijiji husika kushirikiana na kampuni za simu kulinda miundombinu ya mawasiliano na minara ili mawasiliano yaweze kupatikana muda wote.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King ametoa rai kwa mamlaka zinazosimamia haki na vyombo vya ulinzi viambata vya Jeshi la Polisi na mahakama kufanya uchunguzi na kuendesha kesi kwa wakati ili kuharakisha kutoa haki. “Ukichelewa kutoa shauri la hukumu kwa jambo la umma linalogusa maslahi ya wananchi unachelewesha maendeleo ya wananchi,”amesema Prof. Norman Sigalla King. Ameongeza kuwa wananchi washirikiane na kampuni za simu za mkononi kulinda minara na kutoa ardhi bila migogoro ili waweze kupata huduma za mawasiliano kwenye vijiji vyao kwa wakati.


Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King ameitaka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kukamilisha ujenzi wa minara yake ya simu kwa wakati kwenye vijiji mbalimbali nchini ili wananchi wa maeneo husika waweze kupata huduma za mawasiliano. Hayo ameyasema Prof. Norman Sigalla King wakati wa ziara ya Kamati yake walipotembelea kijiji cha Sigino kata ya Singo iliyopo wilaya ya Babati Mjini mkoani Manyara. 

Naye Meneja wa TTCL Mkoa wa Arusha na Manyara Bwana Brown Japhet amesema kuwa TTCL imekamilisha ujenzi wa minara kwenye vituo vyote vya Mkoa wa Arusha na viko hewani wananchi wanapata mawasiliano. Bwana Japhet ameilieza Kamati kuwa kwa vituo viwili vilivyobaki vya TTCL kama pale Saitabau, Arusha kulikuwa na mgogoro wa ardhi ambapo Serikali ya Mkoa imeingilia kati na kumaliza mgogoro huo na vituo vingine viwili vipo kwenye hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ambapo vinasubiri tathmini ya mazingira ikamilike ili ujenzi wa minara kwenye vituo hivyo uweze kuanza na suala hili limefikishwa Wizara ya Maliasili na Utalii ili liweze kukamilishwa.

Prof. Norman Sigalla King ameyataka makampuni ya simu kuhakikisha kuwa mawasiliano yanasambaa nchi nzima. Pia ameitaka TTCL kukamilisha ujenzi wa minara yake kwa wakati na kuhakikisha kuwa kila wanapopatiwa ruzuku na Serikali wakamilishe jukumu lao kwa wakati na wafanye kazi kwa ushindani. Ameoneza kuwa Kamati yake imeridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na TTCL. Kamati inazitaka mamlaka nyingine zinazohusika na ujenzi wa minara na upatikanaji wa mawasiliano vijijini washirikiane kwa pamoja na kufanya maamuzi kwa wakati ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za mawasiliano vijijini kwa wakati. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King (wa kwanza kushoto) na wajumbe wengine wa Kamati wakiwa wamekalia mnara wa Halotel wakipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Bwana Philemon Joel (hayupo pichani) kuhusu utayari wa kampuni hiyo kujenga mnara baada ya mgogoro wa ardhi kumalizika kwenye kijiji kijiji cha Timbolo, kata ya Sambasha Wilaya ya Arumeru mkoani Manyara
Meneja wa TTCL Mkoa wa Arusha na Manyara Bwana Brown Japhet (wa pili kushoto) akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) ilipofanya ziara ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini kwenye kijiji cha Sigino kata ya Singo iliyopo wilaya ya Babati Mjini mkoani Manyara. Wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Eng. Peter Ulanga.
Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya simu ya Halotel wa Mkoa wa Arusha Bwana Philemon Joel (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) kuhusu utayari wa kampuni hiyo kujenga mnara kwenye kijiji cha Timbolo, kata ya Sambasha Wilaya ya Arumeru mkoani Manyara baada ya mgogoro wa ardhi kumalizika. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Bwana Albert Richard.
Mwenyekiti wa kijiji cha Timbolo, kata ya Sambasha wilaya ya Arumeru mkoani Manyara Bwana Samwel Saning’o akisisitiza umuhimu wa uwepo wa mawasiliano vijijini mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ziara ya Kamati kwenye kijiji hicho ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini.

15 WAIBUKA KIDEDEA KATIKA MCHEZO WA GOFU KATIKA MASHINDANO MM GOLF TANZANIA.

$
0
0



WACHEZAJI 15 kati ya 50 wa mchezo wa gofu wa mashindano ya MM Gofu Tanzania ambapo mwishoni mwa wiki walitamatisha mashindano ya Robo fainali waliibuka kidedea baada ya kufanya vizuri katika mashindano  yaliyodhaminiwa
 na Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania yaliyokuwa katika viwanja vya Mchezo wa Gofu, Lugalo jijini Dar es salaam.



Wachezaji walioshinda katika mchezo huo ni Steve Lokono, 
Samweli Miginda, 
Patrick, Karimi, 
Sande Walter, na k


wa upande wa wasaidizi ni Wamungu Wagochochi,  MpT Sheko na Kain Mbaya 

Washindi wa mchezo huo wengine ni Fred Laizer na T. Wiliamu.
Z.Hamis, L. Juma, Karim Rasho na kwa upande wa wanawake (MMS), alikuwa ni Karobia.

 Na kwa upande wa watoto  wakiume mshindi ni Wambugu Wagichochi na mshindi kwa watoto wa kike ni A.Eaton, N.Pin na Kain Mbaya

 na mshindi wa Mitupo Mingi ni Mulani Njeru.


Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Mkurugeanzi Mtendaji wa Kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato alisema wameamua kudhamini mashindano hayo kutokana na kuwa wadau wakubwa wa michezo nchini pamoja na utoaji huduma ya mafuta na vilainishi vya magari hapa nchini.

Muhato alisema udhamini wao wa mashindano hayo kwa mwaka huu si mwanzo bali wataendelea kuyadhamini kila mwaka ili kuweza kuuendeleza mchezo huo nchini. 
Mmoja ya wanawake walioibuka kidedea katika mchez wa Gofu akipokea zawadi mara baada ya kutanazwa kushinda katika kitengo cha Gofu wanawake.

 Wachezaji wa timu Gofu inayoshiriki mashindano ya MM Golf Tanzania, Mashindano yanadhaminiwa na Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania yanayoendelea kwa hatua ya robo fainali, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao, kwenye viwanja vya Mchezo wa Gofu, Lugalo jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2017.
 Mchezaji wa timu Gofu inayoshiriki mashindano ya MM Golf Tanzania yanayoendelea kwa hatua ya robo fainali, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta Engen Tanzania, Paul Muhato akipiga moja ya mitupo katika uliofanyika viwanja vya Mchezo wa Gofu, Lugalo jijini Dar es salaam Septemba 23, 2017. Mashindano hayo yanadhaminiwa na Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania.
 Mkurugeanzi Mtendaji wa Kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato akizungumza kabla ya kutoa zawadi kwa washindi wa mchezo wa Gofu wa mashindano ya MM Golf Tanzania yaliyokuwa wakifanyika katika viwanja vya Gofu ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 25,2017

Rais Magufuli amaliza ziara ya siku 6 Mkoani Arusha

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA JUMUIYA YA MADOLA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu leo amefungua mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa Jumuiya ya Madola  katika ukumbi wa mkutano wa Benki Kuu (B.O.T) jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo ambao umezinduliwa leo Septemba 25 hadi,2017  amnbao utafanyika kwa siku tatu ukiwa na kauli mbiu isemayo 'Mahakama Madhubuti, inayowajibika na Jumuishi'. ambapo kutakuwa na maada mbalimbali kutka kwa viongozi ambao ni Majiji na mahakimu.

Akizungumza mara baada ya kufungua mkutano huu Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanzania, Ignas Hatusi amesema kuwa Mkutano huo una lengo la Kujenga mahakama shirikishi, mahakama inayowajibika na mahakama Dhabiti kiutendaji  kwa kuimarisha utendaji wa taasisi za kimahakama.

Pia amesema wanachama hao wa jumuiya ya madola watajifunza kutoka kwa majaji na mahakimu mbalimbali kutoka nchi mbalimbali za jumuiya ya hiyo na ikiwa pamoja kutoa huduma bora kwa wananchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa Jumuiya ya Madola  unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam kwa siku tatu mfurulizo ambapo kauli mbiu ya Mkutano huo ni  'Mahakama Madhubuti, inayowajibika na Jumuishi'.Mkutano huo umehudhuriwa na majaji pamoja na mahakimu wa nje mwanachama wa Jumuiya ya Madola.
Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma  akizungumza katika Mkutano wa Mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa Jumuiya ya Madola  unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu (B.O.T) jijini Dar es Salaam kwa siku tatu Mfurulizo Mkutano huo unakauli mbiu inayosema  'Mahakama Madhubuti, inayowajibika na Jumuishi'.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Majaji pamoja na mahakimu wanawake waliohudhuria mkutano Mkuu wa Mwaka wa Majaji na mahakimu wa Jumuiya ya Madola Unaofanyika jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki kuu (B.O.T) leo Septemba 25, 2017 hadi Septemba 28, 2017.
 Bendi ya Jeshi la Polisi wakiimba wimbo wa Taifa katika mkutano wa Majaji na Mahakimu unaofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ambao umejumuisha wajaji na mahakimu wa wa nchi mwanachama wa jumuiya ya madola.
Baadhi ya Majaji na Mahakimu wakiwa katika mkutano wa Mwaka wa Jumuiya ya Madola leo katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu(B.O.T) jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

RUTAINURWA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA JUMUIA YA WAZAZI WILAYA YA ILALA

$
0
0

NA BASHIR NKOROMO

Lucas Rutainurwa ametawazwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika jana.

Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo, amesema katika Uchaguzi huo uliofanyika Segerea, Rutainurwa (pichani), alipata kura 278 dhidi ya Mohamed Honelo aliyepata kura 148 baada ya hao wawili kuingia katika kinyang'anyiro kwa mara ya pili kufuatia kutopatikana mshindi aliyepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa  katika uchaguzi wa awali.

Wakati katika awamu ya kwanza  Lutainurwa alipata kura 277 Honelo alipata kura 243 huku Celestine Nyalusi akipata kura 67.

Nafasi ya Mjumbe wa Halimashauri Kuu aliyeshinda ni George MJtambalike ambaye amepata kura 195 dhidi ya Edward Haule aliyepata kura 181. PICHA ZA UCHAGUZI HUO/>BOFYA HAPA

Airtel yatoa punguzo ya bei kwa bidhaa zake.

$
0
0
Meneja wa huduma kwa wateja,Celine Njuju akionesha simu na vifaa vilivyopunguzwa bei katika maduka yote ya Airtel nchini, kulia ni Meneja mauzo wa bidhaa za mawasiliano Airtel Bw, Pascal Maziku. Ofa ya simu na vifaa hivyo vya mawasiliano pia inaambatana na ofa ya dakika za muda wa maongezi pamoja, bando la intaneti na SMS bila kikomo kwa miezi sita

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetoa rai kwa wateja kuhakikisha wananunua bidhaa bora zinazopatikana kwenye maduka yake kwani imetoa punguzo kubwa ya bei kwa bidhaa hizo.

Haya yamesemwa na Meneja wa Huduma kwa wateja Celina Njuju huku akithibitisha kuwa bidhaa hizo zitakuwa zikipatikana kwenye maduka yote ya Airtel na hivyo kuwashauri wateja kuhahakisha kuwa wanatumia nafasi hiyo kujipatia bidhaa bora kwa punguzo la bei.
 ‘Tunataka wateja wafaidi fedha zao, siku zimepita ambapo Watanzania walikuwa wanaenda madukani na kununua bidhaa feki kwani kwa sasa tunazo bidhaa halisi kabisa ambazo zinapatikana kwa bei nafuu, alisema Njuju.
Kulingana na Njuju, Wingle USB Modem ambayo hapo awali ilikuwa ikipatikana kwa Tshs60,000 kwa sasa itakuwa ikipatikana kwa Tshs45,000 pamoja na kifurushi cha intaneti cha bure cha 5GB. Uzuri wa hii modem ni kwamba unaweza ukatumiwa na watu mpaka kumi kwa wakati mmoja, alisema Njuju huku akiongeza ya kwamba modem hii inafaa sana kwa watu wanaofanya kazi maofisini, wafanya biashara na wanafunzi.

Kampuni ya Airtel Tanzania pia imetoa punguzo la bei kwa Magnus Bravo Z11 ambapo hapo awali ilikuwa inauzwa Tshs79,000 lakini kwa sasa ni Tshs69,000 ambapo pia itakuwa na kifurushi cha bure cha 12GB, dakika 300 kupiga mitandao yote na sms 300 kwa muda wa miezi sita. Pia kwenye punguzo ni simu ya Huawei Y3C ambapo hapo awali ilikuwa ikipatikana kwa Tshs140,000 na kwa sasa itakuwa inauzwa Tshs100,000 na itakuwa na kifurushi cha 12GB, dakika 300 kupiga mitandao yote na sms 300 kwa muda wa miezi sita.

Wateja pia watajipatia simu aina ya FERO 280 kwa Tshs30,000 kutoka bei ya awali ya Tshs38,000 ambapo itakuja na 150MB, dakika 150 kupiga Airtel kwenda Airtel na sms 150 kwa muda wa miezi mitatu.
 ‘Natoa wito kwa wateja wa Airtel kujitokeza na kufaidika na punguzo la bei ya bidhaa hizi kwenye maduka yote ya Airtel nchi nzima kwani muda wa punguzo ni mdogo, alisema Njuju.

TPSC YAASWA KUFANYA TAFITI ZA KUSAIDIA JAMII

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza katika mahafali ya 27 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) yaliyofanyika mkoani Singida mwishoni mwa wiki
Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakiwa katika mahafali ya 27 ya Chuo hicho hivi karibuni mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema( wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wa pili kushoto ni Mkuu wa chuo hicho na Mtendaji Mkuu Dkt. Henry Mambo. 


Na  mwandishi Wetu, Singida
Serikali imekitaka Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzani (TPSC) kufanya tafiti, kutoa mafunzo na kutoa ushauri unaolenga kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwa sasa ikiwamo umasikini.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika mahafali ya 27 ya TPSC kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Angellah Kairuki, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi alisema kuwa  mafunzo yanayotolewa na chuo hicho pia yalenge katika kukabiliana na Rushwa, mmomonyoko wa maadili na kufanya kazi kwa mazoea katika sekta ya umma.

“Ni matumaini yangu kuwa aina ya mafunzo na shauri za kitaalam zinazotolewa na zinazoendelea kutolewa na chuo hiki zitakwenda sambamba na maboresho katika sekta ya umma na pia kuwawezesha watumishi wa serikali na na wale watakaoingia serikalini siku za usoni kukabiliana na mabadiliko yanayoendelea hapa nchini na Duniani kote,” alisema.

Alisema kuwa katika kuelekea Tanzania ya Viwanda serikali inasisitiza mafunzo na tafiti zinazofanywa na chuo hicho kujikita katika kuandaa watu mahiri , wenye weledi na ujuzi utakaotumika kuisaidia kuendana na kasi ya ukuaji wa viwanda na hivyo kutimiza ndoto za Rais Dkt.John Pombe Magufuli za kujenga Tanzania ya Viwanda.

Alisema kuwa   serikali inaunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na taaisi hiyo zenye lengo la kuboresha huduma mbalimbali zitolewazo na chuo baadhi ya maboresho hayo yakiwa ni kuanzishwa ka kozi za shahada katika fani za Uhazili na Menejimenti ya Kumbukumbu,Ukamilishaji wa mchakato wa ujenzi wa jengo la Maktaba katika Tawi la Tabora sanjari uandaaji wa mpango wa ujenzi (Master Plan) Tawi la Singida.

Awali katika Mahafali hayo Mtendaji Mkuu wa TPSC Dkt.Henry Mambo alisema kuwa  wahitimu 6332 walihitimu mkatika mahafali hayo wakitoka katika matawi sita ya chuo hicho yaliyoko katika mikoa ya Singida, Dar es Salaam, Mtwara, Tanga,Mbeya na Tabora.

Dkt. Mambo alizitaja aina za vyeti na idadi ya wahitimu kwenye mabano kuwa ni Astashahada ya Awali (2,368),Astashahada (1,781) na Stashahada (2183).
Alisema katika kuelekea Uchumi wa kati, ifikapo mwaka 2025 chuo kimeendela kuboresha huduma zake mbalimbali ikiwamo usimikazi wa utoaji elimu bora yenye viwango  vya kukidhi hali ya soko la ajira na kiushindani.
“Pia tunaendeleza watumishi wetu ili wafikie viwango vinavyohitajika,” alisema.
Mkuu huyo wa Chuo alisema kuwa TPSC imeendelea kufanya vizuri katika eneo la tafiti na machapisho na shauri za kitaalam ili kubaini changamoto zilizopo katika utumishi wa umma na kutoa majawabu ya changamoto hizo kupitia tafiti.

TANESCO KANDA YA KASKAZINI YAUNGANISHA WATEJA WA MUDA MREFU KWA ASILIMIA 89.9

$
0
0


IMEELEZWA kuwa, kati ya wateja 48,661 waliolipia huduma ya kuunganishiwa Umeme na  TANESCO kupitia Ofisi yake ya Kanda ya Kaskazini, tayari wateja 43,733 ambao ni sawa na asilimia 89.9 wameshaunganishiwa huduma hiyo kufikia Agosti 31 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Meneja wa TANESCO, Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Stella Hiza wakati akiwasilisha ripoti kwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe kuhusu utekelezaji wa Maagizo ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini aliyoyatoa kwa watendaji wa TANESCO tarehe 2 Septemba, 2017 mjini Dodoma.

Miongoni mwa  maagizo yaliyotolewa na Dkt. Kalemani ni kuhakikisha wateja wote waliolipia huduma ya kuunganishwa Umeme wameunganishwa  ifikapo mwezi Desemba mwaka huu na kubadilisha mita za zamani  na kuweka mita mpya za LUKU kwa wateja wote wa umeme pamoja na kufikisha huduma karibu na wananchi.

Mhandisi Hiza aliongeza kuwa katika wateja  waliounganishiwa Umeme, 35577 walikuwa hawahitaji nguzo na 8156 walihitaji nguzo za Umeme. 

Akizungumzia suala la uanzishwaji wa ofisi ndogo katika kila wilaya ili kusogeza huduma karibu na wateja, Hiza alisema kuwa katika baadhi ya wilaya Ofisi zimekwishaanzishwa na mpaka kufikia Tarehe 31, Agosti mwaka huu, kulikuwa na jumla ya ofisi ndogo 14 katika kanda hiyo. 
Aidha alibainisha kuwa, ifikapo tarehe 1 mwezi Oktoba mwaka huu, wanatarajia kufungua ofisi ndogo nyingine 11 katika Kanda husika.

Kuhusu zoezi la ubadilishaji wa mita kwenda kwenye mfumo wa LUKU, alisema kuwa mkoa wa Manyara umeshabadilisha mita kwa wateja wote na kueleza kuwa jumla ya mita 39,860 zinahitajika ili kukamilisha zoezi hilo ambapo mkoa wa Arusha zinahitajika mita 10,730,   Kilimanjaro mita 23,130 na Tanga mita 6,000.

Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe, aliagiza Watendaji wa TANESCO kufanya kazi kwa bidii na kuwa wazalendo ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma stahiki.

Pamoja na kuipongeza TANESCO kwa kutekeleza majukumu yao,  Prof. Mdoe aliwataka watendaji hao kuwa wabunifu na kutafuta njia  zitakazowasaidia kubaini watu wanaojihusisha na wizi wa Umeme ili kuliwezesha Shirika kupata mapato yake.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini akiwa  katika ofisi ya TANESCO, mkoa wa Tanga. Anayesalimiana naye ni Meneja Wa TANESCO mkoa wa Tanga, Mhandisi Abdulrahman Nyenye na kulia kwake ni Meneja wa TANESCO kanda ya Kaskazini, Mhandisi Stella Hiza.
 Mhandisi Stella Hiza akisoma ripoti ya utekelezaji wa majukumu katika Kikao na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James Mdoe.
 Kaimu Katibu Mkuu akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa TANESCO, Mkoa wa Tanga, Mhandisi Abdulrahman Nyenye.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe akizungumza wakati wa kikao chake na Watendaji wa TANESCO,  Kanda ya Kaskazini.

NAIBU SPIKA ATOA ZAWADI YA PIKIPIKI NA PESA TASLIMU KWA WASHINDI WA TAMASHA LA TULIA TRADITIONAL FESTIVAL 2017

$
0
0
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wa tatu kulia) akimkabidhi funguo ya Pikipiki Kiongozi wa Kundi la Ngoma la Kannengwa Rungwe, Nolbert Mwandinga, baada ya kundi lake kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Ingoma Kituli, wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Katika Tamasha hilo jumla ya washindi 10 wa kwanza kutoka kila kundi walizawadiwa Pikipiki.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akicheza ngoma ya asili ya kundi la  Banyampulo ya kabila la Wanyakyusa, wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Katika Tamasha hilo jumla ya washindi 10 wa kwanza kutoka kila kundi walizawadiwa Pikipiki.
 Wacheza Bao Gabriel Mwasankinga wa timu ya CCM (kushoto) akichuana na Pascal Mbwelembweta wa timu ya Kawechele, kutafuta mshindi wa tatu katika mchezo wa fainali za mchezo huo kuadhimisha Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Picha na Muhidin Sufiani.

Dkt. Harrison Mwakyembe awapongeza JWTZ katika Uhifadhi wa Kumbukumbu za Kitaifa.

$
0
0
Na Benedict Liwenga-WHUSM.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amelipongeza Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kuhifadhi vema kumbukumbu za Mashujaa wa Tanzania waliopigana vita na kusaidia ukombozi katika baadhi ya nchi za jirani ikiwemo nchi ya Msumbiji.

Pongezi hizo amezitoa leo Mkoani Mtwara wakati alipotembelea maeneo ya kumbukumbu ya Kitaifa ambapo kwa Mkoani hapo ametembelea eneo la Mashujaa lililopo Nailendele lengo likiwa ni kujionea maeneo yaliyoweza kuhifadhiwa kumbukumbu zake za ukumbozi wa Bara la Afrika ikiwemo mahitaji ya ziada ya maeneo hayo.

Mhe. Mwakyembe amesema kwamba, kazi kubwa inayofanyika katika kuyatembelea maeneo hayo ni kujua kumbukumbu za maeneo hayo ikiwemo kuongea na mashuhuda wa matukio ya kumbukumu za maeneo husika kwa ajili ya kuandika historia ya Afrika kwa ushahidi uliotafutwa na Waafrika wenyewe.

“Tunakipinid kifupi kuhakikisha kuwa kumbukumbu zote tuizonazo tunazihifadhi, tunaandika historia yetu sisi wenyewe Waafrika badala ya kuandikiwa na Waliotutawala huko nyuma kwa ushahidi tulioutafuta wenyewe”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Ameongeza kuwa JWTZ imefanya kazi kubwa ya kuhifadhi baadhi ya maeneo ya kumbukumbu za kitaifa, jambo ambalo litarahisisha utunzaji wa kumbukumbu hizo kwa ajili ya Mradi wa Ukumbozi wa Bara la Afrika.

“Tumeanza kukubaliana wote katika SADC na katika nchi za Afrika, ni lazima tuingize katika mitaala ya shule zetu hizi harakati za ukombozi wa Bara la Afrika ili vizazi vijavyo viweze kufahamu mambo haya hususani tulikotoka na tunakoelekea”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha, katika ziara hiyo Mhe. Mwakyembe alipata wasaa wa kuongea na Uongozi wa Mkoa wa Mtwara ambapo ameupongeza kwa uongozi huo kwa kuja na Mpango wa Usajili wa Vizazi vya Watoto waliopo chini ya Umri wa Miaka Mitano ambapo Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kesho Wilayani Tandahimba.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia baadhi ya picha za Mashujaa wa Ukombozi waliopigana Vita nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akionyeshwa ramani iliyotumika wakati wa Ukombozi nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiangalia bango linaloelezea kumbukumbu za Mashujaa wa Ukombozi waliopigana Vita nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia mchanga wa makaburi yaliyofukuliwa ya Mashujaa wa Ukombozi waliopigana Vita nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia moja ya silaha za kivita iliyotumiwa na Mashujaa wa Tanzania wakati wa Vita vya Ukombozi nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

MWILI WA MAREHEMU PRAIVETI MUSSA JUMANNE WAAGWA HOSPITALI KUU YA JESHI LUGALO

$
0
0
 
 Askari wa JWTZ wakibeba Jeneza la mwili wa marehemu Praiveti Mussa Jumanne Muryery tayari kwa safari ya kuelekea Dodoma kwa ajili ya mazishi. Mwili wa Marehemu uliagwa leo katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT.MAGUFULI AWASILI JIJINI DAR ES SALAAM MARA BAADA YA KUMALIZA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda pamoja na viongozi wengine wa Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam wakati akitokea Mkoani Arusha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam wakati akitokea Mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam wakati akitokea Mkoani Arusha. PICHA NA IKULU

CRDB BANK YACHANGIA MIL. 100 ZA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU JIJINI DAR

$
0
0
Mkurungenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 100 kwa ajili ya kusaidia Ujenzi wa ofisini za walimu wa Shule za msingi na Sekondari za jijini Dar es salaam, leo Septemba 25, 2017. Makabidhoano hayo yamefanyika kwenye ofisi ya ya Mkuu wa Mkoa. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa ofisi hizo za waalimu, Kanali Charles Mbuge na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kupokea mchango wa shilingi milioni 100 uliotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Ujenzi wa ofisi za waalimu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurungenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa ofisi hizo za waalimu, Kanali Charles Mbuge.
Mkurungenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam wakati wa kukabidhi mchango wa shilingi milioni 100 uliotolewa kwa ajili ya Ujenzi wa ofisi za waalimu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akifafanua jambo wakati akihamisha pesa kuchangia Ujenzi wa ofisi za walimu jijini Dar es Salaam kwa kutumia Huduma ya SimBanking, ambapo alichangia shilingi milioni moja.
Picha ya pamoja na kamati ya Ujenzi wa ofisi za walimu jijini Dar es Salaam. 

Serikali Kuendelea Kuiwezesha Muhimbili Kutoa Huduma za Kibingwa

$
0
0

Na John Stephen, Muhimbili

Dar es Salaam, Tanzania. Serikali imesema itaendelea kuiwezesha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) katika mikakati yake ya kutoa huduma bora za afya zikiwamo za ubingwa wa hali ya juu pamoja na upasuaji katika maeneo mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katika hospitali hiyo wakati akizindua vyumba viwili vya upasuaji wa watoto wadogo (Pediatrick operating theatres) vyenye thamani ya Dola za Marekani 675,000 sawa na Tsh. 1.5 bilioni pamoja na uzinduzi wa wodi ya watoto yenye vitanda 25.

Katika uzinduzi huo Waziri Mwalimu ameitaka Muhimbili kutokutoa rufaa kwa mgonjwa yoyote ambaye anaweza kupatiwa mabatibabu katika hospitali hiyo.

“Narudia tena, hata kama ni mimi au kiongozi yoyote asipewe rufaa kama ugonjwa wake unaweza kutibiwa hapa, mimi naweza kuja hapa nikawashinikiza mnipeleke nje, msikubali, simamieni taaluma yenu. Kama madaktari wamezibitisha mgonjwa anaweza kutibiwa hapa, hakuna haja ya kupelekwa nje,” Mhe. Ummy.

Vyumba hivyo vya upasuaji vimewekewa vifaa vya upasuaji kwa msaada wa mfuko wa ARCHIE WOOD FOUNDATION ya Scotland. “Napenda kuwashukuru kwa namna ya pekee wahisani wetu Sir.Ian Wood na mtoto wako Garret Wood ambao mlipoletewa wazo la kuisaidia Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia taasisi yenu ya Archie Wood Foundation mlilipokea kwa mikono miwili na kulitekeleza. Nichukue nafasi hii kwa niaba ya Serikali chini ya Uongozi wa wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwashukuru sana kwa msaada huu,” amesema Waziri Ummy Mwalimu.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akizindua vyumba viwili vya upasuaji wa watoto wadogo leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Wood na Archie, Sir. Ian Wood na maofisa wengine wakiwa kwenye uzinduzi huo leo.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiangalia baadhi ya vifaa vilivyotolewa na Mfuko wa Wood na Archie katika vyumba vya upasuaji wa watoto wadogo kwenye hospitali hiyo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza kabla ya kuzindua vyumba vya upasuaji wa watoto. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dk. Julieth Magandi na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wood na Archie, Ian Wood akiwa kwenye mkutano huo leo.
 Baadhi ya watoto wanaotibiwa katika hospitali hiyo wakiwamo madaktari, wauguzi na baadhi ya watumishi wakimsikiliza Waziri Ummy Mwalimu leo.

USAFI WA VYOO NI MUHIMU KWA AFYA YA WATUMIAJI WAKE.

$
0
0
Matumizi ya vyoo vya kulipia ni changamoto kubwa kwa wahisani wanaothubutu kujenga miradi ya vyoo katika masoko kadhaa katika manispaa ya kigoma ujiji, ikiwemo choo hiki kama kionekanavyo pichani, kilichopo soko la mwalo wa Kibirizi .Pamoja na choo hicho kuwa cha kulipia lakini mandhari yake si salama hata kidogo kwa watimiaji wake,kutoka na kuzungukwa na taka taka ambazo zingeweza kuondolewa na choo kikabaki safi na salama kwa watumiaji.Picha na Magreth Magosso kigoma.

MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA USAFIRI WA MAJINI DUNIANI YAFANYIKA MKOANI KIGOMA

$
0
0
Ofisa habari wa shirika la meli Zanzibar (ZPC) Rabia Khamis akiwaelimisha wakazi wa Mkoa wa Kigoma juu ya huduma wazitoazo katika kampuni hiyo leo kwenye maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Usafiri wa Majini Duniani uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mlole halmashauri ya manispaa ya kigoma ujiji . Picha na Magreth Magosso kigoma.

DC HANDENI, GONDWIN GONDWE AKABIDHI ARDHI YENYE HEKARI 282 KWA UZALENDO KWANZA

$
0
0
Na Kajunason/MMG-Handeni-Tanga. 

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Godwe amekabidhi ardhi yenye ukubwa wa hekari 282 katika kijiji cha Kitumbi kwa wasanii na wadau wengine wanaofanya kampeni ya UZALENDO KWANZA. 

Akizungumza wakati akikabidhi ardhi hiyo katika kijiji cha Kitumbi, Handeni mkoani Tanga, alisema kuwa hatua hiyo inalenga kukuza kilimo na maendeleo katika kijiji hicho ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Dkt. John Pombe Magufuli kuendeleza nchi ya viwanda na biashara. Wadau wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza wakiwemo wasanii wa filamu, muziki na wachezaji mpira wa zamani wameamua kushiriki katika maendeleo ya taifa kwa kujihusisha na kilimo tofauti na kazi zao za kila siku za sanaa. 

 "Handeni ni sehemu ambayo korosho, alizeti, ndizi vinakuwa sana na niwaambie tu mapema mwakani kiwanda kutengeneza juisi ya nanasi kinafunguliwa Kwa Msisi, tena kitakuwa na uwezo wa kuchukua tani 80,000 za nanasi kwa mwaka na kitakuwa cha pili Afrika kwa kuzalisha juisi ya nanasi, hapo kazi kwenu kuchangamkia fursa," Alisema Mhe. Gondwe. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, msanii Steve Nyerere alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Gondwe na vingozi wa kijiji kwa kuwapa eneo la kuwekeza katika sekta ya kilimo. 

 "Sisi tunawashukuru wote kwa moyo mliotuonyesha, hatuna cha kuwalipa bali tutapambana kwa nguvu zetu ili kutimiza malengo ya eneo mlilotupa, Uzalendo Kwanza Oyeeee!," alisema Msanii Steve Nyerere. Nae diwani wa Kata ya Kitumbi, Charles Abeid amewakaribisha wasanii hao kwa mikono miwili na kuwaomba wawasaidie kumalizia ujenzi wa zahanati yao ambao umekuwa ukisua sua kutokana na kukosekana kwa fedha.
UZALENDO KWANZA wakiongozwa na mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Gondwe wakielekea katika kijiji cha Kitumbi wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga, ambapo walipatiwa Mashamba yenye ukubwa wa hekari 282 za ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa Kilimo. Picha zote na Kajunason/MMG-Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Godwe akiongea mara baada ya kuwakabidhi ardhi yenye ukubwa wa hekari 282 katika kijiji cha kitumbi kwa wasanii na wadau wengine wanaofanya kampeni ya UZALENDO KWANZA. Tukio hilo lilifanyika kijijini Kitumbi, Muheza - Tanga mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Msanii Steve Nyerere akitoa shukrani zake za pekee kwa mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Gondwe mara baada ya kuwakaribisha wana- UZALENDO KWANZA na kuwapatia hekari 282 za ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo katika kijiji cha Kitumbi wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga.
Diwani wa Kata ya Kitumbi, Charles Abeid akiwakaribisha wasanii na wadau wengine wanaofanya kampeni ya UZALENDO KWANZA.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJARIWA AHANI MSIBA WA ALIYEKUWA MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM WILAYA YA RWANGWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa Pole, Bi. Maudia Abdaallah ambaye ni Mjane wa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Ruangwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya ya Ruangwa, Marehemu Selemani Bakari wakati alipokwenda kuhani msiba huo, Majohe, Ilala jijini Dar es salam Septemba 25, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO 9669 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji katika msiba wa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Ruangwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ruangwa , Marehemu Selemani Bakari wakati alipokwenda Majohe wilayani Ilala jijini Dar es salaam kuhani msiba huo, Septemba 25, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 109921 articles
Browse latest View live




Latest Images