Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1914 | 1915 | (Page 1916) | 1917 | 1918 | .... | 3348 | newer

  0 0

  When I asked the General Manager of Business Times Newspaper, Aga Mbuguni, to give me a column in his newspaper, it was the beginning of an exhilarating journey into the life of a vocal coach, in that not only was I inspired to write, I was motivated.

  I wanted to bring what was happening in my classroom, or shall we say—studio, to readers all across Tanzania in written content and with links to supporting audio and video illustration.

  What you’re now about to enjoy is a book filled with a collection of my very best articles, containing an array of scintillating tips for singers.

  And so—finally, here's a warm welcome to the highly anticipated must-have book for singers all around the world, 101 Letters from a Vocal Coach!

  Walking you through almost every conceivable vocal problem imaginable, and zeroing in on solutions as they unfold in my voice studio, is probably the most essential fabric of this book, because in the pages of this extraordinary memoir lie the answers to seemingly insurmountable problems concerning the voice, and most importantly, singing.

  101 Letters from a Vocal Coach is stacked with riveting case studies and is written in a style that is not only informal, it is an easy read. And that is the beauty of it... as the last thing you want is a publication that looks more like an ostensibly boring text book.

  The book, whose release date is yet to be announced, will be rolled out in two phases: the first being a digital release via Canadian bookstore platform Lulu; followed by a paperback release on the same platform several months later.

  Included with the eBook is a collection of audio vocal training exercises, namely, the English version of Joett Vocal Drills Vol. 1-7 in MP3 format; Whilst, the publication in paperback is to include the exact same audio files on CD.

  I have thoroughly enjoyed working on this book project over the past couple of years, and I’m certainly hoping you will enjoy reading my memoirs. I guarantee that you will come away with loads of helpful information to help you become a better singer.


  You Are the Instrument, Learn to Sing Like a Pro!

  JOETT
  101 Letters from a Vocal Coach
  Private Singing Lessons

  0 0

  Na Fredy Mgunda,Iringa.

  Wadau wa kilimo na wakulima wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma wamenufaika utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) uliokuwa na lengo la Kutambua na kuelewa vigezo vinavyochangia katika upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima wadogo na kutathimini mfumo wa kikanuni/ kisheria wa udhibiti wa pembejeo.

  Akizungumza wakati wa mkutano huo mkuu wa idara ya miradi ya ANSAF, Edna Lugano alisema kuwa waliamua kufanya utafiti kwa lengo la kumkomboa mkuliwa mdogo kuondokana na changamoto zinazomrudisha nyuma kimaendeleo.

  “tunatekeleza mradi wa miaka miwili unaolenga uimarishaji utekelezaji wa sera wezeshi za kilimo na uratibu unawezesha upatikanaji wa pembejeo (mbegu, mbolea na viuatilifu) kudhibiti soko na kuhamasisha upatikanaji wake kwa wakulima wadogo” alisema Lugano.

  Lugano alisema kuwa utafiti ulilenga kutazama mahitaji ya pembejeo na kiwango cha usambazaji kwa kutazama aina chache za mazao, Ufanisi wa mfumo wa kudhibiti ubora wa pembejeo za kilimo na jitihada zinazofanywa na serikali pamoja na wadau wengine katika kudhibiti biashara ya pembejeo zisizo na ubora.

  “Kumekuwa na malalamiko mengi yanayohusu uwepo wa mbegu na mbolea zisizo na ubora zinazowasababishia hasara kubwa wakulima wadogo wadogo ili kutatua changamoto hizo tumekuja na huu utafiti unaoweka mambo mengi wazi na jinsi gani ya kutatua kero hizo” alisema Lugano.
  Mkuu wa idara ya miradi ya ANSAF, Edna Lugano akizungumza wakati wa mkutano na Wadau wa kilimo na wakulima wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma wamenufaika utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) ambao una lengo la kutatua changamoto za wakulima wadogo wadogo kufikia kuwa wakulima wa kati ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuelewa vigezo vinavyochangia katika upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima. 
  Baadhi ya washiriki walioshiriki mkutano wa kutambulisha utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) uliokuwa na lengo la Kutambua na kuelewa vigezo vinavyochangia katika upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima.  0 0

  Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Francis Massawe (katikati) 'akinyakuanyakua' na askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa wanaulinda mwenge wa uhuru baada ya kumaliza mbio zake Mkoani humo kwa kutembelea miradi 53 ya thamani ya sh6.874 bilioni na kuingia Mkoani Kilimanjaro.  Picha na Joseph Lyimo

  0 0

  Mwakilishi wa Jimbo Tunguu Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said akizungumza na wananchi wa Jimbo lake katika Tawi la CCM Unguja Ukuu Kae Pwani Wilaya ya Kati Unguja wakati wa hafla ya kukabidhi fedha Vikundi 13 vya Ushirika vya Wananchi wa Kae Pwani Unguja. Mchango huo umetolewa na Mbunge na Mqwakilishi kuchangia vikundi hivyo kwa ajili ya kutunisha mifuko ya vikundi vya vinavyojishughulisha na ujasiriamali wa kutengeneza bidhaa na kilimo na kukupeshana, hafla hiyo imefanyika katika Tawi la CCM Ungua Ukuu Kae Pwani.

  Vikundi vilivyokabidhiwa fedha hizo ni Tushikamane,Hatutaki Shari, Nia Njema,Aso Mtu Ana Mungu,Siri Moyoni, Tuwe Nao,Pita na Zako,Hatutaki Kero,Hapa Kazi Tu, Mkorofi Sio Mwezetu,Hawavumi, Imani Moja na Wajibu Wetu.
  Baadhi wa Viongozi wa Vikundi vya Ushirika katika Shehia za Kae Pwani Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja wakati wa hafla hiyo. 
  Sheha wa Shehia ya Kae Pwani Ndg. Khamis Ibrahim akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi fedha kwa Vikundi vya Ushirika vua Shehia hiyo zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo la Tunguu Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika Tawi la CCM Unguja Ukuu Kae Pwani.
  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohamrd Said akimkabidhi fedha Mwenyekiti wa Kikundi cha Tushikamano wakati wa hafla hizo kukabidhi fedha hizo zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi kutunisha Mfuko wa Kikundi Chao.


  0 0

  Mawakala wa Benki ya CRDB maarufu kama Fahari Huduma Wakala mjini Songea, wakifuatilia kwa makini mafunzo ya uborosheji wa huduma kwa wateja yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB. Pichani Ofisa wa benki hiyo, Willy Kamwela, akifafanua jambo kuhusu mafunzo hayo.
  Mawakala wa benki ya CRDB maarufu kama Fahari Huduma Wakala mjini Songea, wakiwa katika mafunzo ya uborosheji wa huduma kwa wateja yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB.

  Ofisa wa Benki ya CRDB, Tom Mwaisenye, akitoa mafunzo kwa Fahari Huduma Wakala-Mjini Songea kuhusu namna bora ya uendeshaji na usimamizi wa biashara ya Uwakala wa Benki ya CRDB.

  Ofisa wa Benki ya CRDB, Hemed Kiluvia, akitoa mafunzo kwa Mawakala wa Fahari Huduma mjini Songea kuhusu namna bora ya kuzingatia taratibu za Uwakala.


  0 0
  0 0


  Mratibu wa Kongamano la CCCB,Shabani Yusuph (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu
  ufunguzi wa kongamano hilo litakalo fanyika Septemba 19-20 mwaka huu katika hoteli ya Ramada Mbezi Beach jijini Dar es Salaam,a,ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Hamis Kigwangalla.kushoto ni Mkufunzi wa Vijana,Hamza Jabir
  Mkufunzi wa Vijana,Hamza Jabir akifafanua jambo kwenye mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Mchungaji Ipyana Mwamugobole wa  mjini Wuppertal nchini Ujerumani ameandika na kuchapisha kitabu kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa vyuo na wa sekondari katika kushinda majaribu au challenges wanazokabiliana nazo wawapo kwenye mazingira ya masomo. Kitabu kinaitwa:NGUVU YA MUNGU DHIDI YA MAJARIBU YANAYOWAKABILI WANAFUNZI VYUO VYA ELIMU YA JUU . Yeyote anayetaka kitabu hiki awasiliane naye kwa whatsapp namba hii: +4915216408459.  0 0

  Kutoka Kulia Mwenyekiti wa Watanzania Korea Bw Othman Hailey, Afisa Balozi Japan John Kambona Balozi Batilda Masuka na Katibu wa Tanzania Korea Bi Debora wakiwa VIP launch baada Balozi kuwasilisha na kufanya Mahojiano na magazini ya Korean Post.
  Balozi Batilda Masuka mwenye Maua Akiwa na Uongozi wa Watanzania Korea wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mkurugenzi wa Namtho Trading Bw Othman Hailey, Katibu wa watanzania Korea Bi Debora na Mjumbe Bi Isebella Katondo Pamoja na Afisa Balozi Bw John Kambona.
  Baada ya kuwasili Kituo cha Kazi Korea ya Kusini.

  0 0

  Ndugu wasanii, jamaa, marafiki, wadau wa sanaa na haki za watoto Tanzania 
  Kamati ya Maandalizi ya Mazishi inapenda kutoa tangazo rasmi la shughuli 
  ya kuuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu
  Sista Jean Pruitt itakayofanyika siku ya Jumatano tarehe 20/09/2017 katika viwanja vya Karimjee hall jijini Dar es salaam.

  Wadau wote mnaombwa kuwasili mapema kwa ajili ya kutoa heshima zetu za mwisho. Shughuli za kuuaga mwili zitaanza kuanzia saa 3:30 asubuhi.
  Ibada ya mazishi itafanyikia hapo hapo viwanja vya Karimjee na baada ya  hapo Mwili Utakabidhiwa kwa Watawa wa Maryknoll kwa hatua nyingine za maziko.
  Raha ya milele umpe Ee… Bwana 
  na mwanga wa milele umwangazie,
  apumzike kwa Amani,
  Amina!
  Kamati ya Maandalizi ya Mazishi.


  Dear Friends,
  You are respectfully invited to attend the funeral service of Sr. Jean Pruitt, which will take place on Wednesday 20th September at Karimjee Hall, Posta, along Sokoine drive, Dar es Salaam. The service is expected to start at 9:30am where we invite you to pay your final respects.
  Prayer session will be conducted at Karimjee and after last respects; Sr. Jean's coffin will be taken by the Maryknolls to her final resting place.
  Let’s come together to celebrate the life of Sr. Jean Pruitt as we bid her farewell and pray for her soul to rest in eternal Peace.
  Please share the information with others who have also been touched by her life and saddened by her passing
  Preparation Committee

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameyataka makampuni ya simu nchini kuhakikisha mawasiliano ya simu yanapatikana wakati wote katika ubora unaotakiwa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma inayowiana na thamani ya fedha wanayolipa.

  Akikagua na kuzindua minara ya simu ya kampuni za TTCL, VODACOM, HALOTEL, na TIGO katika Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, Profesa Mbarawa amesema Serikali itaendelea kushirikiana na kampuni za simu kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF ili katika kipindi cha miaka mitatu ijayo sehemu zote za Tanzania ziwe zimefikiwa na huduma ya mawasiliano ya simu ya uhakika.

  “Tumieni mawasiliano ya simu kufanya biashara, kuboresha huduma za jamii kama elimu na habari ili kukuza ustawi wa maisha yenu”, amesema Profesa Mbarawa.Waziri Prof. Mbarawa amewaonya wananchi kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya simu kwani ipo sheria kali inayodhibiti matumizi mabaya ya simu.

  Amezungumzia umuhimu wa kampuni za simu kujenga minara katika maeneo mapya na kukarabati minara ya zamani ili kuwezesha mawasiliano kuwa katika ubora maeneo yote ya nchi.Amewataka wakazi wa vijiji vya Letugunya, Leshata na Chakwale kutumia fursa ya upatikanaji wa mawasiliano kuongeza uzalishaji wa mazao na kuyauza kwa bei nzuri na hivyo kukuza uchumi wao.

  Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote Mhandisi Peter Ulanga amemhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa mfuko huo umejipanga kukamilisha miradi yote kwa wakati na kufanya uhakiki wa takwimu za mawasiliano nchi nzima ili kubaini maeneo ambayo yana changamoto kubwa ya mawasiliano na kuyatatua.

  Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe amemshukuru Waziri Mbarawa kwa kuboresha huduma za mawasiliano katika Wilaya hiyo na kumhakikishia wananchi watailinda miundombinu hiyo ili idumu kwa muda mrefu.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akikagua jenereta linalowezesha mnara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), katika eneo la eneo la Gairo Hill,wilayani Gairo, Mkoani Morogoro. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bibi. Siriel Mchembe.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bibi. Siriel Mchembe, kabla ya kuzungumza na wananchi wa kata ya Leshata, wilayani Gairo, Mkoani Morogoro.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akimsikiliza Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF), Mhandisi Peter Ulanga (kulia) alipokagua minara ya simu wilayani Gairo, Mkoani Morogoro.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akitoa maelekezo kwa Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania mara baada ya kufungua mnara wao katika kijiji cha Chakwale wilayani Gairo, Mkoani Morogoro.

  0 0  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa  Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.


   Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Juma (Mabodi) alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) kuzungumza na Wajumbe wa kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 18/09/2017.
  Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakiwa katika kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani)
   Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakifuatilia kwa makini taarifa zilizotolewa katika kikao hicho kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea na ushahidi wa upande wa utetezi dhidi ya kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji kwa kuwa Hakimu anayeendesha kesi hiyo anamajukumu mengine ya kiofisi.

  Kutokana na hayo, kesi hiyo sasa itasikilizwa kwa siku tatu mfulukizo, Septemba 25, 26, na 27 ambapo mashahidi wa utetezi watafika kutoa ushahidi wao kwa kuanza na Manji. Wakili wa Serikali Mwandamizi Timon Vitalis ameileza mahakama kuwa, kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikiliza shahidi wa upande wa utetezi ambapo Manji mwenyewe alitakiwa kuanza kujitetea lakini kutokana na kuchelewa kuanza asingeweza kuendelea kwa kuwa anasafiri kikazi.

  Hakimu Cyprian Mkeha alimuuliza Manji kwa nini alichelewa kufika na hali alitakiwa kufika asubuhi ya saa tatu, alisema kuwa aliambiwa na wakili wake kuwa Hakimu ameenda kwenye kikao Mahakama kuu na hakujua kama amerudi mapema.

  "Samahani mheshimiwa niliambiwa haupo, nikadhani haujarudi, samahani sana Mheshimiwa" amesema Manji.

  "Ni kweli, nilienda kwenye kikao Mahakama kuu lakini nilirudi mapema na sasa natakiwa kwenda tena huko" amesema Mkeha.
   Yusuf Manji akiwasili Mahakani hapo kusikiliza kesi inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya.
  Yusuf Manji azungumza na Nahodha wa Timu ya Yanga, Nadir Haroub nje ya Mahakama ya Hakumu Mkazi Kisutu, Mchana huu.

  0 0

  Wadau wa sekta ya bima nchini wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (aliyekaa wa tatu kulia) katika mkutano wa 20 wa siku ya bima nchini uliofanyika mwisho wa wiki jijini Tanga. Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania.

  TANGA: Taasisi ya Bima Tanzania imesherehekea mkutano wa 20 wa siku ya bima nchini kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali katika ufufuaji wa viwanda vya zamani nchini.

  Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania, pia ulikutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya bima wa ndani na nje ya nchi, wizara mbalimbali na taasisi za umma na sekta binafsi mwishoni wa wiki jijini Tanga. Raisi wa Taasisi hiyo, Bosco Bugali alisema Taasisi hiyo inatambua umuhimu wa ujenzi wa viwanda vipya pamoja na ufufuaji wa viwanda vya zamani kwani viwanda huleta mabadiliko kiuchumi na maendeleo kwa binadamu.

  “Mada kuu ya mwaka huu ni ‘Bima – Nguzo ya Viwanda’, mada hii inaonesha sera ya Serikali ya viwanda na inaonesha ahadi yetu kuelekea ajenda hii. Tunajiunga na Raisi wetu, Dk. John Pombe Magufuli ambaye alisisitiza mara kwa mara juu ya kukuza viwanda kwani viwanda huleta mbadiliko ya kiuchumi na maendeleo kwa binadamu”, alisema Bugali.

  Aliongeza kuwa huduma za bima zinajumuisha jitahada ambazo serikali inafanya katika kukuza uchumi kwenda hatua nyingine. Nayo Serikali imeipongeza Taasisi ya Bima Tanzania kwa kuandaa mkutano huo na kutoa wito kwa makampuni ya bima yaliyopo nchini kutanua wigo wa huduma zake kwa kutoa huduma kwa mashirika yanayokuja kufanya uwekezaji wa viwanda ili kumudu ushindani wa soko hilo kimataifa na kuwanufaisha wananchi walio wengi wakiwamo wakulima, wafugaji, wavuvi na wajasiliamali wadogo. Waziri wa Fedha na Mipango, Dr Philip Mpango alitoa wito huo kupitia hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela.

  “Iwapo makampuni ya hapa nchini yataweza kutoa huduma ya bima katika uwekezaji mkubwa unaotarajiwa kufanyika nchini ni wazi kuwa licha ya kukuza biashara, kuongeza ajira lakini faida kubwa itabaki Tanzania na hayo ndiyo matarajio ya Rais wetu John Magufuli”, alisema.

  Kamishna wa Bima nchini, Dr Baghayo Saqware alisema ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kufanyika nje ya Dar es salaam tangu mwaka 1987 na kwamba itakuwa ikifanyika mikoani lengo likiwa ni kufuata karibu fursa za kiuchumi ziliko. Alisema wadau wa sekta ya bima walioshiriki mkutano huo pia waliweza kutembelea kiwanda cha saruji cha Rhino, Mapango ya amboni na hospitali ya bombo ambako walitoa msaada kwa wagonjwa.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela akifungua mkutano mkuu wa 20 wa siku ya bima nchini uliofanyika mwisho wa wiki jijini Tanga. Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania ambapo mada kuu ya mwaka huu ilikuwa ni “Bima – Nguzo ya Viwanda”.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (kulia) akifurahia tuzo ya shukurani aliyopewa na Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania, Rukia Adamu (kushoto) kama utambuzi wa mchango wa Serikali katika sekta ya bima katika mkutano wa 20 wa siku ya bima nchini uliofanyika mwishoni wa wiki jijini Tanga.
  Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima, Rukia Adamu akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 20 wa siku ya bima nchini uliofanyika mwisho wa wiki jijini Tanga.
  Wadau mbalimbali wa sekta ya bima wakifwatilia kwa makini mkutano wa 20 wa siku ya bima nchini uliofanyika mwisho wa wiki jijini Tanga. Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania ambapo mada kuu ya mwaka huu ilikuwa ni “Bima – Nguzo ya Viwanda”.
  Wadau mbalimbali wa sekta ya bima wakifwatilia kwa makini mkutano wa 20 wa siku ya bima nchini uliofanyika mwisho wa wiki jijini Tanga. Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania ambapo mada kuu ya mwaka huu ilikuwa ni “Bima – Nguzo ya Viwanda”.

  0 0

  Ujerumani imeipatia Tanzania kiasi cha Euro milioni 198.5 sawa na Sh. Bilioni 520.86 zilizotumika kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo ya Maliasili na Mazingira, Afya, Maji, Nishati, Udhibiti wa Fedha za Umma (Good Financial Governance) na Kusaidia Huduma za Wakimbizi katika mkoa wa Kigoma, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

  Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban wakati wa tukio la Tanzania na Ujerumani kusaini kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano ya Kimaendeleo (Bilateral Development Consultations) ambapo Ujerumani imeonesha nia ya kuendelea kuisaidia Tanzania katika Sekta hizo kuanzia mwaka 2018 hadi 2021.

  Kumbukumbu za Mashauriano hayo zimesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Naibu Mkuu wa Idara ya Kanda ya Afrika Mashariki katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani Bw. Georg Rademacher kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani. 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto) na Naibu Mkuu wa Ushirikiano wa kiuchumi Kanda ya Afrika Mashariki kutoka Ujerumani Bw. Georg Rademacher wakibadilishana kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano baada ya kusainiwa katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
   Wajumbe kutoka Ujerumani waliohudhuria Mkutano wa Mashauriano ya Maendeleo kati ya Tanzania na nchi hiyo wakisikiliza kwa makini maelezo ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (hayupo pichani) akieleza mafanikio ya msaada wa nchi hiyo katika Nyanja za Afya, Maji, Nishati na Utawala wa Fedha, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
   Maafisa waandamizi kutoka Tanzania wakifuatilia kwa makini Mkutano wa Mashauriano ya Kimaendeleo kati ya Tanzania na Ujerumani yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
   Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt. Detlef Wachter (wa pili kushoto) akizungumza kuhusu nia ya nchi yake kuisaidia Tanzania katika miradi ya Nishati, Maji, Utawala wa Fedha na Afya kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka 2018, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (wa nne kushoto) na Naibu Mkuu wa Ushirikiano wa kiuchumi Kanda ya Afrika Mashariki kutoka Ujerumani Bw. Georg Rademacher (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa waandamizi kutoka Ujerumani na Tanzania baada ya kusainiwa kwa kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano, katika ofisi za  Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
   Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mamelta Mutagwaba akipeana mkono na Naibu Mkuu wa Ushirikiano wa Kiuchumi Kanda ya Afrika Mashariki kutoka Ujerumani Bw. Georg Rademacher (kushoto) baada ya kusainiwa kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano ya Maendeleo kati ya nchi hizo mbili Jijini Dares Salaam.
  Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mamelta Mutagwaba akisalimiana na Wajumbe wa Mkutano wa Mashauriano ya Maendeleo kati ya Tanzania na Ujerumani, katika viunga vya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).
  0 0


  0 0


  Mawakala wa Benki ya CRDB maarufu kama Fahari Huduma Wakala mjini Songea, wakifuatilia kwa makini mafunzo ya uborosheji wa huduma kwa wateja yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB. Pichani Ofisa wa benki hiyo, Willy Kamwela, akifafanua jambo kuhusu mafunzo hayo.
  Mawakala wa benki ya CRDB maarufu kama Fahari Huduma Wakala mjini Songea, wakiwa katika mafunzo ya uborosheji wa huduma kwa wateja yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB.
  Ofisa wa Benki ya CRDB, Tom Mwaisenye, akitoa mafunzo kwa Fahari Huduma Wakala-Mjini Songea kuhusu namna bora ya uendeshaji na usimamizi wa biashara ya Uwakala wa Benki ya CRDB. 


  0 0
 • 09/18/17--04:39: Article 0
 • Karibu kilimo joint upate huduma mbali mbali za kilimo na ufugaji- mbolea, madawa ya wadudu, chakula cha samaki, vifaranga vya samaki, upimaji wa udongo na kukupa ushauri wa kilimo BURE - wasiliana nasi kwenda - 0683556677  unaweza pia kufollow page yao ya Instagram na Facebook @kilimojoint

  0 0

   Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii inaeleza kwamba, Ajali mbaya iliyohusisha magari mawili (Lori la Basi ndogo aina ya Toyota Coaster) imetokea karibu na mto Katonga, barabara ya Masaka huko Kampala Uganda usiku wa kuamkia leo na kudaiwa kupoteza maisha ya Watanzania takribani 13. 

  Tangazo la Ajali ya Gari TZ 540 DLC

  Gari tajwa hapo juu lilipata ajali karibu na mto Katonga, barabara ya Masaka kuamkia leo tarehe 18/09/2017.

  Lilikuwa likiwarudisha Watanzania wa Familia ya Bw Gregory Teu ambao walikuja kwenye harusi tarehe 16/09/2017 hapa Kampala. Bibi harusi ni mtoto wa Bw na Bibi Gregory Teu wa Dar es salaam.

  Jumla ya abiria waliokuwa kwenye gari ni abiria 19. Kati yao 13 wamefariki dunia na 6 wamelazwa Nsambya hospital.

  Ubalozi unaendelea kufuatilia msiba huu pamoja na kupata majina yote ya waliokufa na kunusurika.

  Naibu Balozi  Mh. Maleko pamoja na Brigedia Generali S S Makona wameelekea Nsambya Hospital kuona Walio nusurika.

  Asante sana
  Ofisi ya Ubalozi
  Majina yaliyopatikana kufuatia ajali hiyo.

  MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI -AMEN

older | 1 | .... | 1914 | 1915 | (Page 1916) | 1917 | 1918 | .... | 3348 | newer