Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1915 | 1916 | (Page 1917) | 1918 | 1919 | .... | 3272 | newer

  0 0

  MCHEZAJI na Mwalimu wa Mchezo wa mpira wa Mgongo (Hoki), Osman Bairu aiomba Serikali kusaidia kujenga viwanja vya mpira wa Magongo hapa nchini. 

  Hayo amesema wakati akizungumza wa Michuzi Tv katika viwanja vya Tanganyika Pekazi jijini Dar es Salaam wakati wa mashindan ya mchezo wa Magongo uliohusisha Timu A na Timu B za shule ya Msingi Kawe jijini Dar es Salaam.Pia amewaomba wazazi kuwaruhusu watoto wao kwenda kufanya mazoezi pamoja na ili mchezo huo upate kwenda mbali zaidi.
  Mwalimu na Mchezaji wa mpira wa Magongo (Hoki), Osman Bairuakiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa Timu A na Timu B kabla ya mashidano yati ya Timu Hizo mbili za kutoka Shule ya msing Kawe B jijini Dar es Salaam.

  Mwalimu na Mchezaji wa mpira wa Magongo (Hoki), Osman Bairu akizungumza na Michuzi TV jijini Dar es Salaam wakati wa mchuano wa mchezo wa Magongo kati ya Timu A na Timu B ya shule ya Msingi Kawe B jijini Dar es Salaam .Ambapo Mchezo huo ulifana sana na Timu ya ya mchezo huo waliweza kufungana 5-2 Timu A walifunga mabao matano na Timu B walifuga mawili.
  Wachezaji wa Timu A wakijaribu kunyang'anya Mpira Mchezaji wa Timu B wakati wa Mashindano ya Kirafiki  uliofanyika katika viwanja vya Tanganyika Pekazi jijini Dar es Salaam. 
   Mchezo ukiendelea kati ya Tmu A na Timu B za shule ya Msingi Kawe B jijini Dar es Salaam.  0 0  0 0

  Jiji la Mwanza limepima viwanja 24,000. Ikiwa ni utekelezaji wa dhana ya kuondokana na Makazi Holela katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

  Akizungumzia mafanikio hayo hivi karibuni; Mratibu wa masuala ya Urasimishaji, jijini Mwanza, ambaye ni Afisa Mipango Miji; Athuman. S. Simba alisema; “Katika kufanikisha utekelezaji uliofanyika; Halmashauri ya Jiji iliunda vikosi kazi vipatavyo kumi na tatu (13) na kuvipangia majukumu mbalimbali. Vikosi kazi hivyo vilifanya kazi za uandaaji wa michoro ya mipangomiji, upimaji, ukaguzi wa viwanja na kumilikisha”

  Aidha, Katika zoezi zima la upimaji wa viwanja 24,000. Taarifa yake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza; Hosiana B. Kusiga; imesema kuwa; Viwanja 19417 vimepimwa (Approved), maeneo ya Kata za Buhongwa, Mkolani, Igoma, Mhandu, Luchelele, Mahina, Isamilo, na Nyegezi. Vile vile, Viwanja 5515 vimefanyiwa upimaji wa awali (Dermation). 

  Kazi ya upimaji inaendelea katika kata za Butimba, Mahina, Mkolani, Lwahnima, Igoma, Mhandu, Kishiri na Luchelele. Ambapo Idadi ya viwanja vilivyokamilika na vilivyo kwenye upimaji wa awali (demarcation) jumla yake ni 25,032. Utekelezaji wa upimaji huu ni kutoka kwa agizo la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mhe. William Lukuvi, kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kuandaa Hati Miliki za viwanja 35,000 kupitia mradi wa urasimishaji makazi holela .
  Wataalam wa Upimaji/ Wapima kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiendelea na zoezi la upimaji - Mahina, ambapo Ukuta unaoonekana pichani unategemewa kuondolewa kupisha utengenezwaji wa barabara za Mitaa.
  Wataalam wa Upimaji/ Wapima kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiendelea na zoezi la upimaji - Mahina, ambapo beckon zimekuwa zikiwekwa katika viwanja.
  Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipuli, Kata ya Mahina; Rajabu Jumanne (mwenye shati la bluu) akishuhudia zoezi la upimaji linavyoendelea katika Mtaa wake, likiongozwa na Mratibu/ Mpima; Yohana Cleophace wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
  Muonekano wa Barabara iliyochongwa rasmi na Wataalam wa Upimaji/ Wapima kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiendelea na zoezi la Urasimishaji katika kata ya Ipuli, Mahina.

  0 0


  Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia umetoa msaada wa vitabu vya ziada 285 kwa wanafunzi 200 wa Shule ya Sekondari Bugisha, ikiwa ni sehemu ya jitihada za mgodi huo kusaidia maendeleo ya elimu nchini.Msaada huo ni sehemu ya ufadhili ndani ya programu ya CanEducate inayoendeshwa na kampuni hiyo.

  CanEducate ilianzishwa mwaka 2010 lengo kuu likiwa ni kudhamini wanafunzi wa shule za sekondari kutoka katika familia maskini. Chini ya programu hiyo, wafanyakazi huchangisha fedha chini ya mfuko maalumu na kisha kampuni ya Acacia hutoa kiwango sawa na kile kilichochangishwa. Fedha hutumika kulipa ada za shule, kununua sare, vitabu na vifaa vya shule kwa wanafunzi.

  Wakati wa kuanzishwa kwake, mpango huo uliwasaidia wanafunzi 158 walio karibu na Mgodi wa Dhahabu ya Bulyanhulu. Hata hivyo, kutokana muitikio mkubwa kutoka kwa wafanyakazi na makandarasi wa Acacia, programu imeweza kukua zaidi na kuwafikia zaidi ya wanafunzi 800 kutoka shule zinazoizunguka Buzwagi.

  Moja ya sababu ambazo zinachangia kufanya vibaya kwa wanafunzi katika mitihani yao ya kidato cha nne na cha sita, ni ukosefu wa vitabu mashuleni, na gharama za vitabu ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa kifedha wa wazazi na walezi.
  Katika eneo la Buzwagi, mpango huo unahusisha shule tatu za sekondari; Shule ya Sekondari ya Bugisha, Shule ya Sekondari ya Mwendakulima, na Shule ya Sekondari ya Nyasubi ambazo zimetoa wanafunzi bora katika mitihani ya kidato cha nne na kidato cha sita.

  Msaada uliotolewa kwa Shule ya Sekondari ya Bugisha ulisimamiwa na maafisa mahusiano ya jamii wa mgodi wa Buzwagi, Yunia Wangoya na Antonia Kiondo.

  Msaada huo ulitolewa mbele ya walimu, wazazi na wanafunzi ambao kwa pamoja walitoa shukrani zao za dhati kwa kampuni ya Acacia kwa kuwezesha upatikanaji wa msaada huo mkubwa.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kwa kushirikiana na sekta wa usafiri wa anga wameandaa kongamano usafiri huo kwa lengo kujadili namna ya kuinua na koboresha zaidi sekta ya usafiri wa anga katika uchumi wa taifa.

  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamza Johari amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kutokana na sekta ya Usafiri wa Anga katika kufikia uchumi wa kati 2025.

  Amesema kuwa katika mada watakazo jadili ni  kupungua kwa shehena zinazosafiri kupitia viwanja vya ndege ikiwemo Samaki zinazovuliwa katika Ziwa Vicktoria kutumia kiwanja cha ndege cha Entebe  cha nchini Uganda na Maua ya Mkoa wa  Kilimanjaro na Arusha   kutumia uwanja wa ndege wa Mombasa nchini Kenya.Hamza amesema mkutano huo ndio utatadhimini hali ya usafiri  ili kuboresha masuala mbalimbali ya usafiri wa anga katika kufanya uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere  kiunganisha  kwa safari za ndege.

  Amesema  kuwa mkutano huo unafanyika mara mbili kwa mwaka ili kuangalia masuala mbalimbali ya usafiri wa anga kutokana na umuhimu wa sekta hiyo katika ukuaji wa uchumi.Mgeni Rasmi katika Mkutano huo atakuwa ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi , Profesa Makame Mnyaa Mbarawa  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi- Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho.

  Amesema katika ukaguzi wa Shirika la Usafiri wa Anga (ICAO)  kwa Mamlaka hiyo  imepata asilimia 64.4  katika mwaka huu  kutoka asilimia 37. 5  mwaka 2013.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), Hamza Johari akizungumza  leo na  waandishi wa habari juu ya mkutano wa wadau wa usafiri  anga utaofanyika Septemba 18 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
  Wandishi wa habari wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), Hamza Johari wakati akitangaza mkutano wa wadau utaoanza kesho, jijini Dar es Salaam

  0 0


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Uongozi wa Simba umesema kuwa hauna mpango wa kuachana na kocha mkuu wa timu yao Mcameroon Joseph Omog kama kwenye vyoimbo vya habari na mitandao ya kijamii  walivyoandika kuwa wana mpango wa kumtema.

  Akizungumzia suala hilo, Afisa habari wa Simba Hajji Manara, amesema Kamati ya utendaji ya klabu hiyo sambamba na Kaimu Rais Salim Abdallah wamezungumza na kocha Omog na kumueleza kuwa afanye anachoona kinawezekana katika kusaidia timu kufanya vizuri.

  Manara amesema uongozi na kamati tendaji unamuamini kocha huyo huku wakiwataka mashabiki kumuacha kocha afanye kazi yake na kuacha kutunga maneno ambayo si kauli za viongozi wa klabu hiyo.

  "Kumekuwa na tabia ya mashabiki kufurahia timu ikishinda na kuona ni timu yao lakini timu inapofanya vibaya wanamsukumia kocha na kuzusha kwenye mitandao mbalimbali kwa kusingizia uongozi umesema ili watugombanishe na benchi la ufundi", alisema Manara.

  Mbali na hilo Manara amedai kuwa kwa sasa hawapo tayari kumfukuza kocha kwa kuwa wamejifunza kubadilisha makocha kila mara sio sababu ya kupata ushindi bali ni kujiweka pabaya zaidi.

  Kuhusu mechi ya Simba na Mbao timu inaondoka kesho alfajiri huku akidai kuwa watakosa huduma ya wachezaji wao wawili akiwepo Said Mohamed 'Ndunda' ambaye anaenda India kwa matibabu na Shomari Kapombe ambaye ataanza mazoezi wiki hii.
  Afisa habari wa Simba Haji Manara akizungumzia maamuzi ya kamati ya utendaji ya kutokuachana na kocha mkuu wa timu hiyo Mcameroon Joseph Omog.

  0 0

   Mshindi wa Sh 15 Milioni kupitia  promosheni ya Tusua Mapene inayoendeshwa na Vodacom Tanzania PLC,Bw. Imani Makundi, akifurahia kwenye duka la kampuni hiyo lililopo PPF jijini Mwanza jana baada ya kukabidhiwa kitita chake.
   Meneja Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Mkoa wa Mwanza Victoria Chale(kulia) akimakabidhi pesa zake Mshindi wa Sh 15 Milioni ya promosheni ya Tusua Mapene Imani Makundi, kwenye hafla iliyofanyika jijii Mwanza jana.
  Imani Makundi ambaye ni Mshindi wa Sh 15 Milioni kupitia  promosheni ya Tusua Mapene inayoendeshwa na Vodacom Tanzania PLC, Akiondoka na kitita chake huku akifurahia jambo na wateja wa Vodacom Tanzania  kwenye duka la kampuni hiyo lililopo PPF jijini Mwanza jana baada ya kukabidhiwa kitita chake na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Mkoa wa Mwanza Victoria Chale(Hayupo pichani) .  0 0

  Mkufunzi Nuria Mshare akitoa mada kuhusu ushawishi na utetezi kwa maafisa miradi wa asasi za vijana kuhusu namna ya kufanya shughuli ushawishi, utetezi na ufuatiliaji wa haki za vijana katika ngazi ya serikali za mitaa, kitaifa na kimataifa kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Saddam Khalfan (Afisa wa Program - UNA Tanzania) akielezea kuhusu sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na mchakato wa kupitia upya sera hiyo na mchakato wa kukusanya maoni ya sera ya maendeleo ya vijana kwenye mkutano uliowakutanisha asasi mbalimbali za vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society ili kuwajengea uwezo katika ushawishi na utetezi na ufuatiliaji wa haki za Vijana.
  Rais Wa Chama ca Walimu wenye Uziwi(CWUT), Theresia Nkwera(kulia) akipata ufafanuzi wa mafunzo kwa vitendo kutoka kwa Bi Eliza William wakati wa uwasilishwaji wa mada  kuhusu usashwishi na utetezi kwa maafisa miradi wa asasi za vijana kuhusu namna ya kichambua sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na mchakato wa kupitia upya sera.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO. 

  Chama cha Wazazi na Watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo,Akili na Viungo Tanzania (CHAWAUMAVITA) kitafanya maadhimisho ya siku ya mtindio wa ubongo duniani kwa lengo la kuipa jamii uelewa juu ya changamoto wanazozipata watoto wenye matatizo hayo na kuwaleta pamoja familia zinazolea watoto hao ili wabadilishane uzoefu.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa chama hicho, Hilali Said alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo.

  “Kwa kawaida Siku ya Mtindio wa Ubongo duniani huadhimishwa kila Jumatano ya kwanza ya mwezi Oktoba lakini kwa mwaka huu itaadhimishwa tarehe 6, ambapo yanategemewa kufanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mjimwema vilivyopo wilaya ya Kigamboni na tunategemea mgeni rasmi wa maadhimisho hayo atakuwa Mkuu wa Wilaya hiyo”, alisema Said.

  Said ameongeza kuwa nchi mbalimbali Duniani huadhimisha siku hiyo kwa kutoa elimu ya ulemavu wa aina hiyo kwa wananchi ili kupunguza athari zinazojitokeza kwa wazazi na watoto wenyewe pamoja na kuwasaidia wanachama kutetea na kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (CHAMAUMAVITA) Bw. Hilally Said (katikati), akisisitiza jambo mbele ya Waaandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya maadhimisho ya Watoto wenye Mtindio wa Ubongo yatakayofanyika tarehe 6 oktoba mwaka huu leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa CHAMAUMAVITA Taifa, Bi. Mwanahamis Hussein, na Mweka Hazina wa CHAMAUMAVITA Taifa Bi. Jane Kim.
  Katibu wa Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (CHAMAUMAVITA) Taifa, Bi. Mwanahamis Hussein (katikati) akizungumza mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya maadhimisho ya watoto wenye Mtindio wa Ubongo yatakayofanyika tarehe 6, Oktoba mwaka huu leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa CHAMAUMAVITA Bw. Hilali Said na Mweka Hazina wa CHAMAUMAVITA Taifa Bi. Jane Kim.
  Mweka Hazina wa Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (CHAMAUMAVITA), Bi. Jane Kim akielezea maadhimisho ya Watoto wenye Mtindio wa Ubongo yatakayofanyika tarehe 6, Oktoba mwaka huu mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani, Kushoto ni Mwenyekiti wa CHAMAUMAVITA Bw. Hilali Said. Picha zote na Thobias Robert, MAELEZO.  0 0

  Kocha wa timu ya soka ya Taifa ya wanawake wenye umri wa chini ya miaka 20 (Tanzanite), Sebastian Nkoma, ameipongeza kikosi chake kwa kiwango walichokionyesha kwenye mechi dhidi ya Nigeria iliyofanyika Jumamoisu kwenye Uwanja wa Samuel Ogbemudian mjini hapa.

  Akizungumza baada ya mchezo huo, Nkoma, alisema kuwa kufungwa ni sehemu ya mchezo, lakini aliweka wazi vijana wake walipambana ila hawakuwa na bahati ya kupata matokeo waliyoyatarajia.

  Kocha Nkoma alisema anaamini watafanya vizuri katika mechi ya marudiano itakayofanyika jijini Dar es Salaam huku akisema wana nafasi ndogo ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
  Mchezo wa marudiano utafanyika Oktoba mosi, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam, uliko Chamazi, Dar es Salaam.

  "Kazi haijamalizika, mmefanya kazi kubwa na mmewashangaza wote walioiangalia mechi hii, waliamini wangepata ushindi mnono zaidi ya huu, naamini tutafanya vyema katika mechi ya marudiano," alisema kocha huyo ambaye pia anafundisha timu ya wakubwa ya wanawake ‘Twiga Stars’.

  Mkuu wa Msafara, Amina Karuma, alisema kuwa mapambano bado yanaendelea na anaamini kikosi chake kitashinda katika mechi ya marudiano itakayochezwa baada ya wiki mbili.

  "Msife moyo wanangu, huu ndio mpira na unamatokeo ya aina tatu, naamini mtawashangaza tena tukia nyumbani," alisema Karuma ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake Tanzania (TWFA) .

  Aliongeza kuwa anashikuru wachezaji wote ni wazima na wataendelea na kambi ili kujiandaa na mchezo wa marudiano huku akiahidi kuwatafutia mechi ya kirafiki kabla ya kuwakaribisha Nigeria.
  Kocha wa timu ya soka ya Taifa ya wanawake wenye umri wa chini ya miaka 20 (Tanzanite), Sebastian Nkoma.

  0 0

  We are devastated to inform our clients, partners and stakeholders of the death of our very own, Muganyizi Mutta, who was our Public Relations Director. 

  Mutta passed away on Saturday afternoon, September 16, 2017 at Mwananyamala Hospital in Dar es Salaam after a sudden illness. We have not only lost a member of Aggrey & Clifford family, but also a friend. 

  Always in suits, Mutta was gregarious, charismatic and a hard worker with a big heart. Mutta joined Aggrey & Clifford-Tanzania in January 2016 until his sudden passing. 

  We will always remember and treasure the time that we have had the pleasure of knowing and working with him. 
   May his soul rest in eternal peace - AMEN.

  Issued by the management of
   Aggrey & Clifford-Tanzania

  UPDATES ZA MSIBA

  Misa: Kinondoni Roman Catholic (Hananasif) saa 5 asubuhi.

  Kuaga:  kanisani Roman Catholic (hananasif) saa 8 mchana

  Maziko: Makaburi ya kinondoni.


  Siku: Jumanne (kesho)

  0 0


  Na. Neema Mathias-MAELEZO.

  Askofu wa kanisa la Good News For All, Dkt. Charles Gadi ametoa wito kwa wananchi na serikali kuyatunza mazingira na uoto wa asili ili kuchangia uwepo wa hali nzuri ya hewa.

  Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Askofu Gadi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo aliongoza maombi maalum kwa lengo la kuombea tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa juu ya uwezekano wa kutokea kwa upungufu mkubwa wa mvua za vuli katika mikoa mingi hapa nchini.

  Askofu Gadi amesema kuwa wananchi wote wanapaswa kulinda mazingira ikiwemo kupiga vita ukataji ovyo wa miti na badala yake wapande miti kwa bidii ili kuilinda mazingira kutokana na uharibifu unaosababisha ukame unaotokana na ukosefu wa mvua.

  Aidha askofu huyo amesema kuwa wao kama viongozi wa dini wanakubaliana na utabiri wa kisayansi uliotolewa ambao mara nyingi umekuwa ukifanikiwa, lakini haitokuwa sawa kusubiri hadi hali hiyo ya ukame itakapotokea wakati Mungu amewapa Imani na mamlaka ya kuomba dhidi ya majanga kama hayo.

  “Good News for All kwa kushirikiana na madhehebu mbalimbali tumekuwa tukiendesha mikutano ya kuiombea nchi dhidi ya ukame tangu mwaka 2006 ambapo ni zaidi ya miaka 11 sasa tunamshukuru na Mungu amekuwa akijibu maombi yetu,” alisema Askofu Gadi.
  Mwenyekiti wa Kanisa la Good News For All Ministry Askofu Dkt. Charles Gadi (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akifanya maombi maalumu ya kuombe mvua mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu wa kanisa hilo Mchungaji Palemo Massawe na kushoto ni Mchungaji wa kanisa hili Andrew Thomas.
  Mwenyekiti wa Kanisa la Good News For All Ministry Askofu Dkt. Charles Gadi (wa pili toka kulia) pamoja na wachungaji wa kanisa hilo wakifanya maombi maalumu ya kuombe mvua mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kanisa la Good News For All Ministry Askofu Dkt. Charles Gadi wakati akifanya maombi maalumu ya kuombe mvua mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.


  0 0

  WAKAZI  wa Mtaa wa Sinza uliopo katika Mhakama ya Mazese walalamikia  kero wanayoipata kutokana na miundombinu mibovu ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) yanayosababisha maji kutapakaa barabarani hususani katika mtaa huo ambao ndani yake ipo Mahakama ya Mazese Mpaka njiapanda ya kuelekea Ukumbi wa Mirado jijini Dar es Salaam.

  Malalamiko hayo yametolewa na Wakazi wa Maeneo hayo ambao hawakutaka kujulikana wakati Akizungumza na mwandishi wa Michuzi Blog jijini Dar es Saalam leo. 

  Pia amewaomba watendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Maji  taka(DAWASCO) watembelee katika eneo hilo ili waweze kufanya marekebisho ya bomba hilo kwani maji mengi sana yanapotea katika eneo hilo ambapo yakikanyagwa na magari yanakuwa machafu sana yanayoleta kinyaa pamoja na usumbufu kwa wapita njia.

  "Tunawaomba watendaji wa DAWASCO watembelee eno hiyo ili waweze kufanya marekebisho ya bomba linalotiririsha maji mengi sana yanayofika mpaka barabara ya Shekilango-Sinza."

  Pia amesema kuwa  "nikiasi gani cha maji yanayopotea katika eneo hilo kwani yanaharibu hata barabara za mitaa mtaa wetu kama vile kunamvua  hadi tunaonekana wakazi wa mtaa huu waa Sinza ni wachafu kupindukia"

  Pia amewaasa wafanyakazi wa DAWASCO watembelee maeneo mbalimbali ili kujionea upotevu wa maji ambayo ni mhimu kwa matumizi ya binadamu pamoja na wanyama.
   Mwonekano wa Maji ambayo yamefanya Matope Mbele ya Geti la Mahakama ya Mazese liyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
   Maji yaliyotuwama kandokando ya ukuta wa Mahakama ya Mazese jijin Dar es Salaam.
  Maji yametuama karibu kabisa na Geti la mkazi wa maeneo hayo yanayosababisha mkazi huyo kutoweza kutokea geti hilo.
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  0 0  Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd imezindua Mradi mkubwa wa ufugaji kuku unaosimamiwa na Kikundi cha Ujasiriamali cha Shinyanga,Kishapu na Kahama (SHIKIKA) uliopo katika mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga.

  Uzinduzi wa mradi huo umefanyika leo Jumatatu Septemba 18,2017 katika mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha manispaa ya Shinyanga.Kikundi cha SHIKIKA kinachotekeleza mradi huo,kilianzishwa Machi 16,2017 baada ya kampuni ya Namaingo Business Agency Co.Ltd kuwaelekeza wanachama wake kuunda vikundi vya wanachama hamsini hamsini ili wakubaliane kuendesha mradi wanaoupenda.

  Wanakikundi hao waliamua kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji ndipo kampuni hiyo ikawachangia vifaranga 200,wakaanza ufugaji tarehe 9.6.2017 na mpaka sasa kikundi kina kuku zaidi ya 1300.Akizungumza wakati wa kuzindua mradi huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim aliwapongeza wanakikundi hao kwa kuchangishana fedha shilingi milioni 8 na kuamua kuanzisha mradi huo.

  “Ndugu zangu jambo hili mlilofanya na mlilolitekeleza kwanza ni jambo la kitaifa kwa sababu wananchi wakiwa na uchumi mzuri serikali nayo inapata kodi lakini pia tunakuwa tumetengeneza ajira”,alisema Ibrahim.

  “Pamoja na jitihada hizi mlizochukua kwa muda mfupi,Tunatamani kuona kila mtu anakuwa na kuku walau 1000 kwenye banda lake,najua changamoto kubwa iliyopo ni mitaji na riba kubwa kwenye mikopo lakini kuna fedha kwa ajili ya maendeleo ya akina mama na vijana zenye riba ndogo sana zipo kwenye benki mbalimbali,serikali inafanyia kazi suala la mikopo hiyo”,aliongeza.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akishikana mkono na Katibu wa SHIKIKA,Gelard Egwaga baada ya kukata utepe.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akiangalia kuku wenye umri wa miezi miwili katika moja ya mabanda ya kundi la SHIKIKA.

  Viongozi wa kundi la SHIKIKA wakimwongoza Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim kuangalia kuku hao.

  Ndani ya banda la kuku,mgeni rasmi Biubwa Ibrahi na waangalizi wa kuku (vijana watatu kulia).


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori pamoja na Diwani wa Kimara, Paschal Manota  wakizindua mradi wa usambazaji majisafi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), katika eneo la Kilungule B. Zaidi ya wakazi 5000 wanatarajia kunufaika na mradi huo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori pamoja na Diwani wa Kimara, Paschal Manota wakifurahia.
  Majiiiiiiiiiiiiiiiiii hayo...
  Akina mama wakifurahi maji.


  0 0

  UONGOZI wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), leo umefanya ziara Wizara ya Fedha na Mipango na kufanya mazungumzo na Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Philip Mpango, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  Ujumbe huo wa Shirika la Posta uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Kanal Mstaafu Dkt. Harun Kondo, akiwa na Kaimu Postamasta Mkuu Bw. Deogratius Kwiyukwa,Kaimu Meneja Mkuu wa Rasilimali za shirika, Bw. Macrice Mbodo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bw. Elia Madulesi.

  Katika mazungumzo hayo, ujumbe kutoka Shirika la Posta ulimweleza Waziri hali halisi ya Shirika, zikiwemo changamoto , mafanikio na maendeleo ambayo shirika limeyapata tangu lilipoanzishwa mwaka 1994 baada ya kutenganishwa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Benki ya Posta ambao kwa sasa ni taasisi zinazojitegemea kama ilivyo Shirika la Posta.

  Mwenyekiti alieleza juu ya hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Shirika katika kulifanyia mabadiliko makubwa ya kimuundo na kiutendaji ili liweze kukabiliana na changomoto za ushindani wa huduma na biashara kwa jumla.Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Harun Kondo, alimwomba Waziri Mpango, alisaidie Shirika katika kutatua changamoto mbali mbali.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali mstaafu, Dkt. Harun Kondo (kushoto), akimweleza jambo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati Uongozi wa shirika hilo, ulipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Bw. Deo Kwiyukwa na kulia ni Mkurgenzi wa Sera wa wizara hiyo, Bw. Mgonya Benedicto.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali mstaafu, Dkt. Harun Kondo (kushoto), akimweleza jambo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati Uongozi wa shirika hilo, ulipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Bw. Deo Kwiyukwa.

  Baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa makini, mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango na Uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mchumi Mkuu wa wizara, Dionisia Mjema.(Picha zote na Bw. Elia Madulesi).

  Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Posta wakiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango(wa pili kushoto) baada ya ujumbe huo kumtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amekabidhi vifaa vya ujenzi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake alizotoa katika ziara yake ya siku tano iliyomalizika tarehe 15/09/2017.

  Katika makabidhiano hayo Mhe. Gambo amekabidhi jumla ya mifuko 700 ya saruji, nondo za ukubwa wa milimita 16 na 12 tani moja moja na bati 200 kwenda kukamilisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali.

  *“Katika ziara yangu nimekutana na wananchi wetu wamejitahidi kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo na Halmashauri ya Arusha Vijijini imefanya kazi kubwa, wakaniomba mimi kama Mkuu wa mkoa niweze kuchochea shughuli za maendeleo……na msaada huu utaenda kusaidia maeneo mbalimbali mfano ujenzi wa daraja Mateves na nyumba za walimu Oldonyosambu”* alisema Mhe. Gambo.
  Mkuu wa Mkoa amemaliza ziara zake za kikazi katika mkoa wa Arusha kwa kutembelea Halmashauri 7 na wilaya zote 6, ziara hizi zikiwa na lengo la kujitambulisha kwa wananchi na kusukuma shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

   RC Gambo akikabidhi mifuko ya saruji kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha Ndg Charles Mahera (katikati) aliyeambatana na Katibu Tawala wa wilaya ya Arumeru Ndg. Timoth Mzava
   Lori lililosheheni mifuko 700 ya saruji tayari kuelekea makao makuu ya Halmashauri yaArusha
   RC Gambo akikabidhi mabati kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha

  RC Gambo akikabidhi nondo tani mbili kwa wananchi wa wilaya ya Arumeru


  0 0


  Na Benedict Liwenga-WHUSM
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura amelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ufanisi wao wa kazi huku akiwataka kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya Awamu ya Tano ili kuleta maendeleo katika soka.
  Mhe. Wambura ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea ofisi za Shirikisho hilo ili kujua namna wanavyotekeleza majukumu yao ikiwemo changamoto za shirikisho pamoja na maendeleo ya soka nchini.
  Akiongea na Viongozi mbalimbali na wadau wa soka katika ziara yake hiyo, amesema kwamba anaridhishwa na kazi wanazofanya TFF na amewapongeza kwa kupata uongozi mpya wa Shirikiho hilo na kuwasisitizia kujenga mahusiano ya karibu na wadau wa soka ikiwemo kuwajengea uwezo vijana ili kukuza vipaji vyao na hatimaye kuleta heshima kwa Taifa.

  “TFF hongereni kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya, hakika mnajitahidi sana lakini niwaombeni muzidi kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kwamba tunapata maendeleo mazuri katika soka, hivyo ni vema mkawa mnajenga mawasiliano na Viongozi wa Serikali mara kwa mara ili na sisi tupate kujua mambo yanayofanyika”, alisema Mhe. Wambura.
  Sambamba na hilo, Naibu Waziri Wambura amesisitiza juu ya suala la ugawaji wa vifaa vya michezo ikiwemo mipira ya kuchezea katika maeneo mbalimbali nchini huku akisema kuwa, ugawaji huo uwe wa uwiano sawa ili pasitokee eneo moja likawa linakosa vifaa hivyo kwakuwa vijana wote ni Watanzania na wana haki sawa ya kushiriki katika michezo.
  Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Bw. Kidao Wilfred amesema kwamba, TFF imejitahidi kuwasaida vijana mbalimbali wakiwemo Serengeti Boys kwa kuwapatia vitendea kazi na amepokea ushauri wa Naibu Waziri wa kuendelea kujenga uhusiano wa karibu na Serikali ili kukuza soka nchini.
  “TFF tumekuwa tukiwaandaa vijana mbalimbali ili kuweza kuwapata wenye vipaji vizuri na tumepanga kuwa vijana hawa waweze kupatiwa shule ambapo watakuwa wanajifunza masuala mazima ya soka na nikieleze tu Mheshimiwakwamba ushauri wako wa kujenga ushirikiano na Serikali tumeupokea na tunaufanyia kazi”, alisema Wilfred.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akiongea na Vijana wa Serengeti Boys wanaochipukia wakati alipotembelea Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) 18 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura(aliyekaa katikati) pamoja na baadhi ya Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiwemo wengine toka Wizarani wakiwaangalia vijana wa Serengeti Boys wanaochipukia katika Viwanja vya Karume 18 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura(kushoto) akisalimiana na Kocha Kim Paulsen wakati alipotembelea ofisi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) 18 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam. 
  PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM


  0 0

  Kama ulipitwa na matukio ya wiki nzima yaliyojili mkoani Ruvuma na nje ya mkoa wa Ruvuma kuanzia Sep 11 hadi Sep 17, 2017 basi usipate tabu tumekusogezea , Matukio ni haya hapa kazi yako ni kubonyeza hii video uweze kuyafahamu na kuyatazama.

older | 1 | .... | 1915 | 1916 | (Page 1917) | 1918 | 1919 | .... | 3272 | newer