Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1913 | 1914 | (Page 1915) | 1916 | 1917 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mbuzi wakipigana vibega wakati wakitimua mbio kutafuta mshindi wa shindano lililopewa jina la 'The Southen Sun Fillies Frolic' lililodhaminiwa na Hoteli ya Southen Sun, wakati wa mashindano ya mbio hizo za mbuzi kwa mwaka 2017, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Farasi, jijini Dar es Salaam leo na kihudhuliwa na wadau mbalimbali. Mashindano haya ya mbio za mbuzi huadhimishwa kila mwaka hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kuchangisha fedha za kusaidia jamii mbalimbali zenye uhitaji.
  Mbuzi wakiendelea kutimua vumbi katika mchuano mkali.
  Mmoja wa Mbuzi akiwa kabebwa baada ya kushindwa mbio hizo na kugoma kutembea.
  Mbuzi Bingwa wa 'The Southen Sun Fillies Frolic' akipongezwa na wadau.
  Shangwe tupu baada ya kuibuka kidedea.

  0 0

  Tupokigwe Abnery Mwampondele amezaliwa,Seronera - Serengeti mkoani Mara.Alisomea shahada ya Isimu ya lugha ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). 

  Kwa sasa ni mwalimu wa somo la Kiswahili katika shule ya Sekondari ya Wasichana Precious blood iliyopo mkoani Arusha-Tanzania. 

  N’je na kazi ya uwalimu Tupokigwe Abnery ni mtunzi wa vitabu vya hadithi, mbunifu wa mavazi ya kiasili, mjasiriamali na mwandishi wa gazeti tando (blogger) inayoitwa Sinyati Blog.

  Tupokigwe Abnery alikuwa na kawaida ya kupenda kujibembeleza au kujifariji akiwa anatembea kwa kutengeneza hadithi katika fikra zake ili kuweza kulala au kufika anakoelekea bila kuchoka,ndipo siku moja baada ya kushiriki shindano la uandishi wa Riwaya fupi kwa wanafunzi wa shule ya msingi,sekondari na vyuo vikuu Tanzania kwa ajili ya Tuzo ya mama Salma Kikwete iliyoandaliwa na TASAKI(Tamasha la Sauti ya Kiswahili) aliibuka mshindi wa pili wa riwaya fupi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania.

  Hivyo hiki kitabu ni muendelezo wa Riwaya aliyopatia Tuzo.Soma kitabu hiki uweze kujionea ubunifu wa hali ya juu wa fani pamoja na mshikamano wa maudhui uliyopo ndani ya kitabu hiki. 

  Mapenzi Kaburini ni kitabu chenye mtazamo yakinifu,ni kitabu ambacho maudhui yake yamezitazama nchi za Afrika Mashariki na changamoto zilizopo katika nchi kwa upande wa viongozi pamoja na wananchi.Kimebeba maudhui yanayowalenga wananchi wote bila kujali utabaka.Kwa upande wa fani kimetumia majina ya halisi na kubuni hasa kwa upande wa maeneo ya miji mfano kuna miji kama Kinyonga,kupe,chatu ambayo ni majina yaliyopo katika nchi ya Simba.Nchi hii ya Simba ni nchi inayosimamia nchi zilizopo Afrika Mashariki.

  Mbali na hilo pia visa na matukio vimepewa majina ya hifadhi za Taifa zilizopo katika nchi ya Tanzania.Mfano hifadhi ya Ruaha,Sanane,Manyara na kitulo kama ukisoma kitabu hiki utagundua kuwa sifa ya hifadhi inaendana na visa na matukio yaliyopo katika sehemu hiyo iliyoandikwa kwa jina la hifadhi.Mfano hifadhi ya Kitulo inasifika kwa kuwa na maua,kama tujuavyo maua huashiria sifa nyingi moja wapo hapo ni upendo,watu wengi hutumia maua katika kuwapa wapenzi wao,mfano kuomba msamaha,kumfariji mtu,hata kuonesha upendo kwa mtu unayempenda.

  Utakaposoma kitabu hiki utaburudika na kufundishwa baadhi ya mambo kama Kukuza imani yako kwa Mungu,uaminifu katika ndoa,uzalendo katika nchi yako na Madhara ya kujihusisha katika mahusiano na mtu usiye mjua.
  Nitakupatia kionjo kidogo katika sura ya kwanza ili kuweza kuona mwanzo tu wa hadithi hii ambayo hutapenda kuacha kuifuatilia:  Nicheki kwa mawasiliano haya:+255756377940
  Instagram: @sinyatiblog
  Facebook:Tupokigwe Abnery 

  0 0

  Benki ya CRDB leo imekutana na wafanyabiashara wadogo na wa kati mkoani Mwanza na kuwahakikishia kwamba itaendelea kutoa huduma bora ikiwemo mikopo ili kukuza mitaji yao.

  Akisoma hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dkt.Charles Kimei, Mkurugenzi wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba huduma za mikopo zitatolewa kwa wakati wote katika benki hiyo kwa kuzingatia kanuni za kibenki nchini.

  Amesema benki hiyo imeendelea kutanua na kuboresha huduma zake ikiwemo uwepo wa Matawi 20, vituo vya kutolea huduma 50, ATM 135, mawakala wa Fahari huduma zaidi ya 649 katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

  Aidha amesema kwa mkoa wa Mwanza benki ya CRDB ina matawi manne, vituo vya huduma 13 pamoja na Mawakala wa Fahari Huduma zaidi ya 105 na hivyo kusaidia kuwafikia wateja wake kwa urahisi.

  Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo, Agapiti Malya pamoja na Doroth Baltazari wameipongeza benki hiyo kwa namna ilivyowawezesha kwa njia ya mikopo na kuinua biashara zao ambapo wameomba benki hiyo kuendelea kuboresha zaidi huduma zake ili kuwanufaisha wafanyabiashara wengi zaidi.
  Baadhi ya wafanyabiashara (wajasiriamali) wadogo na wa kati walioshiriki mkutano ulioandaliwa na benki ya CRDB mkoani Mwanza kwa ajili ya kujadili pamoja masuala mbalimbali ya kibenki ili kusaidia kuboresha huduma zinazotolewa na benki hiyo.

  Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Mkoani Mwanza, Wambura Calystus akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huu, hii leo Jijini Mwanza
  Mmoja wa watoa mada kutoka benki ya CRDB akiwasilisha mada kwenye mkutano huo
  Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada kwenye mkutano huo


  0 0
  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu yaJamii

  WAFANYAKAZI 17 wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa Nchini Uganda wamehitimu mafunzo ya kozi mbalimbali katika Chuo cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga  nchini (CATC).

  Akizungumza katika mahafali ya 270 ya Chuo hicho ,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA) , Hamza Johari amesema kuwa waliohitimu mafunzo katika chuo hicho wakatumie elimu ambayo italeta mabadiliko katika usafiri wa anga.

  Amesema chuo cha CATC kinatambulika na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) hivyo mafunzo yanayotolewa ni bora kutokana nakutambulika kwa nchi mbalimbali kuleta watalaamu wao kuja kujifunza masuala ya usafiri anga nchini Tanzania.

  Hamza amesema tofauti kinachofanya kwa watalaam hao kuwa wameiva ni kuonyesha mikakati yauekelezaji kwa kile walichojifunza katika maendeleo ya nchi yao pamoja na Afrika Mashariki katika utoaji wa huduma ya usafiri wa anga.

  Amesema mikakati iliyopo kwa chuo hicho ni kuingia ubia na Chuo cha Nchini Singapore kwa ajili ya kutoa mafunzo ya usafiri wa anga kwa nchi za Afrika hali ambayo itafanya Chuo kuongeza idadi ya wanafunzi wanakuja kusoma na kuifanya Tanzania kutambulika zaidi katika utoaji wamafunzo ya usafiri wa anga.

  Nae Mkuu wa Chuo CATC, Dk. Daniel Karenge amesema kuwa wahitimu waliohitimu chuo hicho tangu kilipoanzishwa mwaka 2000 niwahitimu 3056 katoka nchi mbalimbali zaAfrika .

  Amesema kuwa wanaopata mafunzo hayo kwa asilimia kubwa ni watu wa nje ya nchi hivyo amewasaa watanzania kutumia fursa ya kupata mafunzo ya usafiri wa anga katika chuo chao.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA) , Hamza Johari akizungum za katika mahafali 270 ya Chuo cha Usafiri wa Anga CATC yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA),jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Chuo cha Usafri wa Anga (CATC), Dk. Daniel Karenge akitoa taarifa ya Chuo hicho katika mahafali ya 270 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA), jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari akitoa cheti kwa Mhitimu wa Kozi ya Watoa Taarifa za Usafiri wa Anga, Stella Kabagenyi katika mahafali ya Mahafali ya 270 ya Chuo cha UsafiriwaAnga Tanzania(CATC) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA, Jijini , Dar es Salaam.
  Sehemu ya wahitimu wakionesha vyeti vyao katika mahafali ya 270 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA, Jijini , Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA) , Hamza Johari akiwa katika picha pamoja na wahitimu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) katika mahafali ya 270 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA, Jijini , Dar es Salaam.

   

  0 0

  Klabu ya Simba inawatangazia waandishi wote wa habari za michezo,kuwa kesho siku ya Jumatatu 18/9/2017 kutakuwa na mkutano.

  Mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi mdogo wa klabu kuanzia majira ya saa 6 mchana, pamoja na mengine yatakayozungumzwa hiyo kesho,mkutano huu ni muhimu sana kwako/kwenu kuhudhuria kwani kuna mengi ya umuhimu ya kuyatolea ufafanuzi na kuyaweka wazi kwa umma wa mashabiki na wanachama wetu kupikia kwako/kwenu.
  Tunasisitiza kuwahi,kwani mkutano huo utaanza katika muda uliotajwa hapo juu  na utazingatia muda.

  Mwisho Klabu inapenda kuwapa taarifa rasmi,kuwa kuanzia sasa kila siku ya Jumatatu tu tutakuwa na mkutano na nyinyi/wewe kuanzia majira ya saa 6 mchana kwenye ukumbi wa klabu,hivyo basi ni vyema mkaiongeza ratiba hii kwenye ratiba zenu za kazi za kila siku.

  Imetolewa na Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano
  Haji Sunday Manara.
  Simba Nguvu Moja..!!!

  0 0
 • 09/17/17--01:04: Zenj FM yapeta.
 •  Baada ya kuwasilishwa ripoti ya utafiti ya usikivu na kukubalika, ZENJ FM  kwa Pemba, Unguja, Handeni, Dar es Salaam na Bagamoyo na wafanyakazi wa BBC Media Action, ikapigwa picha ya pamoja.
  Waliosimama kutoka kushoto Mwita Mwaikenda,Ramadhani Tuwa, Alice Mbelwa na Winie Mayao.Walioketi Lebert Bunce,Dr.Muhammed Seif Khatib, Doreen Bangapi na Ramadhani Senda.

  0 0
 • 09/17/17--01:12: Article 9
 • Na Richard Mwaikenda,Lindi 
   JESHI la Polisi limeahidi kushirikiana na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), kuwakamata wanaowanyanyasa na kuwabaka Watoto wa Kike. 
   Kauli hiyo ilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Renata Mzinga katika hafla ya kuwaapisha wanafunzi wa kike 230 waliojiunga na TGGA mkoani Lindi jana. 
  " Hilo siyo ombi bali ni wajibu wa jeshi la Polisi kushirikiana na chama hicho pamoja na jamii kuhakikisha wale wote wanaowatendea vitendo vibaya watoto wa kike wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria. 
   "Msiombe msaada kwetu, bali sisi tunahitaji sana msaada mkubwa kutoka kwenu, kwani huku kwetu watoto wa kike wanakuja wakiwa wameharibikiwa, ushauri wenu kwao umesaidia sana," alisema Kamanda Mzinga
  Amewataka waendelee kutoa elimu hiyo kwenye Tarafa, Kata, Kijiji na vitongoji ili kumkoboa mtoto wa kike. Kamanda Mzinga, aliipongeza TGGA kwa kitendo cha kuwapatia mafunzo takribani wasichana 1200 ya jinsi ya kuepukana na vitendo vibaya vya kubakwa na kupewa mimba, magonja kama vile Ukimwi na ndoa za utotoni. 

   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Renata Mzinga (kushoto), akiwavisha beji miongoni mwa wanafunzi 230 waliojiunga na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi Mjini.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG. 
   Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Macha akiwavisha beji miongoni mwa wanafunzi 230 waliojiunga na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi Mjini. 
   Timu ya soka ya wanawake mkoani Lindi wakitambulishwa katika hafla hiyo. Nao wanatarajia kujiunga na Girl Guides
   Mkufunzi Mkuu kutoka TGGA Makao Makuu Dar es Salaam, Emmiliana Stanslaus akitambulishwa wakati wa hafla hiyo
   Girl Guides wapya wakila kiapo
   RPC Mzinga akihutubia wakati wa hafla hiyo.
  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Afisa maendeleo ya vijana Temeke, Anna Marrica amezindua mradi wa sauti ya vijana katika Halmashauri ya wilaya ya Temeke na kuwataka vijana hao kutokata tamaa katika kutafuta maendeleo ili kujikwamua kiuchumi.

  Marrica amesema hayo katika uzinduzi wa mradi uliofanyika kwenye ukumbi wa manisapaa ya Temeke, lengo likiwa ni kutaka kuwapa moyo na kuwapongeza vijana hao kwa hatua nzuri waliofikia katika kuhakikisha wanaleta maendeleo ambapo mradi huo umelenga kuanzia ngazi ya kata ambazo ni Buza, Makangarawe, Kilakala pamoja na Tandika.

  Nae Mwenyekiti Mtendaji MYIDC, Ismae Mnikite amesema kuwa lengo pia ni kutaka kuishawishi Halmashauri ya Manispaa hiyo kufanya mchakato wa kutoa taratibu huru za wazi zinazofaa kuwaingiza vijana katika mfumo rasmi wa kutoa maamuzi ikiwemo kushirikisha hatua mbalimbali za uundwaji wa baraza la vijana kunzisha nganzi ya kata na hata hadi kiwilaya kwa mujibu wa tamko la sera ya Taifa ya maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007.

  Vile vile Mratibu wa mradi MYIDC, Kissango Mario ametanabaisha kuwa upo umuhimu wa vijana kujengewa uwezo wa kuhamasishwa, utetezi na ushiriki katika maamuzi pamoja na kuandaliwa kimaadili.

  Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi msaidizi mafunzo na maendeleo ya ujuzi kutoka ofisi ya Waziri mkuu kazi vijana ajira na wenye ulemavu, Julius Tweneshe amesema kuwa Serikali inathamini na kutambua mchango wa vijana hasa katika swala la kimaendeleo na ametoa ame toa wito kwa vijana wachangamkie fursa mbalimbali zianazojitikeza.
  Afisa maendeleo ya vijana Temeke, Anna Marrica akizungumza na vijana wa mradi wa sauti ya vijana MYIDC na kuwapongeza kwa hatua waliofikia na kuwataka wasikate tamaa katika swala la kutafuta maendeleo. Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam .
  Afisa Habari wa chama cha mbio za polepole Manispaa ya Temeke (Jogging) akiuliza swali kwa Mkurugenzi msaidizi mafunzo na maendeleo ya ujuzi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Julius Tweneshe.
  Vijana wa Mradi wa sauti ya vijana MYID wakisikiliza kwa makini mazungumzo ya viongozi wakati wauzinduzi wa mradi wa sauti ya vijana MYID uliofanyika katika harmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam.
  Picha ya pamoja wakiwa ni viongozi, vijana wa mradi wa sauti ya vijana MYID, wageni waalikwa pamoja na waandishi wa habari.


  0 0
  0 0

  Majaji nchini wameagizwa kumaliza kesi zote za muda mrefu Mahakamani ifikapo Disemba 15, mwaka huu ili kuendana na azma ya Mahakama ya kutoa haki  kwa wote na kwa wakati.
  Akizungumza katika Mkutano wa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali alisema kuwa Kanda zote za Mahakama Kuu nchini tayari zimeshaainisha idadi ya kesi zote za kuanzia miaka miwili kuendelea (kesi za mlundikano) ambazo zitafanyiwa kazi.

  “Nawaagiza Majaji wote nchini kuendelea na zoezi la kusikiliza kesi hususani kesi za muda mrefu Mahakamani, na zoezi hili lianze kufanyika Oktoba 16,mwaka huu na kazi hii nataka ikamilike kufikia Desemba 15,mwaka huu,” alisisitiza.

  Mhe.Jaji Kiongozi amezitaja Kanda za Mahakama Kuu ambazo zinaonekana kuelemewa na mzigo wa mashauri kuandaa orodha ya mashauri ‘causelist’wanayohitaji kusaidiwa.

  Mahakama hizo ni Mahakama Kuu-Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama Kuu-Kanda ya Mwanza, Mahakama Kuu-Kanda ya Bukoba, Mahakama Kuu-Kanda ya Mbeya, Mahakama Kuu-Kanda ya Shinyanga, Mahakama Kuu-Divisheni ya Ardhi na Mahakama Kuu-Divisheni ya Kazi.

  Aidha Mhe. Wambali ameagiza zoezi hilo lifanyike ndani ya wiki moja kuanzia Jumatatu, Septemba 18 ili kuwezesha kujua uhitaji wa msaada wa Majaji wengine kutoka Kanda nyingine watakaoenda kusaidia kusikiliza na kumaliza mashauri hayo katika maeneo tajwa.

  Aidha Mhe. Jaji Kiongozi amewataka Majaji Wafawidhi kuitisha vikao na Wadau wa Mahakama ili waweze kujua juu ya kuwepo kwa Programu maalum ya kusikiliza na kumaliza kesi zote za muda mrefu Mahakamani.

  Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahimu Hamis Juma amewataka Majaji na Watumishi wa Mahakama kwa ujumla kufanya kazi kwa kuzingatia nguzo tatu za Mpango Mkakati wa Mahakama ili kutekeleza majukumu kimkakati na hatimaye kupata matokeo chanya.

  “Majaji Wafawidhi ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa Mpango Mkakati hususani katika nguzo namba mbili ambayo ni Upatikanaji na utoaji wa Haki kwa wakati, kupitia Majaji na Mahakimu waliopo chini yao” alisema Mhe. Jaji Mkuu.

  Akiongelea juu ya jukumu kuu la utoaji haki nchini, Mhe. Jaji Mkuu amesisitiza juu ya kuwa na kumbukumbu sahihi ya takwimu za mashauri zilizopo katika Mahakama husika hali ambayo itawezesha kujua ni msaada utakaohitaji, bajeti na kadhalika.

  Kwa upande mwingine Mhe. Jaji Mkuu amesisitiza juu ya matumizi ya TEHAMA katika uendeshaji wa kesi ili kuendeana na kasi ya Teknolojia hali ambayo itawezesha huduma ya haki kuwafikia wananchi kwa wakati.

  Mambo mengine aliyoyasisitiza Mhe. Jaji Mkuu alipokuwa akifunga Mkutano wa Majaji Wafawidhi ni pamoja na ufanyaji kazi kwa ushirikiano kwa Watumishi wote wa Mahakama na kubadili mtazamo hasi ‘change of attitude’ na kuzingatia maadili katika utendaji kazi.

  Mkutano wa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, uliofanyika kwa siku mbili (2), Septemba 15&16 ni mwendelezo wa Vikao mbalimbali ambavyo vimekuwa vikifanyika mara kwa mara vyote vikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa azma ya Mahakama ya Tanzania ya kutoa haki kwa wakati inaonekana kutekelezeka.

   Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa neno alipokuwa akifunga Mkutano wa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa-AICC jijini Arusha, Septemba, 15 na 16, 2017. 
   Sehemu ya Waheshimiwa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu nchini wakimsikiliza kwa makini Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani) 
  Waheshimiwa Majaji Wafawidhi pamoja na Wasajili wakiwa katika Mkutano huo uliokamilika Septemba 16, 2017
   Waheshimiwa Majaji Wafawidhi pamoja na Wasajili wakiwa katika Mkutano huo uliokamilika Septemba 16, 2017
   Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania,Mhe. Hussein Kattanga akitoa neno, akisisitiza juu ya ufanyaji kazi kwa malengo.

   Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akiongea katika Mkutano wa Majaji Wafawidhi
   Mkuu wa Kitengo cha Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama,Mhe.Zahra Maruma akitoa mara ya utekelezaji wa kazi mbalimbali za Mradi mbele ya Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
  Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania mara baada ya kuhitimisha kikao cha siku mbili cha kujadili juu ya mikakati ya kuondosha mashauri ya muda mrefu Mahakamani. aliyeketi katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kushoto ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali, wa kwanza kushotoni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Iringa pia ni Jaji namba moja wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wa pili kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi,Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi na wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga.Picha na Habari na Mary Gwera wa Mahakama


  0 0

  Shirika lisilokuwa la kiserikali la Empower Society Transform Lives (ESTL) la Mkoani Singida limesema kwamba ukeketaji wa wanawake na watoto ni tatizo kubwa Afrika,Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi 28 zinazotajwa kuendeleza mila hiyo mbaya.

  Hayo yalisemwa na Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Mkoani Singida,Joshua Ntandu kwenye risala aliyosoma wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutokomeza ukeketaji katika vijiji 14 vilivyopo katika kata za Itaja,Mgori,Ntonge na Ughandi,uliofadhiliwa na The Foundation For Civil Society na kufanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Singida.

  Aidha Ntandu alifafanua kwamba inakadiriwa kuwa Tanzania ina zaidi ya wanawake milioni 7.9 waliogundulika kuwa wamekeketwa huku Mkoa wa Singida ukishika nafasi tano za juu za mikoa inayoongoza kwa ukeketaji hapa nchini.

  Alisema tafiti zinaonyesha pia kwamba vitendo hivyo vinaendelea kuongezeka katika Mkoa wa Singida na sababu kubwa zinazotajwa ni pamoja na imani kwamba ukeketaji ni sehemu ya makuzi ya mtoto wa kike na kwamba humzuia mtoto wa kike asiingie katika mahusiano ya mapenzi kabla ya kuolewa.
  Mwenyekiti wa Bodi ya ESTL,Bi Rose Mjema akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo ya kupinga vitendo vya ukeketaji huku akitoa tahadhari juu ya madhara yatokanayo na vitendo hivyo vya ukeketaji.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).
  Baadhi ya Mangariba na wakunga wa jadi kutoka katika Tarafa ya Mgori, wilayani Singida ambao wameamua kuachana na shughuli za kukeketa baada ya kupatiwa elimu na Shirika lisilokuwa la kiserikali la ESTL la Mkoani Singida,wakitoa ushuhuda kwenye uzinduzi wa mradi wa kutokomeza ukeketaji kwa wanawake katika Mkoa wa Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Singida.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Kwaya ya St. Albans Cathedral ya Anglican jijini Dar es salaam ipo mjini Lusaka, Zambia, ambako imeungana na wenzao  kutoka Pembroke College Choir ya Uingereza katika kusherehekea sikukuu ya Cathedral Holly Cross ya Lusaka na kushiriki kwa pamoja katika misa ya asubuhi leo
   Kwaya ya St. Albans Cathedral ya Anglican jijini Dar es salaam ikiimba katika kusherehekea sikukuu ya Cathedral Holly Cross ya Lusaka na kushiriki kwa pamoja katika misa ya asubuhi leo

  Kwaya ya Pembroke College Choir ya Uingereza ikiimba katika kusherehekea sikukuu ya Cathedral Holly Cross ya Lusaka na kushiriki kwa pamoja katika misa ya asubuhi leo
    Kwaya ya St. Albans Cathedral ya Anglican jijini Dar es salaam ikiimba katika kusherehekea sikukuu ya Cathedral Holly Cross ya Lusaka na kushiriki kwa pamoja katika misa ya asubuhi leo


  0 0

  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia mwenye makazi jijini Kuala Lumpur Mheshimiwa Dkt. Ramadhani Kitwana Dau amewasilisha Hati za Utambulisho  (Letters of Credence) kwa Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo katika sherehe zilizofanyika siku ya Jumanne ya tarehe 12 Septemba 2017 katika Ikulu ya Indonesia maarufu kama Istana Maderka.
  Kuwasilishwa kwa Hati hizo kunatoa ruksa wa Balozi Dkt. Dau sasa ya kufanya shughuli za uwakilishi nchini Indonesia kwa uhuru pasipo kuvunja taratibu za Kidiplomasia.

  Imetolewa na:
  Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
   Kuala Lumpur

   Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia mwenye makazi jijini Kuala Lumpur Mheshimiwa Dkt. Ramadhani Kitwana Dau akiwasili katika Ikulu ya Indonesia maarufu kama Istana Maderka tayari kuwasilisha Hati za Utambulisho  (Letters of Credence) kwa Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo
   Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia mwenye makazi jijini Kuala Lumpur Mheshimiwa Dkt. Ramadhani Kitwana Dau akiwasilisha Hati za Utambulisho  (Letters of Credence) kwa Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo
  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia mwenye makazi jijini Kuala Lumpur Mheshimiwa Dkt. Ramadhani Kitwana Dau akipeana mikono na  Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho  (Letters of Credence)
    
  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia mwenye makazi jijini Kuala Lumpur Mheshimiwa Dkt. Ramadhani Kitwana Dau akiongea  na  Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.

  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia mwenye makazi jijini Kuala Lumpur Mheshimiwa Dkt. Ramadhani Kitwana Dau akiagana  na  Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.

  0 0

  Serikali ya Brazil imesamehe Tanzania deni la jumla ya Dolaza Marekani milioni 203 ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania zaidi ya Bilioni 445. Deni hilo lilitokana na mkopo uliotolewa kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Morogoro-Dodoma mwaka 1979 pamoja Riba.

  Balozi wa Tanzania Nchini Brazil Dkt. Emmanuel Nchimbi alisaini mkataba huo kwa niaba ya Tanzania huku Wakili wa Hazina ya Taifa Dkt. Sonia Portella Nunes akisaini kwa niaba ya Serikali ya Brazil.

  Balozi Nchimbi alishukuru Serikali ya Brazil kwa Msamaha huo ambao alisema umeunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli kujenga uchumi imara wa Tanzania.

  Balozi Nchimbi pia aliihakikishia Serikali ya Brazil utayari wa Tanzania katika kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uchumi na Brazil.

  Kiongozi wa ujumbe wa Brazil kwenye sherehe hiyo Bw. Guilheme Laux, Undersecretary of Credit and Guarantee kutoka Wizara ya Fedha ya Brazil alimtamka rasmi kufunguliwa kwa milango ya ushirikiano wa kifedha na kibiashara iliyokuwa imefungwa kutokana na Deni hilo lililofanya Tanzania kuwa moja ya nchi zenye madeni sugu ya Brazil.

  Hivyo kutoka sasa Makampuni ya Brazil yanaruhusiwa kukopa katika Benki za Brazil kwa ajili ya kutekeleza miradi nchini Tanzania lakini pia Serikali ya Tanzania inaruhusiwa kuanzisha majadiliano ya miradi mipya ya maendeleo.
  Balozi Dkt. Emmanuel J. Nchimbi akisaini Mkataba kwa niaba ya Serikali ya Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania wa Msamaha wa Deni la Tanzania kwa Serikali ya Brazil .Kwa upande wa Brazil mkataba huo ulisainiwa na Dkt. Sonia Nunes, Wakili wa Serikali ya Brazil. 
  Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akibadilishana mkabataba huo na Dkt. Sonia Nunes, Wakili wa Serikali ya Brazil mara baada ya kusaini mkataba wa msamaha wa deni.
  BaloziDkt. Emmanuel Nchimbi akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo na Serikali ya Brazil. 
  Balozi Dkt. Emmanuel J.Nchimbi pamoja na Mkuu wa Ujumbe wa Serikali ya Brazil Bw.Guilheme Laux (kulia kwa Balozi Nchimbi) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapande zote mbili (Tanzania na Brazil)
  1. Balozi Dkt. Nchimbi akiendelea na mazungumzo na ujumbe wa Serikali ya Brazil (Hawapo pichani) .

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Viongozi wa Serikali wasiokuwa na mashamba ya mikorosho kutojihusisha na biashara ya uuzaji wa zao hilo.
   “Kama huna shamba, huwezi kuwa na korosho, unauza umepata wapi. Jukumu lenu ni kufuatilia, kukemea na kuchukua hatua stahiki penye udhaifu na si vinginevyo.”
   Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Septemba 17, 2017), wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa korosho uliofanyika mkoani Tanga.
  Amesema kama viongozi hao wanahitaji kuuza korosho watumie muda huu ambao Serikali inahamasisha watu wafungue mashamba mapya nao watumie fursa hiyo na kulima.
   Amesema ni vema kila mdau akahahakikisha anatimiza wajibu wake ipasavyo kama ni mkulima alime kwa kuzingatia stadi za kilimo na mnunuzi azingatie taratibu zilizopo.Waziri Mkuu amesema Bodi ya Korosho inatakiwa kuhakikisha inaimarisha zao hilo na kuishauri vizuri Serikali kuhusu namna bora ya kuliendeleza.
   Amesema Serikali inaamini kuwa iwapo kila mdau wa zao la korosho atatimiza wajibu wake kikamilifu katika kuliendeleza zao hilo kila upande utanufaika kikamilifu.Hivyo, ni vizuri kila mdau ajitathmini kama anatimiza wajibu wake kikamilifu, huku akiwaagizaviongozi wa Ushirika waendeshe Ushirika kwa uadilifu mkubwa.
   Waziri Mkuu amesema Serikali haitakuwa tayari kusikia mkulima yeyote akilalamika kuhusu malipo iwe kwa kupunjwa, kuchelewa ama kutolipwa. 
  Amesema katika msimu huu wa biashara ya korosho Serikali haitarajii kusikia mambo ambayo yalikwaza ufanisi katika misimu iliyopita kama wakulima kukatwa unyaufu kwa namna yoyote.
   “Sheria ya unyaufu ni miezi sita kutoka korosho inapoanza kuvunwa hadi kuuzwa na korosho haifiki miezi sita, hivyo wakulima hawahusiki unyaufu kwa namna yoyote ile na tusisikie tena.”Amesema hali hiyo ikitokea hawatasita kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika. “Nawaagiza viongozi wa ngazi zote kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa jambo hili.”
   Pia amepiga marufuku Bodi ya Maghala kutoza ushuru wa kuhifadhi mazao kwani hilo si jukumu lao bali ni la mpangaji wa ghala na wao washughulikie utoaji wa leseni tu.Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa maghala ya kuhifadhia korosho kutowazuia Viongozi wa Serikali kuyakagua kabla na wakati wa biashara.
   Amesema viongozi hao wanatakiwa wasizuiwe kuyakagua maghala hayo hata baada ya minada ili kujiridhisha na mwenendo sahihi wa uhifadhi wa mazao.Pia ameagiza kukamatwa na kutaifishwa kwa korosho zote zitakazonunuliwa kwa njia ya kangomba. Korosho zitaendelea kuuzwa kupitia mfumo wa stakabadhi gharani.
   Awali, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage amesema korosho ya Tanzania inaongoza kwa ubora duniani, hivyo wazalishaji wahakikisha sifa na ubora wa zao hilo katika soko la dunia haushuki.Amesema Serikali inaendelea kuwakaribisha wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika viwanda vya kubangulia korosho ili kuiongezea thamani kabla ya kuisafirisha nje ya nchi.
   Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Mwijage, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Bw. January Makamba.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Bi. Anna Abdallah, Wakurugenzi wa Bodi ya Korosho, Wakuu wa mikoa na wilaya zinayolima korosho, Wabunge wanaotoka katika mikoa inayolima korosho, wanunuzi, wasafirishaji na wenye viwanda vya ubanguaji.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  JUMAPILI, SEPTEMBA 17, 2017. 
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa wadau mahususi wa korosho katika hotel ya Tanga Beach mjini Tanga unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza 0ctober 01, 2017 ambapo mkutano huo ulihusisha wakuu wa mikoa inayolima zao la Korosho,wilaya na Halmashauri.
  Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Dkt Charles Tizeba akizungumza katika mkutano huo unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza Octoba 1 mwaka huu. 
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Hassani Jarufu akizungumza wakati wa mkutano huo unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza 0ctober 01, 2017 ambapo mkutano huo ulihusisha wakuu wa mikoa inayolima zao la Korosho,wilaya na Halmashauri .
  Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania,Mama Anna Abdallah akizungumza wakati wa mkutano huo unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza 0ctober 01, 2017 ambapo mkutano huo ulihusisha wakuu wa mikoa inayolima zao la Korosho,wilaya na Halmashauri .
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa katika akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo leo.Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.


  0 0

  We are devastated to inform our clients, partners and stakeholders of the death of our very own, Muganyizi Mutta, who was our Public Relations Director. 

  Mutta passed away on Saturday afternoon, September 16, 2017 at Mwananyamala Hospital in Dar es Salaam after a sudden illness. We have not only lost a member of Aggrey & Clifford family, but also a friend. Always in suits, Mutta was gregarious, charismatic and a hard worker with a big heart. Mutta joined Aggrey & Clifford, Tanzania in January 2016 until his sudden passing. 

  We will always remember and treasure the time that we have had the pleasure of knowing and working with him. May his soul rest in eternal peace.

  0 0

    Mandhari ya ukumbi wa Hekima Garden ulioko Mikocheni Industrial area jijini Dar es salaam wakati wa Send Off ya Dkt. Chrida Duncan Ndanshau Jumamosi usiku
    Bibi wa Bi Harusi Mtarajiwa akitoa wasia kwa mjukuu wake katika ukumbi wa Hekima Garden ulioko Mikocheni Industrial area jijini Dar es salaam wakati wa Send Off ya Dkt. Chrida Duncan Ndanshau Jumamosi usiku. Wazazi wa Dkt. Chrida wakisikiliza kwa makini.

   Bibi wa Bi Harusi Mtarajiwa akitoa wasia kwa mjukuu wake katika ukumbi wa Hekima Garden ulioko Mikocheni Industrial area jijini Dar es salaam wakati wa Send Off ya Dkt. Chrida Duncan Ndanshau Jumamosi usiku.

    Familia ya Bi. Harusi Mtarajiwa wakipata picha  katika ukumbi wa Hekima Garden ulioko Mikocheni Industrial area jijini Dar es salaam wakati wa Send Off ya Dkt. Chrida Duncan Ndanshau Jumamosi usiku.
   Wadau wa Familia ya Bi. Harusi Mtarajiwa wakipata picha  katika ukumbi wa Hekima Garden ulioko Mikocheni Industrial area jijini Dar es salaam wakati wa Send Off ya Dkt. Chrida Duncan Ndanshau Jumamosi usiku.

   Madada wa Bi. Harusi Mtarajiwa wakipata picha  katika ukumbi wa Hekima Garden ulioko Mikocheni Industrial area jijini Dar es salaam wakati wa Send Off ya Dkt. Chrida Duncan Ndanshau Jumamosi usiku.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Against the backdrop of one of Frances most iconic landmarks, right opposite the Arc du Triomphe, over 80,000 people - comprising adults, youths and community leaders gathered at the Place de la Concorde, for the annual Printemps Solidaire event. 
   This year's theme was enunciating the power of youths in France and the position of their voice in talking up the need for social changes that would provide for the underprivileged, the uneducated, while pressing for more government involvement in funding Girls Education globally. 
   By far the youngest on the stage was 15 year old Zuriel Oduwole, who electrified the crowd with her simple but profound analogy of why more needs to be done, for the needy around the world, especially in the area of Girls Education.

older | 1 | .... | 1913 | 1914 | (Page 1915) | 1916 | 1917 | .... | 3272 | newer