Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1912 | 1913 | (Page 1914) | 1915 | 1916 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda jana  ametembelea na kukagua Ukarabati wa Magari 26 ya Polisi yaliyopelekwa Mkoani Kilimanjaro yakiwa Mabovu kwaajili ya kukarabatiwa na kubadilishwa Mwonekano ambapo hadi sasa Magari 18 yapo hatua ya mwisho kukamilika.

  Magari hayo ambayo yalipelekwa Moshi yakiwa Chakavu kwa sasa baadhi yanatembea ambapo yamepakwa Rangi huku yakifungwa vifaa mbalimbali ikiwemo Magurudumu Mapya, Taa,Vioo,Bodi, Side Mirrow na vifaa vingine muhimu.

  Makonda amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na kusema kuwa atakabidhiwa Magari hayo mwanzoni mwa mwezi October ili ayakabidhi kwa Jeshi la Polis.Amesema Magari hayo yenye mwonekano kama yale ya UN yatakuwa na uwezo wa kubeba Askari Tisa nyuma wakiwa wamekaa ambapo Watatu watakuwa wakitazama Nyuma, Watatu Kushoto, Watatu Kulia na Mmoja Mbele wote wakiwa wamebeba silaha.

  Aidha Makonda amesema kupatikana kwa Magari hayo yatasaidia kupunguza vitendo vya Uhalifu kwa Wananchi.RC Makonda amesema kuwa lengo lake ni kuona hakuna Mwananchi yoyote anaeibiwa au kuporwa kitu.

  Hata hivyo amesema Baadhi ya Askari walikuwa wakipoteza maisha na kuporwa Silaha kutokana na aina ya Magari waliyokuwa wakitumia kutowapa uwezo wa kukabiliana na wahalifu hivyo Magari hayo yatamaliza matukio hayo.

  Ameishukuru kampuni ya RSA Limited kwa kumuunga mkono kwa kujitolea kukarabati Magari 56 ya Jeshi la Polisi kwa kuyafanya kuwa ya kisasa na Mapya.Sanjari na hayo amesema Magari hayo yataenda kufanya Doria kwa masaa 24.

  Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya RSA Bwana Manmohan Bhamra amesema kwa sasa Magari hayo ni sawa na Mapya kwakuwa yamewekwa vifaa vipya.
  Amesema Magari yote watayakabidhi kwa wakati iliyakaongeze tija katika kuimarisha Ulinzi na Usalama kwa Wananchi.
  Askari Pilisi wakiwa tayari kwa kazi katika moja ya magari 18 yaliyokamilika kwa ukarabati kati ya magari 26 yaliyopelekwa kwenye Gereji la RSA mjini Moshi na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda kwa matengenezo makubwa wakati alipoyakagua leo mkoani Kilimanjaro.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akikagua moja ya magari 18 kati ya 26 ya polisi Dar es salaam yaliyopelekwa mjini Moshi katika Gereji ya RSA kwa matengenezo makubwa Mkuu wa mkoa huya ameyakagua magari hayo na atakabidhiwa magari 18 ambayo yamekamilika.
  Baadhi ya magari ambayo tayari yamekamilika kwa matengenezo.

  0 0
  0 0

  Jopo la Majaji Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na Uliotukuka ya Daudi Mwangosi mwaka 2017 limeitangaza Clouds Media Group kuwa mshindi wa Tuzo hiyo kwa mwaka 2017. 
  Tuzo hiyo imetolewa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC wakati wa mkutano wake mkuu wa unaofanyika katika ukumbi wa Tanga Beach Resort mkoani Tanga. 
  Tuzo hiyo imekabidhiwa  kwa uongozi wa Clouds Media Group na Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation, Bw. Ernest Sungura. 
  Mbali na kupewa tuzo hiyo, pia Clouds fm imekabidhiwa hundi ya shilingi milioni 10 kama pole kwa changamoto waliyopitia baada ya kituo cha matangazo kuvamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda aliyekuwa ameambatana na askari polisi. 
  Mwenyekiti wa Jopo la Majaji Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na Uliotukuka ya Daudi Mwangosi mwaka 2017, Jenerali Ulimwengu alisema madhumuni ya Tuzo ya Mwangosi ni kumuenzi na kumkumbuka kwa kumpa mwanahabari au chombo cha habari tuzo yenye jina lake. 
  “Jopo la majaji mwaka huu tunaitangaza Clouds Fm kuwa mshindi wa tuzo ya Daudi Mwangosi mwaka 2017 kwa sababu tarehe 17 Machi,2017 wanahabari wa Clouds walivamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akiwa na askari polisi akiwataka kutangaza habari ambayo hawakuitaka lakini wafanyakazi hao wakakataa kutangaza habari hiyo. Huu ni ushujaa kwani hawakukubali kutii amri ambazo zilikuwa kinyume na kazi waliyofundishwa na uandishi wa habari”,alisema Ulimwengu. 
  “Lengo la tuzo hii iliyoanzishwa mwaka 2013 na UTPC ni kupinga vitendo viovu wanavyofanyiwa waandishi wa habari , hutolewa kwa mwandishi wa habari anayefanya kazi nchini aliyekutana na madhila katika utendaji kazi wake ama chombo cha habari ambacho kimekutana na madhila”,alieleza Ulimwengu. 
  Aliongeza kuwa tuzo hiyo inalenga kuwafanya wadau wa habari ikiwemo serikali kutambua kazi ya waandishi wa habari. 
  “Daudi Mwangosi alikuwa mwenyekiti Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa. Aliuawa Tarehe 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo mkoani humo, akitekeleza majukumu yake. Ni mwandishi wa habari wa kwanza nchini Tanzania kuuawa akiwa kazini, Kifo chake kilishtua na kusikitisha watu wengi duniani”, alieleza.

  Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation Bw. Ernest Sungura akikabidhi  Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na Uliotukuka ya Daudi Mwangosi mwaka 2017 kwa  Afisa Mahusiano wa Clouds Media Group Simalenga Simon leo Jumamosi Septemba 16, 2017 mkoani Tanga
  Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,Ernest Sungura akikabidhi tuzo Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na Ulitukuka ya Daudi Mwangosi mwaka 2017 kwa  Afisa Mahusiano wa  Clouds Media Group Simalenga Simon
  Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,Ernest Sungura cheti cha ushindi kwa  Afisa Mahusiano wa Clouds Media Group Simalenga Simon

  Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,Ernest Sungura akikabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kwa  Afisa Mahusiano wa Clouds Media Group Simalenga Simon. 
  Habari/Picha na Oscar Assenga na Kadama Malunde

  0 0


  0 0

  Shindano la “Mwagika Challenge” lililoendeshwa na kampuni ya bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager hivi karibuni limefikia tamati ambapo Iddi Kidungwa, Michael Mwalembe na Nasma Msangi wakiibuka washindi. 
  Washindi hao wanatarajiwa kuonekana kwenya video mpya ya msanii mkubwa wa bongo Fleva, G-Nako Warawara ‘Mwagika Challenge’ iliyokuwa na lengo la kuwapa fursa vijana kuonesha vipaji vyao pia liliungwa mkono na mastaa kama Shettah na Shilole waliokuwa mstari wa mbele kuhimiza mashabiki kushiriki shindano hilo pia ni miongoni mwa wasanii watakaonekana kwenye video hiyo. 
   Video hiyo inayotarajiwa kutoka 17.09.2017 itakuwa ya aina yake kutokana na vionjo mbalimbali vilivyotumika. Sitaki kukuchosha na stori nyingi, tizama teaser hapa chini na endelea kufuatilia mitandao ya kijamii ya Kilimanjaro kuona safari ya Mwagika challenge hadi kutengeneza video hii.

  0 0

  KAMPENI ya Uzalendo Kwanza iliyoanzishwa na Wasanii wa Filamu nchini, a.k.a Bongo Muvi inazidi kupanua wigo wake baada ya kuongeza matawi yake kwa mikoa yote ya Tanzania huku ikipata wanachama wakongwe waliowahi kutamba ndani ya Soka hapa nchini. 

  Akizungumza na wanahabari wakati akiwapokea wanachama wapya, Mwenyekiti wa Chama hicho, Steve Mengele 'Steve Nyerere' amesema kuwa, lengo la Chama hicho ni kuwafikia Watanzania wote kufahamu umhimu wa uzalendo, kuipenda nchi yako ikiwa ni pamoja na kushirikiana kikamilifu na Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kumuunga mkono wa kizalendo katika kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kimaendeleo. 

  "Taifa la wazalendo linaanzia darasani, tunawaomba walimu wote wawe wazalendo kufundisha darasani, manesi na madakatari wawe wazalendo kutoa huduma zao, uzalendo pia ni mhimu kusapoti vilabu vyetu vya soka na Timu ya Taifa,na Wasanii wetu wa muziki ni lazima wawe wazalendo kwa kuitangaza nchi yao kwa mambo ya Kizalendo," alisema Nyerere. 

  Wacheza soka ambao wamejiunga na Uzalendo Kwanza ni; Mwanamtwa Kihwelo, Monja Liseki, Abdallah Kaburu, Dotto Mokili na wengine.Aidha Nyerere amewaasa wanachama hao na Watanzania wote kuunganisha nguvu ya pamoja ili kulinda kazi zao za sanaa sambamba na kuwafanya Watanzania kupenda vilvivyo vyao mfano, kazi za wasanii wa ndani ili kukuza kipato chao na kuinua uchumi wa nchi. 

  Mbali na hao, msanii wa Bongo Fleva, atambulikae kwa jina la Ruby pia amejiunga na kampen ya Uzalendo Kwanza,Msanii huyo amepewa jukumu la kutunga nyimbo za Uzalendo na video zake ili kufikisha ujumbe kwa wananchi wote.

  Katika hatua nyingine,Uongozi wa Uzalendo kwanza umetoa msaada wa vyakula mbalimbali na kiasi cha fedha tasilimu Laki tano kwa aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News),Athuman Hamis ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majuku yake ya Kazi ikiwa yapata miaka kumi sasa tangu kutokea kwa tukio hilo.

  Steve Nyerere amemaliza kwa kuwaasa Wasanii wenzake kuendelea kuwa Wazalendo na kuwakumbusha kujiunga katika mifuko ya hifadhi ya kijamii,amesema kuwa mfuko wa hifadhi ya Jamii PPF wameanza kwa kuidhamini kampeni yao ya Uzalendo Kwanza,huku wakionesha utayari mkubwa wa kuwasaidia iwapo wataamua kuendelea kujiunga katika mfuko huo na ukawa mkombozi kwao.
  Mmoja wa Mabalozi wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza akiwasili kwenye mkutano,Athuman Hamis aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News), ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majuku yake ya Kazi ikiwa yapata miaka kumi sasa tangu kutokea kwa tukio hilo.
  Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo kwanza Steve Mengele almaarufu kwa jina la Steve Nyerere akimkabidhi bahasha yenye kiasi cha fedha shilingi laki tano pamoja na msaada wa vyakula mbalimbali kwa aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News),Athuman Hamis ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majuku yake ya Kazi ikiwa yapata miaka kumi sasa tangu kutokea kwa tukio hilo.
  Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo kwanza Steve Mengele almaarufu kwa jina la Steve Nyerere akimnyanyua Mzee Rajab Shabani mkazi wa Mburahati ambaye ni mlemavu wa miguu (kwa miaka mitano sasa),kumkalisha kwenye kiti cha matairi matatu (Wheel chair),ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na Wadau wa kampeni hiyo wakishirikiana na uongozi wa kampeni ya Uzalendo kwanza. 
  Pichani kati ni Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo Kwanza , Steve Mengele 'Steve Nyerere' akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini dar,wakati akiwapokea wanachama wapya walioamua kujinga na kampeni hiyo.Pichani kulia ni Mjumbe Halima Yahya na kushoto ni Misayo Ndumbagwe. 
  Pichani kati (njano) Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo Kwanza , Steve Mengele 'Steve Nyerere' akiwatambulisha wanamichezo wazalendo wa zamani katika Soka na Waigizaji wengie mahiri mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini dar,walioamua kujiunga na kampeni hiyo ya Uzalendo Kwanza.
  Pichani Kati ni Msanii wa bongofleva Hellen Majeshi a.k.a Ruby ambaye pia ametangazwa kujiunga na kampeni hiyo ya Uzalendo Kwanza. 

  Baadhi ya Wasanii mbalimbali wa Bongo movie wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo na Waandishi wa Habari uliofanyika mapema leo,jijini Dar.

  0 0


  0 0

  Diwani wa Kata ya Matuli Halmashauri ya Morogoro Vijijini, Tafarani Ngerengere akizungumza na wananchi katika shule ya Sekondari iliyopo kwenye Kata ya Matuli. Shule hiyo ya sekondari licha ya kuwa na madarasa mawili, ofisi ya walimu na matundu manne ya vyoo yaliyokamilika lakini bado haijapata usajili na kuanza kupokea wanafunzi, hali ambayo inalalamikiwa na Diwani huyo na wananchi wa kata hiyo.
  Mwananchi wa Kijiji cha Matuli kata ya Matuli akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kata ulioitishwa kujadili hatma ya sekondari yao ya kata ya Matuli.
  Wananchi wa Kata ya Matuli wakimsikiliza Diwani wa Kata hiyo, Lukas Lemomo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Matuli kata ya Matuli Halmashauri ya Morogoro Viijini.
  Majengo ya Shule ya sekondari ya kata ya matuli yaliyokamilika ambayo wananchi wanadai bado shule hiyo haIjapata kibali cha kufunguliwa.

  0 0

   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na Watumishi wa Bunge kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma. kulia ni katibu wa Bunge, Dkt. Thomas kashililah, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge, Mhe. Magdalena Sakaya (wa pili kulia) na kushoto ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge, Mhe. Mary Chatanda
   Watumishi wa Ofisi ya Bunge wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (hayupo kwenye picha) wakati wa kikao cha pamoja cha Watumishi wa Bunge na Tume ya Utumishi wa Bunge kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na Watumishi wa Bunge kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma. PICHA NA OFISI YA BUNGE

  0 0

  Ilikuwa ni siku ya furaha mno kwa wananchi wa jamii ya wafugaji kitongoji cha Endevesi, kata ya Njoro, Wilayani Same. Ambapo Septemba 12, 2017 wakati Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule akipokea majengo ya Shule ya msingi kwa niaba ya serikali. Pamoja Na mradi wa Maji kwa ajili ya wananchi hao wasiopungua 6,000. Shule hiyo yenye madarasa 6, ofisi za walimu, vyoo Na nyumbani za walimu. Imejengwa kwa ushirikiano wa masista wa Grail, Joy of faith Na Korea Hope Foundation. 
   
  Jamii hii ya Endevesi walikuwa wakipata Huduma hizi umbali wa km. Zaidi ya 5 Na kupelekea watoto wengi kuwa watoro. "Shule tumejengewa, serikali tutahakikisha tunapanga walimu Na shule hii inaanza 2018. Wananchi wakikishe wanaleta watoto shuleni. Nasi tutawachukulia hatua wote watakaokuwa watoro." Aliwashukuru pia kwa kuunga mkono juhudi za Mh. Rais wa Tanzania katika kuhimiza elimu. Miradi hiyo imegharimu zaidi ya Tshs. 800M.
  Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule akiongea mara baada ya kupokea majengo yaliyojengwa kwa ushirikiano wa masista wa Grail, Joy of faith na Korea Hope Foundation.
  Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule akipanda mti wa 
   kumbukumbu.

    
   Mkuu wa wilaya na kiongozi wa Korea Hope Foundation wakinawa mikono katima bomba ambalo ni moja ya mradi waliokabidhiwa.


  0 0

  Afisa TEHAMA wa Taasisi ya NORDIC, Dickson Leonard akiongea na wanahabari kumtambulisha Hilary Daudi ‘Zembwela’ kuwa Balozi wa Nordic Foundation Tanzania Dar es Salaam Septemba 15 2017. Balozi Zembwela atafanya kampeni ijulikanayo kama ‘AfyaBando’. Kushoto ni Mtaalam Mwelekezi wa Afyabando-Nordic Foundation Tanzania, Dkt. Resipicius Salvatory. 


  Balozi Zembwela akionesha namba ya kampuni na kumbukumbu kwa ajili ya kushiriki bahati nasibu ya kucheza 'Afyabando' ili kupata kadi ya Bima ya afya kwa shilingi 500. Imeandaliwa na Robert Okanda Blogspot

  0 0


  0 0  0 0


  0 0

  Ndugu, jamaa, marafiki na wadau wa sanaa na haki za watoto Tanzania.

  Kamati ya Maandalizi ya Msiba inapenda kutoa Tangazo rasmi la shughuli ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa mpendwa wetu marehemu Sister Jean Pruitt itakayofanyika siku ya Jumatano tarehe 20/09/2017.

  Shughuli hii itafanyika katika Ukumbi wa Karimjee uliopo Posta, Mtaa wa Sokoine, mkabala jijini Dar es salaam. Wadau wote tunaombwa kuwasili mapema kwa ajili ya kutoa

  heshima zetu za mwisho na kuaga mwili saa 3:30 asubuhi siku hiyo.

  Baada ya hapo Mwili utasindikizwa kwenda kanisa la Mt. Joseph kwa ajili ya misa itakayoanza saa 9 Alasiri siku hiyo ya Jumatano.


  Tunawaomba tuzidi kumwombea mama yetu Sista Jean Pruitt apumzike kwa Amani. Raha ya milele umpe eh Bwana na mwanga wa milele umwangazie,
  apumzike kwa Amani - Amina

  Kamati ya Maandalizi ya Msiba  0 0

  The financial support for awareness and patients support can be sent through Bank Account Name: Tanzania Breast Cancer Foundation, Bank: CRDB Azikiwe Branch, Account No: 01J2029384901, Tanzania Shillings and Account No: 02J2029384900 USD  Account. 
  Swift Code: CORUTZTZ.TBCF 
  M Pesa number is +255 768895694

  0 0

  Wanafunzi mbalimbali wa shule za sekondari na za msingi kutoka mikoa ya Tanzania wakiwa katika fainali ya mshindano ya 'Genius Cup' ambayo yanafanyika katika shule ya Secondari ya Feza jijini Dar es Salaam leo. Mikoa ambayo imeshiriki ni Dar es Salaam,Tanga, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Mtwara, Pwani, Arusha na Zanzibar.
  Wanafunzi mbalimbali wa shule za sekondari na za msingi kutoka  mikoa ya Tanzania wakiwa katika fainali ya mshindano ya 'Genius Cup' ambayo yanafanyika katika shule ya Secondari ya Feza jijini Dar es Salaam leo.

  Wanafunzi mbalimbali wa shule za sekondari na za msingi kutoka  mikoa ya Tanzania wakiwa katika fainali ya mshindano ya 'Genius Cup' ambayo yanafanyika katika shule ya Secondari ya Feza jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Robert Okanda Blogspot

  0 0

  Violet Brown
  Emma Morano 

  Violet Brown aliyezaliwa tarehe 10 March 1900  na kufariki dunia  jana Ijumaa tarehe 15 September 2017 ni mwanamke wa Jamaica ambaye hadi mauti yanamkuta ndiye aliyethibitishwa kuwa mtu mwenye umri mkubwa kuliko watu wote duniani kufuatia kifo cha aliyekuwa anashika rekodi hi mwanamama wa Italia Emma Morano  aliyezaliwa tarehe 29 November 1899  na kufa tarehe 15 April 2017  akiwa na umri wa miaka 117 na siku 189.


  Mama Violet pamoja na Nabi Tajima (pichani kulia) wa Japan  (aliyezaliwa   tarehe 4 August 1900)   walikuwa watu wawili wa mwisho duniani waliojulikana kuwa walizaliwa katika karne ya 19. Hivyo rekodi hiyo ya uhai mrefu inashikiliwa sasa na Mama Tajima.


  Akiwa mmoja wa watoto wane wa mzee John Mosse, mchemsha sukari katika kiwanda kwenye shamba la  miwa, na mama Elizabeth Riley, Mama Violet aliolewa na Bw. Augustus Gaynor Brown na wakajaaliwa kupata jumla ya watoto sita, wane wao  wakiwa hai wakati wa kifo chake jana.


  Kwenye Mahojiano Mama Violet alisema yeye alikuwa na afya bora kuliko wanawe na hakuwa na maradhi yoyote. Alipoulizwa siri ya uhai wake mrefu alisema hakuna siri kwa kweli.

  “Haki ya nani tena ni kweli watu wakiniuliza nakula nini na kunywa nini, nawaambia nakula kila kitu isipokuwa kitomoto na kuku. Pia sinywi pombe na    y ale mambo Fulani (ganja) situmii…”alisema Mama Violet.


   parent.[15] Death Brown died on 15 September 2017 at a hospital in Montego Bay, Saint James Parish, of heart failure complicated by dehydration at the age of 117.[16]

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua miongozo ya Kitaifa ya Kusimamia Mafunzo ya Vitendo kwa  Wahitimu (Internship Guidelines) na Mafunzo ya Uanagenzi (Apprenticeship Guidelines) mahala pa kazi, leo (Jumamosi, Septemba 16) mjini Dodoma. 
  Amesema miongozo hiyo inalenga kuongeza ari kwa waajiri na wadau wengine kushiriki katika  kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi na stadi za kazi ili kuhakikisha wahitimu na wanagenzi wanapata stadi  za kazi na ujuzi stahiki wa kuajirika au kujiajiri. 
  Waziri Mkuu amesema miongozo hiyo ambayo inakwenda kuboresha mafunzo ya uanagenzi na kwa wahitimu itachochea ukuzaji wa viwanda na kupunguza ukosefu wa ajira kwa watanzania hususan vijana. 
  Amesema Serikali imekua ikipokea malalamiko kutoka kwa waajiri kwamba wahitimu wengi wa ngazi mbalimbali za mafunzo wanaingia katika soko la ajira wakiwa hawana ujuzi unaohitajika na hivyo waajiri kulazimika kutafuta wafanyakazi kutoka nje ya nchi.

  Amesema baada ya kupokea malalamiko hayo Serikali, Waajiri na Wafanyakazi na walikubaliana kuimarisha mfumo wa utoaji mafunzo yanayofanyika maeneo ya kazi ili kuhakikisha mafunzo yatolewayo maeneo ya kazi yana ubora unaohitajika. 
  “Kuimarisha uwezo wa nguvu kazi ya Taifa ni muhimu na njia bora ni kuboresha utoaji mafunzo kwa vitendo mahali pa kazi kwa kuweka miongozo bora itakayowaongoza wadau wote wakiwemo Serikali, Waajiri, Wafanyakazi na Vijana kutoa Mafunzo.” 
  Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Magufuli alipoanza kuweka malengo ya ujenzi wa viwanda, mbali na kuwezesha kukua kwa kilimo na kuongeza thamani mazao, pia alilenga kupanua wigo wa ajira za viwandani ambapo kiwanda kinaweza kuajiri watu zaidi ya 1000.

  Amesema miongozo hiyo itasaidia kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kuhakikisha Taifa linakuwa na nguvu kazi yenye weledi wa kutosheleza mahitaji ya soko la ajira na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. 
  Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama amesema miongozo hiyo inaweka mfumo madhubuti wa kuandaa, kutekeleza, kusimamia, kuratibu na kufuatilia mafunzo husika mahala pa kazi. 
  Pia miongozo hiyo inabainisha majukumu ya wadau muhimu wa mafunzo hayo ambayo ni pamoja na kuweka bayana utaratibu wa kugharamia mafunzo ikiwa ni pamoja na kushirikisha Serikali, waajiri na wazazi. 
  “Miongozo imebainisha majukumu ya wadau katika kutoa mafunzo ambao ni Serikali, waajiri, taasisi za mafunzo, taasisi za mitaala na wanagenzi na wahitimu. Pia imebainisha vigezo vya kuwapata washiriki wa mafunzo na muda wa mafunzo.” 
  Pia miongozo hiyo imebainisha mfumo wa kitaasisi wa kuratibu na kuhakikisha ubora wa mafunzo kwa kuunda kamati ya Utatu wa Taifa ya kuratibu, kufuatilia tathmini ya mafunzo chini ya usimamizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
    Baadhi ya washiriki wa uzinduzi  wa Miongozo ya Mafunzo Katika Maeneo ya Kazi uliofanywa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa LAPF mjini Dodoma leo.
    Baadhi ya washiriki wa uzinduzi  wa Miongozo ya Mafunzo Katika Maeneo ya Kazi uliofanywa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa LAPF mjini Dodoma 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bibi Mary Kawar kitabu baada ya kuzindua Miongozo ya Mafunzo Katika Maeneo ya Kazi kwenye  ukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 16, 2017. Watatu kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na wapili kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na  Uwekezaji, Charles Mwijage. Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Mhandisi Stella Manyanya na kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua  Miongozo ya Mafunzo katika Maeneo ya Kazi kwenye ukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba   16, 2017. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Dunia wa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanbda na Burundi, Mary Kawar
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshiriki katika  Uzinduzi wa  Miongozo ya mafunzo Katika Maenneo ya Kazi alioufanya  kwenye ukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 16, 2017.(Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu)

  0 0


older | 1 | .... | 1912 | 1913 | (Page 1914) | 1915 | 1916 | .... | 3272 | newer