Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

Bunge lapitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali

$
0
0
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa mwaka 2017.

Akiwasilisha Bungeni Muswada huo leo Mjini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa lengo la marekebisho yaliyopendekezwa ni kuboresha utekelezaji wa Sheria hizo kwa kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kutumia sheria hizo na kuongeza masharti mengine ili kuleta uwiano kati ya Sheria zilizorekebishwa na sheria zilizopo.

"Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa mwaka 2017 unapendekeza kufanya marekebisho katika sheria 11 na kufuta sheria moja" amefafanua Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

Aidha, Masaju amesema kuwa masuala muhimu yaliyozingatiwa katika Muswada huo ni pamoja na kubadilisha vifungu vya Sheria kwa kufuta baadhi ya vifungu vya sheria hizo na kuviandika upya, kufuta baadhi ya maneno kwenye vifungu vya sheria, kuzingatia maneno mapya, kuongeza vifungu vipya na kufuta sheria moja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mohamed Mchengerwa amesema kuwa Kamati inashauri Serikali kuhakikisha Kamati maalumu ya kumshauri Waziri kuhusu misamaha ya kodi iundwe na wataalamu waliobobea kutoka katika fani na maeneo tofauti tofauti ili kujenga uwezo wa kamati hiyo katika kumshauri Waziri husika kuhusu misamaha hiyo ya kodi.

Nae Ally Saleh Ally kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Wizara ya Katiba na Sheria amesema kuwa kambi hiyo inashauri kuwa haitoshi kuifuta RUBADA pekee bali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu malalamiko ya wananchi wanaoituhumu kupora ardhi na hatua stahiki kwa wote waliohusika zichukuliwe.

Cuba yaipongeza Muhimbili kwa kutoa huduma bora

$
0
0
Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hernandez Polledo akizungumza na baadhi ya wakurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakati akiitembelea leo. Kushoto ni Mratibu wa madaktari wa Cuba nchini, Dk Maylen Lopez. Kutoka kushoto wa tatu ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Muhimbili, Makwaia Makani, Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk. Julieth Magandi, ofisa Idara ya ufundi, Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Hedwiga Swai, Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Lawrence Museru na Mkurugenzi wa Ufundi, Gaudence Aksante.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na Balozi wa Cuba nchini, Profesa Lucas Domingo Hernandez Polledo. Kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi, Gaudence Aksante.
Balozi wa Cuba nchini, Profesa Lucas Domingo Hernandez Polledo akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Museru leo kabla ya kutembelea maeneo ya kutoa huduma katika hospitali hiyo.
Balozi wa Cuba na baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo wakiwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).

TUME YA MUFTI YAKABITHI RIPOTI YAKE KWA WAZIRI LUKUVI

$
0
0
 Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akimkabidhi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi Ripoti ya Tume ya Mufti ofisini kwa Waziri.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi amekutana na Mufti Sheikh Abubakar Zubeir pamoja ujumbe wake wa Tume ya Mufti iliyoundwa kuhakikisha kwamba mali za waislam zinazomilikiwa na BAKWATA zinarejeshwa.

Waziri Lukuvi amepokea ripoti hiyo ikiwa ni kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli la kumtaka Waziri Ardhi afuatilie kwa makini maeneo yote ya waislam yanayomilikiwa na BAKWATA na yaliyomilikiswa watu kinyume cha utaratibu yanatafutiwa ufumbuzi.

Katika ujumbe huu Mufti ameongozana na Kaimu Katibu Mkuu wa BAKWATA Mwalimu Salim Abeid, Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Sheikh Ally Ngeruko, Makamu mwenyekiti wa Tume ya Mufti na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Sheikh Issa Othman Issa na Katibu wa Tume ya Mufti Alhaj Omary Igge.

Baada ya kukabithi ripoti hii Mufti Sheikh Abubakar Zubeir amemshukuru Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi kwa kupokea Ujumbe wake wa Tume ya Mufti na kumuomba achunguze na kuchambua kwa makini maeneo yote ya Bakwata yanayohusiana na migogoro ya ardhi.

Tume hii ya Mufti ya Kuhusu urejeshaji wa mali za waislam iliundwa na Mufti Sheikh Abubakar Zubeir mara baada ya kukukutana Mheshimiwa Rais na kumuomba awasaidie kuhakikisha kwamba mali za waislam zinazomilikiwa na BAKWATA zinarejeshwa BAKWATA.

Mara baada ya kupokea ripoti hii Waziri Lukuvi amemuahidi Mufti Sheikh Abubakar Zubeir kwamba atatekeleza agizo hilo la Mheshimiwa Rais na ataifanya kazi hii katika muda mfupi ujao na kusimamia kikamilifu kwa kufuata sheria.
 Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akimsisitiza kufuatilia kwa makini maeneo yote ya waislam yanayomilikiwa na BAKWATA na yaliyomilikishwa watu kinyume cha utaratibu yanatafutiwa ufumbuzi kama alivyoagiza Mheshimiwa Rais.
 Ujumbe wa Tume ya Mufti ukiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi ofisini kwake.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akimsikiliza Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir mara baada ya kupokea Ripoti ya Tume ya Mufti ofisini kwake, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa BAKWATA Mwalimu Salim Abeid na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Sheikh Ally Ngeruko.
 Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi baada ya kumkabidhi Ripoti ya Tume ya Mufti.

KESI YA MDEE UPELELEZI UMEKAMILIKA.

$
0
0
 Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu mara baada ya kusomewa Mashtaka yanayomkabiri Mahakama hiyo kusema kuwa upelezi wa Kesi yake umekamilika.
 Mbunge wa Jimbo la Kawe (CHADEMA), Halima Mdee akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bunda (CHADEMA), Ester Bulaya akimsindikiza Mbunge wa Kawe.  Mara baada ya Mhakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na imesema kuwa  upelelezi dhidi ya kesi hiyo umekamilika.
 Mbunge wa Jimbo la Kawe (CHADEMA), Halima Mdee akiwa na Mbunge wa Jimbo la Bunda (CHADEMA) wakiwa wamekaa katika Mhakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.


Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii. 

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya kutumia lugha chafu ya matusi inayomkabili, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (39) kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na aMaendeleo (Chadema) umeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo umekamilika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amesema hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Kishenyi amedai upelelezi katika kesi hiyo umekamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa huyo maelezo ya awali.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala akisaidiana na mawakili, Jeremiah Ntosebya na Hassan Kiangio, amedai kuwa waliiambia mahakama kuwa watawasilisha mapingamizi ya awali ikiwemo makosa ya kisheria kwenye hati ya mashitaka.

Amedai mapingamizi hayo sio ya kimaandishi bali waliiambia mahakama kwamba watawasilisha mapingamizi hayo, lakini kutokana kesi inavyoenda wameona bora waondoe mapingamizi hayo na kusikiliza kesi ya msingi.

Kibatala amedai watakapotaka kuwasilisha mapingamizi hayo watasema na kwamba kwa sasa wanaona faida ya kisheria ni kusikiliza kesi ya msingi.  

Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 11, mwaka kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Katika kesi ya msingi, Mdee anadaiwa kumtukana Rais Dk John Magufuli kwamba "anaongea hovyohovyo anatakiwa afunge break", kitendo ambacho  kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

JAMES KAJUGUSI:SERA MPYA YA VIJANA KUTATUA CHANGAMOTO ZA VIJANA

Serikali Kununua Mashine za DNA kwenye Maabara za Kanda

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

Serikali imedhamiria kununua mashine tatu za vipimo vya vinasaba (DNA) ili zitumike katika maabara za Kanda na hivyo kusogeza huduma karibu na wananchi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala wakati akijibu swali la Mbunge wa Chumbuni Mhe. Ussy Pondeza kuhusu ucheleweshwaji wa matokeo ya uchunguzi wa sampuli ikiwemo sampuli za makosa ya jinai.

Dkt Kigwangala amesema kuwa Serikali ina mkakati wa kuongeza mashine hizo ili kuwezesha uchunguzi kufanyika kwa wakati kwa vielelezo vya makosa ya jinai ikiwa ni pamoja na vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto.

" Sampuli za uhalali wa watoto kwa wazazi zinafanyika kwa wepesi zaidi kuliko sampuli za makosa ya jinai kwani sampuli hizo zinachukuliwa moja kwa moja toka kwa wahusika hivyo kurahisisha uchunguzi wake endapo wahusika wa uchukuaji watachukua kwa umahiri na uhifadhi utafanyika kwa namna stahili" amefafanua Dkt. Kigwangala.

Aidha, Dkt. Kigwangala amesema kuwa sampuli za uchunguzi wa makosa ya jinai zinachukuliwa toka maeneo ya matukio hivyo uchunguzi wake unaweza kuchukua muda zaidi kutegemeana na aina ya sampuli na eneo zilipotoka.

Vilevile Dkt. kigwangala aliongeza kuwa Serikali inampango wa kuanzisha kituo cha kupima vinasaba (DNA) Mkoani Mbeya kwa lengo la kupunguza ucheleweshaji wa matokeo ya uchunguzi.

Mbali na hayo akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Vijijini Mhe. Hawa Ghasia kuhusu Serikali kuagiza tohara kuwa lazima kwa wanaume nchini, Dkt. kigwangala amesema kuwa si rahisi kwa Serikali kuagiza tohara  kuwa lazima japo kuwa inafaida kiafya kwa wananchi.

" Tohara inasaidia kupunguza maambukizi ya Saratani ya shingo ya Uzazi kwa wanawake pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi" ameongeza Dkt. kigwangala.

Aidha, amesema kuwa elimu kuhusu tohara imefikishwa kwa wananchi kwa kiasi kikubwa ambapo Serikali kwa kushirikiana na wadau katika Mikoa ya kipaumbele  imekuwa ikitoa elimu kabla na baada ya huduma ya tohara katika vituo vya kutolea huduma za afya.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA NAMERA

$
0
0
Aahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi ambaye ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao.

Amekutana na Bw. Pardesi leo (Jumanne, Septemba 12, 2017)  kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam na amesema kwamba tayari Serikali imeanza kuwahamasiha wakulima kuongeza uzalishaji kwa kuwa kuna soko la uhakika.

Waziri Mkuu amempongeza Bw. Pardesi kwa kuiunga mkono Serikali katika mpango wake wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda. Kampuni ya Namera Group of Industries inamiliki kiwanda cha nguo cha NIDA na cha Namera vya jijini Dar es Salaam.Kampuni inatarajia kufungua kiwanda kingine cha nguo wilayani Kahama.

Pia Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha zao la pamba linapewa kipaumbe alikutana na wakuu wa mikoa yote inayolima pamba Ijumaa, Septemba 8, 2017 na aliwaagiza wasimamie zao hilo kwa karibu ili kuinua uzalishaji wake na kuwaongezea kipato wananchi hususan wakulima wa zao la pamba.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao. Waziri Mkuu amekutana naye leo Septemba 12/ 2017 Ofisini kwake Dar es Salaam

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi   ambaye ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao.(L) Ni Meneja wa Namera Bwana Muhammad Waseem. Waziri Mkuu amekutana nao leo Septemba 12/ 2017 Ofisini kwake Dar es salaam. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

MAREKEBISHO VIDEO-ERIC SHITINDI:SERA MPYA YA VIJANA KUTATUTA CHANGAMOTO ZA VIJANA


GREAT EAST AFRICAN DESIGN TALENTS EMERGE AS HEINEKEN(R) CONCLUDES MAIDEN AFRICA INSPIRED FASHION CHALLENGE.

$
0
0
General Manager Heineken East Africa Mr Uche Unigwe with the Africa Inspired Fashion Challenge 2017 Winners, Lulu Muturi and Azra Walji.
 Tanzanian fashion designer,stylist and fashion editor Rio Paul (centre) sharing a light moment with Njeri Mburu, Heineken’s Brand Manager – Kenya, Tanzania &Uganda.
Sights of colors,fashion and patterns from the Africa Inspired Fashion Design Cocktail in Nairobi,Kenya where the winners were announced. 

Lulu MUTULI & Azra WALJI impressed judges and earned a ticket to Africa’s largest fashion and design festival in Lagos
Lulu MUTULI and AZRA WALJI have reason to smile as they emerged tops at the maiden Heineken® Africa Inspired Fashion Challenge, a three day event built around creativity and innovation of East Africa’s finest fashion design talents.

 Speaking as he announced the winners, HEINEKEN East Africa General Manager Uche UNIGWE termed the three day design challenge as an amazing experience for the brand, designers and the regional fashion industry at large. Through our “open your world” Heineken® tagline noted Uche, we sought a co-creation opportunity for the regional fashion scene through an open-design challenge that saw over 100 portfolio reviews that were narrowed down to 10 participants from which the winners have emerged. 

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ngugai  akisisitiza jambo wakati wa Kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
 aziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akilieleza Bunge leo mjini Dodoma kuhusu mkakati wa Serikali kukamilisha ujenzi wa nyumba elfu kumi za makazi kwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  (JWTZ )  ambapo kati ya hizo zaidi ya elfu sita zimeshakamilika.
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid (wakwanza  kulia)  akifuatilia kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma wakati wa ziara yake .
 Mbunge wa Mtwara Vijijini Mhe . Hawa Ghasia akichangia hoja Bungeni leo mjini Dodoma kuhusu maboresho katika sekta ya Afya hasa suala la tohara kwa wanaume ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kupunguza  maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akisisitiza jambo mara baada ya kuwasilisha muswaada wa sheria ya marekebisho ya Sheria mbalimbali  namba 3 wa mwaka 2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia  Katiba na Sheria Mhe.  Mohamed Mchengerwa (Mb) akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo kuhusu  muswaada wa sheria ya marekebisho ya Sheria mbalimbali  namba 3 wa mwaka 2017 leo Bungeni mjini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu, Kazi,  Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi.
( Picha zote na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma ).

ZANZIBAR KUIMARISHA KANUNI ZA KUKATAZA MATUMIZI YA TUMBAKU KATIKA KULINDA AFYA ZA WANANCHI

$
0
0

Na Ramadhani Ali - Maelezo.

Wizara ya Afya Zanzibar inaendelea kuimarisha kanuni za kupunguza matumizi ya tumbaku baada ya kuundwa sheria ya Afya ya Jamii ya mwaka 2012 na kuridhia Azimio la Shirika la Afya ulimwenguni (WHO) kupiga vita bidhaa zinazotokana na tumbaku katika kunusuru afya za wananchi.

Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib amesema Wizara hiyo tayari imeweka kanuni ya kukataza kuvuta sigara kwenye mikusanyiko ya watu katika kuwanusuru waathirika wa moshi wa sigara bila ya kuwa wavutaji.

Dkt. Jamala ameeleza hayo alipokuwa akifungua warsha ya siku tatu ya kuimarisha kanuni za kupambana na matumizi ya tumbaku katika Hoteli ya Golden Tulip iliyopo Malindi iliyowashirikisha wadau kutoka taasisi mbali mbali za Serikali.

Mkurugenzi Mkuu alisema uvutaji wa sigara umeonekana kuwa chanzo kikubwa cha ongezeko la maradhi yasiyoambukiza ikiwemo saratani, sukari maradhi ya mapafu na maradhi ya ini.Alisema pamoja na kwamba Zanzibar haizalishi tumbaku na haina viwanda vinavyohusika na bidhaa za tumbaku bado wananchi wamekuwa waathirika wa moshi wa sigara.

Alieleza kuwa tafiti zilizofanyika zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu wanaofariki kutokana na maradhi hayo yanatokana na kuvuta sigara ambapo asilimia 15 ya vifo hivyo vinawafika watu wanaovutishwa moshi na wavutaji wa sigara bila ya wao kushiriki kuvuta.

Katika kufanikisha lengo  hilo Dkt. Jamala alizishauri taasisi za Serikali, Jumuiya za kiraia na jamii kwa jumla kuunga mkono kanuni inayokataza sigara kuvutwa kwenye mikusanyiko ya watu  na nyengine zinazoundwa ili kulinda afya zao.

Mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmay Andemichael alisema Zaidi ya watu milioni saba wanapoteza maisha kila mwaka duniani kutokana na matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku ambapo asilimia 80 ya vifo vinatokea katika mataifa yanayoendelea.

 Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dkt Ghirmay Andemichael akitoa maelezo ya Shirika hilo kwenye warsha ya siku tatu ya kuimarisha kanuni za kupambana na matumizi ya tumbaku inayofanyika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib akifungua warsha ya kuimarisha kanuni za mapambano ya matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
 Dkt. William Maina kutoka WHOAFRO akitoa maelezo ya Azimio la WHO na sheria za kimataifa dhidi ya mapambano ya matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku katika warsha ya kuimarisha kanuni za mapambano hayo katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi.
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya kumiarisha mikakati ya kanuni za kupiga vita matumizi ya tumbaku inayofanyika Hoteli ya GoldenTulip Malindi Mjini Zanzibar.

Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki wa warsha ya kuimarisha mikakati ya kupiga vita matumizi ya tumbaku inayofanyika Hoteli ya Goden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.

LORI LA MAFUTA LAGONGANA NA GARI NDOGO NA KUSABABISHA FOLENI KIMARA BUCHA, DAR USIKU HUU

$
0
0
 Lori lenye namba za usajili T483BHZ lililokuwa likisafirisha mafuta kuelekea nje ya nchi limepata ajali baada ya kuigonga gari ndogo aina ya Toyota IST yenye namba T727CVM eneo la Kimara Bucha jijini Dar es Salaam na kupelekea tela la Lori hilo kupinduka na kumwaga mafuta barabarani. Picha zote na Kajunason/MMG.
 Baadhi ya vijana wakichota mafuta yaliyokuwa yakimwagika kutoka katika tera lililodondoka.
 Muonekano wa gari lilivyokuwa limefunga njia na kusababisha foleni magari kupita barabara ya pembeni. 
Msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro.

UTT AMIS ILIVYOSHIRIKI MKUTANO WA WAHANDISI MKOANI DODOMA

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, akijiandikisha katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la UTT AMIS katika Mkutano wa Wahandisi uliofanyika Septemba 7-8 mjini Dodoma. Kulia ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa UTT-AMIS, Martha Mashiku. 
Ofisa wa UTT AMIS, Waziri Ramadhani, akitoa elimu kwa watu waliofika katika banda la UTT AMIS huku mwananchi mwingine aliyekaa akifungua akaunti wakati wa mkutano wa Wahandisi mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Masoko Mwandamizi wa UTT AMIS, Daud Mmbaga akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, alipotembelea banda hilo wakati wa Mkutano wa Wahandisi uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MKURUGENZI WA MAENDELEO YA JAMII AWAONGOZA WANANCHI WA KIJIJI CHA MONDO KUSHIRIKI KATIKA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA KATA YA MONDO, MISUNGWI.

$
0
0

Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW

Sera ya Maendeleo ya Jamii pamoja na mambo mengine, inaelekeza jamii kushiriki kazi za kujiletea maaendeleo yao wenyewe maana jamii ndiyo kitovu cha maendeleo.

Kwa kutambua hilo, Mkurugenzi wa Maendelo ya Jamii Bw. Patrich Golwike ametembelea katika Kijiji cha Mondo, Kata ya Mondo, kilichopo katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kuhamsha ari ya wananchi kushiriki katika ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya cha kijiji chao.Bw. Golwike alibainisha kuwa maendeleo ya mtu ni mtu mwenyewe na hakuna mtu kutoka nje ya eneo fulani ataleta maendeleo katika eneo husika.

“Sisi hatukuja hapa kijijini Mondo kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya Mondo, bali tumekuja kuhamsha ari ya wananchi wa kijiji hiki kuwa tayari kushiriki kazi za maendeleo yao kwa kutumia rasilimali zilizopo” alisema Bw. Golwike.

Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Mondo Bi. Aziza Omary alibainisha kuwa mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mondo uliibuliwa kwenye kikao cha Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mondo, ndipo iliporidhiwa kujenga kituo hicho ili kupunguza tatizo la vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua, na pia kuondokana na kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya za rufaa zikiwemo za wazazi na wagonjwa wengine.

Awali wananchi walishiriki kubaini changamoto, kupanga, kutekeleza na kusimamia mradi wa ujenzi kuhakikisha kuwa wananchi wanajitolea kuchangia nguvu kazi zao katika zoezi la ujenzi. 

Kazi nyingine zinazofanywa na wananchi ni kukusanya vifaa vya ujenzi kama vile mawe, kokoto, mchanga, mafundi, na utoaji uchangiaji wa rasilimali fedha.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mondo Bw. Philipo Suleiman ameipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuchagua kutembelea kijiji cha Monde mio ngoni mwa vijiji takribani 900 vilivyopo katika mkoa wa Mwanza.

Jengo la Kituo cha Afya cha Kata ya Mondo linakadiriwa kukamilika mwaka 2018 na litagharimu takribani shilingi 150,460,540/- fedha ambayo itatoka kwa wahisani na wananchi wenyewe.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akishiriki ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya katika Kijiji cha Mondo, kilichopo kata ya Mondo, Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza, mapema.
Mratibu wa Masuala ya Maendeleo ya Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI Bibi Mwajina Lipinga(kulia) aliyeshika chepeo) akishirikiana na wananchi kujenga jengo la Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mondo Wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza kutatua kero ya ukosefu wa huduma za afya katika kata ya Mondo kwa kutumia nguvu za wananchi wenyewe. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Atupele Mwambene(kushoto walioshika chepeo) akichanganya saruji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mondo, Kata ya Mondo kilichoko Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza katika kuhamsha ari ya kushiriki kazi za maendeleo kwa kutumia rasilimali zilizopo katika mazingira husika.
Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi, Misungwi Mhandisi Harold J. Mtyana akishiriki kujenga jengo la Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mondo, kata ya Mondo, wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akikabidhi mifuko 50 ya simenti kwa niaba ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mondo Bw. Marthias Lumwagila kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa Kituo hicho cha Afya. 
Sehemu ya jengo la kituo cha Afya cha Mondo, Kata ya Mondo,Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kama linavyoonekana na wananchi wakiendelea na kazi ya ujenzi. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW.


DC KILOLO AWATAKA WAZAZI KUWASOMESHA WATOTO WAO

$
0
0
Na Fredy Mgunda,Iringa

Wanachi wa kijiji cha mwatasi wamekuwa kikwazo cha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo ya shule ya msingi kutokana na wazazi kutowatimizia mahitaji muhimu watoto wao pindi waendepo shule.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika shule hiyo mwalimu mkuu wa shule ya msingi mwatasi Seth Mfikwa alisema kuwa wazazi wengi wa kijiji hicho wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.

“Hapa kijijini wazazi wengi hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa uhuru” alisema Mfikwa

Mfikwa alimuomba mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi wa kijiji cha Mwatasi ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa kijiji hicho.

“Ukiangalia hali ya ufaulu wa shule hii sio mzuri kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu lakini tunaendelea kuwaelimisha kidogo kidogo hivyo kwa kuwa mkuu leo umefika kwenye shule yetu tunaomba msaada wako wa kutoa elimu kwa wazazi ili kukuza elimu kwa wanafunzi wa kijiji hiki” alisema Mfikwa.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akiwa katika ziara ya kuzitembelea shule za msingi za kata ya Bomalang'ombe na kujionea jinsi gani shule hizo zinavyoongozwa na kuzitambua changamoto zinazowakabili walimu,wanafunzi,wanachi na viongozi wanaozizunguka shule hizo lengo likiwa ni kuboresha utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi wa wilaya ya kilolo.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Bomalang'ombe.

UTAFITI: KIWANGO CHA NIKOTINI KINACHOPATIKANA KWENYE ASALI HAKINA UWEZO WA KUDHURU MWILI WA BINADAMU

$
0
0
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetoa ripoti ya tafiti ya asali zilizokusanywa zenye chembechembe za nikotini kuwa zimefanyiwa majaribio na  zimedhihirisha kuwa chembechembe  hizo ni chache sana na hazina uwezo wa  kudhuru mwili wa binadamu.

Akizungumza na Vyombo vya habari, Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Glory Mziray amesema  TFS wamekuwa wakukisanya sampuli kila baada ya miaka miwili  kutoka kwa wafugaji nyuki na kuzipeleka kwenye  Maabara za kimataifa na mara zote  zimekutwa zikiwa na ubora wa hali ya juu unaokidhi masoko yote ya kitaifa na kimataifa.

Amezitaja tafiti  mbili zilizofanyika mwaka 2016 kuwa  lengo lake lilikuwa ni kuainisha madhara ya  ufugaji nyuki kwenye maeneo yanayolima Tumbaku na ameyataja maeneo yaliyofanyiwa utafiti huo kuwa  ni mkoa wa Tabora na Kigoma

Mziray  amesema tafiti hizo zimebainisha kuwa kiwango cha nikotini kinachopatikana  kwenye asali iliyochavushwa katika mikoa inayolima Tumbaku ni sawa na nikotini iliyopatikana kwenye asali  ilivyochavushwa na mimea mingine kama vile  nyanya na miombo hivyo kiwango hicho cha nikotini hakina madhara kwa binadamu.

Amesema  watumiaji wa asali wamekuwa wakihukumu uwepo wa nikotini   kwenye asali kwa kuangalia rangi ya asali sambamba na uchungu wa asali lakini asali za Tanzania zinatengenezwa kwa mchanganyiko wa maua ya mimea mbalimbali  jambo ambalo linathibitishwa si nikotini peke yake ndiyo inasababisha uchungu bali mimea mingine kama vile muarobaini. 

Mziray amewataka watumiaji wa asali kuendelea kuitumia kwa vile  asali ni chakula cha kiasili kinachotengenezwa kutokana na mchanganyiko wa mimea mbalimbali.Ameongeza kuwa, asali ni mchanganyiko uliotokana na maji, Sukari (fruktosi, glukosi, sakrosi) madini pamoja na vitamin.
Baadhi ya Sampuli ya asali inayopatikana katika maeneo mbalimbali za nchi. Asali hutumika kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali kwa binadamu.

SALAMU ZA SHUKRANI NA MWALIKO WA HITMA YA MAREHEMU HAJAT MWL. BATOUL ABDALLAH MBAROUK

$
0
0
Familia ya Alhaj Sudi Suleiman Madega, Katibu Mkuu (Mst) Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU). Inapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa msaada wa hali, mali na faraja walioipatia familia katika kipindi kigumu cha kuuguza, msiba na hatimaye kumpuzisha kwenye nyumba yake ya milele mpendwa wao Hajat Mwalimu Batoul Abdallah Mbarouk aliyefariki tarehe 16 Agosti, 2017 na kuzikwa tarehe 17 Agosti, 2017. Hajat Batoul A. Mbarouk alikuwa Mke wa Sudi S. Madega; na Mama wa Suleiman, Amir, Dr. issa, Maryam, Zuhura na Asha Madega. Pia, Mkwe wa Maryam Hamza Chum, Nuru Kassim Kisesa, Daud Buswelo na Hawa Kadyanji. 
Kwa kuwa ni ngumu kumshukuru kila mmoja, itoshe kusema ahsanteni sana nyote. Hata hivyo, kipekee familia inapenda kufikisha salamu maalum kwa wafuatao:-
i.Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wa Taasisi ya Saratani Ya Ocean Road ambako marehemu alikuwa akitibiwa tangu mwaka huu mwanzoni na hatimaye kuaga dunia tarehe 16 Agosti, 2017. Hususa, Dr. Steve, Dr. Kezia , Dr. Mathew, Dr. Chacha, Dr. Ruta  Dr. Abdi Sangali , Sister Sapine,  Sister Wema , Sister Ester , Sister Doris , Sister Kimath , Sister Eliza , Joel Makanyaga, Mkulia, Alawi, Solomon na wengine wote;
ii.Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako marehemu alikuwa akitibiwa tangu mwezi Agosti, 2016;
iii.Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais (Mst) wa Jamhuri Muungano wa Tanzania na mkewe Mh. Mwl. Salma Rashid Kikwete (Mb) na familia yao; 
iv.Katibu Mkuu, Uongozi na Wafanyakazi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU);
v.Katibu Mkuu, Uongozi na Wafanyakazi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT). Hususan, Makao Makuu, Mkoa wa Dar es Salaam, Mkoa wa Pwani na Walimu wote;
vi.Mh. Jaji (Mst) Harold R. Nsekela (Kamishna wa Maadili), Uongozi na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma; 
vii.Mkurugenzi wa Uchaguzi Ndg. Kailima Ramadhani na Mkurugenzi wa Utawala Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndg. Hamis A. Mkunga; 
viii.Vile vile, tunapenda kutambua familia zifuatazo:- 
Familia ya Mh. Luteni (Mst) Abdallah Kihato, familia ya Mh. Mohamed S. Jegame, familia ya Marehemu Balozi Isaya Bakari Chialo, familia ya Dr. Hamza Juma Chum, familia ya Brigedia Jenerali (Mst) Ussi Khamis wa Zanzibar, familia ya Kisesa, familia ya Masoud Sultan, familia ya Bakari O. Sangali, familia ya Issa Sechonge, familia ya Kisarazo, familia ya Idris Mavura, familia ya Marehemu Mwl. Hemed Ally Kimeah, familia ya Mbaruku Nguzo, familia ya Mbegu na wengine wote. 

Pamoja na salamu hizi, familia inawaarifu na kuwaalika rasmi katika Arobaini ya Marehemu Mwalimu Mbarouk itakayofanyika nyumbani kwake Mbagala siku ya jumapili tarehe 24 Septemba, 2017 kuanzia saa 5 asubuhi mpaka 8 mchana. 

Kwa mawasiliano tafadhali wasiliana na Ndg. Amir Sudi Madega kupitia Namba 0716875737.

Innalilahi Wainailahi Rajioun,
Ahsanteni Sana

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBA) pamoja na Short Stature of Kenya zikionyesha maigizo Tamasha la JAMAFEST

$
0
0
 Kikundi cha burudani ya Uchekeshaji kutoka nchini Kenya maarufu kama Short Stature Society of Kenya kikitoa igizo lake la kuchekesha mbele ya washiriki mbalimbali wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) toka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki 12 Septemba, 2017 Mjini Kampala, Uganda.
Kikundi cha Sanaa cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Tanzania (TaSUBA) kikionyesha igizo lake mbele ya washiriki mbalimbali toka nchi wanachama wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) ambapo igizo hilo likimaanisha namna gani nchi hizo zinavyopaswa kuonyesha ushirikiano wa karibu katika masuala mbalimbali kwa manufaa ya nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki 12 Septemba, 2017 Mjini Kampala, Uganda.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM, KAMPALA-UGANDA)

BREAKING NYUZZZZ.....: BOSI WA ZAMANI WA ATCL, DAVID MATAKA NA MWENZAKE WAHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MIL 70 AU KIFUNGO CHA MIAKA SITA JELA

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka na mwenzake Elisaph Mathew, aliyekuwa Kaimu Afisa Mkuu kitengo cha fedha cha ATCL kulipa faini ya jumla ya sh. Milioni 70 ama kutumikia kifungo cha miaka sita jela. Pia mahakama imewaamuru kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo in USD 143,442.75.

Pia Mahakama imemuachia huru William Haji ambaye alikuwa ni Mkaguzi Mkuu wa hesabu za ndani za ATCL

HABARI KAMILI ITAFUATA.
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images