Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1905 | 1906 | (Page 1907) | 1908 | 1909 | .... | 3272 | newer

  0 0

  THE WORSHIPPERS TANZANIA ni umoja wa makanisa yote wanaopenda kumwabudu Mungu wameandaa mkesha mkubwa kwa ajili ya kumwabudu Mungu katika jiji la Dar es salaam kwa Wana Dar es Salaam wote wapendao kuabudu utakaofanyika 1.12.2017 siku ya Ijumaa kuanzia saa 3 usiku Upanga CCC. 

  Je wewe ni muimbaji ama una kipaji cha kuimba ama wapiga vyombo kanisani? 
  Uko tayari kumwabudu Mungu? 

  Ikiwa umejibu ndiyo basi wewe ni kati ya wale 200 tunaowahitaji kujisajili kushiriki mkesha huu. Jisajili kwa kupiga simu ziziopo hapa chini, Usaili utafanyika tarehe 16.9.2017 Jumamosi saa 2 hadi saa 8 mchana. JISAJILI SASA +255657266777 au +255768570703

  0 0

  Na Mwandishi wetu, Tabora.

  MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameteua Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Queen Mlozi kuongoza Kamati aliyoichagua kwa ajili ya kufuatilia viwanda mbalimbali ili kuangalia hali halisi na kama vimeshindwa kufanyakazi viweze kupewa Wawekezaji wengine. Mwanri aliteua Kamati hiyo jana mjini Tabora wakati wa Mkutano na wadau mbalimbali na Mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi cha Tabora.

  Wengine waliochaguliwa ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philipo Ntiba, Afisa Biashara Mkoa Lucas Kusare ambaye ni Katibu wa Kamati, Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Richard Lugomela na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini, Tiganya Vincent.

  Alisema kuwa Kamati hiyo itaanza na Kiwanda cha Nyuzi Tabora ambapo itaangalia mpango kazi wake , itakagua mashine zote kama zinafanyakazi na uwezo wa kifedha wa mwekezaji huyo kama anao mtaji wa kutosha wa kuendesha kiwanda.Mambo mengine yatakayofuatiliwa na Kamati hiyo ni pamoja na kuangalia matatizo ambayo Mwekezaji huyo aliyaeleza kuwa ukosefu wa soko la nyuzi zake kutokana na viwanda ambavyo ndio vilikuwa vikinunua kwake kuanza kuagiza toka nje bidhaa hizo.

  Mkuu huyo Mkoa aliongeza kuwa mambo mengine ambayo Kamati itayafanya ni kuangalia fursa za masoko ya bidhaa za Kiwanda hicho kama vile Bohari Kuu za Dawa (MSD), Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU) na wafanyabiashara wengine wanaweza kununua bidhaa zake.Alisema kuwa Kamati hiyo itatakiwa kila baada ya siku tatu impelekee taarifa ya maendeleo ya kazi yao.

  Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ametoa mwezi mmoja kwa Mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora kuhakikisha mashine zake zinafanyakazi.Alisema kuwa baada ya kipindi kuisha atakwenda kukagua na akikuta hakuna kitu atalazimika kumuomba Waziri wa Viwanda aje kuchukua hatua ikiwemo kumpa mwekezaji mwingine.

  Mkuu huyo Mkoa alisema kuwa hata kama mali ghafi kwa sasa hivi hakuna anataka ni kujiridhisha kuwa mashine zote ni zima wakati akiwa anasubiri msimu wa pamba ujao ili apate mali ghafi.Mkuu wa Mkoa wa Tabora yuko katika zoezi la kuhakiki viwanda vyote ili kujiridhisha kama vinafanyakazi na vile ambavyo wamiliki wake wameshindwa waweze kuvirudisha Serikalini
   Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akitoa ufafanuzi jambo kwa mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora alipotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kujionea hali halisi ya uzalishaji wa nyuzi. Kulia ni Mkurugenzi wa Kiwanda Mtendaji wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora Urveshi Rajani.
   Kaimu Meneja wa Manunuzi kutoka Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU) Bernard Makhanda (kushoto) akitoa utaratibu wa kufuatwa na Mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora ili aweze kupata fursa ya kuwauzia nyuzi kwa ajili ya wakulima wa tumbaku. Kulia ni Meneja wa Kanda wa Bodi ya Pamba Jones Bwahama.
   Mkurugenzi wa Kiwanda Mtendaji wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora,  Urveshi Rajani akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri mitambo ya kutengeneza nyuzi alipotembelea kiwanda hicho kujionea hali ya uzalishaji.
  Mitambo ya Kiwanda cha Nyuzi Tabora ambayo hivi sasa haifanyi kazi licha ya kuwa mizima.

  0 0

  RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Mh. Anthony Mtaka, kwa kutambua mchango mkubwa wa wadau mbalimbali katika maendeleo ya mchezo wa riadha hapa nchini, ameandaa kusanyiko (kikao cha pamoja), na waandaaji mbalimbali wa mbio ndefu hapa nchini.

  Waandaaji wa matukio mbalimbali ya mchezo wa raidha hapa nchini, kwa namna moja ama nyingine wamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya mchezo wa riadha hapa nchini na jamii kwa ujumla, hivyo kwa kutambia hilo, RT imeona kuna umuhimu mkubwa Kamati yake ya Utendaji ikakutana na waandaaji hao katika uboreshaji

  Itakumbukwa kwamba, hivi sasa kumekuwa na uibukaji mkubwa wa watu mbalimbali kuandaa matukio hayo ya riadha bila kufuata taratibu na kanuni zilizopo kisheria na kikanuni hivyo kupoteza lengo tajwa la mchango wa kimaendeleo katika mchezo na jamii kwa ujumla.

  Hivyo RT inaamini kupitia kusanyiko hilo litakalofanyika Septemba 16 mwaka huu kwenye ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi litaibuka na maazimio chanya ya kuweka taratibu na miongozo sahihi kwa pande zote, ikiwamo taratibu za uandaaji wa matukio ya riadha, viwango vya matukio hayo, pia mpishano wa tukio moja na jingine bila kuingiliana (Kalenda).

  Hivyo tunapenda kutoa wito kwa waandaaji wote, ambao tayari tunaamini wameishapata wito ‘official’ watajitokeza bila kukosa. RT inapenda kuwashukuru Kampuni ya MultChoice Tanzania ‘DStv’ kufanikisha tukio hili kwa manufaa ya maendeleo ya mchezo wa Riadha Tanzania.

  Itakumbukwa, DStv kwa muda sasa, wamekuwa washirika wazuri katika kuchangia maendeleo ya mchezo wa raidha Tanzania, ikiwamo kufadhili kambi za timu zetu za Taifa na hata kwa wanariadha mmoja mmoja, akiwamo Mshindi wa Medali ya Shaba katika mashindano ya Dunia, Alphonce Felix Simbu .

  MBIO MBALI MBALI ZINAZOENDESHWA
  HAPA NCHINI

                                  JINA LA MBIO                                 INAKOENDESHWA

  1.      KILIMANJARO INTERNATIONAL MARATHON -           KILIMANJARO
  2.      KILFM HALF MARATHON                                -           KILIMANJARO
  3.      HEART HALF MARATHON                               -           DAR ES SALAAM
  4.      NGORONGORO  HALF MARATHON                -           MANYARA
  5.      KARATU  10KM                                                -           MANYARA
  6.      BABATI  HALF  MARATHON                            -           MANYARA
  7.      TULIA HALF MARATHON                                 -           MBEYA
  8.      SEREBUKA  HALF  MARATHON                       -           SONGEA
  9.      TANGA HALF MARATHON                               -           TANGA
  10.    MT. MERU MARATHON                                  -           ARUSHA
  11.    DAR  ROTARY  INT. MARATHON                    -           DAR ES SALAAM
  12.    BAGAMOYO  HALF  MARATHON                    -           PWANI
  13.    10KM                                                               -           ARUSHA
  14.    KIA  HALF  MARATHON                                   -           KILIMANJARO
  15.    SERENGETI MARATHON                                 -           SIMIYU
  16.    ROCK CITY  MARATHON                                 -           MWANZA
  17.    IGOMBE  HALF  MARATHON                          -           TABORA
  18.    MEI  DAY HALF MARATHON                           -           DAR  ES  SALAAM
  19.    IKUNGI  HALF MARATHON                              -           SINGIDA
  20.    NAMTUMBO HOSPITAL FUND RAISING          -           SONGEA
  21.    ARUSHA TOURISM HALF MARATHON            -           ARUSHA

  IMETOLEWA NA WILHEM GIDABUDAY
  KATIBU MKUU RT
  SEPTEMBA 12, 2017

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi Leseni ya Usajili wa machapisho mwakilishi wa Jarida la PLUS 255 MAGAZINE Bw. Francis Maduhu mara baada ya kukamilisha taratibu za usajili leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi la utoaji wa Leseni kwa machapisho linafuatia utekelezaji wa kifungu namba 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Usajili Bw. Patrick Kipangula.
   Mwakilishi wa Jarida la PLUS 255 MAGAZINE Bw. Francis Maduhu akionyesha Leseni ya machapisho aliyokabidhiwa kwa ajili ya Jarida lake leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi la utoaji wa Leseni za machapisho linafuatia utekelezaji wa kifungu namba 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimpongeza mwakilishi wa Jarida la PLUS 255 MAGAZINE Bw. Francis Maduhu baada ya kumkabidhi Leseni ya Usajili wa machapisho kufuatia kukamilisha taratibu za usajili leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi la utoaji wa Leseni za machapisho linafuatia utekelezaji wa kifungu namba 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Usajili Bw. Patrick Kipangula.

  Picha na: Idara ya Habari - MAELEZO

  0 0

  Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akifurahi jambo wakati akimsikiliza Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid alipomtembelea ofisini kwake, Bungeni Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (wa kwanza kulia) akifurahi katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid alipomtembelea ofisini kwake, Bungeni Mjini Dodoma na Mheshimiwa Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Watu wenye Ulemavu .


  0 0

  Na David John Mwanza

  KIJANA Ruyendela Barugali mkazi wa Nyamagana mkoani Mwanza anamuomba rais Dkt. John Magufuli kumsaidia kwani anaishi katika mazingira magumu na amepotezana na mama yake mzazi tangu akiwa mdogo.

  Pia baba yake mzazi alishafariki miaka mingi hivyo anamkumbuka rais Magufuli kwani kuna wakati aliwahi kuzamia na Treni hadi Dar es Salaam ambapo aliwahi kupewa sh 20000 katika eneo la Magomeni wilaya ya kinondoni wakati huo akiwa waziri wa Ujenzi.

  Ruyendera Ameyasema haya leo jijini Mwanza katika eneo la Makoroboi ambapo maisha yake yote yanapatikana hapo ambapo anamiaka kumi analala nje huku akisema hapendezwi na hali hiyo .Amesema kuwa kimsingj hapendi maisha anayoishi na anatamani kuona rais wake John Magufuli anamsoma ili aweze kumsaidia huku akidai kutokana na ngumu aliyonayo anatamani kusoma lakini hayupo mtu wa kumshika mkono.

  "Simjuwi mama yangu niliwahi tu kuwaambiwa kwamba mama yangu anaitwa Zawadi na nasikia anaishi Nyarugusu.na baba yangu mkubwa anaitwa Kanyikalila Mtalemwa anaishi Mganza wilayani chato. "amesema Ruyendela .Pia anasema baba yake alishafariki siku nyingi tangu yeye akiwa mdogo na kudai bahati mbaya aliyonayo hana ndugu wa jamaa hali inayomfanya kuonekana kama mtoto wa mtaani.

  Anasema msaada pekee anaouna ni rais Dtk John Magufuli kwani anasema kwakuwa alishawahi Kumsaidia na akamtaka arudi chato mkoani Geita na akafanya hivyo lakini bahati mbaya mazingira aliyokutana nayo kwa baba yake mkubwa Mzee Kanyikali yalikuwa sio rafiki.

  Pia ameomba viongozi na wadau wengine kujitokeza kumsaidia kwani hata maeneo anayolala anasumbuliwa na polisi kila wakati hali ambayo inamhuzunisha nakusababisha amkumbuke mama yake.

  Kushoto ni Naibu katibu mkuu wa taasisi ya kutetea Haki Za Binadamu Tanzania (TAHURA) akifanya Mahojiano na kijana Ruyendela Barugali.( Kulia),Kijana ambaye anahitaji msaada wa rais Dkt.John Magufuli picha David John. 

  0 0

  Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akifurahi jambo wakati akimsikiliza Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid alipomtembelea ofisini kwake, Bungeni Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (wa kwanza kulia) akifurahi katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi  Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid alipomtembelea ofisini kwake, Bungeni  Mjini Dodoma na Mheshimiwa Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Watu wenye Ulemavu .

  0 0

  Na Georgina Misama – MAELEZO

  Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imewaonya watumishi wa Umma kutoa taarifa za serikali za siri na za kawaida kwa watu ambao sio walengwa wa taarifa hizo.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Maadili kutoka Wizara hiyo Lambert Chialo alisema kwamba kwa mujibu wa sheria ya Usalama wa Taifa Na. 3 ya mwaka 1970 na marekebisho yake, Ibara ya 5(a) na (b), adhabu ya uvujaji wa siri ni kifungo kisichozidi miaka 20.

  “Hivi karibuni tumeshuhudia taarifa za serikali za siri zikitumwa katika vyombo vya habari pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii kitu ambacho ni kosa kisheria na ni kinyume cha Kanuni za Maadili ambapo inasisitizwa kuwa na matumizi sahihi ya taarifa”, alisema Chialo.

  Chialo aliongeza kwamba lengo la serikali si kuficha taarifa kwa wadau wake, bali taarifa zinazotolewa zinapaswa kutolewa kwa utaratibu maalumu na kupelekwa kwa watu wanaopaswa kupokea taarifa hizo (walengwa). Aidha, taarifa zinazotolewa na taasisi husika lazima zipate idhini kwa Uongozi husika kabla ya kupelekwa kwa wadau.

  Akiongelea suala la matumizi mabaya ya Ofisi, Chialo alisema kwamba baadhi ya watumishi wamekuwa wakitumia nafasi walizonazo kwa manufaa yao binafsi na sio ya Umma, kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na watumishi watakaogundulika watawajibishwa kwa mujibu wa Kanuni na taratibu.

  Watumishi wa Umma wanapaswa kufahamu kwamba serikali inaendelea kufatilia matendo yote yasiyo ya kimaadili na kuchukua hatua kila inapobidi. Aidha, wananchi wanaombwa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za ukiukwaji wa maadili katika taasisi za umma kila wanaposhuhudia matukio hayo.

  “Tunalo dawati la msaada kwa ajili ya kupokea maoni, malalamiko, ushauri na taarifa mbalimbali katika kuhakikisha utoaji wa huduma za serikali kwa wananchi unaboreshwa” alisema Chialo.

  Chialo alitoa rai kwa wananchi wote kwa ujumla, kuzingatia swala la maadili kuanzia ngazi ya familia. Aidha, inasisitizwa viongozi na wasimamizi wa kazi kuendelea kuelimisha watumishi kuhusu suala la maadili na kuhakikisha watumishi wanaishi kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo kwa vitendo.
  Kaimu Mkurugenzi wa Maadili toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Lambert Chialo (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akieleza umuhimu wa watumishi wa Umma kuzingatia maadili kazini, kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Bi. Mary Mwakapenda. Picha na Eliphace Marwa - Maelezo.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

  Serikali imedhamiria kununua mashine tatu za vipimo vya vinasaba (DNA) ili zitumike katika maabara za Kanda na hivyo kusogeza huduma karibu na wananchi.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala wakati akijibu swali la Mbunge wa Chumbuni Mhe. Ussy Pondeza kuhusu ucheleweshwaji wa matokeo ya uchunguzi wa sampuli ikiwemo sampuli za makosa ya jinai.

  Dkt Kigwangala amesema kuwa Serikali ina mkakati wa kuongeza mashine hizo ili kuwezesha uchunguzi kufanyika kwa wakati kwa vielelezo vya makosa ya jinai ikiwa ni pamoja na vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto.

  " Sampuli za uhalali wa watoto kwa wazazi zinafanyika kwa wepesi zaidi kuliko sampuli za makosa ya jinai kwani sampuli hizo zinachukuliwa moja kwa moja toka kwa wahusika hivyo kurahisisha uchunguzi wake endapo wahusika wa uchukuaji watachukua kwa umahiri na uhifadhi utafanyika kwa namna stahili" amefafanua Dkt. Kigwangala.

  Aidha, Dkt. Kigwangala amesema kuwa sampuli za uchunguzi wa makosa ya jinai zinachukuliwa toka maeneo ya matukio hivyo uchunguzi wake unaweza kuchukua muda zaidi kutegemeana na aina ya sampuli na eneo zilipotoka.

  Vilevile Dkt. kigwangala aliongeza kuwa Serikali inampango wa kuanzisha kituo cha kupima vinasaba (DNA) Mkoani Mbeya kwa lengo la kupunguza ucheleweshaji wa matokeo ya uchunguzi.

  Mbali na hayo akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Vijijini Mhe. Hawa Ghasia kuhusu Serikali kuagiza tohara kuwa lazima kwa wanaume nchini, Dkt. kigwangala amesema kuwa si rahisi kwa Serikali kuagiza tohara  kuwa lazima japo kuwa inafaida kiafya kwa wananchi.

  " Tohara inasaidia kupunguza maambukizi ya Saratani ya shingo ya Uzazi kwa wanawake pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi" ameongeza Dkt. kigwangala.

  Aidha, amesema kuwa elimu kuhusu tohara imefikishwa kwa wananchi kwa kiasi kikubwa ambapo Serikali kwa kushirikiana na wadau katika Mikoa ya kipaumbele  imekuwa ikitoa elimu kabla na baada ya huduma ya tohara katika vituo vya kutolea huduma za afya.

  0 0

  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa mwaka 2017.

  Akiwasilisha Bungeni Muswada huo leo Mjini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa lengo la marekebisho yaliyopendekezwa ni kuboresha utekelezaji wa Sheria hizo kwa kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kutumia sheria hizo na kuongeza masharti mengine ili kuleta uwiano kati ya Sheria zilizorekebishwa na sheria zilizopo.

  "Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa mwaka 2017 unapendekeza kufanya marekebisho katika sheria 11 na kufuta sheria moja" amefafanua   Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

  Aidha, Masaju amesema kuwa masuala muhimu yaliyozingatiwa katika Muswada huo ni pamoja na kubadilisha vifungu vya Sheria kwa kufuta baadhi ya vifungu vya sheria hizo na kuviandika upya, kufuta baadhi ya maneno kwenye vifungu vya sheria, kuzingatia maneno mapya, kuongeza vifungu vipya na kufuta sheria moja.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mohamed Mchengerwa amesema kuwa Kamati inashauri  Serikali kuhakikisha Kamati maalumu ya kumshauri Waziri kuhusu misamaha ya kodi iundwe na wataalamu waliobobea kutoka katika fani na maeneo tofauti tofauti ili kujenga uwezo wa kamati hiyo katika kumshauri Waziri husika kuhusu misamaha hiyo ya kodi.

  Nae Ally Saleh Ally kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Wizara ya Katiba na Sheria amesema kuwa kambi hiyo inashauri kuwa haitoshi kuifuta RUBADA pekee bali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu malalamiko ya wananchi wanaoituhumu kupora ardhi na hatua stahiki kwa wote waliohusika zichukuliwe.

  0 0

  Mhazini wa chama cha waigizaji Taifa (TADFAA), Lydia Mgaya akizungumza na mwandishi wa Michuzi blog jijini Dar es Salaam leo baada ya kumaliza kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Kuhusiana na Ubadhirifu wa fedha ndani ya  chama cha waigizaji Taifa (TADFAA).

  Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii.
  TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza upelelezi kuhusiana na kiasi cha sh. Milioni tano fedha ambazo zilitolewa na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF mwaka jana kwenda kwa  chama cha waigizaji Taifa (TADFAA) kwa ajili ya kuwahamasisha wasanii wote nchini kujiunga na mfuko huo na kunufaika na mambo mengi ikiwemo matibabu.

  Upepelezi huo unafuatia taarifa iliyowasilishwa na mjumbe wa bodi na Mhazini wa chama hicho, Lydia Mgaya ambaye mapema leo amehojiwa na Takukuru, kwenda kwa Rais wao Simon Mwakifwamba mwaka huu, kufuatia hela hizo kutoonekana bila ya kujua zimetumikaje tangu zilipoingizwa katika akaunti ya chama hicho iliyopo  benki CRDB Februari mwaka jana.

  Akizungumza na Michuzi blog leo, Lyidia amesema, “Nilipeleka barua katika shirikisho la filamu Tanzania (TAF), kulalamikia ubadhirifu wa fedha unaofanywa na mwenyekiti wetu, Elia Mjata na Katibu wake Twiza Mbaruku ambapo ziingie hazionekani zimeenda wapi na je kama zipo zinafanya nini, kama zipo ina maana hazina matumizi”.

  Amesema, kuwa akiwa kama muhazini, alienda pamoja na Mwakifwamba katika benki hiyo tawi la millennium Tower ili kupata taarifa za akaunti (Bank statement) lakini ilishindikana baada ya kuambiwa kuwa, akaunti yao hiyo ina shilingi 28,000 tu na ili kupata taarifa za akaunti (Bank statement) lazima wawe na  shilingi 90,000/- ila walihakikishiwa kuwa fedha za PPF kweli ziliingia.

  “Chama cha wasanii kimechafuka, wasanii wamechafuka, serikali na Wizara yetu haituamini tena, ili kurudisha heshima lazima tuanze kuwaondoa viongozi wote wabadhirifu wa fedha ili kurudisha chama katika hadhi yake tuweze kuaminika upya na tukipewa mradi wowote tuufanye kwa wakati”. Amesema Mgaya.

  Aidha amewaasa watu ambao wanampango wa kuombea uongozi kwenye chama hicho na wanampango wa kuiba ni vema wakabadili mawazo na kufikiria zaidi kufanya mazuri ndani ya chama na kurudisha heshima.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Septemba, 2017 ametembelea hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Jijini Dar es Salaam na kumjulia hali Meja Jen. Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni Jijini Dar es Salaam.  Meja Jen. Mstaafu Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana tarehe 11 Septemba, 2017 majira ya mchana na kisha kukimbizwa katika hospitali ya Jeshi Lugalo kwa matibabu.  Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa Meja Jen. Mstaafu Vincent Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa risasi alizopigwa mkononi, kiunoni na tumboni.

  Meja Jen. Mstaafu Mritaba amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumjulia hali    na kumuombea dua ili apone haraka.  Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jen. Venance Mabeyo pia ametembelea wodi ya majeruhi na kuwajulia hali wagonjwa wanaotibiwa katika wodi hiyo na baadaye akawasalimu wananchi waliofika hospitali hapo kwa ajili ya kupata matibabu.

  Mhe. Dkt. Magufuli amewapongeza Madaktari wa hospitali ya Jeshi Lugalo kwa huduma za matibabu wanazotoa kwa askari na wananchi wengine                           na amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe Meja  Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba akielezea alivyoshambuliwa kwa  risasi mkononi, tumboni na mguuni  wakati akiingia  nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
   ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) wakioneshwa na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe Brigedia baadhi ya risasi  zilizotolewa kwenye mwili wa  Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba  baada ya kushambuliwa wakati akiingia  nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe,  Brigedia Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba na wauguzi wakiomba dua wakiongozwa na Mama Margareth Vicent Mritaba hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa Meja Jenerali Mritaba akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni  wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mtoto Nathan Martin  wakati akitoka kumjulia hali Meja jenerali Mstaafu Vicent Mritaba aliyelazwa Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni  wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwalimu  Aloys Konolipa wa Shule ya Msingi Kidugalo wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani alipopita kuwapa pole wagonjwa wengine baada ya kumjulia hali Meja  Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba aliyelazwa Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni wakati akiingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni. Picha na IKULU

  0 0

  Katika kuboresha huduma za kibenki nchini Maendeleo Bank lao imetoa zawadi kwa washinidi wake wanne wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya ‘Maendeleo pamoja na wewe’ iliyochezeshwa tarehe 31/8/2017 Jijini Dar es salaamHafla ya kuwapatia washindi hao zawadi ilifanyika leo katika ukumbbi wa ‘Mviringo hall’ uliopo makao makuu ya Benki hiyo ‘Luther House’ posta Jijini hapa ambapo washindi hao wanne walijishindia zawadi tofauti tofauti ikiwemo Ada za shule, tani za Saluji,Mabati pamoja na kiwanja, 
  Akizungumza katika hafla hiyo fupi mkuu wa kitengo cha biashara Maendeleo Bank Peter Tarimo amesema katika kuhakikisha Maendeleo Bank inakuwa karibu na wateja wao imeamua kuwahamasisha hasa wazazi kufungua Account za Benki kwa ajili ya watoto wao ili kuweza kuwajengea utamaduni wa kuhifadhi fedha
  “Mtakumbuka kuwa kampeni hii ilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi wa nane na wateja wengi walishiriki, Droo ilichezeshwa chini ya usimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha (Gaming Board) na kuwapata washindi hawa wanne ambao leo tunakwenda kuwakabidhi zawadi zao” 
  Aidha tarimo aliongeza kuwa Droo ya pili ya bahati na sibu hiyo inatarajiwa kuchezeshwa mwezi wa Novemba mwaka huu na ya tatu itakuwa mwezi Disemba ili kupisha zoezi la uuzaji wa Hisa litakaloanza tarehe 18/9/2017 na kutarajiwa kumalizika mwezi October 

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  KOCHA wa makipa wa timu ya Azam Fc, Idd Abubakar, amekiri upinzani mkali kwa makipa wake kikosini kwani wana jumla ya makipa wanne kikosini, Mghana Razak Abalora, Mwadini Ally, Benedict Haule na Metacha Mnata aliyepandishwa, wote wakiwa wanaunda kikosi cha timu kubwa kwenye eneo hilo.

  Kwa sasa tokea Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ianze Agosti 26 mwaka huu, Abalora ameonekana kuwa chaguo la kwanza, akiwa mpaka sasa hajaruhusu wavu wake kuguswa kwenye mechi zote mbili za mwanzo, Azam FC ikiifunga Ndanda bao 1-0 kabla ya juzi kutoka suluhu na Simba. 

  Abubakar alisema kuwa upinzani huo ulidhihirika wakati wakiwa kwenye kipindi cha maandalizi ya msimu mpya nchini Uganda, ambapo kila kipa aliyepewa nafasi aliweza kukaa imara langoni.

  “Upinzani upo mkubwa sana na isitoshe vilevile baada ya kuziangalia mechi za pre season tulizocheza kila mmoja anataka nafasi, hawa makipa wote wanne wanahitaji kucheza na viwango vya vyote mazoezini na mechi wanazopewa kila mmoja mechi yake ameitendea haki. 

  “Tulianza mechi ya kwanza na Mwadini (Ally) amecheza vizuri tu tumekuja tumecheza na Razak (Abalora) mechi mbili amecheza vizuri kwa hiyo kiwastani kiujumla kabisa upinzani upo mkubwa sana kwamba hakuna golikipa ambaye amebweteka kwamba hapa amefika katika hii nafasi,” alisema. 
  Kocha wa makipa wa timu ya Azam Fc, Idd Abubakar (pili kulia) akiwa pamoja makipa wanaounda kikosi cha timu hiyo.  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  MSANII wa muziki wa kizazi kipya Shaban Mpute 'Ne-Mo' amesema amedhamiria kurudi katika familia ya muziki kivingine, huku akitarajia kuachia wimbo wake mpya unaitwa 'Kipotabo'Septemba 19 mwaka huu ambayo imetengenezwa katika studio za Combination Sound chini ya mtayarishaji Man Water na video kutengenezwa na Kwetu Studio.

  Akizungumzia ujio wake  mpya Ne-Mo chini ya lebo ya 'Digital City Drimz' alisema kuwa amedhamiria kuirejesha RnB ya Bongo katika viwango na pia kuipeleka nje ya mipaka ya Tanzania, kwa sababu anahifahamu vizuri na  kwa sasa kuna wasanii kama Diamond Platnumz, Ali Kiba, Vanessa Mdee, Navy Kenzo na wengineo wameubeba muziki wa Bongofleva na kusaidia kuupenyeza kimataifa, naye ana matumaini makubwa ya kufika walipo wasanii hao.

  Ne-mo ujio wake utakuwa wa aina yake na Watanzania hawatajutia kumsubiri Ne-Mo arudi kwa muda wote huo, kwamba ukimya wake umetokana na masomo ambapo aliamua kutulia amalizie masomi kisha aendelee na Harakati za Muziki na  alikuwa masomoni akiwa amesomea  masuala ya  'Mass Communication' na anaeleza kuwa sasa ametulia na amepata 'Mameneja ' ambao wanamsimamia na kumrejesha kwa kishindo katika muziki.

  "Nimejipanga vuzri pamoja na mameneja wangu narudi kimuziki kikweli kweli, naomba mashabiki wa muziki Tanzania wanipokeekwa mara nyinyingine, nilitoka kidogo kwenda masomini lakini sasa nimerudi rasmi katika muziki"alisema Ne-mo.

  Alisema kwa upande wa mtindo wa Rap na Hip Hop mwanzoni mwa miaka ya 2000 Profesa Jay alichangia kuuweka muziki wa Hip Hop mtaani na kukubalika na kila kundi la jamii., miaka michache iliyopita waliibukakina Child Benz na Nako 2 Nako ambao walisaidia kujenga misingi ya kuufanya muziki wa Hip Hop kukubalika kibiashara.


  0 0


  KIASI cha shilingi milioni tatu na laki saba, Hati za wateja tofautitofauti pamoja na nyaraka mbalimbali za ofisi ya mawakili ya Prime Attorney advocate zilizopo upanga jijini Dar es Salaam zaibwa na watu wasiojulikana wakati walipovamia ofisi hiyo majira ya saa tisa na nusu usiku.

  Hayo yamesemwa na wakili, Asia Charles akizungumza kwa niaba ya Wakili Hudson Ndusyepo wakati akizungumza na Michuzi Blog leo amesema kuwa “Ni kweli Majambazi hao walifanikiwa kuvunja milango ya ghorofa ya kwanza na ya pili hawakuchukua kitu chochote na wakafanikiwa kupanda mpaka ghorofa ya tatu upande wa kushoto  waliingia ofisi ya Mhasibu na kufanikiwa kuchukua kabati binafsi (Self) ambalo lilikuwa na Nyaraka za Ofisi, pesa shilingi milioni Tatu na laki saba pamoja na Nyaraka mbalimbali za Wateja".

  Amesema kuwa Watu hao wamecheza zaidi na Vitasa vya Milango na kufanikiwa kufungua Milango na kuiba Kabati Binafsi (Self) walilokuwa wanalitaka.

  Asia maesema kuwa Mlinzi alieleza kuwa walipofika katika ofisi hizo alijitahidi kuwazuia lakini wakamshinda kutokana na kumzidi nguvu pamoja na uwingi wao, pia mlizi amesema aliwaambia kuwa walimwambia asiongee kitu chochote na wakamuamlisha awapeleke wanakotaka na baadae baada ya kufika wakamziba mdomo na Plasta Nyeusi ili asiweze kupiga kelele.

   "Tunasubiri  Uchunguzi wa Polisi Ukamilike ndio tunaweza tukatoa taarifa kamili" Amesema Asia. Wakili, Asia Charles akizungumza na Mwandishi wa Michuzi Blog jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa Kiasi cha shilingi Milioni Tatu pamoja na Nyaraza za ofisi ya Prime Attorney advocate  pamoja hati mbalimbali za wajeja wao zimeibwa na watu wasiojulikana walipovamia Ofisi hiyo Usiku wa Kuamkia leo Upanga jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Sehemu zilizoharibiwa na watu waliovamia Ofisi ya Prime Attorney advocate iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam na kuchukua Nyaraka za ofisi hiyo zilizokuwa kwenye kabati binafsi (Self). 
  Baadhi ya haribifu uliotokea katika ofisi ya Prime Attorney advocate.
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua  Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano 2017/18 - 2021/22 kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango ambapo pia ilishuhudiwa na Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Zubeir Ali Maulid, Naibu Waziri Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo, Naibu Waziri Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji na Wadau wa Maendeleo kwenye Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. 


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati uzinduzi wa Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano 2017/18 - 2021/22 katika Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. 
  Sehemu ya Waliohudhuria wakipiga makofi mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano 2017/18 - 2021/22 katika Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango wakati akiwasili kwenye uzinduzi wa Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano 2017/18 - 2021/22 katika Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0


  0 0

  Kampuni ya Zuku imezindua huduma ya Intaneti yenye uwezo mkubwa wa kuweza kufanya kazi kwa vitu vitatu kwa wakati mmoja.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mtendaji wa Zuku Fiber, Thomos Hintze amesema kuwa Zuku Fiber inawezo mkubwa kuliko mitandao mengine iliyopo nchini.

  Amesema kuwa wamejipanga kutokana na kampuni hiyo kuwa na miundombinu inayojitosheleza ambapo mtu akilipia anapata huduma muda huo huo

  Hata hivyo amesema kifurushi cha Zuku fiber triple Play 100 mbps kimeundwa ili kukidhi mahitaji ya mtandaoni kama video fupi, sinema , michezo ya kuigiza na video za mawasiliano.

  Hintz amesema kuwa gharama za mtandao huo ni sh .79,000 ambapo Mteja anapoanza  kutumia uwezo wake ni uleule mpaka mwisho.

  Amesema kampuni hiyo imekwenda mbali baadhi ya nchi za Afrika ambazo ni Zambia, Malawi, Uganda pamoja na Kenya.

  Afisa Mtendaji wa Zuku Fiber, Mhandisi Thomos Hintze akizungumza na waandishi katika uzinduzi wa Intaneti  Fiber iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Meneja wa Zuku Fiber Thomas Wenanga  pamoja na Mkuu wa kitengo cha Fiber, Michael Debaly 
  Meneja Uendashaji wa Zuku Fiber, Mcharo Mlaki akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya Intaneti iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Zuku Fiber, Mhandisi Thomos Hintze akiwa na watendaji wa kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 1905 | 1906 | (Page 1907) | 1908 | 1909 | .... | 3272 | newer