Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

IGP SIRRO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MA IGP NA MAKAMISHNA WA POLISI WASTAAFU NA WALIOPO KAZINI

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro (wapili kulia), akizungumza na Ma IGP wastaafu na makamishna wastaafu na waliopo kazini (hawapo pichani) wakati alipokutana nao leo jijini Dar es salaam ikiwa ni mpango wa kubadilishana uzoefu wa kikazi pamoja na kupeana mbinu na mikakati ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu pamoja na mikakati ya kuboresha utendaji wa Jeshi hilo, kulia ni IGP mstaafu Said Mwema, wa kwanza kushoto ni IGP msataafu Ernest Mangu na IGP mstaafu Omari Mahita. 

 Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu (IGP) Ernest Mangu (kushoto), akizungumza mbele ya makamishna wastaafu na waliopo kazini (hawapo pichani), kwenye kikazo kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (wapili kulia) kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu na mikakati ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu pamoja na mikakati ya kuboresha utendaji wa Jeshi hilo leo jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni IGP msataafu Said Mwema na wapili kulia ni IGP msataafu Omari Mahita. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu (IGP) Omari Mahita (wapili kushoto), akizungumza mbele ya makamishna wastaafu na waliopo kazini (hawapo pichani), kwenye kikazo kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (wapili kulia) kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu na mikakati ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu pamoja na mikakati ya kuboresha utendaji wa Jeshi hilo leo jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni IGP msataafu Said Mwema na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu (IGP) Ernest Mangu. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu (IGP) Said Mwema (wa kwanza Kulia), akizungumza mbele ya makamishna wastaafu na waliopo kazini (hawapo pichani), kwenye kikazo kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (wapili kulia) kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu na mikakati ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu pamoja na mikakati ya kuboresha utendaji wa Jeshi hilo leo jijini Dar es salaam kutoka kushoto ni IGP mstaafu Ernest Mangu na anayefuata ni IGP msataafu Omari Mahita. 
 Kamishna wa Utawala ndani ya Jeshi la Polisi DCP Leonard Paul (aliyesimama), akiwasilisha mada mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro na ma IGP wastaafu na Makamishna wastaafu wa Jeshi hilo na waliopo kazini, kwenye kikazo kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Jeshi hilo kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kupeana mbinu na mikakati ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu  pamoja na mikakati ya kuboresha utendaji wa Jeshi hilo leo jijini Dar es salaam. 
Ma IGP na Makamishna wa Polisi wastaafu na waliopo kazini wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi hilo (IGP) Simon Sirro, wakati alipokutananao leo jijini Dar es salaam ikiwa ni mpango wa kubadilishana uzoefu wa kikazi pamoja na kupeana mbinu na mikakati ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu pamoja na mikakati ya kuboresha utendaji wa Jeshi hilo 
Ma IGP na Makamishna wa Polisi wastaafu na waliopo kazini wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi hilo (IGP) Simon Sirro, wakati alipokutananao leo jijini Dar es salaam ikiwa ni mpango wa kubadilishana uzoefu wa kikazi pamoja na kupeana mbinu na mikakati ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu pamoja na mikakati ya kuboresha utendaji wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Polisi. 

Sherehe za miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Skuli ya Nungwi, Zanzibar

$
0
0
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewagiza wasomi nchini kwa kushirikiana na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuzifanyia tathmini za kitaalamu mara kwa mara skuli walizosoma kwa lengo la kuzisaidia kupata maendeleo endelevu ya elimu.

Balozi Seif ameyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi wa Nungwi wakati wa kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Skuli ya Nungwi ambayo aliwahi kuwa mwalimu Mkuu wa kwanza.

Makamo wa Pili amesema tathmini ni nyenzo muhimu ya kielimu itakayozisaidia Skuli na wataalamu wa Elimu nchini  kurekebisha mapungufu yaliyopo kwenye Skuli hizo kwa wakati pamoja na kujipangia mikakati mipya ya kurekebisha mapungufu hayo. 

Amesema  utoaji wa elimu na tathmini ni vitu vinavyokwenda sambamba na kwa kuanzia amewagiza wasomi wa Nungwi kumpatia tathmini ya kitaalamu ya Skuli yao ndani ya wiki tatu.

Akizungumzia elimu kwa jumla katika kijiji cha Nungwi balozi Seif amewahimiza wanafunzi wa Skuli hiyo kupania katika masomo yao ili kuendelea na masomo ya juu.

Amesema Nungwi imebarikiwa na mazingira mazuri yanayowavutia wageni kuwekeza katika sekta ya utalii  jambo ambalo linatoa fursa nyingi za ajira kwa vijana. Hata hivyo Balozi Seif amesema fursa hizo hazitopatikana kwa wanaNungwi ikiwa hawatajibiidisha katika masomo yao. 

Amesema fahari ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuona hoteli zote za Nungwi zinaendeshwa na vijana wa Nungwi, kwa hivyo amewataka vijana hao kujiunga na vyuo vya utalii nchini kwa wingi kwa mafunzo ya shahada ya utalii.

Wakati wa sherehe hizo za miaka 50 ya kuanzishwa Skuli ya Nungwi Makamo wa pili wa rais Balozi Seif Ali Iddi alipata nafasi kuweka  jiwe la msingi la ukumbi wa kufanyia mitihani mradi ambao unaendeshwa kwa nguvu za wananchi na wafadhili mbali mbali chini ya usimamizi wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Kijiji cha Nungwi (TAMEN)

Akimkaribisha Makamo wa Pili wa Rais, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Riziki Pembe Juma amewataka wananchi wa Nungwi kushikiana kwa hali na mali katika miradi mbali mbali ya skuli ikiwemo ujenzi wa ukumbi wa kufanyia mitihani, ujenzi wa mabanda ya madarasa na ujenzi wa ukuta ambao utakuwa ni uzio wa eneo linalozunguka skuli.

Amesema maendeleo ya elimu hayawezi kupatikana bila ya mashirikiano ya wanajamii na kuwasihi wanaNungwi kushikamana katika kuwasomesha vijana wao.

Aidha Waziri huyo wa Elimu amezitaka skuli zote nchini kuimba wimbo wa sisi sote wakati wa paredi  kama ilivyokuwa zamani na kusisitiza kuwa skuli itakayoshindwa kutii amri hiyo itachukuliwa hatua. 

  Makamo wa pili wa rais Balozi Seif Ali Iddi akiweka jiwe la msingi la ukumbi wa kufanyia mitihani ikiwa ni kumbukumbu ya Skuli ya Nungwi kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake. Makamo wa Pili alikuwa mwalimu Mkuu wa kwanza kusomesha skuli hiyo
 Kikundi cha Sarakasi cha vijana wa Nungwi kikitoa burudani kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa
 wanafunzi wa Nungwi waliofurika kusherehekea miaka 50 ya skuli yao tangu kuanzishwa

REPOA YAWASILISHA MATOKEO YA UTAFITI KUHUSU UGATUAJI WA MADARAKA TANZANIA.

$
0
0
Taasisi ya utafiti ya REPOA, imezindua Ripoti ya Utafiti Kuhusu Ugatuaji wa Madaraka kwa Wananchi  (Understanding Decentralization and Devolution in Tanzania) Katika Warsha iliyowakutanisha Wasomi na Wadau mbalimbali wa maendeleo Mkoani Dodoma.
​Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo (MB) akitoa Hotuba ya Ufunguzi wa warsha ya uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Kuhusu Ugatuaji wa Madaraka kwa Wananchi  (Understanding Decentralization and Devolution in Tanzania) .Warsha iliyowakutanisha Wasomi na Wadau mbalimbali wa maendeleo Mkoani Dodoma.
Baadhi ya wadau walioshiriki katika warsha ya uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Kuhusu Ugatuaji wa Madaraka kwa Wananchi  (Understanding Decentralization and Devolution in Tanzania) Mkoani Dodoma.
 ​Mkurugenzi wa Repoa  Dk. Donald Mmari Akifungua Warsha mkoani Dodoma iliyowahusisha wadau mbalimbali.
​Picha ya Pamoja ya Washiriki wa Warsha hiyo pamoja na Mgeni rasmi mkoani Dodoma.
Mwakilishi Kutoka Taasisi ya Utafiti ya KIPPRA ya Nchini Kenya, akielezea Jinsi Kenya inavyogatua Madaraka kwa Umma.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA WAKUU WA MIKOA INAYOLIMA PAMBA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa 10 inayolima pamba nchini wasimamie zao hilo kwa karibu ili kuinua uzalishaji wake na kuwaongezea kipato wananchi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Ijumaa, Septemba 8, 2017) wakati akizungumza na wakuu hao wa mikoa kwenye kikao alichokitiisha mjini Dodoma kujadili mbinu za kufufua zao hilo. Wakuu wa mikoa walioitwa kwenye kikao hicho ni kutoka mikoa ya Shinyanga, Singida, Kagera, Tabora, Morogoro, Mara, Mwanza, Simiyu, Katavi na Geita.

“Serikali imeamua kufufua mazao makuu matano ya biashara ambayo ni pamba, chai, kahawa, korosho na tumbaku na leo nimetaka nianze na ninyi wakuu wa mikoa ili mwende mkawasimamie watu wenu tunapokaribia kuanza msimu mpya,” alisema.

Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kusimamia kilimo cha pamba kuanzia maandalizi ya shamba, kupanda, matumizi ya pembejeo na dawa, kuvuna na kutafuta masoko na akawataka wasimamie katika maeneo yao ili kilimo cha zao hilo kiweze kubadilika.

“Kuna maafisa kilimo kwa kila Halmashauri iliyoko kwenye mikoa yenu. Maafisa kilimo hawa lazima wahusike kikamilifu. Moja ya majukumu yake kwa cheo chake, kazi kubwa aliyonayo ni kusimamia zao la pamba. Kama hajafanya kazi hiyo, usiridhike kuwa na afisa kilimo wa aina hiyo,” alisema.

“Ni lazima kila mmoja awe na mpango kazi, ausimamie na atoe matokeo ya kuwa zao hili limefanikiwa katika eneo lake. Tunataka zao hili lichukue nafasi yake ya namba moja. Heshima ya “Dhahabu Nyeupe” lazima irudi lakini pia ni vema mkumbuke kuwa zao la pamba ni uchumi, zao la pamba ni siasa katika mikoa yenu,” alisisitiza. 

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba; Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI; Bw. Suleiman Jafo, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Kilimo, Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Dkt. Tito Haule na Mkurugenzi Msaidizi wa Uhamasishaji Mazao, Bw. Beatus Malema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
40480 DODOMA, 

JUMAMOSI, SEPTEMBA 9, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakuu wa Mikoa inayolima zao la pamba nchini kwenye makazi yake mjini Dodoma Septemba 9, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba, watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo na wanne kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KENYA NA TANZANIA ZAONDOLEANA VIKWAZO VYA KIBIASHARA

$
0
0
Katibu Mkuu wa biashara na uwekezaji nchini Tanzania, Adolph Mkenda akizungumza wakati wa majadiliano ya kibiashara kati ya Tanzania na Kenya na kuondoa vikwazo vilivyopo vya kibiashara kati ya nchi hizi mbili. Majadiliano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Biashara wa Kenya, Dr Chris Kiptoo akizungumza makubaliano waliyokubaliana kati ya Kenya na Tanzania kuhusiana kuondoa vikwazo vilivyopo katika biashara ya nchi mbili.
Katibu Mkuu wa biashara wa Kenya, Dr Chris Kiptoo akimkabidhi repoti za kibiashara za nchini kwenya Katibu Mkuu wa biashara na uwekezaji nchini Tanzania, Adolph Mkendajijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kuondoa vikwazo vilivyopo vya kibiashara.
kibiashara
 Baadhi ya Wadau wa Biashara kutoka Tanzania na Kenya wakiwa katika mkutano wa majadiliano ya kuondoa vikwazo vya kibiashara kati ya nchi hizi mbili.
 Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. Pindi Chana akizungumza na wadau wa biashara kati ya Kenya na Tanzania jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Nchi za Tanzania na Kenya zimetimiza agizo la maraisi wake na kukubaliana kuondoa vikwazo vya biashara katika bidhaa za unga wa ngano na gesi ya kupikia kutoka Kenya na zile za Maziwa na Sigara kutoka Tanzania.
Aidha masuala mengine 15 kutoka Tanzania na 16 ya Kenya bado yako mezani na majadiliano yanaendelea.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakati wa kuhitimisha mazungumzo ya kibishara baina ya nchi hizo ya Siku mbili, Katibu Mkuu wa biashara na uwekezaji nchini Tanzania Adolph Mkenda amesema wamefikia makubaliano hayo ya kibiashara ili kuhakikisha wanatimiza matakwa ya viongozi  wakuu, Rais John Pombe Magufuli na Uhuru Kenyata, yaliyoyowataka wafanye kazi na kuondoa vikwazo vya  biashara mara moja katika nchi hizoi mbili kubwa ndani ya jimuiya ya Africa Mashariki,

Amesema, baada ya maagizo yao, kwa kushirikia na Katibu Mkuu wa biashara wa Kenya, Dr Chris Kiptoo walianza kuwasiliana kwa karibu ambapo kwa kuanzia walifanya mkutano katika mpaka wa Namanga kuangalia biashara inavyokwenda na vikwazo vilivyopo katika nchi hizo ambavyo vilitatuliwa baada ya kupitia masuala mbali mbali,

 Aidha amesema kupitia majadiliano hayo, wameweza kupatia ufumbuzi mambo mengi ikiwemo biashara ya ngano, ambapo amesema wamekubaliana kifungua biashara ya ngano katika nchi hizi na kuhahakikisha wanaiboresha zaidi ikiwamo kutoa kipaumbele kwa wakulima wa zao hilo.

"Tulipata fursa ya kukaa na wadau wa biashara ya unga na ngano yenyewe kutoka nchi hizi mbili, wakiwemo wadau wenye viwanda vya kusaga ngano, wakulima na maafisa wa wizara za kilimo kutoka nchi zote ambao tumekubakiana kufungua biashara ya unga wa ngano kati ya Kenya na Tanzania, na sasa hivi unga wa ngano unapita unavuka mpaka bila vikwazo vyovyote." Amesema Mkenda

Kenya sasa hivi inazalisha ngano nyingi kuliko Tanzania na Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuzalisha ngano kuliko Kenya hivyo tukiunganisha biashara na uwezeshaji,ngano ya Kenya itaongezeka na maeneo mengi Tanzania ambayo yanauwezo wa kuzalisha ngano yataongeza uzalishaji wa ngano

Aidha alisema wamekubaliana na wenye viwanda waanze kutumia ngano za kutoka nchini kabla kuagiza kutoka nje ya nchi hizi mbili na waonyeshe nia nzuri ya kujenga ushirikiano Wa jumuiya hii ya Africa Mashariki..

Kwa upande wake, katibu Mkuu Wa Kenya, Dr Chris's Kaptoo amesema, Kenya imewekeza zaidi dola bilioni moja na nusu nchini Tanzania kwa ajili ya masuala mbali mbali ya kibiashara na viwanda ambapo watu zaidi ya elfu 50 wameajiriwa.

 Ameogeza katika kuendeleza biashara katika nchi hizi mbili, watatumia Uchumi na Nakumati supermarket na kuhakikisha zinafanya kazi inavyopaswa na wale wanaopeleka bidhaa zao wanalipwa kwa wakati.
"Tunafanya bidii kuona Uchumi Supermarket inaimarika, tunataka matawi yake yote yaliyokuwepo Tanzania yanaendelea kama yalivyokuwa awali na pia wale wote watakao kuwa wanapeleka bidhaa zao huko wanalipwa kwa wakati" amesema Dr Kiptoo"

Amesema, siyo wajibu wake yeye katibu kuingilia biashara za watu binafsi kama Nakumat na Uchumi lakini kwa umuhimu wa biashara wanaingilia kati kuhakikisha iko salama na inatimiza matakwa ya nchi.

GREEN BIRD SECOMDARY SCHOO IN MWANGA, KILIMANJARO REGION

MAHAFALI YA 44 YA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI YA WATOTO WENYE ULEMAVU YA JESHI LA WAOKOVU JIJINI DAR ES SALAM LEO.

$
0
0
VIFIJO na ndelemo vilivyochangamana na majozi kwa wanafunzi wanaohitimu masomo ya shule ya msingi 2017 katika shule ya watoto wenye ulemavu ya Jeshi la Wokovu jijini Dar es Salaam leo.

Furaha iliyoje kwa watoto waliohitimu masomo ya msingi na majozi kwa waliobakia, ikiwa risala ya wahitimu imetoa changamoto mbalimbali kwa watoto wenye ulemavu ikiwemo vifaa visaidizi kwa watoto hao pamoja na mafuta ya kupaka kwa watoto wenye ulemvu wa ngozi(Albino).

Akizungumza katika mahafali hayo jijini Dar es Salaam leo, Mwalimu wa Michezo katika shule ya Msingi Jeshi la Wokovu, Emmanuel Ibrahim ameiomba serikali kuwaruhusu watoto hao wenye ulemavu na wanavipaji mbalimbali washiriki mashindano ya Kitaifa pamoja na ya kimataifa kama watoto wengine.

Pia wameomba kuongezewa Madaktari watakaotoa huduma ya afya kwa watoto hao wenye ulemavu ilikukidhi mahitaji ya watoto wenyeulemavu shuleni hapo.
Mkurugenzi wa shule ya msingi ya Jeshi la wokovu iliyopo Tameke jijini Dar es Salaam, Luteni Thomas Sinana akisoma risala ya shule hiyo kwa mgeni rasmi na kutaja changamoto mbalimbali zinazoikabiri shule hiyo inayohudumia watoto walemavu katika hafla ya mahafali ya wanafunzi wanao hitimu masomo yao ya shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo.
Watoto wenye ulemavu wakitoa burudani mbele ya Mgeni rasmi pamoja na wazazi wa watoto hao waliohudhuria katika mahafali ya wanafunzi wa Darsa la saba 2017 jijini Dar es Salaam leo.
wahitimu wa shule ya msingi Jeshi la Wokovu na Watoto wenye ulemavu tofauti tofauti wakitumbuiza ngojera mbele ya mgeni rasmi zilizokuwa na mahusia mazuri kwa wazazi wenye watoto wenye ulemavu pamoja na kuwashuru walezi na walimu wao kwa kuwalea tangu walipokuwa Darsa la kwanza mapaka sasa wanahitimu masomo yao ya shule ya msingi.
 Wahitimu wa Shule ya Msingi Jeshi la wokovu wakimsiliziza mgeni rasmi jijini Dar es Salaam leo wakati wa mahafali ya kuwaaga.
Picha zote na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

TANZIA: KAMISHNA MSTAAFU WA OPERESHENI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KUAGWA KESHO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini – Thobias Andengenye, ataongoza Maafisa na Askari katika zoezi la kuuaga mwili wa Marehemu na kutoa heshima za mwisho (Kwa Paredi Maalum), kwa aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CF (OPS) Rogatius Peter Kipali, ambaye alifariki dunia Semptemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake Mombasa, Ukonga Jijini Dar es Salaam.

Zoezi la kuuaga mwili wa Marehemu litafanyika kesho Semptemba 10, 2017 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika viwanja vya Kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala eneo la (FIRE) Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anapenda kuvitaarifu Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Maafisa, Askari na Watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, , familia ya Marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine kujitokeza kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho.


IFUATAYO NI RATIBA NZIMA YA MSIBA

Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe

Amina.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.



WANANCHI WAENDELEA KUMIMINIKA KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA KUPIMA AFYA

$
0
0
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt.Grace Magembe akitoa maelekezo kwa wananchi waliofika katika upimaji wa afya kwenye  viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.
 Wazazi na walezi wakiendelea kumiminika kusajili watoto wao na bima ya afya ya Toto Afya Kadi  kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni kampeni ya Afya Mkoa wa DSM. Pichani watumishi wa NHIF wakiendelea na uandikishaji .
 Maafisa wa NHIF wakitoa maelekezo kwa wazazi namna ya kujaza fomu za bima ya Toto Afya Kadi, leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Masoko wa Tanga Fresh Ltd, Ally Sechonge akigawa maziwa kwa wananchi  waliofika katika upimaji wa afya ndani ya viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.


Sehemu ya wananchi waliofika katika upimaji wa afya ndani ya viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

MAKONDA AWEKA JIWE MSINGI LAUJENZI WA VIWANDA VIDOGO VIDOGO KATIKA KARAKANA YA JIJI LA DAR ES SALAAM.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezitaka Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam zitengeneze mazingira rafiki kwa wajasiriamali wadogo ili kuwawezesha na fursa mbalimbali za biashara . 

Makonda ameyasema hayo leo wakati wa kuweka jiwe la msingi katika uzinduzi wa viwanda vidogovidogo katika Karakana ya Jiji iliyopo Mwananyamala Jijini Dar es Salaam, amesema kuweka mazingira rafiki ya viwanda kutasaidia wajasiriamali kujitokeza na kuyatumia na nchi kuweza kupata maendeleo pamoja na kukuza uchumi wa kufikia uchumi wa kati. 

"Niwapongeze kwa kazi mnayoifanya kwa manispaa lakini pia kuunga mkono jitihada za wajasiriamali kwa kuwapa mikopo kupitia vikundi vyao na nitoe wito pia kwa watendaji msitoe mikopo holela itakuwa kazi kuzirejesha" Amesema RC Makonda. 

Aidha amesema kuwa Halmashauri ya Jiji imejenga mazingira rafiki kwa kuanza kutoa Ruzuku kwa manispaa ambapo ilikuwa hafanyi hivyo katika miaka iliyopopita.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,Sipora ya Liana amesema kuwa kupitia mradi huo Jiji la Dar es Salaam limeendelea kutoa kipaumbele kwa wanawake, vijana na walemavu wanaopata mikopo kutoka Halmashauri ya Jiji kwa kuona mazingira wanayofanyia kazi sio rafiki na wanahangaika sana kupata masoko.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es`Salaam Paul Makonda akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa viwanda vidogo vidogo katika karakana ya jiji la Dar es Salaam iliyopo Mwananyamala leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya majengo ya mradi wa viwanda vidogo vidogo katika karakana ya jiji iliyopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China ,Dk. Lu Youqing akipiga mpira katika uwanja bandari wakati makabidhiano ya uwanja huo na Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda. 
Monekano wa Uwanja wa Bandari uliokarabatiwa na Ubalozi wa China leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

RC MASENZA: MARUFUKU WENYEVITI WA MITAA NA VIJIJI KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA ARDHI

$
0
0

Na Fredy Mgunda, Iringa

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametaka wenyeviti wa vijiji au wa mitaa kutojihusisha na uuzaji wa ardhi ili kuondoa migogoro ambayo imekuwa ikisababishwa na viongozi hao.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa Mafinga, Masenza alisema kuwa kumekuwa na migogoro ambayo inasababishwa na wenyeviti wa serkali za vijiji au mtaa hivyo ni marufuku viongozi hao kujihusisha na swala hilo.

“Sipendi kusikia mwenyekiti wa mtaa au mwenyekiti wa kijiji akihusisha kuwa shahidi wa uuzwaji wa ardhi kwa kuwa hilo sio jukumu lao waichie mamlaka ya ardhi kufanya kazi kwa utaalamu wao”alisema Masenza

Aidha Masenza alimtaka wakurugenzi wote wa mkoa wa iringa kuwaambia ukweli viongozi juu ya sheria ya uuzaji wa ardhi ili kuondoa migogoro inayosababisha maumivu kwa upande unaonewa na kudhurumiwa haki yao ya msingi na kusababisha kumrudisha nyuma kimaendeleo.

“Wakurugenzi waambieni vijana wetu waache ujanja ujanja wa kupokea,kuchora,kuonyesha na kuelekeza swala lolote linalohusu uuzwaji wa ardhi ili hii mipango kabambe ya halmashuri ziende vizuri kama serikali inavyopanga”alisema Masenza

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza na wadau mbalimbali wa wilaya ya mufindi wakati wa kutambulisha mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa Mafinga uliokuwa na lengo la kuonyesha dira ya miaka ya hamsini (50) ya maendeleo ya mji wa Mafinga ambapo inasemeka ni moja kati ya miji inayokuwa kwa kasi .

hawa ni baadhi ya wadau waliojitokeza katika ukumbu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya mufindi kushuhudia utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa mafinga.

SHAKA AMTEMBELEA WAZIRI MKUU MSTAAFU JOHN MALECELA NYUMBANI KWAKE MJINI DODOMA.

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akizungumza na Kaimu Katibu wa umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka (kushoto) wakati alipomtembelea, nyumbani kwake mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akimwonyesha kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka kinyango chenye uzito wa tani 1 wakati alipomtembelea, nyumbani kwake mjini Dodoma
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akimwelezea kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka picha iliochorwa na Mwanafinzi wa darasa la saba Mwaka 1982 wakati wa hali ngumu ya uchumi nchini.
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akimwelezea kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka picha iliyochorwa na mjuu wake ikimuonesha yeye na Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

CHINA KUONGEZA NGUVU ZOEZI LA UPIMAJI AFYA BURE DSM

$
0
0
Balozi wa Jamhuri ya watu wa China anaemaliza Muda wake nchini amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo zoezi la upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Dar es Salaam limeingia siku ya Nne.

Mhe Balozi wa China akiwa ameambatana na Maofisa wa Ubalozi huo hapa nchini Ameshangazwa na UBUNIFU wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda wa kuwasaidia wananchi wengi wa Mkoa kwa WAKATI MMOJA hususani ni wenye vipato vya Chini ambao idadi kubwa hawawezi kumudu Gharama za matibabu nje ya mifumo rasmi iliyowekwa na Serikali mfano wa Bima ya Afya.

Kutokana na Mkusanyiko huo wa Maelfu ya wananchi Mhe Balozi wa China amesema Serikali ya Jamhuri ya watu wa China imeamua KUUNGA mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda na kuanzia sasa na kuendelea serikali ya ya Jamhuri ya watu wa China itaungana na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam katika kusaidia zoezi upimaji Afya BURE kwa kufanya yafuatayo :-
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akiongeza na Balozi wa China Nchini Tanzania Dr.Lu Youqing na ujumbe wake katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo zoezi la upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Dar es Salaam limeingia siku ya Nne. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akizunguza na wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmooja kwa ajili ya kupima afya.



MAGAZETI YA NDANI NA NJE YA TANZANIA LEO SEPT 9, 2017

BODI YA CHAKULA DAWA NA VIPODOZI YAANGAMIZA CHAKULA AINA YA SOSEJI ZILIZOKWISHA MUDA WAKE KIBELE WILAYA YA KUSINI UNGUJA.

$
0
0
Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi wakiteremsha boksi za Chakula aina ya Soseji zilizokwisha muda wake kwa ajili ya kuangamizwa baada ya kugundulika katika Ghala la chakula linalomilikiwa na Kampuni ya Best Inmport Maruhubi na wakaguzi ,Kibele Wilaya ya Kusini Unguja.
Chakula aina ya Soseji zilizokwisha muda wake zikiwa zimekusanya kwa ajili ya kuangamizwa baada ya kugundulika katika Ghala la chakula linalomilikiwa na Kampuni ya Best Inmport Maruhubi na wakaguzi ,Kibele Wilaya ya Kusini Unguja.
Mkuu wa kitengo cha Ufatiliaji madhara ya Chakula Aisha Suleiman akizungumza na Waandishi wa Habari katika zoezi la kuangamiza Chakula aina ya Soseji zilizokwisha muda wake na kwamba hazifai kutumiwa na maisha ya Binaadamu ,Kibele Wilaya ya Kusini Unguja.
Mkaguzi wa Chakula Bi Amina Ramadhan Salim akizungumza na Waandishi wa Habari katika zoezi la kuangamiza Chakula aina ya Soseji zilizokwisha muda wake na kwamba hazifai kutumiwa na maisha ya Binaadamu ,Kibele Wilaya ya Kusini Unguja.
Chakula aina ya Soseji zilizokwisha muda wake zikisangwa na baadae kufukiwa baada ya kugundulika kua hazifai kutumiwa na maisha ya Binaadamu ,Kibele Wilaya ya Kusini Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Wanachama TEN/MET watoa hoja nzito kwa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii

$
0
0
MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) umekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na kuwasilisha hoja mbalimbali za kufanyiwa kazi na Serikali kupitia sekta ya elimu lengo likiwa ni kuhakikisha elimu bora inapatikana nchini Tanzania.

Akiwasilisha hoja hizo mahususi 14 mjini Dodoma, Mwanachama wa TEN/MET toka taasisi ya FAWETZ, Bi. Neema Katundu alisema hii ni mara ya pili kuwasilisha hoja na lengo la msingi ni kuitaka serikali kuingiza katika utekelezaji.

Bi. Katundu alisema wanaikumbusha Serikali kuhakikisha inatenga hadi asilimia 20 ya bajeti ya taifa kwenye sekta ya elimu na pia kuwekeza zaidi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato na matumizi mabaya ya fedha toka mapato ya ndani ili iweze kutumika uboreshaji elimu ya msingi nchini.

Alisema hoja zingine walizowasilisha Serikalini ni pamoja na kutaka utoaji wa ruzuku shuleni hali halisi ya mahitaji ya sasa na kuhakikisha mchakato wa kuanzishwa kwa Bodi ya Taaluma ya uwalimu itakayoongeza tija na kulinda maslahi ya walimu katika sekta hiyo.

Aidha, hoja zingine walizowasilisha kwa kamati hiyo ni kutaka kuimarishwa kwa idara ya kudhibiti ubora (ukaguzi) na ipewe mamlaka na vitendea kazi kiuhalisia ili iweze kufanya kazi yake kiufasaha, uzingatiwaji wa haki za watoto na pia kuundwa kwa chombo maalumu cha usimamizi, utungaji na utekelezaji wa sera ya elimu.
Mwanachama wa TEN/MET toka taasisi ya FAWETZ, Bi. Neema Katundu (kulia) akiwasilisha hoja mbalimbali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii jana mjini Dodoma juu ya maboresho katika sekta ya elimu. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba (kushoto) na katibu wake kulia wakizungumza na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) jana mjini Dodoma.
 
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii ikiwa katika kikao na Wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET).

RC TABORA ANZENI MAPEMA KUWAANDA WAKULIMA WA PAMBA ILI TUPATE MAVUNO MAZURI.

$
0
0

Na Tiganya Vincent- RS-Tabora

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeawaagiza Maafisa Ugani kuanza mapema maandalizi ya kilimo cha pamba kwa wakulima kutoka wilaya tano mkoani hapo zilichaguliwa kulima zao ili waweze kuzalisha pamba nyingi na nzuri kwa ajili viwanda mbalimbali hapa nchini.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri jana wilayani Igunga wakati alipokwenda kujionea hali halisi ya Kiwanda cha Pamba cha Manonga wilayani Igunga ambacho kimekuwa hakifanyi kazi kwa miaka zaidi ya 20 kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa pamba ya kutosha.

Alisema kuwa watendaji wote wanaohusika na usimamizi wa zao la pamba ni vema wakahakikisha kuwa wakulima wanapanda mbegu zinazotakiwa na kwa nafasi inayoshauri kitaalamu na kutimia mbolea na dawa za kuua wadudu zinazotakiwa.

Mwanri alisema kuwa Tabora imepata mbegu bora tani 500 ambazo zitasaidia kusambazwa katika Wilaya ambazo zimechaguliwa kulima zao la Pamba za Kaliua, Urambo, Nzega, Igunga na Uyui.

Alisisitiza pamba itakayolimwa na kuvuna itauzwa kupitia Vyama vya Ushirika na sio vinginevyo ili kuepuka mkulima kunyonywa.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alipiga marufuku matumizi ya mbegu ambazo hazikuidhinishwa na Bodi ya Pamba na kuingiza mkoani hapa dawa ambazo zimepitwa na wakati.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye shati jeupe ) akiongozana na viongozi mbalimbali kukagua mitambo ya Kiwanda cha Pamba cha Manonga jana wilayani Igunga kwa ajili ya kujionea hali halisi kilivyo hivi na mahitaji yake ili kianze upya uzalishaji.


MWANRI ATOA MWEZI MMOJA KWA WAMILIKI WA KIWANDA CHA MANOGA KUHAKIKISHA KINAANZA KAZI.

$
0
0
Na Tiganya Vincent-RS-Tabora.

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imetoa mwezi mmoja kwa wamiliki wa Kiwanda cha Pamba cha Manonga kuhakikisha wamekikarabati ili kiweze kuanza tena uzalishaji wa mafuta ya pamba na uchambuzi wa Pamba na kutengeneza ajira kwa vijana mkoani hapo.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri jana wilayani Igunga wakati alipokwenda kujionea hali halisi ya kiwanda hicho ambacho kwa maika zaidi ya 20 hakifanyi kazi.

Alisema kuwa baada mwezi mmoja huo kukamilika atafanya ziara Kiwandani hapo ili kuhakikisha kama ukarabati umeshakamilika na mitambo imeshaanza kufanya kazi na kinyume cha hapo atalazimika kumwandikia Waziri wenye dhamana na viwanda ili wamiliki wake wanyang’anye kwa ajili ya kumpa mwekezaji mwingine.

Mwanri aliwaagiza Wamiliki wa Kiwanda hicho ambao ni Rajani pamoja na Chama Kikuu cha Ushirika cha Igembensabo kupanga ratiba ya mpango kazi wa utekelezaji shughuli zitakazoonyesha mipango ya ufufuaji na muda wa ukamilishaji kwa ajili kufanikisha zoezi hilo ndani ya muda ulipangwa , vinginevyo watashindwa.
Baadhi ya mitambo ya Kiwanda cha Pamba cha Manonga wilayani Igunga ambayo ilikuwa ikutumika kuchambua Pamba na kuzalisha mafuta yake ambayo hafanyi kazi kwa kipindi kirefu baada ya wamiliki wake kusimamisha uzalishaji. Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri( hayupo katika picha) jana ametoa mwezi mmoja mitambo hiyo ianze kufanya kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (aliye mbele) akiangalia mmoja wa mitambo baaya kutembelea Kiwanda cha Pamba cha Manonga jana wilayani Igunga kwa ajili ya kujionea hali halisi kilivyo hivi na mahitaji yake ili kianze upya uzalishaji.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU) Robert Mayongela Jongera (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo (kulia) baada viongozi mbalimbali kutembelea Kiwanda cha Pamba cha Manonga jana wilayani Igunga kwa ajili ya kujionea hali halisi kilivyo hivi na mahitaji yake ili kianze upya uzalishaji.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia) akiwasisitiza wamiliki wa Kiwanda cha Pamba cha Manonga kilichopo wilayani Igunga kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja mitambo ya kiwanda hicho iwe imeshaanza kazi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo. Mkuu wa Mkoa alitoa maelezo hayo jana alikwenda kutafuta sababu za kwanini hakiendelei na uzalishaji kwa zaidi ya miaka 20.



Breaking nyuzzzz.......: Rais Dkt. Magufuli amteua Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma

UFUNGUZI WA UCHUNGUZI WA KINYWA NA MENO WAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0

Na Khadija Khamis –Maelezo

Jamii inatakiwa kuweka utaratibu wa kupima afya ikiwemo afya ya kinywa na meno ili kupatiwa uchunguzi wa awali pamoja na elimu sahihi ya afya angalau mara mbili kwa mwaka .

Hayo aliyaeleza na Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Dr Fadhil Mo’hd Abdalla huko katika Kituo cha Afya Rahaleo, wakati akifungua zoezi la uchunguzi wa afya ya kinywa na meno linaloendeshwa na Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno kutoka Tanzania .

Alisema afya hiyo ni muhimu kufanyika awali kabla ya madhara, kwa kupatiwa ushauri wa mapema kabla ya athari kujitokeza na kusababishwa kupoteza meno .Alifahamisha kuwa katika miaka ya nyuma elimu ya afya ya kinywa na meno zilikuwa zikitolewa katika maskuli ,wataalamu hutoa elimu kwa wanafunzi pamoja na kung’oa meno kwa wale ambao meno yao yameadhirika .

Aidha alisema mpango huo wa uimarishaji afya ya jamii iko haja kurejea utaratibu wa kizamani , wataalamu wa afya ya kinywa na meno kutoa huduma za matibabu katika maeneo mbali mbali ikiwemo maeneo ya maskuli na vijijini .

“Huu usiwe mwanzo wa kuonyesha njia kwa jamii na wala msisubiri kuumwa kila muda mujiwekee utaratibu wa kujichunguza afya zenu ikiwemo afya ya kinywa na meno pamoja na maradhi yasioambukiza ili muweze kupata ushauri mapema kwa Madaktari ,”alisema Mkurugenzi Kinga.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dokt,Lorna Carneiro kulia akitoa hotuba ya makaribisho katikaUfunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.

Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil Abdalla akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil Abdalla katikati akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari kutoka Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).pamoja na madaktari wa Zanzibar katika Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images