Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1904 | 1905 | (Page 1906) | 1907 | 1908 | .... | 3286 | newer

  0 0


  Na Mathias Canal, Dar es salaam

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu leo Septemba 10, 2017 amefanya kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani ili kuwaeleza dhamira ya kuanzishwa kwake ikiwa ni pamoja na kukuza ufanisi na kiwango cha ufaulu katika Wilaya hiyo.

  Katika kikao hicho wadau wamechangia jumla ya shilingi milioni 3,900,000 ikiwa ni ahadi, Mifuko 100 ya saruji na rasilimali hamasa kwa vijana wa waliohitimu masomo ya sayansi katika vyuo mbalimbali nchini watakaojitolea kufundisha katika shule zenye upungufu wa walimu sayansi katika Wilaya ya Ikungi.

  Mhe Mtaturu amewaeleza washiriki wa kikao hicho namna ambavyo Uongozi wa Wilaya umejipanga kwa kuhusisha michango ya wadau na nguvu za wananchi kwa ujumla kwa kuchangia rasilimali fedha ama viwezeshi kama vile saruji, mchanga, kokoto na vitu vifaa vingine vya ujenzi.

  Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Lamada Hotel Jijini Dar es salaam akiwa ameambatana na Mwalimu Athumani Salum ambaye ni Afisa elimu Sekondari wa Wilaya ya Ikungi, Mhe Mtaturu alisema kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu Wilayani Ikungi ikiwa ni pamoja na Upungufu wa nyumba za walimu, Vyumba vya madarasa, Ofisi za walimu, Maabara, Thamani mbalimbali, Matundu ya vyoo vya walimu na wanafunzi.
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
  Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi ambaye pia ni Afisa elimu Mkoa wa Dar es salam Mwalimu Khamis Lissu akichangia namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
  Wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam.


  0 0

  Uzalendo limekuwa neno kuu katika siku za karibuni. Na wengi wetu tunatafsiri kama ni kuipenda na kuiweka Nchi yako mbele. Lakini sifa nyingine muhimu sana ya uzalendo ni kujitolea kwa faida au maendeleo ya wengi.
  Salasala Vision Group ( SVG) iliasisiwa miaka 5 iliyopita na wakazi wachache wa Salasala Kilimahewa lengo likiwa ni kisaidia masuala ya ulinzi, mazingira, miundombinu, michezo na kuchochea maendeleo ya wanachama wake.
  Hadi leo SVG imepanda miti zaidi ya 10,000, imetengeneza barabara za mitaa pamoja na kurekebisha barabara kuu, imetoa msaada vitendea kazi kwa polisi, kutengeneza viwanja vya michezo na pia kununua aridhi kwa wanachama wake zaidi ya hekari 250 huko Bagamoyo.
  Wiki hii kwa mwaliko wa Spika wa Bunge SVG imetembelea Bungeni na kisha kucheza mechi na timu ya Bunge na kuibuka na ushindi wa bao 2 - 1.

  0 0

  Na Faustine Ruta, Bukoba.

  Timu ya soka ya Kagera sugar imelazimisha sare ya kufungana bao 1 kwa 1 na timu ya soka ya Ruvu shooting katika mzunguko wa Ligi kuu Vodacom Tanzania bara ikiwa ni mzunguko wa kwanza tangu ligi imeanza mwezi uliopita mchezo ambao umepigwa katika uwanja wa nyumbani wa Kaitaba Bukoba Mjini.

  Ligi kuu Vodacom Tanzania bara timu ya kagera sugar kwa mara ya kwanza katika mzunguko huo ulioanza August 26 kagera sugar ilifungwa na Mbao Fc ya Jijini Mwanza bao 1 kwa 0 huku Ruvu shooting  ikifungua Dimba vibaya kwa kupigwa na timu ya Simba Sc bao 7 kwa 0 ambapo timu zote mpaka sasa  zina Alama sawa ya  moja moja.

  Katika mchezo huo ulichezeshwa na mwamuzi Shomari Lawi ulianza kwa saa kumi za jioni huku wachezaji wa kagera sugar wakianza mchezo huo wakiwa wamepoa na timu ya ruvu shutingi wakianza kwa mashambulizi makali dhidi ya Kagera Sugar

  Ruvu shooting walikuwa wa kwanza kwa kufungua lango la timu ya kagera sugar kwa kujipatia goli la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wa timu hiyo Ishara Juma dakika 16.

  Licha ya timu ya Ruvu shooting kuwa wa kwanza kupata bao 1 kipindi cha kwanza pia ilikuwa ya kwanza mchezaji wake namba 13 George Wawa kupewa kadi nyekundu muda mfupi baada ya kumfanyia rafu mbaya Mchezaji wa Kagera Sugar V. Ludovick aliyeingia kipindi cha pili cha mchezo huo. 


  Dakika ya 75 kagera sugar wamepata fursa ya kusawazisha kupitia kwa mchezaji huyo huyo  Venance Ludovick na mtanange kumalizika kwa kwa sare ya bao 1-1. 
  Kipindi cha pili Kagera Sugar waliliandama mara kwa mara Lango la Timu ya Ruvu Shooting na huku Ruvu wakiwa pungufu 10 uwanjani.

  Patashika kwenye lango la Timu ya Ruvu Shooting.
  Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar kilichoanza leo dhidi ya Timu ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba leo hii kwenye Mchezo  wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara.
  Kikosi cha Timu ya Ruvu Shooting kilichoanza leo dhidi ya Timu ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba leo hii kwenye Mchezo wa pili wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Na Ramadhani Ali – Maelezo 

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendeleza dhamira yake ya kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya afya kwa kuimaisha huduma za afya na kujenga vituo vyenye hadhi vijijini.Dhamira hiyo inaendelea kutekelezwa kwa pamoja na wafadhili wa maendeleo wanaunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika kufikiaq malengo hayo.

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo ameeleza hayo alipotembelea vituo vitatu vipya vya afya vya Kiboje, Kijini Matemwe na Chaani kubwa na kituo cha Uroa kinachofanyiwa ukarabati mkubwa.Amesema serikali ya Uholanzi kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia mradi wa Orio hivi sasa unaendelea na ujenzi wa vituo 15 vya afya nane vikiwa vinajengwa Unguja.

  Waziri Mahmoud aliwaeleza wananachi wa sehemu hizo kuwa lengo la kujengwa vituo hivyo nikuwasogezea huduma za afya karibu na sehemu wanazoishi na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali kuu za mijin.Amewahakikishia wananchi kuwa vituo vinavyojengwa kupitia mradi wa Urio vitakapomalizika vitakuwa na vifaa vya kisasa na vitatoa huduma zote muhimu zikiwemo wodi za kujifungulia.

  Aliongeza kuwa Wizaara ya Afya inajiandaa kuhakikisha kuwa vituo vyote vinavyojengwa vinakuwa na wafanyakazi wa fani zote muhiumu ili kuwapunguzia shida.“Wananchi wa Kijini kituo chenu ambacho ni cha daraja la pili kitakapomalizika kitatoa huduma zote muhimu na wagonjwa watatoka mjini kuja kutafuta matibabu hapa,”Waziri aliwahakikishia.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Rans Nassor Salim Khamis inayojenga vituo 15 vya afya vya Mradi wa Orio alipotembelea kituo cha Kiboje wa pili (kulia) Meneja Ujenzi wa Kampuni ya Rans Ali Nassor.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitembelea ujenzi wa kituo kipya cha afya Kiboje akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kati Mashavu Sukwa (kushoto) meneja wa Ujenzi wa Kampuni ya Rans Ali Nassor.
  Meneja wa Ujenzi wa Kampuni ya Rans Ali Nassor akimpa maelezo Waziri wa Afya juu ya ukarabati wa kituo cha afya cha Uroa alipofanya ziara ya kutembelea vituo vya Mradi wa Orio.
  Muonekano wa kituo kipya cha afya cha Kijini Matemwe kinachojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Uholanzi kupitia Mradi wa Orio.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kijini Matemwe baadaya kuangalia maendelea ya ujenzi wa kituo kipya cha afya cha kijiji hicho.


  0 0

  UONGOZI WA TAASISI YA NORDIC FOUNDATION TANZANIA UNAPENDA KUWAJULISHA WATANZANIA NA UMMA AMBAO WENGI WAMESHIRIKI NA WANAENDELEA KUSHIRIKI KAMPENI YA AFYABANDO KWA KUCHEZA BAHATI NASIBU YA KIJAMII KUPATA KADI YA BIMA BURE KUWA DROO YA KWANZA ITAFANYIKA JUMAPILI WIKI IJAYO NA KURUSHWA KUPITIA VITUO VYA T.V   VYA EAST AFRICAN TELEVISION NA STAR T.V MUDA WA SAA MOJA NA NUSU USIKU (7.30PM). 
  BAADA YA HAPO KILA JUMAPILI KUTAKUWA NA DROO KWA KIPINDI CHOTE CHA KAMPENI. KADI ZA BIMA KUMI NA ZAIDI KUTOLEWA BURE KILA WIKI HIVYO KUFANYA WASHINDI KUWA WENGI.

  HIVYO BASI, KUSHIRIKI BAHATI NASIBU HII YA KIJAMII YENYE WASHINDI WENGI, TUMA TSHS 500/= KUPITIA MIAMALA YA TIGO PESA, MPESA NA AIRTEL MONEY NAMBA YA KAMPUNI NI 406044 NA KUMBUKUMBU NAMBA NI 1234 UPATE BIMA YA AFYA. USIDHARAU UWEZO WA JERO KATIKA KULINDA AFYA YAKO.  KUMBUKA SIKU YA DROO NI KILA JUMAPILI SAA MOJA NA NUSU USIKU, EAST AFRICAN T.V NA STAR T.V .


  IMETOLEWA NA

  Ms. MWASITI  ISSA


  AFISA UHUSIANO WA NORDIC FOUNDATION TANZANIA


  0 0

  VIONGOZI wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wameishukuru serikali kwa kukarabati sekondari ya Mpwapwa ambayo majengo yake yalikuwa yana hali mbaya.

  Viongozi hao wametoa shukrani hiyo mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua ukarabati wa shule hiyo.Shule hiyo ni miongoni mwa shule 88 kongwe zinazokarabatiwa na serikali ambapo katika awamu ya kwanza ukarabati umeanza kwa shule 43.

  Katika shule hiyo, Serikali imefanikiwa kujenga bweni moja jipya la wasichana, ukarabati wa mabweni 12 ya wavulana, ukarabati wa vyumba vya madarasa 22, bwalo la chakuka pamoja na jiko, maktaba, maabara tatu, ofisi za walimu, mfumo wa maji na umeme ambapo jumla ya sh.bilioni 1.2 zimetumika.

  Akizungumza na viongozi katika ziara yake,Naibu Waziri Jafo ameipongeza Kamati ya ujenzi kwa kufanyakazi bila kuchoka na kufanikisha kuibadili kabisa shule hiyo ambayo kwasasa imegeuka kuwa shule bora ya kisasa tofauti na ilivyokuwa awali.

  Naibu Waziri Jafo amewataka wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii kwani serikali ya Dk. John Magufuli imeamua kuboresha miundombinu pamoja na vifaa vya kutolea elimu kwa lengo la kufanikisha elimu bora hapa nchini.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua majengo yaliyo karabatiwa na serikali katika sekondari ya mpwapwa.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua jiko la kisasa linalo jengwa.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na wanafunzi wa Mpwapwa sekondari.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Kamati ya ujenzi wa Mpwapwa sekondari.
  Baadhi ya madarasa ya Mpwapwa sekondari yaliyo karabatiwa.

  0 0

  Baadhi ya wanafamilia wa Africans Rising wakizungumza na wanahabari baada ya kukamilisha mafunzo na kubadilishana uwezo ya mwezi mmoja yaliyofanyika mkoani Arusha -MS TCDC. Toka kushoto ni M'bongo Ali toka Burundi, Amina Teraz toka Morocco, katikati ni kiongozi wa harakati Mr Muhammed Lamin Saidykhan toka Ghambia ambaye kwa sasa anaishi Senegal, Julie  toka Liberia, Mr Omboki Otieno toka Kenya..

  0 0

  Serikali imetakiwa kuweka mkakati wa kuzilinda, kutunza na kuhifadhi barabara zote zinazojengwa kwa kiwango cha lami nchini ili kuziwezesha kudumu kwa muda uliokusudiwa na hivyo kuepuka gharama za ukarabati wa mara kwa mara.

  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu mheshimiwa Moshi Suleman Kakoso amesema hayo mara baada ya kukagua barabara ya Dodoma – Babati yenye urefu wa kilomita 263, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika.

  “Hakikisheni ujenzi wa barabara unaendana na uboreshaji wa huduma na maisha ya wananchi sehemu ambapo barabara hizo zinapita ili kuchochea maendeleo”, amesema mheshimiwa Kakoso.

  Makamu mwenyekiti huyo amesema Kamati yake imeridhishwa na hatua zilizofikiwa za ujenzi wa barabara Dodoma –Babati KM na daraja la Kelema linalounganisha Wilaya za Chemba na Kondoa ambalo litawezesha barabara hiyo kupitika kwa uhakika wakati wote.

  “Nimefurahishwa na taarifa aliyoitoa Meneja mradi wa barabara hii kwamba pamoja na kujenga barabara pia mkandarasi amechimba visima vya maji katika maeneo haya kwa ajili ya kusaidia wananchi jambo ambalo ni jema na la kuigwa na makandarasi wengine”, amesisitiza Makamu Mwenyekiti Kakoso.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga, akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu hatua zinazochukuliwa katika ulindaji wa miundombinu ya barabara wakati walipokagua barabara ya Dodoma – Mayamaya iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma.
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Moshi Kakoso akitoa maoni kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga, juu ya ulindaji wa miundombinu na kuzingatia usalama wa mazingira wakati walipokagua barabara ya Dodoma – Mayamaya iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga, (watatu kushoto), akiwaonesha kingo za barabara baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati walipokagua barabara ya Dodoma – Mayamaya iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma.


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakitoka kukagua daraja la Kelema linalounganisha Wilaya ya Chemba na Kondoa, mkoani Dodoma. Daraja hilo limekamilika kwa asilimia 98.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa wadau wa Mafuta na Gesi ambapo wadau wa Gesi na Mafuta watapata nafasi ya kujadili Fursa zilizopo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt. Medard Kalemani wakati wa  mkutano wa siku mbili wa wadau wa Mafuta na Gesi uliofanyika kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa msaada wa sh. milioni 10 ili kumuwezesha Bw. Ernest Masenga kutatua changamoto zinazomkabili. Masenga alikuwa msanii wa muziki wa dansi ambaye sasa anasumbuliwa na maradhi ya miguu. Pia makazi anayoishi si salama yanahitaji kukarabatiwa.

  Waziri Mkuu ametoa msaada huo leo (Jumatatu, Septemba 11, 2017) katika makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar Es Salaam. Ametoa msaada huo baada ya kuguswa na hali ya maisha ya msanii huyo aliyemuona kupitia kipindi maalumu kilichoonyeshwa na TBC Septemba, 5, 2017. Kipindi hicho kiliongozwa na Godfrey Nago.

  “Nawaomba Watanzania wenzangu tumsaidie mwezetu ili aweze kuishi vizuri kwa sababu sanaa yake imesaidia katika kuelimisha na kuburudisha umma .”

  Kwa upande wake Nago ambaye amepokea msaada huo kwa niaba ya Masenga amesema atahakikisha anasimamia vizuri fedha hizo ili zitumike kama ilivyokusudiwa.

  Pia Nago amesema anamshukuru Waziri Mkuu kwa kuwaunga mkono na kutoa msaada huo kwa sababu ameonesha kwamba Serikali inawajali wananchi wake na TBC itaendelea kuwaomba wadau mbalimbali wajitokeze na kumsaidia msanii huyo.

  Naye Mjomba wa msanii huyo, Kanuti Mloka ambaye ameiwakilisha familia amemshukuru Waziri Mkuu kwa msaada huo kwa kuwa familia imeshindwa kumsaidia Bw. Masenga kutokana hali duni ya maisha waliyonayo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhi msaada wa sh. milioni 10 kwa Meneja wa TBC 2, Godfrey Nago ili kumsaidia Msanii wa muziki wa dansi, Ernest Masenga.  Nago amepokea kwa niaba ya msanii huyo. Kushoto ni mjomba wa msanii huyo, Kanuti Mloka. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Septemba 11/2017 katika ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es salaam.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania
  Miongoni mwa majengo yake mengi yakiwa yamejengwa mnamo karne ya 18 na 19, Mji Mkongwe wa Zanzibar bado haujapoteza taswira yake halisi mpaka hivi leo. Na kutokana na muonekano huo, kutembea na kuvinjari mitaa na majengo mbalimbali kunakufanya ujihisi kama kweli ulikuwepo kipindi cha nyuma pindi inajengwa.
  Kati ya majengo maarufu ambayo Jumia Travel inakuhakikishia utayaona pindi utakapoingia kwenye mji huu ni pamoja na Ngome Kongwe iliyojengwa kwenye eneo la mwanzo la Kanisa la Wareno; nyumba ya maajabu; kasri kubwa iliyojengwa na Sultan Barghash; zahanati ya kale; Kanisa Kuu Katoliki la Mtakatifu Joseph; Kanisa Kuu la Kristu la Waanglikana likiwa limejengwa kukumbuka kazi ya David Livingstone katika kukomesha biashara ya utumwa na kujengwa eneo lilipo kuwepo soko la watumwa; makazi ya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa watumwa Tippu Tip; Msikiti wa Malindi Bamnara; jengo la Jamat Khan lililojengwa kwa ajili ya dhehebu la Ismailia; eneo la makaburi ya Kifalme; na mabafu ya Kiajemi.
  Kwa pamoja, mitaa na barabara nyembamba zikiwa na kona nyingi, na majengo makubwa yanayotazamana na bahari ndyo yanaufanya mji huu kuwa wa kipekee ukiakisi shughuli za muda mrefu za kibiashara kati ya Waafrika na Waarabu. Kwa ujumla, Mji Mkongwe unatambulika kama sehemu ambayo hatimaye biashara ya utumwa ilikomeshwa.

  Kutokana na upekee na umaarufu wake mamia ya maelfu ya watalii kutoka kona mbalimbali za dunia husafiri kuja kujionea vivutio vya kila aina vinavyopatikana kwenye mji huu mkongwe wa Zanzibar.

  Kwa ufupi takribani kila kitu ndani ya Mji Mkongwe kina historia ya kuvutia na kusisimua. Kuanzia mila na tamaduni za watu wake, shughuli wanazozifanya, vyakula vyao na majengo ni utalii tosha ambao hauwezi kupatikana sehemu yoyote duniani.
  Huchukua muda wa saa moja na nusu kusafiri kwa kutumia boti kutoka Dar es Salaam mpaka kufika Zanzibar na usafiri huanzia saa moja asubuhi mpaka saa 12 za jioni. Hivyo basi kumbe inawezekana kwa mtu kutokea jijini Dar es Salaam akaenda kule, akatalii na kurudi siku hiyo hiyo. Na kama una mpango wa kuufaidi zaidi mji huo pia inawezekana kwani vyakula na malazi vya gharama nafuu kabisa ambayo kila mtu anaweza akamudu.
  Uzuri wa Mji Mkongwe ni kwamba ni rahisi kuuzunguka kwani mitaa yote inapitika kwa urahisi kabisa aidha kwa kutumia ramani ya karatasi au simu (google map) au muongozaji wa kitalii utayempata. Ni vizuri kuwa na muongozaji mzuri kama ni mara yako kwanza kufika kule ili iwe rahisi na pia kutembelea sehemu nyingi zaidi ambazo hauzifahamu.

  Kikubwa cha kushangaza zaidi ni namna majengo yalivyojengwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia vifaa mbalimbali kama vile chokaa, matumbawe na miti. Na cha kuvutia zaidi ni umri wa majengo hayo ambayo yamekuwepo karne na karne bila ya kupoteza uhalisia wake. Pongezi kubwa ziende kwa serikali na shirika la Umoja wa Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kuweka jitihada kubwa na sheria za kuulinda mjii huu. Kutokana na jitihada hizo mnamo mwaka 2000 UNESCO liliutangaza Mji Mkongwe wa Zanzibar kama eneo la urithi wa dunia. 
  Utakuwa haujaufaidi Mji Mkongwe endapo hautopata fursa ya kula vyakula mbalimbali (vya baharini) vinavyopatikana katika migahawa tofauti. Eneo maarufu ambalo unaweza kuvipata vyakula vya aina hiyo kwa pamoja ni kwenye bustani ya Forodhani. Litakuwa jambo la ajabu kama umefika Zanzibar na hukuenda kutembelea eneo hili. Umaarufu wa bustani ya Forodhani umetokana na mkusanyiko wake wa aina lukuki za vyakula vya baharini vinavyopatikana pale kila siku kuanzia jioni. Na ni eneo ambalo huwakutanisha watu kutokea sehemu mbalimbali za visiwa vya Zanzibar, hivyo inawezekana kukutana na watu ambao mlikuwa mkipishana mchana kutwa.

  Kutembelea, kuogelea na kutazama jua likizama kwenye fukwe ya bahari ya Hindi ukiwa Zanzibar nazo ni miongoni mwa shughuli ambazo watalii wengi hufurahia. Baadhi ya hoteli ambazo ukiwa kwenye Mji Mkongwe unaweza kuyafanya hayo ni kama vile Mizingani Seafront Hotel, Africa House Hotel na Seyyida Hotel & Spa.
  Kwa kumbukumbu zako itakuwa ni vema zaidi ukibeba kamera kwa ajili ya kupiga picha matukio mbalimbali unayoyaona njiani. Kwa majengo inakuwa ni rahisi zaidi ila kwa watu itakuwa ni busara ukaomba ruhusa ili kuepuka matatizo kwani sio wote watakuwa tayari kufanya hivyo. Zanzibar ni kubwa na ina maeneo mengi ya kutembelea ila kwa leo Jumia Travel inaamini angalau utakuwa umeipata picha ya Mji Mkongwe wa Zanzibar na shughuli za kufanya na kufurahia ukiwa kule.

  0 0  Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mhongo wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu wa kwanza kushoto, Makamu Mwenyekiti Charles Ngereza wa tatu kutoka kushoto na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu Bw. Mourice wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa APC 2017 uliofanyika ukumbi wa KKK Karatu.(Picha na PamelaMollel Arusha).
  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa APC wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mhongo(hayuko pichani),
  Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mhongo akielekea kupiga picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kufungua mkutano mkuu wa APC 2017 katika ukumbi wa KKKT Lutherani Karatu 


  0 0

   Mhifadhi katika hifadhi ya Taifa ya Tarangire Beatrice Ntambi akizungumza na waandishi wa chama cha waandishi mkoani Arusha(APC)waliokwenda kutembelea  hifadhi hiyo kwa lengo la kujifunza na kutangaza utalii wa ndani
   Sehemu ya waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini
   Picha ikionesha fuvu la mnyama aina ya Tembo
   Sehemu ya makundi makubwa ya tembo wanaopatikana katika hifadhi ya Taifa ya Tarangire
   Twiga wakionekana vizuri katika hifadhi ya Tarangire
   Tembo wakizunguka ndani ya hifadhi ya Tarangire.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Chama cha Wanayansi wa Elimu Bahari ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi (WIOMSA) kwa ushirikiano kati ya WIOMSA, Taasisi ya Sayansi Bahari (IMS) na Idara ya Sayansi Akua na Teknolojia ya Uvuvi (DASF) zote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) na Mkataba wa Kimataifa wa Uhifadhi, Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na ya Ukanda wa Pwani wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi (Mkataba wa Nairobi), kinaandaa Kongamano la 10 la Kisayansi. 

  Kongamano hilo litafanyika kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi tarehe 4 Novemba katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere ulioko Dar es Salaam, Tanzania.


  Katika Kongamano hili la 10 kutakuwa na mashindano ya kazi za sanaa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za mikoa ya ukanda wa pwani wa Bahari ya Hindi. Kwa upande wa Tanzania Bara itahusisha mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara na kwa Zanzibar itahusisha shule zilizopo Unguja na Pemba. Dhamira ya mashindano hayo ni: “Umuhimu wa Mazingira ya Pwani na Bahari kwa Tanzania”. 

  Bahari ni muhimu sana kwa jamii zetu na kwa ustawi wa maisha yako. Kwa hiyo tumia mawazo yako, ubunifu wako na maarifa uliyo nayo katika kuwasaidia wengine waelewe mawazo yako kuhusiana na umuhimu wa mazingira ya ukanda wa pwani na ya bahari kupitia kazi yako ya sanaa. Chora, paka rangi, tumia program za kompyuta za uchoraji au eleza mawazo yako hayo kwa kutunga wimbo.

  Wanafunzi watumie ubunifu wao wenyewe kueleza maoni yao juu ya dhamira husika. Uwasilishaji wa ubunifu huo unaweza kufanyika kwa njia zifuatazo: michoro (zikiwemo katuni/vibonzo) au utunzi wa nyimbo.


  Kazi zote za sanaa ziwasilishwe kabla ya tarehe 30 Septemba 2017 kwa njia ya mtandao ambao ni http://symposium.wiomsa.org/art-competition/


  Kwa maelezo zaidi juu ya vigezo na masharti ya kushiriki na mfumo wa uwasilishaji wa sanaa, pakua tangazo kamili la shindano hili kwa kubofya link hii chini:

  0 0

   .Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Mkonda (kulia)akikagua eneo  lililotengwa kwa ajili ya kuuza magari (Show Room) kwa jiji Dar es Salaam   lililopo Kigamboni-Kisarawe leo jiijini Dar es Salaam, ambapo show room  zilizo katika sehemu mbalimbali zinatakiwa kwenda katika eneo hilo na hawatalipa kodi ya maeneo hayo ndani ya miaka mitatu.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Mkonda akizungumza mara ya baada ya kukagua eneo la lililotengwa kwa ajili kuuzia magari Kigamboni –Kisarawe jijini Dar es Salaam.
  Muonekano wa eneo hilo lililotengwa kwa ajili kuuzia magari Kigamboni –Kisarawe jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasunga (CCM)

  Serikali imesema kuwa kushuka au kupanda kwa thamani ya shilingi nchini hakusababishwi na bidhaa na huduma mbalimbali kutozwa kwa dola bali kunatokana na misingi ya shughuli mbalimbali za kiuchumi (Macroeconomic fundamentals) pamoja na hali halisi ya uchumi wa nchi zinazofanya biashara na Tanzania. 

  Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasunga (CCM), aliyetaka kujua mikakati ya Serikali katika kuimarisha thamani ya shilingi ya Tanzania na kupiga marufuku matumizi ya fedha za kigeni nchini. 

  Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji aliainisha kuwa nakisi ya urari wa biashara, mfumuko wa bei na tofauti ya misimu (seasonal factors) ni sababu kuu zinazosababisha kushuka na kupanda kwa thamani ya shilingi nchini.
  Dkt. Kijaji aliliambia Bunge kuwa ili kuimarisha thamani ya shilingi Benki Kuu inaendelea kuthibiti mfumuko wa bei ili usitofautiane sana na wabia wa biashara nchini. 

  “Benki Kuu imethibiti biashara ya maoteo (speculation) katika soko la fedha za kigeni ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa miamala ya fedha za kigeni inafanywa na benki kwa ajili ya shughuli za kiuchumi tu na sio biashara ya maoteo, hali hii itasaidia upatikanaji wa fedha za kigeni katika soko la rejareja ili kupunguza shinikizo la kuporomoka kwa thamani ya shilingi.”Alisema Dkt Kijaji. 

  Dkt. Kijaji alifafanua kuwa pamoja na hatua zinazochukuliwa na Benki Kuu ufumbuzi wa kudumu wa kutengamaa kwa thamani ya shilingi nchini hutegemea zaidi kupungua kwa nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho wa mali nchi za nje. 
  Imetolewa na: 

  Benny Mwaipaja
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Fedha na Mipango
  11/9/2017

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimwangalia Profesa Ibrahim Hamis Juma akitia sahihi hati ya kiapo baada ya kumuapisha kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka sahihi hati ya kiapo baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai, Profesa Ibrahim Hamis Juma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba kabudi na Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman katika picha ya kumbukumbu baada ya Rais kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai, Profesa Ibrahim Hamis Juma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba kabudi na Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman katika picha ya kumbukumbu na Majaji wa Mahakama ya Rufaa na wa Mahakama kuu baada ya Rais kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017.
  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mbunge wa kawe,Halima Mdee, Mbunge jimbo Bunda, Ester Bulaya na Msaanii Wa bongo Movie,Wema Sepetu wakiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam leo. Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya walikuwa wametoka kusomewa mashtaka yanayowakabili, huku Wema Sepetu akiwa amewasili kwa ajili ya kusikiliza kesi yake.

  0 0

  Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (The United Nations Capital Development Fund-UNCDF), ikishirikiana na kampuni ya Ensol Tanzania Ltd. (Ensol) wamezindua mfumo wa umeme wa nishati ya jua katika kijiji cha Mpale kilichopo wilaya ya Korogwe, na hivyo kuwezesha umeme katika eneo hilo kwa mara ya kwanza. 

  Mradi huo ulizinduliwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dk. Juliana Pallangyo ambaye aliipongeza kampuni ya Ensol na washirika wake ikiwemo UNCDF kwa juhudi zake kubwa za ushawishi wa umeme hasa umeme mbadala wa jua ili kuboresha ustawi wa jamii na kukuza uchumi wa mtu binafsi na taifa. 

  Dk. Pallangyo alisema kwamba serikali ya Tanzania inawashukuru watu wa Ensol kwa juhudi zao kubwa za kupeleka umeme vijijini. Alisema kwa Ensol kuweza kufikisha umeme katika maeneo ya ndani kabisa ya kijiji cha Mpale, kuwaunganisha wananchi na umeme wa saa 24 na wamefanikiwa kubadili maisha ya wananchi hao.  Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhandishi Robert Gabriel (kushoto) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt Juliana Pallangyo kuzindua rasmi mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga.

   Alitoa wito kwa jumuiya hiyo kutumia umeme sio kwa kuwasha taa pekee bali pia katika kusukuma mbele kazi za uzalishaji. Dk. Pallangyo alifurahishwa na kituo cha afya Mpale kuunganishwa na mfumo wa nishati ya jua na kuwataka maofisa wa wilaya kulipa Ankara zao kwa wakati ili kuhakikisha kwamba huduma zinapatikana bila kukoma kwa wananchi. 

  Kijiji cha Mpale kipo katika maeneo ya milimani katika kata ya Mpale wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. Kijiji chenye wakazi 9000 na nyumba 730, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1972 hakijawahi kuwa na umeme. Wengi wa wanavijiji walikuwa wakitegemea mno mafuta ya taa ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa si masafi kwa ajili ya kuwashia taa zao.  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana Pallangyo akitoa nasaha wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga. Kulshoto ni Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (UNCDF), Peter Malika.

  Mpaka sasa Ensol imeshaunganisha umeme kwa kaya 50. Aidha mpango unafanyika wa kutanua mradi ili ifikapo Juni 2018 nyumbna 250 ziwe zimeunganishwa. Mreadi huo wa kuunganisha wanakijiji na nishati inayozalishwa kwa nguvu za jua ulianza mwaka 2014 wakati Ensol walipozuru vijiji kadhaa vya mkoa wa Tanga kuangalia uwezekano wa kupata kijiji cha mfano na kubaini kuwapo kwa kijiji cha Mpale. 

  “Ushirikiano wa UNCDF ulikuwa muhimu katika mradi huu gridi ndogo ya nishati ya jua. Pamoja na kwamba tulipokea fedha kutoka UNCDF na wadau wengine, UNCDF imekuwa ndio chombo cha kuingiza masuala ya kitaalamu na ushauri mwingine. Kushirikiana na UNCDF kumeongeza kuaminika miongoni mwa wadau na taasisi za kifedha,” anasema Prosper Magali, Meneja wa mradi wa Mpale. Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (UNCDF) nchini, Peter Malika akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale, wilayani Korogwe mkoa wa Tanga.

  Bw. Magali aliongeza, "Ninaamini kama si msaada wa UNCDF huu mradi usingekuwepo hapa ulipo. Tumepokea fedha kutoka EEP na wafadhili wengine. Lakini ni kwa sababu ya UNCDF tumeweza kupata fedha kutoka katika taasisi nyingine za ufadhili". Mkuu wa UNCDF Tanzania, Peter Malika alisema kwamba umeme ni chanzo cha maendeleo na kwamba sekta binafsi ina nafasi ya kusaidia serikali katika juhudi zake za kuangaza maeneo ya vijijini. 


older | 1 | .... | 1904 | 1905 | (Page 1906) | 1907 | 1908 | .... | 3286 | newer