Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1902 | 1903 | (Page 1904) | 1905 | 1906 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa New Life In Christ Mkoani Kilimanjaro, Bi. Elly Makyao (kulia) akikabidhi misaada ya kibinadamu ya Wafungwa waliopo Magerezani nchini kwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa. Hafla fupi ya Makabidhiano ya Misaada hiyo imefanyika leo Septemba 08, 2017 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga – Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba fupi wakati wa hafla ya kupokea misaada ya kibinadamu kwa Wafungwa waliopo Magerezani iliyotolewa na Asasi ya "New Life In Christ" leo Septemba 08, 2017 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga - Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akiwakabidhi cheti cha shukrani Viongozi wa Asasi ya "New Life In Christ" kwa kutambua mchango wao kwa niaba ya Jeshi la Magereza Tanzania na Serikali kwa ujumla.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akimsukuma askari ambaye ameketi kwenye Baiskeli Maalum ya kubebea wagonjwa wasiojiweza ambayo ni miogoni mwa vifaa mbalimbali vilivyotolewa kama msaada kwa Jeshi la Magereza na Asasi ya "New Life In Christ"(kushoto) ni Mkurugenzi wa Doricas Aide International anayeshughulikia Miradi ya Afya katika nchi za Africa, Bi. Mirjam Verwij.


  0 0

  Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma

  Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa leseni kwa vituo 32 vya televisheni hapa nchini ikiwa ni kuongeza muonekano na usiku katika maeneo mbalimbali  ya nchi.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Martin Alexander Mtonda Msuha Mbunge wa Mbinga Vijijini ambapo alitaka kujua idadi ya vituo vinavyorusha matangazo kwa njia ya televisheni na Makampuni yanayomiliki vituo hivyo.

  Aliongeza kwa kuvitaja vituo hivyo vya Televisheni vilivyosajiliwa nchini kuwa ni pamoja na Independent Television (ITV), Star Television Channel Ten Television, TBC 1, TBC 2, East Africa Television (EATV), Agape Television (ATV), C2C Television, Dar es Salaam Television (DTV), Abood Television, CTN Television, Capital Television, Clouds TV, VIASAT 1 Television, Sibuka Television, Sokoine University of Agriculture Television (SUATV) na Tumaini Television.

  Vituo vingine ni Mlimani Television, Tanga City Council Television, Imaan Television, Morning Star TV, Africa Internet Television Ltd, Uhai Television Limited, Barmedas TV, Target Television, Tabibu Television, Africa Swahili Television, Cable and Satellite Consultancy Limited, WRM Television Network, Dira Television, Parliament Media Trust (Bunge TV), Mahaasin Television.

  Aidha alifafanua kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) ndio yenye dhamana ya kutoa leseni ya maudhui ya utangazaji wa Televisheni za aina mbili ambazo ni Leseni za maudhui yanayotazamwa bila kulipia na maudhui ya Kulipia. Alizidi kueleza kuwa leseni hizo zimegawanywa kimasoko ambapo kuna leseni za Kitaifa ambazo zinapaswa kuonekana nchi nzima na leseni za Kimkoa ambazo huruhusiwa kutangaza mikoa 10 ya Tanzania Bara, na leseni za kiwilaya ambazo huonekana Mkoa mmoja.

  Mgawanyo huu wa kimasoko unatoa fursa kwa waombaji kutangaza maeneo wanayochagua kutokana na uwezo wao wa kifedha na kiundeshaji ambapo maudhui hayo ya bila kulipia yanapaswa kuonekana kupitia visimbuzi vya Makampuni ya Agape Associates Limited, Basic Transmission Limited na Star Media (Tanzania) Limited. Visimbuzi hivyo ni TING, STARTIMES, DIGITEK na CONTINENTAL.

  Naibu Waziri Wambura amevitaja vituo vyenye leseni ya soko la Kitaifa kuwa ni TBC1, Channel Ten, East Africa Televisheni, Independent Televisheni, Star Televisheni, Clouds TV na Bunge TV wakati vituo vyenye soko la kimkoa ni TV Imaan, Agape TV (ATV) na TV1 na vituo vilivyobaki vina soko la kiwilaya.

  Aidha, Kituo cha TBC1 ambacho ni kituo cha Umma kinapatikana bila malipo ya mwezi kwenye ving’amuzi vyote vya miundombinu iliyosimikwa ardhini na vile vinavyotumia mitambo ya satelaiti kama vile Azam TV, DSTV na Zuku. Kituo cha TBC 1 kinalazimika kuonekana bila malipo kwa mujibu wa masharti ya leseni za makampuni ya miundombinu ya utangazaji ya ardhini (DTT) na Satellite (DTH).
                          
  Kuhusu muonekano na wa TBC1 maeneo yote nchini, Naibu Waziri Wambura amesema kuwa Serikali kupitia Bunge la Bajeti ya mwaka 2017/2018 imetenga jumla ya Sh. Bilioni 3 ambazo ni fedha za miradi ili kuboresha muonekano wa matangazo ya TBC1 nchi nzima.  

  0 0

  Hugoline Martin Mtambachuo jina maarufu kama DJ CHOKA anatarajia kuachia wimbo wake mpya alioupa jina la BILA SABABU ukiwa umefanyika pale Mbagala kwa Prod Dupy. DJ Choka amesema ameamua kuachia wimbo huo tarehe hiyo kwa sababu ni tarehe ya kumbukumbu yake ya kuzaliwa.

  Wimbo huu utakuwa wimbo wa kwanza kuutoa kwa mwaka huu 2017 toka ameinuka kutoka kitandani kwa kujiuguza ugonywa wa KIFUA KIKUU (TB) kwa takribani miezi 6 hadi 8. Wimbo wa mwisho kuuachia ulikuwa unaitwa NITALALA UZEENI ambapo aliuachia mwaka 2014 uliokuwa umewashirikisha wasanii kama COUNTRY BOY, YOUNG LUNYA, B GWAY na CLIMAX BIBO chini ya Prod Gard kutoka A.M Rec.

  Wasanii walioshirikishwa kwenye wimbo huu mpya amesema ni mapema kuwataja kwa sasa lakini wimbo ukitoka watajulikana, anaomba mashabiki kuupokea ujio huu mwingine mpya kutoka kwake pamoja na nyingine zitakazo kuja.

  0 0

  Balozi wa China aliyemaliza Muda wake nchi, Dk.Lu Youqing akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarsit Ndikilo wakati wa Mkuu wa Mkoa huyo na Viongozi wa Mkoa huo walivyokwenda kumuaga Balozi wa China aliyemaliza muda wake.  Balozi wa China aliyemaliza Muda wake nchi, Dk.Lu Youqing akipokea zawadi ya Cheti cha kutambua mchango wa serikali ya China kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo leo jijini Dar es Salaam.

  Balozi wa China aliyemaliza Muda wake nchi, Dk.Lu Youqing akipokea zawadi ya kinyago cha Twiga kutoka kwa Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega ikiwa ni kutambua mchango wa balozi huyo kwa wananchi wa Mkuranga kwa misaada mbalimbali.

  Balozi wa China aliyemaliza Muda wake nchi, Dk.Lu Youqing akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Pwani pamoja na watendaji wa Ubalozi huo leo jijini Dar es Salaam.(picha na Emmanel Massaka , Globu ya Jamii).

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Balozi wa China, Dk. Lu Youqing ametoa msaada wa mashine ya X-Ray katika Hospitali ya Wilaya Mkuranga iliyotokana na ombi la Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega.

  Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo , wakati walikwenda kumuaga Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing ambaye amemliza muda wake nchini.

  Katika mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Ndikilo Balozi huyo amemshukuru Rais Dk. John Pombe Magufuli katika ajenda ya Tanzania ya viwanda na maendeleo ya wananchi.

  Amesema kuwa maendeleo ya viwanda yataboresha hali ya uchumi wa nchi pamoja na wananchi kutokana na viwanda vitavyojengwa.

  Balozi huyo amewahakikishia viongozi wa Mkoa wa Pwani ataendelea kuwa ushirikiano na kuwaomba waendelee kuwasaidia wawekezaji mbalimbali wanaokwenda kuwekeza mkoa huo wasipate usumbufu na hivyo kuharakisha maendeleo ya wananchi.

  Aidha Dk. Lu ametoa shukurani katika ushirikiano wa miradi maendeleo ya Viwanda,afya,maji na Elimu.

  Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo na Mbunge wa Mkuranga na Abdallah Ulega leo kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wamemshukuru kwa ushirikiano mzuri Balozi wa China wa China aliyemaliza muda wake..

  Mkuu wa Mkoa wa Pwani na mbunge wa Mkuranga walimtakia Balozi wa China safari njema ya kurejea nyumbani na kumuomba akawe Balozi wa kuendelea kuitangaza Tanzania na Mkoa wa Pwani akiwa nchini mwao.

  Abdallah Ulega amesema katika maombi kwa Balozi huyo ni pamoja na kuwasaidia kufanya ukarabati hospitali ya wilaya Mkuranga.

  0 0

  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwajulisha wazee wote wa mkoa wa Dar-es-salaam Wilaya ya Ubungo kuwa zoezi la Usajili na Utambuzi lenye lengo la kuwapatia Vitambulisho vya Taifa linaendelea sambamba na zoezi la Usajili wa Kadi za Bima ya Afya kwa wazee chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. 
  Wahusika ni wazee wote wanaoishi Wilaya ya Ubungo. Unachotakiwa kufanya ni kuchukua na kujaza fomu ya maombi ya  Usajili. Fomu zinapatikana ofisi ya Mtaa unakoishi au Ofisi ya Kata. Unapojaza fomu ya maombi unatakiwa kuweka na nakala ya  viambatisho muhimu vinavyokutambulisha vile ulivyonavyo mathalani Kadi ya Kupigia kura, Barua ya Serikali ya Mtaa, vyeti vya shule na kisha fika na fomu yako ikiwa imejazwa pamoja na vivuli (photocopy) ya viambatisho hivyo kwenye kituo cha karibu kusajiliwa. 
  Unapofika kusajiliwa unashauriwa kwa ajili ya ubora wa picha kutovaa nguo nyeupe, kijivu, bluu, pinki, au rangi yoyote inayoshabihiana na nyeupe, nguo zenye nembo, kofia aina yeyote ama kupaka hina kwenye viganja vya mikononi. 
  Kwa kuanza wiki ijayo Ratiba ya Usajili itakuwa ni kama ifuatavyo:-


  Na

  KITUO CHA USAJILI

  MUDA

  TAREHE

  1.

  Kata ya  Makurumla


  Saa 3:00 – 11:00 jioni

  11/09/2017

  2.

  Kata ya Manzese


  Saa 3:00 – 11:00 jioni

  12/09/2017

  3.

  Kata ya Sinza

  Saa 3:00 – 11:00 jioni

  13/09/2017

  4.

  Kata ya Makuburi

  Saa 3:00 – 11:00 jioni

  14/09/2017


  Utaratibu wa Usajili katika Kata zingine tutaendelea kuwafahamisha. Kupata maelezo zaidi tafadhali wasiliana na mtendaji wako wa Mtaa au Mtendaji Kata. 
  Kwa taarifa zaidi kuhusu Vitambulisho vya Taifa tembelea Tovuti yetu www.nida.go.tz au ukurasa wetu wa facebook -nidatanzania au twitter @nidatanzania 
  Wazee jitokezeni kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa ili mtambulike na kupata huduma za kijamii kwa haraka na kwa uhakika zaidi.


  Limetolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)


  0 0

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda jana amekabidhi Pikipiki za Traffic 10, Computer 100 na Baiskel za kisasa 200 kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Jeshi la Polis Dar es Salaam na kulifanya kuwa la kisasa.

  Kupatikana kwa Vitendeakazi hivyo ni matokeo ya jitihada binafsi za RC Makonda kutafuta Wahisani.Makonda amesema amedhamiria kuleta Mapinduzi Makubwa kwa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na Vifaa vya kutosha ikiwemo Magari, Pikipiki za kawaida na zile za Traffic,Baiskeli za Doria,Silaha na Computer ilikuwafanya kufanya kazi katika Mazingira mazuri.
  Amesema amechoka kuona Askari wakipoteza Maisha wakitekeleza majukumu yao kwa kuvamiwa na Majambazi na kuporwa Silaha ndio maana anapambana kutafuta vitendeakazi ili Askari wake wajivunie kufanya kazi katika Mkoa wake.Aidha amesema Pikipiki za Traffic zitaenda kusaidia kwenye Misafara ya Viongozi, Misiba na kuwahisha wagonjwa Hospital.
  Kuhusu Computer 100 alizotoa amesema zitagawanywa kwenye Vituo vya Polisi 20 na kufungwa mfumo wa kisasa wa kupokea taarifa za Uhalifu, kubainisha maeneo yaliyoshamiri Uhalifu, kutambua wahalifu Sugu ambapo mfumo huo utatoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa,Kamanda wa Mkoa,Wilaya na Mkuu wa kituo ili kuwezesha Viongozi kufanya maamuzi.
  Amesema Baiskeli 200 alizozitoa zitaendelea kuimarisha Doria mitaani na kuongeza kuwa Baiskeli nyingine za kisasa 1,000 zipo Nchini China zikifanyiwa Maboresho ambapo zikikamilika zitakuja kuongeza nguvu kupambana na Uhalifu.Sanjari na hayo amesema Magari Mabovu 15 ya Polisi kati ya 26 yaliyopelekwa Kilimanjaro kufanyiwa marekebisho yamekamilika ambapo yatakuwa na Mwonekano wa kisasa kama ilivyo kwa Magari ya Jeshi ya UN.
  Pamoja na kuligusa Jeshi la Polisi kama Taasisi ameona pia aguse maisha ya Askari mmoja mmoja kwa kuwatafutia Mkopo wa Viwanja sababu gharama ya Viwanja ni kubwa hivyo kufanya Askari kushindwa kumudu gharama hali inayosababisha baadhi yao kustaafu wakiwa hawana makazi na kuishi kwa tabu.

  Viwanja hivyo vilikuwa vikiunzwa kwa Tsh 20,000/= kwa Square meter lakini RC Makonda amepambana hadi kufikia Tsh 5,000/= kwa Square Meter ambapo Askari watakuwa wakilipa mkopo huo kidogokidogo kwa muda wa Miaka Mitano na wataruhusiwa kujenga hata kama hawajamaliza mkopo wao.

  0 0

  Fuatulia matangazo ya moja kwa moja (Live!!!) Kutoka uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amefanya ziara ya kushtukiza, kufuatilia Almasi iliyokamatwa ikisafirishwa kwenda nje ya nchi. Fuatilia ili uone almasi iliyokamatwa na maelekezo ya Serikali. Matangazo haya yatarushwa moja kwa moja kupitia TBC1 na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz kuanzia saa 3:30 asubuhi hii ya tarehe 09 Septemba, 2017.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa vyerehani 25 kutoka katika Taasisi ya African Releaf Organization ya nchini Kuwait.

  Amepokea msaada huo leo (Ijumaa, Septemba 9, 2017) kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Ruangwa.

  Waziri Mkuu ameishukuru taasisi hiyo kwa msaada huo wa vyerehani ambavyo vitagawiwa kwenye vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wilayani Ruangwa.Amesema vyerehani hivyo vitawawezesha wajasiriamali wanaojishughulisha na ushonaji kupata vitendeakazi vitakavyotumika kama njia ya kujiongezea kipato.

  Waziri Mkuu amesema mbali na kutoa msaada huo wa vyerehani pia taasisi hiyo inajenga Zahanati katika kijiji cha Mbecha kata ya Nanganga wilayani Ruangwa.“Taasisi hii ni rafiki na Halmashauri yetu na Wanaruangwa wamefarijika kwa kupata zahanati na vyerehani vitakavyotumika kama njia ya kujiongezea kipato.”

  Awali, Mkurugenzi wa Miradi wa Taasisi ya African Releaf Organization, Bw. Khamis Mkanachi alishukuru kwa ushirikiano wanaoupa kutoka Halmashauri ya Ruangwa.Pia Bw. Mkanachi amesema taasisi yao itaendelea kuvisaidia vikundi mbalimbali vya ujasiriamali katika Halmashauri hiyo kwa lengo la kuvikwamua kiuchumi.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alimtembelea na kumpa pole mbunge wa jimbo la Newala Vijijini, Bw. Rashidi Akbar aliyelazwa katika Taasisi Moyo ya Jakaya Kikwete.Kwa upande wake Bw. Akbar alimshukuru Waziri Mkuu kwa kumtembelea hospitalini hapo na kwamba hali yake kwa sasa inaendelea vizuri ukilinganisha na alivyofikishwa.

  Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kumjulia hali Bw. Anzigar Kambanga ambaye ni mwananchi wa wilaya ya Ruangwa aliyelazwa katika Taasisi Moyo ya Jakaya Kikwete.

  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  IJUMAA, SEPTEMBA 9, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipeana mkono na mkurugenzi wa taasisi ya African Relief Organization, Wakati akipokea cherehani ikiwa ni sehemu ya vyerehani 25 vya msaada, zilizo tolewa kwa Wananchi wa Ruangwa kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Septemba 8, 2017, (kulia) ni Mratibu wa miradi wa African Relief Organization Bw. Khamis Mkanachi.

  0 0


  Na David John -Mwanza.

  KATIBU wa Chama cha Michezo wilaya ya Nyamagana Daddy Gilbert amewataka wanasiasa kuacha tabia ya kuitumia michezo pindi wanapotafuta nafasi za uongozi na wakishapata hawana habari.
  Amesema wanasiasa wengi wamekuwa wakitumia michezo kama tiketi yao ya kutaka uongozi na wakifanikiwa hawanahabari na michezo jambo ambalo halipendezi.

  Kiongozi huyo wa michezo ametoa dukuduku lake hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo walifika katika ofisi za chama cha soka wilaya hiyo kutaka kujua namna walivyojipanga kuendeleza michezo.
  Daddy amesema anakerwa na baadhi ya wanasiasa ambao wanatumia michezo kupata uongozi na pindi wanapofanikiwa hawajari tena.

  "unajuwa kama wenzetu wanasiasa wangekuwa wanatuunga mkono naamini hata kwa hapa Mwamza tungefika mbali ,lakini bahati mbaya wakishapata wanachokipata hawana muda tena na sisi". amesema Daddy.

  Pia bosi huyo wa chama wilaya ametoa rai kwa wananchi wa mkoa wa mwanza kujitokeza katika viwanja vya michezo hususani uwanja wa Nyamagana ambapo ligi ya Willya kutafuta timu zitakazo cheza ligi ngazi ya mkoa.

  "kama mmavyoona hapa kuna ligi ya Wilaya ambayo imeshirikisha timu 25 inaendelea lakini mwamko wa mashabiki Kama mnavyoona."amesema Daddy.
  Mwenyekiti wa Chama cha Soka wilaya ya  Nyamagana Daddy Girbat( kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwandishi wa Habari hizi David John leo mara baada ya kumtembelea ofisini kwake ulipo uwanja wa michezo wa Nyamagana. Mkoani mwanza


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza Mwananchi wa Wilaya ya Ruangwa Bw. Anzigar Kambanga, wakati alipoenda kumjulia hali katika Taasisi ya Jakaya Kikwete, iliyopo Muhimbili Septemba 8, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimjulia hali Mbunge wa Newala Vijijini, Razak Rashid Akbar, wakati alipoenda kumjulia hali katika Taasisi ya Jakaya Kikwete, iliyopo Muhimbili Septemba 9, 2017.

  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0
  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Tanzania Dr. Philip I Mpango akitowa maelezo na kuzungumza kuhusiana na mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kuufungua mkutano huo, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Kupiga vita Utakasishaji wa Fedha Haramu na ugaidi katika Nchi za Mashariki na Kusini Mwa Afrika uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar. na kuhudhuriwa na Mawaziri wa Fedha wa Nchi 18 za Mashariki na Kusini Mwa Afrika uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
  .
  Wajumbe wa Mkutano huo wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk/ Ali Mohamed Shein, wakati akifungua mkutano huo wa Mawaziri wa Fedha.
  Ujumbe wa Mawaziri wa Tanzania wakifuatlia Mkutaho huo wa ufunguzi wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein akihutubia. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Fedha wa Nchi za Mashariki na Kusini Mwa Afraka baada ya kuufungua mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Nchi hizo 18 uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar. 
  0 0

  Baada ya Msanii wa Bongo Fleva, Nasib Abdul (Diamond Platinumz) kumwimba Mzee Onyango kuwa zilipendwa sasa mzee huyo ameibuka na kukana kuwa yeye sio Zilipendwa.
  Hatimaye Mzee Onyango ambaye ni mwigizaji mkongwe nchini Tanzania amemjibu Diamond Platinumz kwa vitendo baada ya kuachia filamu yake mpya ya iitwayo BABU THE PERFECT MAN kupitia kampuni yake ya  ONYANGO PRODUCTION.
  "Nashangaa sana kusikia Diamond Platinumz kuimba kwamba mimi na Mzee Jangala zilipendwa, mtoto huyu amenikosea sana mimi bado napendwa na mashabiki zangu bado wanaamini kuwa nina uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi ya uigizaji bila tatizo lolote" alisema Mzee Onyango.


  0 0  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wanahabari baada ya kufanya  ziara ya kushtukiza, kufuatilia Almasi iliyokamatwa ikisafirishwa kwenda nje ya nchi huku ikiwa imethaminiwa chini ya kiwango katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Naibu Kamishna Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere na Kushoto kwake ni Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamini Mchwampaka Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano na kulia kabisa ni Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Bw. John Biswalo. Taarifa kamili kuwajia punde.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwasilisha maelezo ya Muswada wa Sheria ya Reli wa mwaka 2017 kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Rashid Chuachua.
  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwasilisha maelezo kuhusu Muswada waSheria ya Reli wa mwaka 2017 ambao umeshasomwa Bungeni kwa mara ya kwanza.

  0 0


  Na Ismail Ngayonga-MAELEZO-DAR ES SALAAM

  SERIKALI za Tanzania na Kenya zimekubaliana kwa pamoja kumaliza vikwazo vya kibiashara katika usafirishaji na uingizaji wa bidhaa katika mipaka baina ya nchi hizo mbili hatua inayokusudia kuimarisha ushirikiano wa biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo.

  Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara, Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji) Prof. Adolf Mkenda mara baaada ya kumalizika kwa mkutano wa pamoja yao ulioshirikisha Viongozi Waandamizi wa Serikali hizo, Wafanyabiashara na Wakulima kutoka Mataifa hayo.

  Anasema katika mkutano huo Serikali ya Tanzania iliwasilisha mapendekezo 15 kwa Serikali ya Kenya yanayopaswa kupatiwa ufumbuzi, ambapo kwa upande wa Kenya waliwasilisha mapendekezo 16 ambapo kwa kiasi kikubwa hoja hizo zimekubaliwa na kupatiwa majibu yake katika mkutano huo.

  Prof. Mkenda alisema kupatikana kwa mwafaka wa majadiliano hayo ni maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Mataifa hayo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa Tanzania na Uhurru Kenyatta wa Kenya kwa kuwa Viongozi hao wametaka suala hilo lipatiwe mwafaka wa haraka ili kuweza kuendeleza ushirikiano na uhusiano katika nyanja mbalimbali baina ya nchi hizo.
  Baadhi ya Maafisa Waandimizi wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za Kilimo kutoka wakulima kutoka Tanzania na Kenya wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizotolewa na Wenyeviti wa Mkutano huo uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo.
  Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Pindi Chana akitoa taarifa ya majadiliano ya mkutano baina ya Watendaji Wakuu wa Serikali ya Tanzania na Kenya uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika Mataifa. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam. Wengine katika Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Kenya Dkt. Chris Kiptoo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Baishara na Uwekezaji), Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Watendaji Wakuu wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika Mataifa hayo. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam. Wengine katika Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Kenya Dkt. Chris Kiptoo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Ushirikiano wa Kenya, Dkt. Chris Kiptoo akizungumza na Watendaji Wakuu wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika Mataifa hayo. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam. Wengine katika Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Kenya Dkt. Chris Kiptoo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Uwekezaji na Ushirikiano wa Kenya, Dkt. Chris Kiptoo na Mwenjeji wake Prof. Adolf Mkenda wakionyesha Sera ya Taifa ya Biashara ya Kenya wakati mkutano baina ya Watendaji Wakuu wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika Mataifa hayo uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA ELIPHACE MARWA-MAELEZO).

  0 0


  Kumekuwa na taarifa potofu katika mitandao ya kijamii kuwa wafuasi 11 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Ikungi walikamatwa kwa kosa la kuendesha michango kwa ajili ya Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu aliyejeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana. 
  Ukweli ni kwamba taarifa hizi ni potofu na zenye lengo la kuwafitinisha wana Ikungi na jimbo la Singida Mashariki kwa ujumla. Viongozi waliokamatwa na ambao baadaye walihojiwa na kuachiwa kwa dhamana hawakuwa wakiratibu michango yoyote bali walikutwa wakiandika mabango yenye uchochezi dhidi ya viongozi wa Serikali na wakitaka kuandamana bila kibali. 
  Wakati Mhe Lissu anaendelea kupatiwa matibabu nje ya nchi na Serikali ikiwa inalifuatilia jambo hili kwa karibu ili kuwachukulia hatua kali wote waliohusika, natoa rai kwa wana Ikungi kuwa ni vyema tukaungana badala ya kuingiza siasa na mihemko katika jambo hili kama Taifa lilivyoungana katika tatizo la Kibiti ambalo sasa limemalizika. 
  Aidha, kwa kuwa tayari viongozi wa kitaifa wa Chadema wameshatangaza utaratibu wa kuchangia, nawashauri viongozi wa chama hicho wilaya kutumia mkondo huo. Vile vile, kwa wadhifa wangu, nimeshamwagiza Mwenyekiti wa Halmashauri yetu ya Ikungi ili aitishe kikao cha madiwani wote kuweka utaratibu wa pamoja wa namna gani ya kuchangia matibabu ya mbunge wetu. 
  Nichukue fursa hii kumpa pole Mhe. Lissu na wananchi wenzangu wa Ikungi na mahsusi jimbo la Singida Mashariki kwa tukio hili baya. Serikali ya Wilaya inalaani vikali wote waliohusika katika tukio hili ambalo linakwenda tofauti na mila na desturi za Kitanzania.  
  Tunamwombea Mhe Lissu nafuu ya haraka ili aweze kurejea kwenye majukumu yake ya kuwatumikia wananchi.


  Imetolewa na: 
  Ndugu Miraji J. Mtaturu 

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi.


  0 0

  Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.

  Kituo cha radio cha Efm kimewatembelea wakati wa Kigamboni  pamoja na kufanya vipindi moja kwa moja kupitia radio hiyo na kusikiliza changamoto mbalimbali za wakazi na kuzifanyia utatuzi ukiwa pia lengo ni kuwa karibu na wasikilizaji wao.

  Tamasha hilo la  muziki Mnene Njendani limehudhuriwa na Mkuu wa wilaya Kigamboni Hashim Mgandilwa, Mkurugenzi Manispaa ya Kigamboni Stephen  Katemba wakiambatana na Mstahiki Meya wa Dar es Salaam Isaya Mwita ili kuweza kuongea na wananchi moja kwa moja kupitia Kituo cha radio cha Efm katika Viwanja vya Machava  Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

  Viongozi nao wa meweza kuzungumza na wakati wa Manispaa kisikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi nao wa Kigamboni waliojitokeza kwa wingi katika Viwanja hivyo.

  Vile vile pia kituo hicho kimelenga hasa kukuza vipaji chipikizi vya miziki maarufu kwa jina la  Singeli, kwa kufanya mashindano  na kwa atakae ibuka Kidedea kati ya washiriki nao atapata fursa ya  kurekodi kazi zake bure  kwa gharama za kituo hicho cha redio ya Efm.
   Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni  Hashim Mgandilwa(kushoto)  akisalimiana na Mstahiki Meya wa Dar es Salaam  Isaya Mwita(kulia)  katika tamasha hilo la Muziki  Mnene njendani lililokuwa linafanyika kwenye Viwanja vya Machava Kigamboni.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni,  Stephen Katemba akizungumza na wakazi wa Kigamboni katika kipindi cha Joto la  asubuhi ambacho kilirushwa moja kwa moja  kutoka  Viwanja vya Machavya wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
  Watangazaji wa kipindi cha joto  la asubuhi  wakiongozwa na Gerard Hando pamoja na Maulid Kitengewakirusha kipindi hicho  mubashara  kutoka katika Viwanja vya Machava Kigamboni.
   Watangazaji wa kipindi cha uhondo wakiongozwa na Dina Marius  wakirusha kipindi hicho  mubashara kutoka wiwanjani hapo sambamba na kutoa burudani kwa mashabiki wao waliojitokeza  kwa wingi katika Tamasha Njendani Viwanja vya Machava wilaya ya Kigamboni jijini Dar  es salaam.
   Mtangazaji wa kipindi cha Sport HQ, Tunnu Shenkome akizungumza na  mashabiki wa timu ya Yanga Fc, Simba Fc  pamoja na Azam Fc wakionyeshana tambo kila mmoja  akijinadi kuwa timu yake ndio itakayoibuka kidedea kunyakua  kombe hilo la VPL katika msimu huu.
   Msanii wa muziki wa Singeli,  Dogo Niga  akitoa burudani kabambe kwa wakazi wa Kigamboni katika tamasha la  Njendani lililofanyika kwenye Viwanja vya Machava Kigamboni.
  Mashabiki wa Efm watu wazima kwa watoto  walijitokeza kwa wingi kupata burudani pamoja na kuonana na Watangazaji mbalimbali  wa kipindi vya radio hiyo katika tamasha la  Njendani lililofanyika kwenye Viwanja vya Machava Kigamboni. (Picha na Na Agness Francis, Blogu ya Jamii)


older | 1 | .... | 1902 | 1903 | (Page 1904) | 1905 | 1906 | .... | 3285 | newer