Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Maparoko kutoka Wilayani Ruangwa wamtembelea Waziri Mkuu Kassim majaliwa

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maparoko kutoka Wilayani Ruangwa, wakati alipo waalika kwa ajili ya chakula cha usiku ku kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Septemba 08, 2017.  Viongozi hao walimtembelea na kumuaga wakiwa katika maandalizi ya kwenda hija nchini Israel, Jordan na Misri Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

MAGAZETI YA IJUMAA LEO SEPT 8,2017

MKUTANO WA 17 WA BARAZA LA MAWAZIRI UMOJA WA NCHI ZA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA KUHUSU UDHIBITI WA BIASHARA FEDHA HARAMU

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake ya  Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo  katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake ya  Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo  katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi (Picha na Ikulu)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali wajkati wimbo wa Taifa Ukipigwa katika  Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
 Washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,kutoka Nchini South Afrika wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TAARIFA KAMILI YA SPIKA KUHUSU KUSHAMBULIWA KWA MHESHIMIWA TUNDU LISSU

$
0
0


Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa CHADEMA na rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

UTAPIAMLO NI JANGA LA KITAIFA – DK. MPANGO

$
0
0
 WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema utapiamlo ni janga la Kitaifa na kwamba theluthi moja ya vifo nchini inasababishwa na tatizo hilo.

Ametoa kauli hiyo juzi jioni (Jumatano, Septemba 6, 2017) wakati akitoa nasaha kwenye mkutano wa nne wa mwaka wa wadau wa lishe wa kutathmini afua za lishe nchini kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.

“Haipendezi kuona katika kila watoto 100, watoto 34 wana udumavu wa akili na katika kila watoto 100, watoto 59 wenye umri kati ya miezi sita na miaka mitano wana upungufu mkubwa wa damu,” alisema. Alisema Serikali inatumia asilimia mbili ya pato la Taifa sawa na dola za Marekani milioni 518 kununua dawa za vitamin A na folic acid (vidonge vya kuongeza damu).

Alisema kuna haja ya kubuni mbinu za kilimo ambazo zitainua kiwango cha upatikanaji wa lishe nchini (nutrition smart agriculture) kama njia ya kudumu ya kukabili tatizo la utapiamlo na udumavu.

Amesema kwa vile Serikali imetenga sh. bilioni 11 ili kukabiliana na utapiamlo, wizara yake itahakikisha inatafuta fedha zilizotengwa na hata ikibidi kutafuta fedha na misaada ya kitaalamu kutoka nje ya nchi ili kuhakikisha suala hilo linatekelezwa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bw. Selemani Jaffo aliziagiza Halmashauri zote nchini zitoe taarifa za kila mwezi za matumizi ya fedha za afua ya lishe kwenye Kamati zake za Fedha. “Hizi fedha si za kufanya masikhara, Serikali iko committed katika suala hili,” alisema.

“Zamani katika bajeti za Halmashauri tulikuwa tukitenga sh. 500 kwa kila mtoto, lakini katika bajeti ya mwaka 2017/2018 tumetenga sh. 1,000 kwa kila mtoto, ambazo ni sawa na sh. bilioni 11 kwa mwaka,” alisema wakati alipopewa fursa ya kutoa nasaha zake.

“Wiki iliyopita, Makamu wa Rais alituagiza tuandike performance contracts kwa Wakuu wote wa Mikoa nchini ili tuweze kufuatilia utekelezaji wao katika suala zima za kuboresha upatikanaji wa lishe nchini. Kazi hiyo tumeshaianza na tarehe 22 Septemba, 2017 itakuwa ni siku ya mwisho ya kukamilisha zoezi hilo,” alisema.

Bw. Jaffo aliwataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya waifanye ajenda ya afya ya lishe kuwa kipaumbele chao.

Wakati huohuo, Naibu Waziri Jaffo amesema kuwa maafisa lishe 660 wataajiriwa nchini kote hivi karibuni. Amesema waliopo hivi sasa ni wataalamu 121 tu ambao kati yao 17 wako mikoani na 104 wako kwenye Halmashauri mbalimbali.

Naye Mkurugenzi wa USAID hapa nchini, Bw. Andrew Karas aliipongeza Serikali kwa uamuzi wake wa kuchukua umiliki na usimamizi wa masuala ya lishe ikiwa ni hatua muhimu ya uratibu wa suala hilo baina ya wahisani, wadau na Serikali.

Alisema ushirikishwaji wa wadau ni suala muhimu na ambalo haliepukiki lakini akaonya kuwa kuna haja ya kuangalia namna ya kuongeza uwezo wadau kwa vitendo ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

“Lengo leni ni letu, na kipaumbele chenu ni chetu. Tukisaidiana tutaweza kufanikisha suala la kuongeza lishe na kupunguza atahari za utapiamlo hapa nchini,” alisema Bw. Karas kwa Kiswahili fasaha na kuamsha shangwe katika ukumbi huo.

Bw. Karas ambaye alizungumza kwa Kiswahili kwa zaidi ya dakika tano, alikuwa akitoa salamu kutoka mtandao wa wahisani wa wenye lengo la kufuta utapiamlo kwa kuboresha lishe nchini (Scaling Up Nutrition -SUN) ambao unajumuisha mashirika ya Children Investment Fund, DfID, Umoja wa Ulaya (EU), Global Affairs Canada, Irish Aid na USAID.

Naye Mwakilishi Mkazi wa UNICEF, Bibi Maniza Zaman, akitoa salamu kwa niaba ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyo chini ya mtandao wa SUN, alisema kufutwa kwa utapiamlo na kuimarishwa kwa uapikanaji wa lishe bora nchini kunaenda sambamba na utekelezaji wa malengo 17 endelevu ya maendeleo.

“Kipengele kimojawapo kikidumaa, kinakwamisha utendaji kazi wa kingine,” alisema na kuongeza: “Mpango uliozinduliwa unahitaji kuwa na fedha za uhakika ili uweze kutekelezeka. Inatia moyo kuona Halmashauri na Sekretarieti za Mikoa zimetenga bajeti kwa ajili ya mpago huu.”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Masuala ya Lishe Tanzania (Partnership for Nutrition in Tanzania - PANITA), Bw. Tumaini Mikindo aliiomba Serikali iziwekee uzio maalum wa kibajeti (ring-fence) fedha za masuala ya lishe ili kuzilinda zisitumike kinyume na matumizi yaliyopangwa.

“Tunaomba fedha za kasama ya lishe ziwe ring-fenced ili ziweze kutumika kama zilivyopangwa. Watendaji watakaofanya vizuri wapongezwe na wale watakaoharibu wachukuliwa hatua za kinidhamu kwa sababu wanataka kuua Taifa letu,” alisema wakati akitoa salamu kwa niaba ya mashirika yasiyokuwa ya Serikali zaidi ya 300 yaliyo chini ya mtandao wa SUN.

Alisema mtandao wao umeenea nchi nzima na akiomba Serikali ilisimamie suala la kupambana na utapiamlo na kuboresha lishe kwa wananchi wake kama ambavyo ilisimamia suala la uhaba wa madawati nchini.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
40480 DODOMA, 
IJUMAA, SEPTEMBA 8, 2017.

TASWA kufanya uchaguzi Novemba 5, mwaka huu

$
0
0
KAMATI ya Utendaji ya Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), iliyokutana Dar es Salaam jana Septemba 7, 2017, imepanga Uchaguzi Mkuu wa chama hicho ufanyike Novemba 5, mwaka huu.

Uchaguzi huo utafanyika Dar es Salaam katika ukumbi ambao utatangazwa na tayari kamati imeaigiza sekreterieti ya TASWA, ifanye maandalizi kuhusu uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na kulishirikisha Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa ajili ya usimamizi wa karibu.

Kikao kimekubaliana watakaoshiriki uchaguzi huo ni wanachama wote wa TASWA waliopo katika leja kuanzia Juni mwaka 2007 hadi Juni mwaka 2017, wakiwemo walioingia uanachama wakati wa semina ya waandishi chipukizi iliyofanyika Dar es Salaam Agosti mwaka 2015 na sharti kubwa ni kila mwanachama kulipia ada ya mwaka mmoja.

Kwa wanachama wengine wapya wanaotaka kujiunga, watafanya hivyo baada ya uongozi mpya kuingia madarakani na kupewa utaratibu kulingana na Katiba ya chama inavyoeleza na pia kwa kadri uongozi mpya utakaoingia madarakani utakavyoona inafaa.Kutokana na hali hiyo wanachama wote wenye sifa hizo, wanatakiwa kulipia ada zao kwa Mhazini Msaidizi, Zena Chande kuanzia leo hadi Septemba 30, mwaka huu.

Uongozi wa sasa wa TASWA uliingia madarakani mwaka 2014, ambapo Juma Pinto alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Egbert Mkoko (Makamu Mwenyekiti), Amir Mhando (Katibu Mkuu), Grace Hoka (Katibu Mkuu Msaidizi), Shija Richard (Mhazini) na Zena Chande (Mhazini Msaidizi).

Wajumbe ni Rehure Nyaulawa, Chacha Maginga, Mussa Juma, Mwani Nyangassa, Mroki Mroki, Ibrahim Bakari na Majuto Omary anayeingia kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa TASWA FC.

Juma Pinto
Mwenyekiti TASWA
08/09/2017

SIMU TV: YALIYOJIRI KATIKA KUKABIDHIWA RIPOTI YA UCHUNGUZI WA BIASHARA YA ALMASI NA TANZANITE

$
0
0


*Hotuba ya waziri mkuu Kassim Majaliwa wakati wa kuwasilisha ripoti ya uchunguzi wa biashara ya  almasi hii leo Ikulu Dar es Salaam. https://youtu.be/eq_2APWbmUk

*Rais Magufuli akizungumzia kuhusu wizi biashara ya Almasi, ombi la Spika la kuwachukulia hatua kali viongozi wanaotajwa katika kashfa za wizi hii leo Ikulu Dar es Salaam. https://youtu.be/91VDw022I1w

*Rais Magufuli akisimulia namna Prof.Mruma alivyotumwa kuchunguza suala zima la biashara ya madini ya Almasi. Bofya hapa kufahamu alivyofanya. https://youtu.be/iEMUb-IG8ww

TRA, CTI WAKUTANA NA WADAU WAFANYABIASHARA KUJADILI NAMNA YA KUTATUA CHANGAMOTO MBALIMBALI ILI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA WA KATI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru (katikati) akiwa meza kuu na Viongozi wa TRA na CTI wakiongoza Mkutano wa Msamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Wadau wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini CTI, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulikuwa na lengo la majadiliano kuhusu namna ya kutatua changamoto mbalimbali ili kufikia Uchumi wa Viwanda wa Kati pamoja na vikwazo vya ulipaji na ukusanyaji Kodi nchini. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru, akizungumza wakati wa Mkutano wa Msamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Wadau wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini CTI, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo. Mkutano huo ulikuwa na lengo la majadiliano kuhusu namna ya kutatua changamoto mbalimbali ili kufikia Uchumi wa Viwanda wa Kati pamoja na vikwazo vya ulipaji na ukusanyaji Kodi nchini. 
Kamishina Mkuu wa TRA, Charles Kichele, akizungumza wakati wa Mkutano wa Msamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Wadau wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini CTI, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo. Mkutano huo ulikuwa na lengo la majadiliano kuhusu namna ya kutatua changamoto mbalimbali ili kufikia Uchumi wa Viwanda wa Kati pamoja na vikwazo vya ulipaji na ukusanyaji Kodi nchini.
Mkurugezni Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini, Leodger Tenga, akizungumza wakati wa Mkutano wa Msamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Wadau wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini CTI, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo. Mkutano huo ulikuwa na lengo la majadiliano kuhusu namna ya kutatua changamoto mbalimbali ili kufikia Uchumi wa Viwanda wa Kati pamoja na vikwazo vya ulipaji na ukusanyaji Kodi nchini. 


VIJANA NCHINI WATAKIWA KUTUMIA MUDA VIZURI ILI KUFIKIA MALENGO WALIYOJIWEKEA

$
0
0
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura amewataka vijana nchini kutumia muda vizuri na mazingira yanayowazunguka ili kufikia azma ya malengo waliojiwekea katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Naibu Waziri Wambura ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma alipokuwa akimpongeza Mlimbwende Witness Teddy Kavumo ambaye ni Mtanzania anayeishi Afrika Kusini kwa kushinda taji la Miss Garden Route 2017/2018  Mei 6 mwaka huu nchini humo katika mji wa George.

Mlimbwnde Witness aliibuka mshindi wa Miss Garden Route 2017/2018 akiwa ni miongoni mwa washindani 14 walioingia fainali baada ya mchujo wa awali wa washiriki 600.“Ni dhahiri umetumia ujuzi, ubunifu, sanaa, imani, bidii, desturi, maadili, na sheria ambavyo umevipata  kutoka kwa familia, jamii ya Kitanzania na pia kwa jamii ya watu wa  Afrika Kusini” amesema Naibu Waziri Wambura.

“Vijana wa Kitanzania, Mlimbwende Witness Mshindi wa taji la Miss Garden Route 2017 la Afrika Kusini amewaonesha njia, mjenge utamaduni wa kupambana na mazingira ili kufikia azma mnazojiwekea” alisistiza Naibu Waziri Wambura.

Aidha, Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa Bi Witness ameonesha uzalendo kwa nchi yake kwa kuamua kuja Dodoma na kutoa taarifa ya mafanikio yake kama Mtanzania kwa ushindi alioupata katika mashindano ya ubunifu mavazi huko Afrika ya Kusini.

Hatua hiyo inaonesha Mlimbwende huyo ameumeuthamini Utanzania wake na kuonesha kujali kutumia muda wa ziada kwa masuala ya fani ya urembo licha ya kwamba jukumu lake la msingi nchini humo ni la Kimasomo.
Zaidi ya hayo Naibu Waziri Wambura amesema kuwa fani ya ubunifu na mitindo inatambulisha utamaduni, kuongeza kipato, kuinua uchumi na kukuza utalii kwa kuongeza juhudi, maarifa na kufanya kazi kwa bidii hatua nambayo inaleta matokeo mazuri yenye tija.

Aidha, Naibu Waziri Wambura amemshauri Witness, kutumia bidhaa zenye asili ya Tanzania katika fani yake, ili kuzitangaza katika soko la ndani na la nje, kuvutia utalii, kuingiza kipato na  kukuza uchumi katika ngazi zote za mnyororo wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo kwake yeye binafsi na kwa Taifa.

Kwa upande wake Miss Garden Route 2017/2018 Mlimbwende Witness amesema kuwa anajivunia kuwa Mtanzania na kuonesha uzalendo kwa nchi yake na amewashauri Watanzania kusimama kwa kujiamini na kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Mashindano ya Miss Garden Route 2017/2018 yaliandaliwa na ‘The RoleModels Foundation” kwa kushirikiana na Wakala wengine akiwemo “Gemini Modelling Agency” iliyopo Mossel Bay  Afrika Kusini.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akimvisha taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo leo mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akimpongeza Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo kwa ushindi wa taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini leo mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akipokea nyaraka za ushindi wa taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini kutoka kwa mshindi wa taji hilo Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo leo mjini Dodoma.
 Mshindi wa taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mjini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura. 

Mshindi wa taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo. (Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma)

JOCKTAN MAKEKE KUSHIRIKI MAONESHO YA UTAMADANI NCHINI NIGERIA

$
0
0
 Mkurugenzi wa bodi ya Utalii nchini, Tanzania Devotha Mdachi  akikabidhiwa bendera Msanii wa mitindo, Jocktan Makeke.
Msanii wa mitindo inayohusu utamaduni wa Mwafrika Jocktan Makeke / MAKEKE INTERNATIONAL anatarajia kwenda Abuja Nigeria kwa ajili ya maonesho makubwa ya utamaduni ya FACE OF CULTURE NIGERIA, ambapo ataonesha mavazi yenye ubunifu wa hali ya juu ambayo yanakwenda kwa jina la #OTOSIM2017

Tamasha hilo litafanyika siku ya tarehe 09/09/2017 katika ukumbi wa Sheraton Hotel ya mjini Abuja.Aidha maonesho hayo yataambatana na utoaji wa tuzo kwa watu mbalimbali ambao wamefanya vizuri kwenye mambo ya utamaduni.

WANYAKYUSA MPOO...HII NI NGOMA KUTOKA TUKUYU MBEYA

SHAKA AZINDUA PROGRAMU YA USHIRIKISHWAJI KWA VIJANA DODOMA

$
0
0
Na Mathias Canal, Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Septemba 7, 2017 Amezindua Programu maalumu kwa Vijana wa CCM katika ushiriki wa shughuli za miradi ya Kimaendeleo, Kiuchumi na Kijamii katika ukumbi wa CCM (NEC) Mjini Dodoma.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Shaka alisema Wazo hilo limeibuliwa wakati muafaka huku serikali ya CCM awamu ya tano chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ikiweka mkazo na vipaumbele kadhaa vinavyomtaka kila mtanzania hususani vijana kujituma, kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha Mali.

Alisema dhana ya kufanya kazi kwa bidii, malengo na shabaha si ngeni lakini kwa wakati huu inahubiriwa kwa nguvu kulingana na changamoto nyingi zilizopo, fursa, ushirikishwaji kwa kuzingatia mahitaji halisi kutokana na mabadiliko ya dunia Kiuchumi na Kimaendeleo.

Aliwasisitiza Vijana kutambua wajibu wa kukuza shughuli za kazi na maisha zikiongozwa na nguvu ya uzalendo, kujali utaifa na kutambua dhamana iliyopo ya kudumisha amani, Umoja, Mshikamano na Maendeleo."Ili kusihi yote hayo hatimaye Vijana waweze kuyafanikisha tunapaswa kuwa na mioyo isiyopwaya au kukosa rutuba ya kutodumisha uzalendo, tunalazimika kwa pamoja kutambua mpango wowote wa kuyafikia maendeleo ya kweli utabaki ni hadithi na ndoto Kama hatutaongozwa na shime ya uzalendo au kutothamini utaifa wetu Kama ambavyo viongozi wanatuhimiza siku Hadi siku" Alisema Shaka.


Shaka aliwaeleza Vijana kuwa pamoja na kuwepo juhudi kubwa za mara kwa mara kuchukuliwa na serikali, mashirika hiari ya Kijamii na yasiyokuwa ya kiserikali, kuelimisha juu ya dhana ya ushirikishwaji na ushiriki wa Vijana katika miradi ya Kiuchumi na Kijamii wanapaswa kuwa na utayari, uthubutu, uzalendo, na Utaifa.

IGP SIRRO AZUNGUMZIA TUKIO LA KUPIGWA RISASI MH. TUNDU LISSU,AAHIDI KUWAKAMATA WOTE WALIOHUSIKA

SPIKA NDUGAI ATEMBELEWA NA BALOZI WA VIETNAM NCHINI TANZANIA OFISINI KWAKE MJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Balozi wa Vietnam nchini Tanzania, Nguyen Doanh pale ugeni kutoka Vietnam ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini Tanzania, Nguyen Doanh pale ugeni kutoka Vietnam ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kazi pamoja na kuboresha urafiki baina ya nchi hizi mbili.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Vietnam nchini Tanzania, Nguyen Doanh pale ugeni kutoka Vietnam ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kazi pamoja na kuboresha urafiki baina ya nchi hizi mbili.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akiwa katika picha ya pamoja​ na ugeni kutoka Vietnam uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kazi pamoja na kuboresha urafiki baina ya nchi hizi mbili. Katikati ni Balozi wa Vietnam nchini Tanzania, Nguyen Doanh na kushoto ni katibu wa Balozi huyo, Ndg. Nguyen Binh.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

POLISI: WALIOTAJWA RIPOTI YA MADINI YA ALMASI NA TANZANITE, DCI AFUNGUA JARADA


JESHI LA POLISI MAKAO MAKUU LAUNDA TIMU YA KUPELELEZA TUKIO LA TUNDU LISSU.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

JESHI la Polisi  Makao Makuu  imeunda timu ya upelelezi ya kufatilia tukio la kushambuliwa kwa risasi  kwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Dodoma.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema ameunda  timu ya kufatilia tukio la  kushambulia kwa risasi kwa  mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu  jana mkoani Dodoma.

Amesema timu ya makao makuu ya Polisi inaenda kuongeza nguvu zaidi ili kuhakikisha kuwa watuhumiwa waliofanya kitendo hicho wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
IGP Sirro amesema kuwa waliomshambulia  Mwanasheria huyo na   Rais wa Chama Wanasheria Nchini (TLS) ni watu wasiofahamika  ambapo  hivi sasa anaendelea na matibabu.

Hata hivyo amesema kuwa Lissu alidai kuwa kuna watu wanafuatilia lakini hakuweza kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi hivyo akipona anatakiwa kupeleka taarifa hizo.

IGP Sirro amewataka wananchi kuacha kusambaza ujumbe na picha video za taarifa zisizo za ukweli kwenye mitandao ya jamii na matukio mbalimbali yanayotokea nchini kutokana na kuibua hofu kwa wananchi  pamoja na kuweza kuharibu upelelezi wa tukioa lilomtokea Lissu.

 Aidha amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi  kwa kutoa taarifa zitakazofanikisha kwa kukamatwa watuhumiwa wote waliohusika na tukio la Lissu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kutangaza kuwa Jeshi la Polisi  limeunda Timu maalum kwaajili ya kuchunguza na kufuatilia tukio la kushambuliwa kwa risasi hapo jana Mkoani Dodoma nyumbani.

MFANYABIASHARA MANJI HATAMBUI KUVULIWA UDIWANI KATA YA MBAGALA KUU.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
 MFANYABIASHARA maarufu  nchini, Yusuf Manji mapema leo amesema kuwa hatambui kuvuliwa kwake udiwani wa Kata ya Mbagala Kuu na kwamba yeye bado ni diwani.
Manji ameyasema hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
wakati kesi ya yake uhujumu uchumi inayomkabili yeye na wenzake watatu ilipokuja kutajwa.
Kabla ya kusema hayo, wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi ameieleza mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo, bado haujakamilika.
Akielezea kuhusu udiwani, Manji aliongeza kuwa, aliona habari kupitia gazeti la Mwananchi kwamba amevuliwa udiwani ila hajui kama ni kweli au la.
Amedai, mahakama imuagize Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), awaambie Halmashauri ya Wilaya ya Temeke kwamba walimkamata na sababu za kutohudhuria vikao kwa miezi miwili  ni kwa kuwa hana dhamana.
Amesema, yeye amechaguliwa na wananchi na kwamba kama wanataka aende kwenye vikao, DPP aombe hati ya kumtoa gerezani ili akaudhurie vikao au wamuandikie barua yenye ajenda na kumbukumbu za vikao ili ajibu akiwa gerezani.
Ameongeza kuwa, ametumia zaidi ya milioni 70 za kwake binafsi na sio za halmashauri kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake na alikuwa anahudhuria vikao kabla hajakamatwa kwa kesi hizo nzito.

“Kwa kuwa naheshimu mahakama na ukubwa wa kesi hii sikuomba dhamana," amedai Manji.
Akijibu hoja hiyo, Hakimu Shaidi amewataka upande wa mashitaka kufuatilia suala hilo na kumueleza mshtakiwa kuwa maombi yake yamechukuliwa.
Wiki iliyopita Meya wa Temeke, Abdallah Chaurembo alitangaza kumvua udiwani Manji kwa kutohudhuria vikao.
Mbali na Manji.
Manji anashtakiwa pamoja na Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda, Mtunza stoo, Abdallah Sangey na Thobias Fwere.
Awali, Wakili wa washitakiwa, Seni Malimi aliiomba mahakama kutoa ahirisho fupi kwa washtakiwa kwa kuwa wanamaombi maalumu.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 18, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Manji na wenzake wanakabiliwa na tuhuma za uhujumu uchumi ambapo wanadaiwa kukutwa na vifaa mbali mbali za jeshi la polisi zikiwemo sare.
 Mfanyabiashara maarufu  nchini, Yusuf Manji Mwenye Shati Nyeupe akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo
amesema kuwa hatambui kuvuliwa kwake udiwani wa Kata ya Mbagala Kuu na kwamba yeye bado ni diwani.
 Mfanyabiashara maarufu  nchini, Yusuf Manji Mwenye Shati Nyeupe akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii 

BREAKING NYUZZZ....: MOTO WAZUKA DUKA LA VIFAA VYA UJENZI MJINI MOSHI MCHANA HUU

$
0
0

Moto umezuka katika duka la vifaa vya ujenzi la Chavda lililopo Double road katika manispaa ya Moshi na kutekeketeza bidhaa mbalimbali.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinadai moto huo ulianza majira ya Saa 6: 47 za mchana hata hivyo jeshi la zima moto kutoka Kiwanda cha TPC kwa kushirikiana na jeshi la polisi wanaendelea na jitihada za kuzima moto huo. Picha na Dixon Busagaga.

Sehemu askari Polisi na kikosi cha zimamoto pamoja na wananchi wakisaidiana kutafuta mbinu za kuudhibiti moto uliozuka katika duka la vifaa vya ujenzi la Chavda lililopo Double road katika manispaa ya Moshi na kutekeketeza bidhaa mbalimbali.

MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI AGOSTI 2017 UMEPUNGUA-NBS

$
0
0

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusianaMfumuko wa bei wa Mwezi Agosti Mwaka huu(2017) kwa kipimo cha Mwezi umepungua kwa asilimia 0.4

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na mfumuko wa bei kwa mwezi Agosti Mwaka huu.Kulia ni Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei Ruth Minja

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti 2017 umepungua zaidi hadi kufikia asilimia 5.0 ikilinganishwa na asilimia 5.2 ilivyokuwa mwezi Julai2017.

Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema hii inamanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2017 imepungua zaidi ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Julai,2017.

Kwesigabo alisema Mfumuko wa Bei wa Bidhaa za Vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Agosti, 2017 umepungua hadi asilimia 8.6 kutoka asilimia 8.9 ilivyokuwa mwezi Julai, 2017.

"Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 108.46 mwezi Agosti, 2017 kutoka 103.28 mwezi Agosti, 2016" alisema Kwesigabo.

Akizungumzia mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Agosti,2017 umepungua hadi asimilia 9.1 kutoka asilimia 9.3 mwezi Julai 2017. Ambapo badiliko la Fahirisi za bei zisizo za vyakula umebaki kuwa asilimia 3.1 mwezi Agosti, 2017 kama ilivyokuwa mwezi Julai, 2017.

Kwesigabo ameongeza kuwa mfumuko wa bei ambao haujumuishi vyakula na nishati kwa mwezi Agosti, 2017 umepungua hadi asilimia 1.8 kutoka asilimia 2.2 Julai, 2017.

Fahirisi inayotumika kukokota aina hii ya mfumuko wa bei haijumuishi vyakula vinavyoliwa nyumbani na migahawani, vinywaji baridi, petroli, dizeli, gesi ya kupikia, mafuta ya taa, mkaa kuni na umeme.

Amesema vyakula na bidhaa za nishati vinasifa ya kuwa na bei ambazo hubadilika mara kwa mara, hivyo vikiondolewa kwenye fahirisi ya bidhaa na huduma zote hubakia fahirisi ambayo ina mwelekeo imara kwa watunga sera.

KAMPUNI YA GROOVJOINT YALETA VIUNGANISHI VYA MABOMBA KUTOKA NCHINI MAREKANI

$
0
0
Wakala wa wauzaji wa Vifaa Vya kuunganishia mabomba yanayotoka nchini Marekani, David Robert Mwamsojo akionyesha waandishi wa habari moja ya kiunganishi cha mabomba yanayotengenezwa na kampuni ya GroovJoint ya nchini Marekani katika mkutano wa kuitambulisha kampuni ya GroovJoint ya nchini Marekani iliyoleta nchini Tanzania teknolojia mpya ambayo itasaidia kuokoa miundo mbinu ya maji. Pembeni ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya GroovJoint ya nchini Marekani iliyokuja kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya viwanda. Picha na Kajunason/MMG.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye akitoa shukrani zake za pekee kwa kampuni ya GroovJoint iliyokuja nchini Tanzania kuwekeza upande wa viunganishi vya mabomba ambapo alisema kuwa wameamua kuwapokea kwa mikono miwili kampuni hiyo kwa vile viunganishi vitasaidia wananchi kupata maji safi na salama. Pembeni ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya GroovJoint ya nchini Marekani iliyokuja kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya viwanda na Wakala wa wauzaji wa Vifaa Vya kuunganishia mabomba yanayotoka nchini Marekani, David Robert Mwamsojo. Makamu wa Rais wa Kampuni ya GroovJoint ya nchini Marekani, David Newman iliyokuja kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya viwanda kwa kuleta viunganishi vya mabomba.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye akimshukuru Makamu wa Rais wa Kampuni ya GroovJoint ya nchini Marekani, David Newman mara baada ya mkutano na waandishi wa habari kuelezea malengo ya kampuni yao. Pembeni ni Wakala wa wauzaji wa Vifaa Vya kuunganishia mabomba yanayotoka nchini Marekani, David Robert Mwamsojo.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images