Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

WAKIMBIZI RAIA WA BURUNDI WAANZA KUREJEA NYUMBANI

0
0
Zoezi la kuwarejesha wakimbizi raia wa Burundi waliohiari kurejea nyumbani limeanza leo ambapo jumla ya wakimbizi 301 wamerejeshwa nchini humo. Zoezi hilo la kuwasafirisha limesimamiwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshugulikia wakimbizi (UNHCR), Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IMO) na washirika wengine wakiwemo Shirika la Mpango wa Chakula (WFP) na Shirika la Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (IRC).

Msafara wa wakimbizi hao ambao wote wametoka kambi ya Nduta iliyoko wilayani Kibondo Mkoani Kigoma yenye wakimbizi 127,000 uliondoka kambini hapo saa nne asubuhi kwenda Mabamba mpakani mwa Tanzania na Burundi.

Katika eneo la Mabamba wakimbizi hao walipokelewa na viongozi wa Serikali ya Burundi na washirika mbalimbali wakiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi Terance Nahiragiye na wawakilishi wa shirika la UNHCR nchini Burundi.

Naibu Waziri wa Ndani ya Burundi katika maelezo yake kwa wakimbizi hao aliwahakikishia kuwa hali ya usalama ni nzuri na kuwa mali zao zikiwemo nyumba na ardhi zimehifadhiwa na watarejeshewa wenyewe watakapofika nyumbani.

Akizungumza na MAELEZO kwa njia ya simu kutoka mpakani wa Tanzania na Burundi Mkuu wa Mkoa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga alisema zoezi hilo limekwenda vizuri kama lilivyopangwa na wakimbizi waliorejea walionesha furaha kwa kupata fursa ya kwanza kurejea.

Mkuu wa Mkoa huyo alibainisha kuwa taarifa za hivi karibuni zinaonesha kuwa wakimbizi zaidi ya 6,000 wa kambi ya Nduta wamejiandikisha kurejea nyumbani wakiwa ni miongoni mwa wakimbizi 12,000 wa nchi hiyo waliojiandikisha kwa hiari hadi sasa kurejea nchini Burundi.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Wakimbizi kanda ya Kigoma Tonny Laizer, zoezi hilo litaendelea tena Jumane ijayo tarehe 12 Septemba, 2017 ambapo litajumuisha wakimbizi 350.

Hivi sasa kuna wakimbizi raia wa Burundi 256, 850. Zoezi hilo linafanyika kufuatia kutiwa saini makubaliano ya kuwarejesha wakimbizi hao kati ya Serikali za Tanzania, Burundi na shirika la UNHCR hivi Karibuni jijini Dar es Salaam.

WAJUMBE WA KAMATI MAALUM ILIYOUNDWA NA RAIS DKT.MAGUFULI WAENDELEA NA MAJADILIANO NA TIMU KUTOKA KAMPUNI YA BARRICK GOLD CORPORATION

0
0
Wajumbe wa kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiendelea na majadiliano na timu kutoka kampuni ya Barrick Gold Corporation leo Septemba 7, 2017 kuhusu madai ya Tanzania juu ya upotevu wa fedha nyingi katika biashara ya madini ya dhahabu inayofanywa na kampuni hiyo hapa nchini. Majadiliano hayo yanafanyika jijini Dar es salaam

SERIKALI KURAHISISHA MAISHA YA WASTAAFU

0
0

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mtambile Mhe. Masoud Abdallah Salim (CUF), aliyetaka kujua mpango wa Serikali katika kuboresha mafao ya uzeeni ili kuondoa malalamiko ya hali ngumu ya maisha wanayoishi Wastaafu.

Mhe. Salim alisema kuwa kumekuwepo malalamiko mengi kutoka kwa Wastaafu ambao wakati wa utumishi wao walilitumikia Taifa kwa uwaminifu na uadilifu mkubwa, kuhusu kuishi maisha magumu yanayotokana na kucheleweshewa mafao yao ya uzeeni yasiyolingana na kupanda kwa gharama za maisha.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa, Serikali kwa sasa imejielekeza zaidi katika kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, nishati ya umeme, maji, huduma za afya, elimu na kiuchumi hususan katika ukusanyaji mapato kwa lengo la kuboresha maisha ya Wastaafu na Wananchi kwa ujumla.“Tuendelee kuiunga mkono Serikali yetu katika juhudi zake za kujenga uchumi imara, uchumi wa viwanda ambao ndio msingi mkuu wa kuimarisha mapato ya Serikali”. Alisema Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa maboresho ya viwango vya pensheni kwa Wastaafu yasiyoendana na maboresho ya miundombinu ya kiuchumi na huduma za kijamii hayawezi kuondoa malalamiko ya Wastaafu hivyo Serikali imelenga zaidi kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii ili kupunguza malalamiko hayo.

Dkt. Kijaji alifafanua kuwa nyongeza ya pensheni kwa Wastaafu, mishahara na maslahi mazuri kwa Watumishi wa Umma itaongezeka kama mikakati na azma ya Serikali ya kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi itafanikishwa.Aidha Dkt. Kijaji aliongeza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kuboresha viwango vya pensheni ili kukidhi mahitaji muhimu ya Wastaafu, kwa kutambua hilo Mwezi Julai 2015, Serikali iliboresha kiwango cha pensheni kutoka Sh. 50,114 hadi Sh. 100,125 kwa mwezi.

Imetolewa na:

Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
Serikali imeahidi kuendelea kuboresha mifumo ya kukusanya mapato pamoja na kuboresha miundombinu ya kiuchumi na kijamii ili kuleta unafuu wa maisha ya Wastaafu na Wananchi kwa ujumla.

TANZIA: KAMISHNA MSTAAFU WA OPERESHENI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI AFARIKI DUNIA MAPEMA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini– Thobias Andengenye anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna wa Operesheni Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CF (OPS) Rogatius Peter Kipali, kilichotokea mapema leo Semptemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake Mombasa, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anatoa pole kwa Maafisa, Askari na Watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, familia ya Marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna tofauti tofauti.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na familia ya Marehemu linaendelea kuratibu shughuli za msiba huo na taarifa za Mazishi zitatolewa baadaye baada ya taratibu zote kukamilika.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amina.


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA LEO

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Muungano na Mazingira) Mhe.January Makamba akizungumza  jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde katika kikao cha tatu cha Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo  Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe.Dk.Suzan Kolimba  akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba  na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline  Mabula katika kikao cha tatu cha Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo  Mjini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum(CCM) Halima Bulembo akiuliza swali katika kikao cha tatu cha Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo  Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama  akimskiliza Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba katika kikao cha tatu cha Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo  Mjini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Makame Mbarawa akizungumza jambo na Mbunge wa Chalinze Mhe.Ridhiwani Kikwete katika kikao cha tatu cha Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo  Mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tatu cha Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo  Mjini Dodoma.
Picha na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.

MICHUZI TV: MFAHAMU EVODIA NCHIMBI, MWANADADA ANAYEJISHUGHULISHA NA UDEREVA WA BAJAJ JIJINI DAR

TAMISEMI YATENGA BILIONI MOJA

0
0
Na Silvia Hyera

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa TAMISEMI imetenga bajeti ya Shilingi Bilioni 1 katika mpango wa lishe wa mwaka 2017/18 wenye lengo la kupeleka agenda ya lishe kitaifa na kutokomeza udumavu na utapia mlo nchini.

Mhe. Jafo alisema hayo jana kwenye mkutano wa nne wa wadau wa sekta ya lishe katika kufanya mapitio ya mpango jumuishi wa lishe 2016/17- 2020/2021 wenye kauli mbiu ya lishe bora ni msingi wa maendeleo ya viwanda nchini Tanzania , uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Hazina Mjini Dodoma.Alisema kuwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)

Imepewa jukumu la kuratibu mpango wa lishe katika ngazi za Mkoa na Wilaya hivyo mpango huo utatekelezeka kwa kina na uweledi mkubwa katika kuboresha lishe nchini kupitia dhana ya ugatuaji wa madaraka.

“ Tumejielekeza vya kutosha katika kuboresha afya ya kila mtoto, bajeti ya awali ilikuwa shilingi 500 kwa kila mtoto chini ya miaka 5 lakini katika bajeti ya sasa 2017/18 TAMISEMI imetenga bajeti ya elfu moja kwa kila mtoto na kuweka jumla ya Shilingi bilioni 1 “

Aidha alisema ni wajibu wa kila Mkuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa afua zilizoanishwa katika mpango jumuishi wa utekelezaji wa masuala ya lishe ili kuboresha afya na kuendeleza agenda ya lishe katika kuleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla. 

Aliongeza kuwa Taifa linahitaji watu wenye afya bora ili waweze kuchangia katika kuleta maendeleo nchini , mpango huu jumuishi wa lishe 2016/17- 2020/2021 una lengo la kutokomeza utapia mlo na boresha afya ya mtoto hivyo ni wito wa kila mdau wa afya kuhahakisha anasimamia kikamilifu utekelezaji wa mpango huu.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasim Majaliwa alisema kuwa Serikali imejipanga vya kutosha katika kutokomeza utapia mlo nchini hivyo aliwataka wadau kutoa elimu sahihi ya lishe na kulipa kipaumbele suala zima la lishe kwa kubuni sera na mikakati bora ya kilimo na lishe.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Chakula na Lishe Tanzania ( TFNC) Bi. Joseline Kaganda alisema kuwa ili kutokomeza utapia mlo nchini lazima kuwepo na mpango thabiti wa kupambana na chanagamoto hii pamoja na ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa lishe.

Naye Mkurugenzi wa USAID na mwakilishi wa Msukumo mpya katika masuala ya lishe (SUN-NETWORK) Bw. Andrew Karas amesema kuwa ushirikishwaji wa wananchi ,wadau na Serikali ni muhimu mno katika kutokomeza utapia mlo Tanzania hivyo ni lazima kuimarisha mahusiano na mifumo iliyopo ili kufikisha huduma kwenye maeneo yaliyo na upungufu.

Mkutano wa nne wa wadau wa sekta ya lishe katika kufanya mapitio ya mpango jumuishi wa lishe 2016/17- 2020/2021 utakaodumu kwa siku tatu katika ukumbi wa mikutano Hazina Mjini Dodoma umehudhuriwa na Maafisa lishe wa Mikoa na Wilaya nchini,Asasi na mashirika ya kiraia yanayotekeleza afua za lishe,sekta binafsi na Wizara mtambuka pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kwa siku tatu .
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh. Profesa Seleman Jafo akizungumza kwenye wa mkutano wa nne wa wadau wa sekta ya lishe katika kufanya mapitio ya mpango jumuishi wa lishe 2016/17- 2020/2021 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Hazina Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasim Majaliwa akimkabidhi Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh. Profesa Seleman Jafo mpango mpango jumuishi wa lishe 2016/17- 2020/2021 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Hazina Mjini Dodoma.

TAARIFA YA CCM KUFUATIA TUKIO LA KUSHAMBULIWA MBUNGE MH.TUNDU LISSU MJINI DODOMA LEO


RAIS DKT MAGUFULI AVIAMURU VYOMBO VYA DOLA VIWASAKE WALE WOTE WALIOHUSIKA TUKIO LA MBUNGE TUNDU LISSU

DAWASA YAKABIDHI VYOO KWA WAKAZI WA VINGUNGUTI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Mhandisi wa Maji toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Gratius Haule (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa vyoo katika Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti, vyoo hivyo vimejengwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Cambridge Development Initiative (CDI).
Mhandisi wa Maji toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Gratius Haule akisisitiza jambo kwa wakazi wa Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti (hawapo pichani) wakati wa sherehe za kukabidhi vyoo kwa baadhi ya wakazi hao ambavyo vimejengwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Cambridge Development Initiative (CDI) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti wakimsikiliza Mhandisi wa Maji toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Gratius Haule wakati wa sherehe za kukabidhi vyoo kwa baadhi ya wakazi hao ambavyo vimejengwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Cambridge Development Initiative (CDI) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi Bridge for Change Bw. Ocheck Msuva akifafanua jambo kwa wakazi wa Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti (hawapo pichani) wakati wa sherehe za kukabidhi vyoo kwa baadhi ya wakazi hao ambavyo vimejengwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Cambridge Development Initiative (CDI) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

ISAYA MWITA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MEYA WA JIJI LA HIN’AN NCHINI CHINA,ZHU HUAN DAR ES SALAAM

0
0

NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amekutana na kufanya mazungunzo na Meya wa Jiji la Xin’an Nchni China Zhu Huan ofisini kwake Karimjeee.

Katika mazungumzo hayo , Meya Mwita na mgeni wake wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kukuza na kutangaza utalii wa ndani na nje ya Dar es Salaam.

Aidha Meya Mwita amesema jiji la Dar es Salaam lina kila aina ya vivutio vya utalii wa ndani na nje ambavyo vinaweza kuwavutia wageni mbalimbali kutoka nje ya Nchi kufika jijini hapa na kutalii badala ya kwenda Zanzibar , Kilimanjaro na maeneo mengine.

Ameongeza kuwa anaamini kuwa mazungumzo hayo na mgeni wake yataleta tija na kwamba jiji la Dar es Salaam litapata watalii kutoka sehemu mbalimbali na hivyo kuliwezesha jiji kupata mapato makubwa kupitia vivutio vilivyopo.

“ Tunania ya kulitagaza jiji letu kwenye sekta ya utalii, kutokana na rasilimali za vivutio vilivyopo, ukienda kwenye maeneo mengi ndani ya jiji letu utaona kuwa tunavyo vivutio vyakutosha kabisa ambavyo vikitangazwa kila mmoja atapenda kutalii katika jiji hili” amesema Meya Mwita.

“ Yapo maeneo mengi ambayo watanzania hawayajui, lakini kupitia mpango huu ambao nimekuja nao hivi sasa ninaimani kwamba watu ambao walikuwa wanafika kwenye jiji letu na kupanda ndege kwenda Zanziba ama Arusha na maeneo mengine, sasa watafanya utalii hapa kwetu” amesisitiza.

Meya Mwita ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa , hivi karibuni jiji la Dar es Salaam linaratajia kupokea magari ya utalii ambayo yamenunuliwa kupitia fedha za jiji, ambapo baada ya kufika yatazinduliwa na hivyo kuanza kutangaza utalii wa ndani.

Kwaupande wake Meya wa jiji la Xin’an Zhu Huan amempongeza Meya Mwit kutokana na uendeshaji wake wa jiji, ambapo amesema jiji la Dar es Salaam limepata Meya bora ambaye anaamini kwamba ataleta mabadiliko makubwa ndani jiji hili.

Mbali na pongezi hizo, pia ameahidi kushirikiana nae katika sekta mbalimbali ikiwemo kutangaza utalii wa jijini hapa ili uweze kutambulika katika maeneo mengine Nchini China.
Mstahiki Meya wa jiji la Xn’an Nchini China Zhu Huan akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kufaya mazungumzo na mwenyeji wake Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita alipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya mbalimbali.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari leo ,mara baada ya kufanya mazungumzo na Meya wa jiji la Xin’an Zhu Huan alipomtembelea ofisini kwake leo. wa kwanza kulia ni Meya wa jiji la Xin’an,
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akisalimiana na Meya wa jiji la Xin’an Zhu Huan alipomtembelea ofisini kwale leo na kufanya nae mazungumzo.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mwenye suti nyeusi akiwa na Meya wa jiji la Xin’an Zhu Huan akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya mazungumzo leo alipomtembelea mfisini kwake.

SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 11 KUKABILI UTAPIAMLO

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 11 ili kukabiliana na utapiamlo na amemtaka kila mdau wa lishe aonyeshe bayana mchango wake katika kukabiliana na utapiamlo nchini.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Septemba 6, 2017) wakati akifungua mkutano wa nne wa mwaka wa wadau wa lishe wa kutathmini afua za lishe nchini kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. Pia alizindua Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe wa mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 (Joint Multisectoral Nutrition Review).

“Viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali wabaini kiwango cha utapiamlo katika maeneo yao, waonyeshe mbinu za kukabiliana na hali hiyo, wafanye tathmini ya ufanisi na watoe taarifa za ufanisi,” amesema.

Amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote, wahakikishe shilingi 1,000 ambazo Halmashauri zilielekezwa kutenga kwenye bajeti kutoka kwenye vyanzo vyao vya mapato kwa ajili ya kuboresha lishe kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano, zinatolewa na kutumika kama ilivyopangwa.

“Tulikubaliana kila Halmashauri lazima ikusanye makusanyo ya ndani kwa asilimia zaidi ya 80. Nilisema kiwango cha chini kisipungue asilimia 80. Na kupitia makusanyo hayo, ndipo tunapata fedha za kutenga kwa masula kama haya,” alisisitiza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango nakala ya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya Waziri Mkuu kuuzindua kwenye ukumbi wa hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde. Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo, wapili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini, Minaz Zaman na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini, Andy Karas.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini nakala ya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya kuzindua Mpango huo kwenye ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango(kushoto kwake) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia kwake) wakionyesha vitabu vya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya Waziri Mkuu kuuzindua kwenye ukumbi wa hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo, wapili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini, Minaz Zaman na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini, Andy Karas
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katia Uzinduzi wa Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe uliofanywa na Waziri Mkuu, kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.




RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA MADINI YA ALMASI NA TANZANITE KUTOKA KWA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Madini ya Tanzanite kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Kamati Maalumu ya Bunge ya Kuchunguza Madini ya Almasi kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipitia Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Madini ya Almasi na Tanzanite mara baada ya kukabidhiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi Taarifa hiyo kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


 

SHUKURANI/APPRECIATION

Dkt. Augustine Mahiga aagana na Balozi wa China Dkt. Lu Youqing.

0
0
 Na Bushiri Matenda- MAELEZO 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga ameagana na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing. 
Katika hafla fupi iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Dkt. Mahiga alimshukuru Balozi Dkt. Lu kwa kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali ya nchi yake na Tanzania kwa muda wote alipokuwa nchini akitekeleza majukumu yake. 
Dkt. Mahiga alimueleza Balozi huyo kuwa Tanzania na China ni ndugu kwani tangu Tanzania ilipopata Uhuru imekuwa ikishirikiana na nchi hiyo yenye maendeleo makubwa kiuchumi. 
“Kwa muda mrefu wizara zetu zimekuwa zikifanya kazi kwa karibu sana ambapo sasa tumekuwa washirika wa karibu. Wewe Balozi umekuwa kielelezo tosha cha kutekeleza tafsiri ya sera nzuri ya nchi yako kwa mataifa mengine ikiwamo Tanzania” alisema Dtk. Mahiga. 
Aidha, Dkt. Mahiga alisifu utendaji wa balozi huyo kuwa wa ni wa kipekee kwani amekuwa mnyenyekevu, msikivu na anafanya kazi zake kwa utaratibu na uhakika. 
Alimshukuru balozi huyo kwa jitihada zake za kuhakikisha watushishi wa wizara kuendelea kupata mafunzo nchini China na kuomba kuendelea kushirikiana katika masuala ya tafiti mbali mbali baina chuo cha Diplomasia nchini na vyuo vyao vya Diplomasia vya China.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi tuzo ya kutambua mchango wake katika kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na China Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini Dkt. Lu Youqing alipotembelea ofisi kwake leo Jijini Dar es Salaam.  

MAGAZETI YA IJUMAA LEO SEPT 8,2017

SERIKALI KUONGEZA FURSA ZA WAHANDISI

0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi, amesema Serikali inafanya jitihada za kipekee kuongeza idadi ya wahandisi nchini ili kuiwezesha nchi kuwa na rasilimali watu ya kutosha katika fani ya Uhandisi, Sayansi, Hisabati na Teknolojia na hivyo kuharakisha ujenzi, ustawi, maendeleo ya viwanda na miundombinu.

Akizungumza katika madhimisho ya 15 ya Wahandisi yaliyoanza leo mjini Dodoma, Mhandisi Balozi Kijazi ameitaka Bodi ya Usajili wa Wahandisi Nchini (ERB), kuhakikisha wahandisi wanaoongezeka wanakuwa na viwango vya kutosha vya kitaaluma, kiujuzi na maadili ili kuleta matokeo chanya ndani na nje ya nchi.

“Serikali itahakikisha inafanya kila namna kuongeza nguvu kazi ya kutosha hasa katika kipindi hiki cha kujenga uchumi wa viwanda ili kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto za miundombinu, kiuchumi na kijamii”, amesema Mhandisi Balozi Kijazi.

Ameongeza kuwa kutokana na mahitaji makubwa ya mafundi sanifu kwenye uendelezaji wa viwanda, Serikali kupitia Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), itatenga fedha kwa ajili ya kusomesha wataalamu hao kwa kiwango cha Stahahada (Diploma), katika vyuo mbalimbali nchini ili kupunguza uwiano baina ya wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo.

Aidha, ameipongeza Bodi hiyo kwa kusimamia utoaji wa mafunzo ya kuendeleza taaluma ya kihandisi yenye lengo la kuhakikisha wahandisi wanaendana na mabadiliko ya kisayansi na kiteknolojia katika utekelezaji wa majukumu yao.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, amesema kuwa Sekta ya Ujenzi itahakikisha taaluma ya uhandisi inakua kwa kuwaendeleza wahandisi kielimu na kimitaji ili waweze kujenga uchumi imara wa nchi na kuharakisha maendeleo.

Ameongeza kuwa Wahandisi wanaunga mkono nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kufikia uchumi wa kati kwa kupitia viwanda ili kukidhi matarajio ya wananchi katika nyanja mbalimbali ifikapo 2025.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ERB Mhandisi Prof. Ninatubu Lema, amemhakikishia Katibu Mkuu Kiongozi kuwa wahandisi wataendelea kufanya kazi zao kwa weledi, nidhamu na kuzingatia maadili yao ya kazi kama wanavyoapa kufanya hivyo.

Amemuomba Katibu Mkuu Kiongozi, kuboresha mazingira ya Wahandisi nchini kwa kuwapa miradi mikubwa ya ujenzi wahandisi wazalendo ili kuwajengea uwezo wa ujenzi na usimamizi wake.

Zaidi ya wahandisi 2000 wameshiriki katika maadhimisho hayo ya 15 ya wahandisi yenye kauli mbiu “Jukumu la Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati katika Kukuza Viwanda kwa Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi”, ambapo wahandisi 150 wamekula kiapo cha utii na uaminifu.

Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi, akihutubia wahandisi (hawapo pichani), katika sherehe za ufunguzi za Mkutano wa 15 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika leo mjini Dodoma.
Baadhi ya wahandisi wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi (hayupo pichani), katika sherehe za ufunguzi za Mkutano wa 15 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika leo mjini Dodoma.
Baadhi ya wahandisi wakila kiapo cha utii cha kihandisi katika Mkutano wa 15 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika leo mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi, akimkabidhi cheti Mbunge wa Bagamoyo ambaye pia ni Mhandisi Dkt, Shukuru Kawambwa mara baada ya kula kiapo katika sherehe za ufunguzi za Mkutano wa 15 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika leo mjini Dodoma. Watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Edwin Ngonyani, akishuhudia tukio hilo.

Wizara ya Afya Malawi Yatembelea Muhimbili , Waipongeza Kwa Kutoa Huduma Bora

0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea ujumbe wa wataalamu wa Afya kutoka Wizara ya Afya ya nchini Malawi.

Ujumbe huo umeongozwa na Katibu wa Afya nchini humo , Dk. Dan Namarika umehusisha Madaktari , viongozi pamoja na wataalam mbalimbali kutoka katika Wizara hiyo pamoja na taasisi nyingine za afya .

Akizungumza baada ya kupokea ujumbe huo , Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru amesema ujio wa watalaamu hao unatoa fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Juliethi Magandi amesema katika mwaka wa Fedha 2016-2017 Hospitali imehudumia wagonjwa wa nje Laki Nne , Thelathini na Sita Elfu na Miatatu Tisini na Nne wakati wagonjwa wa ndani waliohudumiwa ni Hamsini na Tisa Elfu na Miatano Hamsini na Tano.

Akizungumzia lengo la ujio wao , Katibu wa Afya wa nchi hiyo Dk. Dan Namarika amesema wamekuja kujifunza jinsi ambavyo MNH inafanya kazi na kutekeleza mipango yake .

Lengo la serikali ya Malawi na Wizara ya Afya kwa ujumla ni kuhakikisha inaboresha utoaji wa huduma hususani katika Hospitali za Umma nchini humo.Ujumbe usema kuwa umefurahishwa jinsi Muhimbili inavyotoa huduma za kibingwa na kusomesha wataalamu wa afya nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa mafunzo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na ujumbe kutoka Malawi ambao umetembelea hospitali hiyo LEO ili kujifunza jinsi inavyoboresha huduma za afya. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini Malawi, Dk. Dan Namarika.
Ujumbe kutoka Malawi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Museru.
Wakurugenzi wa Muhimbili wakiwamo watalaamu wengine wa afya wakimsikiliza Dk Magandi leo.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali (EMD), Dk Juma Mfinga akitoa ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na idara hiyo.
Ujumbe kutoka Malawi ukiwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili.

DC ASIA APIGA MARUFUKU WILAYA YA KILOLO KUTOA WAFANYAKAZI WA KAZI ZA NDANI

0
0
Na fredy Mgunda,Iringa.

Wananchi wa wilaya ya kilolo mkoani iringa watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamemalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza uchumi wa taifa.


Akizungumza wakati wa kuangalia amani ya wanafunzi wa darasa la saba waliokuwa wanafanya mitihani ya kuhitimu elimu ya shule ya msingi mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alisema sasa imefika mwisho wa wilaya hiyo kuwa soko la wafanyakazi wa ndani.


“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka iringa kilolo sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawakamata na kuwafungulia kesi serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Abdallah.Abdallah aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kuwapeleka shule watoto waliofaulu kinyume cha hapo wazazi watachukulia hatua kali.

“Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubari hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Abdallah


Aidha Abdallah aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo.“Acheni kuwavulia chupi wanaume mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu kama mimi ambavyo leo hiii nimekuwa kiongozi wenu kwa kwasababu nilikataa kuvua chupi nikiwa na umri kama wenu ndio maana leo hii nipo hapa”alisema Abdallah

Aidha Abdallah aliwapongeza walimu wa shule za msingi za wilaya ya kilolo kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza vizuri wilaya ya kilolo kupitia elimu.“Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu wa wilaya hii kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika wilaya yangu ya kilolo na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Abdallah

Kwa upande wake diwani wa kata ya boma la ng’ombe Anderson Mdeke alikiri kuwepo kwa tatizo la mimba shuleni limekuwa sugu hivyo wameanza kuridhibiti na limepungua kwa kiasi kikubwa.“Kwa kweli tatizo la mimba kwenye shule za kata yangu ya lipo na tumeanza kutafutia ufumbuzi ili kulikosesa kabisa ili watoto wetu wasome bila kuwa na buguza” alisema Mdeke

Naye mwalimu wa shule ya msingi Mwanzala Grace Magawa alikiri kuwepo kuwepo kwa mimba za utotoni katika  baadhi ya shule za msingi za wilaya ya kilolo kutokana mazingira yanayowakabili baadhi ya wanafunzi ndio husababisha mimba za utoto.“Mwanafunzi akirudi nyumbani anawakuta wazazi wake washakunywa pombe na hawana habari ya kuulizia maendeleo ya mtoto wake hivyo mtoto anaamua kufanya anachotaka kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha kutoka kwa wazazi wake au walezi wake” alisema Magawa.
Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa katika moja ya shule za msingi wilayani kilolo akiwa amefika kaunagalia hali ya mitihani inaendeshwani na usalama wake upoje 
 Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akizungumza na wanafuzi waliohitimu elimu ya shule ya msingi katika shule ya msingi Boma la ng'ombe wilaya kilolo mkoani Iringa 

KAIRUKI HOSPITALI YAZINDUA KITENGO CHA KUCHUJA DAMU KWA WAGONJWA WENYE MATATIZO YA FIGO

0
0
SPIKA Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda, amewataka watanzania kutumia Mfuko wa Taifa wa Bima hiyo ili kupata unafuu wa matibabu pindi wanapougua.

Wito huo alitoa jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti huyo wakati alipozindua kitengo cha kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo katika Hospitali ya Kairuki.Alisema, kutokana na gharama ya matibabu kupanda kila siku,kadi za  bima ya afya zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupata unafuu wa matibabu kipindi mgonjwa anapokuwa hana fedha.

Makinda, alisema bima hiyo inatoa fursa kwa wanachama kupata huduma za matibabu katika hospitali wanazoona zinatoa huduma nzuri na kumjali mgonjwa.

“Vituo vyenye huduma ya NHIF vinapaswa kutibia wagonjwa kwa kuwajali , kuwapenda pamoja na kuwa wakarimu kwa wagonjwa kwani huduma hii inasaidia sana watu hasa wale wanaougua magonjwa yenye kulipia  gharama kubwa,”alisema Makinda.

 Aidha alisema ni watu wachache ambao wanauwezo wa kujitibu bila bima ya afya lakini watu wengi wanategemea huduma hiyo kulingana na gharama kubwa za matibabu katika baadhi ya magonjwa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki Dk. Asser Mchomvu, alisema nchini Tanzania watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa  na magonjwa yanayosababishwa na matatizo ya figo.

“Kwa hivi sasa ugonjwa huo umeonekana kuathiri  kati ya asilimia 7 hadi 13 ya watanzania, wengi wao wakiwa wagonjwa wa  kisukari (Diabetes Mellitus)na shinikizo la damu(Acute Kidney  injury) ,”alisema.

Alisema kwa muda mrefu hospitali yao  imekuwa ikipokea wagonjwa wenye matatizo ya figo na kulazimika kuwapa rufaa kwenda nje ya hospitali hivyo kupitia kitengo hicho kitaweza kutibu wagonjwa 40 kwa siku.

Alisema kuwa kutakuwa na mashine  10 zenye uwezo wa kuwahudumia wagonjwa na hadi kufikia sasa wamepata kibali cha wizara husika ambapo miongoni mwa mashine hizo ipo ya  kuchuja damu itakayosaidia kuzuia uharibifu wa figo wa kudumu na wa muda hivyo kuokoa gharama.

Dk. Mchomvu, alisema hospitali hiyo inatarajia  kuongeza idadi ya mashine ili kuweza kuwahudumia wagonjwa wengi  pamoja na kutoa huduma ya kupandikiza figo na kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda (kushoto), akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha Kuchuja Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijjini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki, Kokushubila Kairuki.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda (kushoto), akipata maelezo alipotembelea kitengo cha kuchuja damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo.
 Dk. Muga akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda.
Dk. Muga akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Muuguzi wa Kitengo cha Kuchuja Damu, Eva Beatus.
 Jengo la Kitengo hicho.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live


Latest Images