Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1893 | 1894 | (Page 1895) | 1896 | 1897 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017. Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Mifuko ya Jamii ya PPF na NSSF limeingia ubia katika mradi huo wa uchumi wa viwanda chini ya Kampuni ya MKULAZI.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) akiangalia mbegu za miwa kabla ya kuzipanda katika eneo la Shamba la miwa alipowasili Gereza Mbigiri katika ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hotuba fupi kwa  Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Morogoro, Watendaji wa Kampuni ya MKULAZI pamoja na Wananchi wanaoishi jirani na Gereza Mbigiri katika ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim(hayupo pichani) namna Jeshi hilo lilivyojipanga katika kuhakikisha kuwa ufufuaji wa Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro unakamilika kama ilivyopangwa ambapo matarijio ni kuwa Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha sukari tani 50,000 kwa mwaka.


  0 0  0 0
  0 0

  WANAFUNZI wa shule ya Msingi ya Tusiime ya Tabata jijini Dar es Salaam, wametoa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa watu wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha Mama Teresa cha Mburahati, Dar es Salaam.

   Msaada huo ambao umetokana na michango ya wanafunzi wa shule hiyo ni pamoja na unga, mchele, mafuta ya kupikia na vinywaji vya aina mbalimbali.Akizungumza punde tu baada ya kukabidhi msaada huo, mmoja wa wanafunzi wa Tusiime, Agnes Heke  amesema walianza kuchangishana wenyewe kwa wenyewe muda mrefu lengo ikiwa ni kusaidia watu wanaolelewa kwenye kituo hicho.

  Alisema dhamira ya kusaidia wenzao wa kituo hicho inatokana na mafundisho ya upendo wanayofundishwa wakiwa shuleni Tusiime.“Tumekuwa tukifundishwa kuwajali wenye shida na kwa kweli tulianza kuchangishana muda na leo hii tumeona hiki tulichopata tuwape wenzetu, huu ni mwanzo maana kadri tutakavyokuwa tunapata tutarudi kuwasaidia,” alisema Agnes.

  Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo, Mkuu wa Taaluma wa shule hiyo, Maxon Wilson amesema  msaada uliotolewa na wanafunzi hao ni sehemu tu na wameahidi kuendelea na moyo huo wa upendo kwa wenzao.Alisema msaada uliotolewa na wanafunzi hao unadhihirisha kuwa mafunzo ya maadili na kuwapenda wenzao wanayoyafundisha yamewaingia vema na wanayazingatia kwa dhati.

  Mmoja wa wazee wanaolelewa na kituo hicho, Elizabeth Daudi, aliishukuru shule ya Tusiime kwa namna ambavyo imewafundisha wanafunzi wake kuwa na upendo kiasi cha kuamua kuchanga kwa ajili yao.“Msaada huu ni ishara kwanza mafunzo ya upendo mnayoyapata shuleni yamefanyakazi, hatukutarajia kupata msaada kama huu tunawashukuru na Mungu awazidishie,” alisema kwa niaba ya wenzake.

  Alishukuru msaada huo wa wanafunzi wa Tusiime kwani umekuja wakati muafaka kwani huwa wanaishiwa na vyakula mara kwa mara.“hatuna maneno ya kutosha kuelezea furaha yetu , tunaomba watu wengine waige mfano wa Tusiime, waone watu  wanaolelewa hapa ni wajamii nzima,” alisema.
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi  Tusiime, ya Tabata Dar es Salaam, Agnes Heke na Ibrahim Shaban wakikabidhi vyakula mbalimbali kwa Bi. Elizabethi Daudi asiyeona ambaye ni mmoja wa watu wasiojiweza wanaolelewa kwenye kituo cha Mama Teresa Mburahati jijini Dar es Salaam.Msaada huo umetokana na michango ya wanafunzi wenyewe.
   Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya  Tusiime ya Tabata wakiwa wamebeba vyakula mbalimbali na sabuni kwa ajili ya kutoa msaada kwenye kituo cha watu wasiojiweza wanaolelewa kwenye kituo cha Mama Teresa Mburahati jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetokana na michango ya wanafunzi wenyewe.      

                    

  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN akiangalia kofia iliofumwa kwa mikono wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Coco Blue Jambiani.

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa Mkoa wa Kusini Unguja liliofanyika jana kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani.


   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa Mkoa wa Kusini Unguja liliofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani.

  0 0


  0 0


  0 0

  Wakimbizi wa Burundi waliokimbia machafuko nchini kwao wataanza kurejea nchini kwao ifikapo Septemba 7 hadi Desemba 31, mwaka huu mara baada ya pande tatu ikiwemo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), kutiliana saini Mpango wa Kuwarejesha wakimbizi baada ya mkutano uliochukua takribani siku tatu katika kuandaa mpango huo.

  Wakitiliana saini makubaliano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania, Chansa Kapaya, mwishoni mwa wiki wote walikubaliana kutekeleza vipengele vilivyopo katika makubaliano hayo yakiwa na lengo la kuwarudisha wakimbizi walioomba kurejea nchini Burundi, baada ya hali ya Amani na utulivu kurejea.

  Akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano hayo Waziri Mwigulu, alisema umefika wakati wa wakimbizi wa Burundi kurudi nchini kwao kuungana na familia zao na ndugu waliobaki ili kusaidia kujenga uchumi wa nchi yao baada ya kuwa katika machafuko yaliyosababisha kukimbia nchi yao kwa muda mrefu.

  “Mimi kama mwanauchumi ninaona madai yao ya kurudi nchini Burundi kujishughulisha na shughuli za kilimo ni maamuzi mazuri huku pia wakisisitiza kurejea kwa Amani na Utulivu nchini kwao kuwa ni sababu ya msingi ya kufikia kuomba kurejea, sisi kama Serikali tutahakikisha zoezi hilo la urejeaji nchini kwao linaenda salama tukishirikiana na Serikali ya Burundi kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchini Burundi,” alisema Mwigulu.

  Naye Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye, amesema anaishukuru Serikali ya Tanzania na Watanzania wanaoishi kwenye maeneo yaliyotumika kuwahifadhi wakimbizi kwa ukarimu wao walioonyesha muda wote kwa raia kutoka nchini Burundi huku akisisitiza kurejea kwa hali ya Amani na utulivu ambao hapo mwanzoni ilitoweka.

  “Nawaomba wananchi wetu warejee nchini ili tuweze kuijenga Burundi yetu ambayo hivi sasa kuna Amani na utulivu, pia naishukuru Serikali ya Tanzania na Watanzania ambao wamekua wakiwaonyesha ukarimu wakimbizi kutoka Burundi na kuwapa hifadhi nchini hapa,”alisema Barandagiye.

  Kwa upande wao Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) kupitia kwa Mwakilishi wao nchini,Chansa Kapaya, wameahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha wakimbizi wa Burundi 6,800 walioomba kurejea nchini kwao wanasahiliwa na kurejeshwa kwao katika hali ya utu na usalama huku shirika hilo likizishukuru Serikali za Tanzania na Burundi kwa msaada wao walioupata katika kushughulikia masuala ya wakimbizi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba,akibadilishana nyaraka na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania,Chansa Kapaya(kulia) zenye makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye, akibadilishana nyaraka na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania, Chansa Kapaya (kulia) zenye makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Wajumbe kutoka Serikali ya Burundi wakiongozwa na Balozi wa Burundi nchini Tanzania,Gervais Abayeho wakiwa katika Mkutano wamakubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki,Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Wajumbe kutoka Mashirika mbalimbali ya kimataifa wakiwa katika Mkutano wa makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Na. Benedict Liwenga-WHUSM.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa pongezi za dhati kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youking kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka katika kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na China hususani katika nyanja za masuala ya habari, utamaduni, sanaa na michezo.

  Pongezi hizo amezitoa hivi karibuni wakati wa hafla ya kumuaga balozi huyo iliyowakutanisha baadhi ya Viongozi wa Chama cha Ushirikiano wa Rafiki wa Tanzania na China wakiwemo Waandishi wa habari.

  Moja ya mambo makubwa muhimu yaliyofanyika chini wakati wa kipindi cha Balozi Lu Youking ni tukio la utiaji saini mwezi Machi mwaka huu ambapo Serikali ya Tanzania na China zilitiliana saini Mkataba wa Ushirikiano wa Kiutamaduni wa Miaka mitatu ambao utawapa fursa vijana 200 kutoka Tanzania kila mmoja kwenda China kwa ajili ya kupata mafunzo katika nyanja mbalimbali za habari, sanaa na utamaduni.

  “Balozi Lu Youking umetuachia zawadi kubwa sana sisi Wanahabari wa Tanzania, sasa hivi mimi na wenzangiu Wizarani tunakamilisha utaratibu wa utekelezaji wa Mkataba huu ili tuanze kuutekeleza mapema iwezekenavyo”, alisema Dkt. Mwakyembe.

  Aliongeza kuwa, Balozi Lu Youking hivi karibuni ameshirikiana na Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki katika kuhakikisha kwamba Waandishi wa habari 10 kutoka Tanzania wanaondoka mwezi ujao kuelekea nchini China kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya habari.

  Kwa upande wake Balozi Lu Youking alisema kwamba, urafiki kati ya Tanzania na China umekuwa wa afya na imara zaidi ya nusu karne akikumbushia kuwa, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake aliwahi kusema kwamba, Tanzania ina marafiki wengi, lakini China ni zaidi ndiyo maana Rais wa China, Mhe. Xi Jinping alichagua Tanzania kuwa kituo chake cha kwanza Afrika wakati wa ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu kuwa mkuu wa nchi.


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia) akimpongeza Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youking wakati alipowasili kwa ajili ya kushiriki hafla ya kumuaga balozi huyo iliyofanyika katika mgahawa wa Great Wall Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wageni waalikwa pamoja na Viongozi mbalimbali waliohudhulia hafla ya kumuaga balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youking iliyofanyika katika mgahawa wa Great Wall Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youking akiongea na wageni waalikwa pamoja na Viongozi mbalimbali waliohudhulia hafla ya kuagwa kwake iliyofanyika katika mgahawa wa Great Wall Jijini Dar es Salaam
  Mwenyekiti wa Chama cha Ushirikiano wa Urafiki baina ya Tanzania na China, Dkt. Salim Ahmed Salim (kushoto) akimpongeza Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youking mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kumuaga balozi huyo iliyofanyika katika mgahawa wa Great Wall Jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)


  0 0  SERIKALI imesema hivi sasa inatoa sh. bilioni 22.2 kila mwezi ili kuboresha elimu ya msingi na sekondari hapa nchini.

  Kauli hiyo imetolewa jana (Jumamosi, Septemba 2, 2017) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. George Simbachawene wakati akizungumza na wahitimu 166 wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Martin Luther, kwenye sherehe za mahafali ya 10 zilizofanyika shuleni hapo katika Manispaa ya Dodoma.

  Waziri Simbachawene ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alisema Serikali itaendelea kuboresha elimu ya sekondari kwa kuajiri walimu wengi zaidi wa masomo ya sayansi.

  “Wazazi wa wanafunzi wanaohitimu tunawakaribisha kwenye shule za sekondari kwa sababu zote zina walimu wa kutosha, madawati na vifaa vya kufundishia. Kila mwezi tunatenga sh. bilioni 22.2 kuendesha shule za msingi na za sekondari hadi kidato cha nne,” alisema.Alisema hivi sasa, baadhi ya shule zinakabiliwa na changamoto ndogo ya upungufu wa walimu wa sayansi lakini nayo itatuliwa hivi karibuni kwa sababu vibali vya ajira vimeanza kutolewa.

  “Tunaendelea kuziboresha na tumeshuhudia miaka ya karibuni wanafunzi bora kitaifa wakitoka katika shule za Serikali ambazo wengi wamezoea kuziita ni shule za kata. Hakuna shule za kata. Zote ni zimejengwa na Serikali,” alisisitiza.“Ukienda vyuo vikuu, wanafunzi na ufaulu wa juu wengi wao ni wale waliotoka kwenye shule za Serikali,” aliongeza.


  0 0

                                         
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji katika mikoa yote nchini kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya viwanda mbalimbali katika maeneo yao.

  Amesema mpango wa Serikali wa kujenga uchumi wa viwanda unalenga kuinua uchumi wa Taifa kutoka wa chini kwenda wa kati, hivyo ni muhimu kuvifuatilia.Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumamosi, Septemba 2, 2017) alipozungumza na watendaji na wananchi wa mkoa wa Morogoro alipofanya ziara katika kiwanda cha Moproco.

  Alisema licha ya kukuza uchumi wa Taifa, viwanda vitasaidia katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana kwani vinauwezo wa kuajiri watu wengi.“Viwanda hivi vinatupa uhakika wa ajira nchini kwa sababu vinauwezo wa kuajiri watu wengi na wa kada mbalimbali, hivyo ni muhimu tukafuatilia utendaji wake.”

  Waziri Mkuu aliongeza kuwa mbali na kutoa ajira nyingi, pia viwanda vitawezesha wakulima kupata soko la uhakika la mazao yao na kukifanya kilimo kuwa na tija.Alisema kwa muda mrefu sekta ya viwanda nchini ilikuwa haifanyi vizuri jambo ambalo lilisababisha kuongezeka kwa tatizo la ajira na mazao yalikosa soko.

  Hata hivyo Waziri Mkuu alitoa wito kwa wafanyakazi walioajiriwa katika viwanda mbalimbali kuwa waaminifu ili kuviwezesha viwanda hivyo kuendelea na uzalishaji.Pia aliwataka wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ili kuviwezesha viwanda kuwa na uhakika wa upatikanaji wa malighafi ndani ya chini.

  Awali Meneja Mkuu wa kiwanda cha Moproco, Bw. Arif Abood aliiomba Serikali kuongeza kodi kwa mafuta yanayotoka nje ya nchi ili kulinda viwanda vya ndani.Alisema uingizwaji wa mafuta kutoka nje ya nchi kwa kiasi kukubwa ulichangia kufungwa kwa viwanda vya ndani vya mafuta kutokana na kukosa soko.

  Katika ziara hiyo Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mheshimiwa Charles Mwijage pamoja na maofisa wengine wa Serikali.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S.L.P 980,
  40480-DODOMA 
  JUMAPILI, SEPTEMBA 3, 2017.


  Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa akishiriki kupanda mbegu za miwa katika Shamba la Gereza Mbigiri kwa ajili ya maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro jana Septemba 2, 2017.Picha na ofisi ya Waziri Mkuu


  0 0

  Bodi ya Wadhamini wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, imekutana na viongozi wakuu wa Shirikisho katika Ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Sea Scape, Kunduchi, Dar es Salaam.

  Bodi hiyo imekutana na uongozi wakuu wa TFF jana Septemba 2, mwaka huu kwa mara ya kwanza tangu ithibitishwe na Mkutano Mkuu wa TFF.Madhumuni ya Bodi hiyo kukutana na viongozi wa TFF – Rais Wallace Karia; Makamu wa Rais, Michael Wambura na Kaimu Katibu Mkuu, Kidao Wilfred ni kufahamiana.

  Kwa upande wa Bodi walikuwa Mhe. Mohammed Abdulaziz, Mhe. Balozi Dk. Ramadhani Dau, Mhe. Abdallah Bulembo na Mhe. Stephen Mashishanga. Mjumbe Dk. Joel Bendera hakuhudhuria kwa udhuru.Kadhalika Bodi hiyo kwa mujibu wa katiba ya TFF, walipata nafasi ya kuchagua Mwenyekiti wa Bodi ambako Mhe. Mohammed Abdulaziz alichaguliwa kushika wadhifa huo. Mhe. Abdulaziz alikuwa Mlezi wa timu ya Daraja la Kwanza ya Kariakoo ya Lindi

  Kwa niaba ya Wajumbe wa Bodi, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhe. Mohammed Abdulaziz ambaye ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Lindi Mjini, aliupongeza uongozi mpya wa TFF ulioingia madarakani Agosti 12, mwaka huu akisema: “Mmeanza vizuri.”Kadhalika Mwenyekiti ambaye alipata kuwa Mkuu wa Mikoa ya Tabora, Tanga na Iringa kwa nyakati tofauti , aliahidi ushirikiano kwa uongozi wa TFF ambako kwa upande wa TFF, Rais Karia alipokea pongezi hizo na baraka tele za kuanza vema na ushirikiano.

  Mhe. Balozi Dk. Dau – alikuwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ni mwanafamilia ya mpira wa miguu aliyejitolea hata kwa nguvu zake binafsi kusaka vipaji vya mpira wa miguu kwa vijana.

  Mhe. Joel Bendera ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Ni Kocha wa zamani wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ aliyekuwa na mchango mkubwa kuifikisha kucheza fainali za Kombe la Mataifa Huru ya Afrika (CAN 1980) sasa michuano hiyo inafamika kwa jina la AFCON. Fainali za mwaka 1980 zilifanyika Lagos, Nigeria.

  Mhe. Stephen Mashishanga ni Mkuu wa zamani wa Morogoro mwenye historia nzuri ya unafamilia wa mpira wa miguu akitoa mchango mkubwa katika maendeleo tangu alipokuwa kiongozi hadi sasa. Pia alipata kuwa Mlezi wa timu ya Milambo ya Tabora iliyoshiriki Ligi Kuu Bara.

  Mhe. Abdallah Bulembo ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliyepata kuwa Makamu Mwenyekiti wa kilichokuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) – kwa sasa ni Shirikisho (TFF).
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mhe. Mohammed Abdulaziz (wa tatu kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wenzake na viongozi wa TFF mara baada ya chakula cha mchana na wachezaji wa Taifa Starts kwenye Hoteli ya Sea Scape, Kunduchi, Dar es Salaam Septemba 2, 2017. Wengine mstari wa mbele kutoka kushoto ni Ofisi Meneja wa TFF, Bi. Miriam Zayumba, Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Kidao Wilfred, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mhe. Abdallah Bulembo; Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mhe. Stephen Mashishanga; Rais wa TFF, Bw. Wallace Karia; Makamu Rais wa TFF, Bw. Michael Wambura na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mhe. Balozi Dk. Ramadhani Dau. Taifa Stars baadaye Jumamosi ilicheza na Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa na kushinda mabao 2-0. (Picha na TFF).


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua zoezi la Ulipaji wa fidia kwa Wakazi wanaopitiwa na Mradi wa uboreshaji wa Barabara kwa maeneo yasiyopangwa DMDP,ambao wataanza kulipwa Fedha zao kuanzia kesho sambamba na kufanya ziara ya ukaguzi wa Miundombinu ya Barabara.

  Mradi huo utahusisha  uboreshaji wa Barabara,Mabonde ya Mito, Ujenzi wa Mitaro ya Maji, Taa za Barabarani, Njia za watembea kwa Miguu, Vizimba vya taka, alama za Barabarani na Soko la Mwananyamala ambapo unagharimu kiasi cha Shilingi Billion 230.

  Miongoni mwa Barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami ni Barabara inayoanzia Morocco hotel hadi Sinza Kijiweni Km 5, Barabara ya Tandale Kisiwani kuelekea Mwananyamala na Barabara za Makumbusho, , TANESCO Msasani, Simu200, Kilungule na MMK.

  Makonda amesema mradi huo utafanya jiji la Dar es Salaam kuendelea kuwa la kisasa na kufikia azma yake ya Dar Mpya.Amewataka wananchi watakaolipwa fidia kuhakikisha wanazitumia fedha hizo vizuri kwa kutafuta makazi bora sehemu nzuri zaidi na pia kufanyia shughuli zingine za kimaendeleo zitakazo waingizia kipato.

  Aidha Makonda amesema kuwa Kata za Tandale, Mburahati na Mwananyamala zitaingizwa kwenye idadi ya Kata 14 zinazopandishwa viwango kwa kuwa Barabara za kisasa maana ya kuwa na Lami,Taa na Mitaro ya Maji.Hata hivyo amesema Mto Ng’ombe pia utatengenezwa kwa kiwango cha kisasa urefu wa Km 7.5 ili kuwezesha Maji kwenda moja kwa moja hadi Baharini kupitia eneo la Jangwani kutakapojengwa mfumo wa kusafirisha maji taka.

  Makonda amempongeza Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta na Manispaa hiyo na kuwataka kuhakikisha kila anaestahili kulipwa fidia analipwa kile anachostahili bila usumbufu.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akipata maelezo mafupi kutoka kwa baadhi ya Wananchi kuhusu maeneo ambayo miundombinu yake imekuwa kero kwa wananchi,ikiwemo makaravati yaliyoziba na mitaro 
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Watendaji wa wilaya ya Kinonondi akizungumza na baadhi ya wananchi walioko kwenye kituo cha daladala cha Simu 2000 
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Watendaji wa wilaya ya Kinonondi wakikagua miondombnu mingine ikiwemo madaraja na makaravati yaliyoziba,ambayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho 
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Watendaji wa wilaya ya Kinonondi wakikagua barabara ya Makumbusho mapema leo jijini Dar.Picha na Emmnanuel Masaka-Globu ya Jamii.


  0 0

  MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewataka watoto wanaojiandaa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu, waongeze bidii kwani dunia ya sasa hivi inataka wasomi.

  Mama Majaliwa ametoa wito huo jana (Jumamosi, Septemba 2, 2017) wakati akizungumza na wahitimu 166 wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Martin Luther, kwenye sherehe za mahafali ya 10 zilizofanyika shuleni hapo katika Manispaa ya Dodoma.

  “Ninawapongeza wanafunzi wanaohitimu lakini ni lazima mtambue kwamba huu siyo mwishi wa safari yenu ya masomo kwani dunia ya sasa inataka wasomi. Kwa hiyo, muongeze bidii hadi mfike elimu ya vyuo vikuu,” alisisitiza.

  Aliushukuru uongozi wa shule hiyo na walimu wote kwa malezi mema wanayoyatoa kwa watoto hao na kwamba mafunzo yao yanadhihirika miongoni mwa watoto kwa jinsi walivyolelewa kimwili, kiroho na kiakili.“Mtoto wangu nilimleta akiwa na miaka mitano, ameanza elimu ya chekechea na sasa anahitimu darasa la saba. Sasa hivi amekua na ana hofu ya Mungu, anatambua mema na mabaya, tunawashukuru sana,” alisema.

  Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Gilbert Nhuguti wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji ya shule, alisema kwa zaidi ya miaka mitano, shule hiyo ambayo ni ya kutwa na ya bweni, imekuwa na rekodi ya kufanya vizuri kiwilaya na kimkoa kwa kushika nafasi za kwanza.

  “Mwaka jana tulishika nafasi ya kwanza kimkoa na nafasi ya saba kitaifa kwa wastani wa daraja la ‘A’. Hata mwaka huu, kwenye mitihani ya majaribio (mock exams) tumeshika nafasi ya kwanza, tumepania kuchukua nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mwaka huu,” alisema.Alisema mafanikio hayo yanachangiwa na ubora wa walimu wa shule hiyo ambao wana shahada, astashahada na stashahada.

  Aliwataka wahitimu hao wawe mfano huko waendako, wamtangulize Mungu katika kila walifanyalo na wasiwe watu wa kutaka kupata makubwa bila kufanya kazi kwa bidii. “Fanyeni kazi kwa bidii na mafanikio yatakuja,” alisisitiza. Pia aliwataka waendeleza tabia ya kutunza mazingira popote pale waendapo.

  Naye Mbunge wa Mtera, Bw. Livingstone Lusinde ambaye alipewa nafasi kutoa nasaha kwa niaba ya wazazi, aliwataka wahitimu hao watambue kuwa wanapohitimu elimu ya msingi wajione kuwa wamejengewa msingi imara.“Kuhitimu elimu ya msingi ni sawa na kujengewa msingi imara wa nyumba. Kwa hiyo, mkauendeleze kwa kujenga matofali imara, hautakuwa na maana kama mtaujenga kwa kutumia matofali mabovu juu yake,” alisema.

  Wanafunzi wa darasa la saba kote nchini, wanatarajiwa kufanya mitihani yao ya kitaifa Septemba 6 na 7, mwaka huu.

  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  L. P. 980, 
  40480 – DODOMA. 
  JUMAPILI, SEPTEMBA 3, 2017.

  0 0  0 0


  Na Beatrice Lyimo- MAELEZO,DODOMA.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua mfumo wa kielektoniki wa kuandaa Mipango , Bajeti na Ripoti kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa(PlanRep) na Mfumo wa Uhasibu wa Utoaji wa Taarifa za Fedha kwenye Vituo vya Kutolea Taarifa(FFARS).

  Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, Mkurugenzi msaidizi anayeshughulikia masuala ya TEHAMA Ofisi ya Rais – TAMISEMI Baltazar Kibola amesema kuwa mifumo hiyo inatarajiwa kuzinduliwa Septemba 5, 2017 katika ukumbi wa LAPF Mkoani Dodoma.

  Akifafanua Bw. Kibola alisema kuwa lengo la mifumo hiyo ni kusaidia kuja na mfumo mmoja wa kitaifa utakaowezesha kuwa na utaratibu wa kuandaa mpango na bajeti ambapo utasaidia Hamlashauri zote nchini kuwa na muundo mmoja wa uandaaji wa mipango na Bajeti za Serikali.

  Aidha alisema kuwa lengo la Mradi wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) ni kushirikiana na Serikali katika kuimarisha mfumo ili kusaidia uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa katika ngazi ya kila kituo husika.

  Kwa upande wake Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha kutoka Mradi wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Dkt. Gemin Mtei alisema kuwa lengo la mradi huo ni kufanya maboresho ya mifumo katika Sekta za Umma ili kuongeza ufanisi.

  “Mradi huu unalenga kufanya maboresho katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la Utawala Bora, Rasilimali watu, Rasilimali Fedha na pia katika maeneo ya TEHAMA ambapo utasaidia ni namna gani mifumo inawezeshwa kufanya kazi kwa urahisi” amesema Dkt. Mtei.
  Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya TEHAMA toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Baltazar Kibola akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa kuandaa Mipango,Bajeti na kutoa Ripoti za Malaka ya Serikali za Mitaa utakaozinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Septemba 5,2017 mjini Dodoma kulia ni Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha kutoka mradi wa PS3 Dkt. Gemini Mtei na kushoto ni Mtaalamu kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Elisa Rwamiago.
  Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha kutoka mradi wa PS3 Dkt. Gemini Mtei akizungumzia faida za mfumo huo wakati wa mkutano na vyombo vya habari leo mjini Dodoma. Kushoto ni.Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya TEHAMA toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Baltazar Kibola.
  Mmoja wa Wataalamu kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Elisa Rwamiago akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo mjini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya TEHAMA toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Baltazar Kibola.(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo ,Dodoma.  0 0

  Kitengo cha Usajili wa Hati na Nyaraka katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kimefanya maboresho katika upatikanaji wa Hati na Nyaraka kwa muda mfupi zaidi na ilivyokuwa hapo awali.

  Akizungumza wizarani hivi karibuni; Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Hati; Bwn. Kastor Ngonyani alisema; Katika zoezi la usajili wa Hati mpya zilizokuwa zikiandaliwa kwa muda wa miezi mitatu toka tarehe ya kuwasilishwa kwa Msajili, sasa zoezi hilo linachukua wiki mbili tu. Ameeleza utaratibu huo umerahisishwa kwa kutumia mfumo wa Kielektroniki.

  Aidha, Bwn. Ngonyani alisema kwa nyaraka nyingine zinazohusu Ardhi, kama zile za Uhamisho, Mikopo na zile zisizohusu Ardhi/za mali zinazohamishika zinatumia wiki moja tu kuwa tayari kutoka tarehe ambapo nyaraka husika iliwasilishwa kwa Msajili wa Hati.

  Vile vile, Msajili alisema kwamba utoaji wa taarifa nyingine za upekuzi/ Search ambazo huhusisha taarifa mbalimbali kama vile; Kujua kiwanja ni cha matumizi gani, kina Hati au hakina, Mmiliki wake ni nani na taarifa zinazofanana na hizo kuhusu Historia ya kiwanja husika; " Sasa taarifa hizo zinapatikana kwa siku mbili tu, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo zoezi hilo lilikuwa linachukua wiki mbili, mwezi mzima au hata zaidi," alisema Bwn. Ngonyani.

  Bwn. Ngonyani alieleza jinsi ambavyo ofisi yake imekuwa na Hati na nyaraka mbalimbali za Wananchi ambao bado hawajafika kuchukua Hati na Nyaraka hizo, licha ya nyaraka hizo kuwa tayari kwa muda mrefu uliopita. Bwn. Ngonyani alitoa rai kwa Wananchi wote ambao walishafika katika ofisi yake kwa ajili ya kupatiwa huduma hizo wafike kuchukua Hati na Nyaraka hizo muhimu kwao.

  Ofisi ya Kitengo cha Msajili wa Hati ipo kisheria . Sheria zinazoainisha uwepo wake sambamba na majukumu yake ni ; Sheria ya Usajili wa Ardhi , Sura ya 334 ya Sheria za Nchi; Sheria ya Usajili wa Nyaraka, Sura 117 ya Sheria za Nchi; Sheria ya Uhamisho wa Mali/Usajili wa Mali zinazohamishika, Sura 210 ya Sheria za Nchi na Sheria za Usajili wa Majengo ( Unit Tittle Act).

  Na kitengo cha Mawasiliano Serikalini -Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi .

  Msajili wa Kitengo cha Hati; Bwn. Kastor Ngonyani akizungumzia Maboresho yaliyofanyika katika ofisi yake.

  Afisa katika Kitengo cha Hati akimhudumia mteja aliyefika katika dawati lake.

  Maafisa mbalimbali katika Kitengo cha Hati. Na wengine wa Idara mbalimbali za Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiendelea kuhudumia Wananchi katika Kituo cha Huduma kwa Mteja Wizarani hapo.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, Jumanne wiki hii ataanza ziara rasmi nchini Tanzania ambapo anategemewa kufanya mikutano na mazungumzo na maofisa waandamizi wa serikali na wadau. 

  Bw. Graziano da Silva anategemewa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.

  Mkurugenzi Mkuu wa FAO amepanga kufanya mikutano na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Tanzania Bara), Dkt. Charles Tizeba, na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed.

  Ziara hii ya Mkurugenzi Mkuu inakuta wakati FAO ikiadhimisha miaka 40 toka kuanza shughuli zake hapa Tanzania. Wakati wa ziara hii, Bw. Graziano da Silva atakutana na uongozi na wafanyakazi wa FAO hapa Tanzania kabla ya kuhudhuria hafla maalum hapa Dar es Salaam kusherehekea maadimisho hayo. Hafla hiyo itahudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan. 

  Mwakilishi Mkazi wa FAO hapa nchini, Bw. Fred Kafeero, amethibitisha kuwa Bw. Graziano da Silva atakuwa hapa nchini kufuatia mwaliko wa Serikali ya Tanzania. “Mkurugenzi Mkuu wa FAO atabadilishana mawazo na Serikali ya Muungano wa Tanzania kwenye masuala makuu yanayohusiana na uhakika wa chakula na maendeleo ya kilimo, ikijumuisha juhudi za FAO kitaifa na kikanda,” alisema. Bw. Graziano da Silva pia atajadili mambo mengine yanayohusiana na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na FAO, pia masuala mengine ya umuhimu kati ya pande hizo mbili, aliongeza. Mbali ya Maafisa wa Serikali, Mkurugenzi Mkuu atakutana na wadau wengine wa FAO hapa nchini wakiwa ni pamoja na asasi za kiraia, taasisi za elimu, na taasisi za utafiti. 

  Baadae Mkurugenzi Mkuu ataenda Zanzibar ambapo, miongoni mwa mambo mengine, anategemewa kuweka jiwe la msingi katika jingo la Mradi wa Kuzalisha vifaranga vya samaki unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Korea kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa KOICA. Pia Bw. Graziano da Silva atapata fursa ya kutembelea mradi wa kilimo cha mwani na pia kuona maonesho ya bidhaa mbali mbali zilizotengenezwa na wanawake wanaojihusisha na kilimo cha mwani. 

  Tanzania ilijiunga na FAO mwaka 1962, na mwaka 1977 FAO ilifungua ofisi zake hapa Tanzania. Katika miaka 40 ya uwepo wake, FAO imeisadia Serikali ya Tanzania katika kupanga na kutekeleza sera, mikakati na mipango ya kilimo hapa nchini. Kazi ya FAO imejikita katika kuboresha usalama wa chakula na lishe pamoja na maisha ya wakulima wadogo na hivyo kuwa chachu ya kukua kwa uchumi kupitia sekta ya kilimo.

  0 0

  NA HAMZA TEMBA - WMU.
  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imeunga mkono uamuzi uliofikiwa na kamati maalum iliyoundwa na Serikali ya Wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya kumaliza mgogoro wa ardhi baina ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan na wananchi wa kitongoji cha Uvinje walioanzisha makazi ya kudumu ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan kinyume cha sheria.
  Kamati hiyo iliyoundwa na wajumbe watatu ambao ni Serikali ya Wilaya ya Bagamoyo, Uongozi wa Kitongoji cha Uvinje na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) kupitia Hifadhi ya Taifa ya Saadan ilifikia maazimio kuwa wananchi wa kitongoji hicho walioanzisha makazi ndani hifadhi hiyo waondolewe kwa utaratibu wa kulipwa fidia ili kumaliza mgogoro huo.


  Akizungumza na waandishi wa habari jana Wilayani Bagamoyo, Mwenyekii wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Ndetiye alisema baada ya kutembelea eneo hilo wamejiridhisha kuwa Kitongoji hicho cha Uvinje kimeanzishwa ndani ya eneo la hifadhi ambapo ni kinyume cha sheria. 


  "Kiuhalisia tumeona kuna kitongoji ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan, tumewasikiliza wananchi, tumesikiliza upande wa Serikali, kwa mujibu wa taratibu na sheria wale wananchi wanapaswa watoe ushirikiano, tunaamini kuna taratibu za Kiserikali zinafanywa kuhakikisha wale wananchi wanalipwa ili waondoke kwa usalama" alisema Ndetiye.


  Aliongeza, "tumeona jinsi ambavyo baadhi ya wananchi hawako tayari kulipwa, lakini nadhani wakieleweshwa vizuri wataelewa kuwa ile ni hifadhi ya Taifa, na kama ni hifadhi ya Taifa basi inahusu maslahi ya Taifa, hivyo kila mwananchi anatakiwa atoe ushirikiano ili angalao Serikali ifanye uwekezaji wa kueleweka"


  Ndetiye alisema kamati hiyo imeshaweka maazimio kwa ajili ya kushauri Bunge ili liazimie ni nini kifanywe na Serikali kumaliza mgogoro huo. Alisema, "Kwa udharura wake na kutokana na maelezo ya mkuu wa Wilaya, kwa ujumla kamati inakubaliana nayo kwasababu ameeleza vitu ambavyo tumeona vina tija zaidi kwa watanzania na tunaenda kulishauri Bunge na Serikali haraka iwezekanavyo ili hatua ziweze kuchukuliwa kumaliza mgogoro huo".
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Ndetiye kwa ajili ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan hususan eneo lenye mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji cha Uvinje na Hifadhi hiyo wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa tatu kushoto) akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Uvinje wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani humo jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.Wengine pichani ni Naibu Waziri,Wizara ya Maliasili, Mhandisi Ramo Makani(wa pili kulia) na  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga (kulia).
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kushoto) akiongoza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kutembelea eneo lenye mgogoro baina ya Kitongoji cha Uvinje na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye eneo hilo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa nne kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga (wa pili kushoto).
   Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Uvinje wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani humo jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.  Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye.

  Nyumba inayodaiwa kuwa ni ya muwekezaji anaeshikilia moja ya eneo katika hifadhi ya taifa ya Saadan kwa madai kuwa alipimiwa eneo hilo na Serikali. Taarifa zilitolewa ni kuwa eneo hilo lilipimwa kiholela bila ya kufuata taratibu za kisheria. Hata hivyo licha ya muwekezaji huyo kutoka nchini Botswana kukaa katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka tisa ameonekana hajaendeleza eneo hilo kwa lengo lililokusidiwa.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1893 | 1894 | (Page 1895) | 1896 | 1897 | .... | 3282 | newer