Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia) akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, kutembelea Mapango ya Amboni Jijini Tanga leo. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Atashasta Ndetiye (wa pili kushoto), Wajumbe wa kamati hiyo, Nape Nnauye (kushoto) na Shaban Shekilindi (kulia).
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia sehemu ya barabara iliyomeguka ndani ya eneo la Mapango ya Amboni.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakisikiliza maelezo kuhusu mapango hayo kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Jumanne Gekora.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii muda mfupi kabla ya kuanza ziara ya kuingia ndani ya mapango ya Amboni. Mhandisi Makani alisema mipango ya Serikali ni kutambua vivutio vya aina mbalimbali ikiwemo vya mambo ya kale kama yalivyo mapango ya Amboni kuviboresha na kuvitangza ili vichangie zaidi katika pato ta taifa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani na baadhi ya wajumbe wa msafara huo wakiwa ndani ya mapango ya Amboni.