Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 187 | 188 | (Page 189) | 190 | 191 | .... | 3270 | newer

  0 0

  DSTV pamoja na AIRTEL wanakuletea special Viewing party ya Big Brother Eviction Show Kila Jumapili ndani ya NYUMBANI LOUNGE kuanzia saa mbili usiku. Wiki hii Ndani ya Big Brother Rapper Mtanzania WAKAZI atatumbuiza.

  0 0

   Tofauti na tamaduni za mikoa mingine, huku Mkoani Kilimanjaro wakinamama ndio wafanyabiashara wakubwa wa biashara za mtaani a.k.a Machinga. Kamera Yetu leo hii ilikuwa ikivinjari katika kona mbali mbali za Mji wa Moshi mjini na kushuhudia harakani mbali mbali za wakinamama hao wa mkoa huu wakiwajibika katika biashara hizo. 
   Mwanamama akipanga Biashara yake ya Mabegi.
   Hapa napo ni Biashara ya Soksi za kina Baba.
   Kina Mama hao pia wanauza Viatu vya Kinadada pia.


  0 0

  Wananchi mbalimbali wakipita katika banda la Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC kuangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wajasiriamali wahapa nchini kwenye maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
  Wananchi wakipita kuangalia bidhaa za wajasirmalai wadogo hapa nchini walioko kwenye banda la Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio akimpa maelezo Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo alipotembelea katika banda la PPF katika maonyesho ya 37 ya kimataifa ya biashara katika viwanja vya Sabasaba.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi Joyce Mapunjo, pembeni yake ni Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade Bi Jacqueline Maleko.
  Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio akimsindikiza Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue na ujumbe wake mara baada ya kutembelea banda la PPF.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira Mh. Eric Shitindi akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa PPF Bwana Thomas Chissanga. Katikati ni Meneja Uhusiano na Masoko wa PPF Bi Lulu Mengele.
  Meneja Uratibu wa Ofisi za Kanda za PPF Bwana Mbaruku Magawa akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira Mh. Eric Shitindi alipotembelea banda la PPF. Kulia ni Meneja Uhusiano na Masoko Bi Lulu Mengele.
  Afisa wa Sheria wa PPF Bi Nyambilila Ndoboka akimpa maelezo Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira Mh. Eric Shitindi. Pembeni ni Mameneja wa PPF, Bwana Mbaruku Magawa na Bi Lulu Mengele.

  0 0

   Mshindi wa Redd's Miss Temeke 2013, Sviona Nyameyo (katikati), ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akiwa na mshindi wa pili,  Narietha  Boniface, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS), na mshindi wa tatu,  Latifa Mohamed ambaye ni muhitimu wa kidato cha sita baada ya kutangazwa washindi katika shindano hilo lililofanyika TCC Club Chang'ombe, Dar es Salaam 

  0 0

  BINGWA wa mchezo wa Kick Boxing nchini Chapion Japhert Kaseba ameingia katika fani ya utoaji filamu za mapigano Live akianzia na picha yake ya kwanza itakayo mtambulisha inakwenda kwa jina la Bongo Mafia

  Filamu hiyo iliyo rekodiwa katika ubora wa hari ya juu sasa ipo mtaani Ikisambazwa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya wapenzi wa filamu nchini wajionee vitu tofauti kidogo kwani kuna wakali kibao alio washirikisha 
  Picha hiyo ni mfululizo za picha zake nyingine ambazo zipo njiani kwani amekuja kufanya kazi katika jamii  ili watambue ipi pumba na upi mchele
  Bongo mafia ilioshilikisha wasanii kama vile ,Dotnata,Kelvin,Muhogo Mchungu,Pendo Njau Champion na Rogers MASTER SHIVO,na Wasanii wengine kibao

  Amesema filamu hiyo kwa sasa ni gumzo mtaani wakati ndio kwanza inamaliza wiki moja tangu kuingia sokoni 

  Kaseba ambaye hivi karibuni ali mdunda bondia Rasco Simwanza wa Malawi amejitamba kuendeleza ubabe  kwa mabondia wengine huku akifanya kazi zake za sanaa ambazo kwa kiasi kikubwa anamshukuru sana Dotnata kwa kuona kipaji chake hicho ambacho kilikuwa kimejificha na sasa kipo mtaani

  Kaseba amesisitiza kwa mashabiki wake wamuunge mkono kwa kununua kazi hiyo kwani ndio kwanza ananza kulishika soko la filamu hapa nchini endapo wataendelea kumunga mkono na ndipo watakapofuraia kazi zake nyingi zilizopo jikoni kwani nina kazi tofauti tofauti Nne hivi na sijui nianze na ipi ndio mana nimeamua kutoa hii kwanza alisema Kaseba

  0 0

  Mrakibu wa Magereza na Mtaalam wa Kilimo wa Jeshi la Magereza, Daimu Mmolosha akiwaeleza Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania aina mbalimbali za mbegu zinazozalishwa katika Mashamba ya Jeshi la Magereza  zikiwemo Mbegu za Mahindi, Maharage na Karanga kama zinavyoonekana katika picha( mwenye Vazi la Pinki) ni Mhe. Jaji. Imani Abooud na wa pili kutoka kulia ni Mhe. Jaji. Ibrahim Mipawa( wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Julius Sangu'di( Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Mdau Steve Kileo na Mai Waifu wake Neema wakibeba keki kuipeleka kwa wazazi,katika mnuso wa kumeremeta kwao unaoendelea hivi sasa kwenye ukumbi wa Hellenic club jijini Dar. Video na Picha zaidi zitawajia baadae.

  0 0  0 0

   Pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Malawi, mheshimiwa Patrick Lusiano Tsere, akitoa msaada wa chakula cha mahindi, kwa wananchi wa Malawi ambao ni wakazi wa wilaya ya Mangochi walioathirika na mafuriko. Balozi Tsere aliongozana na mabalozi wa Msumbiji, Zambia na Zimbabwe kukabidhi msaada huo.

  0 0

   Mmoja wa Wafanyakazi wa Kampuni ya Smile Wauzaji wa Router kwa ajili ya matumizi ya intaneti akiwa na tabasamu la nguvu kama jina la kampuni anayoifanyia kazi katika banda lao lililopo katika Viwanja Vya Sabasaba
   Bwa Deogratias Kabeho, Meneja wa Mauzo wa Kampuni ya Smile (Wa kwanza Kushoto) akiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake katika banda lao lililopo Katika Viwanja Vya Sabasaba barabara ya Kilwa Jijini Dar Es Salaam.
   Wafanyakazi wa Smile wakiwahudumia wateja waliofika katika banda lao kwaajili ya kupata maelezo juu ya kufungiwa router za smile ambazo zina spidi ya hali juu kabisa kuliko mitandao mingine ya intanet hapa nchini,nyuma yao ni runninga inayoonyesha video za muziki unaochezwa katika laptop iliyounganishwa na intanet ya Smile yenye Spidi ya 4G LTE
  Wafanyakazi wa Kampuni ya Smile inayohusika na ufungaji na uuzaji wa router za intanet zenye spidi ya 4G LTE wakimuelekeza mteja wao aliyefika katika banda lao lililopo katika viwanja vya sabasaba kwaajili ya kupata huduma ya kufungiwa intanet na kampuni ya Smile ambayo ina spidi ya hali ya juu ya 4G LTE.Picha na Josephat Lukaza wa http://josephatlukaza.blogspot.com
  ..............
  Smile ni Moja ya Kampuni inayotoa huduma za ufungaji wa Intanet kwa kutumia router ambazo unaweza kuunganisha mpaka kompyuta sita hadi 10 na zaidi na kwa spidi ya juu kabisa ya 4G LTE.
  Smile ndio kampuni pekee ya inayotoa huduma ya kufunga intanet yenye spidi ya juu ya 4G LTE peke yake nchini Afrika Mashariki.
  Vilevile Smile wanauza router zao kwa bei nafuu kabisa ambapo mteja akinunua router pamoja na modem zaoo anapata kifurushi cha GB 20 ambacho mteja ataweza kuperuzi mitandao mbalimbali kwa spidi ya Juu kabisa ya 4G LTE.
  Watembelee katika banda lao lililopo sabasaba kwaajili ya kupata maelezo na vilevile kujipatia modem na router zao ili uweze kupata huduma nzuri na bei nafuu kuliko zote nchini Tanzania.

  0 0


  Mpango wa Afrika Kujithmini Kiutawala Bora (APRM) umesema kuwa Serikali ya Tanzania imeanza kutekeleza maoni ya wananchi yaliyotolewa kwa nyakati mbalimbali nchini na kuingizwa katika ripoti ya Mpango huo.

  Maoni hayo yalihusu masuala ya katiba, siasa demokrasia, namna nchi inavyosimamia uchumi na pia wananchi wengi walizungumzia masuala ya upanuaji wa huduma za kijamii kama afya, elimu na nishati uwekezaji na migogoro mbalimbali.

  Akizungumza kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa APRM Tanzania, Bw. Hassan Abbas alisema ingawa ripoti hiyo itazinduliwa rasmi hivi karibuni, tayari baadhi ya masuala yameanza kufanyiwa kazi na Serikali.

  “Ripoti yetu ya APRM baada ya Rais Jakaya Kikwete kuiwasilisha kwa wakuu wenzake wa APRM Januari mwaka huu hivi sasa inasubiri kuzinduliwa rasmi. Hata hivyo tayari Sekretarieti ya APRM Tanzania ilipeleka baadhi ya masuala yaliyomo na kuingizwa katika baadhi ya Bajeti za Serikali.

  “Pia masuala yote yanayohusu Katiba yaliwasilishwa kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kote huko tumeona masuala kadhaa ya msingi kutoka Ripoti ya APRM yamefanyiwakazi,” alisema Bw. Abbas.

  Kwa mujibu wa Bw. Abbas kabla na hata baada ya uzinduzi huo miongozo ya uendeshaji ya APRM imeainisha kuwa ni muhimu kuwapa mrejesho wananchi walioshiriki katika kuishauri Serikali yao.

  “Kwa hiyo tunaandaa namna ya kuhakikisha tunawapa mrejesho wananchi wote walioshiriki zoezi la awali na hata ambao hawakushiriki ili wafahamu masuala ya msingi yaliyoingizwa kwenye Ripoti ni yapi ili nao wafuatilie utekelezaji wa masuala hayo kadiri Serikali inapokuwa inafanya hivyo,” aliongeza.

  Aliongeza kuwa utafiti wa APRM umehusisha wananchi na wataalamu ambapo maoni yalitolewa katika maeneo makuu manne ya utafiti ambayo ni demokrasia na utawala bora katika siasa; utawala bora katika mashirika ya umma; utawala bora katika uendeshaji wa makampuni na utoaji wa huduma za kiuchumi na kijamii.

  Akieleza chimbuko la APRM, Bw. Abbas alisema kuwa ni mpango endelevu uliobuniwa na viongozi wa Afrika katika kikao chao cha mwaka 2003 ambapo walikubaliana kuweka utaratibu wa kila nchi kuanzisha taasisi hiyo na kisha kuipa jukumu la kufanyakazi ya kujitathmini mara kwa mara katika nyanja za utawala bora.

  Bw. Abbas aliongeza kuwa kwa mujibu wa Mkataba huo wa Afrika, APRM sio kitu cha mara moja, ni taasisi yenye malengo ya kudumu ambapo kila nchi iliyojiunga itaendelea kuwa ikitathminiwa kila baada ya miaka minne.
   
  Taarifa zinaoneshan kati ya nchi 33 za Umoja wa Afrika zilizojiunga na APRM, tayari nchi za Kenya, Rwanda, Ghana na Nigeria zilikwishakamilisha tathmini ya mwanzo na sasa zinajiandaa kufanyiwa tathmini ya pili ili kubaini changamoto mpya na kuzifanyikakazi.

  0 0

  US President Barack Obama responds to a question regarding DRC during a joint press conference with President Jakaya Kikwete at the State House in Dar es salaam on July 1, 2013

  0 0

   Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki akiongea na waandishi wa habari juu ya siku ya LAPFiliyofanyka katika viwanja vya Saba Saba jijini Dar es salaam. Alizungumzia pia juu ya juu ya tuzo iliyotolewa na SSRA kwa LAPF kwa kuwa mfuko wa Hifadhi ya Jamii unaokua kwa kasi zaidi kwa idadi ya wanachama ukilinganisha na mifuko mingine.
   Maofisa wa LAPF wanashiriki katika Maonesho ya Saba Saba wakiwa tayari  kuwahudumia wananchi watakaotembelea banda lao
   Afisa wa LAPF John Masawe akitoa maelezo kwa mwanachama aliyetembelea banda la LAPF.
   Afisa Masoko wa LAPF Rehema Mkamba akitoa maelezo kuhusu Ushiriki wa LAPF katika maonesho ya Saba Saba.
  Wanahabari wakipata maelezo juu ya mafanikio na utendaji wa LAPF

  0 0

  I want to once again congratulate and thank all of you on behalf of Ambassador Sefue and myself - whether you were able to join us in Dar es Salaam or not - for all your Pre-Dialogue contributions, which helped to make Global 2013 one of our most successful Dialogues to date.  The theme of "Leveraging Technology for Africa's Socio-Economic Transformation - The Smart Partnership Way" provided the foundation for stimulating and invigorating discussions throughout.  

  0 0

  Kama ilivyo ada ya kila jumapili kufanya mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) pamoja, leo Wanabiafra wamekimbia zaidi ya kilomita nane katika kuadhimisha sikukuu ya saba saba. Mbio hizo zilianza majira ya saa 12:25 asubuhi yalipo makao makuu ya klabu kupitia barabara ya Kawawa hadi Moroko, barabara ya Kibaki hadi kwa Mwalimu Nyerere, barabara ya Rose Garden Hadi Sayansi, brabara ya Maji Machafu na kufuata barabara ya Akachube mpaka Peace Mwananyamala, barabara ya kwa Kopa, barabara ya Dunga hadi Hombus kisha barabara ya Kawawa hadi Msikiti wa Mtambani tukaingia "service road" ya upande Kinondoni Hospital mpaka Manyanya (Chimbinga) ambapo mbio ziliishia. Fuatilia matukio kwa picha mbalimbali!
  Maeneo ya kwa Nyerere


  Barabara ya kuelekea Rose Garden.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 07/07/13--03:59: Ramadhan
 • Inline images 1
  To all wadaus
  Enjoy peace and spirituality of the sacred month of Ramadhan.
  Its time to reboot your souls system and hit the restore button of your life

  0 0

   Nyota wa mchezo wa mpira wa miguu wa Marekani(American Football) Rays Lewis akimpa  RaisDkt. Jakaya Kikwete zawadi ya kofia yenye nembo ya timu yake wakati nyota huyo alipomtembelea Rais Kikwete mjini Arusha.Nyota huyo yuko nchini ambapo ni mmoja wa wafadhili wakubwa wa huduma kwa wagonjwa wenye ulemavu wa kusikia inayotolewa na taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani.Wagonjwa zaidi ya 3500 wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo inayotolewa bure na taasisi hiyo.
   Muasisi wa Taasisi ya Strakey Hearing Foundation  Bwana Bill Austin Starkey akimhudumia mtoto Lissa Frank(9) ambaye alikuwa kiziwi tangu kuzaliwa na kuweza kusikia baada ya kupata tiba na huduma ya kuwekewa kifaa maalumu katika kliniki maalumu iliyofanyika katika hospitali ya Seliani mkoani Arusha leo.
   Waasisi wa Taasisi ya Starkey Foundation Bwana Bill Austin Starkey(kulia aliyeinama) na Mkewe Tani Austin(Wapili kushoto) pamoja na mhudumu kutoka hospitali ya Seliani(kushoto) wakifurahi baada ya mtoto Lissa Frank(9) kuweza kusikia vyema baada ya kupatiwa matibabu katika kliniki maalumu iliyofanyika katika hospitali ya Seliani mjini Arusha leo(picha na Freddy Maro)
  ======  =====  =========
  WALEMAVU WA KUSIKIA WANUFAIKA NA HUDUMA ILIYOTOLEWA NA TAASISI YA STARKEY HEARING FOUNDATION.

  Na.Freddy Maro,Seliani Arusha.
  Julai, 7 ,2013.

  Zaidi ya Watanzania 3500 wenye maradhi ya kusikia wanatarajiwa kunufaika kwa huduma ya tiba inayotolewa na Taasisi ya Starkey Hearing Foundation yenye makao yake jijini Washington nchini Marekani.

  Muasisi wa Taasisi ya Starkey Hearing foundation  Bwana Bill Austin  Starkey ameyasema hayo wakati wa kliniki maalumu ya kuwatibu watu wenye maradhi mbalimbali ya kusikia iliyokuwa ikifanyika Katika hospitali ya Seliani mjini Arusha baada ya kutoa huduma hiyo katika miji ya Dar es Salaam na Moshi mkoani Kilimanjaro. 

  “Nimefurahishwa sana na kutiwa moyo kwa kazi tuliyoifanya ya kuwahudumia watu na kuwawezesha kusikia ambapo wengine ndiyo wameweza kusikia kwa mara ya kwanza tangu walipozaliwa.Furaha yao ni kitu cha kutia moyo sana katika juhudi zetu.Madaktari wa kitanzania tulioshirikiana nao wamefanya kazi kubwa na nzuri” alisema Bwana Starkey ambaye ameambatana na timu ya wataalamu na watu mashuhuri kutoka nchini Marekani ambao wametoa misaada mbalimbali kugharamia kampeni hiyo.

  Bwana Starkey amesema kuwa watu wengi walijitokeza wakati wa kliniki hiyo maalumu kwa watu wenye ulemavu wa kusikia na kuongeza kuwa katika siku tatu walizokuwa mjini Arusha wagonjwa zaidi ya 600 walipatiwa huduma hiyo ya matibabu  kwa kuwekewa vifaa maalumu katika masikio yako na kuwawezesha kusikia vyema na kusema kila mwaka shirika lake litafanya mipango ya kuhakikisha kwamba huduma hiyo inakuwa endelevu.

  Mwandishi wa habari hizi alishuhudia wazazi wenye furaha baada ya kuona watoto wao wenye umri kati ya miaka mitano na kumi wakiweza kusikia vyema kwa mara ya kwanza katika maisha yao  baada ya kupatiwa matibabu kwa kuwekewa vifaa maalumu katika masikio yao huduma ambayo imetolewa bure na shirika hilo na isingekuwa rahisi kuipata kwa watu wengi walio na kipato cha chini.

  Bwana Bill Austin Starkey aliwashukuru wafadhili mbalimbali waliowezesha mpango huo wa matibabu kufanikiwa  na kuongeza kuwa falsafa ya taasisi yake ni “Ili Dunia ipate kusikia” imeweza kutekelezwa kwa vitendo kwa sababu  anaamini kuwa kukiwa na nia ya dhat na moyo wa kushirikiana kutekeleza jambo fulani mafanikio ni bayana na mabadiliko mengi chanya yatawezekana katika ulimwengu.

  Bill Austin Starkey  na mkewe Tani Austin ambaye ni muasisi mwenza wa taasisi hiyo pamoja na washirika wao wanatarajia kwenda nchini Malawi kutoa huduma kama hiyo na baadaye kurejea tena nchini kutoa huduma  kabla ya kuondoka kurejea nchini marekani.

  Mmoja wa wataalamu wanaotoa huduma katika kliniki hiyoDkt. Ron Brouillete alisema mbali na kuzaliwa na ulemavu wa kutosikia wangojwa wengine waliotibiwa katika kliniki hiyo walipata madhara ya kutosikia kutokana na matumizi holela ya dawa ya kutibu Malaria aina ya Quinine.

  “Napenda kutoa ushauri kwa madaktari na wahudumu katika sekta ya afya kuepuka kuwapa dawa ya Quinine wagonjwa wa Malaria.Dawa hii itumike kwa uangalifu mkubwa na pale ambapo dawa nyingine zimeshindwa kumtibu Mgonjwa,” alisisitiza mtaalamu huyo kutoka nchini Marekani .


  Mmoja wa wafadhili wa mradi huo anayefuatana na Bwana Bill Austin Starkey ni mcheza mpira  wa miguu maarufu wa Marekani(American Professional Football) Bwana Ray Lewis ambaye pia anachezea ligi ya taifa ya mpira wa miguu ya nchi hiyo(National Football League).
   
  Awali Mchezaji huyo alimtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa mapumzikoni mjini Arusha na kusema kuwa Rais Kikwete ni mmoja kati ya viongozi mashuhuri barani Afrika wenye maono ya mbali na nia ya dhati ya kuwahudumia wananchi wake.

  “Nimesoma habari nyingi mambo mangi yenye mafanikio makubwa anayoyafanya Rais Kikwete na nilipopata fursa ya kuja nchini Tanzania nikatumia nafasi hiyo kuja kumsalimia,kumsikiliza na kumpongeza.Ni mtu mnyenyekevu sana na nimefurahi sana kumtembelea na kuongea naye,” alisema nyota huyo wa mpira wa miguu Marekani muda mfupi baada ya kukutana na Rais Kikwete ambapo alimzawadia kofia yenye nembo ya timu yake.

  Bill Austin Starkey na mkewe Tani Austin waliunda Taasisi ya Starkey Hearing foundation mwaka 1984 kwa lengo la kusaidia watu wenye maradhi ya kusikia na mpaka sasa maelfu ya watu katika sehemu mbalimbali duniani wamenufaika na huduma inayotolewa na taasisi hiyo.

  0 0

  Waimba injili Ambwene Mwasongwe (kulia) na Edson (kushoto) wakiimba sambamba katika Tamasha la Matumaini 2013.
  Edson kazini.
  Ambwene Mwasongwe.
  Sehemu ya nyomi ikilipuka kwa burudani.

  0 0

  Rais kikwete akifungua tamasha la matumaini hivi sasa uwanja wa Taifa,jijini Dar. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 187 | 188 | (Page 189) | 190 | 191 | .... | 3270 | newer