Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live

Taswira ya Kilele cha Mlima Kilimanjaro jioni ya leo kutokea Himo


sehemu ya maonesho ya sabasaba 2013

Abiria 18 wanusurika katika ajali milima ya usambara, Lushoto

$
0
0
Na Mashaka Mhando,Lushoto 
ABIRIA waliokuwa wakisafiri na basi dogo lijulikanalo kwa jina la Morama lenye namba za usajili T 284 AUH, wakitokea Tanga kwenda Lushoto, Alhamisi ilopita nusura wapinduke chini ya milima ya Usambara, baada ya basi hilo kukwepa fuso wasigongane uso kwa uso. 
 Tukio hilo limetokea majira ya saa 4:00 usiku katika kona iliyopo katika kijiji cha Bangala, nusura lisababishe maafa makubwa kwa abiria waliopakiwa kutokana na dereva aliyekuwa akienda basi hilo kukata ghafla kulikwepa fuso lililokuwa limesheheni makabichi kutokea Mlalo. 
 Mmoja wa abiria aliyekuwemo kwenye basi hilo, Bw. Shadrack Thobias alisema kabla ya kutokea tukio hilo dereva wao alikuwa akiyumba na kupotexza mwelekeo katika barabara hiyo ndogo nyembamba kulikosababisha na madai kwamba alikuwa amelewa viroba tangu aanze safari ya kupandisha katika milima hiyo. 
 "Tulipopita kwenye kizuizi cha polisi eneo la Bangala, askari polisi walitusimamisha wakazungumza na dereva pamoja na kondakta wake, walichukua muda mrefu, tulipoondoka kwenye kizuizi hicho dereva alianza kwenda mwendo wa kasi," alisema Thobias. 
 Alisema ghafla walikutana na fuso lililokuwa limebeba makabichi lakini sehemu ya barabara ilikuwa ndogo na walipopishana dereva wa basi ilibidi atoke barabarani lakini kule alipokuwa akikwepa fuso hilo, gari hilo liliserereka na kutaka kutumbukia chini ya milima lakini bahati nzuri difu ya gari iligonga chini ikawa inaning'inia kwenye miti iliyoizuia gari isitumbukie chini. 
 "Kwa kweli ni rehema za mungu tu ndizo zimetuokoa vimnginevyo ile gari ingetumbukia chini umbali karibu wa mita 200 kutoka juu ya barabara ni hatari sana lakini tatizo dereva wetu alikuwa aemekunywa viroba," alisema Thobias. 
 Waandishi wawili wa habari kutoka Jijini Dar es salaam, ambao hawakutaka majina yao yasitajwe hapa kwa kuwa walikuwa kwenye safari zao za binafsi, walisema kwamba tatizo kubwa lililosababisha ajali hiyo kutokea ni umakini mdogo wa dereva kulikosababishwa na kunywa pombe. "Kwa kweli jeshi la polisi linahitajika kufanya kazi zao ipasavyo kwa madereva wanaoonekana kukiuka sheria...Polisi waliokuwa kwenye kizuizi kile kama wangekuwa makini kwenye kazi zao pengine wangemropoa dereva asiendelee na udereva lakini hawakumpima wala kusikia harufu yake ya pombe," alisema mmoja wao ambaye anatangaza televisheni moja kubwa. 
Hata hivyo, Mkuu wa polisi wa wilaya ya Lushoto Bw. Zuberi Madafu alipoulizwa kuhusu kutokea ajali hiyo, alikiri kutokea lakini akasema kwamba basi hilo halikuwa na abiria hata mmoja wakati likipata ajali hiyo hata alipothibitishiwa kuhusu waandishi wa habari wawili kupanda humo bado alitetea kwamba halikuwa na abiria. 
 "Ni kweli basi la Morama limepata ajali lakini nilimtuma mkuu wa usalama barabarani amekwenda asubuhi leo (Ijumaa Julai 5) amekutana na wafanyakazi wa basi wamemwambia kwamba hawakuwa na abiria isipokuwa walikuwa wakilijaribu gari lao na walikuwa wakitokea Mombo kuja Lushoto," alisema OCD Madafu na kuongeza; 
 "Kama wapo abiria walipanda kwenye basi hilo na wakapata misukosuko hiyo waje kituoni waripoti ili tufungue kesi lakini tumeenda na wamesema hawakuwa na abiria wowote mle ndani,".
 basi la Morama likiwa limeziba barabara.
 Coaster liitwalo Tende Sheki likipita kwa tabu baada ya Morama kupata ajali eneo hilo
 mabasi yakiwa yamesimama.
 foleni ya mabasi yanayokwenda Lushoto
wafanyakazi wa Morama wakitafuta njia za kuliondoa gari lao

CRDB YAMWAGIWA SIFA KWA KUZIELIMISHA ASASI ZA KIFEDHA MKOANI IRINGA

$
0
0
 Mjumbe  wa bodi  kutoka  Faraja  Saccos Mafinga  Macelina Mkini akiishukuru  CRDB kwa mafunzo
Afisa  ushirika mkoa  wa Iringa John Kiteve

Na Francis Godwin
WAJUMBE  wa  bodi   za asasi za  kifedha mkoani  Iringa  wameipongeza  benk ya  CRDB nchini  Tanzania  kwa  kuanzisha utaratibu mzuri  wa kutoa elimu  kwa  wajumbe wa  bodi  za asas za kifedha  .
i
Pongezi hizo  zimetolewa na wajumbe hao  na mwakilishi  kutoka faraja  Saccos mjini Mafinga  wilaya ya Mufindi Bi Macelina Mkini  wakati akizungumza kwa niaba ya  wajumbe  wengine.

Amesema  kuwa hatua ya  CRDB nchini  kuendelea  kuzijali asasi  za kifedha ni sawa na kuisaidia  serikali ya  Tanzania katika kuwajengea  uchumi  wananchi kupitia  asasi za kifedha.

Hivyo  alisema kati ya benk zote nchi ni  CRDB pekee ambayo  imeendelea  kuwasaidia  wanachama wa Asasi za kifedha vijijini jambo ambalo  wao  wanalipongeza  zaidi.

Kwa upande  wake  afisa  ushirika  mkoa  wa Iringa  John Kiteve  alisema  kuwa mbali ya  kuwapongeza CRDB kwa jitihada hizo  ila bado yeye kama afisa ushirika hatawavumilia  viongozi wazembe ambao  wataonyesha  kukwamisha ushirika mkoani Iringa .

Aliwataka  viongozi  wa asasi za kifedha  mkoani Iringa na Mbeya  kuendelea  kujifunza namna ya  utunzaji wa fedha za wanachama na  iwapo hawatajifunza kwenda kisasa  wanaweza  kuyumba katika  utunzaji wa  fedha za wanachama.

Alisema kuwa suala la ubunifu na kujituma kwa wanachama ni mwanzo  wa Asasi  hizo kufanikiwa  zaidi na  kuwataka  viongozi  kuepuka kukata tamaa katika  kuziendesha  asasi hizo.

Hata  hivyo amewataka  wajumbe  wa  bodi  za asasi za kifedha  kuwa makini na matumizi ya  fedha  za  wanachama na kuepuka kukimbilia maisha ya  juu  kupitia fedha  za wanachama.

Alisema kuwa suala la uaminifu linahitajika  zaidi kwa  viongozi ikiwa ni pamnoja na viongozi hao  kuendelea  kujifunza na kutoa mafunzo kwa wanachama wake  ili kuwajengea uwezo  zaidi.

Kiteve  aliwataka  viongozi  wa Asasi za kifedha  kujenga utamaduni  wa kujitegemea zaidi  ili  siku ambayo CRDB itasitisha mpango  huo  wa kuziwezesha Asasi hizo  kuweza  kusimama  wenyewe kwa miguu yao.

mkaa ukisubiri kuingia mjini

$
0
0
Serikali imekuwa ikipiga vita sana kuchomwa kwa misitu katika maeneo mbali mbali hapa nchini,lakini kauli hiyo imeonekana kuwa kama haina nguvu sana kwenye maeneo mengi ya vijijini,kwani zoezi la kuchoma moto misitu na kuzalishwa magunia kwa maginia ya mkaa imekuwa ikichukua nafasi kubwa siku hadi siku.Kikubwa kinachostaajabisha ni pale kauli ya Serikali inapokuwa inapingana na baadhi ya watendaji wake,kwani kuna maeneo mbali mbali humo njiani kuna vituo vya kukusanya ushuru wa mkaa huu huu.....!!!ambao wateja wake wakubwa ni wakazi walio katika maeneo ya mijini.sasa nini kifanyike kuhakikisha misitu yetu inatunzwa na haichomwi tena??

KAMPUNI MPYA YA ROAD TO WELLNESS YAJA NA "LIPWA KWA WIKI"

$
0
0
 Muwakilishi wa Kampuni mpya ya Road to Wellness inayotoa fursa kwa watu mbali mbali juu ya Afya zao,Beatrice Owen (kulia) akitoa maelezo ya namna ya kuweza kupata fursa hiyo kwa mmoja wa wateja walioweza kuwatembelea katika banda lao namba 63 Jengo la Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa,yanayoendelea jijini Dar es Salaam.Kampuni hiyo ambayo ni changa kabisa yenye maskani yake Mwenge karibu na Stendi ya Daladala Mkabala na Tamal Hotel,imejitokeza kwenye Viwanja vya Sabababa ili kuweza kuwapatia watu mbali mbali fursa ya maswala ya afya.unaweza wasiliana nao kwa Namba hizi 0654 083977 au Tembelea kwenye Banda lao ili uwezo kufahamu zaidi na zaidi mambo ya Afya.
Mmoja wa Wafanyakazi wa Kampuni hiyo toka nchini Uganda,Murshid  Galiwango akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja wao.
Mwanadada Catherine Melkior wa Kampuni ya Road to Wellness (kulia) akielezea jambo kwa wateja wao waliowatembelea kwenye banda lao.
Wadau wa Kampuni ya Road to Wellness
Bango lao.

kwa wale watakaopenda kupata ripoti za namna hii inayotolewa kwa njia ya kidigitali,inapatikana kwa gharama ndogo kabisa.

IN LOVING MEMORY

$
0
0
THE LATE MZEE EUGENE SHIO 

It is 7 years down the line since you departed from us but still looks like yesterday. Remembering you is easy, we do it everyday. But missing you is a heartache which never goes away. We know you now live in our hearts and you have always continued to watch over us. We have to hide our heartache when someone speaks your name. Sad are the hearts that love you; silent tears that fall.

Living without you is the heartache part of all; you did so much for us, your heart was so kind and true and when we needed someone we always counted on you.

Thank you for the selfless love and kindness you shared with us all.

Greatly loved and missed by YOUR WIFE MAMA VERONICA, sons; Fr. Shio, Innocent, Eva, Furaha, Amani, Mapendo and Neema, Sisters Mkarubia, Anna and Matonoi, in-laws and the entire family.

In God’s hands you rest, in our hearts you remain forever.

SUMAYE AONGOZA WAPANDA MLIMA KILIMANJARO KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA UKIMWI

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi. 
 Jumla ya watu 38 wanashiriki zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro lijulikanalo kama Kili Challenge 2013 kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa UKIMWI. 
 Kundi hilo ambalo linaongozwa kwa kiasi kikubwa na wafanyakazi wa kampuni ya kuchimba madini ya  Geita wanaendelea na safari yao wakiwemo watoto 2 walioathirika na maambukizi ya VVU/UKIMWI wanaolelewa na Kituo cha Watoto Yatima cha Moyo wa Huruma wenye umri wa miaka 14 na 17. 
 Katika kundi hilo wamo pia raia sita kutoka Afrika kusini, raia mmoja kutoka Ghana, raia mmoja kutoka Australia na watanzania 27.
 Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akiwasili katia maeneo ya geti la kupandia mlima Kilimanjaro la Novatus Makunga
 Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akizungumza na wapanda mlima kutoka Geita Gold Mining.(hawako pichani) wakati wa uzinduzi wa changamoto ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangia fedha kwa waathirika wa VVU na UKIMWI.
 Wapanda mlima ambao wengi wao ni wafanyakazi wa Geita Gold Mining wakimsikiliza mgeni rasmi katika changamoto hiyo.
 Wapandaji wakipata picha ya pamoja na mgeni rasmi.
 Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akizindua changamoto hiyo mahususi kwa ajili ya kuchangia fedha kwa waathirika wa VVU na UKIMWI.
 Bango la wafadhili
Lango la Machame ambalo hutumika pia kwa kampuni ya Geita Gold Mining kuanzia safari ya kupanda mlima kwa lengo la kuchangisha fedha. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi


profesa lipumba aongoza mazishi ya mfanyakazi wa cuf muharami tanganyika

$
0
0
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akikabidhiwa daftari la michango wakati alipowasili Tabata, jijini Dar es salam, nyumbani kwa Marehemu Muharami Abdallah Shaaban Tanganyika aliyefariki juzi katika hospitali ya Amana. Marehemu alikuwa ni mfankazi ya ulinzi katika makao makuu ya CUF, Buguruni. Mwenye pama ni Naibu katibu Mkuu wa CUF Mhe. Julius Mtatiro
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiandika kwenye daftari la michango. Mwenye pama ni Naibu katibu Mkuu wa CUF Mhe. Julius Mtatiro na kulia ni kaka wa marehemu Ismail
 Sehemu ya waombolezaji
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akipata chakula na waombolezaji weng 
ine

 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiongea machache kabla ya safari ya kuelekea makaburini kuanza. Alimsifia marehemu Tanganyika kama mmoja wa wafanyakazi waaminifu na makini waliojituma sana. Pia alisema wamepoteza askari hodari ambaye alikuwa nguzo muhimu ya ulinzi katika makao makuu ya chama hicho cha ulinzi

Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiongoza mazishi hayo yaliyofanyika kwenye makaburi ya familia ya mama wa marehemu huko Segerea

MWAKILISHI WA FAO NCHINI ATEMBELEA BANDA LA UMOJA WA MATAIFA KWENYE MAONESHO YA SABASABA.

$
0
0
IMG_8897 
Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman (katikati) akipata maelezo ya kazi mbalimbali za Shirika hilo kutoka kwa Afisa Habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama wakati alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
IMG_8935
Mkufunzu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) Marwa Wambura (katikati) akimuonyesha Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman (kulia) malighafi za ngozi zinazotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali na wanafunzi wa Chuo hicho ambapo mafunzo hayo yanadhaminiwa na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza viwanda Duniani (UNIDO).
IMG_8946
Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman akiangalia viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na wanafunzi wa Chuo cha DIT kwenye banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
IMG_9000
Baadhi ya bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na Wanafunzi wa Chuo cha DIT cha Mwanza.
IMG_8976
Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman akizungumza na waandishi habari ambapo amefafanua changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia katika mabadiliko ya tabianchi ambapo wao kama Umoja wa Mataifa wanafanya kazi ya kuelemisha Umma, Wakulima, Wafanyabiashara na Wasindikaji jinsi ya kuelelewa mabadiliko ya tabianchi katika kukabiliana na tatizo la uhaba wa njaa duniani na upatikanaji wa chakula. Kulia ni Mratibu wa kazi za vijana vijijini katika masuala ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji wa FAO Bw.Eliamoni Lyatuu.
IMG_8968
Afisa habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akitoa ufafanuzi wa vipeperushi mbalimbali vinavyozungumzia kazi zinazofanywa na shirika hilo hapa nchini kwa baadhi ya vijana na watoto waliotembelea banda hilo leo kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar.
IMG_8980
Baadhi ya watoto waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa wakifurahia picha.

mnada wa hadhara....

CHEKA KUZICHAPA NA MMAREKANI KUWANIA UBINGWA WA DUNIA

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya 'Macho Yanacheka' na Bi Shakila si mchezo

mkataa kwao mtumwa

miondoko ya kumeremeta kwenye mnuso


rais kikwete na rais obama katika mkutano na wanahabari ikulu, dar es salaam, julai 1, 2013

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ATEMBELEA TAASISI ZA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KATIKA MAONESHO YA SABASABA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga (kulia) akimkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wizara pamoja na taasisi zake. Silima alitembelea taasisi zote za wizara zilizoshiriki maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akipimwa kilevi kwa kifaa maalum na Askari Polisi (kulia) wakati alipotembelea banda la Jeshi la Polisi katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakitoa vipeperushi vya wizara hiyo kwa wananchi na wanafunzi wa shule ya awali waliotembelea banda hilo katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia) akipewa taarifa za kazi mbalimbali zinazofanywa na Idara ya Uhamiaji na Afisa wa idara hiyo wakati alipotembelea maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji akimfundisha mwanafunzi wa shule ya awali jinsi ya kuzima moto wakati wa maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Julius Sang’udi (katikati) akimuonesha samani za ndani Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia) wakati alipotembelea banda la Jeshi la Magereza katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Picha zote na Felix Mwagara.

NMB wanogesha fainali Gambo Cup Korogwe

$
0
0
 Sehemu ya zawadi walizokabidhiwa washindi ambapo ilikuwa ni ng'ombe mmoja na mbuzi watatu.
 Waandaji na wasimamizi wa mashindano hayo viongozi wa KDFA wakipeana majukumu wakati wa fainali.
 mashabiki na wachezaji wa Mtonga FC wakishangilia ushindi
  mabingwa wapya wa mashindano ya Gambo Cup Mtonga FC baada ya kutawazwa mabingwa.
 baadhi ya wafanyakazi wa NMB tawi la Korogwe wakifuatilia utoaji wa zawadi.
 Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe Chiku Galawa akizungumza kabla ya kutoa zawadi.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akimpongeza mchezaji bora wa mashindano hayo aliyepata zawadi ya mpira.


Picha na Habari na
 Mashaka Mhando, Korogwe
MASHINDANO yaliyodumu kwa miezi mitano ya kugombea kombe la Mkuu wa wilya ya Korogwe Mrisho Gambo, 'Gambo Cup', yamefikia tamati kwa timu ya soka ya Mtonga FC, kutwaa kombe, Ng'ombe, jezi na mpira walizokabidhiwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni (mstaafu) Chiku Gallawa.
Fainali hiyo ilizozikutanisha timu zenye historia tofauti huku Mtonga timu iliyoundwa na vijana wadogo ilionekana kabla ya mchezo kuanza itafungwa na wapinzania wao Manundu United ambayo tayari imekuwa na udhoefu mkubwa hasa kutokana na kushiriki mashimndano makubwa yakiwemo Ligi ya Taifa ngazi ya Mkoa wa Tanga.
Lakini, vijana hao waliuanza mchezo huo mithiri ya nyati aliyejeruhiwa kisha kumsaka mbaya wake pale alipopata bao la kwanza lililofungwa na Selemani Msagama aliyeihadaa ngome ya Manundu kisha kuutumbukiza mpira kimiani kuandikia timu yake bao la kwanza dakika ya 29.
Manundu timu yenye mashabiki lukuki iliyoingia uwanjani kwa mbwembwe zote kuwagonga majirazi zao hao, walisawazisha bao hilo dakika ya 35 baada ya mchezaji wao mmoja kuwatoka mabeki wa Mtonga na kumimina majalo yaliyoungwanishwa vizuri kwa kichwa na Abdallah Shauri.
Mtonga ambao baada ya kunywakua kombe hilo, wameaahidi kujisajili mwakani ili washiriki Ligi ngazi ya wilaya, iliandika bao lake la ushindi dakika ya 43 lililopachikwa kimiani na Charles Daffa ambaye kabla ya kufunga bao hilo alimvika kanzu beki wa Manundu kisha kufunga kwa shuti kali.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, katibu wa Cha Soka wilayani Korogwe (KDFA) Zaina Hassain, walimshukuru Mkuu wa wilaya kwa kuanzisha mashindano hayo ambayo yame;leta changamoto mpya kwa vijana wilayani humo na kuibua vipaji kutokana na timu 84 kushiriki mashindano hayo katika ngazi ya kata.

Mkuu wa mkoa alisema kwamba mshindano hayo yamemfanya afikirie kuanzisha mashindano yake akishindanisha wilaya zote lengo likiwa ni kuibua vipaji na kuwafanya vifanya waweze kucheza wakiamini kwamba mpira wa soka miaka ya hivi karibuni ni ajira mojawapo kwa vijana.
"KWA kweli nimependa jinsi mlivyojipanga hadi mkafanikisha fainali hii nakupongeza Mkuu wa wilaya (Gambo) kwa kuandaa michuano hii...Nami nitaanzisha ya kwangu nitayaita Gallawa Cup, najua mtanisaidia kwa vile mmepata udhoefu na mna halmshauri mbili hapa," alisema Mkuu huyo wa mkoa.
Mashindano ambayo yamedhaminiwa na benki ya National Micro-Finance (NMB) waliotoa zawadi za vifaa pamoja na kombe, yalitia fora kwa kujaza watu wengi kwenye fainali hiyo ambayo msemaji mmoja alisema kwamba idadi ya watu walijitokeza kushuhudia fainali hiyo haijawahi kutokea kwenye uwanja wa Chuo Cha Ualimu Korogwe. Mashindano hayo yamefanyika kwa gharama ya shilingi milioni 21.
Mshindi wa kwanza alipata Kombe, Ng'ombe, Jezi seti moja na mpira, wakati mshindi wa pili alipata mbuzi wawili, jezi na mpira huku mshindi wa tatu akipata mbuzi mmoja, jezi na mpira, sambasamba na waamuzi kupewa zawadi ya fulani, firimbi huku viongozi wa KDFA wakipewa zawadi ya nyavu kwa ajili ya magoli.


Tanzania/Japan meet for their Annual Consultation meeting on Economic Cooperation

$
0
0

Dr. Philip Mpango, Executive Secretary of the President's Office Planning Commission gives his opening remarks during the meeting between Tanzania and Japan on economic cooperation of the two countries held yesterday at Hyatt Regency (Kilimanjaro) Hotel in Dar es Salaam.  Also in the photo is Ambassador Rajabu Gamaha (2nd right), Deputy Permanent Secretary of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.  

The Tanzania/Japan annual consultation meeting on economic cooperation is in session.  The two countries have been cooperating in various sectors that include water and sanitation, agriculture, roads projects, education and energy sectors as part and parcel of incorporating and implementing the Fifth Tokyo International Conference on Africa Development (TICAD V) declarations held a month ago in Yokohama City, Japan.  It is in that spirit that these projects are entwined with the Tanzania Development Vision of 2025, as continued efforts to revitalize the economic growth of the country.

Deputy Permanent Secretary Ambassador Rajabu Gamaha introduces himself during the meeting.  Also in attendance is Ambassador Salome Sijaona of the United Republic of Tanzania in Japan.

The meeting was also participated by Ambassador Mbelwa Kairuki (2nd left), Director of the Department of Asia and Australasia in the Ministry of Foreign Affairs, Mr. Kambona (3rd left), Foreign Service Officer in the Ministry of Foreign Affairs and Mr. Clifford K. Tandari (4th left), Deputy Executive Secretary  - International Trade and Economic Relations in the President's Office Planning Commission. 

Also in attendance is Mr. Ottaro (right), Assistant Director of the Department of Policy and Planning in the Ministry of Foreign Affairs. 

Ms. Yoshiko Kijima, Director - Third Country Assistance Planning Division, International Cooperation Bureau, Ministry of Foreign Affairs in Japan and H.E. Ambassador Masaki Okada of Japan to the United Republic of Tanzania. 

Mr. Kambona and Ambassador Kairuki. 


Tanzania delegation that included H.E. Ambassador Salome Sijaona, Ambassador of the United Republic of Tanzania in Japan. 

Japanese delegation that was led by Ms. Yoshiko Kijima, Director - Third Country Assistance Planning Division, International Cooperation Bureau, Ministry of Foreign Affairs in Japan and also included Mr. Motoharu Watanabe, DIrector of Africa Division 2/Africa Department in Japan Itnernational CooperationH.E. Masaki Okada, Ambassador of Japan to the United Republic of Tanzania. 

Secretariat team that included Mr. Khatib Makenga (left seating), Foreign Service Officer in the Ministry of Foreign Affairs and Mr. Senya R. Tuni (right), Senior Policy Analyst of the President's Office Planning Commission.
All photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.

July Night Skies and First Crescent Visibility Over Tanzania

Viewing all 109981 articles
Browse latest View live




Latest Images