Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 188 | 189 | (Page 190) | 191 | 192 | .... | 3272 | newer

  0 0


   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabibidhi kombe, Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume baada ya kuibuka washindi wa jumla katika Maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam
   Meneja Kiongozi, Uhusiano Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume akionesha vikombe walivyopata baada ya kuibuka washindi
    Meneja Kiongozi, Uhusiano Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume akipokea kikombe cha ushindi kwa upande wa taasisi za fedha.
     Meneja Kiongozi, Uhusiano Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume akimkabidhi Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu.  
   Furaha ya ushindi.
   Ilikuwa ni siku nzuri kwa wafanyakazi wa NSSF. 
  Wafanyakazi wa NSSF wakielekea kaika banda la NSSF baada ya kukabidhiwa zawadi zao.


  0 0

   Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM wa Mikoa ya Unguja,katika Viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti mjini Zanzibar,katika mkutano huo  ulizungumzia uwepo wa Serikali mbili kwa Serikali ya mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano wa Tanzania.
   Wanachama wa CCM wa maskani ya Kisonge wakishangilia katika Mkutano wa hadhara uliofanyika leo na kuhutubiwa na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa
  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,Uwanja wa Kibandamaiti Mjini Zanzibar.[Picha na Ramahan Othman,Ikulu.]
   Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais Mstaafu wa  Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (Komandoo) Dk.Salmin Amour Juma.alipokuwa akiwasalimia na kuwahutubia katika Mkutano wa hadhara Kibandamaiti Mjini Zanzibar katika uwanja wa Demokrasia Kibanda maiti mjini Zanzibar, [Picha na Ramadhan Othman.Ikulu.]

  0 0

   Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(Vazi la Kitenge)akiangalia Samani mbalimbali za Majumbani ambazo zinapatikana katika Banda la Jeshi la Magereza zilizotengenezwa kwa ubunifu mkubwa na Wafungwa kwa kushirikiana na Askari wa Jeshi la Magereza( aliyepo kushoto) ni Mkuu wa Banda la Maonesho la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi wa Magereza Julius Sang'udi akimuonyesha Kamishna Jenerali Samani hizo zilizopo katika Banda la Magereza.
  ========  ======  ========
  Na Inspekta Lucas Mboje,  Jeshi la Magereza
  Jeshi la  Magereza Nchini limeibuka Mshindi wa Pili katika Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa kwa upande wa Samani za Majumbani(Home Furnitures) ambapo Mshindi wa Kwanza ni Jeshi la Kujenga Taifa na Mshindi wa Tatu ni Funiture Centre ya Jijini Dar es Salaam.

  Hafla ya Kutangazwa Washindi Walioshiriki Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa imefanyika leo katika Ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa uliopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba, Jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda.

  Awali, Mhe. Waziri Mkuu kabla ya kukabidhi Zawadi kwa Washindi Walioshiriki Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa alizundua Rasmi Nembo ya Zao la Asali ya Tanzania na "Bar Codes" itakayotumika kutambulisha Asali ya Tanzania Kimataifa.

  Katika hotuba yake kwa Wananchi wa Tanzania, Mhe. Waziri Mkuu amewataka kujivunia na kuitumia ipasavyo fursa hii ya zao la Asali katika Biashara Kimataifa ambapo ametolea mfano wa kuigwa na hata kwenda mbele zaidi ya Nchi ya Ethiopia ambayo ni ya kwanza kwa Afrika na ya Nne Kimataifa katika kuzalisha na kuuza Asali katika Masoko ya Kimataifa.

  Aidha ameyashukru Makampuni mbalimbali ya Ndani na Nje ya Nchi pamoja na Wananchi mbalimbali ambao wamejitokeza kikamilifu kushiriki katika Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa na amewataka Watanzania kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili kuinua Uchumi wa Mtanzania Mmoja Mmoja na wa Taifa kwa Ujumla.

  Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea yalizunduliwa Rasmi na Mfalme Mswati wa III wa Swaziland tarehe 1 Julai, 2012 katika Ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa uliopo Viwanja vya Sabasaba, Jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda akiwaonyesha Asali ya Tanzania ikiwa tayari kwenye kifungashio chake Wageni Waalikwa na Wananchi ambao hawapo pichani mara tu baada ya kuzindua Nembo ya Asali ya Tanzania na "Bar Codes" zake zinazotambulika Kimataifa(kulia kwa Waziri Mkuu) ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdalah Kigoda. Hafla hiyo imefanyikia katika Ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa uliopo katika Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda akiangalia "Barcode" itakayotumika katika Zao la Asali ya Tanzania( kulia kwa Waziri Mkuu) ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdalah Kigoda. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo katika Ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa uliopo Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam (Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0


  0 0

   
  Mjumbe wa NEC Phares Magesa akikagua timu za mpira wa miguu (Flamingo Vs Kichepekichepe) katika mchezo wa fainali ya ligi ya soka kata ya Mji Mwema, Kigamboni (W)Temeke.Michezo ni Kazi na inasaidia kuimarisha Mahusiano katika Jamii zetu bila kujali dini, Kabila au uwezo wa mtu, hivyo wote tushiriki na tusaidie VIJANA wetu na kupitia michezo tujenge Jamii bora zaidi.

  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia) akimkabidhi tuzo Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Orio kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo wa kufadhili sherehe za kufunga Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.Katikati ni Dk. Abdallah Kigoda Waziri wa Viwanda na Biashara.
                                                                              Orio akifuara tuzo hiyo
  Orio akiwa na washiriki wa maonesho hayo kabla ya kupokea tuzo

  0 0
  0 0

  Rais Kikwete akielekea kukagua timu.
  Rais Kikwete akisaini mpira utakaotumika.
  ...Akiwakagua Yanga.
  ..Akiwakagua Simba.
  Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Eric Shigongo, Waziri Fenella Mukangara, marefarii na manahodha wa Simba na Yanga.
  Vikosi vya Simba na Yanga.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Global Publishers leo 7.7.2013 waliandaa Tamasha la Matumaini. Bahati mbaya sana sikuweza kuwahi kutokana na safari nilizonazo. Hii ni hotuba niliyopanga kuitoa na kuwatumia waandaaji. 

  TAMASHA LA MATUMAINI

  Leo nilikuwa niwe nanyi kwa ajili ya siku hii muhimu sana kwa nchi yetu, siku ya matumaini kama inavyoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa ndugu yangu Erick Shigongo kwa kuandaa tamasha hili kila mwaka. 
  Nasikitika kuwa sitaweza kufanya pambano la ngumi na ndugu Ray na pia kuchezea timu yangu ya Wabunge wa Simba dhidi ya watani zetu Yanga. Hata hivyo naamini kuwa tamasha litakuwa na mafanikio makubwa na nipo nanyi japo sipo Dar es Salaam.
  ZITTO KABWE.

  Ilikuwa niwepo Dar es Salaam leo, lakini nimeshindwa kuondoka Marekani kwa sababu Spika wa Bunge Mama Anna Makinda ameniagiza kwenye safari nyingine ndefu kwenda visiwa vya Cayman na baadaye Namibia kwa shughuli za Umoja wa Wabunge wa Jumuiya ya Madola. Sikuweza kukwepa jukumu hili la kitaifa maana limekuja ghafla na mimi nipo huku jirani na maeneo hayo. Naomba radhi sana kwamba sipo nanyi leo.
   
  Huyu  ndie Ray  aliyepaswa  kupambana na Zitto

  Nawaomba muiombee amani nchi yetu na msimamie haki kwa wananchi wote bila kubagua dini zao, rangi zao, hali yao kimaisha na ufuasi wa vyama vya siasa. Mwaka huu tumeshuhudia matukio ambayo yanatikisa msingi wa Taifa letu – Umoja.
   Hivi sasa msingi wetu una nyufa ambazo kwa kweli hatujajua bado nini kinacholeteleza mambo haya kama kulipua makanisa, kulipua mikutano ya vyama vya siasa na kuua viongozi wa dini. 

  Matukio haya yanatuelekeza kuwa makini sana na kauli zetu kwani baadala ya kuunganisha wananchi tunawezajikuta tunawagawa zaidi Watanzania na hivyo kuwa na mzunguko wa machafuko (vicious circle of violence). 
  Ni wajibu wa viongozi wa kisiasa na wananchi kuepuka kabisa kuanza kurushiana maneno na lawama kuhusu matukio haya, kwani inawezekana lawama na maneno yetu yakawa yanampa nguvu adui wetu ambayo hatujamjua bado.

  Napenda niwakumbushe kwamba ni rahisi sana kusambaza chuki na ni vigumu sana kuondoa chuki miongoni mwa wananchi.
    Viongozi hatari kama Hitler walitumia sana mbinu ya kueneza chuki dhidi ya jamii ya Jews na matokeo yake yalikuwa ni vita vikuu vya pili vya dunia na zaidi ya watu milioni 6 wasio na hatia kupoteza maisha.
   Sisi sote tuna jukumu moja la kuhakikisha tunajenga Taifa lenye kujali HAKI na lenye mshikamano mkubwa miongoni mwa raia. Kwa nia hii tu ndio tutaweza kuwa na Taifa imara lenye heshima mbele ya mataifa mengine duniani. Ni kwa njia hiyo tu ndio tutaweza kutokomeza umasikini uliokithiri mijini na vijijini hapa nchini kwa kuongeza uzalishaji na kupanua ajira. Ikumbukwe bila HAKI hakuna AMANI na bila UWAJIBIKAJI hakuna UTULIVU.

  Tukiegemea siasa za CHUKI. Tukashindwa kuwa na mahusiano ya kawaida miongoni mwa viongozi kuhusu masuala ya msingi ya nchi. Tukashindwa kujadiliana kwa hoja kuhusu sera zetu. Tutapata viongozi aina ya Hitler nchini mwetu. Wote tukatae. Sisi ni Watanzania. Muwe na Tamasha jema la Matumaini.

  Zitto Kabwe
  7.7.2013, Aspen Colorado, USA.

  0 0

  A fire truck sprays water on Asiana Flight 214 after its crashed at San Fransisco International Airport on Saturday July 6, 2013  in San Fransisco.Photo By AP/BERGER

  SAN FRANCISCO (AP) — An Asiana Airlines flight from Seoul, South Korea, crashed while landing at San Francisco International Airport on Saturday, forcing passengers to jump down the emergency inflatable slides to safety. It was not immediately known whether there were any injuries.
  The Boeing 777 was supposed to land on runway 28 left at the airport, said Federal Aviation Administration spokeswoman Laura Brown. She said the sequence of events was still unclear, but it appeared the plane landed and then crashed.
  A video clip posted to YouTube shows smoke coming from a silver-colored jet on the tarmac. Passengers could be seen jumping down the inflatable emergency slides. Television footage showed debris strewn about the tarmac and pieces of the plane lying on the runway. Fire trucks had sprayed a white fire retardant on the wreckage. A call to the airline seeking comment wasn't immediately returned.
  Asiana is a South Korean airline, second in size to national carrier Korean Air. It has recently tried to expand its presence in the United States, and joined the oneWorld alliance, anchored by American Airlines and British Airways.
  The 777-200 is a long-range plane from Boeing. The twin-engine aircraft is one of the world's most popular long-distance planes, often used for flights of 12 hours or more, from one continent to another. The airline's website says its 777s can carry between 246 to 300 passengers. The last time a large U.S. airline lost a plane in a fatal crash was an American Airlines Airbus A300 taking off from JFK in 2001.
  Smaller airlines have had crashes since then. The last fatal U.S. crash was a Continental Express flight operated by Colgan Air, which crashed into a house near Buffalo, N.Y. on Feb. 12, 2009. The crash killed all 49 people on board and one man in a house.

  0 0

  Ufunguzi wa Tamasha la Matumaini Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo. Kwa mapicha zaidi BOFYA HAPA

  JK akijiandaa kuanzisha mechi kati ya wabunge wapenzi wa Yanga na Simba Uwanja wa  Taifa jijini Dar es salaam leo. Kwa mapicha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mshindi walikuwa Yanga dhidi ya Simba kwa bao 4-3 kwa penati

  0 0

  Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akimsikiliza Meneja Uhusiano wa TTCL,Bw. Amin Mbaga wakati alipotembelea banda hilo kabla ya kufunga maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam jana.
  Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akimkabidhi Meneja Uhusiano Bw. Amin Mbaga tuzo ya ushindi katika sekta ya habari na mawasiliano.
  wafanyakazi wa TTCL katika Picha ya pamoja baada ya kupokea tuzo ya Ushindi katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam jana.
  Wafanyakazi wa TTCL wakiwa ndani ya banda lao pamoja na tuzo ya ushindi.

  0 0

  HOST "DMK" (DICKSON MKAMA)
  GLOBAL ENTERTAINMENT SHOW
  IS ALL ABOUT 
  LIFESTYLE , FASHION & ENTERTAINMENT AROUND THE WORLD.
  Will be Aired Live on DCTV under the Umbrella of the Bridge Show Starts in August and will be available Online exclusively through SWAHILI TV at www.swahilitv.info .
  DCTV is available on these Channels:-
  COMCAST # 95 & 96
  VERIZON # 10 ,11 & 28 
  RCN # 10 & 11

  DMK IN THE STUDIO FILMING THE SHOW
  BEHIND THE CAMERA IS EXCUTIVE PRODUCER - MR AUGUSTINO MALINDA
  LEFT-PROGRAM DIRECTOR ALEX KASUWI EXCHANGING IDEAS WITH DMK
  THE HOST DMK ON THE SET

  THE SHOW IS PRODUCED UNDER THE PRODUCTION COMPANY CALLED 
  " MMK MEDIA GROUP "

  0 0

  Diwani wa Kata ya Mlandizi, Euphrasia Kadala akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Mlandizi Veterani, Norbet Mshiu baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mbunge wa Kibaha Vijijini, (Hamoud Cup 2013) uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mlandizi. Katikati ni Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa. 

  Timu ya soka ya Mlandizi Veterani ikiwa na kombe la baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi.
   Diwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya Kibaha Vijijini, Mwajuma Denge akipokea zawadi ya khanga kutoka kwa mgeni rasmi baada ya kushinda katika mchezo wa kuruka kamba.
   Mshambuliaji wa timu ya Mlandizi Veterani, Kindema Salum akitafuta mbinu za kumtoka kiungo wa timu ya Muungano, Shaban Juma katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa, uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mlandizi mkoani Pwani.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Meneja Mauzo wa kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi aina ya TECNO, Patrick Karogila, akionyesha moja ya simu za teknolojia ya hali ya juu “Smartphone” ambayo imeingizwa katika soko la Tanzania hivi karibuni, Simu hiyo pamoja na nyingine zimebuniwa ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wa simu nchini, pamoja nae ni Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo Boukali Mounir.
  Meneja Uhusiano wa kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi aina ya TECNO, akionyesha moja ya simu zenye teknolojia ya hali ya juu “Smartphones” ambayo imeingizwa katika soko la Tanzania hivi karibuni, Simu hiyo imebuniwa kukidhi mahitaji ya mawasiliano kwa watumiaji wa simu nchini, pamoja nae ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo Patrick Karogila.
  Meneja Mauzo wa kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi aina ya TECNO, Patrick Karogila, akizungumza na waandishi wa habari, (hawapo pichani) katika hafla ya kutambulisha simu zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu kutoka katika kampuni hiyo, Simu hizo zimebuniwa kukidhi mahitaji ya mawasiliano kwa Watanzania wa aina zote. Pamoja nae ni meneja mahusiano wa kampuni hiyo, Boukali Mounir.

  0 0

  Meya wa jiji la Mwanza (pili shoto),Mh.Stanslaus Mabula akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu walioibuka katika mashindano ya kucheza,kwenye tamasha la Wazi la Filamu la Grand Malt Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ lililokuwa likifanyika kwa wiki nzima kwenye uwanja wa Nyamagana,jijini Mwanza.Mshindi wa kwanza pichani kati ni Laulencia Francis aliyejinyakulia kitita cha sh laki 2,Mshindi wa pilia ni Victoria Pascal (kwanza kulia) aliyeibuka na sh laki moja,na watatu ni Mariam Vincent aliyejinyakulia shilingi elfu hamsini.Pichani nyuma kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo,Mussa Kisoky wakiwa na wadau wengine wa jiji la Mwanza.Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Mkutano wa 32 wa Wadau wa Posta kwa Nchi za Afrika, ulioanza jijini Arusha leo, Juliai 8, 2013. Mkutano huo umehudhuriwa na wadau wa Posta kutoka nchi za Afrika.  
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Viongozi, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) Katibu Mkuu wa Shirikisho la Posta kwa Nchi za Afrika (PUPA) Younouss Djibrine (kulia) na Prof. John Nkoma, Mkurugenzi wa Mawasiliano Tanzania (wa pili kulia), wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Julai 8, 2013 kwa ajili ya kufungua Mkutano wa 32 wa Wadau wa Posta kwa Nchi za Afrika, ulioanza jijini Arusha leo.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Posta kwa Nchi za Afrika (PUPA) Younouss Djibrine, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 32 wa Wadau wa Posta kwa Nchi za Afrika, ulioanza jijini Arusha leo, Juliai 8, 2013. Mkutano huo umehudhuriwa na wadau wa Posta kutoka nchi za Afrika
    Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akifungua rasmi mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa AICC, jijini Arusha. 
   Kikundi cha Kwaya cha Jijini Arusha kikitoa burudani.
   Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mhe. Makamu wa Rais kufungua mkutano huo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki baada ya kufungua mkutano huo. Picha na OMR.

  0 0
 • 07/08/13--03:43: mboga mboga kwa afya zaidi.
 •  Baadhi ya akina mama wakiwa katika shughuli zao mbalimbali za kibiashara katika soko kuu la zamani la jijini Mwanza,eneo la barabara ya Pamba roadmapema leo kama walivyonaswa na Globu ya jamii ilipokuwa ikijivinjari maeneo hayo.Akina mama hao kama waonekanavyo pichani wakiwa katika biashara ya kuuza mboga mboga katika suala zima la kujitafutia mkate wao wa kila siku.

older | 1 | .... | 188 | 189 | (Page 190) | 191 | 192 | .... | 3272 | newer