Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1883 | 1884 | (Page 1885) | 1886 | 1887 | .... | 3283 | newer

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha, leo Agosti 28, 2017(Wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kulia) ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mhe. Gobless Lema.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akitoa hotuba mbele ya Maofisa na askari wa Magereza Mkoani Arusha katika hafla ya uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha. 

   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kutoa hotuba fupi ya uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(katikati) akikagua nyumba za askari Magereza zilizojengwa kwa kutumia fedha iliyopatikana katika miradi ya Shirika la Magereza(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha, Khamis Nkubasi.
   Muonekano wa nyumba zilizozinduliwa za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Bi. Ana Teressa .jana Agosti 27/2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Havana ,baada ya kumaliza ziara ya kikazi Nchini Cuba. Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  BMG Habari.
  Jumamosi iliyopita, Agost 19,2017 Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ilizindua rasmi “Mfuko wa Elimu Ikungi” ulioanzishwa wilayani humo kwa lengo la kusaidia utatuzi wa kero za elimu ikiwemo uhaba wa maabara, madarasa, vyoo pamoja na nyumba za waalimu.

  Katika uzinduzi huo, pia zilifanyika shughuli kadhaa ikiwemo uzinduzi wa ligi ya soka ya “Ikungi Elimu Cup 2017” yenye lengo la kuhamasisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali kuchangia Mfuko wa Elimu Ikungi, uzinduzi wa zoezi la ufyatuaji wa matofali ambapo kila Kata wilayani Ikungi imeazimia kufyatua matofali elfu kumi.

  Karibu kwa dakika chache kutazama yaliyojiri kwenye uzinduzi huo ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala mkoani humo Dkt.Angeline Lutambi huku mwenyeji wake akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi na mlezi wa Mfuko wa Elimu Ikungi, Mhe.Miraji Jumanne Mtaturu. Tazama video hapo chini.

  0 0


  Klabu ya Simba inapenda kuwajulisha wanachama na mashabiki wake kuwa,Golikipa wake wa kimataifa,Said Mohamed Nduda amepata matatizo ya goti ambayo yamempelekea kueleka India kwa ajili ya matibabu.

  Nduda aliumia mazoezini wakati timu ikijiandaa kuelekea mchezo dhidi ya Yanga wiki ilipita,Matibabu hayo yatamuweka mchezaji huyo nnje kati ya wiki nne hadi sita kabla ya kujiunga tena na wenzake kwa ajili ya mazoezi na anatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa wiki hii.

  Klabu pia inayofuraha ,kuwaambia kuwa wachezaji wake John Bocco na Haruna Niyonzima ,ambaye alipata majeraha madogo juzi wameshaanza mazoezi na wenzao hii leo.

  Huku pia Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi wa muda mrefu naye anatarajiwa kuanza mazoezi siku chache zijazo baada ya madaktari kuthibitisha uzima wa afya yake.

  Mwisho,Klabu inaufahamisha umma wa watanzania kupitia vyombo vya habari kuwa taarifa zote rasmi za klabu ya Simba zitakuwa zikitolewa katika mfumo na barua hii (Heading paper)

  Pia Klabu inawaomba washabiki wake kote nchini kuendelea kuiunga mkono timu yao ili iendelee kufanya vizuri kwenye ligi kuu iliyoaanza wikiendi iliyopita.

  Imetolewa na Mkuu wa Habari na Mawasiliano

  Haji.S.Manara
  SIMBA NGUVU MOJA

  0 0

  Na David John Mwanza

  JESHI la Polisi mkoa wa Mwanza limewaasa waandishi wa habari nchini,  kuhakikisha wanatumia kalamu zao kwa uweledi na uadilifu mkubwa katika kuhabarisha umma, mambo muhimu ya nchi na kwamba waepuke kutumiwa na watu wachache ambao mara zote hawalitakii mema Taifa.

  Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Rpc Mohamed Msangi wakati wa mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi ambaye aliongozana na Naibu katibu kuu wa Taasisi ya kutetea haki za binadamu nchini TAHURA Habibu Rajabu jana.

  Kamanda Msangi mbali na mambo mengine alisema kuwa waandishi wa habari wanadhamana kubwa katika kuhakikisha Taifa linaendelea kuwa salama kwani kama kalamu zao zitatumika vibaya ni rahisi kuvunja usalama ambao umejengwa na waasisi wa Taifa.

  "Nitowe wito kwa waandishi wa habari ni vema wakaongeza uzalendo na uchungu kwa nchi yao na hasa kuhakikisha mnatumia kalamu zenu kwa ustadi wa hali ya juu na kuepuka kutumiwa na watu ambao hawalitakii mema taifa,".alisema Msangi

  Aliongeza kuwa katika suala la kulinda amani linatakiwa kwa kila mtanzania, kwani hata mwandishi wa habari ni mtanzania na pindi usalama utakapokosekana haitajalisha nafasi ya mtu hivyo lazima waandishi wa habari wanatakiwa kuwa wazalendo la kuhakikisha wanapigania taifa lao kwa nguvu zote.

  Msangi alifafanua kuwa watanzania wasidanganywe kwani uhuru ambao unapatikana hapa nchini huwezi kupata mahala pengine popote hivyo ni lazima kujiepusha na watu ambao wanataka kujipatia umaalufu kwa mgono wa watu wengine wakiwemo wandishi wa habari.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya askari wa Jeshi hilo wanaoshiriki mafunzo ya wiki mbili ya kuwajengea Uwezo na Ujasiri wakati wanapotekeleza majukumu yao muda mfupi kabla ya kufungua rasmi mafunzo hayo yanayofanyika katika chuo cha Polisi Moshi CCP mkoani Kilimanjaro jana. Picha na Jeshi la Polisi.
  Baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi nchini kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) wanaoshiriki mafunzo ya wiki mbili ya kuwajengea Uwezo na Ujasiri wakati wanapotekeleza majukumu yao wakiwa tayari kumuonyesha Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (hayupo pichani), moja ya mbinu mahiri za kukabiliana na matishio ya kiuhalifu na wahalifu, mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi CCP. Picha na Jeshi la Polisi.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na ujumbe kutoka China Leo. Ujumbe huo umejadiliana na uongozi wa MNH jinsi watakavyotoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa.
  Wataalamu wa afya kutoka China wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa MNH leo.
  Baadhi ya wakurugenzi wa MNH wakifuatilia mazungumzo hayo leo.
  Watalaamu na baadhi ya wakurugenzi wa MNH wakiwa kwenye picha ya pamoja leo.

  0 0

  The Town Planners Registration Board announces the Fourth Annual General Meeting which will take place on 26th - 27th October, 2017.


  Venue:                           Bank of Tanzania (BOT) - Kilimanjaro Auditorium,

  Dar es Salaam. 
  Participants:                Town Planners, Surveyors, Land Officers, Architects, Valuers and other Land Development Stakeholders.

  Participation Fee:         Tanzanian shillings 200,000.00 per participant; those paying after 15th October 2017 will be required to pay Tanzanian shillings 250,000.00 
  Mode of payment:        Through Bank Account of the Board, or M-Pesa or in cash at the Office of the Board which is located in the 2ndfloor, Matasalamat Building, Samora Avenue in Dar es Salaam

  Account Details:         Name: Town Planners Registration Board, Account Number: 20101000085 (NMB); M-Pesa No: 0753504222 

  The Registrar,

  Town Planners Registration Board,

  Matasalamat Building – Samora Avenue,

  P. O. Box 77496, Dar es Salaam,


  Tel: 2127976, 0753 504222.


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ndugu Andrew W. Massawe anasikitika kutangaza kifo cha mtumishi Digna Baltazar Mallya (Afisa Usajili) kilichotokea ghafla Jumamosi 26/08/2017.

  Marehemu atasafirishwa kwa mazishi mkoani Kilimanjaro wilayani Rombo, Jumatano 30/08/2017, 

  NIDA tunatoa pole za dhati kwa muwe wa marehemu, watoto, wazazi, ndugu na marafiki wote walioguswa na msiba huu mzito. Kabla ya umauti marehemu alikuwa akifanya kazi ofisi ya Usajili  Wilaya ya Kinondoni. Tutakukumbuka kwa ucheshi wako, uchangamfu na moyo wa kujituma. Mwenyezi Mungu akupokee na akupumzishe kwa amani. 
  AMINA 


  0 0

   Nahodha wa timu Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuf akiwa anajaribu kuwatoka wachezaji wa timu ya TMT katika mchezo wa nne kati ya mitano katika fainali ya Sprite BBall Kings uliyopigwa kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ulimalizika kwa TMT kutoka na ushindi wa pointi 80-79.


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  Timu ya TMT imefanikiwa kurejesha furaha kwa mashabiki zake baada ya kuwafunga Mchenga BBall Stars kwa pointi 80-79 mchezo wa nne kati ya mitano katika fainali ya Sprite BBall Kings uliyopigwa kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

  TMT imefanikiwa kushinda mchezo huo wa pili kati ya minne na kuzima matumaini ya Mchenga ga kutwa ubingwa mapema baada ya kuwa tayari wakiwa wameshashinda michezo miwili kati ya mitatu.

  Katika mchezo wa kwanza Mchenga walitoka na ushindi wa pointi 101- 70 za TMT, mchezo wa pili TMT wakashinda kwa pointi 82-79, na mechi ya tatu Mchenga wakashinda kwa alama 87-82 za TMT.

  Kutokana na matokeo hayo timu ya TMT imeweza kusimamisha ubingwa uliokuwa unategemewa na Mchenga BBall Stars kwa siku ya juzi na kupelekea kwenda katika Game 5 siku ya Jumamosi Ijayo.

  Pamoja na hayo, mechi hiyo iliweza kuonyesha utofauti na ufundi mkubwa kutokana na timu zote mbili kujifua vizuri na kusababisha kumaliza mchezo kwa tofauti ya pointi moja.

  Manahodha wa timu zote mbili wamewaahidi mashabiki wao kuja kwa wingi siku ya Jumamosi kwa ajili ya kushuhudia mchezo huo wa mwisho na wenye kutoa hatma ya bingwa Sprite BBall Kings 2017 na kila mmoja akijinasibu kufanyia makosa pale walipokosea ili waweze kuondoka na kitita cha shiling milion 10.

  Mchenga na TMT zitakutana tena Septemba mbili (Jumamosi) ya mwaka huu kucheza game 5 ambapo mchezo huo ndiyo utakoweza kuamua mshindi ni nani kati ya wawili hao.

  Nahodha wa timu Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuf akiwa anajaribu kumtoka nahodha wa  timu ya TMT Isihaka Masoud katika mchezo wa nne kati ya mitano katika fainali ya Sprite BBall Kings uliyopigwa kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ulimalizika kwa TMT kutoka na ushindi wa pointi 80-79.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi wa Makao Makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Upanga jijini Dar es salaam leo Agosti 28, 2017 . Wengine ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora)Mhe. Angela Kairuki, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dr. Laurean Ndumbaro, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Valentino Mlowola, na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa TAKUKURU Bw. Alex Mfungo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi wa Makao Makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Upanga jijini Dar es salaam leo Agosti 28, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Valentino Mlowola
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa risala nzuri Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Valentino Mlowola alipowatembelea makao makuu yao Upanga jijini Dar es salaam leo Agosti 28, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Valentino Mlowola alipowatembelea makao makuu yao Upanga jijini Dar es salaam leo Agosti 28, 2017. Wengine ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora) Mhe. Angela Kairuki na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro. Picha na IKULU

  0 0  Timu za Soka wilaya ya Magharibi A Unguja zimetakiwa kufika katika ofisi za Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) za Wilaya ya Magharibi A Unguja hiyo ili kukamilisha masuala mbali mbali yanayohusiana usajili wao kabla ya Agosti 31, 2015.

  Katibu Mkuu wa ZFA Zainab Omar Mussa ameeleza kuwa pamoja na kukamilika kwa zoezi la usajili ameona haja ya kutoa muda huo ili kutoa nafasi kwa timu hizo kusawazisha dosari katika fomu zao sambamba na kukamilisha malipo ya baadhi ya ada zinazostahiki. 

  Zainab ameeleza kuwa zoezi hilo katika wilaya hiyo lilienda vyema na kwamba klabu hizo zinatakiwa a kufanya marekebisho hayo kabla ya Kamati Tendaji kukutana na kuzipitia fomu hizo mwanzoni mwa mwezi ujao. 

  Katibu Zainab ameeleza kuwa katika kipindi cha usajili kilichoanzia Julai 17 - Agosti 17, 2017 timu 35 zilichukua fomu za usajili wa kushiriki mashindano ya ligi daraja la pili na tatu katika msimu ujao. 

  Msimu wa 2017/18 utakuwa ni wa pili toka kuasisiwa kwa ZFA hiyo mwishoni mwa mwaka 2015 naada ya kugawanywa kwa iliyokuwa wilaya ya Magharibi, Unguja ambapo katika msimu uliopita klabu 30 zilishiriki ligi daraja la pili wilayani humo. 

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefanya mabadiliko kidogo katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kama ifuatavyo.

  Michezo ambayo imefanyiwa mabadiliko ni kati ya Tanzania Prisons na Majimaji ya Songea; Azam FC na Simba, Njombe Mji na  Young Africans; Mtibwa Sugar na Mwadui FC ambayo sasa itachezwa Septemba 6, 2017.

  Pia tarehe hiyo ya Septemba 6, mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Lipuli na Stand United; Singida United na Mbao; Kagera Sugar na Ruvu Shooting wakati Mbeya City na Ndanda FC .

  Michezo mingine ambayo imesogezwa hadi Septemba 11, 2017 ni kati ya Azam na Kagera Sugar wakati Mbao na Tanzania Prisons utachezwa Septemba 21, mwaka huu.

  Kadhalika mechi nyingine zitachezwa Oktoba 11, mwaka huu ni kati ya Mbao na Azam FC; Kagera Sugar na Mwadui; Mbeya City na Ruvu Shooting; Ndanda na Singida United.

  Tarehe hiyo pia Oktoba 11, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Njombe Mji na Simba; Mtibwa na Tanzania Prisons; Lipuli na Majimaji wakati Stand United na Young Africans watacheza Oktoba 12, mwaka huu.

  Novemba 15, 2017 Mbao itacheza na Young Africans; Kagera na Mbeya City; Stand United na Azam; Mwadui na Ruvu Shooting; Singida na Njombe Mji; Lipuli na Tanzania Prisons; Mtibwa Sugar na Majimaji wakati Novemba 16, Ndanda itacheza na Simba.

  0 0

   Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa haabari juu ya ziara yao ya kutembelea mradi wa ukusanyaji fedha katika kituo cha Feri cha mabasi yaendayo Haraka.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Max Com Africa Juma Rajabu  akimuonyesha Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia namna ya  mfumo wa kutumia kadi unavyo fanya kazi katika vituo vya Mabasi yaendayo haraka katika kituo cha Mabasi ya haraka cha Feri jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Mtendaji Mkuu DART, Ronald Lwakatare, akifafanua Jambo kwa wabunge  wa kamati ya Bajeti walipotembelea Mradi wa ukusanyaji mapato wa Max Malipo katika Vituo vya Mabasi ya Endayo Haraka.

  0 0

  Tanzanian-American youth Zul Manzi, developed his own entertainment website titled www.zmasterproductions.com. ZMaster Productions is a creative platform, that serves the purpose to entertain people through comedic skits, music, and cartoons. Based from Springfield, MA, the main mission behind the content is to inspire youths to become more creative and more collaborative. Check out the trailer for ZMaster Productions, as they prepare themselves to release original material by this September.

  0 0


  0 0


  0 0

  Na.Agness Moshi na Bushiri Matenda-MAELEZO.

  Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kupokea madaktari wengine wanne kutoka China kwa ajili ya kuendelea kusaidiana na madaktari wazawa katika taasisi hiyo baada ya madaktari wengine wanne kutoka China kumaliza muda wao. 
  Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt.Peter Kisenge katika hafla ya kuwaaga madaktari wanne kutoka China waliomaliza muda wao wa utumishi hapa nchini ambao walikua wakishirikiana naTaasisi hiyo kwa takribani miaka miwili.  

  “Wanarudi nchini China baada ya kumaliza muda wao, Tunawashukuru kwa kushirikiana nasi kwa kipindi chote walichokua nasi tunaishukuru Serikali ya China kwa misaada mbalimbali wanayotupatia ikiwemo ujenzi wa jengo la Taasisi ya Moyo, madaktari,wataalam pamoja na vifaa tiba”, alisema Dkt.Kisenge.
  Dkt.Kisenge aliongeza kuwa hivi karibuni Taasisi inatarajia kupokea madaktari wengine wanne kutoka China kwa ajili ya kuendelea kushirikiana nao   katika utoaji huduma ili kuweza kuifanya Taasisi hiyo ya kimataifa.
  Naye Kiongozi wa timu ya Madaktari kutoka China kwa Mkoa wa Dar Es Salaam Dkt.Sun Long amesema kwa miaka miwili waliyofanya kazi na Taasisi hiyo wamefanikiwa kufanya oparesheni  takribani 373 jambo ambalo limesaidia kupunguza  gharama za matibabu na idadi ya wagonjwa wa Moyo kwenda kutibiwa nje ya Nchi kama vile India.
  “Sasa hakuna haja ya kutumia fedha nyingi kwa ajili ya matibabu ya Moyo, Matibabu yote yanapatikana katika taasisi hii, hakuna Matata, Hapakazi Tu”, alisisitiza Dkt. Long.

  Aidha, Dkt.Long amesema kuna haja ya nchi hizi mbili kuendelea kushirikiana ili kuendelea kusaidiana katika utoaji huduma ikiwa ni pamoja na kubadilishana wataalam ili kukuza uwezo katika utoaji huduma.
  Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa jopo la madaktari waliomaliza muda wao Dkt. Gu Zhigiang ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kujitegemea katika matibabu ya magonjwa ya Moyo kwa wananchi wake na ameshukuru ushirikiano walioupata kutoka kwa taasisi hiyo kwa kipindi chote walichofanya kazi hapa nchini. 
  “Ninamshuru kila mmoja na ninafurahi kuhudumia Nchi hii nzuri, ninatumaini tutaendelea kushirikiana zaidi”, alisema Dkt. Gu Zhigiang.
  Dkt. Gu Zhigiang ameongeza kuwa anatarajia kukua kwa ushirikiano baina ya nchi hizi mbili kwani tunaelekea kuadhimisha miaka 50 ya ushirikiano kati ya Serikali ya China na Tanzania.

  0 0

  Na Alfred Mgweno (TEMESA MWANZA)

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu, ameshiriki katika zoezi la kuweka msingi wa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma ya usafiri katika Ziwa Victoria kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. 

  Zoezi hilo linaloashiria kuanza rasmi kwa ujenzi huo limefanyika Pasiansi katika eneo linalotumika kwa ajili ya ujenzi wa meli, vivuko na boti linalomilikiwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Limited ya Mwanza iliyoshinda zabuni ya kujenga kivuko hicho kwa gharama ya Shilingi Bilioni 8.9 za kitanzania. 

  Tukio hili la kihistoria lilihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka TEMESA Mhandisi Japhet Y. Maselle, Mhandisi Amos Mutahiwa kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bwana Salehe Songoro Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro, na wafanyakazi wa Kampuni ya Songoro na wale wa TEMESA.

  Akiongea baada ya zoezi hilo, Dkt. Mgwatu amesema wakazi wa Mwanza wana kila sababu ya kujivunia kuanza kwa ujenzi wa kivuko hicho kwani kitakapokamilika kitasaidia kurahisisha usafiri wa abiria na mali zao na hivyo kuimarisha uchumi wao. Aidha Dk. Mgwatu amemtaka Mkandarasi kuhakikisha anamaliza kujenga kivuko ndani ya muda uliopangwa kwenye mkataba na kuzingatia ubora wa hali ya juu. 

  Pia ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutenga fedha za maendeleo kwa ajili ya miradi ya vivuko kwa lengo la kuboresha huduma za usafiri. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro ameahidi kukamilisha mradi huo kwa wakati huku akisisitiza kuwa kampuni yake imejipanga vyema kufanya kazi kwa kasi kwa kuwa malighafi kwa ajili ya ujenzi wa kivuko tayari ipo kwenye eneo la ujenzi.

  Kivuko hicho kipya kitakapokamilika kitafanya idadi ya vivuko vinavyotoa huduma katika eneo la Kigongo Busisi kufikia vinne vikiwemo vile vya MV. Sengerema, MV. Misungwi, pamoja na MV. Sabasaba.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akiwa ameshikilia vifaa vya kuchomelea vyuma kuashiria kuanza kuweka msingi wa kivuko ‘’Keel Laying’’ katika eneo la Pasiansi ikiwa ni kumbukumbu ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.


  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akichomelea vyuma kuashiria kuweka msingi wa kivuko ‘’Keel Laying’’ katika eneo la Pasiansi ikiwa ni kumbukumbu ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
  Meneja wa Miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Major Songoro (kushoto) akitoa maelezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kulia) kuhusu kuanza kwa mradi wa ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
  Meneja wa Miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Major Songoro (kulia) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) michoro itakayotumika katika Ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
  Meneja wa miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Major Songoro (kulia) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (katikati) michoro itakayotumika katika Ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Songoro Bwana Salehe Songoro. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Bwana Salehe Songoro (wa pili kulia aliyenyoosha mkono) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wa tatu kushoto) mojawapo ya malighafi itakayotumika katika ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.

  PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA MWANZA)


  0 0


older | 1 | .... | 1883 | 1884 | (Page 1885) | 1886 | 1887 | .... | 3283 | newer