Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1882 | 1883 | (Page 1884) | 1885 | 1886 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0


  0 0

   Kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko akichezewa rafu na  Beki wa Lipuli, Novalty Lufung, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. mchezo huo umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
   Malimi Busungu wa Lipuli Fc, akimdhibiti kiungo mkabaji wa Yanga, Papy Tshishimbi wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. mchezo huo umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
  Beki wa Timu ya Lipuli, Asante Kwasi akiwa chini huku akiusindikiza mpira kwa macho baada ya kupigwa chenga ya mwili na Juma Abdul wa Yanga, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. mchezo huo umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
   Beki wa Yanga, Kelvin Yondani na Mshambuliaji wa timu ya Lipuli, Ramadhan Madebe wakiruka juu kwa pamoja kuwania mpira wa juu, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. mchezo huo umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
  Mshabiki wa timu ya Yanga akionekana ni mwenye huzuni sana baada ya timu yake kutoka sare ya bao 1-1 na timu ya Lipuli katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.


  0 0

  *Asisitiza nia ya kufungua ubalozi nchini humo

   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Gladys Bejarano na kumuhakikishia ufunguzi wa ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini humo.
  Amesema Tanzania inayatambua na kuyathamini mahusiano mazuri ya kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi, kielimu, kiafya na kiutamaduni kati yake na Cuba, hivyo inatarajia kufungua ubalozi nchini humo ili kurahisisha utendaji wa kazi za kibalozi.
  Waziri Mkuu alikutana na Mhe.  Gladys jana jioni (Jumamosi, Agosti 26, 2017) wakati alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kikazi nchini Cuba. Malengo ya ziara yalikuwa ni kuimarisha na kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
  “Tunatambua mahusiano mazuri yaliyopo kati Tanzania na Cuba, ambayo yalikuwepo kuanzia Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere, hivyo lazima tufungue ofisi za ubalozi na tutamleta balozi wetu hapa.”
  Pia Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Cuba kwa ujenzi wa kiwanda cha dawa za kuulia vijidudu vya maralia pamoja na ufadhili wa masomo ya udaktari inaoutoa kwa wanafunzi wa Kitanzania ambao wanasoma katika vyuo mbalimbali nchini humo.
  Hata hivyo aliiomba Serikali hiyo iendelee kutoa ufadhili wa masomo kwa madaktari hao hadi ngazi ya shahada ya uzamili kwa sababu Serikali ya Tanzania inawahitaji madaktari bingwa wengi kwani walioko nchini ni wachache.
  Kwa upande wake, Bi. Gladys alimshukuru Waziri Mkuu kwa kufanya ziara nchini Cuba na alimuhakikishia kwamba uhusiano wa Serikali yake na Serikali ya Tanzania utaendelea kuimarishwa kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.
  Alisema Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli inafanya jitihada kubwa za kuhakikisha uchumi wake unakua kwa kasi jambo ambalo ni tofauti na mataifa mengine. “Nawapongeza kwa hatua za kimaendeleo mnazozifanya.”
  Makamu huyo wa Rais alisema Serikali ya Cuba itaendelea kushirikiana na Tanzania katika uboreshaji wa Sekta za Afya, Utamaduni, Kilimo, Uchumi na Elimu. Kuhusu ombi la kuongeza ufadhili wa shahada ya uzamili kwa madaktari  alisema amelipokea na atalifanyia kazi.
  Awali Balozi wa Tanzania nchini Canada, ambaye anasimamia na nchi ya Cuba, Balozi Jack Zoka alisema Serikali ya Cuba ni miongoni mwa nchi zinazoshirikiana na Tanzania katika uboreshaji wa shughuli za maedndeleo, hivyo uwepo wa ofisi za ubalozi nchini humo utazidi kuimarisha mahusiano.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  JUMAPILI, AGOSTI 27, 2017.
    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo ya Kikazi na Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Gladys Bejarano katika mji wa Havana nchini Cuba jana August 26/2017.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo ya Kikazi na Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Gladys Bejarano. katika Mji wa Havana Nchini Cuba jana August 26/2017. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0


  0 0


  Maisha ya ndoa huja na changamoto nyingi sana. Moja kati ya changamoto kubwa wanazo zipata wanandoa ni pale mmoja kati ya wanandoa hao anapo patwa na mtihani wa kuugua maradhi mazito kama vile kisukari au kiharusi.
  Jambo hili linapotokea ndoa huyumba kwa kiasi kikubwa sana na mwisho wa siku huweza kufikia hatua ya kuvunjika kabisa.
  Hata hivyo si wanandoa wote huwakimbia wenzi wao pindi wanapo patwa na matatizo makubwa hususani maradhi mazito. Mfano mzuri ni kwa mwanadada Tina ( 33 ) mkazi wa Tabata jijini Dar Es Salaam.
  Wakati baadhi ya wanawake huwakimbia waume au wapenzi wao pindi wagunduapo kuwa waume au wapenzi wao hao wanakabiliwa na maradhi mazito kama vile kisukari, moyo, kiharusi nakadhalika, hali ni tofauti kwa mwanadada Tina.
  Mwanadada huyu , licha ya kuendelea kuiheshimu na kuitunza ndoa yake, lakini pia amejitolea bega kwa bega kushiriki katika tiba dhidi ya maradhi mazito yanayo msumbua mume wake.
  Tina anameapa kuwa atahakikisha anapambana hadi tone la mwisho la damu yake ili mradi tu mumewe aweze kupona maradhi hayo mazito yanayo msumbua.
  JE NI MARADHI GANI HAYO ? NA JE TINA ANASHIRIKI VIPI KATIKA KUHAKIKISHA MUMEWE ANAPATA TIBA DHIDI YA MARADHI YANAYO MSUMBUA ?
  Kuyafahamu yote haya BONYEZA :

  https://neemaherbalist.blogspot.com/2017/08/kutana-na-mwanamke-aliye-jitolea_26.html

  0 0
  0 0

  Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa kupambana kupunguza vifo vya Mama na Mtoto, unaofanyika mjini Jaipur nchini India.
  Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari alipokwenda kushiriki mkutano wa kupambana na kupunguza vifo vya Mama na Mtoto, unaofanyika mjini Jaipur nchini India.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Shule ya Genius Kings Nusery& Primary School, Machage Kisyeri, (Kulia) akisoma hotuba.

  Wakati serikali ya Tanzania inao mkakati wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda,wanafunzi wanaohitimu masomo wametakiwa kujiona sehemu ya mkakati huo na kusoma kwa bidii kupata ujuzi wa taaluma mbalimbali ikiwemo kutoogopa kusoma masomo ya hesabu na sayansi.

  Ushauri huo umetolewa na daktari bingwa nchini wa magonjwa ya nevu (Neurosurgery) kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili,Profesa Joseph Kahamba, wakati wa mahafali ya darasa la saba ya msingi ya Genius Kings yaliyofanyika Segerea jijini Dar es Salaam .

  Profesa Kahamba alisema kuwa nchi yetu bado inakabiliwa na changamoto ya kuwa na wataalamu waliobobea katika nyanja mbalimbali ambapo aliwataka wanafunzi wanaohitimu masomo na waliopo mashuleni na vyuoni kujipanga kuhakikisha wanapata utaalamu wa fani mbalimbali tayari kwa kutumikia taifa la Tanzania.
  Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Aloyce Siame (kulia) akikabidhiwa zawadi ya kikombe na Profesa Joseph Kahamba.

  “Wanafunzi waliopo mashuleni na vyuoni mnapaswa kujipanga kwa kuhakikisha mnasoma kwa bidii na kupata ujuzi wa fani mbalimbali kwa kuwa mapinduzi ya kuendeleza taifa letu yanayoendelea yanahitaji wataalamu wa fani mbalimbali na wanaotegemewa kuchukua majukumu hayo hawatoki nje ya nchi bali ni nyinyi vijana wa kitanzania”Alisema Profesa Kahamba.

  Aliongeza kusema kuwa kinachotakiwa kwa wanafunzi waliopo mashuleni na vyuoni kujibidisha kusoma kwa bidii na kupata taaluma za fani mbalimbali na wahakikishe wanajiamini na kuhakikisha ndoto zao walizojiwekea zinatimia na wanakuwa na uzalendo wa kuitumikia nchi na kuleta maendeleo chanya katika jamii kupitia elimu waliyoipata.

  Profesa Kahamba aliupongeza uongozi wa shule ya Genius Kings kwa kufanya uwekezaji katika sekta ya elimu kwa kuwa umelenga kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha elimu nchini na kuleta mabadiliko wenye jamii kwa kuwa elimu ni njia pekee ya kuleta maendeleo kwa haraka katika ujenzi wa taifa . “Naupongeza uongozi wa shule kwa kuwekeza katika elimu na nawapongeza wazazi ambao wanawekeza katika elimu kwa kusomesha watoto wao maana elimu bora katika jamii inachangia kuleta mabadiliko ya nchi haraka”.Alisema
  Mgeni rasmi akiangalia wanafunzi wakifanya majaribio ya sayansi.


  Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw. Aloyce Siame, alisema kuwa katika kipindi cha miaka 10 tangu shule ianzishwe imeweza kushikilia rekodi ya kufanya vizuri kwa kufaulisha wanafunzi wa darasa la saba na la nne kwa kiwango cha juu na kuingia katika shule tano bora wilayani Ilala na shule bora 20 mkoani Dar es Salaam mfululizo hali ambayo imewajengea hari ya kuzidi kufanya vizuri kwa mwaka huu na miaka ijayo.


  0 0

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani (kulia) akifafanua jambo wakati akizungumza na Mtangazaji wa Azam Tv, Nurdin Selemani kupitia kipindi cha Mizani ya Wiki kilichorushwa jana Jumapili hii.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando baada ya kushirikia kwenye kipindi cha Mizani ya Wiki kinachorushwa na Azam Tv Jumapili usiku.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani (kushoto) , akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi huo.Picha na Hussein Makame.

  Na Mwandishi Maalum

  MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhan amevitaka vyombo vya Habari vya Tanzania viige mfano wa wenzao wa Kenya kwa kutumia muda mwingi kutoa Elimu ya Kupiga kura. Akizungumza kwenye kipindi cha Mizani ya Wiki kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha AZAM Jumapili usiku, Ramadhan alisema moja ya mambo aliyojifunza katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya ni jinsi vyombo vya Habari vilivyoshiriki katika Uchaguzi huo na kuchangia watu wengi kujitokeza kupiga kura..

  “Natamani na sisi vyombo vya hapa nyumbani viige wenzao wa Kenya ambao walitoa muda mwingi kwa kutoa Elimu ya Mpiga kura,” alisema Ramadhani. aliongeza kuwa baadhi ya mambo ambayo amejifunza kwa Tume Huru na Mipaka ya Kenya (IEBC) katika uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni ni usambazaji wa vifaa katika vituo vya kupigia kura. Alifafanua kuwa licha ya kuwa Kenya wana vituo vichache takribani 40,000 vya kupigia kura ukilinganisha na vya Tanzania ambako kuna vituo 65,000, lakini alisema walifanya vizuri kwenye kusambaza vifaa.

  Eneo lingiine ambalo lilimvutia ni namna wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi katika Kituo cha kupigia kura wanavyokuwa na uelewa mkubwa kuhusu taratibu za kupiga kura. Kuhusu kuruhusu wafungwa na Wakenya walioko nje kupiga kura, Kailima alisema kwa sasa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi hairuhusu jambo hilo na akaongeza kuwa Tume haina pingamizi iwapo wabunge watatunga sheria inayoruhusu makundi hayo kujiandikisha na baadaye kupiga kura. “Tume ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuamua ni nani apige kura, ila tunaongozwa na katiba pamoja na sheria,” alisema.

  Akizungumza utaratibu wa kupiga kura uliotumika Kenya, alisema ni mzuri lakini akaongeza kuwa utaratibu unaotumiwa na NEC uko wazi ukilinganisha na ule uliotumiwa na IEBC. “Utaratibu wetu ni mzuri zaidi kwani unatoa fursa ya mawakala kujiridhisha kwamba mtu aliyeenda kupiga kura ndiye mwenyewe, unapunguza kelele,” alisema .

  Akilinganisha teknolojia iliyotumiwa na IEBC, Ramadhan alisema inawezeshwa mtu akipiga kura inahesabiwa jambo ambalo ilisababisha IEBC kutangaza matokeo ya awali ambayo hayajathibitishwa na akaongeza kuwa hilo ni jambo la hatari kwa kuwa matokeo ya pili yakibadilisha matokeo ya awali inaweza kuleta sintofahamu. Alisisitiza kwamba mfumo ambao unatumiwa na NEC bado pia ni mzuri kwa kuwa unalenga kutangaza matokeo ambayo yameshathibitishwa na yanaleta amani kwa jamii.

  “Uchaguzi ulipita tulitangaza matokeo ya urais ndani ya saa 72 kwa hiyo tuliwahi kuliko wenzetu wa Kenya.”

  0 0

  Hayawi hayawi sasa yamekuwa, ile safari ya kusherekea miaka 10 ya mafanikio ya jukwaa kubwa la mitindo Afrika Mashariki na Kati imeanza rasmi.

  Kwa miaka 9 maonesho ya Swahili Fashion Week yamebaki kuwa jukwaa kuu kwa Afrika Mashariki katika kuvumbua vipaji vya kipekee na mitindo maarufu ya baadae duniani. Ni ukweli usiopingika kuwa maonesho ya Swahili Fashion Week yana nia na shauku kubwa ya kuwatafuta na kuwakuza wabunifu bora wa baadae, ndio maana  jukwaa la shindano la mbunifu chipukizi lijulikanalo kama Washington Benbella Emerging Designer Competition  lilifikiriwa ili kutoa nafasi kwa wabunifu chipukizi na kuupeleka mbele ubunifu wao.

  “Tuna furaha sana kusherekea miaka 10 ya shindano la Washington Benbella Emerging Designer Competition, tumekuwa mashaidi wa mafanikio makubwa ya washindi waliopita sababu tunashauku ya kukuza nyota wa ubunifu. Tumefarijika sana kuanza mashindano haya, katika kukamilisha miaka 10 ya uwepo wa maonesho ya mavazi “Swahili Fashion Week” tunatarajia kuona vitu vizuri Zaidi ya ubunifu wa kawaida, na Zaidi, kila kitu kiwe cha kupendeza.”.

  Kila mwaka Ubora na upekee wa mitindo ya washiriki unaendelea kushangaza na kuwavutia watazamaji. Kutokana na dhamira ya maonesho ya mwaka huu ni “ Maadhimisho ya miaka 10 ya Swahili Fashion Week”  hivyo basi  kuna vitu vingi vya kutegemea katika maonesha haya haswa katika shindano hili la mbunifu chipukizi sababu litaonesha mitindo ya washindi wote waliopita.

  “tunajitahidi kuvumbua vipaji na kuifanya kazi yao kuwa ya kimataifa, tuna wasihii wabunifu vijana kuchukua nafasi hii adimu kwa umakini na kukusanya kazi zao bora za ubunifu ambazo zitawapatia nafasi ya kuwa kati ya washiriki 10 watakaochaguliwa kuweka historia kwa kuonesha mavazi yao katika maonesho ya  10 ya Swahili Fashion Week mwezi disemba”

  Kwa wabunifu chipukizi watakao vutiwa kushiriki kwenye shindano hilo watapata taarifa Zaidi kupitia fomu zetu zilizopo kwenye tovuti yetu ya www.shwahilifashionweek.com, mwisho wa kukusanya fomu hizo ni tarehe 9 Septemba mwaka huu.

  0 0

  Bw. Martin Gabone Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Women On Wheel - Africa akizungumza na wanawake akina mama kwa wasichana wakati wa semina ya iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya udereva wa kibiashara ambao utawawezesha kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji.

  Bw. Martin Gabone amesema Semina hii ina lengo la kuwaandaa wanawake watanzania na Afrika kwa ujumla kupata ujuzi katika taaluma ya udereva wa kibiashara ambapo wanawake hawa watapata mafunzo maalum katika programu ya Women On Wheel - Africa ili kujiwezesha na kujitegemea kiuchumi kupitia taaluma hii ya udereva wa kibiashara na wenye tija kwa maisha yao na taifa kwa ujumla wake.

  Women On Wheel - Africa inawakaribisha wanawake akina mama kwa wasichana kujisajiri ili kujiunga na mpango huu muhimu ambapo mafunzo yanatarajiwa kuanza mwezi wa tisa mwaka huu 2017 jijini Dar es salaam katika ofisi za taasisi ya

  Kwa mawasiliano zaidi unaweza kutumia namba hizi
  0712 156 933: 022 2664618: 022 2664587
  OFISI ZA TAASISI HIYO ZIPO KINONDONI ADA ESTATE KARIBU NA BAKWATA HIGH SCHOOL.

  Bw. Martin Gabone Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Women On Wheel - Africa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanawake akina mama kwa wasichana wakati wa semina ya iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na kuwawezesha kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji.

  Mjasiriamali Bi Tedy Daniel mmoja wa washiriki wa semina hiyo akifafanua jambo kwa wanasemina wenzake wakati wa mafunzo hayo.
  Bw. Martin Gabone Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Women On Wheel - Africa akiwaelekeza jambo baadhi ya washiriki wakati wa semina ya iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na kuwawezesha kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji.

  0 0

  Mahakama ya Juu nchini Kenya imeukubalia muungano wa upinzani nchini humo National Super Alliance (Nasa) kupekua sava zilizotumiwa na tume ya uchaguzi nchini humo wakati wa uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti.

  Mahakama hiyo imesema muungano huo utaweza kusoma data kwenye sava hizo chini ya uangalizi kuhakikisha usalama wa mitambo ya IEBC hauhujumiwi.

  Mgombea wa Nasa Raila Odinga aliwasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee.

  Mawakili wa Odinga wameruhusiwa na mahakama kunakili data kutoka kwenye sava hizo kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusu uchaguzi huo.

  Miongoni mwa mengine, upinzani utapata utambulisho wa sava zilizotumiwa wakati wa uchaguzi, ukuta wa kinga uliotumiwa kulinda sava hizo pamoja na mitambo ya dijitali ya uchaguzi wa Kenya (KIEMS) dhidi ya wadukuzi na mfumo endeshi wa mitambo hiyo pamoja na nywila zilizotumiwa kuingia katika mitambo hiyo.

  Kadhalika, wataweza kupata taarifa kuhusu yaliyojiri katika mitambo hiyo ya uchaguzi kuanzia Agosti tano hadi leo.

  Aidha, wataruhusiwa kusoma nakala za Fomu 34A na 34B (fomu za matokeo katika vituo vya kupigia kura na ngazi ya maeneo bunge) ambazo zilitumiwa kutangaza matokeo.

  Taarifa kuhusu mchakato wa upinzani kupekua sava na mitambo hiyo ya IEBC itawasilishwa kwa mahakama hiyo kesho jioni.
  Majaji saba wa mahakama hiyo ya juu wameanza kusikiliza kesi hiyo iliyowasilishwa na Bw Odinga leo.


  Kwa mujibu wa matokeo ya IEBC, Rais Kenyatta alipata kura 8,203,290 huku naye Raila Odinga akipata kura 6,762,224. Chanzo: BBC

  0 0

  Muonekano wa jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu linaloendelea kujengwa mkoani Dodoma.
  Muonekano wa jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu linaloendelea kujengwa mkoani Dodoma.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akikagua ujenzi wa ofisi hiyo unaoendelea mkoani Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mhandisi John Ainainyi Njau kutoka Benki ya Dunia nchini Tanzania.
  Mkandarasi wa majengo kutoka kampuni ya Hainan International Ltd inayojenga Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoani Dodoma akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina chuwa wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa ofisi hiyo.
  Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa waandamizi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) walioambatana na Mkurugenzi Mkuu wa ofisi hiyo Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Makao Makuu ya ofisi hiyo mkoani Dodoma. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

  0 0

  The NMB Bank’s Managing Director - Ms Ineke Bussemaker making opening remarks at the Executive Network event organized by NMB Bank in Dar es Salaam over the weekend. Over 150 high end customers attended the event where they also benefited from TAX training organized by Pricewaterhousecoopers. NMB Bank Managing director, Ms Ineke Bussemaker exchages views with Checknoctras Limited Head of Operations Mr Balraj Bhatt (left) and Head of Finance for the same company at the Executive Network event organized by NMB Bank in Dar es Salaam over the weekend. Over 150 high end customers attended the event where they also benefited from TAX training organized by Pricewaterhousecoopers.

  NMB Bank Plc has today organized a customer networking meeting with its top end Business Customers and Corporates. The meeting attracted over 150 customers from Dar es Salaam. The discussion of the meeting focused on ways to improve business and the impact of the 2017/2018 budget for businesses relationship between the bank and its customers.

  The NMB Business Executive Network is organized in large commercial cities of Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Morogoro, Mbeya, Mtwara, Kilimanjaro and soon to launch in Dodoma. The NMB Managing Director – Ineke Bussemaker, said that the aim of holding such meetings is to strengthen business relations with its top end business and corporate customers.

  “NMB is committed in ensuring that customers get the best service while the bank supports to their business growth. The bank has done major improvements and innovations to suit the need of customers. Private Banking and the launch of business centers in big cities are among the improvements,” said Ineke.

  Ms Bussemaker further said “the improvements done by the bank so far will help to bring services more closely to this segment of customers. They will not only get the best services but also acquire financial, regulatory, business and forex information in order to become and remain competitive.” She further said after the banks successfully implemented the business clubs which targeted Micro, Small and Medium Enterprises (MSME), the bank decided to start the business executive network to bring in the large business customers. [caption id="attachment_81124" align="aligncenter" width="500"] NMB Bank Managing Director - Ms Ineke Bussemaker exchages views stockholders at the Business Executive Network event organised by NMB Bank in Dar es Salaam over the weekend. Over 150 high end customers attended the event where they also benefited from TAX training organized by Pricewaterhousecoopers. NMB Bank Managing Director - Ms Ineke Bussemaker exchages views stockholders at the Business Executive Network event organised by NMB Bank in Dar es Salaam over the weekend. Over 150 high end customers attended the event where they also benefited from TAX training organized by Pricewaterhousecoopers.

  0 0


   Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Farreo (kushoto)  akimshuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei  Mengdong Gao,(kulia) akimkabidhi jezi  nahodha wa timu ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc, Ngayama Matongo (katikati) wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya kampuni hizo,uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Vodacom Tanzania Plc ilishinda magoli 7-1.
   Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania Plc, Ian Ferrao (kushoto) akisaini mpira wa mfungaji bora wa mchezo wa kirafiki kati ya Vodacom na Huawei uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, ambapo Vodacom Tanzania Plc iliiadhibu Huawei magoli 7-0.Kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei  Mengdong Gao.


  Kikosi cha timu ya  wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Ian Ferrao(katikati) aliyeshika mpira wakipozi kwenye picha kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya  kampuni ya Huawei  uliofanyika kwenye viwanjwa vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Vodacom Tanzania iliilaza Huawei  magoli 7-1.
   Wachezaji wa timu ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, wakishangilia ushindi wao  baada ya kuiadhibu timu ya wafanyakazi wa Huawei mabao 7-1 wakati wa mchezo wa kirafiki ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

  0 0
 • 08/28/17--03:50: Article 12


 • 0 0

   Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa kwanza kushoto) akizungumza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa tawi la kampuni mpya ya kimataifa toka nchini China iitwayo Guilin Pharmaceuticals Tanzania Limited itakayotengeneza na kusambaza dawa za kukabiliana na ugonjwa wa Malaria kali iitwayo Artesun nchini Tanzania. (wa pili kulia ni Mwakilishi Mkuu wa China kwenye masuala ya uchumi na biashara nchini Tanzania (wa pili kushoto) Makamu mkuu wa Rais wa kampuni ya Guilin Pharmaceutical Tanzania Lily Su (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Ashok Pandey.
   Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akipitia baadhi ya nakara za karatasi zilipewa katika uzinduzi wa uzinduzi wa tawi la kampuni mpya ya kimataifa toka nchini China iitwayo Guilin Pharmaceuticals Tanzania Limited itakayotengeneza na kusambaza dawa za kukabiliana na ugonjwa wa Malaria kali iitwayo Artesun nchini Tanzania.
  Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya uzinduzi wa tawi la kampuni mpya ya kimataifa toka nchini China iitwayo Guilin Pharmaceuticals Tanzania Limited itakayotengeneza na kusambaza dawa za kukabiliana na ugonjwa wa Malaria kali iitwayo Artesun nchini Tanzania. (Wa pili kulia ni Mwakilishi Mkuu wa China kwenye masuala ya uchumi na biashara nchini Tanzania (wa pili kushoto) Makamu mkuu wa Rais wa kampuni ya Guilin Pharmaceutical Tanzania Lily Su (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Ashok Pandey.

  0 0


  Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imepokea taarifa ya mkemia wa Serikali iliionesha kwamba sampuli ya mkojo wa Video Queen, Agnes Gerald "Masogange" una chembechembe za dawa za kulevya.

  Mahakama imepokea sampuli hiyo kama kielelezo namba moja kwa cha ushahidi upande wa mashtaka ambapo baada ya pingamizi la upande wa lilitokuwa likitaka kisipokelewe kutupiliwa mbali

   Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema pingamizi la upande wa utetezi kuwa fomu zilizopelekwa kwa mkemia hazikufata sheria limetupiliwa mbali.

  Amesema shahidi wa kwanza ambaye ni Elia Mulima anahaki ya kuandaa ripoti, kupima sampuli na kutoa ripoti mahakamani.
  Ameongeza polisi walipeleka maombi kwa mkemia wa serikali na kwamba ni wazi mshitakiwa alienda kwa mkemia na askari wawili na kumpatia kontena kwa ajili ya kuweka sampuli ya mkojo.
  Kesi imeahirishwa kwa muda.
  .........UP DATES........
  Shahidi namba mbili katika kesi hiyo, mpelelezi kutoka kituo cha polisi cha Kati, WP Judith ameieleza mahakama kuwa  alishuhudia Masogange akitoa sampuli ya mkojo kwa kuwa alisimama mlangoni.
  Amedai kuwa alipewa chupa ya plastiki yenye namba ya maabara 446/2017 na kumuelekeza Masogange jinsi ya kufanya ambapo alipata sampuli ya mkojo huo.
  Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, amedai Februari 15, mwaka huu aliitwa na Kaimu Mkuu wa Upelelezi, Ramadhan Kingai amchukue mshitakiwa Masogange na kumpeleka kwa Mkemia wa Serikali ambapo yeye akifuatana na Askari Polisi, Sospeter pamoja Masogange walienda kwa mkemia na kwamba saa 7 mchana walifika.
  Akihojiwa na Wakili wa utetezi, Reuben Simwanza ambaye alimtaka shahidi huyo kueleza  alikabidhiwa na nani chupa hiyo na kwamba mkojo ulikuwa na rangi oshahidi alieleza kuwa ulikuwa na rangi ya njano mpauko.
  Kesi hiyo itaendelea Agosti 31, mwaka huu.

  0 0

  WATOTO wanajengwa kwa kiakili  kwa kusoma vitu vinavyomuandaa katika kupenda shule katika ukuaji wa na kuleta matunda kwa taifa kutokana na msingi wa kusoma vitu mbalimbali.

  Hayo ameyasema Afisa Mtendaji Mkuu wa Toto Magazine, Jacqueline Lesika wakati wa Tamasha la Kuogelea kwa wanafunzi wa Awali ya Shule ya  Shree Hindu Mandal amesema kampuni ya Toto Magazine  imeamua kudhamini tamasha hilo na kutoa zawadi ya jarada la watoto ili waweze kusoma.

  Amesema kuwa jarida la watoto wanaweza kujifunza vitu ambavyo vitafanya watoto kupenda kusoma jarida hilo na kuacha kutumia muda wa kuangalia Luninga zenye katuni ambazo hazimjengei msingi wa elimu.

  Jacqueline amesema kuwa wataendelea kushiriki matamasha mbalimbali yanayohusu watoto katika kuweza kuwapa elimu katika majarida ya watoto.

   Amesema kampuni ya Toto Magazine ni kampuni pekee ambayo imejikita kutoa elimu kwa watoto katika kuwajengea msingi wa elimu wa kupenda shule.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Toto Magazine, Jacqueline Lesika akimkabidhi cheti  na Jarirda la Toto kwa  Mwanafunzi wa awali katika shule ya Shree Hindu Mandal, Hussein Swedi kwa ushindi wa mashinadano ya kuogelea katika shule hiyo kwa udhamini wa Toto Magazin iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Toto Magazine, Jacqueline Lesika akimkabidhi cheti  na Tshirt ya Toto Magazine  Jarirda la Toto kwa  Mwanafunzi wa awali katika shule ya Shree Hindu Mandal, Rabil Faraji kwa ushindi wa mashinadano ya kuogelea katika shule hiyo kwa udhamini wa Toto Magazin iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Toto Magazine ,Jacqueline Lesika akizungumza na waandishi habari hawapo pichani juu udhamini wa Tamasha la Kuogelea kwa Wanafunzi wa Shule ya Awali ya Shree Hindu Mandal jijini Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 1882 | 1883 | (Page 1884) | 1885 | 1886 | .... | 3278 | newer