Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1884 | 1885 | (Page 1886) | 1887 | 1888 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0


  0 0

  Na Agness Moshi na Bushiri Matenda –MAELEZO.

  Watanzania na wadau  mbalimbali wa sekta ya Afya nchini wameombwa kuendelea  kuisaidia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ili iendelee kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa huduma bora. 

  Hayo yamesemwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Mfuko wa Tulia Trust Mhe.Tulia Akson, wakati akikabidhi msaada  runinga nne na katoni mbili za maziwa vyenye thamani ya  shilingi 1,000,000 vilivyotolewa kwa watoto waliopo kwenye  Taasisi hiyo kwa  ushirikiano na Dstv, TSN na Kampuni ya Twincity.
   Dkt.Tulia amesema msaada  wa runinga unatimiza ahadi waliohaidi kwa taasisi hiyo na unamaana kubwa sana kwa sababu utawasaidia watoto wanaokaa hospitalini hapo kwa muda mrefu  kujifunza ,na kuwaburudisha  kwa kipindi chote cha matibabu ya awali  kabla ya kufanyiwa upasuaji.
  “Watoto hawa wanakaa muda mrefu hospitalini wakitibiwa hivyo wanashindwa kujumuika na wenzao kwa michezo jambo ambalo linawafanya wahisi upweke  kwa kuwapatia runinga kutawasaidia kuondoa hali hiyo , kuwaburudisha na kuwapa nafasi ya  kujifunza kupitia vipindi mbalimbali vinavyorushwa na king’amuzi cha DSTV”, alisema Dkt.Tulia
   Naye Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt.Mohammed Janabi amesema kuwa si watoto tu watakaofaidika kwani hata wazazi wao wataweza kujua mambo mbalimbali  yanayoendelea Nchini kwa kuangalia taarifa za Habari zitakazokua zinaonyeshwa kupitia chaneli mbalimbali. 
   “ Sio watoto wote wanaokuja hapa wanatatizo la moyo peke yake wengine wanakuja wakiwa na Magonjwa mengine  ambapo inabidi  tuanze kuwatibia kwanza magonjwa hayo ambapo wakati mwingine yanachukua muda mrefu  hivyo basi kwa kipindi chote hicho runinga hizi zitakua zikiwapa burudani, elimu kwa masomo mbalimbali kama vile kiingereza, hesabu  kwa watoto wakubwa na kwa wale wadogo wataburudika kupitia katuni”,alisema Dkt.Janabi.
   Dkt.Janabi ameongeza kuwa msaada wa maziwa waliopewa utasaidia kuimarisha afya za watoto wadogo wanaotibiwa kwani wapo wengine wamekuja wakiwa na Afya duni ,wengine wana magonjwa ya utapia mlo hivyo kupelekea kuchelewa kupatiwa matibabu.
  Aidha,Dkt.Janabi amemshukuru Dkt.Tulia kupitia Mfuko wake wa Tulia Trust kwa kuendelea kuhamasisha wadau mbalimbali kuipatia misaada Taasisi hiyo. 
   Kwa upande wake mtoto Mwamvita Hassani mwenye umri wa miaka 13 kutoka wilayani Kondoa kwa niaba ya watoto wanaotibiwa kwenye Taasisi hiyo ametoa shukrani zake kwa Naibu Spika na wadau waliowapa misaada hiyo.“Ninawashukuru sana kwakutuletea Tv na Maziwa,Tumefurahi na tunawaombea watuletee Tv zingine”, alisema Mwamvita.
  Dkt.Janabi  amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia upatikanaji wa vitanda kwa ajili ya Taasisi hiyo kwani wanakabiliwa na  changamoto mbalimbali ikiwemo swala la upungufu wa vitanda kwa wagonjwa kwani wanavitanda 128 tu ambavyo havikidhi mahitaji kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika kwa ajili ya matibabu.

  0 0


  Courtesy of KIM TV

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amesema kuanzia Agosti 30 mwaka huu, Serikali itatangaza zabuni ya kuanza ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Umeme wa megawati 2100 katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji mkoani Pwani  eneo la Stiegel’s Gorge
  Akizungumza jijini Dar es Salaam Dkt. Kalemani  amesema,  taratibu za awali zimeshaanza ambapo wataalaumu  wa ndani na nje wameshakutana na kuchagua sehemu za kujenga mradi huo katika Mto Rufiji, ambapo tayari Shirika la Umeme Nchini ( Tanesco ) limeanza upembuzi yakinifu wa kujenga miundombinu ya umeme na Wakala wa barabara nchini  (Tanroad) kujenga miundombinu ya  barabara.
  Ujenzi wa mradi wa umeme wa megawati 2100 kutoka maporoko ya maji ya Mto Rufiji Mkoani Pwani ( Stiegler’s Gorge)unatarajiwa kuanza ndani ya kipindi cha  miezi miwili ijayo baada ya taratibu za zabuni kukamilika, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amewambia watanzania kuwa, tayari Serikali imetenga fedha za kutekeleza mradi huo, na hatua za awali za utekelezaji zimekwisha fanyika, ambapo tarehe 30 ya mwezi  huu wa Agosti Serikali itatangaza zabuni kwa wakandarasi wa ndani na nje ya nchi ili waweze kuomba kufanya kazi .
  Dkt. Kalemani amesema mkandarasi atakayepewa kazi ya kujenga mradi huo ni yule tu atayeridhia kujenga kwa gharama nafuu na kwa muda mfupi zaidi ya uliowekwa Pia Dkt. Kalemani anatoa ufafanuzi namna ambavyo Serikali imejiandaa katika kutekeleza mradi huo.
  Kwa mujibu wa Dkt Kalemani, mradi huo utakapokalimilika utakasaidia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme nchini  na kwamba Serikali haitarajii kuongeza bei ya umeme. 
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani akishuka kwenye boti kwa ajili ya kuelekea kwenye eneo la Stieglers Gorge kutakapojengwa mradi huo.

  0 0

   The much anticipated show 'UNTOLD' is now officially available on our YouTube channel UNTOLD. Our main goal is to Educate, Inspire and Entertain. You can now watch the first episode featuring Wasia Maya, who shares his life journey from Tanzania to the United States and talks about all the adversity he faced in his younger days. His story is truly exceptional and many of us can learn from it.

  0 0

  Mtindo wa karate mkongwe  duniani, Okinawa Goju Ryu wa chama cha  Jundokan  Tanzania chini ya mwakilishi wake Sensei Rumadha Fundi  mwenye Dan 4,“Yondan” pia mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 38 ya mafunzo ya sanaa ya Karate mtindo wa Goju Ryu chini ya walimu wakuu wengi maarufu toka Okinawa, Japan kama vile Master Mario Higaonna(IOGKF), Master Masataka Muramatsu( Goju Ryu Kyokai), Teruo Chinen( Jundokan International), na hatimae Kancho Yoshihiro Miyazato, mwenyekiti wa (Jundokan So Honbu, Naha, Okinawa)Master Tetsunosuke Yasuda, Master Tsuneo Kinjo na Master Tetsu  Gima.

  Tunatarajia kufanya mitihani ya mikanda mieusi miezi ijayo madaraja tofauti kupitia dojo za “ Kaizen dojo” Jamhuri na dojo dada ya Hekalu la Kujilinda Zanaki dojo. Hii ni moja ya jitihada za kusambaza mwenendo huu kwa kina na pia ufundishaji wa mbinu za utumiaji wa tafsiri za “Kata” uijulikanao kama “Bunkai”, au uchambuzi wa matumizi ya mbinu za kujilinda. Mitihani yote itafanywa na sensei Rumadha Fundi chini ya utaratibu wa “Syllabus”  ya Jundokan, Okinawa.

  Lengo pia ni kuzungumzia yale yote yaliojiri katika semina kuu ya Jundokan bara la Ulaya chini ya master wake toka jijini Naha, Okinawa mwezi wa Julai 2017. Ufundishaji sahihi wa mfumo huu ni moja ya malengo kuhakikisha tu kwamba wana Jundokan duniani mkote wapo kwenye msimamo mmoja katika uchambuzi na ufanyaji wao wa Kata na matumizi yake.

  Pia wakati huohuo, kutakuwa na semina ya wanafunzi wa ngazi za mikanda mieusi wa Jundokan Tanzania ikiwemo na dojo ya Zanaki katika kuwawezesha wanafunzi wake kuuliza na kupata majibu ya matumizi yao ya ufanyaji Kata kama jinsi ipasavyo chini ya chama hicho chenye ufahasa wa mtindo huo unaofuata nyanyo za mafunzo ya Master Chojun Miyagi, mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu.

  Hivyo, hii ni moja ya fursa kubwa kwa wana Jundokan kuweza kushiriki semina hii chini ya mwakilishi wa Jundokan Tanzania, ama kamaijulikanavyo “Tanzania Shibu-Cho”, sensei Rumadha Fundi. Sensei Rumadha, amesisitiza kwa niaba ya chama hicho kwamba Kila mwanafunzi wa mkanda mweusi, hana budi kuhudhuria semina za walimu angalau mara moja kila miaka miwili na kupata usahihisho muhimu kimafunzo. Hilo ndio lengo kuu hata kipindi kile kwa mwanzilishi wa Okinawa Goju Ryu Tanzania, marehemu Sensei NC Bomani kufanya ziara za mara kwa mara kwenda huko Naha, Okinawa kupata marekebisho toka kwa magwiji wa Karate duniani na chimbuko lake.

  Pia vilevile, Tanzania imepatiwa mwaliko wa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 65 tokea kuanzishwa kwa chama cha Jundokan itayofanyika November 2018 mjini Naha, Okinawa, Japan. Chama hicho kilianzishwa na mwanafunzi mkuu wa Master Miyagi aitwae Master Eiichi Miyazato sensei 1957 ambae pia alikuwa ndio mwalimu wa sensei Nantambu C Bomani. “ Chuo kinacho fundisha nyayo au mwenendo wa Master Chojun Miyagi”. Ikimaanisha, hamna mabadiliko yeyote kimafunzo na Kata zake kama jinsi alivyokuwa akifundisha mwanzilishi wake Chojun Miyagi sensei.
  0 0
  0 0


  0 0

  Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Zanzibar wameitembelea Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa lengo la kudumisha ushirikiano na kujifunza mbinu mbalimbali zinazotumiwa na Bodi katika kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi. 

  Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii, Bw. Geofrey Meena alitoa ufafanuzi wa kina kuhusu shughuli zinazofanywa na Bodi ikiwa pamoja na namna inavyoshirikiana na Balozi za Tanzania zilizopo katika nchi mbalimbali, Mabalozi wa Hiari wa Utalii wanavyosaidia kutangaza utalii wa Tanzania katika nchi zao, Namna Bodi inavyoshirikiana na vyombo mbalimbali vya Habari vya ndani na nje katika kutayarisha vipindi vya utalii wa Tanzania. 
   
  Aidha Bw, Meena alisisitiza kuwa mialiko ya Timu maarufu za mchezo wa mpira wa miguu kuwa moja ya njia yenye manufaa makubwa katika kuitangaza Tanzania

  Ujumbe huo uliyongozwa na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mhe. Rashid Ali Juma ambaye alionyesha kuridhishwa na juhudi zinazofanywa na Bodi, alisema “ziara yetu imekuwa ni ya mafanikio kwani tumeweza kujifunza mikakati inayotumiwa na Bodi katika kutekeleza jukumu lake la kutangaza utalii wa Tanzania hasa Utalii wa Ndani”.
   
   Pia ujumbe huo uliipongeza Bodi kwa kuwa na mipango madhubiti ya utangazaji pamoja na kutengeneza video maalumu inayotumika kuvitangaza vivutio hivyo katika matukio mbalimbali ya kimataifa. Ziara hiyo Ilifanyika tarehe 28/08/2017.
  Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii, Bw. Geofrey Meena akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati ya Baraza la wawakilishi ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utaliiya Zanzibar walipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii, Dar es Salaam.
  Mjumbe wa Kamati ya Baraza Wawakilishi ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Zanzibar akitumia lugha ya alama kutafsiri jambo kwa moja ya mjumbe wa Baraza Hilo.
  Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mhe. Rashid Ali Juma (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya  Baraza la Wawakilishi ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Zanzibar.

  0 0

  Today, August 28th, 2017 H.E. Ambassador Wilson Masilingi received at the Tanzania House  the new Ambassador of the Republic of Uganda to the United States of America, H.E. Mull Sebujja Katende, who paid a courtesy call to him in Washington, D.C.
   H.E. Ambassador Wilson Masilingi with H.E. Mull Sebujja Katende , Ambassador of the Republic of Uganda to the United States of America.
  H.E. Ambassador Wilson M. Masilingi with H.E. Mull Sebujja Katende , Ambassador of the Republic of Uganda to the United States of America and Uganda Embassy’s Minister Counselor Mr. Dickson Ogwang (right)

  0 0

  Beatrice Lyimo- Maelezo,Dodoma

  Watendaji wa wa Serikali wametakiwa kufanya kazi kwa kujituma na weledi ili kuendana na dhana ya Serikali ya awamu ya Tano inayosisitiza uwazi na uwajibikaji katika kuwahudumia wananchi katika maeneo yakutolea huduma.

  Akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa watumiaji wa mfumo wa kielektroniki wa kuandaa Mipango,Bajeti na Ripoti (PlanRep)za Mamlaka za Serikali za Mitaa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bibi Rehema Madenge amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuongeza tija katika kuwahudumia wananchi.

  “Sasa ni lazima watumishi wa umma katika maeneo yakutolea huduma mbadilike na muendane na Dhana ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa Kazi Tu inayosisistiza kutoa huduma bora zinazolenga kuboresha maisha ya wananchi wa chini” Alisisitiza Bi Rehema

  Akifafanua Bi Rehema amesema kuwa matokeo ya matumizi ya mfumo huo ulioboreshwa yanaonekana na yatagusa maisha ya wananchi wote katika maeneo yao kwa kuwa yatasaidia kuongeza tija na uwajibikaji hali itakayosaidia kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.

  Aliongeza kuwa mfumo wa PlanRep ulioboreshwa utatumika kuanzia ngazi ya msingi yaani vituo vya kutolea huduma za kijamii ikiwemo Zahanati,Hospitali na Shule.Mfumo huu wa kuandaa Mipango,Bajeti na Kutoa Ripoti utapunguza gharama kwa kiasi kikubwa zilizokuwa zikitumika awali kabla ya kuanza kwa mfumo huu mpya.

  Kwa upande wake, Kiongozi wa Timu ya Mifumo ya TEHAMA kutoka mRadi wa PS3 Desderi Wengaa amesema kuwa lengo la mradi huu ni Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unatakekelezwa na Serikali ya Tanzania ukilenga kuimarisha Mifumo katika Sekta ya Umma ili kuboresha utoaji wa huduma za Serikali za Mitaa kwa Jamii hasa zile zenye uhitaji zaidi.

  “Mradi huu unafanya kazi katika maeneo makuu matano ambayo ni Utawala Bora, Ushirikishwaji wananchi, Rasilimali watu, Rasilimali Fedha, Mifumo ya TEHAMA pamoja na Tathimini na ufutiliaji” alisema Desderi Wengaa.

  Kiongozi huyo aliongeza kuwa, mfumo huu umesukwa na wataalamu wazalendowa hapa nchini na upo tayari kupokea mabadiliko kulingana na mahitaji ya wakati, na vilevile utasaidia kupunguza muda na gharama za uaandaaji wa Mipango na Bajeti.

  Mradi wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma(PS3) ni mradi wa miaka mitano ulia mnamo Julai 2015 na kutarajiwa kukamilika Julai 2020 ambapo utarahisisha utendaji kazi na kusaidia kutatua changamoto zilizokuwepo awali.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bibi Rehema Madenge akifungua mafunzo kwa watumiaji wa Mfumo mpya wa Kielektroniki ulioboreshwa (PlanRep) yanayofanyika mjini Dodoma yakiwashirikisha Waganga Wakuu wa Mikoa,Halmashauri,Maafisa Mipango,Makatibu wa Afya,Wachumi na Wahasibu.
  Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Erick Kitali akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
  Kiongozi wa Timu ya Mifumo kutoka Kutoka mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bw. Desderi Wengaa akitoa maelezo kuhusu utendaji wa Mfumo huo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo mjini Dodoma.
  Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bibi Rehema Madenge akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo mara baada ya hafla ya ufunguzi.Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo Dodoma.

  0 0


  Kampuni ya Acacia, kwa ushirikiano na TANESCO, imejenga kituo cha kupozea umeme kilichopo katika mgodi wake wa dhahabu wa Bulyanhulu ambacho kimeweza kuongeza uhakika wa upatikanaji wa umeme katika maeneo ya mgodi huo.

  Acacia imewekeza shilingi bilioni 5.5 katika mradi huo ambao utanufaisha maeneo yanayozunguka migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na maeneo mengine ikiwa ni pamoja na Kahama, Shinyanga, Msalala, na sehemu nyingine za Geita.


  Ujenzi wa Kituo hicho ulianza Desemba 2016 na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

  Haya ni maendeleo makubwa kwa viwanda na biashara zinazozunguka eneo hilo ambazo zitafaidika na uwepo wa umeme wa uhakika jambo litakalosaidia kuboresha ufanisi na kuongeza uzalishaji.


  Mkuu wa kitengo cha miradi ya maendeleo wa mgodi wa Bulyanhulu, Jiten Divecha ameeleza kuwa tatizo la mabadiliko ya nguvu ya umeme limekuwepo kwa muda mrefu na limekua likisababisha uharibifu mkubwa wa mashine.“Ujenzi wa kituo hiki utasaidia kupunguza athari zinazotokana na kuongezeka au kupungua kwa nguvu ya umeme katika migodi yetu hivyo kuboresha shughuli za uzalishaji. Wakazi na viwanda vinavyotumia umeme katika wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga na wilaya zingine za mkoa wa Geita zitafaidika na uwekezaji huu pia,” alisema Jiten.

  Aliongeza: "Acacia inajitahidi kuleta manufaa ya kiuchumi ya pamoja kwa jamii zinazotuzunguka na wadau wake kupitia miradi endelevu."

  Wakati wa ujenzi wa kituo hicho, ajira mbalimbali zilitolewa kwa jamii zinazozunguka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu.
  Akizungumzia fursa hiyo, David Nyanda alisema: “tunathamini sana ujenzi wa mradi huu kwa sababu tumepata fursa za ajira. Japokuwa fursa hizi ni za muda, tunaweza kupata mapato ili kuendesha familia zetu hasa katika kipindi hiki cha ukame.”

  0 0

  Na Ali O. Ali

  Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mh. Khatibu Juma Mjaja ameelezea  matumaini yake ya mafanikio katika sekta ya utalii kisiwani Pemba kupitia tamasha la michezo na utamaduni lililoandaliwa na Taasisi ya Rafiki Network.

  Akizungumza mara baada ya kupokea cheti cha shukrani Ofisisni kwake Chake Chake Bwana Mjaja amesema Rafiki Network imefungua njia katika kuimarisha utalii wa ndani na nje ya nchi kutokana na kuandaa na kusimamia Tamasha la kimichezo liloandaliwa kwa ubunifu na ustadi huku likijumuisha michezo mbali mbali ya asili ambayo niburudani kwa wenyeji na kivutio kwa wageni.

  Mh. Mjaja ameuomba uongozi wa Taasisi ya Rafiki Network kuhakikisha kwamba Tamasha hili linakua endelevu ambapo amebainisha kwamba kuendelea kwa tamasha hilo kila mwaka kutasaidia kukuza hali za watu katika Nyanja mbali mbali kiuchu na kiutamaduni.

  Akifafanua ubunifu uliofanyika katika maandalizi ya Tamasha la kimichezo Kisiswani Pemba, Mh. Mjaja amesifu uteuzi na mpangilio wa barabara zilizotumika katika mchezo wa mbio za Baiskeli nakuongeza kwamba mpangilio huo uliwapa fursa wananchi waliowengi kuweza kushiriki kikamilifu katika michezo mbali mbali. Afisa huyo pia amewapongeza Azam TV kwa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bonanza hilo.

  Nae Afisa Mdhamini Kamisheni ya Utalii Pemba Maalim Suleiman Amour Suleiman amepokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa Taasisi ya Rafiki Network kutokana na mchango wake mkubwa katika kufanikisha Tamasha hilo.

  Taasisi ya Rafiki Network iliandaa Tamasha la kimichezo Kisiwani Pemba mnamo Julai 28-30 ambalo lilijumuisha michezo mbali mbali ikiwa ni pamoja na mchezo wa Ng’ombe, Mashindano ya Baiskeli, Mashindano ya  kuogelea na Resi za Ngalawa.

   Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mh. Khatibu Juma Mjaja akipokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa Taasisi ya Rafiki Network Bw. Ali Othman Ali Ofisini kwake Chake Chake Pemba.

  Afisa Mdhamini Kamisheni ya Utalii Maalim Suleiman Amour Suleiman akipokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa Taasisi ya Rafiki Network Bw. Ali Othman Ali Ofisini kwake Chake Chake Pemba.


  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Juma Homera .
  Serikali ya Wilaya ya Tunduru imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli la kujenga kituo cha Afya kila kata kwa nchi nzima, Ambapo wilaya hiyo tayari imenza ujenzi wa kituo cha Afya katika kata ya Nakayaya . Ujenzi wa kituo hicho cha Afya umefikia hatua ya kuezekwa na unatarajiwa kukamilika mwakani .Hii hapa video yenye habari hiyo.

  0 0

  Asteria Muhozya na Zuena Msuya, DSM

  Serikali imesema kuwa ifikapo tarehe 30 Agosti, mwaka huu itatangaza Zabuni ya kuanza ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 2,100 katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji. (Stiegler’s Gorge).

  Hayo yalielezwa jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani wakati akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

  Dkt. Kalemani alitoa wito kwa Watanzania, Taasisi Binafsi na Kampuni zenye uwezo kutoka ndani na nje ya nchi kujitokeza kuomba zabuni hiyo mara baada ya kutangazwa na kuongeza kuwa, Serikali inazo fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi husika.

  Aliongeza kuwa, tayari taratibu za awali za utekelezaji wa mradi huo zimekwisha anza ambapo Wataalam kutoka ndani na nje ya nchi wamekwishakutana na kupitia nyaraka za mradi ikiwemo kuchagua eneo ambalo mradi husika utajengwa.

   Watalaam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakielendelea na kazi ya kukamilisha nyaraka mbalimbali kuhusu mradi husika.

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kutangazwa Zabuni ya Mradi wa Kuzalisha umeme wa Rufiji. Wanaofuatilia ni Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam mnamo tarehe 26/8/2017 lilitoa taarifa ya awali ya tukio la mlipuko uliotokea katika ofisi za mawakili wa IMMMA zilizopo katika eneo la Upanga jijini Dar Es Salaam.

  Hivyo Jeshi la Polisi linapenda kuufahamisha umma kuwa uchunguzi wa awali uliofanyika umebaini kwamba usiku wa kuamkia tarehe 26/8/2017 majira kati ya saa 7:00-8:00 watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi kamili, walifika katika ofisi za mawakili wa kampuni ya IMMMA (IMMMA ADVOCATES) wakiwa na magari mawili wakijifanya ni askari na kuwarubuni kisha kuwachukua walinzi wa jengo hilo na kuondoka nao kwenye moja ya gari walilokwenda nalo, ambapo baadaye walinzi hao walikutwa maeneo ya Kawe wakiwa hawajitambui.

  Aidha, kundi lililobaki liliingia ndani ya Ofisi hizo na kuweka milipuko iliyotengenezwa kienyeji ambayo baada ya watu hao kuondoka ililipuka na kusababisha uhalibifu wa mali na jengo la ofisi hiyo pamoja na majengo ya jirani.

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm linapenda kuwahakikishia wananchi kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini watu hao waliofanya tukio hilo pamoja na kujua dhamira yao ili wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria.

  Aidha tunapenda ifahamike kuwa wajibu wa Jeshi la Polisi ni kulinda maisha ya watu na mali zao hivyo kamwe haliwezi kutumika kuhujumu maisha ya watu na mali za wananchi.

  Tunaomba waathirika wa tukio hili na wananchi kwa ujumla kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vikiendelea na upelelezi wa tukio. Vilevile, tunatoa rai kwa wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia katika upelelezi waziwasilishe kwa Jeshi la Polisi ili zifanyiwe kazi.

  B.M. KITALIKA- SACP
  KAIMU KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
  DAR ES SALAAM

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  UONGOZI wa klabu ya Mbao Fc umeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya milioni 149 na kampuni ya GF Trucks & Equipments ikiwa ni udhamini wa timu hiyo kutoka Jijini Mwanza.

  Kampuni hiyo imeridhishwa na maendeleo ya timu hiyo na kuamua kuwapatia udhamini kwani hawajawahi kushiriki katika udhamin i wa soka la Kiwango cha ligi kuu.

  Mkataba huo uliosainiwa mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Imrani Karmali amesema kuwa mkataba huo ni wa kihistoria kwani unaenda kuleta na kukuza maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
  Mkurugenzi wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani Karmali na Mwenyekiti wa Mbao Fc Solly Zephania Njashi wakionyesha hati ya makubaliano ya Mkataba ikiwa ni mkataba wa udhamini wa timu hiyo kwa mwaka mmoja wenye thamani ya Milioni 140 sambamba na basi la wachezaji.
  Karmal amesema kuwa, madhumuni makubwa ni kukuza vipaji vya mpira wa miguu na wanatarajiwa kuisaidia Mbao Fc kufikia malengo yao msimu huu, " tunafahamu usafiri umekuwa ni tatizo kwa klabu nyingi ndogo za Ligi Kuu na hicho kimetupelekea kuanza na basi msimu huu ambapo katika mkataba wa milioni 140 utajumuisha sambamba na basi hilo la wachezaji lenye thamani ya milioni 70,".

  "uwezo waliouonesha katika ligi kuu na hata kuingia fainali ya kombe la FA ulituhamasisha kuifuatilia kwa ukaribu sana na tuna imani kwa msaada wetu Mbao itaendelea kufanya vizuri na si hao tu bali hata ajira kwa vijana zitaongezeka,"amesema Karmali.

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mbao Fc, Solly Zephania Njashi ameusifu mkataba huo na kusema kuwa utazidi kuleta chachu ya maendeleo katika klabu yao na hata kupunguza gharama za mahitaji kwa wachezaji.

  Njashi ameishukurui kampuni ya GF Trucks & Equipments kwa mkataba huo na kuwaahidi mashabiki na wapenzi wa Mbao kuwa mwaka huu wataendelea kufanya vizuri na kuendelea kusalia katika Ligi kuu msimu ujao.

  Baada ya kusaini mkataba huo, kampuni ya GF Trucks & Equipments i iliwakabidhi mfano wa jezi zitakazovaliwa na timu ya Mbao tayari zikiwa zimeshaweka nembo ya kamouni hiyo.
  Mwenyekiti wa Mbao Solly Zephania Njashi akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuingia makubaliano ya udhamini wa mkatabwa mwaka mmoja na na kampuni ya GF Trucks & Equipments wenye thamani ya Milioni 140, kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani Karmali 
  Afisa Masoko wa Kampuni ya GF Trucks & Equipments Kulwa Bundala akizungumza na wanahabari baada ya kuingia mkataba na timu ya Mbao Fc wenye thamani ya Milioni 140 kwa mwaka mmoja.
  Mkurugenzi wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani Karmali na Mwenyekiti wa Mbao Solly Zephania Njashi wakionyesha jezi za Mbao zitakazotumikia mwaka huu.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi akimkabidhi vifaa mkulima Trekta ndogo ya mkono (Power tillers) aliyevaa fulana ya rangi ya njano na kofia na wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Zanzibar Nadir Abdul-Latif Yussuf aliyetoa vifaa hivyo kwa wananchi hao.
  baadhi ya wananchi na viongozi waliofika katika hafla fupi ya makabidhiano ya matrekta (Power tillers) mbili na mashine moja ya umeme wa jua(solar).

  Na Is-haka Omar, Zanzibar.

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewataka  wabunge, wawakilishi na madiwani kuhakikisha miradi wanayopeleka majimboni inawanufaisha wananchi wote. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dkt. Abdulla Juma  Mabodi wakati akikabidhi matrekta madogo ya mkono (Power tillers) mbili na mashine ya umeme wa solar moja kwa wakulima wa jimbo la Chaani zilizotolewa na Mwakilishi wa Jimbo hilo Nadir Abdul-Latif Yussuf.


  Dkt. Mabodi alisema ahadi zinazotekelezwa na viongozi mbali mbali wa majimbo nchini ni lazima ziwanufaishe wananchi wote ili kufikia malengo ya mapinduzi kwa vitendo. Alieleza kuwa vifaa hivyo vya kilimo vilivyotolewa na mwakilishi huyo vinatakiwa kutumiwa vizuri na wakulima ili visaidie shughuli za kilimo katika jimbo hilo.

  Aidha Dkt. Mabodi aliwasisitiza viongozi na watendaji wapya waliochaguliwa katika uchaguzi unaoendelea hivi sasa ndani ya chama na jumuiya zake kufanya kazi za taasisi hiyo kwa bidii ili  chama hicho kiweze kushinda katika uchaguzi mkuu ujao.

  “ Nawapongeza viongozi wanaotekeleza Ilani ya Uchaguzi  wa CCM ya mwaka 2015/2020 kwa kasi ili wananchi waweze kunufaika na fursa  mbali mbali za maendeleo zinazofanywa na viongozi wao.”, alisema Mabodi.

  Naye  Mwakilishi  wa Jimbo  hilo ,  Nadir Abdul-Latif Yussuf alisema vifaa hivyo vilivyokabidhiwa vyenye thamani ya shilingi milioni 21 ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi alizotoa kwa wananchi wa jimbo hilo wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita. Nadir aliwapongeza wananchi wa jimbo hilo kwa kumuunga mkono katika masuala mbali mbali ya kijamii hali inayompa nguvu za kuendelea kutatua kero zinazowakabili katika nyanja za kijamii na kiuchumi.

  Alisema lengo la kutoa vifaa hivyo kwa wananchi wa jimbo hilo ni kupunguza changamoto za upungufu wa pembe jeo za kilimo zilizokuwa zikiwakabili wakulima wa jimbo hilo kwa muda mrefu.

  0 0

  Wizara ya Nishati na Madini imetoa mafunzo ya Mfumo wa pamoja wa Kukusanya Maduhuli ya Serikali (GePG) kwa Maafisa Madini na Wahasibu wa Wizara hiyo ili kuboresha shughuli za ukusanyaji maduhuli.

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Anthony Tarimo alisema kuwa mafunzo yamelenga kuwawezesha washiriki kuuelewa vyema mfumo huo ili kuwa na ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali wenye tija.

  Alisema Serikali imeamua kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa maduhuli kuwa wa kielektroniki ili kurahisisha ukusanyaji wa maduhuli na vilevile kuongeza uwazi miongoni mwa Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali.

  “Kupitia mfumo huu, Serikali inao uwezo wa kujua maduhuli yote yanayoingia kwa wakati mmoja kwa sababu umeunganishwa na Wizara na Taasisi mbalimbali,” alisema Tarimo.

  Alibainisha kuwa Mfumo huo wa GePG ulianza kutumika rasmi Julai, 2017 na kwamba kwa upande wa Wizara ya Nishati na Madini mafunzo ya awali yalitolewa kwa watumishi wa Ofisi ya Madini- Kanda ya Mashariki ambayo inahusisha ofisi za madini za Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Handeni na Morogoro.
  Alisema Mfumo huo ni rafiki na kwamba utaboresha na kurahisisha ukusanyaji wa maduhuli na kwamba mara baada ya mafunzo, washiriki watakuwa na uwezo wa kuutumia ipasavyo. Tarimo alisema mafunzo hayo yanawahusu Wahasibu, Maafisa Leseni pamoja na watumishi wengine ambao kwa njia moja ama nyingine wanahusika na utoaji wa hati za madai za malipo mbalimbali.

  Aliongeza kuwa, mafunzo hayo yanahusisha uwasilishaji wa mada mbalimbali kutoka kwa wataalam wa TEHAMA wa Wizara ya Fedha na Mipango na wa Wizara ya Nishati na Madini na pia yatahusisha majadiliano ili kuboresha utendaji kazi wa watumishi wanaohusika na ukusanyaji wa maduhuli.

  “Wanasheria pia watawasilisha mada ili kuelewa vyema mabadiliko katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010 yaliyofanyika hivi karibuni,” alisema  Tarimo. Mafunzo hayo ya siku nne yanafanyikia katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro (SUA) na yameanza Agosti 28, 2017 kwa kushirikisha zaidi ya washiriki 100.

older | 1 | .... | 1884 | 1885 | (Page 1886) | 1887 | 1888 | .... | 3278 | newer