Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

NANI MBABE NGAO YA JAMII KESHO? YANGA KUENDELEZA UBABE AU SIMBA KULIPIZA KISASI?

$
0
0


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KUELEKEA mtanange wa kumaliza ubishi baina ya mahasimu wawili Simb ana Yanga huku kila upande ukijinasibu kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa kesho kuanzia majira ya saa 11 jioni Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Ni mechi ya watani wa jadi inayozungumzwa sana midomoni mwa watu, kila mmoja akijinasibu kumfunga mwenzake kwa idadi kubwa ya magoli na na kuinyakua Ngao ya Jamii.

Simba ikiwa imefanya usajili mkubwa sana na wagharama, wakiwajumuisha nyota wanne kutoka Azam Fc John Bocco, Shomari Kapombe, Aishi Manula na Erasto Nyoni pamoja na Kiungo Mnyarwanda kutoka Yanga aliyekipiga kwa misimu kadhaa Haruna Niyonzima.

Mbali na hao, wamemsajili golikipa wa Timu ya Taifa akitokea Mtibwa Sugar Said Dunda na Emanuel Mseja kutoka Mbao Fc, beki wa kulia Shomary Ally, beki wa kati kutoka Toto Africa Yusuf Mlipili, Salim Mbonde kutoka Mtibwa na Mshambuliaji Emanuel Okwi kutoka Sc Villa ya Nchini Uganda. Nicolaus Gyan kutoka Nchini Ghana na beki wa kushoto kutoka Mbao Jamal Mwambeleko 

Kwa upande wa Yanga, wameweza kufanya usajili kwa kuwasajili Ibrahim Ajib kutoka Simba, Raphael Daud kutoka Mbeya City, Pius Buswita kutoka Mbao Fc, Gadiel Michael kutoka Azam, Papii Kabamba Tshishimbi wa Mbabane Swallows na wameweza kuwapanisha vijana wao kutoka timu B Said Musa, Maka Edward ili kuja kuziba nafasi zilizoachwa wazi na wachezaji walioachwa pamoja na wale waliosajiliwa na timu zingine.


Yanga walifanikiwa kuwabakisha wachezaji muhimu kama Donald Ngoma, Thaban Kamosoku na Amisi Tambwe waliokuwa wamemaliza mikataba ya kuitumikia klabu hiyo ya Yanga.


Nimefunga mjadala wa Rambirambi-RC Gambo

$
0
0
Hatimaye utata uliokuwa umeenea wa kuwepo kwa ufujaji na matumizi mabaya ya fedha kiasi cha milioni 285.49 zilizokuwa zimechangwa na wadau pamoja na serikali kwa ajili ya rambi rambi ya vifo vya ajali ya basi la wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent umekwisha baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kukabidhi milioni 23.27 kwa wazazi wa watoto walionusurika katika ajali hiyo.

Akikabidhi fedha hizo mbele ya waandishi wa habari ambapo kila mzazi amepata Milioni 7.75, Bw. Gambo amesema fedha hizo zilikuwa zimebaki baada ya matumizi ya shughuli za mazishi kwa watoto 32 walimu wawili na dereva waliokuwa wamekufa katika ajali hiyo na matumizi mengine yakiwemo ya wazazi waliokuwa nchini marekani kwa ajili ya kuwauguza watoto wao na kwamba matumizi ya fedha hizo watapanga wao wenyewe.

Katika hatua nyingine Bw Gambo alisema Serikali imekubali kutoa wataam wa saikolojia kwa ajili ya kuendelea kuwasaidia watoto walionusurika katika ajali ya basi la wanafunzi ili kuwaweka sawa na pia kuwaandaa kufanya mtihani wa darasa la saba unaowakabili mnamo mwezi Septemba.

Aidha Bw, Gambo amesema kazi ya kutoa tiba ya kisaikolojia pia ilishafanyika kwa wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent .Wakizungumza baada ya kukabidhiwa Fedha hizo wazazi wa watoto hao wameishukuru serikali na wafadhili kutoka marekani kwa msaada mkubwa kwa watoto wao tangu mwanzo hadi sasa.

Aidha wazazi hao wamesema pamoja na watoto wao kuwa nje ya shule kwa zaidi ya miezi mitatu wako tayari kufanya mtihani na kumaliza ELIMU ya msingi unaotarajiwa kufanyika mwezi September.

Kwa mujibu wa Bw Gambo baada ya kutokea kwa AJALI hiyo MWEZI May 2017 wadau MBALIMBALI na serikali walijitolea na kuchanga fedha na kupatikana zaidi ya milioni 285.49 ambazo nbaada ya matumizi zilibaki milioni 23.27 ambazo zimekabidhiwa leo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RC Gambo akiwakabidhi wazazi wa Doreen Mshana jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi.
RC Gambo akiwakabidhi wazazi wa Wilson Tarimo jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi.
RC Gambo akimkabidhi mzazi wa Shadhia jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi
Kushoto ni mtoto Shadhia na Kulia ni mtoto Wilson wakitoka nje ya jengo la ofisi ya Mkuu wa mkoa
Mhe Gambo akisalimiana na mtoto Doreen Mshana

Mhe Gambo katika picha ya pamoja na manusura wa ajali ya Lucky Vincent walipotembelea ofisi yake mapema hii leo. 

UK Government Pledges More Support to Tanzania

$
0
0

Government of the United Kingdom has expressed its readiness to continue its support to Tanzania’s development programs.

Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, Ambassador Dr. Augustine Mahiga today said that UK which is a major bilateral donor to Tanzania has pledged to increase its support to various socio-economic development programs.

“As a lead bilateral donor after World Bank, UK is also among top five countries leading in investments and business in the country”, said Ambassador Mahiga.

Minister Mahiga was addressing members of the press about a two-day visit of the Minister for Africa at the UK Foreign and Commonwealth Office and UK Department of International Development Mr. Rory Stewart.

He noted that UK is supporting various sectors of development in the country including education, health sectors, rural roads and other special areas.

Ambassador Mahiga further told the press that UK support has moved from previous budget support to special Prosperity Partnership aimed at strengthening economic cooperation based on shared priorities areas including agriculture, infrastructure, renewal energy and water.

He added that apart from supporting development projects and social services, UK is also supporting anti-poaching campaign and environmental conservation.

He paid special tribute to UK government for assisting Tanzania government in addressing special challenges like anti-poaching campaign, human and drug trafficking as well as money laundering. 

Tanzania’s Minister of Foreign Affairs and East African Cooperation, Dr. Augustine Mahiga (right) addressing the members of the press about the visit of UK’s Foreign Minister responsible for Commonwealth Office and UK Department of International Development Mr. Rory Stewart.

ATCL KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA NDEGE ZANZIBAR

$
0
0

Serikali imesema kuwa Shirika la Ndege nchini (ATCL), litaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha inaboresha huduma za usafiri wa anga katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Akizungumza katika kikao kilichokutanisha Baraza la Waakilishi la Kamati ya Mawasiliano na Ardhi kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na uongozi wa Shirika hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, amesisitiza kuwa changamoto ambazo wameziwasilisha katika kikao hicho zitafanyiwa kazi ili kuleta tija kwa pande zote mbili.

“Nawahakikishia wajumbe wa kamati hii kuwa changamoto mlizonazo tutazifanyia kazi haraka kwani ATCL sasa imezaliwa upya na hivyo itahakikisha inaboresha maslahi ya kuliinua na kuliendeleza shirika ili kuweza kukidhi mahitaji ya hapa na visiwani”, amesema Naibu Waziri Ngonyani.

Aidha, Mhandisi Ngonyani ameongeza kuwa katika kuhakikisha huduma za usafiri wa anga visiwani humo zinaimarika, tayari Serikali imeshaanza kulipa deni lililokuwa linadaiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege la shilingi milioni 241 ambalo shirika hilo linadaiwa kutokana na tozo ya maegesho ya ndege na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Hamza Juma, amemwomba Naibu Waziri Mhandisi Ngonyani kuangalia upya suala la ajira katika Shirika la ATCL ili liweze kubeba sura ya Muungano na kuwawezesha wataalam wenye sifa kutoka Zanzibar nao kupata nafasi hizo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akiongea na Baraza la Wawakilishi la Kamati ya Ardhi na Mawasiliano kutoka Zanzibar na uongozi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), (hawapo pichani), wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano kutoka Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma, akizungumza na wajumbe na watendaji, katika ziara ya kikazi kwenye Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Eng. Ladislaus Matindi (katikati) akifafanua jambo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Kamati ya Ardhi na Mawasiliano kutoka Zanzibar, wakati wa ziara ya kikazi kwenye Shirika hilo, jijini Dar es Salaam.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 22.08.2017

MAGAZETI YA JUMATANO LEO AGOSTI 23,2017

ASILIMIA KUBWA YA WANANCHI WAISHIO VIJIJINI HAWANA ELIMU YA KUTOSHA KUHUSU HUDUMA ZA MAWASILIANO -TCRA CCC

$
0
0
 Mjumbe wa Baraza na Mwenyekiti wa kamati ya Elimu na Uhamasishaji Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano,John Njawa akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar kuhusiana na utafiti walioufanya kwa Watumiaji wa huduma za mawasiliano hivi karibuni wakishirikiana na Chuo cha Mipango cha Dododoma.Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano,Mary Shao Msuya na kushoto ni Mjumbe wa Baraza na Kamati ya Elimu Uhamisishaji -Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC),Nyanda Shuji
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo
 Mjumbe wa Baraza na Mwenyekiti wa kamati ya Elimu na Uhamasishaji Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano ((TCRA CCC)),John Njawa akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa Waandishi aaliyeuliza swali kuhusiana na utafiti huo walioufanya,mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar.Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano,Mary Shao Msuya.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano,Mary Shao Msuya pamoja na Mjumbe wa Baraza na Kamati ya Elimu Uhamisishaji -Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC),Nyanda Shuji (kushoto),wakionesha vitabu vyenye utafiti uliofanywa na Baraza hilo kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano,wakishirikiana na chuo cha Mipango cha Dodoma.

 Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano,Mary Msuya alisema kuwa utafiti huo umefanywa ikiwa ni moja ya mipango ya baraza hilo kwa mwaka 2016/2017.

Katika utafiti huo,Mary alisema kuwa utafiti huo ulifanyika katika wilaya tano,ambazo ni Manispaa ya Dodoma (Mjini),Chamwino (vijijini),Mvomero (vijijini),Temeke Manispaa (mjini),na Kaskazini A Unguja,Zanzibar (vijijini),alisema na kuongeza kuwa watu walioshirikishwa kwenye huduma hizo za mawasiliano ni 697,umri kuanzia miaka 15,huku asilimia 50.5 wakiwa wanafunzi wa elimu ya shule ya msingi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano,Mary Shao Msuya akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar kuhusiana na utafiti walioufanya kwa Watumiaji wa huduma za mawasiliano hivi karibuni wakishirikiana na Chuo cha Mipango cha Dododoma.

RAZA AMWAGA ZAWADI MICHEZO YA MASKULI MIKOA

$
0
0
Na Salum Vuai, MAELEZO

MKURUGENZI wa kampuni ya usafiri wa anga na huduma za viwanja vya ndege Zanzibar (ZAT) Mohammedraza Hassanali, ametoa wito kwa kampuni na taasisi mbalimbali kuunga mkono juhudi za serikali kuimarisha michezo maskulini.

Akizungungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vitu mbalimbali kwa ajili ya zawadi za washindi kwenye mashindano ya mpira wa miguu mikoa ya Unguja na Pemba iliyofanyika nyumbani kwake Kibweni, Raza alisema ni wajibu wa kila Mzanzibari kusaidia sekta ya michezo.

Alifahamisha kuwa, iwapo wafanyabiashara wa Zanzibar wataunganisha nguvu kwa lengo la kuinua michezo kuanzia ngazi ya skuli ambako ndiko kwenye msingi wa vipaji vizuri, nchi hii itafika mbali kimichezo na kulitangaza vyema jina la Zanzibar. 

“Hii ninchi yetu sote, tuna wajibu kusaidia juhudi za serikali, na nimpongeze Mhe. Rais kwa kuteua Mkurugenzi makini na mwenye jitihada kuongoza Idara ya Michezo na Utamaduni,” alieleza Raza.
Mkurugenzi Idara ya Michezo na Utamaduni katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Hassan Khairalla Tawakal, akimtambulisha Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wa wizara hiyo Omar Ali Bhai kwa Mwenyekiti wa kampuni ya ZAT Mhe. Mohammedraza Hassanali.
Mwenyekiti wa ZAT ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mhe. Mohammedraza Hassanali akimkabidhi kalkuleta Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Omar Ali Bhai kwa ajili ya washindi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa skuli za mikoa yote ya Unguja na Pemba inayotarajiwa kuanza Septemba 12, 2017 katika uwanja wa Amaan Mjni Unguja. 
Mkurugenzi Idara ya Michezo na Utamaduni Hassan Khairalla Tawakal akitoa shukurani kwa Mhe. Raza kwa msaada alioutoa kuwazawadia washindi wa michuano ya mpira wa miguu kwa skuli za mikoa ya Zanzibar itakayofanyika mwezi ujao mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.


DKT. PALLANGYO AONGOZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI ZIARA KATIKA MIRADI YA GESI LINDI

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ameongoza Kamati y Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika maeneo mbalimbali yenye miradi ya gesi katika mkoa wa Lindi lengo likiwa ni kuona utekelezaji wa miradi hiyo. 

Kati ya maeneo waliyotembelea ni pamoja na Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia cha Somangafungu, Makutano ya Bomba la Gesi Asilia (Somangafungu) mkoani Lindi pamoja na eneo linalotarajiwa kujengwa Mitambo ya Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) lililoko katika Manispaa ya Lindi.
Msimamizi wa Uzalishaji na Ujenzi katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Said Ngongoki akielezea jinsi uzalishaji unavyofanyika kiwandani hapo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti mara walipofanya ziara kiwandani hapo
Meneja Rasilimaliwatu kutoka katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Msafiri Figa ( wa kwanza kulia) akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika eneo la uzalishaji la kiwanda hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mbele kulia) akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye ziara katika eneo la Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.
Meneja Rasilimaliwatu kutoka katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Msafiri Figa (kushoto) akielezea jinsi udongo wa aina mbalimbali unavyochanganywa katika hatua za awali za maandalizi ya utengenezaji wa vigae (tiles) kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.
Sehemu ya Kituo cha Kupokea Gesi kutoka Songosongo na Madimba kilichopo Somangafungu mkoani Lindi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAHUJAJI WA TANZANIA WAANZA KUWASILI SAUDI ARABIA

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, Riyadh, Saudi Arabia.
Mahujaji kutoka Tanzania wameanza kuwasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza nguzo ya tano ya dini ya kiislamu ya kuhiji Makkah inayofanywa na watu mbalimbali duniani, wakiwamo Waislamu kutoka Tanzania.
Baadhi ya mahujaji wakionekana Uwanja wa Ndege baada ya kuwasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya swala ya Hija.
Mahujaji kutoka Tanzania wakiwa wamewasili nchini Saudi Arabia.
Baadhi ya Waislamu wanaoendelea kuwasili nchini hapa wakionekana pichani.
Ibada ya Hijja mwaka huu inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti hadi mwanzoni mwa mwezi Septemba, huku jumla ya mahujaji 977 kutoka Tanzania wameshawasili katika miji ya Madina na Jeddah. Mahujaji hao waliwasili katika viwanja vya ndege vya Madina na Jeddah na kupokelewa na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania.

Tanzania kwa mwaka huu inataraijiwa kupeleka mahujaji wapatao 2,700. Indonesia ndiyo nchi inayoongoza kwa kupeleka mahujaji wengi mwaka huu inatarajiwa kuwa na mahujaji wapatao 168,000. Mwaka huu Saudi Arabia inatarajiwa kupokea mahujaji zaidi ya 2,000,000 kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni.

KHERI YA SIKU YA KUZALIWA MDAU MC BARAKA

$
0
0
Leo Aug 23 ni siku ya kuzaliwa kwake Blogger Mc Baraka #Bukobawadau napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mola kwa kuendelea kunijalia mpaka kufika hapa nilipo.

Shukrani kwa Wazazi/Walezi kwa yote.Nathamini na kukumbuka mengi sana hasa Maneno yenu/Wosia,Upendo ,Ukarimu na Faraja zenu ...Sina lakusema zaidi ya Asanteni na nawaombea kila jema,Inshallam Mwenyezi Mungu azidi kuwajalia afya njema
Shukrani za dhati kwa Ndugu,Jamaa,Marafiki, kwani kwenye Safari ya Maisha yangu nimekutana Ndugu wengi ambao si wakuzaliwa nao kutoka Tumbo Moja /Ukoo mmoja,Lakini kwangu nawathamini sana natambua sana uwepo wenu ,Ni vigumu kutaja kila mmoja lakini wenyewe mnajijua kwa pamoja nasema Nawapenda sanaaa.!Na namshukuru Mungu kwa kunipa watu...!!

Tigo yakabidhi kisima cha maji kwa Wananchi wa Kijiji cha Usongelani wilayani Urambo, Tabora

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry akipampu maji katika kisima cha maji kilichotolewa Msaada na Kampuni ya simu za Mkononi nchini Tigo katika Kijiji cha Usongelani wilayani Urambo mkoani Tabora,Kisima hicho kimegharimu zaidi ya shilingi milioni 18. 
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry akifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi kisima cha maji kilichotolewa Msaada na Kampuni ya simu za Mkononi nchini Tigo katika Kijiji cha Usongelani wilayani Urambo mkoani Tabora. Kisima hicho kimegharimu zaidi ya shilingi milioni 18.
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry akimtwisha ndoo ya maji mmoja kati ya wananchi wa kijiji cha Usongelani ikiwa ni ishara ya kuzindua kisima hicho kilichotolewa msaada na kampuni ya Tigo ambapo kitahudumia wakaazi wa Kijiji cha usongelani na maeneo jirani ikiwa ni hatua muhimu kwa kampuni ya Tigo kurejesha kiasi cha faida kwa wananchi. 

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry (wa pili kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Tigo pamoja na watendaji wa Mkoa huo, baada ya uzinduzi wa kisima kilichotolewa msaada na Tigo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi kisima hicho kwa wakaazi wa kijiji cha Usongelani kilichogharimu zaidi ya shilingi milioni 18.

DKT. PHILIP MPANGO ATEMBELEA KIWANDA CHA KUUNGANISHA MATREKTA YA URSUS-KIBAHA

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (katikati) akiwasili katika kiwanda cha kuunganisha Matrekta ya URSUS-TAMCO, kilichoko Kibaha mkoani Pwani kuangalia kazi ya uunganishaji matrekta zaidi ya 200 pamoja na kusikiliza changamoto zinazoukabili mradi huo.

Na. Benny Mwaipaja-Kibaha

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametembelea mradi wa kuunganisha matrekta ya Ursus, uliopo Kibaha mkoani Pwani na kusisitiza kuwa Serikali imedhamiria kuendeleza kilimo nchini ili kukuza sekta ya viwanda.

Tayari Matrekta 204 yenye uwezo wa HorsePower 50 yamekwisha unganishwa yakisubiri kuuzwa kwa watumiaji hatua ambayo Dkt. Mpango amesema itaongeza tija katika kilimo na kukuza ajira hususan kwa kundi kubwa la vijana.

Ameahidi pia kuwa Serikali itayafanyiakazi haraka maombi ya Shirika la Maendeleo la Taifa NDC la kutaka kupata kibali cha kuajiri zaidi ya wafanyakazi 90 watakaohusika na mradi huo pamoja na kutoa shehena ya Matrekta 267 yaliyokwama katika Bandari ya Dar es Salaam ili yaweze kuuzwa kwa wananchi kuendeleza kilimo.

 Kwa upande wake, Meneja wa Mradi huo kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa-NDC, Mhandisi Adam Mbura, amesema mradi huo utahusisha pia uanzishwaji wa vituo vinane katika kanda mbalimbali kwa ajili kuuza matrekta, zana na vifaa vingine pamoja na  kutoa huduma kwa wateja.

Amesema kuwa kukwamuliwa kwa makontena 64 yaliyokwama bandarini yakiwa na matrekta hayo 267 pamoja na vipuri vya kuunganisha Matrekta hayo pamoja na baadhi yaliyopo katika eneo la Mradi la TAMCO, Kibaha mkoani Pwani, kutawezesha kukamilisha haraka kwa kazi hiyo.

Baadhi ya vijana wanaofanyakazi katika mradi huo wamesema kuwa wamenufaika na ujuzi wanaoupata kutoka kwa wataalamu wa ufundi kutoka nchini Poland na kuahidi kuuendeleza ujuzi huo kwa vijana wenzao ili mradi huo uweze kuwa na manfaa kwa kutatua changamoto mbalimbali za kiufunsi zitakazokuwa zikiwakabili wakulima

Mradi wa kuunganisha Matrekta ya URSUS-TAMCO, Kibaha Mkoani Pwani unafadhiliwa na Serikali ya Poland ambapo kiwanda kikubwa cha kuunganisha matrekta kinatarajiwa kujengwa katika eneo hilo na yatauzwa kwa gharama nafuu, kati ya shilingi milioni 38 hadi milioni 42 kulingana na ukubwa na uwezo wa trekta.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango akiwasha moja ya matrekta yaliyounganishwa katika Mradi wa Kuunganisa Matrekta ya URSUS-TAMCO, uliopo katika eneo la Kibaha mkoani Pwani, alipotembelea mradi huo.
Meneja Mradi wa Kuunganisha Matrekta ya URSUS, Kibaha mkoani Pwani, Mhandisi Adam Mbura, akimweleza Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, moja ya majembe yaliyounganishwa kupitia mradi huo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

SERIKALI KUONDOA KABISA MFUMO WA ZAMANI WA MALIPO YA KODI YA ARDHI NCHI NZIMA

$
0
0
Maafisa kutoka Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa wakijifunza jinsi ya kutumia Mfumo wa GePG katika malipo ya Kodi ya aedhi.

Na. Hassan Mabuye
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishirikiana na Wizara ya Fedha, imesambaza maafisa wake katika halmashauri 169 kote nchini.

Maafisa hawa wanaotoa mafunzo katika vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya ardhi na tozo nyingine kwa kutumia simu ya mkononi ili kuondoa kabisa mfumo wa zamani wa malipo.

Zaidi ya maafisa 170 kutoka makao makuu ya Wizara ya Ardhi, Wizara ya Fedha na kutoka kanda nane za ardhi wameanza kutoa elimu hiyo katika halmashauri na vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya ardhi ili kurahisisha ulipaji kodi ya ardhi kwa wananchi kwa kutumia simu zao na kuondoa usumbufu.

Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi ni mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi ambao utamrahisishia mwananchi kulipia popote walipo kwa kutumia simu zao kwa urahisi zaidi.
Afisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bwana Haruna Kiyungi akitoa mafunzo kwa maafisa Ardhi Manispaa ya Nyamagana jinsi ya kutumia Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi/kielektroniki.

Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kupatiwa hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Ili kujua unadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi kwa kutumia simu ya mkononi bonyeza *152*00# au kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi yaani sms halafu unatuma kwenda namba 15200 na baada hapo unaweza kulipia kwa njia ya Mpesa, Tigo Pesa au kulipia tawi lolote la benki ya NMB na CRDB.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo huu wa kielektroniki wa GePG katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini na kuondoa kabisa mfumo wa zamani.

Mfumo huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Mmiliki wa kipande cha ardhi ataweza kujua anadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.
Maafisa Ardhi kutoka Manispaa ya Nyamagana, Mwanza wakifuatilia kwa makini jinsi ya kutumia Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi/kielektroniki.

Kwa majaribio ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na baada ya mafanikio makubwa kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa mikoani.

Kwa zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile upekuzi katika daftari la msajili (official search), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.

Kwa sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi nchini.

USAILI KWA WALIOOMBA KAZI MFUKO WA PPF KUFANYIWA AGOSTI 28


DKT. KALEMANI AITAKA TANESCO KUUNGANISHA NGUVU KUKAMILISHA MIRADI YA UMEME YA KURASINI NA KIMBIJI

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani,(pichani anayeongea), amelitaka Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kuunganisha nguvu ili kuhakikisha wanakamilisha mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusamabaza umeme kinachotarajiwa kujengwa huko Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kalemani ametoa maelekezo hayo leo Agosti 22, 2017, wakati alipofanya ziara kukagua miradi ya umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini, Kigamboni na eneo panapotarajiwa kujengwa kituo kingine cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.

“Hakikisheni mradi wa uejenzi wa kituo hiki cha Kimbiji unakamilika ifikapo Machi 30, mwakani,(2018), na kuwaondolea adha ya upatikanaji wa umeme wananchi wa Kigamboni, chukueni mafundi waliokamilisha kazi ya kujenga kituo cha umeme kule Mtwara waje hapa, muwaache wale wanaojenga transition (njia ya kusafirisha umeme) wajenge, lakini wale mafundi wengine waleteni hapa ili mradi huu ukamilike.” Alifafanua.
 


Akiwa kwenye kituo cha kupoza na kusamabza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam, Dkt. Kalemani aliipongeza TANESCO kwa juhudi kubwa walizofanya kwa hatua ujenzi waliyofikia ambapo sasa wameanza kufunga mashine kubwa. Kituo cha Kurasini ndicho kinachotegemewa sana na watu wa Mbagala, Kurasini na Kigamboni.

Ongezeko la haraka la wakazi kwenye maeneo ya Mbagala, na Kigamboni kumepelekea uhitaji mkubwa wa umeme ambapo umeme unaopatikana kwa sasa umekuwa haukidhi mahitaji ya wakazi wa maeneo hayo.

“Naomba niwaambie, mradi huu umechelewa sana, hivyo basi ongezeni kasi ili ifikapo Agosti 30, mwaka huu, mradi ukamilike nataka watu wa Mbagala, watu wa Kurasini, na watu wa Kigamboni wanaondokana na kero hii ya umeme, na mimi nitawaambia washeshimiwa wabunge wa Kigamboni Mheshimiwa Ndungulile (Dkt. Faustin Ndungulile) na Mheshimiwa Mangungu (Murtaza Magungu) Mbunge wa Mbagala kuhusu habari hii ili wawaambie wananchi wa maeneo haya wawe wavumilivu kwani mradi huu sasa utakamilika.” Alisema.



Dkt. Kalemani pia aliwaagiza viongozi wa TANESCO, kuhakikisha wanakusanya nguvu kwa maana ya vifaa kutoka ofisi zote za TANESCO mkoa wa Dar es Salaam, ili kuhakikisha wananchi wote wa Kigamboni wanaofikia 350 waliolipia ada za kuunganishiwa umeme wawe wamepelekewe umeme ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Agosti.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, aliwaambia waandishi wa habari kuwa maelekezo ya Mheshimiwa Naibu waziri yatafanyiwa kazi kwa haraka ili kuhakikisha kero hiyo inaondoka.
Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James,(kulia), akimpatia maelezo Naibu waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme Kurasin jijini Dar es Salaam. 
Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James,(kulia), akimpatia maelezo Naibu waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme Kurasin jijini Dar es Salaam.


SERIKALI KUANZA KUTOA LESENI MPYA KWA MAGAZETI NA MAJARIDA NCHINI

$
0
0

SERIKALI imesema inaanza kutoa leseni mpya za machapisho mbalimbali ikiwemo magazeti na majarida yote nchini ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kifungu cha 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 unaokwenda pamoja na Kanuni ya 7 ya Kanuni za Sheria ya Huduma za Habari za mwaka 2017 zilizochapishwa kwa mujibu wa tangazo la Serikali na 18 la Februari 3, 2017.

Akizungumza katika Mkutano na Wanaandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema kuwa utoaji huo wa leseni kwa machapisho yote umeanza rasmi leo Agosti 23, 2017 na utafikia tamati Octoba 15, 2017 na magazeti yote yahakikishe yanakamilisha taratibu ya kupatia leseni mpya kwa kipindi hicho, na baada ya muda huo hawataruhusiwa kuyachapisha kwani watakuwa wanatenda kosa kisheria.



Dkt. Abbas amesema, kwa mujibu wa sheria, utaratibu huu wa sasa unafuta mfumo wa awali wa utoaji wa Hati za Usajili wa magazeti na majarida uliokuwa ukitumika kwa mujibu awali kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.


Fomu za maombi, akaunti ya kulipia pamoja na orodha ya nyaraka zinazohitajika kwa ajili ya usajili huo, vinapatikana kuanzia saa katika ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO za jijini Dar es salaam na Dodoma au katika sehemu ya "Huduma Zetu" katika tovuti ya Idara hiyo BOFYA HAPA.
Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas akizungumza katika Mkutano na Wanaandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo.

JAPAN YAISAIDIA TANZANIA SHILINGI TRILIONI 74 KUTEKELEZA MIRADI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITANO

$
0
0
Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan –JICA, Bw. Shinichi Kitaoka (kushoto), akielezea namna Shirika lake lilivyojipanga kuendeleza ushirikiano na Tanzania alipokutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (wa kwanza kulia), Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango. Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), akisikiliza kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan –JICA, Bw. Shinichi Kitaoka, (hawapo pichani), walipokutana Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango. Dkt. Dkt. Khatibu Kazungu (kulia), na James Andindilile (kutoka Wizara ya Nishati na Madini) wakisikiliza kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan –JICA, Bw. Shinichi Kitaoka, (hawapo pichani), walipokutana Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna wa Idara ya Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo Bi. Susana Mkapa, wakiangalia moja ya nyaraka zilizowekwa mezani wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan-JICA, Bw. Shinichi Kitaoka, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (BU), Prof. Adolf Mkenda (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt, Khatibu Kazungu, wakisikiliza kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan-JICA, Bw. Shinichi Kitaoka, Jijini Dar es Salaam.

NYAMLANI, MGOYI WATEULIWA TFF

$
0
0
 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia amewateua Makamu wa Rais wa zamani wa TFF, Athuman Nyamlani na Ahmed Mgoyi kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF. Rais Karia ameteua kwa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo katika Katiba ya TFF ikiwa ni wiki moja baada ya kupatikana kwa viongozi wa shirikisho katika uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 12, mwaka huu.

Rais Karia aliwatambulisha viongozi hao kwenye Kikao cha Kamati ya Utendaji iliyofanyika Jumanne Agosti 22, mwaka huu jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho pia Rais Karia alitumia fursa hiyo kutangaza viongozi wa kamati mbalimbali za TFF zikiwamo za kinidhamu na kisheria.

Kamati ya Nidhamu: Mwenyekiti Tarimba Abbas, Makamu Mwenyekiti, Peter Hella wakati wajumbe ni Boniface Lyamwike, Dk. Bill Haonga na Kassim Dau.

Kamati ya Rufani za Nidhamu: Mwenyekiti ni Wakili Rahim Zuber Shaban; Makamu Mwenyekiti, Stella Mwakingwe wakati Wajumbe ni Abbas Mtemvu, Amani Mulika na Siza Chenja.

Kamati ya Maadili: Mwenyekiti ni Wakili Hamidu Mbwezeleni, Makamu Mwenyekiti ni Wakili Steven Zangira wakati Wajumbe ni Glorious Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhressa.


Kamati ya Rufaa ya Maadili: Mwenyekiti ni Wakili Ebenezer Mshana; Makamu Mwenyekiti ni DCP. Mohammed Mpinga na wajumbe  ni Wakili Benjamin Karume, George Mayawa na ASP. Benedict Nyagabona.


Kamati ya Uchaguzi: Mwenyekiti ni Revocatus Kuuli; Makamu Mwenyekiti ni Wakili Mohammed Mchengerwa; Wakili Edwin Mgendera; Wakili Kiomoni Kibamba na Wakili Thadeus Karua.

Kamati ya Rufani ya Uchaguzi: Mwenyekiti ni Kenneth Mwenda; Makamu Mwenyekiti ni Jabir Shekimweri na Wajumbe ni Wakili Rashid Sadalla, Irene Kadushi na Mohammed Gombati.

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji: Mwenyekiti ni Elias Mwanjala; Makamu Mwenyekiti ni Wakili Malangwe Mchungahela wakati Wajumbe ni Zakaria Hanspope, Robert Selasela, Goodluck Moshi, Mhandisi Issa Batenga na Hamis Semka.

Kamati ya Fedha na Mipango: Mwenyekiti ni Michael Wambura; Makamu Mwenyekiti ni Francis Ndulane na Wajumbe ni Almas Kasongo, Pascal Kihanga, Maximillian Tabonwa, Paul Bilabaye na Farid Abeid.

Kamati ya Mashindano: Mwenyekiti ni Ahmed Mgoyi; Makamu Mwenyekiti ni James Mhagama wakati Wajumbe ni Kenneth Pesambili, Shafii Dauda, Fortunatus Kalewa na Mhandisi Andrew Makota.

BOFYA HAPA KUONA KAMATI ZINGINE

KIDAO WILFRED KAIMU KATIBU MKUU TFF

$
0
0
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepitisha jina la Kidao Wilfred kuwa Kaimu Katibu Mkuu.

Kidao ambaye ni mchezaji wa zamani wa Taifa Stars ambaye pia Mwenyekiti wa Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA), ameteuliwa rasmi jana Agosti 22, 2017 na Kamati ya Utendaji ya TFF. Wasifu wa Kidao utawajia punde.
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>