Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

Prof. Elisante awataka Maafisa Utamaduni Mkoani Pwani kuzingatia na kuheshimu muda katika kutekeleza majukumu yao

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ( kulia) akipata maelekezo kutoka kwa Mkuu wa kituo cha Makumbusho cha Caravan Serai Bibi. Reinfrida Kapela (kushoto) namna ambavyo wanawake wa Mji wa Bagamoyo walivyokuwa na utamaduni wa kutengeneza urembo wa liwa kwa kutumia jiwe wakati wa ziara yake ya kikazi jana Mjini hapo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ( kushoto) akieleza jambo wakati wa kikao na Maafisa Utamaduni na watendaji wa Mkoa wa Pwani katika ziara yake ya kikazi jana mkoani hapo lengo ikiwa ni kuwahamasisha maafisa hao kufanya kazi kwa kuzingatia utamaduni wa kutunza na kuheshimu muda ili kuleta matokeo chanya kwa jamii kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo.
Baadhi ya wajumbe wa kikao waliohudhuria kikao kazi wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel Jana Mkoani Pwani.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Mkuu wa kituo cha Makumbusho cha Caravan Serai Bibi. Reinfrida Kapela (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi jana Mjini Bagamoyo, katikati ni Katibu Tawala Wilaya ya Bagamoyo Bibi. Erica Yegela.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mkoa wa Pwani wakati wa ziara yake ya kikazi jana mkoani hapo.

DK.KIKWETE SIJAANZA KILIMO/UFUGAJI BAADA YA KUSTAAFU WATAKAOSUBIRI KUANZA UZEENI WAMECHELEWA

0
0
 Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete,akionyesha Kilimo cha mahindi ya njano kwa ajili ya kuongeza rutuba kwa ng'ombe .

 Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete,akionyesha eneo analohifadhi majani ya malisho ng'ombe .



RAIS Mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete ,amesema ameanza kufanya kilimo na ufugaji tangu mwaka 1988/1989 hivyo anaetegemea kufanya shughuli hizo baada ya ustaafu amechelea .

Aidha ameeleza matarajio yake kwa sasa ni kuongeza mifugo ya ng'ombe majike wa maziwa 500 watakaoweza kutoa maziwa lita 2,000 hadi 4,000 kwa siku .

Katika hatua nyingine dk.Kikwete amesema endapo wafugaji watazingati ufugaji wa kisasa kwa kuwa na maji ya kutosha ,malisho ,kinga ya chanjo na kuogeshwa ni lazima watanufaika kwa kupata soko la uhakika hasa maziwa.



MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI NCHINI

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Kaimu Balozi wa Marekani nchini Mhe.Inmi Patterson aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam na kujitambulisha na kufanya mazungumzo kwa mara ya kwanza tangu alipowasili nchini.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Mhe. Inmi Patterson (Katikati) mara baada ya kujitambulisha ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. 

MADIWANI ACHENI KUINGILIA KAZI ZA WATAALAM " DC MBINGA"

0
0
Mkuu wa wilaya ya Mbinga Cosmas Nshenye awajia juu madiwani wanaoingilia kazi za wataalam na kusababisha kurudisha nyuma maendeleo ya wilaya hiyo.

Warsha kuunganisha Mipango ya APRM na Mipango ya Serikali kufanyika Zanzibar

0
0
Tunapenda kuwafahamisha kuwa warsha ya APRM itafanyika tarehe 24 – 25 Agosti 2017, kwenye hoteli ya “Golden Tulip Boutique”, Zanzibar. Warsha hiyo itahudhuriwa na Wakurugenzi na maafisa waandamizi toka idara za Mipango na Sera za Wizara, Idara na Wakala wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wapatao 50. Na pia itakuwa na watoa mada toka nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Zanzibar yenyewe, Afrika ya Kusini, Ghana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa.

Warsha hiyo inalenga kujenga uwezo wa Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), katika kuoanisha (kuunganisha) Mpango Kazi wa APRM na mipango ya Maendeleo ya Zanzibar, hasa Mpango wa Kupunguza Umaskini na Kuleta Maendeleo Na. III. 

Na itajadili masuala yafuatayo: Namna ya kuunganisha Mipango ya Maendeleo ya nchi, Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika, Malengo Endelevu ya Milenia pamoja na Mpango Kazi wa APRM; Uzoefu wa nchi nyingine za Kiafrika katika kuunganisha Mipango yao ya Maendeleo na Mpango Kazi wa APRM na Mkakati wa Tathmini na Ufuatiliaji.




Warsha hiyo inagharamiwa kwa pamoja baina ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Uchumi Barani Afrika pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Mwishoni inatarajiwa kuwa washiriki wataweza kuunganisha Mpango Kazi wa APRM na kuonda changamoto za Utawala Bora pamoja na Mipango ya Maendeleo ya Zanzibar kwa lengo la kutumia vizuri rasilimali zilizopo ili kujenga uhusiano kati ya Mipango hiyo pamoja na kukuza uwezo wa kitaasisi.

Hatua hiyo ni muhimu sana kwani itasaidia kwa kiasi kikubwa kukamilisha Taarifa ya kuondoa changamoto za Utawala Bora zilizobainishwa kwenye Ripoti ya Nchi. Na hatimaye nchi yetu itaweza kuwasilisha Ripoti ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa kuondoa changamoto hizo kwenye kikao cha Wakuu wa nchi wanaoshiriki mchakato wa APRM.

Inatarajiwa kuwa, kwa kutatua changamoto za utawala bora nchi itaweza kuendelea kuwa na amani na utulivu, kukuza uchumi, kuwa na maendeleo endelevu pamoja na kuharakisha Muungano wa Kikanda, na hatimaye kuwaondolea wananchi umaskini.

Tanzania ni mojawapo kati ya nchi 36 za Afrika zinazoshiriki mchakato wa APRM, nayo imeshawasilisha Ripoti yake ya kwanza kwa Wakuu Wenza wanaoshiriki mchakato huu mwaka 2013. Hivi sasa ipo katika hatua ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa kuondoa changamoto zilizobainishwa kwenye Ripoti ya Utawala Bora.

Imetolewa na APRM Tanzania
22 Agosti 2017 

ZAMBI APIGIA DEBE UWEZESHAJI WA KILIMO CHA UFUTA NA MIHOGO.

0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akitambulisha msafara wake kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi (hayupo pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi. Kushoto ni Meneja Mikopo, Bw. Samuel Mshote na  Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (katikati).
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi.
Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Na Mwandishi wetu, Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kukopesha wakulima wa mazao ya ufuta na mihogo ili waweze kulima kilimo cha kisasa na cha kibiashara hasa kwa wakulima wadogo wadogo wa mkoani humo.
 
Bw. Zambi alitoa wito huo wakati wa mkutano wa Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Bw. Zambi alisema kuwa mkoa wa Lindi ni mkoa uliojaaliwa katika kuzalisha mazao ya ufuta na mihogo lakini changamoto kubwa ni mtaji wa kulima kibiashara ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

“Wakulima wa mkoa wa Lindi wapo tayari kushiriki katika kuleta mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara lakini kwa sasa suala la mtaji wa kilimo cha kibiashara ni changamoto kubwa,” alisema Bw. Zambi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa Benki ya kilimo ipo tayari kutoa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo waliokuwa kwenye vikundi ili waweze kukopeshwa.

RIPOTI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI YATHIBITISHA MANJI ANATUMIA DAWA ZA KULEVYA.

0
0

 Mfanyabiashara Maarufu nchini, Yusuph Manji akiteta jambo na Wakili wake, Hudson Ndusyepo wakati wakiwa ndani ya mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam leo kabla ya kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

SHAHIDI wa Kwanza katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara maarufu, Yusuph Manji amedai mahakani kuwa uchunguzi Wa mkemia Mkuu umeonyesha Manji anatumia dawa za kulevya.

Shahidi huyo wa kwanza wa upande wa jamuhuri, Ramadhani Kingai ambaye no Naibu Mkuu wa upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Akiongozwa na Wakili Wa Jamuhuri, Timon Vitalis, Kingai amedai, February 9 mwaka huu aliambiwa kufanya uchunguzi wa suala lililoripotiwa na Mkuu wa mkoa Wa Dar es Salaam Paul Makonda  juu ya watuhumiwa wa dawa za kulevya wakiwemo Josephat Gwajima na Yusuph Manji. 

Amesema alimuelekeza Dutektivu Koplo Sospter kuwapeleka Manji ambaye alifika katika kituo cha polisi mwenyewe na Gwajima kupelekwa kwa Mkemia Mkuu kupimwa juu ya tuhuma hizo za dawa za kulevya ambapo baadae walipata taarifa kuwa Manji anatumia dawa za kulevya.
Alidai baada ya ripoti hiyo, alielekeza Manji afunguliwe jalada la kutumia dawa za kulevya kisha kwa DPP ambaye alimfungulia mashtaka

Hata hivyo shahidi Kingai alipoulizwa nani alielekeza kuwa dawa anazodaiwa kutumia Manji ni Heroine alidai, yeye alifanya upelelezi tu ila anayeandaa mashtaka in DPP.

Naye shahidi wa pili Koplo Sospeter amedai alipokea maelekezo juu ya mtuhumiwa Manji ambapo moja ya maelekezo hayo yalikuwa yakimtaka kumpeleka Manji  kwa mkemia Mkuu kwa ajili ya kupima sampuli  ya mkojo ambapo baada ya kufuata taratibu za ofisi ya mkemia na kupata namba ya maabara alimpeleka Manji msalani ambapo aliweka mkojo kwenye chupa maalumu kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
Amedai Februari 10, mwaka huu  majibu yalitoka na akakuta yanasema mkojo wake una chembechembe za dawa za kulevya.
Kesi hiyo itaendelea kesho.
Mfanyabiashara Maarufu nchini, Yusuph Manji akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akisubiri  kusomewa kesi ya Madawa ya Kulevya inayomkabiri.
 Mfanyabiashara Maarufu nchini, Yusuph Manji akiwa ndani ya ukumbi wa mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu jijini Dar es Salaam akisubiri kusomewa mashtaka yanayo mkabiri.
Mazungumzo yakiendelea.Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

IGP SIRRO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MUFTI WA TANZANIA

0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kulia) akizungumza na Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zubeir (kushoto), alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya BAKWATA jijini Dar es salaam jana. IGP Sirro, alisema Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na viongozi wa kidini katika kuimarisha amani nchini. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kulia), akifurahia jambo na Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zubeir (kushoto), alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya BAKWATA jijini Dar es salaam jana. IGP Sirro, alisema Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na viongozi wa kidini katika kuimarisha amani nchini.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (wanne kulia waliokaa), na Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zubeir, wakiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislamu wakati alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya BAKWATA jijini Dar es salaam jana. IGP Sirro, alisema Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na viongozi wa kidini katika kuimarisha amani nchini. 

ZAMBI APIGIA DEBE UWEZESHAJI WA KILIMO CHA UFUTA NA MIHOGO

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kukopesha wakulima wa mazao ya ufuta na mihogo ili waweze kulima kilimo cha kisasa na cha kibiashara hasa kwa wakulima wadogo wadogo wa mkoani humo.

Bw. Zambi alitoa wito huo wakati wa mkutano wa Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Bw. Zambi alisema kuwa mkoa wa Lindi ni mkoa uliojaaliwa katika kuzalisha mazao ya ufuta na mihogo lakini changamoto kubwa ni mtaji wa kulima kibiashara ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

“Wakulima wa mkoa wa Lindi wapo tayari kushiriki katika kuleta mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara lakini kwa sasa suala la mtaji wa kilimo cha kibiashara ni changamoto kubwa,” alisema Bw. Zambi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akitambulisha msafara wake kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi (hayupo pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi. Kushoto ni Meneja Mikopo, Bw. Samuel Mshote na  Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (katikati).
Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (aliyesimama) akiwasilisha mada juu ya fursa za mikopo zinazotolewa na Benki ya Kilimo kwa Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MWANZA: MTU MMOJA AMEUAWA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KOSA LA WIZI WA KUKU WILAYANI KWIMBA.

0
0
KWAMBA TAREHE 21/08/2017 MAJIRA YA 08:45HRS ASUBUHI KATIKA KITONGOJI CHA BUSULWA KATA YA NGULLA WILAYA YA KWIMBA MKOA WA MWANZA, LEONARD MATHIAS MIAKA 23, MKAZI WA KIJIJI CHA NGULLA, ALIUAWA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KUPIGWA FIMBO NA MAWE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KISHA BAADAE KUCHOMWA MOTO HADI KUPOTEZA MAISHA KWA KOSA LA WIZI WA KUKU WATANO MALI YA ESTER ROBERT, MKAZI WA KIJIJI CHA NGULLA, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

INASEMEKANA KUWA MAREHEMU ALIIBA KUKU WATANO NYUMBANI KWA BI ESTER ROBERT KIJIJINI NGULLA KISHA ALIKIMBILIA KIJIJI CHA JIRANI CHA MWABOMBA. INADAIWA KUWA  WANANCHI WA KIJIJI CHA MWABOMBA WALIPOMUONA MAREHEMU AKIWA NA KUKU HAO WALIPATA MASHAKA KISHA WALIMKAMATA NA BAADAE WALITOA TAARIFA KIJIJI CHA NGULLA NDIPO MWENYE KUKU BI ESTER ROBERT ALIFIKA NA KUKABIDHIWA KUKU WAKE.

INADAIWA KUWA BAADA YA MAREHEMU KUKABIDHI KUKU KWA MWENYE MALI, WANANCHI WALIMCHUKUA NA KWENDA NAE KITUO CHA POLISI LAKINI WAKIWA NJIANI WALIANZA KUMSHAMBULIA KWA KUMPIGA FIMBO NA MAWE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA BAADAE KUMCHOMA MOTO. POLISI WALIPATA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA NDIPO WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO NA TUKIO NA KUFANIKIWA KUKAMATA WATU SABA AMBAO WANADAIWA KUHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA MAUAJI HAYO.

POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO WATUHUMIWA SABA WALIOKAMATWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA KISHA IKITHIBITIKA WATUHUMIWA WALIHUSIKA KATIKA MAUAJI HAYO WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA UPELELEZI NA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WENGINE WALIOHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA MAUAJI HAYO BADO UNAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KOSA LA JINAI, BALI PINDI WANAPOMKAMATA WAHALIFU AU MHALIFU WAMPELEKE KWENYE KITUO CHA POLISI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE. PIA ANAOMBA WANANCHI WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU NA UHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.

IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

RIDHIWANI AKABIDHI ZAWADI YA MCHEZAJI BORA SPORTS EXTRA

0
0
  Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani  Kikwete, akikabidhi tunzo ya Mchezaji bora kwa kocha wa timu ya Misosi FcYenye maskani  yake Manzese.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA),Mulamu Nghambi akikabidhi zwadi kwa Refalii borawa michuano ya Ndondo Cup.
 Mpiga picha bora wa Michuano ya Ndondo Cup , Rachel Palangyo akiwa na Tunzo yake mara baadaya kukabidhiwa.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

WATEJA WA ZANTEL KUFURAHIA HUDUMA ZA SIMU NA INTANETI ZILIZOBORESHWA ZAIDI.

0
0
 Wateja wa Zantel sasa wataendelea kufurahia huduma zenye ubora wa hali ya juu kwenye upigaji wa simu na kunufaika na matumizi ya data yenye kasi. Zantel imekuwa kampuni ambayo imepiga hatua kwa kuboresha huduma yake ya mtandao na kuahidi kuendelea kuleta mabadiliko kwenye sekta ya mawasiliano ili kuendelea kubadili maisha ya mamilioni ya watu nchini Tanzania.

Ofisa Mkuu wa Masuala ya Ufundi na Teknolojia Zantel, Larry Arthur alisema, “ Tumeanza kuboresha mtandao wetu tangu Septemba ya mwaka 2016 na tulikuwa na lengo la kukamilisha kazi yetu mwezi Juni mwaka huu, lakini kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kipindi cha hivi karibuni, ukamilishaji wa kazi hii umechelewa kufanyika kwa wakati”.

Mchakato wa kuboresha mifumo yetu ya mtandao Zanzibar na Tanzania Bara kwa sasa inakaribia kukamilika na tunafurahi kuwaeleza wateja wetu kwamba tayari tumeshaanza kufurahia matunda ya ubora wa usikivu katika kupiga simu na huduma za data kupitia mtandao wa 4G wa Zantel wenye kasi zaidi.

Kuboresha mfumo wetu wa mtandao kumeimarisha mfumo wa mtandao wa Zantel na kufika maeneo mengi zaidi pia watumiaji wa intaneti wamenufaika na huduma ya haraka ya 4G inayopatikana kwa sasa.

Zantel imekamilisha awamu ya kwanza ya uboreshaji wa mtandao Kisiwani Pemba na Mkoa wa Magharibi Unguja kuweka mfumo wa mtandao wa kisasa. Baada ya kukamilisha awamu hii, inayofuata itakuwa ni kuimarisha miundombinu ya Zantel eneo la Kaskazini na Kusini mwa Unguja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Mkuu wa masuala ya Teknolojia na Ufundi Zantel, Larry Arthur (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kisiwani Zanzibar hivi karibuni kuhusu uboreshwaji wa mtandao wa Zantel baada ya Kampuni hiyo kupokea vifaa vipya kutoka Ericsson na Huawei Technologies vitakavyotumika kuboresha mtandao huo. Wengine kutoka kushoto ni William Cheng (Wei) wa Huawei Technologies, Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa (Baucha) na Mwakilishi wa Kampuni ya Ericsson, Frode Dyrdal.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Ashiriki Ujenzi wa Taifa wa Skuli ya Msingi Uzi Ngambwa

0
0
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akizungumza na wananchi wa Kisiwa cha Uzi Ngambwa wakati wa ujenzi wa madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi inayojengwa na Mbunge na Mwakilishi na nguvu Wananchi wa kijiji hicho. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akiwahutubia wananchi wa kisiwa cha Uzi Ngambwa jimbo lake wakati wa ujenzi wa Taifa wa madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa. 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhani Abdallah akizungumza na wananchi wa kisiwa cha Uzi Ngambw wakati wa ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Ngambwa. inayojengwa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo la Tunguu na Nguvu za Wananchi wa Kijiji hicho.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar akishiriki katika ujenzi huo wa Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi.

BALOZI, ADADI NA BITEKO WAKUTANA NA WAJUMBE WA CHAMA CHA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA TAWI LA CANADA.

0
0
 Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu (kulia) akizungumza pale ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Canada ambao ni Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ulipotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  leo Mjini Dodoma, ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi baina ya Mabunge hayo. Ujumbe huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Ndg. Yasmin Ratansi (wa pili kushoto), kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Ndg. Kerry Diotte na wa pili kulia, ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada Ndg. Remi Bourgault.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Mhe. Yasmin Ratansi (wa pili kushoto) akizungumza pale ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Canada ambao ni Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ulipotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  leo Mjini Dodoma, ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi baina ya Mabunge hayo, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dotto Biteko, anaefuta ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu , kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Mhe. Kerry Diotte na katikati ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada Ndg. Remi Bourgault.
Ujumbe wa Wabunge kutoka Bungela Canada ambao ni Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada walipotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Mhe.Yasmin Ratansi (watatu kushoto), Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dotto Biteko (wanne kushoto) na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (wa tatu kulia). Ujumbe ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi baina ya Mabunge hayo.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

TAASISI YA THPS YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUSAIDIA MIFUMO YA AFYA 2016-2020.

0
0
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) Dkt. Augustine Massawe akizungumza katika uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016- 2020. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020 na Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS).  Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa nne toka Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Redempta Mbatia (wa tako kutoka kushoto) pamoja na wadau wa afya wakionyesha chapisho la Mpango Mkakati wa kwanza wa kusaidia mifumo ya afya  wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) inayosaidia Wizara za afya Tanzania Bara na Zanzibar kutoa kinga ya Virusi vya Ukimwi (VVU), huduma, matibabu na msaada kwa kuimarisha mifumo ya afya imezindua mpango mkakati wa kwanza wa miaka mitano.

Akizungumza katika uzinduzi huo wa mpango mkakati uliofanyika Jijini Dar es salaam leo. Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi wa THPS, Dkt. Augustine Massawe alisema mpango mkakati wa kwanza wa taasisi hiyo ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016 mpaka 2020 umelenga kusaidia juhudi za Wizara ya afya, Serikali za mitaa, Washiriki wengine na Wadau kuhakikisha huduma bora za afya zinazoshugulikia afya ya umma ikiwemo magonjwa yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa ili kuboresha matokeo ya afya kiujumla katika jamii. 

Dkt. Massawe alisema anatarajia mpango mkakati utazingatia mawazo kati ya wadau muhimu wa THPS na kujenga uamuzi wa pamoja wenye matokeo mazuri. “tunataka kugusa maisha ya Watanzania wengi kwa kuathiri ubora wa huduma za afya na kujenga taifa huru la VVU/UKIMWI. Nina matumaini kuwa mpango mkakati uliofikiriwa utakuwa kama chombo cha usimamizi wa taasisi katika kuweka vipaumbele, kuzingatia nishati na rasilimali, kuimarisha shughuli mbalimbali na kuhakikisha wafanyakazi na wadau wengine wanafanya kazi kwa malengo.

Akizungumzia juu ya uzinduzi wa mpango mkakati, Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia alielezea malengo ya taasisi kwa miaka ijayo ni kutazamia mbali VVU/ UKIMWI na kushughulika na magonjwa mengine yenye vitisho katika jamii, kulenga katika uhamasishaji wa rasilimali na kuchunguza ushirikiano wa pamoja na sekta binafsi ili kuendelea kutoa huduma zake.

Viwanda 42 Zaidi Kuunganishwa Mfumo wa Gesi

0
0

Na Said Ameir-MAELEZO

Serikali imesema kuwa viwanda vingine 42 vitaunganishwa na mfumo wa matumizi wa matunizi ya gesi asilia katika kipindi cha miaka miwili ili kuongeza tija tofauti viwanda 37 vya sasa ambavyo tayari vinatumia gesi hiyo.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani aliiambia Kamati ya Fedha ya Bunge jana kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa changamoto zinazokwaza zoezi la kuvipatia viwanda nishati hiyo zinatatuliwa haraka.

“Tuna gesi ya kutosha futi za ujazo trilioni 57.25 ambapo hadi sasa tunatumia wastani wa futi za ujazo milioni 70 ikiwa ni kama asilimia kumi tu hivi” alieleza Waziri Kalemani.Kwa hivyo alisema azma ya Serikali ni kuona viwanda vinatumia gesi katika uzalishaji na kubanisha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na nishati hiyo katika Afrika Mashariki. 

Waziri Kalemani aliieleza kamati hiyo kuwa hivi sasa wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda lakini Serikali ipo mbioni kutekeleza mkakati wa kusambaza gesi hiyo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Katika maelezo yake kwa kamati hiyo ambayo ilitembelea kituo cha kupokelea gesi asilia huko Kinyerezi na miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia gesi hiyo ya Kinyerezi I na Kinyerezi II, Naibu Waziri huyo alidokeza kuwa Serikali ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kusindika gesi asilia ili iweze kusafirishwa nchi za nje.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Bunge Hawa Ghasia ameitaka TPDC kutayarisha mpango maalum kwa kuainisha na kutenga maeneo maalum ambayo yatawekewa miundombinu ya gesi ili uwekezaji wa viwanda uzingatie ramani hiyo.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani

NAIBU WAZIRI MPINA AKUTANA NA KAMATI YA ARDHI NA MAWASILIANO YA BARAZA LA WAWAKILISHI KUTOKA ZANZIBAR

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina akiongea wakati wa ziara ya Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar, iliyomtembelea Ofisini kwake jijini Dar Es Salaam wa kwanza kulia nia Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Hamza Hassan Juma na wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar wakimsilikiza Naibu  Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina(hayupo pichani) wakati wa ziara yao Ofisini kwa Waziri huyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina akisiliza kwa makini hoja zilizokua zikitolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Hamza Hassan Juma(kulia) wakati wa ziara hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar, iliyomtembelea Ofisini kwake jijini Dar Es Salaam

Article 8

Mashirika ya ndege, TTB wakubaliana

0
0
Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bibi Devota Mdachi na Meneja Mkazi Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines, Bwana Dahlak Teferi wakibadilishana hati za makubaliano ya kufanikisha maonyesho ya utalii ‘Swahili International Tourism Expo,’ jijini Dar es Salaam jana, maonyesho hayo yatakayofanyika Oktoba 13-15 mwaka huu.
Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya utalii Bi Devota Mdachi akizungumza katika hafla ya kutia saini ushirikiano wa kufanikisha maonyesho ya utalii ‘Swahili International Tourism Expo,’ jijini Dar es Salaam jana, maonyesho hayo yatakayofanyika Oktoba 13-15 mwaka huu, (kushoto) Mhandisi Ladislaus Matindi Mkurugenzi mtendaji Air Tanzania wapili( kulia) Bwana Dahlak Teferi Meneja wa Ethiopian Airlines, (kulia) Lima Silva Mwakilishi wa mauzo mwandamizi Shirika la ndege la Ethiopia, Ethiopian Airlines.
Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devotha Mdachi akiwa kwenye picha ya pamoja na Wadau wa Utalii mda mfupi baada ya hafla ya kutia saini ushirikiano wa kufanikisha maonyesho ya utalii ‘Swahili International Tourism Expo’ iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana’ wa tatu (kulia) Mhandisi Ladislaus Matindi Mkurugenzi Mtendaji Air Tanzania wa pili (kushoto) Dahlak Teferi Meneja wa Shirika la Ndege la Ethiopia, Ethiopian Airlines. Ends

TCAA KUNUNUA RADA NNE ZA KISASA

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) imeingia makubaliano  ya manunuzi ya rada Nne na kampuni ya Thales ya nchini Ufaransa  zenye thamani ya sh.bilioni 61.3.

Akizungumza leo na waandishi wa habari kabla ya kusaini makubaliano ya manunuzi ya rada hizo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,  Profesa  Makame Mnyaa Mbarawa amesema kuwa kampuni hiyo ifunge kwa viwango vilivyoainishwa katika mkataba na watakaosimamia mradi huo wanatakiwa kuwa na uadilifu kutokana fedha hiyo ni nyingi kutolewa na serikali.

Amesema kuwa kufungwa kwa rada hizo kutasaidia serikali kupata mapato ya sh. bilioni moja, kuongeza idadi ya ndege kutumia anga ya Tanzania pamoja na kuongeza idadi ya wataalii kutokana na anga kuwa salama.

Profesa Mbarawa amesema kuwa TCAA imetumia fedha zake pamoja na serikali kuepukana na mkopo ambapo wameweza kuokoa  sh. bilioni 10 ambazo zingetokana ulipaji mkopo katika taasisi ya fedha.Amesema kuwa TCAA wameweza kujibana hadi kufikia ununuzi wa rada hizo na kutaka taasisi zilizo chini ya wizara kutumia vyanzo mapato vyao katika miradi mbalimbali kuliko kuangalia kukopa katika taasisi fedha  benki.

Nae, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari  amesema kuwa rada hizo zitafungwa katika viwanja vya ndege vya Dar es Salaam , Kilimanjaro, Songwe -Mbeya  pamoja na Mwanza.Amesema kuwa TCAA kwa kufungwa rada hizo inakwenda kimataifa kutokana na huduma zinazotolewa na mamlaka hizo kuzingatia viwango vya kimataifa vilivyowekwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).

Aidha amesema kuwa rada hizo ni matokeo ya  serikali ya awamu ya tano katika kufikia uchumi wa kati kufikia 2025 unaoendana na pamoja na usafiri wa anga.Makamu Mwenyekiti wa Bodi wa TCAA, Profesa Longinus Rutasitara amesema kuwa TCAA imejibana katika vyanzo vyake na kuweza kununua rada hizo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza  wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya mkataba  wa ufungaji wa mitambo minne  ya Rada ya kuongozea ndege  baina ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Kampuni ya Thales  Air System  ya nchini Ufaransa. Hafla hiyo pia imeambatana na uzinduzi wa nembo ya mpya ya TCAA  leo jijini Dar es Salaam. Wengine kwenye picha ni Makamu Mwenyekiti Bodi ya TCAA, Prof. Longinus Rutasitara, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari na Meneja Masoko wa Kanda wa Kampuni ya Thales  Air System, Bwana  Abel Curr. 
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa(wapili kushoto aliyesimama), akishuhudia  utiaji wa saini ya mkataba  wa ufungaji wa mitambo minne  ya Rada ya kuongozea ndege  baina ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kupitia Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza S. Johari (Kushoto) na Meneja Masoko wa Kanda wa Kampuni ya Thales Air System ya nchini Ufaransa, Abel Curr .wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa( katikati), akishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza S. Johari (Kushoto) na Meneja Masoko wa Kanda wa Kampuni ya Thales Air System Abel Curr wakibadilishana nyaraka baada ya kutia saini ya mkataba wa ununuzi wa rada nne za kuongozea ndege. wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa(katikati)  akikata utepe kuashiria uzinduzi wa nembo mpya ya TCAA  huku akishuhudiwa na makamu  Mwenyekiti Bodi ya TCCA, Prof. Longinus Rutasitara,(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamza S. Johari.(kushoto) wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya mkataba  wa ufungaji wa mitambo minne  ya Rada ya kuongozea ndege  baina ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Kampuni ya Thales  Air System  ya nchini Ufaransa leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa(kulia)  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamza S. Johari. (Kushoto) wakishangilia mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa nembo mpya ya TCAA, wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya mkataba  wa ufungaji wa mitambo minne  ya Rada ya kuongozea ndege  baina ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Kampuni ya Thales  Air System  ya nchini Ufaransa leo jijini Dar es Salaam. 
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images