Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WAZIRI MAHIGA AMPOKEA WAZIRI WA NCHI WA UINGEREZA AMBAYE YUPO ZIARANI NCHINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza, Mhe. Stewart Rory alipofika Wizarani tarehe 22 Agosti, 2017 kwa ajili ya mazungumzo rasmi na Waziri Mahiga. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Uingereza. Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lale la Kimataifa la Maendeleo (DFID) inaisadia Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Maji, Elimu, Nishati Mbadala na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya. Mhe. Stewart yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 22 na 23 Agosti, 2017. 
Sehemu ya ujumbe ulioambatana na Mhe. Stewart. Kulia ni Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mhe. Sarah Cooke, Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID), Bi. Beth Arthy na Afisa kutoka Ubalozini. 
Sehemu ya ujumbe wa Wizara wakati wa mazungumzo kati ya Waziri Mahiga na Waziri Stewart kutoka Uingereza (hawapo pichani). Kushoto ni Bw. Salvatory Mbilinyi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Bw. Joseph Kapinga, Afisa Mambo ya Nje.
Waziri Mahiga akiagana na mgeni wake Mhe. Stewart mara baada ya kumaliza mazungumzo yao .
Picha ya pamoja
Waziri Mahiga kwa pamoja na Mhe. Stewart wakizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu lengo la ziara ya Mhe. Stewart nchini. 

PROF. ELISANTE AWATAKA MAAFISA UTAMADUNI KUTANGAZA VIVUTIO VYA KIUTAMADUNI VILIVYOPO KATIKA MIKOA YAO

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro jana wakati wa ziara yake ya kikazi ambapo aliwataka watumishi wawe na utamaduni wa kufanya kazi  kwa kushirikiana na wananchi.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo akieleza umuhimu wa filam katika kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ukumla wakati wa kikao na Maafisa Utamaduni na watendaji wa Mkoa wa Morogoro. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (Kulia) akimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Utawala na Fedha Dkt. Yonika Ngaga (kushoto) alipotembelea makaburi ya Wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini yaliyopo Mazimbu Morogoro wakati wa ziara yake ya kazi jana mkoani hapo.  
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa fundi bombo Idara ya Matengenezo Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Bw. Ally Mkopi alipotembelea makaburi ya Wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini yaliyopo Mazimbu mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kazi jana mkoani hapo.  (Picha na Lorietha Laurence –WHUSM).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI KUONDOA KABISA MFUMO WA ZAMANI WA MALIPO YA KODI YA ARDHI NCHI NZIMA

$
0
0

Na. Hassan Mabuye.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishirikiana na Wizara ya Fedha, imesambaza maafisa wake katika halmashauri 169 kote nchini.

Maafisa hawa wanaotoa mafunzo katika vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya ardhi na tozo nyingine kwa kutumia simu ya mkononi ili kuondoa kabisa mfumo wa zamani wa malipo.

Zaidi ya maafisa 170 kutoka makao makuu ya Wizara ya Ardhi, Wizara ya Fedha na kutoka kanda nane za ardhi wameanza kutoa elimu hiyo katika halmashauri na vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya ardhi ili kurahisisha ulipaji kodi ya ardhi kwa wananchi kwa kutumia simu zao na kuondoa usumbufu.

Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi ni mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi ambao utamrahisishia mwananchi kulipia popote walipo kwa kutumia simu zao kwa urahisi zaidi.

Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kupatiwa hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Ili kujua unadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi kwa kutumia simu ya mkononi bonyeza *152*00# au kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi yaani sms halafu unatuma kwenda namba 15200 na baada hapo unaweza kulipia kwa njia ya Mpesa, Tigo Pesa au kulipia tawi lolote la benki ya NMB na CRDB.
 Afisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bwana Haruna Kiyungi akieleza jinsi ya kutumia Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi/kielektroniki
 Afisa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi Bwana David Malisa (katikati) akitoa mafunzo kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi kanda ya Ziwa jinsi ya kutumia Mfumo wa GePG
 Afisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Joines Mhalila akielekeza jinsi ya kutumia simu katika kufanya malipo ya kodi ya ardhi.

  Afisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bwana Haruna Kiyungi akionesha kwa vitendo jinsi ya kutumia Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi/kielektroniki.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Uamuzi kama Manji ana kesi ya kujibu au la katika kesi ya dawa za kulevya kujulikana ijumaa.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii. 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, siku ya ijumaa itatoa maamuzi dhidi ya kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara maarufu nchini Yusuph Manji kama ana kesi ya kujibu ama la.Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema hayo leo mapema baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi dhidi ya kesi hiyo kwa kuita mashahidi watatu.

Kabla ya uamuzi huo kutolewa, shahidi wa tatu na wa mwisho, Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Domician Dominic (49) ameshindwa kuithibitishia mahakama hiyo kama sampuli ya mkojo alioufanyia uchunguzi ni wa Mfanyabiashara Yusufu Manji au Polisi.

Akijubu swali  wakili wa utetezi, Hudson Ndusyepo la kumtaka, kuieleza mahakama kama anatambua mkojo huo ni wa nani alisema, hatambui kama mkojo ni wa Manji au Polisi kwa kuwa hakuwepo msalani wakati sampuli hiyo inatolewa badala yake yeye alitoa kontena na kumpatia Polisi ili Manji aweke sampuli hiyo ambapo baada ya kuipokea  Kutoka kqa Koplo Sospeter 
Alisajili kontena hilo kwa kuipa namba ya maabara 367/2017.

Ameongeza katika uchunguzi wa awali aliofanya aligundua mkojo huo ulikuwa na kemikali inayoitwa benzodiazepines.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Timon Vitalis, Shahidi huyo amedai mahakamani hapo kuwa kemikali zilizokutwa kwenye mkojo Wa Manji ni dawa ambao hutumika kwa ajili ya kupunguza maumivu makali kwa maelekezo ya daktari na pia kumsaidia mgonjwa kupata usingizi.

Ameongeza, katika hatua ya pili ya uchunguzi aligundua dawa inayoitwa Morphine yenye viashiria vya heroine ambayo wakati mwingine hutumika wakati wa upasuaji.

WAJUMBE WA CPA TAWI LA TANZANIA WAKUTANA NA WAJUMBE WA CPA TAWI LA CANADA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
   Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya  Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania Dkt Raphael Chegeni (katikati) akiongoza kikao wakati Wajumbe wa Kamati hiyo walipokutana na Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada  katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam mapema leo.
 Mwenyekiti  wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada  Mhe. Yasmin Ratansi (wa kwanza kushoto) akisisitiza jambo wakati Wajumbe wa Chama hicho kutoka Canada walipokutana na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya  Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam mapema leo.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Mhe. Yasmin Ratansi akimkabidhi  zawadi Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya  Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania Dkt Raphael Chegeni mara baada ya Wajumbe wa pande zote mbili kuzungumza mapema leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati Tendaji ya  Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania katika picha ya pamoja na Wajumbe wa   Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada mara baada ya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
        (Picha na Ofisi ya Bunge)

MSHINDI WA MZUKA JACKPOT AKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA SHILINGI MILIONI 80 JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
MSHINDI  Mkuu wa mchezo wa bahati nasibu ya Tatu Mzuka , Rashid Ally, leo amekabidhiwa sh.milinoni 80 alizojishindia katika droo kubwa  iliyochezwa Jumapili.

Rashid ambaye alijishindia kiasi hicho cha fedha katika mchezo huo wa Tatu Mzuka, alionyesha kutoamini, huku akiwa na furaha na shukrani baada ya ushindi huo wa kihistoria. Rashid, ambaye ana umri wa miaka 21 tu, anaishi na familia yake maeneo ya Temeke, Dar es Salaam. 

Akizungumzia ushindi wake, Rashid ambaye amemaliza kidato cha nne hivi  karibuni, alisema kuwa alikuwa anacheza angalau mara 4 hadi 6 kwa wiki kwa kutumia pesa aliyokuwa anaipata katika  shughuli zake za kila siku.
'Ndoto yangu ni kujenga nyumba, na kuwekeza katika kilimo,  kitu ambacho nitafanya kwa kushirikiana na mama pamoja na Baba yangu. Nia yangu ni kuikuza iwe ni biashara kubwa ' alisema Rashid.

Pia alisema ana mpango wa kuendelea kucheza mchezo na kuwa balozi wa Tatu Mzuka, ili kuwasaidia watu kufurahia mchezo huo na kuuamini. "Watu wengine ni wagumu kuamini kwamba unaweza kushinda kiwango hiki kikubwa cha fedha kupitia shilingi 500 tu. Ninafurahi kuwa miongoni mwa watu wa kwanza  kuthibitisha hili"
 Balozi wa Mchezo wa Bahati Nasibu wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi ya thamani ya shilingi milioni 80 Mshimdi Mkuu wa Mchezo huo, Rashid Ally katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Regence Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed.
Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Lumuliko Mengele, akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto ni mama wa mshindi huyo, Fatma Kavila. Katikati ni mshindi, Rashid Ally.
Baba, mama na mwana wakiwa wameshika mfano wa hundi wa kiasi hicho cha fedha alichoshinda mtoto wao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Hakuna mgogoro wowote pori Tengefu la Mkungunero-DC Kondoa

$
0
0
BAADA ya baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kuwepo mgogoro kati ya wananchi na serikali katika Pori tengefu la Mkungunero wilayani Kondoa mkoa wa Dodoma, mkuu wa wilaya hiyo amejitokeza na kudai taarifa hizo hazina ukweli.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bibi Sezaria Makota, alisema habari zilizosambazwa kuhusiana na wananchi kunyanyaswa katika pori la Mkungunero zinazungumzia matukio ya zamani ambayo kimsingi yameshapatiwa ufumbuzi na serikali.



“Katika taarifa zilizotolewa kwenye vyombvo vya habari imeelezwa kuwa viongozi na wanakijiji katika Kijiji cha Kisondoko na Kata ya KK kuwa wananyanyaswa na kuna wasichana walisema wamebakwa lakini nakanusha taarifa hizi si za kweli, wafanyakazi wa pori la Mkongonero wanajiheshimu na wanafanya kazi kwa nidhamu,” alisema Bi. Makota na kuongeza:



“Nilipofika Kondoa mwaka jana (2016) nilisikia hayo malalamiko lakini nilipofuatilia nikabaini si kweli, viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama waliitisha mkutano kuwahoji wanakijiji wanaosema walinyanyashwa, kupigwa na kubakwa, kulikuwepo na madaktari waliowafanyia vipimo lakini hakuna aliyeonekana amebakwa.”




DK. SHEIN: SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR HAITOMBAGUA MTU YOYOTE.

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa huduma zote muhimu kwa wananchi wake zikiwemo huduma za afya bila ya ubaguzi.

Dk. Shein aliyasema hayo leo, huko Junguni, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba mara baada ya kuzindua Kituo cha Afya cha Mama na Mtoto, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake kiswani Pemba.

Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa kamwe Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitombagua mtu yoyote kwa itikadi yake ya kisiasa na badala yake itahakikisha wananchi wote Zanzibar wanapata huduma muhimu za maendeleo.

Dk. Shein alisema kuwa mwananchi yeyote anaekwenda kituoni hapo kupata huduma za afya hatabaguliwa kwani yeye ni mwananchi wa Zanzibar na akiwa mzazi atazalishwa kwa kufuata taratibu zote kwa mujibu wa taaluma aliyosomeshwa na Serikali.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.

UBALOZI WA KUWAIT WAANZISHA MRADI “KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU”

$
0
0
 Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem kwakushirikiana na  Mkuu wa taasisi ya taaluma ya maendeleo Profesa  Esta  Dugumaro, Mkuu wa Mipango Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Pancras Bujuw  wakikata utepe kuashiria  umezindua wa  kituo cha computer katika Taasisi ya Taaluma za Maendeleo  Chuo Kikuu cha Dar es Salam.
 Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem   (alieekaa)   akifafanua jambo mara baada ya uzinduzi huo.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo mara baada ya kuzindua kituo cha Kompyuta.
 
UBALOZI wa Kuwait nchini Tanzania umeanzisha mradi uitwao ““KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU” ambapo umezindua kituo cha Kompyuta katika Taasisi ya Taaluma za Maendeleo – Chuo Kikuu cha Dar es Salam. Hafla ya uzinduzi wa kituo hicho ambacho ni cha kwanza  ilihudhuriwa na Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Ester Dugumaro, Mkuu wa Uwekezaji na Mipango wa UDSM Dr. Bujuluru   pamoja na baadhi ya waalimu chuoni hapo.

Katika hotuba yake Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem alisisitiza kuwa Mradi Mpya unaolenga kuanzisha chumba cha Kompyuta katika taasisi za elimu ya juu ni muitikio wa wito uliotolewa na viongozi mbali mbali nchini  kuhusiana na kuweka mkazo katika kuinua elimu na kuunga mkono juhudi za Raisi John Magufuli aliyetangaza kutoa elimu bure kwa wananchi wote.

Balozi Al-Najem aliongeza kuwa mradi huu una lengo la kuanzisha idadi kubwa zaidi ya vituo vya Kompyuta katika vyuo mbalimbali nchini kote kwa kushirikiana na Asasi na Jumuiya za misaada za Kuwait na Tanzania, na hii ni kutokana na umuhimu  wa elimu kwa njia ya mtandao, Al-Najem aliongeza kuwa Chuo Kikuu cha Dodoma kitakua ndio kituo cha pili kufaidika na mradi huuu mkubwa, kikifuatiwa na  chuo kikuu cha Zanzibar (SUZA).

Kwa upande wake Profesa Ester Dugumaro alitoa shukurani za dhati kwa Nchi ya kuwait kwa niaba ya uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa misaada mbali mbali inayotolewa kwa Tanzania katika sekta ya elimu, huku akielezea matumaini yake ya kutiwa saini kwa makubaliano ya kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kuwait  na vyuo vyengine nchini humo katika nyanja zote.

Bi. Dogomaro aliongeza kuwa wanafunzi wa Uzamili na Uzamifu ndio watakaofaidika zaidi na kituo cha kompyuta kilichoanzishwa na Ubalozi wa Kuwait   ambapo wataweza kutumia mitandao kutafuta taarifa na maelezo kwa madhumuni ya utafiti.

Yafaa kuweka wazi kuwa Ubalozi wa Kuwaiti hapa Tanzania umeanzisha miradi mbalimbali  katika kipindi cha hivi karibuni kama “Kisima cha Maji kwa Kila Shule” na “Maabara ya sayansi kwa kila shule” yenye lngo la kuisaidia Tanzania katika sekta ya elimu.  

WAZIRI MKUU AWAKARIBISHA WACUBA KUJENGA VIWANDA TANZANIA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Balozi Lucas Domingo Polledo, ambapo amewakaribisha wafanyabiashara wa Cuba kuja kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa. 

Amesema kwa sasa Serikali ya Tanzania inaagiza dawa kutoka nje ya nchi jambo ambalo linasababisha kutumia fedha nyingi, hivyo uwepo wa kiwanda utasaidia katika kupunguza gharama. Pia wawekezaji watakuwa na uhakika wa soko la bidhaa zao. 

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumanne, Agosti 22, 2017) wakati akizungumza na Balozi Polledo mjini Havana. Waziri Mkuu yuko nchini Cuba kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. 

Alisema Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda nchini kama mkakati wa kukuza uchumi na kufikia uchumi wa kati, hivyo wafanyabiashara kutoka nchini Cuba wanakaribishwa kuja kuwekeza nchini, hususani katika viwanda vya dawa na sukari. 

Waziri Mkuu alisema licha ya Tanzania kuwa ni nchi ya amani na yenye utulivu wa kisiasa, pia imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji jambo ambalo litawawezesha watakaokuja kuwekeza nchini kupata tija.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) akisalimiana na Balozi wa Cuba Nnchini Tanzania Bwana Lucas Domingo Polledo walipo kutana kwa mazungumzo ya kikazi jana August 22/2017 akiwa katika ziara ya kikazi Havana Cuba. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

SERIKALI YARIDHIA WAATHIRIWA WA JANGA LA MOTO SOKO LA SIDO KUENDELEA KUBAKI KATIKA ENEO LAO,NAIBU SPIKA ACHANGIA MILIONI KUMI

$
0
0
Baada ya Soko la Sido kuteketea kwa moto,hatimaye Serikali Mkoani Mbeya imeridhia Waathirika wa janga la Moto katika soko hilo kuendelea kubaki katika maeneo yao ya awali na kuagizwa kujenga  vyumba vya kudumu ili kukabilina na majanga ya moto yanapojitokeza.

Akitoa maelekezo ya serikali,Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewaagiza watendaji wa halmashauri kupiga kambi katika eneo la soko la Sido haraka kuanzia siku ya kesho kwa ajili ya kubuni michoro na mpangilio wa soko hilo ili wafanyabiashara waanze ujenzi na hatimae kuendelea na biashara zaoa kama kawaida.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Mbeya Mjini,Mkoa ikiwa ni pamoja na mbunge wa Jimbo  Mbeya Mjini Mh.Joseph Mbilinyi pamoja na Naibu Spika Mhe.Dkt Tulia Ackson ambaye ametoa msaada wa shilingi milioni 10 kwa wathirika hao.Aidha baada ya kutolewa kwa kiasi hicho cha fedha ,Mkutano huo ukaridhiwa kuwa fedha hiyo ibaki kwa Mkuu wa Mkoa huku uongozi wa soko ukipanga matumizi ya fedha hiyo.

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Makala ameliagiza Jeshi la Zimamoto kuendelea kutoa elimu ya zimamoto,kusambaza vifaa vya kuzuia moto na kuchimba visima vya maji vya ziada katika masoko huku akiwataka viongozi wa ngazi zote za mkoa kuchukua tahadhari za moto kwenye masoko kutokana na ripoti kuonesha chanzo cha janga hilo ni mabaki ya moto uliotokea kwenye moja ya vibanda vya mamalishe waliokuwa ndani ya soko hilo.

 Naibu Spika ,Mhe.Dkt Tulia Ackson akimuonesha jambo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Amos Makalla mara baada ya kufanya mkutano na Wanyabiashara wa Soko la Sido-Mwanjelwa jijini Mbeya mapema leo.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, waandishi wa habari, wanasiasa pamoja na jeshi la polisi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa mbeya Mh.Amos Makalla wakitembelea eneo la soko la Sido lililoteketea Kwa Moto hivi karibuni Jijini Mbeya.


Baadhi ya Wananchi wakiwa sambamba na Wafanyabiashara wa soko la Sido-Mwanjelwa,wakifurahia uamuzi uliotoewa na Serikali ya Mkoa wa Mbeya,kuwa Wafanyabiasha hao wabaki katika soko hilo badala ya kuhamishwa katika soko lingine.

Baadhi ya Wananchi wakiwa sambamba na Wafanyabiashara wa soko la Sido,wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Amos Makalla alipokuwa akizungumza nao kwenye mkutano wa pamoja katika kutoa maamuzi ya kuwa Wafanyabiasha hao wabaki katika soko hilo badala ya kuhamishwa katika soko lingine huku utaratibu wa ujenzi ukiendelea kuwekwa sawa.

PICHA ZOTE NA FADHIL ATICK MR.PENGO MBEYA.

USAJIRI MPYA WA MAGAZETI NA MAJARIDA KUANZA RASMI LEO-SERIKALI

KIKAO CHA URATIBU WA MPANGO KAZI WA TAIFA WA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO WAFANA

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bibi Maimuna Tarishi akifungua mkutano wa siku moja wa wadau kuchangia utekelezaji wa mkakati wa Kitaifa wa  miaka mitano wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bibi. Sihaba Nkinga, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bibi. Maimuna Tarishi (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Dkt. Zainabu Chaula, wakiendelea na mkutano wa siku moja wa wadau kuchangia utekelezaji wa mkakati wa Kitaifa wa  miaka mitano wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa kutetea haki za wanawake na watoto wakiendelea na mkutano wa siku moja wa wadau kuchangia utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa  miaka mitano wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

RIPOTI: MAAMBUKIZI YA MARADHI MALARIA YAPUNGUA KWA WASTANI WA ASILIMIA 50

$
0
0
Ripoti ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ugonjwa wa Malaria hapa Nchini, inaonesha Kupungua kwa Maambukizi ya Maradhi Malaria Kwa Wastani wa asilimia 50 tangu Mwaka 2000.

Wakati Maambukizi yakionesha kupungua, inakadiriwa asilimia 90 ya Watanzania Wanaishi kwenye maeneo ambayo kuna maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria.

 Kiongozi wa Uchunguzi na Matibabu kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria nchini, Dkt Sixbert   Mkude akizungumza na waandishi wa habari leo  Jijini Dar es Salaam amesema pamoja na ugonjwa wa Malaria umekuwa ni changamoto kwa sababu unazishambulia zaidi kaya masikini.
Dkt Sixbert  Mkude amesema udhibiti wa Malaria na vifo vinavyosababishwa na Mbu waenezao vimelea vya Ugonjwa ni kuendelea na mikakati ya kutokomeza maradhi hayo.

Kwa upande wake Kiongozi  Mdhibiti  wa Mbu aneezae  Malaria  kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria nchini, Charles Mwalimu amesema  Sababu zinazokwamisha jitihada za kuukabili ugonjwa huo , Ikiwemo jamii kuwa na mwitikio hasi kwenye matumizi ya afua zinazotolewa na Serikali.

“Mpango wa Taifa wa Kudhibiti ugonjwa wa Malaria nchini, mwaka huu Serikali imepanga kuendelea na kampeni ya kupulizia viutalifu ukoko Kwenye Baadhi ya Wilaya zilizopo kanda ya ziwa” amesema Mwalimu
 Kiongozi wa Uchunguzi na Matibabu  kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria nchini, Dkt Sixbert Mkude akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini  Dar es Salaam juu ya Ugonjwa wa Malaria jinsi ulivyokuwa changamoto kwa sababu unazishambulia zaidi kaya masikini.
 Kiongozi  Mdhibiti  wa Mbu aenezae  Malaria  kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria nchini, Charles Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari juu ya  kuendelea kufuatilia tabia, wingi, Aina, Uwepo wa vimelea na usugu wa mbu ili kupanga mikakati ya kuutokomeza ugonjwa huo.
 Wadau mbalimbali wa Afya wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


MTANANGE WA YANGA NA SIMBA NGOMA BADO NGUMU MPAKA SASA

$
0
0
Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima akiwania mpira wa mshambuliaji wa Yanga Donald ngoma katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Ngao ya Jamii unaoendelea hivi Uwanja wa Taifa.
Kiungo wa Yanga Rafael Daud akimruka beki wa Simba Method Mwanjali katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Ngao ya Jamii unaoendelea hivi sasa Uwanja wa Taifa
Beki wa kati wa Yanga Kelvin Yondani na mshabuliaji wa Simba Laudit Mavugo wakigombania mpira katika mchezo wa ufunguzi wa ligi wa Ngao ya Jamii unaoendelea hivi sasa Uwanja wa Taifa.
Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma akimruka beki wa Simba Method Mwanjali katika mchezo wa ufunguzi wa ligi wa Ngao ya Jamii unaoendelea sasa hivi Uwanja wa Taifa
Golikipa Rostand Youthe akiruka juu na  kudaka mpira akiwa sambamba na mshabuliaji wa Simba Emanuel Okwi.
Kiungo wa Simba Haruna Niyonzima akipiga pigo la adhabu nje ya kumi na nane
Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma akipambana na beki wa kati wa Simba Salim Mbonde katika mchezo wa ufunguzi wa ligi Ngao ya Jamii.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

SIMIYU KUFANYA MAPINDUZI YA KILIMO KUPITIA UMWAGILIAJI

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu.

Mkoa wa Simiyu umejipanga kufanya mapinduzi ya Kilimo kupitia skimu kubwa ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni, kwa lengo la kuwainua wananchi Kiuchumi na kukabiliana na upungufu wa chakula.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika kikao kilichofanyika kati ya Viongozi na Wataalam ngazi ya Mkoa,Wilaya na wananchi wa vijiji vya Kata ya Mwamanyili Wilayani Busega kujadili juu ya mipango ya utekelezaji wa skimu hiyo.

Amesema katika Skimu hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Busega itaingia mkataba na kukopa fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) ambayo tayari imekubali kutoa mkopo huo, ili kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya maji kutoka Ziwa Victoria kwenda kwenye mashamba, kuwawezesha wananchi kununua mbegu bora, mbolea, na zana bora za kilimo.

Aidha, ameeleza kuwa wananchi katika skimu hiyo watazalisha mpunga kwa misimu miwili kwa mwaka na kupanda mazao mengine mbadala hususani ya jamii ya mikunde mara baada ya kuvuna mpunga, kwa ajili ya kurutubisha Ardhi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamanyili, juu ya Skimu ya Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
 Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera  akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamanyili, juu ya Skimu ya  Umwagiliaji inaotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwamanyili wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao cha kujadiliana juu ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
 Ndg.Shadrack Yohana Mkazi wa Kijiji cha Nasa Ginnery Kata ya Mwamanyili,akichangia jambo katika kikao cha Viongozi wa Mkoa, Wilaya ya Busega na wananchi kilichofanyika katika Kijiji cha Mwamanyili,  kwa lengo la kujadili juu ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 2 WA TAIFA WA URUTUBISHAJI WA CHAKULA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka wataalamu wa masuala ya lishe na urutubishaji chakula kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya virutubisho kwa wananchi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku mbili wa Kitaifa kuhusu Urutubishaji Chakula uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Samia Suluhu alisema ukosefu wa upatikanaji wa vyakula vyenye virutubisho   unaweza kuathiri Taifa hasa wakati huu nchi inapolekea kuwa Tanzania ya viwanda, Alielekeza ushirikishwaji na wadau malimbali katika kukabiliana na changamoto utasaidia kupunguza tatizo hili , takwimu zinaonyesha hali yetu ya lishe bado hairidhishi ila ni vyema kuweka nguvu pamoja ili watoto wetu ambao ni Taifa la Kesho waweze kujenga Taifa imara.

Makamu wa Rais alisema Tanzania ina asilimia 34 ya watoto wenye udumumavu pamoja na magonjwa mengine kama mgongo wazi na vichwa vikubwa kutokana na lishe duni.Makamu wa Rais alisema atakuwa na mkataba na Wakuu wote wa mkoa kuhakikisha kila mkoa unaweka takwimu zake vizuri na jitihada wanazofanya kuelimisha wananchi wao umuhimu wa lishe bora na virutubishi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Taifa wa Urutubishaji wa Chakula uliofanyika kwenye kituo cha Mikutano Cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata keki iliyopikwa kwa unga wa mahindi wenye vitamini A na ngano mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Taifa wa Urutubishaji wa Chakula uliofanyika kwenye kituo cha Mikutano Cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto waliozaliwa na tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi (Hydrocephalus and Spina Bifida) na wazazi wao wakati ufunguzi wa Mkutano wa Taifa wa Urutubishaji wa Chakula uliofanyika kwenye kituo cha Mikutano Cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 

NCC YATAKIWA KUTOA ELIMU YA UTATUZI WA MIGOGORO

$
0
0

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Mhandisi Edwin Ngonyani, ameitaka Kampuni ya Simu Tanzania TTCL kuongeza juhudi za kutoa huduma kwa Wananchi hasa waliopo katika maeneo ya Vijijini ili kuwawezesha Wananchi kupata Mawasiliano ya uhakika kutoka katika Kampuni yao Umma.

Mhe Ngonyani ametoa maelekezo hayo alipofanya ziara fupi ya kutembelea Makao Makuu ya TTCL ambapo amepata fursa ya kuzungumza na Bodi na Menejimenti ya TTCL ambapo alitumia hadhatra hiyo kutoa mrejesho wa ziara yake ya kutembelea maeneo mbali mbali ya Tanzania Bara na Visiwani kukagua huduma za Taasisi zilizo chini ya Wizara yake.

Mhe Ngonyani amesema, pamoja na mafanikio makubwa ambayo TTCL imeyapata katika Viwango vya ubora wa huduma, kuongeza idadi ya Wateja, usimamizi na uendeshaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) na Kituo cha Kutunzia Kumbukumbu za Kimtandao( NIDC) bado TTCL inakabiliwa na changamoto kubwa ya kufikisha huduma ya Mawasiliano Vijini hasa katika maeneo ambayo kwa sasa hayana Mawasiliano kabisa baada ya kuzimwa mwa mitambo ya Mawasiliano iliyokuwa ikitumia teknolojia ya CDMA.

Aidha, Mhe Ngonyani ameiagiza Bodi na Menejimenti ya TTCL kuongeza kasi ya kusambaza huduma za TTCL 4G pamoja na kufanyia kazi kilio cha muda mrefu cha Watumishi wa TTCL kuomba kuboreshewa Maslahi yao.

“Pote nilipopita Bara na Visiwani, Watumishi wa TTCL wameniomba nifikishe kilio chao kwenu, wamekaa kipindi kirefu sana bila kuboreshewa maslahi yao huku gharama za maisha zikiwa juu. Ninashauri msikie kilio hiki ili pamoja na kuboresha huduma zenu, mazingira ya kazi na maslahi ya Watumishi pia yapewe kipaumbele,”

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) leo Makao Makuu ya kampuni hiyo alipotembelea na kuzungumza na Bodi hiyo katika ziara yake ya kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara yake. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omar Nundu. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mhandisi Omar Nundu (kushoto) akitoa maelezo mafupi kuhusiana na utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) alipotembelea na kuzungumza na Bodi ya TTCL leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw Waziri Waziri Kindamba akiwa katika kikao hicho. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Waziri Kindamba (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) mara baada ya kuwasili katika ofisi yake kusaini kitabu cha wageni.
Sehemu ya menejimenti ya kampuni ya TTCL ikiwa katika kikao hicho na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Mhandisi Edwin Ngonyani alipowatembelea.

Rais Magufuli amteua Luteni Kanali Frederick Felix Milanzi kuwa Kamishna wa Operation wa Mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna Mkuu wa mamlaka ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya Rogers Sianga alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Kamishna Mkuu wa mamlaka ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya Rogers Sianga alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017.

Tanzania yapata Msaada wa Shilingi Trilioni 1 kutoka Uingereza

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe. Rory Stewart alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu   Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID) nchini  Bi. Elizabeth Arthy  aliyeongozana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe. Rory Stewart pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke walipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mazungumzo na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe. Rory Stewart pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke walipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana  na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe. Rory Stewart akiwa na Mkuu   Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID) nchini Bi. Elizabeth Arthy pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana  na akiwa na Mkuu   Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID) nchini Bi. Elizabeth Arthy aliyeongozana na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe. Rory Stewart pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari baada ya kufanya mazungumzo  Waziri wa Mambo ya Nje wa uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe. Rory Stewart akiwa na Mkuu   Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID) nchini Bi. Elizabeth Arthy pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017.
Picha na IKULU
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images