Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Thanda: Kisiwa kinachopatikana Tanzania ambapo kulala usiku mmoja inagharimu zaidi ya shilingi milioni 22!

$
0
0
Na Jumia Travel Tanzania
Inawezekana usiamini kwamba kuna sehemu zinagharimu zaidi ya shilingi milioni 22 za kitanzania kulala kwa usiku mmoja tu! Amini au usiamini sehemu hizo zipo, tena hapa hapa nchini kwetu Tanzania.

Jumia Travel ingependa kukujulisha kwamba kupitia shughuli za kitalii, hakuna kinachoshindikana. Linapokuja suala la kujionea mazingira adimu na ya kuvutia au wanyama wa aina mbalimbali, gharama au umbali wa kuyafanikisha hayo huwa siyo masuala ya msingi.
Thanda, ni sehemu kwa ajili ya mapumziko iliyotengenezwa na mtu binafsi katika eneo la kisiwa cha Shungimbili kilichomo Wilaya ya Kisiwa cha Mafia. Kisiwa hiki kina ukubwa wa takribani hekari 20 ambamo ndani yake imejengwa nyumba moja. Nyumba hiyo ina vyumba vya kulala vitano na vibanda viwili pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya Hindi kusini mwa Tanzania ambapo familia ya watu mpaka 10 inaweza kuishi.
Ili kuweza kuishi kwenye kisiwa hiki, wamiliki hutoza wageni kiasi cha dola za kimarekani 10,000 kwa usiku mmoja ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 22 za kitanzania. Mazingira ya kuvutia, utulivu wa hali ya juu na namna eneo hili lilivyotengenezwa ndivyo vinavyowafanya watalii kulipia gharama hizo lisiwe ni jambo la kushangaza. Ni jambo la kawaida ukiwa mapumzikoni kisiwani humo kuwaona au kuogelea pamoja na viumbe wa baharini kama vile pomboo (dolphin), papa wakubwa (whale sharks) na kobe wa majini.

Wamiliki wa kisiwa hiki binafsi cha mapumziko, wanandoa Bw. Dan na Bi. Christin Olofsson ambao asili yao ni Sweden walipata wazo la kutengeneza sehemu hii ikiwa ni kwa ajili ya kupumzikia pamoja na watoto wao watatu na wajukuu nane. Kikubwa kilichowasukuma kufanya hivyo ni katika jitihada za kubadili mazingira hususani hali ya hewa ukizingatia nchi za Scandinavia wanapotea hukumbwa na baridi kali kwa vipindi virefu vya majira ya mwaka. Walianza kwa kuwekeza Afrika ya Kusini kutokana na kuvutiwa na wanyama na uoto wa asili kabla ya kuja nchini Tanzania.  
Miongoni mwa masuala ambayo yalizingatiwa kabla ya uwekezaji katika kisiwa hiki ni pamoja na kulinda vivutio vya kitalii na kuhifadhi viumbe wa baharini katika eneo hilo. Kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uhifadhi wa Baharini ya Kisiwa cha Shungimbili, wamiliki wa Kisiwa cha Thanda wanashirikiana kwa ukaribu kuhakikisha jitihada za kulinda na kuendeleza uhifadhi wa vivutio vyake unazingatiwa.
Mbali na hayo, Kisiwa cha Thanda kinahakikisha kwamba jamii ya wakazi wanaoishi karibu na sehemu hiyo ambapo ni Kisiwa cha Mafia, wanafaidika na uwekezaji huo. Wakazi wake wananufaika kupitia ajira, uchangiaji kwenye shughuli za maendeleo ya elimu pamoja na uhifadhi wa viumbe wa baharini ambalo ndio kipaumbele kubwa.    
Tanzania inazo fursa nyingi za kitalii ambazo watu kutoka mataifa ya nje wanaziona na kuzitumia ipasavyo. Jumia Travel inaamini kwamba kupitia makala haya utakuwa umejifunza mambo mengi kuhusu Kisiwa cha Thanda ambayo hukuyajua hapo awali. Ni fursa kwako kuendelea kutafuta na kujifunza vivutio vinavyopotikana sehemu nyingine za nchi.  


TAARIFA KWA UMMA

Tanzania rated Africa's best safari country of 2017

$
0
0
THE NETHERLANDS – SafariBookings.com has conducted an in-depth analysis of reviews from safari tourists and acclaimed Africa experts to determine the continent’s best country for safaris. And the winner? Tanzania came out on top – the country is the clear winner and has been awarded our best safari country for 2017.
More than 2,500 reviews were used in this comprehensive research. Contributions came from safari-goers all over the world. And 22 reputable guidebook authors – working for Lonely Planet, Rough Guides, Frommer’s, Bradt and Footprint, who make-up the SafariBookings expert panel – also contributed reviews.

LORI LAACHA NJIA NA KUPIGA MWELEKA ENEO LA KIMARA TEMEBONI, JIJINI DAR

$
0
0
 Lori la Mafuta likiwa limepiga mweleka baada ya kuacha njia katika barabara ya Mororogo eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam leo. Chanzo cha kupiga mweleka kwa lori hilo hakikufahamika kwa haraka.
Lori la Mafuta likiwa limepinduka baada ya kuacha njia katika barabara ya Mororogo eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam leo.

MAGAZETI YA JUMAPILI LEO AGOSTI 20,2017

Introducing brand new video single "KWA AKILI YANGU" by Rama Dee

Masauni: Polisi, Temesa na NIT kuungana kukagua magari nchini

$
0
0
Na Felix Mwagara (MOHA)
MWENYEKITI wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema Baraza lake litakutana kujadili uwezekano wa Jeshi la Polisi, Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) pamoja na Chuo cha Usafirishaji (NIT) ziweze kuungana ili kufanya ukaguzi wa lazima wa magari kwa lengo la kuondoa ajali nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea ofisi za Temesa na Chuo cha NIT, Masauni alisema ziara yake ilikua na mafanikio makubwa, hivyo anatarajia kukutana na Wajumbe wa Baraza lake katika vikao vyao na kuwasilisha uzoefu alioupata mara baada ya kuzitembelea Taasisi hizo za Serikali. 

“Nimeshuhudia Temesa na NIT mambo ambayo sikuyatarajia, inaonyesha kwamba katika vita ya kuzuia ajali nchini hatutaanza sifuri, tunasehemu fulani ya kuanzia, tutaanza na utaratibu wenye mfumo mzuri ambao utaweza kutekelezwa ili kufikia malengo ya kuwa na utaratibu wa lazima wa ukaguzi wa magari yote ambayo yanatumika katika nchi yetu,” alisema Masauni na kuongeza;

“Lengo la mipango hiyo ni kuhakikisha tunakuwa na magari mazuri ambayo hayawezi kusababisha ajali, hivyo nitawasilisha katika kikao hicho chha Baraza uzoefu huu nilioupata baada ya ziara hii ili nijadiliane na wajumbe wenzangu tuone jinsi tutakavyokubaliana kuhusiana na mafanikio niliyoyapata baada ya ziara hii.”
 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Temesa, Mhandisi Sylvester Simfukwe (kulia), wakati Mwenyekiti huyo alipokuwa anatoka kuiangalia Karakana ya Utengenezaji wa Magari iliyopo katika ofisi za Temesa, Keko, jijini Dar es Salaam. Masauni alisema lengo kubwa la ziara yake, kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini.  
 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyekaa), akimsikiliza rubani Edger Mcha (kulia) wa Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT) kilichopo jijini Dar es Salaam, wakati alipokua anamuonyesha jinsi ya kuongoza ndege inapotaka kuruka na kutua kutoka katika kiwanja cha ndege. Mwenyekiti huyo alipata maelezo hayo wakati alipokua katika darasa la kufundishia marubani chuoni hapo. Masauni alifanya ziara katika chuo hicho na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini. Akiwa chuoni hapo aliangalia ukaguzi wa magari na pia kupata mipango mbalimbali waliyonayo kuhusiana na elimu wanayoitoa ya kuhusiana na usalama barabarani. Aliyevaa koti ni Mkuu wa Chuo hicho, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza hilo, Profesa Zakaria Mganilwa. 
 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiangalia mashine ya kukagua magari kwa njia ya umeme iliyokua inaonyeshwa na Mhandisi Yakubu Kibingo wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA. Katikati ni Meneja wa Karakana ya kutengeneza magari na mitambo mbalimbali ya Serikali, Julius Humbe. Masauni alifanya ziara katika ofisi hiyo iliyopo Keko, jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini.  
 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT), Profesa Zakaria Mganilwa (katikati) alipokua anatoa historia ya chuo hicho pamoja na kozi mbalimbali zinazofundishwa katika chuo hicho, kilichopo Mabibo jijini Dar es Salaam. Masauni alifanya ziara chuoni hapo kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini. Kulia ni Naibu Mkuu wa Chuo hicho kwa upande wa Taaluma Utafiti na Ushauri, Dk. Prosper Mgaya. 
 Mkuu wa Idara ya Teknolojia ya Usafirishaji wa Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT), kilichopo Mabibo, jijini Dar es Salaam, Amon Mwasandube, akimuonyesha Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), jinsi gari linavyokaguliwa linapokuja katika Kituo cha Ukaguzi wa Magari chuoni hapo. Masauni alifanya ziara chuoni hapo kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Zakaria Mganilwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Tumesoma "Confession of the Lioness"

$
0
0

Na Profesa Joseph Mbele

Tumo katika wiki ya mwisho ya kozi ya "African Literature," ambayo ni kwa kipindi hiki cha kiangazi. Kati ya vitabu ambavyo tumesoma ni Confession of the Lioness, riwaya ya Mia Couto wa Msumbiji. Couto ni mmoja wa waandishi maarufu kabisa Afrika na ulimwenguni, ambaye amepata tuzo za kimataifa kwa uandishi wake, ikiwamo tuzo ya Neustadt.

Mia Couto anaandika kwa ki-Reno. Ninasoma na kufundisha tafsiri za ki-Ingereza. Kwanza nilifundisha riwaya yake The Tuner of Silences hapa chuoni St. Olaf nikaipenda sana. Niliifundisha tena katika muhula mwingine. Kutokana na hilo, niliamua kufundisha riwaya yake nyingine. Ndipo nikachagua Confession of the Lioness, baada ya kusoma taarifa zake mtandaoni.
Riwaya hii inasimulia habari za eneo la kaskazini mwa Msumbiji, katika jamii ya wa-Makonde. Jamii inaishi kwa hofu na wasi wasi kutokana na kuwepo kwa simba ambao huzunguka na hushambulia watu na mifugo. Wasi wasi umechanganyika na imani za kishirikina kuhusu simba hao. Je, ni simba kweli, au ni simba wa kutengenezwa kiuchawi? Hilo ni moja ya maswali yanayosumbua jamii hii.

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ziarani CUBA

$
0
0
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na naibu waziri wa mambo ya nchi za Nje ya Cuba mheshimiwa Anna Teresita Gonzalez baada ya mazungumzo yao yaliyolenga kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Cuba. Cuba imekubali kutoa nafasi za masomo ya juu kwa madaktari wa Zanzibar waliofundishwa udaktari na madaktari bingwa kutoka Cuba. Mazungumzo ya viongozi hawa wawili yalifanyika katika jumba la itifaki mjini Havana Cuba.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali SADC mjini Pretoria Afrika Kusini

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana tarehe 19 Agosti 2017, amehudhuria  ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC mjini Pretoria Afrika Kusini akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli.
Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa taarifa fupi kuhusu majukumu ya SADC Organ kwa kipindi cha Agosti 2016 - Agosti 2017 kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa SADC Organ anayemaliza muda wake.
Makamu wa Rais amewasilisha kwa Wakuu wa Nchi na Serikali taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya SADC Organ kwa kipindi cha Agosti 2016 hadi Agosti 2017 kwa niaba ya Mwenyekiti wa SADC Organ anayemaliza muda wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Taarifa hiyo inaelezea hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda katika kipindi tajwa hususan katika Nchi za DRC, Madagascar na Lesotho.
Aidha taarifa hiyo pia imetoa mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto zinazoendelea kuikabili Kanda katika maeneo ya siasa, ulinzi na usalama.
Taarifa hiyo pia imeelezea hali ya demokrasia na chaguzi zilizofanyika kwa kipindi cha 2016/2017 kwa nchi wanachama.
Katika Mkutano huu Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amekabidhi Uenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama kwa Angola, baada ya Tanzania kukamilisha kipindi cha Uongozi wake chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Mkutano huu wa SADC uliofunguliwa rasmi  na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ambaye ni Mwenyeji wa Mkutano wa 37 wa SADC, ulitanguliwa na mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili uliofanyika tarehe 18 Agosti, 2017
Mkutano wa Troika Mbili umefanyika kwa kuzingatia mapendekezo ya Mkutano wa Mawaziri wa Kamati ya Asasi ya Ushirikiano wa Siasa,Ulinzi na Usalama (SADC MCO) uliofanyika Dar es Salaam tarehe 20 na 21 Julai, 2017 ambapo Mawaziri waliona ipo haja ya kuitisha Double Troika pembezoni mwa Mkutano huu wa 37 ili kujadili pamoja na mambo mengine, hali ya ulinzi na usalama.
Troika Mbili inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.
Serikali ya Afrika Kusini ambayo ni mwenyeji wa Mkutano huu wa 37 wa SADC na Mwenyekiti imependekeza kuwa kaulimbiu ya Mkutano wa 37 iwe ni Kushirikiana na Sekta Binafsi katika kuendeleza Viwanda na Kuongeza Thamani ya Bidhaa.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa SADC kutoka kwa Mfalme Mswati III, Rais wa Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma amesisitiza nchi wananchama kutekeleza kwa vitendo Kauli Mbiu ya Mkutano wa 37 wa SADC juu ya kushirikiana na Sekta Binafsi katika kuendeleza Viwanda na Kuongeza Thamani ya Bidhaa kuwa ndio njia pekee ya nchi za Jumuiya hiyo kupiga hatua kimaendeleo.
Rais Zuma amesisitiza nchi za Afrika kufanyakazi kwa bidii na kuhakikisha rasilimali za nchi  zinatumika kwa faida ya maendeleo yay a kweli.
Wakuu wa Nchi na Serikali wamepokea taarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda wa SADC 2015 - 2063 ambao ulipitishwa katika Mkutano wa Dharura uliofanyika tarehe 29 Aprili, 2015 mjini Harare, Zimbawe.
Mkakati huu unalenga kuzifanya nchi za SADC kuwa na uchumi wa viwanda na kushiriki zaidi katika  mnyororo wa thamani kikanda na kimataifa  na hivyo kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi wake.
Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC) utahitimishwa hapo kesho Jumapili tarehe 20 Agosti 2017, kwa kutolewa Tamko (Communique) litakaloelezea yaliyojiri katika Kikao cha Wakuu wa Nchi na Serikali.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC mjini Pretoria Afrika Kusini 

KIKAO CHA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI KUKAA LEO NA KESHO

$
0
0
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), inatarajiwa kuketi kwa siku mbili Agosti 20 na 21, 2017 kupitisha usajili, lakini kabla kupitisha itasikiliza malalamiko kutoka baadhi ya timu na vituo vya kuibua na kukuza vipaji vya soka zinazodai fidia baada ya wachezaji wao kusajiliwa na klabu nyingine msimu wa 2017/18.

Viongozi au Wawakilishi wa Klabu zifuatazo hawana budi kufika Azam FC, Pamba FC, African Lyon, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Singida United, Tusker FC, Young Africans, Njombe Mji, Majimaji, KMC, Ndanda FC, Coastal Union,  Stand United, Rhino FC, Mbao FC, Toto Africans, Stand United, Mbeya City na Lipuli. Pia wameitwa wachezaji Mbaraka Yussuf na Frank Hamisi.


Klabu na vituo vya kuibua na kukuza vipaji vilileta malalamiko yao TFF kudai fidia mbalimbali kama vile za mafunzo; ada ya usajili; ada za maendeleo na kuvunjwa kwa mikataba kutoka katika timu walizochezea hadi msimu uliopita.

Baadhi ya malalamiko yaliyopokelwa TFF ni ya Majimaji ya Songea dhidi ya Azam FC ya Dar es Salaam kuhusu mchezaji Idd Kipangwile.

Alliance ya Mwanza imelalamikia Pamba pia ya Mwanza kuhusu mchezaji Juma Nyangi ambako madai hayo yamekwenda mbali zaidi yakisema kuwa mchezaji husika amebadili jina kwa lengo la kudanganya.

Kwa upande wake, African Lyon imeondokewa na wachezaji 19 na inadai fidia katika timu, wachezaji kwenye mabano za Majimaji (Saleh Malande); Lipuli (Hamad Manzi, Lambele Reuben na Mussa Nampoka); Young Africans (Rostand Youthe Jehu); Tusker FC (Abdul Hilal) na Ndanda kwa wachezaji Hamad Tajiri na Baraka Majogoo.

Madai mengine ni dhidi ya Coastal Union kwa wachezaji Baraka Jaffary, Omary Salum, Raizen Hafidh na Fred Lewis huku madai mengine ni kwa Kagera Sugar kwa wachezaji Omar Abdallah, Abdallah Mguhi na Vicent Ludovic na Alhaji Zege .

Madai mengine ni dhidi ya timu ya Kinondoni Municipality Council (KMC) ambayo imewasajili Halfan Twenye, Yussuf Abdul na Rehani Kibingu wakati Singida United inalalamikiwa kumsajili Miraji Adam ilihali Njombe Mji inadaiwa fidia kwa kumsajili mchezaji Salum Juma.

Malalamiko mengine ni ya Kisa Academy ya Kinondoni, Dar es Salaam dhidi ya timu za Mbeya City (Idd Seleman); Majimaji (Jafar Mohammed); Mbao (Ally Rashid); Stand United (Said Mbati) na Friends Rangers (Hassan Abubakar).

Madai mengine dhidi ya timu za Coastal Union (Abubakar Nyakarungi na Ahmed George); The Mighty Elephant (Maliki Hamad); Kagera Sugar (Hussein Idd) na Azam FC (Omary Maunda).

DKT ANGELINE LUTAMBI AZINDUA “IKUNGI ELIMU CUP 2017” AMFAGILIA DC MTATURU KWA UBUNIFU

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akifyatua matofali wakati wa ufunguzi wa zoezi la ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara na madarasa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi akifyatua matofali wakati wa ufunguzi wa zoezi la ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara na madarasa.
Kikosi cha Timu ya Ikungi United
 Kikosi cha Timu ya Puma Combine kilichoshinda goli 3 kwa 2 dhidi ya Ikungi United
Moja ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita kwa kupata Daraja la kwanza akipokea shilingi 100,000 ikiwa ni ahadi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji J. Mtaturu
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimzuia mchezaji wa timu ya Madiwani wa Manispaa ya Singida asipite katika lango la Timu ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakati wa mchezo wa mapema kabla ya mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Ikungi Elimu Cupa 2017.Kwa habari kamili BOFYA HAPA

MTANDAO WA ELIMU TANZANIA WAHITIMISHA KUTOA MAFUNZO KWA WADAU WA ASASI ZA ELIMU KWA MIKOA SITA MORO

$
0
0


Afisa miradi ya elimu kwa masharika yasiyo ya kiserikali ubalozi wa Sweden nchini, Stephen Chimalo akizungumza jambo wakati wa mafunzo ya ufuatiliaji hatua ya chini ya uandaaji wa bajeti na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha katika sekta ya elimu kwa kutumia mfumo wa PETS kwa wadau kutoka asasi za elimu kwa mikoa ya Tanga, Tabora, Dodoma, Singida, Dar es Salaam na wenyeji Morogoro iliyoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/Met).
Afisa miradi wa Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/Met), Alistidia Kamugisha akizungumza jambo katika mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku tatu hoteli ya Flomi mkoani Morogoro.
Mtaalamu wa masuala ya IT Mtandao wa elimu Tanzania, Dominic Dogani akifafanua jambo kwa wadau wa mafunzo hayo wakati wa kujadili mada kupitia vikundi.
Mwanaidi Juma (Katikati) kutoka shirika la Morogoro Saving The Poor Organization (Mosaporg) akiwa na wadau wenzake wa elimu wakati wakiwajibika katika majukumu ya kujifunza mafunzo hayo.

Mratibu wa shirika la Youth Movement For Change (YMC) la mkoani Singida, Fidelis Yonde kushoto akijadiliana jambo na washiriki wa mafunzo hayo.

BENKI YA KILIMO YAKAGUA MIRADI YA KILIMO KILOMBERO

$
0
0

Katika kuhakikisha miradi inayopatiwa mikopo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), uongozi wa Benki hiyo kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Bw. James Ihunyo wametembelea miradi minne iliyopo wilayani humo.

Miradi iliyotembelewa ni Kapolo AMCOS, Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula. Nyingine ni Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa na Hope ya Kidatu.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema ameridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo hali inayochochea ari ya Benki katika kutimiza lengo la Serikali la kukopesha wakulima nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kushoto) akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyokopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wilayani humo. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo. 
Makamu Mwenyekiti wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula, Bw. Mohamed Dadi (kushoto) akionesha maendeleo ya Skimu hiyo wakati Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kulia) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo walipotembelea Skimu hiyo. 
Meneja Ufuatiliaji na Tathamini ya Mikopo wa TADB, Bw. Dickson Pangamwawe (wapili kushoto) akionesha maendeleo ya ukuaji wa miwa ya Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa ambao ni wanufaika wa mikopo ya Benki ya Kilimo. Wanaotazama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa, Bw. Sebastian Sanindege. 
Maafisa kutoka Benki ya Kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero wakingalia Mpunga uliyo tayari kuvunwa katika Skimu ya Umwagiliaji ya Kijiji cha Msolwa Ujamaa.  
Wakulima wa Skimu ya Umwagiliaji ya Kijiji cha Msolwa Ujamaa wakipanda mpunga kwa kutumia njia ya kilimo shadidi. 


Manispaa ya Sumbawanga watakiwa kujenga vituo vya afya zaidi

$
0
0

WAMJW- Rukwa

Manispaa ya Sumbawanga imeelekezwa kuongeza kujenga vituo vya afya kulingana na jiografia ilivyo ili hospitali ya Rufaa ya mkoa ibaki kutoa huduma za kibingwa mkoani hapa.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na watumishi wa sekta ya afya wa Mkoa na Wilaya kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wakati wa majumuisho ya ziara ya siku mbili ya kikazi

Alisema Serikali inaboresha hospitali za Rufaa za Mkoa kwa ajili ya huduma za kibingwa hivyo hospitali hizo ziweze hutoa huduma za kimatibabu ya kibingwa hasa kwa watu wenye huitaji huo,”lakini wananchi wanapaswa kufuata utaratibu wa sera unavyosema kwenda kupata matibabu katika hospitali za Rufaa ni lazima mgonjwa aandikiwe rufaa na sio kila mtu anaenda moja kwa moja kwenye hospitali hizo”

Waziri Ummy alisema kulingana na kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini ni vyema na mkoa kwa ujumla ni vyema kujenga vituo hivyo vitakavyoweza kutoa huduma kwa wananchi waliopo maeneo husika kuliko kujenga hospitali ya Wilaya ambayo wananchi waliopo maeneo ya mbali wapate huduma za afya huko huko karibu na huduma hizo ziwe bora.

“Fanyeni maamuzi yenye manufaa kwa wananchi wa wilaya yenu ili muwasogezee huduma watu wenu,alisema kwa Wilaya ya Nkasi wao wanatakiwa kujenga hospitali ya wilaya ya serikali ambapo Wizara yake itasaidia kutoa milioni 350 kati ya 650 ambayo itajenga wodi ya wazazi,maabara pamoja na nyumba moja ya mtumishi
Waziri wa Afya Ummy Mealimu akiongea na mmoja wa wagonjwa waliofika kupata matibabu kwenye kituo cha afya cha Mazwi kilichopo Manispaa ya Sumbawanga

Waziri Ummy mwalimu akimuuliza mmoja wa mama aliyefika kupata matibabu ya nje kwenye kituo cha afya cha Mazwi kama amefika muda mrefu na hajapata matibabu,waziri huyo yupo mkoani Rukwa kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kukagua huduma za afya zinazotolewa kwenye vituo vya huduma nchini
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na mama mjamzito aliyelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Rukwa.Waziri Ummy alisisitiza watoa huduma kuhakikisha awatoa huduma wa afya wanajitahidi kuepusha vifo vianavyoweka kuepukika kutokana na uzazi.


RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA JOSSAM & CO LTD KUMALIZA BARABARA ZA KATA YA ULEDI NA ISEVYA KWA WAKATI ULIPANGWA.

$
0
0
Na Tiganya Vincent-RS –TABORA

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeiagiza Kampuni ya Jossam & co Ltd kuhakikisha inakamilisha barabara ilizopewa za Uledi na Mwenge katika Manispaa ya Tabora hadi kufikia mwishoni mwa Mwezi Septemba mwaka huu.

Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri baada ya kutembelea ujenzi wa barabara hizo zinazojengwa katika Kata ya Uledi na Isevya ili kujionea maendeleo na kuhakikisha kama mjezni amezingatia upana na urefu ullioandikwa katika makubaliano ya mkataba.

Alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 700 zilizopangwa na Manispaa ya Tabora kutumika kukamilisha mradi huo ni fedha nyingi ni vema Mkandarasi anayejenga mradi huo akahakikisha anajenga katika kiwango bora na kwa upana na urefu uliomo katika mkataba ili thamani ya pesa ionekane.

Mkuu huyo wa Mkoa aliwaagiza Watendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanasimamia kwa karibu ujenzi wa barabara hizo unazingatia matakwa yaliyoelezwa katika Mkataba wa Ujenzi ili barabara hizo ziweze kutumika kwa muda mrefu bila kuharibika.

Awali Mhandisi Msaidizi kutoka Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Tabora Stephen Warioba alisema kuwa ujenzi wa barabara hizo unahusisha njia za waenda kwa miguu na ipaswa inamalize katika kipindi kilichoelezwa katika Mkataba.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwl. Queen Mlozi alimwakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa atafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kuwa kazi inayofanyika katika eneo husika inazingatia mambo yote yaliyomo katika Mkataba na sio nje ya hapo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Ndunguru alisema kuwa baada ya ujenzi wa Mradi huu kukamilika kutakuwepo na zoezi la upandaji wa miti na maua kando kando ya barabara.

SHAKA AMALIZA ZIRA YA KIKZAZI PEMBA, AMTUMIA SALAMU MAALIM SEIF

$
0
0
Na Mathias Canal, Pemba

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka amehitimisha ziara ya siku nne ya kikazi Kisiwani Pemba-Zanzibar kwa kuzuru katika Mikoa yote miwili ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba na Wilaya zake zote za Wete, Mkoani, Chakechake na Micheweni.

Katika ziara hiyo pamoja na mambo mengi alikagua na kushiriki kufanya kazi za kijamii ikiwa ni pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM 2015-2020, kushiriki kuona shughuli mbali mbali za uzalishaji Mali kupitia makundi ya vijana na kuwasaidia kwa kuwaunga mkono ili kuongeza mtaji wa miradi yao.

Alitumia ziara hiyo kuzungumza na makundi ya vijana kwa nyakati tofauti, viongozi wa CCM, jumuiya za CCM Pamoja na kushiriki shughuli zingine mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa na kuwaasa kukaa maskani pekee pasina kufanya kazi za uzalishaji mali jambo ambalo litapeleka mbele maendeleo katika jamii.

Katika maeneo yote aliyozuru Kaimu Katibu Mkuu huyo alitilia zaidi msisitizo kwa vijana kujiunga na vikundi mbalimbali vya kijamii ili kupatiwa mikopo ya vijana inayotolewa na serikali kwa asilimia 5 kila mwezi.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka akiagana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumaliza ziara ya siku nne ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Visiwani Pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka akiagana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumaliza ziara ya siku nne ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Visiwani Pemba. 
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka akiagana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumaliza ziara ya siku nne ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Visiwani Pemba. 


NI MARUFUKU KUINGIZA NA KUCHUNGA MIFUGO NDANI YA MAENEO YA YALIYOHIFADHIWA KISHERIA

ZIARA YA RAIS DK.SHEIN WILAYA YA MAGHARIBI A

$
0
0

DSC_9852
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akifungua pazia kama ishara ya   kuweka jiwe la Msingi Jengo jipya la Skuli ya msingi Kihinani leo akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo
DSC_9919
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza na Wananchi,Wazee na Wanafunzi   wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo jipya katika Skuli ya msingi Kihinani jimbo la Mfenesini  leo,akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,(kulia) Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma na (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud
DSC_0073
Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe.Salama Aboud Talib alipokuwa akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) wakati alipotembelea Mradi wa Visima vya Maji Safi na salama katika Shehia ya Bumbwisudi leo alipofanya ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo.Picha na Ikulu.20/08/2017

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAKINA BABA WATAKIWA KUTOA TAARIFA ZA MAENDELEO YA WATOTO KWA WENZA WAO

$
0
0

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Kumekuwa na tabia iliyojengeka kwa baadhi ya jamii zetu kwamba taarifa za maendeleo ya masomo au ukatili na unyanyasaji wa watoto lazima zitoke kwa mzazi wa kike kwenda kwa mzazi wa kiume.

kufuatia hali hiyo Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mkoani hapa kimetoa ushauri kwa wazazi wa kiume kurudi nyumbani mapema pia kuwa na muda wa kuongea au kukaa na watoto wao na kuwa wa kwanza kutoa taarifa za maendeleo ya watoto kwa wake zao badala ya hali hiyo kufanywa na wenza wao pekee kama ilivyo sasa.

Akizungumza jana Jumamosi katika kikao cha wazazi wa wanafunzi ya Saint Monica iliyopo maeneo ya Moshono jijini hapa, Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na watoto mkoa wa Arusha Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu alisema kwamba, imekuwa kawaida kwa baadhi ya wazazi wa kiume kutokuwa na muda wa kukaa na watoto kwa kile tunachokiita uwajibikaji katika utafutaji na kushindwa kujua matatizo ya watoto wao.

Alisema mara nyingi wazazi wengi wa kiume wamekuwa wakijiweka pembeni katika kuwasikiliza watoto wao kwa masuala madogo madogo na kudhani kwamba wenzi wao pekee ndio wanapaswa kujua masuala hayo na kufikiri wao huwa wanatatua shida kubwa kama vile chakula, mavazi na ulipaji wa ada.
  Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Arusha Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu akitoa elimu juu ya wajibu wa wazazi wa kiume katika malezi ya mtoto katika kikao cha wazazi kilichofanyika jana kwenye shule ya Saint Monica iliyopo jijini Arusha (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
 Mwalimu Mkuu wa shule ya Saint Monica Sister Pauline Etyang Nasike akitoa shukrani zake kwa Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mara baada ya Mkuu wa kitengo hicho kutoa elimu kwa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo juu ya malezi ya watoto wao. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Wazazi wa wanafunzi wa shule ya Saint Monica waliohudhuria kikao hicho wakionekana wakimsikiliza kwa umakini mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Arusha Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu alipokuwa akitoa elimu juu ya umuhimu wa wazazi wa kiume kuwa karibu na watoto wao. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).


Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images