Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1868 | 1869 | (Page 1870) | 1871 | 1872 | .... | 3353 | newer

  0 0


  0 0
  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Makwaia Makani akifungua mafunzo ya Huduma Kwa Wateja yaliofanyika katika hospitali hiyo jana. Kushoto ni mtoa mada, Elizabeth Fupe na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano katika Hospitali hiyo, Neema Mwangomo. Wafanyakazi wametakiwa kutumia lugha nzuri wakati wa kuwasiliana na wagonjwa pamoja na ndugu zao ili kurahisisha utuoaji wa huduma za matibabu.
   Baadhi ya wafanyakazi wakifuatilia mafunzo hayo yaliofanyika katika hospitali hiyo.  

   Baadhi ya wafanyakazi wakifuatilia mafunzo hayo yaliofanyika katika hospitali hiyo.  

  Wafanyakazi hao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupatiwa mafunzo hayo.

  0 0
 • 08/19/17--01:04: msiba marekani na Tanzania

 • Sarah, Sabrina Ally, Khadija Abullah wa New York na Biubwa Marumbo wa WashingtonDC. Wanasikitika kutangaza kifo cha mjomba wao Wilson Charles Amour kilichotokea ghafla nyumbani kwake DMV. Takoma Maryland. 
  Shughuli za mazishi zitatangazwa baadaye. kwa sasa tujumuike pamoja na wafiwa na kuwafariji katika kipindi hiki kigumu.
  Msiba upo nyumbani kwa Biubwa area
  116 Lee ave apt 110. T
  AKOMA PARK, MD, 20912. 
  Kwa maelezo zaidi wasiliana na 
  Sabrina  347 605-3276 au 
  Khadija 347 307-6930 
  Biubwa 12404766498.  
   Alban Abdul-aziz  785 550-2966
  UKIPATA TAARIFA HII MTAARIFU NA MWENZIO

  0 0

  Waziri wa Maliasli na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema serikali imefanikiwa kukamata jumla ya meno ya tembo 28 katika ghala moja lililopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam, yenye uzito wa takribani kilo 376. 

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri Maghembe amesema meno hayo yaliyokamatwa tarehe 13 na 14 mwezi wa nane mwaka huu yanaonekana ni ya tembo waliouawa miaka ya nyuma ikikadiriwa kuuawa miaka ya 2013 au 2014 na wahalifu hao kuyaweka majumbani mwao huku wakiendelea kutafuta masoko.

  Waziri Maghembe amesema tayari hadi hivi sasa watuhumiwa sita wa ujangili wameshakamtwa akiwemo Mohamedi Yahya Mohamed, almaarufu Mpemba, Aboubakar Zuberi Seguni mkazi wa Mbezi Beach ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali za mtaa na imamu wa msikiti wa Huda uliopo Mbezi, Juma Saleh Jebo mkazi wa Manzese jijini Dar es salaam, Hamisi Rashid Omary mkazi wa Mbezi, Amir Bakari Shelukindo Mkazi wa Gairo Morogoro na Ahmed Shabani Bakari mkazi wa Mkuranga.

  Wakati akiwataja watuhumiwa hao, Waziri Maghembe alisema vita dhidi ya ujangili ni ngumu kwa vile hata baadhi ya watu wasiotegemewa katika jamii kujihusisha nayo nao wamo, akitolea mfano wa mtuhumiwa, Bakari Zuberi Seguni mkazi wa Mbezi Beach ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali za mtaa na imamu wa msikiti wa Huda uliopo Mbezi kuwa yeye ni mfano katika jamii kwa kuwa ni kiongozi wa kiserikali lakini pia ni mtu wa Mungu ambaye ni ngumu kufikiria ni miongoni mwa washirika wa biashara hiyo haramu.

  Aliongeza kuwa, Tanzania kupitia Wizara yake inataka kufuta kabisa biashara ya meno ya tembo kama China walivyofanya licha ya kuwa uuzaji wa meno ya tembo kwa sasa mara baada ya kufuta soko la wazi imekuwa ikiendelea kwa njia ya mtandao.

  Katika hatua nyingine , Waziri Maghemba alipaza sauti kwa mataifa kama vile Vietnam na Thailand kuacha kujihusisha na biashara hiyo na kuiomba jumuiya ya Kimataifa kuingilia ili tembo waendelee kuwepo kwa faida ya kizazi kijacho na badae na dunia kwa ujumla.

  Aidha, Waziri Maghembe amesema Tanzania na Dunia kwa ujumla imepata pigo kubwa baada ya kutokea kwa mauaji ya Mkurugenzi wa Palm Foundation, Wayne Lotter raia wa Afrika Kusini yaliyotokea usiku wa jana Masaki jijini Dar es Salaam kwa kuwa alikuwa mstari wa mbele katika kuisaidia serikali katika vita dhidi ya Ujangili.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Mghembe akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokuwa akiwaonesha jumla ya meno ya tembo 28 yakiwa na takribani kilo 376 yaliyokamatwa kwenye ghala katika eneo la Mbezi Beach hivi karibuni. Jumla ya watuhumiwa wa ujangili wapatao 6 tayari wameshakamatwa akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa na Imam wa msikiti wa Huda wa Mbezi Beach, Aboubakar Zuberi Segumi ( Picha na Lusungu Helela- WMU)
  Baadhi ya meno ya tembo yaliyokamtwa hivi karibuni katika ghala moja lililopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam, yenye uzito wa takribani kilo 376.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji J. Mtaturu akifungua mipira itakatumika kwenye ligi ya mpira wa miguu maarufu kama "IKUNGI ELIMU CUP 2017" wakati akivitambulisha vifaa vyote vya michezo vitakavyotumika katika mashindano hayo leo Agosti 19, 2017.
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji J. Mtaturu (Kulia) akiwa na makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu Wilaya ya Ikungi Alhaji Salum Mohamed Chima wakionyesha vifaa vitakavyotumika kwenye ligi ya mpira wa miguu maarufu kama "IKUNGI ELIMU CUP 2017" wakati akivitambulisha vifaa vyote vya michezo vitakavyotumika katika mashindano hayo leo Agosti 19, 2017.
  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu Wilaya ya Ikungi Alhaji Salum Mohamed Chima akionyesha moja ya mipira itakatumika kwenye ligi ya mpira wa miguu maarufu kama "IKUNGI ELIMU CUP 2017" wakati akivitambulisha vifaa vyote vya michezo vitakavyotumika katika mashindano hayo leo Agosti 19, 2017.
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji J. Mtaturu akionyesha moja ya mipira itakatumika kwenye ligi ya mpira wa miguu maarufu kama "IKUNGI ELIMU CUP 2017" wakati akivitambulisha vifaa vyote vya michezo vitakavyotumika katika mashindano hayo leo Agosti 19, 2017.(Picha Zote Na Mathias Canal)

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji J. Mtaturu ametambulisha vifaa vitakavyotumika wakati wa mashindano ya "IKUNGI ELIMU CUP 2017" Inayoanza kurindima hii leo katika uwanja wa Shule ya Sekondari Ikungi.

  Kuanzishwa kwa ligi hii itasaidia kuhamasisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa elimu katika kutatua changamoto za elimu ikiwemo ujenzi wa Madarasa, Maabara pamoja na nyumba za waalimu kupitia mfuko wa elimu.

  0 0

  Na Mathias Canal, Kaskazini Pemba

  Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM umelaani vikali ubaguzi uliofanywa na baadhi ya Wanachama wasikuwa CCM kwa kuwazuia wanachama wa CCM kuswali pomoja katika misikiti kwenye baadhi ya maeneo Mbalimbali visiwani Pemba.

  Umoja huo umesema kuwa kuzuia watu kuswali kisa itikadi za dini zao ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu kwani kufanya hivyo ni kupiga amri ya Mwenyezi Mungu anayetoa onyo Kali katika Quran kwa wale wanaothubutu kuwazuia waini wengine kuswali.

  Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka Wakati akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Wakati alipotembelea Msikiti wa Masjid Lmuhajiriina uliopo Eneo la Kiungoni Kimango Wilayani Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

  Alisema kuwa Imani ya dini yoyote nchini haibagui wala kuchagua watu kuswali kutokana na Itikadi zao za kisiasa ama kikabila kwani dini Ni ibada ya Imani kwa kila mwananchi.

  Shaka Alisema kuzuia watu kuabudu Ni makosa kwa mujibu wa taratibu za nchi lakini pia ni Dhambi kwa Mwenyezi Mungu kwani hakuna maandiko yanazuia watu kushiriki katika ibada.

  Mnamo Mwaka Mwaka 2016 baada ya kura ya marejeo kikundo Cha watu wachache katika baadhi ya maeneo walianza kuwashawishi Wananchi kususia kuswali na Wanachama wanaotokana na CCM ambapo kwa kiasi kikubwa waliwaunga mkono Jambo lililopelekea waumini was kiislamu watokanao na CCM kuanza kusali majumbani mwao.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka akizungumzia kadhia ya kuzuiwa kuswali waumini wa dini ya kiislamu ambao ni wanachama cha chama cha mapinduzi ccm. (Picha Na Fahad Siraj)
  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka akisikiliza taarifa ya kadhia ya kuzuiwa kuswali waumini wa dini ya kiislamu ambao ni wanachama cha chama cha mapinduzi ccm. (Picha Na Fahad Siraj)
   Wanachama wakimlaki Kaimu katibu mkuu mara baada ya kuwasili kuzungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.


  0 0

  Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) limewataja wachezaji 24 wakiume watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa FIFA na wachezi 10 kwa upande wa soka la wakike, huku zoezi hilo likiendeshwa na Makocha wa timu za mataifa mbalimbali Duniani, Manahodha, Waandishi wa habari pamoja na Washabiki wa soka. Zoezi la kupiga kura ili kumpata mwanandinga huyo bora wa FIFA linatarajiwa kuanza Jumatatu Agosti 21 na kufungwa Septemba 7, 2017.

  wachezaji 24 waliotajwa kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa FIFA 2017 kwa upande wa wanaume ni hawa hapa.


  Hawa ndiyo wachezaji 10 waliotajwa kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa FIFA 2017 kwa upande wa wanawake.


  0 0


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitambulishwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 37 wa SADC kwenye ukumbi wa OR Tambo mjini Pretoria, Afrika ya Kusini. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.
   Rais wa Zambia Mhe. Edgar Lungu akiwashukuru washiriki wa mkutano huo wakati wa Utambulisho kwenye ufunguzi wa mkutano wa 37 wa SADC kwenye ukumbi wa OR Tambo mjini Pretoria, Afrika ya Kusini.# Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais. 
  Mkutano huo wa 37  wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit),unawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Dkt John Pombe Magufuli.Katika mkutano huo Tanzania itakabidhi nafasi ya  Uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya.

  Double Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano huo Mfalme Mswati III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu katika Mkutano huu ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Kuelekea Ndanda Day kesho, Timu ya Soka ya Ndanda inatarajia kushuka dimbani kuumana na Kikosi cha Azam katika kuadhimisha siku hiyo kwenye Uwanja wa Chamazi, Jijini Dar es salaam.

  Mchezo huo utakaoanza sa 10 alasiri utatanguliwa na burudani mbalimbali ikiwemo muziki kutoka kwa wasanii wa bongo flava wenye asili ya Mkoani Mtwara.

  Akizungumza kuelekea maadhimisho ya siku hiyo, Afisa habari wa Ndanda Idrisa Bandari amesema kuwa katika siku ya kesho wataanza asubuhi kwa kwenda kutoa huduma za kijamii hospitali ya Temeke wodi ya wazazi na kisha kufuatiwa na burudani kutoka kwa wasanii wa muziki wa bongo Flava.
  Bandari amesema, wasanii hao Wenye asili ya mkoani Mtwara Jay Mo, Amini, TID, Msaga Sumu na Juma Nature anayetokea Mkoa wa Pwani ambapo watatanguliza shughuli hiyo inayofanyika kwa mara ya nne ambapo mwaka huu itakuwa Mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni mara ya kwanza.

  Kwa upande wa Mshauri Masoko wa Ndanda, Peter Simon amesema kuwa kwa mwaka huu Ndanda Day itafanyika mara mbili kwani wameamua kuifanya na Dar es salaam kwani wanaamini kuna mashabiki wengi sana ndani ya Mkoa huu pia ili kuwapa fursa mashabiki wao kuiona Ndanda mpya iliyo chini ya Kocha Ramadhan Nsanzalwino mwenye asilia ya Burundi.

  Meneja Mkuu wa Masoko wa Mitsun Group ambao ni wadhamini wa Ndanda, Erhad Mlyansi amewaahidi uongozi wa Ndanda kuwapatia bidhaa kutoka kampuni yao ya Sayona kwa ajili ya kuwapelea wagonjwa siku ya kesho.
  Nao Wasanii wamewataka mashabiki wa Ndanda kujitokeza kwa wingi siku ya kesho kwa ajili ya kuishuhudia timu yaon na kwa mwaka huu wanaamini kutokana na udhamini walioupata basi timu yao ya Mkoani Mtwara itafanya vizuri huku wakiahidi kutoa burudani ya kutosha.
  Afisa habari wa Ndanda, Idrisa Bandari akizungumza na wanahabari kuelekea Ndanda Day itakayoadhimishwa kesho katika Uwanja wa Chamazi wakicheza na timu ya Azam Fc ikiwa ni mara ya nne kufanyika kwa Tamasha hilo na likisindikizwa na burudani kutoka kwa wasanii wa Bongo Flava wenye Asili ya Mkoani Mtwara pamoja na kutoa huduma za kijamii katika Wodi ya wazazi Hospital ya Temeke. Kushoto ni mshauri wa Masoko wa Ndanda Peter Simon akifuatiwa na wasanii wa Bongo Flava Jay Mo, Richie One na Amini.
  Meneja Mkuu wa Masoko wa Mitsuni Group,Erhard Mlyansi amewaahidi Ndanda kuwapatia bidhaa zinazopatikana kutoka kampuni ya Sayona kwa ajili ya kuwapelekea wakinamama kwenye Wodi ya wazazi Temeke Hospital siku ya Kesho

  Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Khaleed maarufu kama Top In Dar 'TID' akihamasisha mashabiki wa wana Mtwara kujitokeza kwa wingi siku ya kesho Kuadhimisha Ndanda Day akiwa sambamba na wasanii wenzake Jay Mo, Richie One na Amini.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka watoa  huduma za afya katika kituo cha afya cha Matei wilayani Kalambo kutoa huduma bora kwa wanawake wajawazito.

  Rai hiyo imetolewa jana na Waziri huyo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi wilayani hapo na kutembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa sekta ya afya kujua changamoto zinazowakabili. Alisema wajawazito wanapaswa kupata huduma bora kila wanapofika kliniki kila mwezi kwa kuangaliwa mfano dalili za kifafa cha mimba ,wigi wa proteini pamoja na viatarishi vingine  vinavyoweza kusababisha  uzazi pingamizi na hivyo kupelekea vifo kwa mama au mtoto wakatiwa kujifungua.

  “Nawapongeza sana kwa kutenga dirisha la wazee ila kusiwepo tu dirisha bali muwape dawa wazee wasio kuwa na uwezo,hivyo kama kuwakatia mfuko wa bima ya jamii (CHF)ni gharama basi wapatieni vitambulisho vya matibabu bure ili wazee wakija kwenye matibabu wasije na barua za watendaji wa vijiji”.

  Kwa upande wa madawa Waziri Ummy amewaambia watendaji hao hakuna masharti magumu ya ununuzi wa madawa na vifaa tiba kwa kutumia pesa za CHF“nimeshawaambia MSD ndani ya masaa ishirini na nne umeagiza vitu MSD hana,ndani ya masaa hayo kama hana unaruhusiwa kwenda kununua unapotaka kwenda”hivyo ni vyema wakapitisha wadhaburi watakaokuwa wananunua.

  “Tangu serikali hii iingie madarakani imefanya mabadiliko makubwa katika upatikanaji wa dawa kwa kuongezwa bajeti ya dawa kwa asilimia kubwa,hizi changamoto ndogondogo zipo ila mwisho wa siku wananchi wanahitaji dawa,hivyo kuhakikisha dawa zile muhimu zinapatikana wakati wote.

  Hata hivyo amewataka kuwapa kipaumbele wale wanaotumia bima ya afya,nataka kuona mnaongeza wananchi watakaotumia bima ya afya kwenye matibabu ili kuweza kutatua changamoto za sekta ya afya.

  Upande wa Malaria Waziri Ummy vipimo vya haraka vya malaria vya MRTD ni bure pamoja na dawa ya kutibu Malaria’ALU’ ni bure”asije kuwaambia mtu kipimo hicho utoe pesa,sindano kama mtu amezidiwa na maralia kali ni bure”alisisitiza Waziri Ummy. Akiongelea ugonjwa wa Kifua Kikuu”TB” Waziri huyo alisema ni wakati wa kuwaambiwa watu Tb inatibika kwani katika kila watu mia moja wanaoumwa kifua kikuu na kutumia dawa watu tisini wanapona kabisa na wanaendelea na shughuli zao.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya akina mama waliofika kupata huduma kwenye kituo hicho cha afya.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimjulia hali mama aliyejifungua kwenye wodi ya wazazi kituoni hapo.
  Msafara huo wakiangalia jengo la maabara(halipo pichani) wakati wa ukaguzi wa majengo yaliyopo kituo cha afya Matai Kushoto ni waziri Ummy Mwalimu,katikati ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt.Boniface Kasulu na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Julieth Binyura.
  Baadhi ya Watumishi wa Kituo cha afya cha Matai wakimsikiliza Waziri huyo wakati aluipofanya ziara kwenye kituo cha afya kwa ajili ya kujione hali ya utoaji huduma za afya Mkoani Rukwa

  0 0

   Lori la Mafuta likiwa limepinduka mara baada ya kuacha barabara ya Morogoro na kuanguka pembeni katika eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam leo
  Lori  la Mafuta likiwa limepinduka mara baada ya kuacha barabara na kuanguka pembeni katika eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam

  0 0

  Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Ambros Nchimbi'
    Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma, limeazimia kumrejesha kazini mhandisi wa halmashauri hiyo na kumlipa nusu mshahara kwa kipindi cha mwaka mmoja mhandisi VIVIAN MNDOLWA.

  0 0

  Wanafunzi wa wili wa shule ya msingi Chimoko Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na na ukuta wa shimo la mchanga walipokuwa wakichimba,

  0 0

   Meneja mkuu wa Redio ya Efm Ndugu, Denis Busulwa akiwapa vipande wapinzani wake katika mtanange kati ya timu ya E.Fm Redio na timu ya Viongozi wa Serikali katika mchezo ulio chezwa hii leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini mbeya ambapo Timu Ya EFm iliongoza kwa kuibugiza Timu ya Viongozi wa Serikali Gori 6-1.

  Efm redio 103.3 imekuja Mbeya rasmi, ambapo kwa wiki  nzima imekua ikitoa mafuta ya LAKE OIL kwa vyombo vya moto wenye  stika ya 103.3 Efm Mbeya.kila pikipiki, bajaji na magari iliwekewa mafuta full tank. ikiwa ni Shamra shamra za ujio wa kituo hicho cha redio kuingia rasmi na kusikika kwa kishindo mkoani mbeya kupitia mawimbi ya 103.3 fM.
   Kutoka kulia ni Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya Mohamed Mpinga akizungumza jambo kwa wachezaji wa Timu ya Efm Redio Pamoja na Timu ya Viongozi wa serikali hawapo pichani kabla ya mchezo kuanza.

  Kutoka kushoto ni  Meneja mkuu wa Redio ya E.fm Ndugu, Denis Busulwa akipokea zawadi ya Tsheti kutoka kwa wadau na wasikilizaji wa 103.3 Efm Redio Mbeya
  Vile vile siku ya Leo kulikua na jogging club asubuhi na wakazi wa Mbeya kwa lengo la kuhamasisha mazoezi kwa wakazi wa mbeya ili kujijenga kimwili na kiafya kama ambavyo Efm Redio imekuwa ikifanya mazoezi hayo kila siku jijini Dar es salaam.
  madereva wa pikipiki wakisubiri zawadi ya mafuta kutoka Efm redio 103.3 , ambapo kwa wiki  nzima imekua ikitoa mafuta ya LAKE OIL kwa vyombo vya moto vilivyoweka stika ya 103.3 Efm Mbeya. Kila pikipiki na bajaj iliopata fursa hiyo iliwekewa mafuta full tank. 
  PICHA NA MR.PENGO - MBEYA.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0


  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
  Kampuni ya vifaa nishati jadidifu vya Jua ya M-Kopa imefunga vifaa vya Umeme jua katika Shule ya Sekondari  ya Mwinyi iliyoko Mkuranga mkoa wa Pwani vyenye thamani ya shilingi Tshs 4,959,000.
  Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Meneja Msaidizi wa kampuni ya M-Kopa Nchini, June Muli amesema kuwa wameameamua kutoa msaada huo ka sehemu yao ya kurudisha wanachokipata kwa jamii hivyo waliona matatizo ya shule zisizokuwa na Umeme.
  "Kuna Changamoto kubwa sana ya kusoma katika shule amabzo azina umeme hali inayofanya wanafunzi wanaochukua masomo ya Sayansi kushindwa kuifunza vizuri katika maabara zao na hata wakati wa usiku kuhsindwa kujisomea hivyo sisi kama M-Kopa tumeweza kuchangia upatikanaji wa vifaa hivi mpka kuahakisha umeme unawaka shuileni hapa tunamini sasa vijana wetu wataweza kujifunza na kufaulu vizuri"amesema June Muli.
  ameongeza kuwa katika tafiti yao kwa wazazi wamebaini kuwa asilimia 92% ya watoto wanaosoma katika shule zenye umeme ufanya vizuri Darasani kuliko wale wanaosoma kwenye giza.
  kwa upande wake Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwinyi ,Martin Chuwa amewashukuru kampuni hiyo kwa kuweza kutoa Msaada huo ambao utasaidia kuinua taaluma ya shule hivyo na kusema kuwa anawashukuru kwa kuchagua shule hiyo kuwa ya kwanza kufikiwa na mradi huo ambao unalengo la kuboresha elimu nchini  
   Meneja Msaidizi wa M-Kopa nchini  June Muli akikabidhi boksi la Vifaa vya umeme wa jua kma ishara ya makabidhiano ya mradi wa umeme uliojengwa katika shule ya Sekondari ya Mwinyi Mkuranga mkoa wa Pwani kwa kamati ya shule iliyoongozwa na Mwalimu Mkuu Martin Chuwa Mtendaji kata .Juma Difa na Afisa Elimu Iddi Mdoe
   Meneja Msaidizi wa M-Kopa nchini , June Muli akikabidhi zawadi kwa Mtendaji kata Juma Difa mara baada ya kukabidhi mradi wa Umeme jua katika shule ya Sekondari ya Mwinyi

  0 0

  DSC_9106
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akifungua pazia kufungua  Tawi la CCM Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo.
  DSC_9278
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)alipokuwa akipokea risala ya Tawi la CCM Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Abdalla (Mabodi) baada ya kulifungua rasmi Tawi hilo akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,[Picha na Ikulu.] 19/08/2017. 
  DSC_9407
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)alipokuwa akizungumza na Viongozi mbali mbali na Wananchi wa Chama cha Mapinduzi wakati wa ufunguzi wa Tawi la CCM Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo  akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo.
  DSC_9686
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)alipokuwa akiwasalimia Watoto wa maeneo ya Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo baada ya kumalizika shamra shamra za ufunguzi wa Tawi la CCM  la Muembe Matarumbeta  akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo.
  DSC_9691
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)alipokuwa akiwapungia mkono wanachama wa CCM na Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika ufunguzi wa Tawi la CCM la Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo baada ya kumalizika kwa shamra shamra za ufunguzi wa Tawi la hilo  akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,[Picha na Ikulu.] 19/08/2017. 


  0 0
 • 08/19/17--12:03: MZEE MAJUTO NA MKWEWE


older | 1 | .... | 1868 | 1869 | (Page 1870) | 1871 | 1872 | .... | 3353 | newer