Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1864 | 1865 | (Page 1866) | 1867 | 1868 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Vero Ignatus, Arusha. 

  Mwanamke mmoja mkazi wa Levolosi Arusha bi Rehema Juma Kishena (40) anawaomba watanzania wenye mapenzi mema kumsaidia kupata fedha ya matibabu kutokana na tatizo la uvimbe linalomsumbua katika shavu lake la kulia ambalo limezunguka taktibani robo tatu ya uso wake . 

  Mwanamke huyo ambae ni mama wa watoto (4) amesema kuwa tatizo hilo lilimuanza kwa jino kuumua ,akachukua hatua ya kwenda hospitalini kuling’oa , mwaka 2001 uvimbe ulijitokeza katika jino alilong’olewa, na kupelekea kufanyiwa upasuaji, baada ya miaka mitatu uvimbe ulirudi tena kama awali. ‘’Jino lilikuwa linaniuma nikaenda hospitalini kuling’oa, ndipo ukaanza uvimbe kwenye jino nililongoa nikarudi hospitalini wakaniambia nifanyiwe upasuaji ili kuondoa uvimbe ,baada ya miaka mitatu tatizo hilo likajirudia kama lilivyokuwa mwanzo “alisema Bi. Rehema.

  Amesema kuwa kwa sasa hana msaada wowote kwani wazazi wake ni wazee, hawana mwezo wa kumsaidia,yeye mwenyewe hana mume kwani alimkimbia wati alipoona tatizo linaendelea kuwa kubwa. “Nawaombeni msaada ili niweze kujitibu kwani hali yangu kama mnavyoiona nipo kwa dada yangu hapa ,sina msaada wowote” alisema Bi. Rehema. 

  Kwa upande wake dada yake ( Rehema )Aziza Bakari Muyai amewaomba watanzania kushirikiana nae katika kumsaidia mdogo wake ili aweze kupatiwa matibabu kwani hali yake inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyozidi kwenda. Ameomba kwa yeyote aliyepo tayari kumsaidia atumie mawasiliano kwa namba 0653179373.
   Bi. Rehema Juma Kishena akiwa na mtoto wake Sophia Dastan Mandia pamoja na dada yake bi Aziza Bakari Muyai nyumbani kwake Levolosi Mkoani Arusha. 


  0 0

  NA RAMADHANI JUMA.

  HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma imetenga eneo la Makole D-Center lililoko katikati ya Mji wa Dodoma kuwa eneo rasmi kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo maarufu kama Machinga kufanya biashara zao badala ya kupaga bidhaa ovyo mitaani hali inayopelekea kuharibu taswira ya mji.

  Hatua hiyo pia itasaidia kuendana na kasi kubwa ya ongezeko la wafanyabiashara hao kuingia Mjini humo kutoka mikoa mbalimbali nchini tangu Serikali ilipohamia rasmi Dodoma ambako ni Makao Makuu ya Nchi.

  Akizugumza katika mkutano wa Baraza la Madiwani la kufunga wa fedha uliopita lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita  katika ukumbi wa Manispaa hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin aliyewajulisha wajumbe na wananchi kuwa, sasa Manispaa iko katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa  miundombinu muhimu katika eneo hilo ikiwemo vyoo ili shughuli za biashara zifanyike katika mazingira salama na rafiki.

  “Tunatarajia eneo hilo litakuwa tayari kufikia mwisho wa mwezi Agosti au mwanzo wa mwezi Septemba mwaka huu mara moja tutaanza zoezi la kuwahamishia wafanyabiashara hao pale” alifafanua.

  Alisema Manispaa inashirikiana kwa karibu na viongozi wa wafanyabiashara hao katika zoezi hilo, na kwamba endapo eneo hilo halitatosha, wafanyabiashara wengine watahamishiwa katika eneo la Chaduru .

  Tayari Manispaa ya Dodoma ilishaanza zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wa Matunda na chakula katika maeneo yasiyo rasmi na kuwahamishia katika maeneo rasmi ya masoko ikiwemo soko la Sabasaba, Bonanza, na Tambukareli. 
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi akizugumza na wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani la kufunga mwaka wa fedha 2016/2017 uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Manispaa ya Dodoma. PICHA NA RAMADHANI JUMA.

  0 0

  KAMPENI ya kuhakikisha vijiji vyote nchini vinapatiwa umeme, imeendelea jana (Agosti 16, 2017), mkoani Ruvuma, ambapo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, amezindua mradi huo kwenye kijiji cha Litapaswi, wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma, kwa kugawa vifaa vijulikanavyo kama umeme tayari (Ready Board) kwa wanakijiji.

  Katika hafla ya uzinduzi huo, uliofanywa kwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu), Mheshimiwa Jenista Mhagama, Wanakijiji walipatiwa vifaa hivyo vinavyowezesha umeme kuwaka mara moja bila ya kuhitaji (mtandao wa waya kwenye nyumba- (Wiring).

  “Kifaa hiki ni maalum kwa matumizi ya nyumba isiyozidi vyumba viwili na mwanakijiji analipia shilingi elfu 36,000 tu kupata kifaa hiki.” Amefafanua Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji ambaye anafuatana na Naibu Waziri kwenye ziara hiyo.

  Hali kadhalika alisema, kifaa hicho kwa sasa kinapatikana kwenye ofisi zote za TANESCO za Mikoa na Wilaya kwenye mikoa ambayop tayari mradi huo umezinduliwa.Alisema, tayari Naibu Waziri amekwishazindua mradi kama huo kwenye mikoa yote ya Tanzania bara isipokuwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, na Katavi.

  “Jambo la kufurahisha sana ni kwamba mradi huu wa REA III, unafadhiliwa na Serikali yetu kupitia Wakala wa Nishati Vijijini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)” alifafanua Bi. Muhaji.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe.Jenista Mhagama, akikabidhi kifaa kijulikanacho kama umeme tayari(Ready Board) kikichobuniwa na Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kwa mwanakijiji wa kijiji cha Litapwasi, Peramiho, Mkoani Ruvuma wakati wa uzinduzi wa mradi wa Usambazaji umeme vijijini unaoratibiwa kwa pamoja na Wakala wa Umeme Vijijini REA na Shirika la Umeem Tanzania , (TANESCO), ambapo uzinduzi huo ni awamu ya tatu. Uzinduzi huo ni mwendelezo wa kazi kama hiyo ulioanzishwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medad Kalemani(aliyeshika vipaaza sauti) kwenye mikoa mbalimbali nchini.  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA MALIASILI NA UTALII


  TAARIFA KWA UMMA


  Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngorongoro, kwa kushirikisha Hifadhi ya Taifa Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, inaendesha zoezi la kuondoa mifugo na makazi ndani ya hifadhi ya Taifa Serengeti na kwenye mpaka wa Pori Tengefu Loliondo.

  Zoezi hilo lililoanza tarehe 10  Agosti 2017  litadumu kwa siku kumi na nne na linashirikisha Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ngorongoro, Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa Serengeti na Hifadhi ya eneo la Ngorongoro.


  Zoezi hilo linalenga kunusuru uhifadhi ndani ya hifadhi, ndani ya Pori Tengefu Loliondo, na ndani ya mfumo ikolojia wa Serengeti na pia kunusuru utalii katika mfumo ikolojia huo.


  Aidha, hatua hii ya kuondoa makazi na mifugo kutoka katika maeneo ya mipaka ya Pori Tengefu Loliondo kutaongeza uhakika wa kupatikana malisho ya mifugo wakati wa kiangazi kwa kuwa hakutakuwepo na makazi ndani ya Hifadhi na ufugaji holela.


  kimsingi zoezi hili linaendana na wito wa Serikali wa kuondoa mifugo ndani ya maeneo yote yaliyohifadhiwa nchini.


  Katika kutekeleza zoezi hili, Mkuu wa Wilaya  Ngorongoro, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ngorongoro Bwana Rashidi Taka, alitoa maelekezo yafuatayo:  0 0

  tzNOG is a multi-stakeholder project that aims at providing affordable capacity building platform to ICT Professionals in Tanzania. Its organizing committee comprises of members from Tanzania Network Information Centre (tzNIC), Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), Tanzania Internet Service Providers Association (TISPA) and Tanzania Educational and Research Network (TERNET).

  After 4 successful trainings in Arusha (tzNOG1-2013), Mwanza (tzNOG2-2014), Zanzibar (tzNOG3-2015) and Dar es Salaam (tzNOG4-2016), the 5th edition of tzNOG training is scheduled to take place in Dodoma from 3rd to 8th September 2017 at St. Gaspar Hotel.

  The tzNOG5 training will have  2 parallel tracks/sessions, all covering IPv6 basics and configuration concepts:
  1. Scalable Internet Services (SIS) – This track focuses on the design and operation of email, web and other Internet services, in ways that can scale to handle large numbers of end users ;
  2. Systems Network Security (SNS) – This track focuses on security from the network perspective (ingress, egress filters, defeating denial of service attacks, network intrusion detection and network traffic) as well as from the server side (proper admin procedures, firewalls, secure services, etc).
        
  Application requirements
  Application is open to all Technical personnel with the following qualifications:
  i) Linux/UNIX  OS experience;
  ii) Knowledge of TCP/IP protocols and layer 2 & 3 network basics.
  Registration link:
  Participation fee:
  TZS 300,000/= (if you pay before 25thAugust 2017); TZS 350,000/= (if you pay between 25thAugust - 02nd September 2017). Onsite registration is discouraged and will be charged TZS 400,000/=.

  Women are encouraged to apply

  For more  details and registration kindly visit www.tznog.or.tz

  Issued by:
  tzNOG Secretariat

  Phone: +255 22 277 2659


  0 0

  Barabara ya lami ya Kia-Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambayo imeshakabidhiwa kwa Serikali, inaendelea kuwa kwenye kipindi cha matazamio kwa muda wa mwaka mmoja. 

  Mradi huo wa barabara uliokabidhiwa serikali Mei 31 mwaka huu, mkandarasi wake anaendelea na kazi ndogo ndogo za ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua, vivuko na vituo vya basi hasa eneo la Kairo. 

  Meneja wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) mkoa wa Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa aliyasema hayo wakati akisoma taarifa ya mradi huo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi) mhandisi Joseph Nyamhanga alipotembelea eneo hilo. 

  Mhandisi Rwesingisa alisema barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 27 iliyojengwa na kampuni ya China Henan International Cooperation Group (Chico) kwa gharama ya sh32.2 milioni, chini ya usimamizi wa ujenzi mhandisi mshauri M/s LEA International Ltd ya India kwa ushirikiano na kampuni ya DOCH Tanzania Ltd. 

  Alisema kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa kiwango cha lami urefu wa kilometa 27 ikijumuisha Kia hadi Mirerani, Mirerani hadi eneo la uwekezaji la (EPZ), barabara ielekeayo Arusha inayopitia Mbuguni, barabara ya kuingia na kutoka kituo cha mabasi Mirerani na mzunguko kiwanda cha TanzaniteOne. 

  "Ujenzi wa barabara hii umehusisha pia kujenga mifereji ya pembezoni mwa barabara kwenye maeneo ya mji, sehemu za kuvuka mifugo na sehemu za kuvushia huduma muhimu kama waya za simu na umeme," alisema mhandisi Rwesingisa.

  Alisema mradi huo umekuwa na changamoto za migomo ya wafanyakazi, wananchi kugoma kuondoa mali zao ndani ya hifadhi ya barabara. 

  Alisema mipango ya baadaye ni kujenga kilometa 114 barabara kwa kiwango cha lami itakayounganisha eneo la EPZ na mji mdogo wa Orkesumet, makao makuu ya wilaya ya Simanjiro, kama ilivyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015. 

  Akizungumza baada ya kukagua mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia ujenzi, mhandisi Joseph Nyamhanga alipongeza jitihada zilizofanyika kwa pande zote hadi barabara hiyo ikamalizika. 

  Mhandisi Nyamhanga alisema wakati wanasubiri barabara hiyo kuzinduliwa wakati inaendelea kutumika, watumiaji wanapaswa kufuata masharti ya matumizi ya barabara hiyo ili waitunze. 

  Aliitaka jamii ya eneo hilo ambao kwa muda mrefu walikuwa wanalilia utengenezwaji wa barabara na ndiyo wanufaika wa mradi huo, kuutunza vizuri kwani ni kwa ajili ya faida yao na vizazi vijavyo. 
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi) mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati) akizungumza na viongozi wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) Mkoa wa Manyara, alipotembelea eneo la mji mdogo wa Mirerani, (kushoto) ni meneja wa Tanroads Mkoani Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa

  Meneja wa Tanroads Mkoa wa Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa (aliyevaa shati la maua) akimwelezea Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi) Joseph Nyamhanga (kushoto kwake) juu ya barabara ya lami ya Kia - Mirerani, ambayo imemalizika inasubiri kufunguliwa.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho na Bushiri 
  Matenda - MAELEZO.

  Serikali imewapiga marufuku mawakala wa forodha wanaogushi nyaraka kwa ajili ya kuingiza kemikali kwani ni kinyume cha Sheria na pia wanaipotezea Serikali mapato. 

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Prof. Samwel Manyele alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uingizaji wa kemikali nchini kutoka nje ya nchi.

  Prof. Manyele amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Kemikali nchini kila anayeingiza kemikali anatakiwa awe amesajiliwa na kupewa hati ya usajili huo vile vile anatakiwa kupata idhini ya wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kabla ya kuagiza mzigo wa kemikali nchini.

  “Natoa onyo kwa mawakala wote wa forodha wasiofuata taratibu zilizowekwa na Serikali hasa wanaogushi nyaraka zenye lengo la kukwepesha Sheria na kukwepa kulipa kodi na tozo mbalimbali za Serikali hivyo watakaokaidi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” alisema Prof. Manyele.


  0 0

   Mshindi wa Jackpot ya Tatu Mzuka iliyofanyika Jumapili hii Bi Ruth Rodgers Maeda akikabidhiwa hundi ya shilingi Milioni 20 aliyojishindia kutoka kwa balozi wa Mchezo wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein. Mchezo wa Tatu Mzuka umefanikiwa kujizoelea umaarufu kwa kutoa washindi kila saa. Jackpot hiyo inaendelea jumapili hii kwa mshindi kujishindia shilingi milioni 80.
  Mshindi wa Jackpot ya Tatu Mzuka iliyofanyika Jumapili hii Bi Ruth Rodgers Maeda (wa pili kutoa kulia) akishangilia pamoja na familia yake ushindi wake wa zawadi ya shilingi Milioni 20. Mchezo wa Tatu Mzuka umefanikiwa kujizoelea umaarufu kwa kutoa washindi kila saa. Jackpot hiyo inaendelea jumapili hii kwa mshindi kujishindia shilingi milioni 80.

  0 0

   Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
  MAPEMA hii leo, upande wa Mashtaka katika kesi inayomkabili raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61), umeileza mahakama kuwa, mshtakiwa huyo hana uhalali wa kuishi nchini ingawa imethibitika kuwa ni kweli ana makazi eneo la mbezi jiji Dar es Salaam.

  Wakili wa Serikali Nassoro Katuga amesema hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akiwasilisha ripoti ya ya mahakama iliyowaagiza kwenda kukagua makazi ya mshtakiwa pamoja na hati ya mshtakiwa.

  Amesema, kamishna wa Uhamiaji nchini amethibitisha kuwa Tsampos, hana uhalali wa kuishi nchini ila Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi amethibitisha kuwa, mshtakiwa huyo ni kweli anayo makazi ya kuishi eneo hilo.

  Hata hivyo, wakili wa utetezi, Jebra Kambole, ameomba mahakama kumpatia dhamana mshtakiwa huyo kwani imedhihirisha kuwa ni kweli mshtakiwa anaishi Mbezi na pia Kamishna wa Uhamiaji hajaeleza ni kwa nini hana uhalali wa kuishi hapa nchini.

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho kwa ajili ya kutolewa uamuzi kama apatiwe dhamana au la.

  Raia huyo wa Afrika Kusini, anakabiliwa na mashtaka ya kutishia kwa mtandao, kuishi nchini kwa muda wa miaka minne bila kibali na kutumia paspoti yenye visa ya kugushi.
   Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61) aliyekuwa anashikiliwa kwa makosa manne leo tena amesomewa mashtaka katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu, mashtaka yake ikiwemo kuishi nchini bila kibali.  Leo pia  imethibitishwa kuwa Visa yake ya kusafiria si halali na hana uhalali wa kuishi hapa nchini.

   Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61)akiwa amejificha sura yake katika mahakama ya Kisutu jijini  Dar es Salaam.

  0 0


  Mhe. Prof. Elizabeth K. KIONDO, Balozi wa Kwanza Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uturuki Jumatano ya tarehe 16 Agosti 2017, amewasilisha Hati zake za Utambulisho pamoja na zile za Kukoma kwa Muda wa Mtangulizi wake kwa Mheshimiwa Recep Tayyip Erdoǧan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki. Kitendo hicho kinamfanya Mhe. Kiondo kuwa Balozi wa kwanza mkaazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini humo.

  Katika hafla hiyo Mhe. Balozi Kiondo alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Rais Erdoǧan kuhusu namna ya kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili katika maeneo ya uwekezaji, biashara, afya, Elimu, na mengineyo. Aidha, Mhe. Balozi Kiondo alimfahamisha Mheshimiwa Rais Erdoǧan kuwa Ubalozi utakuwa kiungo muhimu katika kuongeza kasi ya utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa wakati wa ziara yake nchini Tanzania mwezi Januari 2017 ambapo mikataba na makubaliano yapatayo tisa yalisainiwa.

  Kufunguliwa kwa Ubalozi mpya wa Tanzania nchini Uturuki na kuanza kufanya kazi kunatoa fursa muhimu kwa wananchi wa mataifa hayo mawili kuongeza shughuli za kiuchumi hususan biashara kwa manufaa ya pande zote mbili.

  Mhe. Balozi anatoa rai kwa Watanzania kujipanga vizuri na kuchangamkia fursa mbalimbali hususan za kibiashara zinazotokana na kuendelea kuimarika kwa mahusiano kati ya Tanzania na uturuki.

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Dar es Salaam, 17 Agosti 2017.

  Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo, Balozi Mteule wa Tanzania nchini Uturuki akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mheshimiwa Recep Tayyip Erdoǧan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki. 
  Mhe. Balozi Kiondo akiagana na Mheshimiwa Rais Erdoǧan, baada ya kufanya mazungumzo kuhusu mahusiano ya Tanzania na Uturuki. 
  Picha ya pamoja.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Balozi wa Korea Kusini Song, Geum Young wakati wa siku maalum ya kuadhimisha urafiki kati ya Tanzania na nchi ya Korea kusini ambapo Balozi huyo amekubali kusaidia kufunga kamera maalum za kufuatilia wahalifu-CCTV katika jiji la Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Polisi)
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Korea Kusini Song, Geum Young (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na maofisa wengine wakati wa siku maalum ya kuadhimisha urafiki kati ya Tanzania na nchi ya Korea kusini ambapo Balozi huyo amekubali kusaidia kufunga kamera maalum za kufuatilia wahalifu-CCTV katika jiji la Dar es Salaam.
  Kamishna wa Polisi, Oparesheni na Mafunzo Nsato Marijani akizungumza na Askari Polisi wanaokwenda kwenye Operesheni ya ulinzi wa amani Darfur Sudan wakati wa zoezi la kuwakabidhi bendera ya taifa ambapo jumla ya Askari 24 wanatarajia kuondoka hivi karibuni.
  Kamishna wa Polisi, Oparesheni na Mafunzo Nsato Marijani akiwakabidhi bendera  ya taifa Askari Polisi wanaokwenda kwenye Operesheni ya ulinzi wa amani Darfur Sudan ambapo jumla ya Askari 24 wanatarajia kuondoka hivi karibuni.

  0 0


  Shamba la miti Sao Hill likishirikiana na Kampuni ya Art International limeanza utafiti wa kugema utomvu wa miti ya Misindano kama njia ya kujiongezea kipato kutokana utomvu huo kuuzwa kwa sh. 750 kwa kilo. 

  Akizungumza na kamati ya Bunge ya Maliasili na Mabadiliko ya Tabia Nchi ya Malawi,Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill, Salehe Beleko  amesema katika kuongeza vyanzo vya Mapato wameingia mkataba na kampuni hiyo kufanya utafiti ni ikibainika kwamba haitaathiri Ukuaji wala Ubora wa miti wataidhinisha kuwa chanzo kipya cha mapato. 

  Beleko amesema kwa kuwa ni utafitiwameanza kwanza na kwa miti iliyokuwa tayari kuvunwa wakiona hakuna Madhara wataendelea kwenye Miti michache yenye umri mdogo na matokeo ya utafiti huo yatapelekea ama kukuza ama kukataza kabisa zoezi hilo. 

  Naye Mtaalam wa Kampuni ya China amesema Taasisi yake imefuata taratibu zote za ugemaji na usafirishaji wa utomvu huo na amefafanua kwamba kampuni yake inahitaji Miti Milioni 2 kwa mwaka ili kupata ujazo wa Utomvu wanaouhitaji. 

  Akijibu swali la Mke wa Rais wa Zamani Bi Patricia Muluzi ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ambaye alitaka kujua matumizi ya Utomvu huo Mtaalam huyo amesema Baada ya kuchakatwa na kuchanganywa na kemikali mbalimbali utomvu huo hutumika kutengeneza dawa mbali mbali Bazoka (chewing gum), pamoja na Gel. 

   Rashid Pemba Msusa, mjumbe wa Kamati hiyo amesema kwa Mara ya kwanza wameshuhudia matumizi mapya kabisa ya zao la mti Teknolojia ambayo hawajawahi kuiona nchini kwao Malawi. Hata hivyo ameahidi kufuatilia matokeo ya utafiti huo ili ukifaa wauhamishie Malawi.

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana (pichani) amewataka watumishi wa umma kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma na kujiepusha na vitendo vya rushwa kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

  Akizungumza katika mahojiano maalum hivi karibuni, Dkt. Bwana amesema Tume katika kutekeleza majukumu yake ya msingi ya ukaguzi wa rasilimali watu na kushughulikia rufaa na malalamiko, imebaini kuwepo kwa ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu miongoni mwa Watumishi wa umma, Waajiri, Mamlaka za Ajira na Nidhamu.

  Amesema kuwa baadhi ya Watendaji Wakuu wanashindwa kuwachukulia hatua kwa mujibu wa Sheria, watumishi wenye utendaji usioridhisha na wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma walio chini yao. Tatizo hili lipo zaidi kwa baadhi ya Halmashauri zetu na Taasisi za Umma.

  “Kumekuwa na udhaifu mkubwa kwa baadhi ya Watendaji Wakuu ambao wameshindwa kuchukua hatua za nidhamu mapema dhidi ya watumishi walio chini yao. Utakuta mtumishi anatoweka tu kazini bila kutoa taarifa wala kuomba ruhusa! Mtumishi kutokuwepo kazini kwa siku tano bila ruhusa wala sababu za msingi adhabu yake ni kufukuzwa kazi. Inashangaza kuona mtumishi wa umma hayupo katika kituo chake cha kazi kwa zaidi ya siku tano, siku 115 na Mwajiri wake hajui, wala hachukui hatua.” Amesema.

  Hata hivyo, Dkt. Bwana ameonyesha kutoridhishwa na hali ya utendaji kazi katika baadhi ya Halmashauri. Alisema, “Rufani nyingi tunazopata zinatoka huko, kuna haja ya kurekebisha mambo mengi sana hasa kwenye Halmashauri zetu, hakuko sawa kwa upande wa usimamizi wa Rasilimali watu. Kuna wizi kule, kuna matumizi mabaya ya fedha za umma na mali za Halmashauri.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Afrika ya Kusini tayari kwa kuhudhuria Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC unaoaanza tarehe 19 na 20 ambapo kesho tarehe 18 atahudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit).

  Mheshimiwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Waziri wa Mawasiliano wa Afrika Kusini Mhe. Ayanda Dlodlo.
  akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli.

  Akizungumza mara baada ya kuwasili kwa Makamu wa Rais, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augastine Mahiga amesema Mkutano huo utapokea na kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama; Hali ya Michango mbalimbali ya Nchi Wanachama na Kupokea taarifa ya Mwenyekiti anayeondoka wa SADC Organ.

  Pia Mkutano utapokea taarifa ya Katibu Mtendaji wa SADC; Kupitia hali ya kiuchumi katika Kanda ya SADC; Kuwasilisha Kaulimbiu ya Mkutano wa SADC; Taarifa kuhusu Mfuko wa Maendeleo wa SADC; Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Viwanda; Kuwezesha Chuo cha Elimu ya Sayansi na Teknolojia; Maombi ya Serikali ya Comoro na Serikali ya Burundi kujiunga na SADC; Utekelezaji wa Mabadiliko ya Kitaasisi ya Umoja wa Afrika na Mkutano wa Mshikamano kati ya SADC na Saharawi ya Magharibi.

  Dkt. Mahiga amesema katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit) Tanzania itakabidhi nafasi ya Uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya.

  Double Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano huo Mfalme Mswati III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu katika Mkutano huu ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.  0 0

  Meneja huduma za Ziada na Tehama wa Vodacom Tanzania,Mathew Kampambe(kushoto) na Msimamizi wa michezo ya kubahatisha nchini, Abdallah Hemed(kulia)wakionyeshwa na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu(katikati) namba ya simu ya mshindi aliejishindia Tsh. Laki 5/- Munira Jumanne Mkazi wa Singida wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya Tusua Mapene inayoendeshwa na kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam leo. Ili Mteja wa Vodacom aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu(kulia)akiongea kwa njia ya simu ya mkononi na mshindi aliejishindia Tsh. Laki 5/- Munira Jumanne Mkazi wa mkoa wa Singida wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya Tusua Mapene inayoendeshwa na kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo,Ili Mteja wa Vodacom aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.Anaeshuhudia kushoto ni Meneja huduma za Ziada na Tehama wa Vodacom Tanzania, Mathew Kampambe.
  Meneja huduma za Ziada na Tehama wa Vodacom Tanzania,Mathew Kampambe(kushoto) na Msimamizi wa michezo ya kubahatisha nchini,Abdallah Hemed(kulia)wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu(katikati)alipokuwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya Tusua Mapene inayoendeshwa na kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam leo ambapo mkazi wa mkoa wa singida Munira Jumanne alijishindia Tsh. Laki 5/- Ili Mteja wa Vodacom aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.

  Niwakati mwingine tena Vodacom Tanzania imewaletea wateja wake na watanzania wote kwa ujumla promosheni mpya kabambe kabisa inayojulikana kama Tusua Mapene. Promosheni hii itawawezesha wateja wetu na wananchi wote kwa wale ambao watajiunga na mtandao wetu kushiriki katika bahati nasibu na kujishindia vitita mbalimbali mpaka kiasi cha shilingi milioni 150 ndani ya siku 150.

  Promosheni hii inampa mteja wa vodacom fursa ya kushiriki kupitia ujumbe mfupi wa maneno, huduma ya M-pesa au mitandao ya kijamii.

  Vodacom itatoa mshindi mmoja wa Sh. 100M/-, washindi watano wa Sh. 20M/- na mshindi moja wa Sh. 15M/- KILA SIKU na mshindi wa mwisho wa promosheni(Grand draw) atajishindia kitita cha shilingi Million 150/-

  Jinsi yakushiriki katika promosheni hii ni rahisi sana mteja anachotakiwa kufanya ni kutuma neno “CHECK” au “VODA” kupitia ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu ikijumuisha kodi kwa kila ujumbe.

  0 0

  Na Agness Francis,Blogu ya jamii.

  Katika kuelekea Tanzania ya viwanda awamu ya tano ipo fursa ya kushirikiana na nchi mbali mbali ili  kuongeza wigo katika  uchumi wa viwanda nchini.

   Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira,  Antony Mavunde amesema hayo katika uzinduzi wa sita wa kokangamano  la  utafiti  barani Afrika(ARCA) kwa kushirikiana na chuo cha biashara (CBE),wakala wa vipimo (WMA) na shirika La viwango Tanzania (TBS)

  Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa  chuo cha biashara (CBE) katika kuelezea umuhimu wa tafiti hizo  na kuleta maendeleo zaidi ya kiuchumi nchini.

  Naibu Waziri Mavunde amesema kuwa serikali amewekeza fedha za kutosha  vyuoni ili kuweza kufanya utafiti na nchi mbalimbali  duniani, ili  kukuza uchumi wa viwanda na kuweza kutoa huduma bora na bidhaa bora hapa nchini.

  Awali Naibu Waziri Mavunde amesema  kuwa  kuwepo kwa ongezeko la viwanda nchini itasaidia kuondoa changamoto za ajira kwa vijana na kuongeza pato la  taifa nchini.

  Nae mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara  (CBE) Profesa Emanuel Mjema, amesema ili kuwa na mahusiano mazuri na mataifa mbalimbali lazima kuwepo na vigezo vya kupima viwango bora ili kuweza kujua takwimu sahihi  kuwa ni watu wangapi wamepata huduma.

  Hata hivyo  Mkuregenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Prof. Egid Mubofu amesema kuwa tunajivunia nchi yetu kwa kukidhi vigezo  vya TBS na viwango bora  kulingana na  viwango   vyote  duniani.
   Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde akifafanua jambo kwa watafiti mbalimbali barani Afrika wakati akifungua mkutano wa sita wa watafiti barani Afrika mapema hii jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde (katikati) akikata utepe kuzindua ripoti ya sita ya utafiti barani Afrika mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sayansi toka taasisi ya Applied Research Conference in Africa (ARCA) Prof. Joseph Mojekwu na kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Biashara Prof. Emanuel Mjema.
   Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde (katikati) akionesha ripoti ya sita ya utafiti barani Afrika mara baada ya kuizindua, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sayansi toka taasisi ya Applied Research Conference in Africa (ARCA)  Prof. Joseph Mojekwu na kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Biashara Prof. Emanuel Mjema.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezi, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wakazi wa na wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga kuanza mapema kuzitumia fursa zilizopo katika mkoa huo kabla ya wageni hawajazitu,ia na kuwaacha wenyeji kuwa watazamaji.

  Waziri Mwakyembe ametoa rai hiyo leo Jijini Tanga wakati akifungua kongamano la siku moja la Fursa za Biashara ambalo lina lengo la kufungua fursa za biashara zilizopo katika mkoa na hasa katika kipindi hiki ambacho ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani jijini Tanga unatarajiwa kuanza.

  “Tusipojipanga leo na kuzitumia vizuri hizi fursa nyingi zilizopo basi tujue fursa hizi zitatumiwa na wageni ili hali Watanzania tunaauwezo”, alisisitiza Waziri Mwakyembe.

  Alieleza kuwa kama kuna changamoto zozote zinazowakabili watu wa Tanga na Watanzania kwa ujumla katika kutumia fursa zilizopo basi ni vema Serikali ya Mkoa, wafanyabishara na wawekezaji waliopo mkoa wa Tanga wakazitafutia ufumbuzi changamoto hizo ili zigeuke kuwa fursa ili Watanzania wazichangamikie.

  Aidha Mwakyembe amewasisitiza Watanzania kuwekeza katika biashara ya huduma na viwanda vya uzalishaji bidhaana bidha ambapo vitakuwa vikihudumia ujenzi wa miradi mbalimbali hususani bomba la mafuta kutoka Hoima-Uganda hadi Chongoleani-Tanga, Tanzania.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongeza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela akitoa neon la utangulizi wakati wa ufunguzi wa ufunguzi wa Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga
  Mhariri Mtendaji wa Tanzania Standard Newspapers Dkt. Jim Yonaz akielezea kuhusu malengo ya kongamano la Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga.  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha 

  Wagombea wa nafasi mbalimbali za ungozi ndani ya chama cha mapinduzi wilaya wa Arusha wametakiwa kufuata kanuni na sheria za zilizowekwa na chama hicho.

  Hayo yamebainishwa na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Arusha Dr, Ramathani Dallo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na tuhuma za kuwepo na baadhi ya wagombea kuja kwenye usahili na watu wanaodaiwa sio wagombea bali ni waganga wa kienyeji

  Alisema kuwa ni muhimu sana wagombea wakifuata kanuni taratibu na sheria zilizowekwa katika uchaguzi kwa mujibu wa kanuni ya muongozo wa uchaguzi ya mwaka 2010.

  Alisema kuwa yeye binafsi hajawaona watu hao wanaodaiwa ni Waganga wa kienyeji na usahili ulienda vizuri katika kipindi hiki uchaguzi unaendelea vyema ,huku akibainisha kuwa iwapo kutakuwa na mgombea yeyote ambae atakwenda kinyume na sheria ya uchaguzi atamuaonea huruma bali atuakali zidi yake itachukuliwa .

  “Nasema kwakweli ili suala na mgombea wa UWT kuja na mganga wa kienyeji kwenye usaili sijaliona, ila ukweli napenda kuchukua nafasi hii kuwasihi iwapo tutamkamata mgombea yeyote yule anaekwenda kinyume na sheria tutamchukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuita kikao kama jambo ni gumu sana, pia itatulazimu tumkate jina lake na asiwepo kwenye kinyanganyiro chochote”alisema Dkt Dallo.

  Alizitaja baadhi ya kanuni kuwa ni pamoja na kutofanya kampeni ,kukusanya watu kufanya mikutano isioyo rasmi kichama pamoja na nyingi 
  Aidha akiongelea baadhi za uchaguzi zilizopita alisema kwa upande wa uchaguzi wa kata ,mitaaa umemalizika vizuri sasa ivi ndio wanaendelea na maeneo mengine yaliyobaki.

  Awali baadhi ya wagombea ambao hawakutaka majina yao yaandikwe walisema kuwa kuna mmoja wa mgombea mwenza sik u ya usahili alikuja akiwa na mganga wa kienyeji kitu ambacho ni kinyume na sheria ya uchaguzi

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Kujenga taifa, Meja jenerali, Michael Isamuhyo akizungumza wakati wa kumpongeza  Mshindi wa tatu wa Mbio za Dunia za London Marathon mwaka huu, Felix Simbu pamoja na wenzake watatu ambao walienda katika mashindano ya Dunia za London Marathon nchini Uingereza.
   Mwanariadha, Alphonce Simbu aliyeshinda medali ya shaba katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka huu 2017 akizungumza wakati wa Jeshi la kujenga taifa limewapongeza  washindi hao walipowasili hapa nchini tangu walipotoka kwenye mashindano ya Riadha ya Dunia yaliyofanyika nchini Uingereza. Amesema kuwa "Ushindi huu si wangu peke yangu bali ni wa wetu sote kutokana tulikuwa na umoja."Huu ni ushindi wa wote, hivyo umoja wetu utazidi kujitahidi kufanya vizuri zaidi hapo baadae,".
  Katibu Baraza la Michezo Tanzania(BMT), Mohamed Kiganja akizungumza wakati wa kuwapongeza washiriki wa mashindano ya Riadha ya Dunia ambapo Tanzania ilikuwa na wanariadha wanne na  Mshindi wa tatu wa Mbio hizo za Dunia za London Marathon kutoka Tanzania ni Alfonce Simbu.
   Mwakilishi wa Multchoice, akizungumza katika hafla fupi iliyoandali na Jeshi la Kujenga Taifa akiwapongeza washiriki wa Mashindano hapo ikiwa mshindi watatu wa mashindano ya riadha ya dunia aliibuka kidedea
  Alfonce Simbu.
   Mwanariadha, Alphonce Simbu aliyeshinda medali ya shaba katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka huu 2017 akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga taifa, Meja jenerali, Michael Isamuhyo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuwapongeza kushiriki mashindano ya Rianda ya Dunia.

older | 1 | .... | 1864 | 1865 | (Page 1866) | 1867 | 1868 | .... | 3272 | newer