Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

JESHI LA POLISI KUENDELEZA MISAKO NA KUFANYA DORIA ILI KUDHIBITI UHALIFU.

$
0
0

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaongeza jitihada za kuzuia na kupunguza matukio ya ajali za moto kwa kuhakikisha wananchi wanachukua tahadhari dhidi ya matukio hayo. Aidha kumekuwa na ajali 01 ya moto kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 15.08.2017 majira ya saa 21:30 usiku huko katika Soko la Sido Mwanjelwa lililopo Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilipokea taarifa ya kuwa Soko hilo lenye wafanyabiashara mbalimbali linaungua moto.

Kutokana na taarifa hizo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama lilifika eneo la Soko la Sido ambalo lina wafanyabiashara mbalimbali wanaouza vitu mbalimbali na kuanza jitihada za kuzima moto pamoja na kuhakikisha usalama watu na mali zao.

Soko hilo limeteketea kwa moto na mali zote zilizokuwa katika soko hilo  ambavyo bado thamani yake haijafahamika. Moto huo ulizimwa majira ya saa 02:40 usiku wa kuamkia leo kutokana na jitihada za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Kikosi cha zima moto na wananchi. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana. Hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo. Hakuna madhara ya kibinadamu yaliyoripotiwa kutokea.

Serikali kupitia Mkuu wa Wilaya ya Mbeya imeunda kamati maalum kwa ajili ya kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo ikiwa ni pamoja na kujua chanzo cha moto huo pamoja na kufanya tathmini ya hasara iliyosababishwa na moto huo.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa pole kwa wafanyabiashara waliopoteza mali zao kutokana na janga hilo la moto na Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu. Pia tunatoa shukurani kwa wananchi kwa ushirikiano mkubwa uliosaidia kufanikisha kuzimwa moto huoili usilete madhara makubwa.

WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa wananchi kuepuka kukimbilia sehemu zenye majanga ya moto kwani ni hatari kwa maisha yao na badala yake wajenge tabia ya kutoa taarifa mapema taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki. Aidha katika matukio kama hayo wananchi wajiepushe na uporaji wa mali za watu badala yake wajikite katika uokoaji pekee.
 Imesainiwa na:
 [MOHAMMED R. MPINGA - DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Wawili kizimbani kwa wizi Wa mafuta ya mawese na sabuni.

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii.

WAFANYABIASHARA wawili  wakazi wa Kimara jijini Dar es Salaam, Jumbo Cheto(39)  na  Anna Kilawe (43) leo wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya wizi wa mafuta ya mawese na sabuni zenye thamani ya milioni 60.

Hati ya mashtaka imesomwa na  wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi ambae amedai siku na mahali pasipojulikana, wote wawili walikula njama ya wizi iloyokuwa safarini.

Imedaiwa, kati ya Mei 19 na 23, mwaka huu,  huko kinondoni washtakiwa hao waliiba magaloni 1056 za mafuta ya mawese ya Lita 20, madumu mengine ya Lita 200 na sabuni 1319 ambapo vitu vyote vina thamani shilingi milioni 60.

Washtakiwa wamekana mashtaka hayo na kwai hiyo itatajwa tena Agosti 30, mwaka huu.
Mfanyabiashara, Jumbo Cheto(39) mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam
amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya wizi wa mafuta ya mawese na sabuni zenye thamani ya milioni 60.
 Mfanyabiashara,  Anna Kilawe (43) mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam (Mwenye nguo ya Pink) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya wizi wa mafuta ya mawese na sabuni zenye thamani ya milioni 60.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

MWANZA: MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMFANYIA UKATILI MTOTO WAKE

$
0
0

¨       MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMFANYIA UKATILI MTOTO WAKE WA KUMPAKA MAVI YA MBUZI KWENYE MAJERAHA ALIYOUNGUA NA  MOTO WILAYANI NYAMAGANA.

KWAMBA TAREHE 15.08.2017 MAJIRA YA SAA 16:30HRS JIONI KATIKA MTAA WA CHAKECHAKE – MKUYUNI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, SOSPETER RAJABU MIAKA 42, MVUVI NA MKAZI WA MTAA WA CHAKECHAKE – MKUYUNI, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMFANYIA UKATILI MTOTO WAKE AITWAYE NEEMA SOSPETER MIAKA 10, MWANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA, WA KUMPAKA MAVI YA MBUZI KWENYE MAJERAHA YA MOTO ALIYOUNGUA MAENEO YA MAPAJA YA MIGUU YOTE MIWILI KWA MUDA WA WIKI MBILI NA KUPELEKEA MAJERUHI KUWA NA HALI MBAYA KIAFYA, KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA.

INADAIWA KUWA TUKIO HILO LA AJALI YA MOTO DHIDI YA MTOTO LILITOKEA TAREHE 04.08.2017 MAJIRA YA SAA 19:45HRS USIKU, KATIKA MTAA WA KITANGIRI WILAYANI ILEMELA AMBAPO MAJERUHI ALIKUWA AKIISHI NA MAMA YAKE KWANI WAZAZI WAKE WALITENGANA KWA MUDA MREFU . INASEMEKANA AJALI HIYO YA MOTO ILITOKEA BAADA YA MAJERUHI KUMWAGIKIWA NA MAFUTA YA TAA PINDI ALIPOKUWA AKIWEKA KWENYE TAA YA KIBATARI NDIPO ALIPOWASHA MOTO NA NJITI YA KIBIRITI MOTO ULILIPUKA NA KUMUUNGUZA KWENYE MAENEO HAYO. 

INASEMEKANA KUWA BAADA YA MAMA WA MWENYE MTOTO KUKOSA FEDHA ZA MATIBABU ALIAMUA KUMPELEKA MTOTO KWA BABA YAKE MTAA WA CHAKECHAKE – MKUYUNI ALIPOKUA AKIISHI NA MKE MWINGINE ILI AMSAIDIE MTOTO APATE MATIBABU, LAKINI INADAIWA KUWA BAADA YA MTOTO KUFIKISHWA KWA BABA YAKE HAKUPELEKWA HOSPITALI BADALA YAKE ALIKUWA AKIPAKWA MAVI YA MBUZI NA KUPELEKEA HALI YAKE KUZIDI KUWA MBAYA.

WANANCHI WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, AMBAPO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI MAENEO HAYO NA KUFANIKIWA KUMKUTA MTOTO  AKIWA KWENYE HALI NGUMU.  ASKARI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI WALIMCHUKUA MTOTO HUYO NA KUMKIMBIZA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE KUPATIWA MATIBABU HUKU BABA WA MTOTO SOSPETER RAJABU AKITIWA NGUVUNI.

POLISI WAPO KWENYE UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA DHIDI YA UKATILI ALIYOKUWA AKIMTENDEA MWANAE, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI. 

MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA, KUWA PALE AMBAPO KUNATOKEA MTOTO AU MTU YEYOTE ANAPATA MAJERAHA AU KUUNGUA NI VIZURI WAKAWAONE MADAKTARI KATIKA HOSPITALI AMBAPO WANAWEZA KUPATA HUDUMA BORA NA STAHIKI ZA MATIBABU KULIKO KUTUMIA NJIA ZA KIENYEJI ZISIZOFAA AMBAZO HAZINA UBORA/USAHIHI, KWANI KUFUATA NJIA AMBAZO SI SAHIHI NA BORA KUNAWEZA KUPELEKEA KIFO KWA MGONJWA.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

RC PAUL MAKONDA AKABIDHIWA MRADI WA MABORESHO YA MTAA SAMORA ULIOGHARIMU ZAIDI YA SHILINGI MILION 840

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amekabidhiwa mradi wa Maboresho ya Mtaa Samora uliogharimu zaidi ya Shilingi Milion 840 zilizofadhidhiliwa na  Serikali ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la maendeleo Japan (JAICA) na Manispaa ya Ilaa uliokamilika kwa 100%.
Mradi huo umehusisha ujenzi wa sehemu za Maegesho, mapumziko ya watu,upandaji wa miti na Maua, maboresho ya mazingira, uwekaji wa alama za barabarani pamoja na maboresho ya mitaa kuanzia Makutano ya Barabara ya Samora na Morogoro ikienda sambamba na kupunguza msongamano.

Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Makonda amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kuhakikisha majengo yote ya Gorofa eneo la Posta yanafungwa Taa na Runinga za Matangazo ili kupendezesha Mji na kuongeza mwanga nyakati za usiku.

Amesema katika nchi zilizoendelea ikiwemo Marekani majengo marefu yamekuwa sehemu ya matangazo hususani nyakati za usiku na kufanya miji kupendeza hivyo hata Dar es salaam tunaweza kufanya hivyo ili kufikia azma ya Rais Magufuli kutaka Dar es salaam kuwa mji wa Biashara.
Aidha amesema mradi huo utakuwa wa awamu ili kuhakikisha mitaa na maeneo ya wazi yanaboreshwa ilikuwafanya wananchi kuwa na maeneo mengi ya kupumzika na kubadilishana mawazo ikiwa ni maono yake ya Dar es salaam Mpya.

Awali eneo hilo lililofahamika kama Kaburi Moja lilikuwa likitumika kama Choo, Maegesho holela na wakati mwingine likitumiwa kwa uhalifu na uchafu wa mazingira.

Amewataka wananchi kutunza vizuri eneo hilo ili liweze kuwanufaisha wengi huku akipiga marufuku wamachinga kutofanya biashara kwenye eneo hilo.
Aidha Makonda amesema anataka kuona vituo vyote vya Daladala mkoa wa Dar es salaam vinaboreshwe kuwa vya kisasa na kuwa sehemu ya matangazo ili kupendezesha mji na kuchangia ongezeko la mapato.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  akizungumza na katika hafla ya  makabidhiano mradi wa Maboresho ya Mtaa wa Samora uliogharimu zaidi ya Shilingi Milion 840 zilizofadhidhiliwa na  Serikali ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la maendeleo Japan (JAICA) leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kushirikiana na  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Isaya Mwita Charles wakikata utepe kuzindua mradi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Isaya Mwita Charles akikangua mradi wa Maboresho ya Mtaa Samora uliogharimu zaidi ya Shilingi Milion 840 zilizofadhidhiliwa na  Serikali ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la maendeleo Japan (JAICA).

KINANA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA QATAR HAPA NCHINI ,LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkaribisha Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsalimia msaidizi wa  Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa na Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam .
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad, baada ya mazungumzo yao,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO. 

Chid Benz awekwa chini ya uangalizi na mahakama kwa kutumia dawa za kulevya.

$
0
0
Na Mwene Said-Globu ya Jamii Dar es Salaam.

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imewaweka chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka miwili Msanii wa Bongofleva Rashid Abdalah maarufu Chidbenzi na wenzake watano baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kiapo dhidi ya maombi hayo.

Aidha, upande wa mashtaka uliwasilisha kiapo hicho kwamba mahakama iwaweke chini ya uangalizi baada ya kubainikia kujihusha na matumizi ya dawa za kulevya.

Maombi hayo yalisikilizwa na kutolewa uamuzi jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,Mfawidhi Ritha Tarimo.Mbali na Chidbenzi, wengine watakaokuwa chini ya ungalizi ni, Hadia Abeid, Said Ally, Athuman Elias na Hassan Mohamed.

Wakili wa Serikali Glory Mwenda, alidai kuwa upande wa Jamhuri unawasilisha hati ya kiapo kutoka kituo cha polisi Msimbazi kwamba watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya hivyo mahakama itoe dhamana kwani wamekuwa na tabia mbaya katika jamii.

Glory alidai kuwa wanaiomba mahakama itoe amri ya kuwaweka wajibu maombi chini ya uangalizi wa polisi na mahakama kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu na kusaidi dhamana ambayo itahakikisha wanakuwa na tabia njema na kutojihusisha vitendo vya dawa za kulevya.
Baaada ya kuwasilishwa kwa maombi hayo, Chidbenz na wenzake hakuwa na pingamizi.

Akitoa uamuzi hakimu alisema wajibu maombi watakuwa chini ya uangalizi wa polisi miaka miwili na kudhaminiwa na wadhamini wawili watakaotia saini ya dhamana ya Sh.milioni mbili kila mmoja na kuripoti kituo cha polisi Msimbazi kwa mwezi mara moja.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ZIARANI NCHINI CUBA

$
0
0
 WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumatano, Agosti 16, 2017) kuelekea nchini Cuba kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Akiwa nchini Cuba Waziri Mkuu anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Cuba kwa lengo la kukuza ushirikiano katika sekta za afya, elimu utalii na Kilimo.

Aidha, nchi ya Cuba ni mojawapo ya nchi zenye ushirikano wa muda mrefu na Tanzania Kisiasa, Kijamii na Kiuchumi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, AGOSTI 16, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke ,Felex Jackson katika Uwanja wa Ndege wa Julias Nyerere Dar es salaam leo August,16/2017 akiwa anaelekea Nchini Cuba Kwa ziara ya kikazi.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
 

WAZIRI MWAKYEMBE AHIMIZA MASHIRIKIANO KATI YA WIZARA NA UNESCO KATIKA KUHIFADHI HISTORIA YA NCHI

$
0
0

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akipokea moja ya kitabu chenye kumbukumbu ya historia ya Afrika ikiwemo Tanzania kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania Bibi. Zulmira Rodrigues wakati wa kikao na watendaji wa Wizara pamoja na UNESCO kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam .

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania Bibi. Zulmira Rodrigues wakati wa kikao na watendaji wa Wizara pamoja na UNESCO kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania Bibi. Zulmira Rodrigues (wapili kushoto) akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na watendaji wa Wizara kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Msaidizi Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Benard Lubogo (katikati) akichangia mada wakati wa kikao na watendaji kutoka UNESCO kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi. Martha Swai 



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara yake na watendaji kutoka UNESCO baada ya kikao na watendaji hao kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania Bibi. Zulmira Rodrigues na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi. Martha Swai

Picha na: Genofeva Matemu -WHUSM

Kwa nini nasita kujiunga na TEF - Fumbuka Ng'wanakilala

$
0
0
Fumbuka Ng'wanakilala 
Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu kuhusu TEF. Licha ya kasoro zake, pengine TEF kwa sasa ndiyo jumuiya ya waandishi wa habari Tanzania yenye umaarufu zaidi kuliko zote. Moja ya tuhuma kubwa dhidi ya TEF ni kuwa jukwaa hili limekuwa linatumika kama *kichaka* ambacho viongozi wa taasisi mbalimbali (hususan za umma) hujificha ili kujikinga na tuhuma za ufisadi.
TEF pia imekuwa inajulikana kwa kutoa matamko ya kufungia au kufungulia watu fulani wasiandikwe na vyombo vya habari nchini. Suala ambalo sisi wengine ambao siyo wanachama wa TEF tumekuwa tunahoji ni kuwa TEF ni jukwaa la wanachama (members only), hivyo basi, wanachama wa TEF wana *haki* ya kualikwa kwenye mikutano ya TEF na semina zinazoandaliwa na TEF na wana *wajibu* wa kupokea na kutekeleza maagizo ya TEF. Kwa muktadha huo huo, wahariri na waandishi ambao sio wanachama wa TEF hawana haki ya kuitwa kwenye vikao vya TEF, na hawana wajibu wa kutekeleza maagizo ya TEF.
Kumekuwa na dhana potofu kuwa maagizo na maamuzi yote ya TEF ni lazima yatekelezwe na waandishi wote wa habari, wahariri na taasisi zote za habari za Tanzania, hata wale wasio wanachama wa TEF bila kuzingatia dhana ya haki na wajibu.

Mara kadhaa tumesikia wahariri au vyombo vya habari vikiitwa wasaliti kwa kutotekeleza maagizo ya TEF bila kujali kama wahariri hao ni wanachama wa TEF au la. Je, ni nani amewapa TEF mamlaka ya kuwa wafanya maamuzi, watoa amri na wasemaji wa waandishi wa habari, wahariri na vyombo vyote vya habari vya Tanzania?*

Lazima ieleweke wazi kuwa wenye wajibu wa kutekeleza maamuzi ya TEF ni wahariri ambao ni wanachama wa TEF tu. Wahariri ambao sio wanachama wa TEF hawana wajibu wowote ule wa kupokea maagizo ya TEF. Ni jukumu la TEF kuwashawishi wahariri hao waungane na msimamo wao kwa kujenga hoja.
Ni vyema TEF ikajitathmini na kurekebisha hii taswira mbaya iliyopo. Je, kuandaa semina ambazo wahariri wanalipwa posho na kufungia/kufungulia watu fulani wasiandikwe na vyombo vya habari ndiyo jukumu kubwa la TEF?
Ningependa kuona TEF ikijikita kukabiliana na matatizo ya msingi zaidi yafuatayo kwenye tasnia ya habari ya Tanzania:

1. Tatizo la rushwa kwenye tasnia ya habari ya Tanzania

2. Kuhakikisha kuwa baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari Tanzania wanaacha kutoa maslahi duni kwa waandishi wa habari na kuhakikisha waandishi wa habari wanakuwa katika mazingira mazuri ya kazi

3. Kuondoa tatizo sugu la kuporomoka kwa maadili na weledi kwenye tasnia ya habari ya Tanzania

4. Kukemea na kukabiliana na kuongezeka kwa vitendo vya kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania

5. Kutoa dira kuhusu hatma ya vyombo vya habari nchini Tanzania kutokana na mazingira magumu ya biashara hiyo nchini kwa sasa

Pale ambapo TEF itakapojitathmini, naamini kwa dhati kuwa ina fursa kubwa ya kuwa jukwaa lenye nguvu na linaloheshimiwa na kuungwa mkono na waandishi wa habari na wananchi wengi zaidi nchini.

Naomba kuwasilisha.
Fumbuka Ng'wanakilala, 15 Agosti 2017

MOTO ULIVYOTEKETEZA SOKO LA SIDO JIJINI MBEYA, HUZUNI YATAWALA...

BARABARA YA KIMARA BARUTI-CHUO KIKUU JIJINI DAR ES SALAAM YATAKIWA KUKAMILIKA NDANI YA SIKU 60

$
0
0
Serikali imetoa siku 60 kwa mkandarasi wa Kampuni ya Hari Singh & Sons kumaliza ujenzi wa kipande cha barabara cha kilomita 1.5 kilichobaki kwa kiwango cha lami katika barabara ya Kimara Baruti-Msewe-Chuo Kikuu yenye jumla ya urefu wa kilomita 2.6.
Akitoa agizo hilo jijini Dar es salaam, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa anamaliza mradi huo haraka na kwa viwango vilivyo kwenye mkataba ili idumu kwa muda mrefu.
"Ikifika mwezi Oktoba nataka unikabidhi barabara hii ikiwa imekamilika kwa kiwango cha lami na vigezo vinavyokubalika, amesisitiza Eng. Ngonyani.


Aidha, Naibu Waziri Ngonyani amefafanua kuwa mkandarasi huyo hatoruhusiwa kutekeleza mradi mwingine wa barabara nchini endapo atashindwa kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa wakati.

Kwa upande wake Mhandisi Mradi kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Ngusa Julius, amesema kuwa TANROADS tayari imeshatoa notisi kwa mkandarasi huyo kuwa kama hatakamilisha kazi ya ujenzi ndani ya muda wa mkataba hatua za kudai fidia kulingana na mkataba zitafuata na baadae kukatisha mkataba.
Ameongeza kuwa mradi wa ujenzi wa barabara hiyo unasimamiwa na TANROADS kupitia kitengo chake cha wahadisi washauri wazalendo (TECU) na unagharimu shilingi Bilioni 5.7 ikiwa ni fedha za Serikali kwa asilimia mia moja.


Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Eng. Ngonyani amekagua daraja la Mlalakuwa lenye urefu wa mita 15 kila upande, lililopo barabara ya Mwai Kibaki jijini Dar es salaam na kusisitiza kwa mkandarasi Milembe & Kika JV kuhakikisha anamaliza ujenzi wa daraja hilo kwa wakati.

Ujenzi wa Daraja la Mlalakuwa unagharimu shilingi Bilioni 4.8 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwakani.

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa kampuni ya Hari Singh & Sons, Jaspal Singh (kushoto), wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kimara Baruti – Msewe – Chuo Kikuu yenye urefu wa KM 2.6 kwa kiwango cha lami, jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa kampuni ya Hari Singh & Sons, Jaspal Signh, akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kimara Baruti – Msewe – Chuo Kikuu yenye urefu wa KM 2.6 kwa kiwango cha lami, jijini Dar es Salaam.

 Muonekano wa sehemu ya barabara ya Kimara Baruti – Msewe – Chuo Kikuu yenye urefu wa KM 2.6 inayojengwa kwa kiwango cha lami, ambapo ujenzi wake umefika asilimia 57.

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Milembe & Kika JV anayejenga Daraja la Mlalakuwa lenye urefu wa mita 15 kila upande, lililoko barabara ya Mwai Kibaki, wakati akikagua ujenzi wake, jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa sehemu ya chini ya ujenzi wa Daraja la Mlalakuwa lenye urefu wa mita 15 kila upande, lililoko barabara ya Mwai Kibaki, jijini Dar es Salaam. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano,

Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)

Hii ni Dar Yetu? Kampeni hii tunaenda kuihitimisha Jumamosi hii

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO AGOSTI 16, 2017

MAGAZETI YA ALHAMIS LEO AGOSTI 17,2017

Vigogo 6 Jijini Mbeya Kortini kujibu mashtaka ya Kutafuna Bilioni 5 za Soko la kimataifa

$
0
0

Na Mbeya Yetu
Vigogo 6 kati ya 12 wanaotuhumiwa kuhusika kwenye kashifa ya ufisadi wa soko la Kimataifa la Mwanjelwa jijini Mbeya wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Mbeya na kusomewa mashtaka matatu ya uhujumu uchumi.
Waliopandishwa kizimbani Mahakamani hapo ni aliyekuwa Meya wa jiji hilo, Athanas Kapunga (70)  aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji hilo, Elizabeth Munuo (65) na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo Dk. Samwel Lazaro ambaye kwa sasa ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe. 
Wengine ni aliyekuwa Mtunza Hazina wa Jiji hilo, James Jorojik (62), aliyekuwa Mwasibu wa jiji hilo, Tumaini Msigwa (47) na Mhandisi wa jiji hilo, Emily Maganga (42). 
Mwendesha mashtaka wa serikali, Shadrack Martin, akisaidiwa na Hebel Kihaka pamoja na Baraka Mgaya wakati akiwasomea mashtaka yanayowakabili vigogo hao alisema wote kwa pamoja walitenda makosa ya uhujumi uchumi kati ya mwaka 2008 na 2013 hivyo kuisababishia serikali hasara kubwa.
Katika Shtaka la kwanza mwendesha mashtaka huyo alisema linawahusu watuhumiwa waili ambao ni Athanas Kapunga ambaye alikuwa Meya wa Jiji la Mbeya na Elizabeth Munuo ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Jiji ambao wanadaiwa kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya Shilingi Bilioni 3.3, ambapo wanadaiwa kusaini mkopo wa kiasi hicho cha fedha kutoka katika Benki ya CRDB ambao ulianza kulipiwa riba kabla ya kuanza kujengwa kwa Soko hilo la Mwanjelwa kinyume cha vifungu vya sheria namba 57 (1) na 60 (1)  na (2)  vya Sheria za uhujumu uchumi Sura ya 200 ya mwaka 2002.

Martini alisema shtaka la pili linawahusu Dk.Samwel Lazaro, James Jorojik, tumain Msigwa na Emily Maganga ambao kwa pamoja wanadaiwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa kuidhinisha malipo ya shilingi milioni 304,470,500 kwa Mkandarasi aliyekuwa anajenga soko hilo, Nandhra Engineering and Constaction ltd wakati kazi hiyo ilikuwa tayari imefanywa na Kampuni ya Tanzania Building Works ltd.

Aidha  Washtakiwa wa Shataka namba mbili pia wanashtakiwa kwa kosa la tatu la kuisababishia Halmashauri ya Jiji hasara ya shilingi 1,140,228,750 kwa kuidhinisha malipo ya fedha hizo kwa wakandarasi Tanzania Building Works na Nadhra Engineering kwa ajili ya ujenzi wa Soko hilo wakati kazi iliyotajwa haikuwemo kwenye Mkataba.

Washtakiwa hao kwa pamoja walikuwa wakitetewa na Mawakili watatu wakiongozwa na James Kyando, Baraka Mbwilo na Secilia Luhanga ambao waliiomba Mahakama hiyo kutoa maelezo kuhusu uwezekano wa wateja wao kupata dhamana. Hata hivyo Mwendesha Mashtaka wa serikali alisema upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo akaiomba mahakama kupanga siku nyingine kwa ajili ya kutajwa tena.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mbeya, Michael Mteite alisema Mahakama haina uwezo wa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi hivyo washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu hadi Agosti 29, Mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Kufikishwa Mahakamani kwa vigogo hao kunatokana na agizo la Waziri mkuu alilotoa Julai 31 mwaka huu wakati wa ziara ya kikazi jijini hapa alipozungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na Jiji na kuwataja wahusika 13 waliotajwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  (CAG) na kupendekeza wachukuliwe hatua.

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA ASHIRIKI KAZI YA UJENZI WA ZAHANATI YA UFYEMBA KATA YA WASA MKOANI IRINGA

StarTimes yazindua msimu wa tatu wa uoneshwaji wa ligi ya Bundesliga 2017/2018

$
0
0

Na Agness Francis, Blogu ya jamii.

Kampuni ya  Startimes Tanzania imezindua uoneshaji wa ligi ya  Bundesliga  mwaka 2017/2018 ambayo itarushwa mubashara kupitia  vipindi vya startimes  kwa wapenzi wa soka hapa  nchini

Uzinduzi huo umefanyika  leo jijini Dar es Salaam lengo ni kuwa  kuwafahamisha wapenzi  wa mpira kununua ving’amuzi na   kujiunga na vifurushi  ili kuburudika na mechi hizo ambazo ligi hiyo itakuwa ikiionyeshwa moja kwa moja na startimes.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif  amesema kuwa ipo fursa kwa waandishi wa habari za michezo  kufanya mashindano ya  uandishi wa mechi  hiyo na kwa mshindi  wa shindano hilo atagharamiwa safari zote za ti ya ndege  kwenda moja kwa moja Ujerumani.

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu nae amesema wana mahusiano mazuri na bundesliga  kwa kuwa na mkataba wa miaka mitano na hadi sasa ni mwaka wa tatu kuonyesha ligi hiyo.

Meneja Uwendeshaji  Startimes, Gaspa Ngowi  amesema kuwa  huduma mpya ya  malipo kwa wale wenye hali ya chini  wanaweza  kulipia siku moja king’amuzi  cha Startimes  kwa gharama ya bei ya shilingi 1000, ambapo kwa wiki utalipia elfu 4000.

Hata hivyo mhariri mkuu wa gazeti la Championi , Salehe Jembe amesema  kuwa  ligi ya Bundesliga  ina ubora na kuburudisha zaidi kulinga na  ligi zingine duniani  kwa kuwa na wachezaji bora 

Nae Meneja mahusiano wa Tabibu TV, Kaki Mwaigomole ametoa shukrani kwa kampuni ya  startimes kwa kuwapa fursa ya kuweza kuonyesha mubashara  mtanange huo ambao utaanza rasmi tarehe  18-27 Agosti mwaka huu
Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa kuonesha ligi ya Bundesliga kwa msimu wa mwaka 2017/18 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif(wa pili kutoka kushoto) akikata utepe pamoja na wadau mbalimbali wa mpira hapa nchini. 
Baadhi ya wafanyakazi wa StarTimes Tanzania wakfuatilia yaliyokuwa yanajiri kwenye uzinduzi huo
Mtangazaji wa kipindi cha michezo Radio Clouds 'Sports Extra' na Clouds Tv 'Sports Bar', Shaffih Dauda akitoa uchambuzi pamoja na kubashiri ligi hiyo itakavyokuwa kwenye msimu wa mwaka 2017/2018.
 Mhariri mkuu wa gazeti la Championi, Salehe Jembe akitolea ufafanuzi kuhusu ligi ya Bundesliga ya nchini Ujerumani itakavyokuwa kwa msimu wa mwaka 2017/18 kwenye uzinduzi wa kuonesha ligi hiyo kwa mwaka wa tatu kupitia kwenye king’amuzi cha Startames.
 Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu akizungumza kuhusu kampuni hiyo wanavyoshirikiana kuonesha ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga
Picha ya Pamoja 

Makamu wa Rais kumuwakilisha Rais mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi SADC

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini leo kwenda Pretoria Africa ya Kusini ambako atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika utakaofanyika Pretoria, Afrika Kusini tarehe 19 na 20 Agosti, 2017. 

Mkutano huo utapokea na kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama; Hali ya Michango mbalimbali ya Nchi Wanachama na Kupokea taarifa ya Mwenyekiti anayeondoka wa SADC Organ.  

Pia Mkutano utapokea taarifa ya Katibu Mtendaji wa SADC; Kupitia hali ya kiuchumi katika Kanda ya SADC; Kuwasilisha Kaulimbiu ya Mkutano wa SADC; Taarifa kuhusu Mfuko wa Maendeleo wa SADC; Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Viwanda; Kuwezesha Chuo cha Elimu ya Sayansi na Teknolojia; Maombi ya Serikali ya Comoro na Serikali ya Burundi kujiunga na SADC; Utekelezaji wa Mabadiliko ya Kitaasisi ya Umoja wa Afrika na Mkutano wa Mshikamano kati ya SADC na Saharawi ya Magharibi. 

Mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit) tarehe 18 Agosti, 2017 ambao Tanzania itakabidhi nafasi ya  uenyekiti kwa mwenyekiti mpya. Double Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano huo Mfalme Mswati III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu katika Mkutano huu ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.

Makamu wa Rais amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfrikaMashariki, Mhe. Balozi Dkt Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijange, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Ashatu Kijaji na watendaji wengine waandamizi Serikalini

Makamu wa Rais na ujumbe wake anatarajia kurudi nchini Agosti 21, 2017.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
17/8/2017
 Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke ,Felex Jackson katika Uwanja wa Ndege wa Julias Nyerere Dar es salaam leo Agosti ,17/2017 akielekea Nchini  Pretoria Africa ya Kusini ambako atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika utakaofanyika Pretoria, Afrika Kusini tarehe 19 na 20 Agosti, 2017.
 Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Temeke ,Felex Jackson katika Uwanja wa Ndege wa Julias Nyerere Dar es salaam leo Agosti ,17/2017 akielekea Nchini  Pretoria Africa ya Kusini ambako atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika utakaofanyika Pretoria, Afrika Kusini tarehe 19 na 20 Agosti, 2017.

SHAKA:JUKUMU LA KULETA MAENDELEO PEMBA NI LA WOTE.

$
0
0
Na Mathias Canal, Kaskazini Pemba


Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema kuwa Jukumu la kuleta maendeleo ya kiuchumi katika jamii ni la kila mwananchi sio jukumu la serikali pekee.


UVCCM imesema kuwa jukumu la serikali ni kuwaonyesha wananchi fursa zilipo na namna bora ya kuzichanganua ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake sambamba na kuwezeshwa kupata mikopo katika vikundi vyao vya ujasiriamali.


Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Agosti 16, 2017 alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.


Alisema kuwa vijana ni nguvu kazi ya Taifa hivyo wanapaswa kutumia nguvu zao vizuri kwa kufanya kazi ili kujikwamua kiuchumi katika familia zao badala ya kukaa maskani kujadili mambo yasiyokuwa na tija kwao.


Aliongeza kuwa UVCCM inaunga mkono vijana kukaa maskani kwa maslahi mapana ya mjadala wa Maendeleo yatakayopelekea kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kujiunga katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali.
 Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza jambo pamoja na mwl,Ally khatibu Hassan Mkuu wa shule ya msingi Michekweni wakati akikagua jengo la Ujenzi wa maktaba pamoja na madarasa ya Shule ya Msingi Micheweni. wakati wa ziara ya kikazi  visiwani pemba.
 Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akiwa Shumba mjini akikagua sehemu itakayo jengwa jeti
 Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akigagua ujenzi wa ofisi ya ccm tawi la njuguni inayojengwa na mwakilishi Jimbo
 Afisa mipango wa halmashauri ya konde (pili kushoto)akitolea ufafanuzi juu ya ujenzi wa soko la mboga mboga la samaki pamoja na mbogamboga kwa Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akiwa katika ziara ya kikazi  visiwani pemba.

TTCL YAZINDUA HUDUMA YA 4G LTE MBEYA

$
0
0
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imezindua huduma mpya ya mawasiliano ya 4G LTE pamoja na kutambulisha huduma nyingine ya TTCL PESA.

Hata hivyo katika uzinduzi huo imeelezwa kuwa mawasiliano bora yanahitajika ili kuendelea kuimarisha shughuli za kiuchumi mkoani Mbeya ikiwa ni pamoja na kuongeza urahisi wa upatikanaji wa taarifa za masoko na bei nzuri kwa wazalishaji na Wakulima.

Hayo yalielezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakati akizindua huduma mpya ya kampuni ya Simu ya TTCL ya 4G LTE katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntika katika ofisi za Kampuni hiyo zilizopo jijini Mbeya.

Alisema mawasiliano bora yanamchango mkubwa katika ukuaji wa sekta za Elimu, Afya, Miundombinu, Biashara, utalii, huduma za jamii na sekta zingine mtambuka hivyo kitendo cha TTCL kuibuka upya kutasaidia kuchochea maendeleo katika Mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla.

Aliongeza kuwa mbali na Mawasiliano kusaidia kukuza uchumi pia Wafanyakazi wa Sekta binafsi na sekta za umma wanahitaji mawasiliano bora ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu yao katika maeneo yao ya kazi.

Aidha alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya kuchangamkia fursa za kibiashara zinazotolewa na TTCL kama vile kuwa wakala wa kuuza vocha, Laini na kuwa Wakala wa huduma mpya ya kifedha ya TTCL Pesa kwani kufanya hivyo kutasaidia kuongeza ajira na vipato vyao.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika akisaidiana na Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Waziri Kindamba kutoa kitambaa kuashiria kuzindua huduma ya 4G mkoani Mbeya.Afisa mtendaji mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba akimkabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika baada ya kuzindua huduma ya 4G LTE mkoani MbeyaMkuu wa Wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika akisaidiana na Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Waziri Kindamba kuonesha bango kuashiria kuzindua huduma ya 4G mkoani Mbeya.Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mbeya pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa 4G LTE mkoani Mbeya.

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images