Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110095 articles
Browse latest View live

Watumishi wa Umma Watakiwa Kubadilika

$
0
0
Frank Mvungi - Maelezo.

Serikali imewataka watumishi wa umma katika mikoa na Halmashuri kubadilika na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia mabadililko ya mifumo yanayofanywa kwa kushirikina na wadau wa maendeleo.

Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya mfumo wa kielektroniki utakaotumika kuandaa mipango,bajeti na kutoa ripoti yaliyowashirikisha washiriki kutoka Mikoa ya Katavi, Rukwa na kigoma, Mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo Dkt. Paul Chote amesema dhamira ya serika ni kuwawezesha watumishi wake kutekelza majukumu yao kwa ufanisi hasa katika kuwahudumia wananchi.

“Mfumo huu sio wa majaribio hivyo ni wajibu wa kila mshiriki kurudi katika mkoa na halmashuri na kuhakikisha kuwa anajenga uwezo kwa watumishi ambao hawakushiriki katika mafunzo haya kwa kuwa mfumo huu unahitaji uwajibikaji wa pamoja” alisisitiza Chote.

Akifafanua Dkt. Chote amesema kuwa washiriki wa mafunzo hayo wana jukumu kubwa lakutumia weledi na ujuzi waliopata kuleta mageuzi chanya katika maeneo yao ili azma ya serikali kutoa huduma bora itime. 

Kwa upande wake Muwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Lisa Rwamiago amesema kuwa vituo zaidi ya elfu 22,000 vya kutolea huduma vitaunganishwa katika mfumo huo wa Kitaifa hali itakayofanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kusini mwa Afrika kwa kuwa na mifumo bora yakutolea huduma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
 Mganga Mkuu wa  Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chote ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo wa kuandaa bajeti, mipango na kutoa ripoti (PlanRep iliyoboreshwa) kutoka mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma akisisitiza  jambo kwa washiriki hao wakati akifunga mafunzo hayo.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akizungumza muda mfupi kabla ya Hafla ya ufungaji mafunzo hayo iliyofanyika Mjini Kigoma. (Picha na Frank mvungi-Maelezo)

MTOTO ALIYEUNGUA MIKONO SASA KUREJEA DARASANI

$
0
0
Mtoto aliyeungua na kushindwa kuendelea na masomo mkoani Mtwara ametibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na sasa anaweza kuendelea na masomo pamoja na kufanya shughuli zake za kawaida.

Mtoto huyo aliungua moto baada ya kusukumwa na mwenzake shuleni na hivyo kuungua mikono yote miwili na kusababisha vidole kujikunja na kushikamana.Baada ya kufikishwa Muhimbili madaktari bingwa walifanyia upasuaji na sasa amepona.

Daktari Bingwa wa Upasuaji, Ibrahimu Mkoma amesema mtoto Mwanahidi Hamisi aliungua miaka saba iliyopita na mikono yake kuadhirika na kushindwa kufanya kazi yoyote.

Amesema mwaka 2015 mtoto huyo alifanyiwa upasuaji mkono wake wa kulia katika Hospitali ya CCBRT na kwamba sasa anaendelea vizuri.Dk Mkoma amesema Juni 7, 2017 Muhimbili ilimpokea mtoto huyo na baada ya kufanyia uchunguzi walimfanyia upasuaji mkono wa kushoto na kunyoosha viungo katika vidole vyake ambavyo vilikuwa vimejikunja.

“Baada ya kuungua moto vidole vyake vilishikana na viungo kujikunja, lakini tumefanikiwa kuvinyoosha viungo hivyo na sasa Mwanahidi anaendelea vizuri na matibabu,” amesema Dk Mkoma.Amesema mtoto huyo sasa anaweza kufanya kazi mbalimbali kama kufua na kwamba anaweza kundelea na shule tofauti na awali baada ya kuungua.

Mama wa mtoto huyo, Amina Mohamed Mkadengile ameambiwa kwamba anapaswa kumfanyia mazoezi mtoto wake ili aimarike zaidi.“Daktari amenielekeza jinsi ya kumfanyia mtoto mazoezi, nitakuwa nafanyia mazoezi katika Hospitali ya Mkoa ya Ligula mkoani Mtwara. Nawashukuru san

MAGAZETI YA IJUMAA LEO AGOSTI 18,2017

Baraza la Hifadhi ya Mazingira lampongeza mshindi wa Biko

$
0
0

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Tanzania, (NEMC), limpongeza mshindi wa droo ya 32 ya Bahati Nasibu ya Biko nchini Tanzania, Edward Gama, mkazi wa Tabata, aliyefanikiwa kunyakua jumla ya Sh Milioni 20 inayotolewa na Biko, huku akitwaa zawadi hiyo katika droo ya Jumatano iliyopita na kumtaka ajihusishe na masuala ya mazingira na ufugaji wa nyuki.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Baraza hilo, Dr Vedast Makota, wakati Gama anapokea hundi yake ya Sh Milioni 20, saa chache kabla ya kukabidhiwa rasmi fedha zake katika benki ya NMB, Tawi la Bank House, Posta, jijini Dar es Salaam leo (jana).

Akizungumzia ushindi huo wa mwanafunzi anayesubiri ajira, Dr Makota, alisema ni furaha kubwa kwa kijana wao kuibuka na ushindi huo wa Sh Milioni 20 ambapo amekabidhiwa, huku akisema ni fursa kubwa zaidi kama Gama atajihusisha pia na masuala ya mazingira kulingana na taaluma yao.

“Ni furaha kubwa kuona kijana wetu amefanikiwa kuibuka na ushindi huu mnono, hivyo namtaka azitumie vizuri fedha zake pamoja na kuwekeza pia katika sekta ya mazingira ikiwamo ufugaji wa nyuki ambao ni biashara nzuri sana,” Alisema.

Naye Gama aliwapongeza Biko kwa kumkabidhi fedha zake haraka, huku akisema wakati anapokea simu ya Kajala Masanja na Mujuni Sylvester ‘Mpoki’, hakuamini kabisa kulingana na bahati nasibu hiyo inavyohusisha watu wengi wanaocheza Biko kila siku.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MHAGAMA AZITAKA HIFADHI ZA TAIFA KUTUMIA WASANII KATIKA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII

$
0
0
Na Pamela Mollel-Arusha 

WAZIRI wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama
amezitaka hifadhi za taifa nchini kuendelea kuwatumia wasanii nchini
katika kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana huku akiipongeza
Mamlaka ya hifadhi za taifa Ngorongoro inavyotangaza vivutio vyake
kupitia msanii Mrisho Mpoto. 

Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni jijini Arusha alipotembelea banda la Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro katika maonesho ya Nanenane. 

Alisema kuwa wasanii wananafasi kubwa ya kuutangaza utalii wa ndani na
kuendelea kuitangaza Tanzania endapo watatumiwa kama mabalozi kupitia
umaarufu wao jambo ambalo litasaidia pia kuiingizia nchi kipato kupitia
watalii. 

Naye Balozi wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Mrisho Mpoto aliwapongeza watanzania kuwa na mwitikio mkubwa wa kutembelea hifadhi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwapeleka watoto wao katika maonesho hayo ili kujifunza na kuona shughuli zinazofanywa na mamlaka hiyo hivyo kuwaandaa watoto hao kuwa wahifadhi kwa baadae. 

“Mfano mzuri ni hili la punguzo la shilingi elfu 50 lililotolewa ili
watanzania waweze kutembelea hifadhi ya Ngorongoro tumeona watu
walivyochangamkia na kwenda kutembelea Ngorongoro hivyo ni jambo zuri
na la kupongezwa kwa watanzania na ninaomba waendelee kutembelea
hifadhi zetu”alisema Mpoto. 

Kwa upande wake Ofisa Utalii wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Peter
Makutian aliwashukuru watanzania kuendelea kuhamasika kutembelea hifadhi hiyo tofauti na awali na kusema kuwa idadi ya wageni toka nje ya nchi wanaotembelea hifadhi hiyo kwasasa ipo sawa na watanzania. 

Aidha aliwaomba watanzania wengine kuendelea kutembelea vivutio vya Tanzania ikiwemo Ngorongoro kwakuwa gharama wanazotoza ni ndogo kwao ukilinganisha na wageni toka nje ya nchi hivyo ni fursa nzuri kwao
kuitumia na kuwa mabalozi wa hifadhi kwa wengine.
WAZIRI wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akiwa anamsikiliza Balozi wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Mrisho Mpoto mara baada ya kuwasili katika banda hilo hivi karibuni jijini Arusha katika maadhimisho ya sikukuu ya nane nane 
Ofisa Utalii wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Peter Makutian aliwashukuru watanzania kuendelea kuhamasika kutembelea hifadhi hiyo tofauti na awali na kusema kuwa idadi ya wageni toka nje ya nchi wanaotembelea hifadhi hiyo kwasasa ipo sawa
na watanzania.

UNESCO YAKABIDHI VIFAA VYA RADIO ZA KIJAMII VYA MAMILIONI

$
0
0
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekabidhi vifaa vya radio kwa radio za jamii nne vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi. Unesco imesema kwamba utoaji wa vifaa hivyo umelenga kuongeza usikivu wa mawimbi ya radio katika maeneo ya vijijini. Shughuli ya kukabidhiana imefanyika Agosti 17 mwaka huu.

 Akizungumza wakati wakukabidhiana vifaa hivyo Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues alisema kwamba UNESCO inatambua kazi nzuri zinazofanywa na radio hizo za jamii za kuwafikia wananchi wengi zaidi. Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Ofisa Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema Kilapilo wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano Unesco Dar es Salaam. Picha juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu kwa pamoja wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa hivyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO Dar es Salaam. Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam. Picha juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya kwa pamoja wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa hivyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO.

WAZIRI UMMY MWALIMU AENDELEA NA ZIARA MKOANI KATAVI

$
0
0
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Leo ameendelea na ziara yake mkoani Katavi, akiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kukagua huduma za Afya zitolewazo nchini.

Katika ziara hiyo Waziri huyo ametembelea kituo cha Afya Nsimbo na Inyonga katika Halmashauri ya Mlele na Usevya Halmashauri ya Mpimbwe. 

Akiwa katika vituo hivyo Waziri huyo alifanya ukaguzi kwenye maendeo mbalimbali ya utoaji huduma,upatikanaji was Dawa na vifaa Tina,miundombinu ya vituo hivyo pamoja na kuongea na watumishi wa Afya kujua changamoto zinazowakabili na kufanyia ufumbuzi ili kuleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi.

Aidha,akizungumza na watumishi hao,Waziri Ummy ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha kuwa dawa zinawafikia wananchi katika vituo vyote vya kutolea huduma.

Waziri huyo amekua akisisitiza Mara kwa Mara katika ziara zake suala ya usimamizi wa Dawa na vifaa Tiba kwenye hospitali na vituo vya Afya nchini ili kuondoa malalamiko mengi toka wa wananchi wanaofika kupatiwa huduma.

Kesho Waziri ataendelea na ziara take Wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa

CHUO CHA UFUNDI ARUSHA CHAZINDUA MTAALA MPYA WA GESI NA MAFUTA

$
0
0

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo amekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kwa uamuzi wake wa kushirikiana na Chuo cha Camosun cha nchini Canada kuandaa mtaala wa ufundi bomba,gesi na mafuta katika ngazi ya Diploma.

Akizindua mtaala huo ambao ni kwanza na aina yake nchini alisema utaisadia serikali kuwapata vijana wengi wenye utaalamu wa sekta ya mafuta na gesi nchini katika ngazi hiyo ambayo imenekana kuna pengo kubwa nchini.

“Mafunzo haya yatasaidia sana kuwapata wataalamu wetu na itaipunguzia serikali mzigo wa kuwaajili wataalamu wa kigeni ambao ulipwa fedha nyingi za kigeni,”alisema

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Dk Richard Masika amesema baada ya kutambua mahitaji makubwa ya wataalamu wa fani hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita walikua wakiaanda mtaala kwa ushirikiano na Chuo cha Camosun na mafanikio yamepatikana.

Alisema kozi hiyo ni nyumbufu itakayowawezesha wanafunzi kufanya kazi baada ya kumaliza mwaka wa kwanza na baadaye kuendelea na masomo jambo ambalo litakua likiwapa maarifa kwa vitendo zaidi badala ya nadharia pekee.

Mmoja wa wanafunzi wanaosoma kozi hiyo ambayo imegharamiwa na serikali ya Tanzania,Latifa Mkombo amesema wanaishukuru serikali kwa kutoa ufadhili huo na kuahidi kusoma kwa bidii kwaajili kuingia katika ajira za gesi na mafuta.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kozi ya ufundi bomba,mafuta na gesi katika chuo
cha Ufundi Arusha(ATC) jijini Arusha,kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Camosun nchini Canada,Sherri Bell na kulia ni Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Richard Masika. 
Afisa wa kitengo cha biashara katika ubalozi wa Canada nchini,Anita
Kundy akisoma hotuba yake,kushoto ni Mshauri wa ufundi kutoka nchini Canada,Dk Alan Copeland. 
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo akionesha nakala ya mtaala mpya wa kozi ya ufundi bomba,mafuta na gesi uliozinduliwa
katika chuo cha Ufundi Arusha(ATC) 
Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi nchini(TVET)Wizara ya Elimu,Sayansi na
Teknolojia,Mhandisi Thomas Katebalirwe akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi huo. 


KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Ukomo wa kushughulikia maombi ya muda mrefu ya kuunganisha Umeme ni Agosti 30- Dkt Kalemani

$
0
0
Na Teresia Mhagama

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani ameeleza kuwa ukomo wa kuunganishia umeme wateja walioomba kuunganishiwa huduma hiyo kwa muda mrefu ni Agosti 30, 2017 na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) atakayeshindwa kutimiza agizo hilo atashushwa cheo.

Dkt. Kalemani aliyasema hayo kwa nyakati tofauti akiwa katika ziara ya kuzindua mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu katika mikoa ya Rukwa, Ruvuma na Mtwara.

"Unakuta kuna wateja wameomba kuunganishiwa umeme miezi kadhaa iliyopita lakini mpaka sasa hawajaunganishwa wakati vifaa vipo, kwa hili lazima tuchukue hatua kwa Meneja kama ni wa wilaya, mkoa, Kanda au Mkurugenzi atayechelewa kuunganishia wateja Umeme," alisema Dkt. Kalemani.

Dkt. Kalemani alisema kuwa muda wa kumuunganishia mteja Umeme mara anapolipia huduma hiyo ni Siku Saba na si vinginevyo."Natambua kuna maeneo ambayo TANESCO mnafanya kazi vizuri lakini katika hili tutawajibishana," alisisitiza Dkt. Kalemani.

Wakati huohuo. Dkt. Kalemani aliwaagiza watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa watu wote wanaofanya kazi ya kutandaza nyaya za umeme ndani ya nyumba wawe wanatambulika na Shirika hilo ili kuondoa tatizo la vishoka kufanya kazi hiyo pasipo ufanisi na baadaye kuleta madhafa kama ya moto.

Vilevile aliwataka watendaji hao kutokukaa maofisini na badala yake wawafuate wananchi sehemu walipo, suala ambalo litafanya Shirika hilo kuongeza idadi ya wateja na kuwaondolea wananchi kero ya kutembea kwa umbali mrefu kufuata huduma TANESCO.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika mkoa wa Ruvuma.

HASSAN MAAJAR TRUST AND RADAR EDUCATION REFURBISHES LIBRARY AT MAJIMATITU SCHOOL

$
0
0
TEMEKE District Commissioner Mr. Felix Lyaniva jointly with Hassan Maajar Trust (HMT) Executive director Ambassador Bertha Semu-Somi cut a ribbon to launch refurbished Library at Maji Matitu Primary School in Dar es Salaam yesterday. HMT and Radar Education funded the refurbishment expenses. Looking on (left) is School Committee member Erick Solo and Temeke municipal Education Officer Sylivia Mutasingwa. 
Temeke District Commissioner, Mr Felix Lyaniva keenly gets a briefing from the Head of Special Education for people with intellectual impairment, teacher Rehema Lemwai after launching a refurbished Library at Maji Matitu Primary School in Dar es Salaam yesterday which has been refurbished by Hassan Maajar Trust (HMT) in partnership with Radar Education. Others are Kayemarie Antoinette from HMT (right) and HMT Executive Director Amb. Bertha Semu-Somi (second left).


Dar es Salaam, 17 th August 2017: Hassan Maajar TRUST (HMT) recently marked its sixth year anniversary by partnering with Radar Education to refurbish the Majimatitu Primary School library along with a 933 books donation. The event was held at the school located in Mbagala, Temeke District, Dar es Salaam.

The HMT Executive Director, Ambassador Bertha Semu-Somi and Radar Education General Manager Arthur Walden on behalf of their organizations presented the refurbished library and books to Majimatitu Head Teacher, Abdul Malik. The Temeke District Commissioner, Felix Lyavia, officiated at the Event.

Speaking at the event yesterday, HMT’s Executive Director said, “This is our third time at Majimatitu. In August 2015, we donated 30 desks for pupils with disability. Then we found that 90% of students sit on the floor due to lack of desks. Committed to solve the problem and sponsored by Bank M, HMT organised a Charity Walk in November 2015”.

Through the Charity Walk, HMT succeeded in 1) raising awareness on the shortage of desks at Majimatitu. Many Education Stakeholders heeded the call”. 2) Collecting funds enough to procure 280 desks that sit three to four students each, thereby lifting over 850 students off the floor on to desks.

HMT’s core objective is to contribute to an improved learning environment for quality education in schools. “We are delighted to have Radar Education on board this project. The Radar Education Chief, Mr Walden stated “We are happy to join HMT for this Library project, which is for us a welcome opportunity to continue to contribute to quality Education in Tanzania. We donated over 900 books.

We hope that students will embrace this support aimed at building the culture of reading” The renovation of this library is a part of HMT’s ‘A Desk For Every Child’ campaign, In six years, the Trust prides in over 9,000 desks donated to 13 regions (Rukwa, Njombe, Singida, Mwanza, Pwani, Shinyanga, Kigoma, Lindi, Mbeya, Iringa, Mtwara, Dar es Salaam and Kilimanjaro) lifting over 30,000 students off the floor.

“We have gone far in realizing HMT’s dual dream of raising awareness on the plight of pupils learning to read and write while seated on the floor, and mobilising the public to join the HMT led initiative to resolve the problem’, added Ms. Semu-Somi.

VIDEO: KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO AKUTANA NA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII NA MAAFISA USTAWI WA JAMII MKOANI IRINGA

JAFO AAGIZA MKANDARASI WA MRADI WA MAJI ITISO ASAKWE

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amemwagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya Chamwino Athumani Masasi kumtafuta mkandarasi wa mradi wa maji Itiso ili akamilishe mradi huo haraka kabla ya kuchukuliwa hatua.

Akizungumza leo katika ziara yake ya kukagua mradi huo, Jafo amesema mkandarasi huyo kutoka kampuni ya Audancia anatakiwa kurudi eneo la mradi haraka kukamilisha kama mkataba wake unavyoelekeza.

“Mmtake arudi haraka hapa kwenye eneo la mradi au kama ikishindikana achukuliwe hatua za kisheria kwa kukamatwa na polisi na kupelekwa mahakamani kutokana na kushindwa kutekeleza mkataba,”amesema Jafo. 

Amesema Mkandarasi huyo ametoweka eneo la mradi huku akiwa amefunga mabomba yenye ubora wa chini kwenye njia kuu (Main line) kinyume cha mkataba.Ameeleza kuwa mkandarasi huyo amelaza mabomba ya Class B(PN 6) badala ya bomba za Class C(PN10) jambo ambalo 

limesababisha mradi huo kushindwa kufanyakazi kwa kuwa mabomba yaliyofungwa yameshindwa kuhimili msukumo wa maji.Kadhalika, Jafo pia ameagiza mkandarasi mshauri wa mradi huo O&A Company LTD kutafutwa kwani ameshindwa kusimamia mradi huo ipasavyo na kuruhusu kazi hiyo ifanyike kinyume cha mkataba na kuruhusu mkandarasi atoke eneo la mradi wakati vituo vinne havitoi maji kati ya vituo kumi vya mradi. 

Hata hivyo Jafo ametoa onyo kwa wakandarasi washauri na wakandarasi wa ujenzi wa maji ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao kwamba hivi sasa kazi zilizo chini ya Ofisi ya Tamisemi watazisikia kwenye bomba.

“Tutakuwa tumebaini makampuni yote yanayofanya kazi kwa ubabaishaji na kutoyapatia kazi tena za usimamizi na ujenzi katika halmashauri zote,”amesema Naibu Waziri Jafo.

Jafo ameagiza kasoro zote za mradi huo zirekebishwe na ifikapo Septemba 15, mwaka huu mradi huo uwe umekamilika.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Seleman Jafo akizungumza na wananchi nakutoa maelekezo watendaji wa Halmashauri ya Chamwino katika mmoja ya kituo cha kuchotea maji kwenye mradi wa maji Itiso. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Seleman Jafo akizungumza na wananchi nakutoa maelekezo watendaji wa Halmashauri ya Chamwino katika mmoja ya kituo cha kuchotea maji kwenye mradi wa maji Itiso. 
Mbunge wa Chilonwa Joel Mwaka akimkaribisha Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo kuzungumza na wananchi katika mradi wa maji Itiso.

Kituo Cha Afya Chalinze Chaanza Kufawanyia Oparesheni Wagonjwa

$
0
0
Na Omary Mngindo, Lugoba

KITUO cha afya cha Chalinze kilichopo Kitongoji cha Bwilingu halmashauri ya Chalinze Bagamoyo Mkoa wa Pwani kimeanza kuwafanyia operesheni wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kituoni hapo.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mwanasheria Ridhiwani Kikwete ndiye aliyechokonoa hoja hiyo alipomtaka Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo kumpatia uhakika wa jambo hilo ambalo analisikia kwa watu kwamba Kituo hicho kimeshaanza zoezi la kuwafanyia upasuaji wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.

"Nimesikia maneno kutoka kwa wakazi wakisema kwamba Kituo chetu cha afya Chalinze kimeshaanza kuwafanyia upasuaji wagonjwa wanaokwenda kwa ajili ya huduma hiyo, Mganga Mkuu tunaomba ulitaarifu Baraza hili taarifa hizo zilizo njema zina ukweli gani?," aliuliza Ridhiwani.

Akijibu swali hilo, Dr. Isaack Makungu aliwathibitishia Madiwani hao kwamba taarifa hizo zina ukweli na tayari akina mama 10 wajawazito wameshapatiwa huduma ya upasuaji kisha kupata watoto wakiwa salama na afya njema pamoja na wazazi wenyewe wakiwa na afya iliyo njema.

"Ni kweli Kituo chetu kimeshaanza kazi ya kuwafanyia upasuaji akina mama wajawazito ambao wamebainika hawana uwezo wa kusukuma mtoto ambapo watu kumi tumeshawapatia huduma hiyo wakiwa salama wao pamlja na watoto wao," alisema Dr. Makungu.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Said Zikatimu aliliambia Baraza hilo kwamba hatua hiyo ni faraja kwao kwani itasaidia mambo mengi kwanza kuwapunguzia saafari ndefu ya kwenda Tumbi, Bagamoyo au Muhimbili, poa mafuta ambayo yalikuwa yanatumika kusafirisha wagonjwa kweda maeneo nayo.

"Taarifa hiyo ni faraja kwetu kwani itasaidia wagonjwa ambao awali walikuwa wanasafirishwa kwenda Tumbi, Bagamoyo au Muhimbili, lakini tunatakiwa kujenga uzio kutoka chumba cha upasuaji kwenda wodini ili mgonjwa anapotoka kufanyiwa upauaji asiwe anaonekana na watu wengine," alisema Zikatimu.

INTRODUCING NEW HIT - SINA JAMBO - BILLNASS


UNESCO YAKABIDHI VIFAA VYA RADIO ZA KIJAMII VYA MAMILIONI

$
0
0
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekabidhi vifaa vya radio kwa radio za jamii nne vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi. Unesco imesema kwamba utoaji wa vifaa hivyo umelenga kuongeza usikivu wa mawimbi ya radio katika maeneo ya vijijini. 

Shughuli ya kukabidhiana imefanyika Agosti 17 mwaka huu. Akizungumza wakati wakukabidhiana vifaa hivyo Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues alisema kwamba UNESCO inatambua kazi nzuri zinazofanywa na radio hizo za jamii za kuwafikia wananchi wengi zaidi.Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya radio jamii iliyofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.

Aidha alisema ni muhimu sana kwa radio hizo za jamii kujiangalia na kujitunza zenyewe ili wasiingie katika matata na kuchapisha au kutangaza stori baada ya kukamilika kwake. Alisema ipo haja kwa vyombo vya habari kufanyakazi kwa mujibu wa taratibu zao na kuhakikisha kwamba hawachapishi habari ambazo zinahatarisha uwapo wa uandishi unaozingatia maadili. Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM, Samada Maduhu aliishukuru UNESCO kwa kusaidia kituo chake na kwamba wanatarajia kufikia wilaya tano.Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu, akitoa neno la shukrani kwa ofisi za Unesco wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika ofisi za Shirika hilo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa mtaalamu wa Mawasiliano Unesco, Nancy Kaizilege Angulo.

Alishukuru UNESCO kwa kuwawezesha kufika katika wilaya tano na kwamba kwa msaada huo wataokoa shilingi laki saba kwa mwezi kuazima transmita. “Radio yetu inawafikia watu 500,000 lakini kwa kupatiwa hivi vifaa tutaweza kufikia watu milioni 1 katika wilaya zaidi ya tano za Kahama, Shinyanga Vijijini, Nyang’wale na Mbogwe mkoani Geita na pia Nzega na Uyui mkoani Tabora ,” alisema meneja huyo . Kwa mujibu wa Maduhu, kama wasingelipata transmita hiyo wangelikuwa wanatumia sh milioni 8.4 kwa mwaka.Ofisa Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema Kilapilo akitoa shukrani kwa uongozi wa Unesco wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya redio iliyofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Ayubu Kalufya wa radio ya jamii Uvinza alisema kwamba kituo chake kilikuwa kinakodisha transmita kwash laki tano na kufanya kwa mwaka mzima kutumia sh milioni 6. Alisema kwa kupata vifaa hivyo walikuwa wanaachama na ukodishaji huo. 

VIONGOZI WAPYA UVCCM WILAYA YA CHAMWINO WAFANYIWA SEMINA KUWAJENGEA UWEZO

$
0
0
Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dodoma Asia Abdulkarim Halamga ameongea na viongozi wa Mashina, Matawi na Kata huko Buigiri Wilayani Chamwino ikiwa ni sehemu ya semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni waweze kutambua majukumu yao, wafanye kazi bila kuingiliana kwa maslahi ya Chama na serikali.

Ameyasema hayo ikiwa ni mpango maalum wa vijana wa Chama cha Mapinduzi kuwapiga msasa viongozi wake ili waweze kuisimamia serikali katika kutekeleza majukumu yake.

Asia Halamga amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa juhudi na uadilifu mkubwa ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na serikali kwa ujumla lakini pia kubuni miradi itakayowawezesha kujitegemea kiuchumi kwani wao ndiyo taswira ya Chama hivyo wanapaswa kuwa mfano bora kwa jamii.

Sambamba na mafunzo hayo pia ametoa kadi 252 za umoja wa vijana UVCCM pamoja na kanuni katika matawi ya Makulu, Buigiri, Mwegamile na Chinangali II ambapo kila tawi limepata kadi 63 kwa lengo la kuongeza wanachama wa UVCCM na sehemu ya malipo yake itumike kutunisha mifuko ya matawi yao.

Naye Diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Kenneth Yindi aliahidi kufanyia kazi Agizo la Katibu wa UVCCM mkoa wa Dodoma la kutatua changamoto ya kutokuwepo kwa ofisi ya Kata kwa kujenga ofisi, Ambapo ujenzi huo unaanza kufanyika mwezi tisa mwaka huu kwa kushirikiana uongozi wa umoja wa vijana na wanachama wake katika Kata ya Buigiri, ambapo Katibu wa UVCCM Mkoa aliahidi mara watakapokuwa tayari atawaunga mkono katika ujenzi wa Ofisi hiyo. 

Pia Diwani alipokea Agizo la kuzitafutia mashamba Jumuiya tatu za Vijana, Wazazi na Wanawake watakayoyatumia kujiingizia kipato ili waweze kujitegea kiuchumi.
  Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dodoma Asia Abdulkarim Halamga akimkabidhi mmoja wa viongozi wa matawi kadi za UVCCM
 Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dodoma Asia Abdulkarim Halamga ameongea na viongozi wa Mashina, Matawi na Kata huko Buigiri Wilayani Chamwino ikiwa ni sehemu ya semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni waweze kutambua majukumu yao, wafanye kazi bila kuingiliana kwa maslahi ya Chama na serikali.

Uamuzi wa kesi ya bangi inayomkabili Wema Sepetu wapigwa kalenda

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, imesema uamuzi wa kupokelewa au kutokupokelewa kwa bangi iliyokutwa nyumbani kwa miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na wenzake wawili utatolewa Septemba 12.

Hakimu Mkazi Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba amesema hayo leo wakati kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Katika kesi hiyo, Wema ambaye pia ni msanii maarufu wa filamu anakabiliwa na mashtaka ya kukutwa na kete mbili za bangi na msokoto mmoja pamoja na wafanyakazi wake wawili, Angelina Msigwa na Matrida Abbas.

Akiahirisha kesi hiyo, hakimu Simba amesema, " nilitakiwa kutoa uamuzi mdogo leo kuhusiana na kielelezo kilichowasilishwa na shahidi wa upande wa mashtaka kama kipokelewe au la, lakini palitakiwa kufanya utafiti wa kutosha kutolea maamuzi, nilijipa muda mdogo sana, tumejadiliana na mawakili wa pande zote mbili na sasa uamuzi utatolewa Septemba 12 na kesi hii itaendelwa hadi  Septemba 13.

Awali ilidaiwa, February mwaka huu, katika makazi ya Wema, Kunduchi Ununio washtakiwa walikutwa na msokoto mmoja na vipisi viwili vya bangi vyenye uzito Wa gramu 1.08

DK.SHEIN ATEMBELEA MIRADI YA WANANCHI WA WILAYA YA KUSINI UNGUJA, ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiangalia Tungule wakati alipotembelea Biashara za Kilimo za Ushirika wa Mtule AMCOS, pamoja na Viongozi wengine wakati alipotembelea katika Ofisi ya Ushirika huo kupata maelezo akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya Wananchi wa Wilaya ya Kusini Unguja,(kulia) Mwenyekiti wa Ushirika wa Mtule AMCOS Bw.Mgana Khamis Zidi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) alipokuwa akiuliza jambo wakati alipotembelea Biashara za Kilimo za Ushirika wa Mtule AMCOS leo pamoja na Viongozi wengine (Pichani) matikiti yaliyouzwa kati ya Shilingi za Kitanzania Elfu tano Mpaka Elfu Nne wakati alipotembelea katika Ofisi ya Ushirika huo kupata maelezo akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya Wananchi wa Wilaya ya Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akifuatana na Mwenyekiti wa Ushirika wa Mtule AMCOS Bw.Mgana Khamis Zidi (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakifuatana mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Ushirika huo leo na kupata maelezo akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya Wananchi wa Wilaya ya Kusini Unguja.

SERIKALI YAAGIZA KUREJESHWA KWA MKANDARASI ALIYEJENGA MRADI WA MAJI CHINI YA KIWANGO

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Or-TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo akizungumza wakati akitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Chamwino wakati wa kukagua mradi wa maji katika Kijiji cha Itiso Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.

Na.Angela Msimbira

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa Mhe Seleman Jafo amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino kumrudisha Mkandarasi na Mtaalam mshauri waliojenga mradi wa maji kijiji cha Itiso kilichopo Wilayani Chamwino kutokana na kujenga mradi huo kinyume na mkataba uliotolewa na Serikali na chini ya kiwango.

Mhe. Jafo Ametoa agizo hilo wakati alipotembelea Mradi wa Maji wa Itiso uliokuwa ukisimamiwa na Kampuni ya Audancia kwa kusimamiwa na Mtaalam Mshauri O&A Company Limited uliogharimu kiasi cha shilingi 338,676,323. Mhe. Jafo amesema kuwa Mkandarasi pamoja na mshauri wameondoka kwenye mradi kabla mradi kukamilika kitendo ambacho kinaisababishia hasara serikali ambapo fedha ambazo zilitakiwa kutumika kukidhi mahitaji ya wananchi zinapotea.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Or-TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo akikagua moja ya kichoteo cha maji wakati wa ziara ya kukagua mradi wa Maji katika kijiji cha Itiso katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.

Mhe Jafo amesema hajaridhika na kazi iliyofanywa na Mkandarasi Audancia aliyejenga mradi wa maji kijijini Itiso kutokanana kulaza mabomba yaliyo chini ya kiwango na ni kinyume na mkataba aliopewa na Serikali.

“Nimesikitishwa na Mkandarasi wa Mradi wa Maji Itiso kwa kuwa amelaza mabomba yaliyo chini ya kiwango tofauti na mkataba aliopewa na Serikali na kusababisha wananchi wa kijiji cha Itiso kukosa kupata maji kwa wakati na kurudisha nyuma juhudi za serikali za kuleta maendeleo kwa wananchi.

Amesema Serikali imekuwa ikiwekeza fedha nyingi ili iweze kutekeleza miradi ambayo itasaidia wananchi lakini miradi mingi hujengwa chini ya kiwango na kutokamilika kwa wakati na hivyo kurudisha nyuma maendeleo kwa wananchi.

“Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika kujenga miradi ya maji lakini miradi mingi imekuwa haikamiliki kwa wakati na kusababisha malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuwa serikali haitimizi ahadi zake“ Amesema.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Seleman Jafo akimsikiliza Fundi Sanifu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bw. Stephen Mzuri akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa kisima cha Maji kilichopo katika Kijiji cha Itiso Halmashauri iya Wilaya ya Chamwingo.

Amewaagiza watumishi waliopewa dhamana yakusimamia miradi ya maendeleo kuhakikisha wanatumia weledi wa kazi yao kuhakikisha  miradi yote  ya  Serikali inamalizika kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa na waache kufanya kazi kwa mazoea. “Watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia Miradi ya Maendeleo wanatakiwa kutimiza wajibu wao katika kuleta maendeleo kwa wananchi”

Akisoma taarifa ya Mradi wa Maji Itiso Fundi  Sanifu Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bw. Stephen Mzuri amesema Mradi wa maji Kijiji cha Itiso ulianza kujengwa mwaka 2013 na kukamilika mwaka 2014 na kujengwa na Kampuni ya Audancia kwa kusimamiwa na Mtaalam Mshauri O&A Company L.T.D uliogharimu shilingi  milioni 338,676,323/=.

Amesema kuwa kulingana na mkataba Mkandarasi alitakiwa kulaza mabomba ya Class C kwenye laini inayotoa maji kwenye kisima na kupeleka kwenye tanki lakini mkandarasi alilaza mabomba ya class B. Pia kuvuja kwa maji na vichoteo viwili kati ya vichoteo nane havikuwa vinatoa maji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Or-TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo akikagua mashine ya kusukuma Maji kwenye ziara ya kukagua mradi wa Maji katika kijiji cha Itiso katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.

Bw.Mzuri amesema mpaka sasa vichoteo vitano kati ya kumi vinatoa huduma ya maji kijijini na vichoteo vilivyosalia vinaendelea kufanyiwa marekebisho vitakapokamilika mradi utahudumia watu zaidi ya wananchi 6000.

Aidha, Mbunge wa Chilonwa Mhe.Joel Mwaka amempongeza Naibu Waziri kwa kutembelea kijiji cha Itiso na kuangalia mradi wa maji uliokuwa ukisuasua tangu mwaka 2013 na kusababisha wananchi kutokupata maji katika kijiji cha Itizo kwa muda mrefu. 
Viewing all 110095 articles
Browse latest View live




Latest Images