Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

TADB yatoa ‘sapoti’ Nane Nane Kitaifa

$
0
0
 Meneja wa Mikopo wa TADB, Samuel Mshote (kulia) akiwaonesha wanahabari ujumbe wa Maadhimisho ya Nane Nane kwa mwaka 2017 kabla ya makabidhiano rasmi ya fulana na kofia kwa Kamati ya Maandalizi ya Nane Nane kitaifa mjini Lindi.
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (wapili kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kulia) wakisoma ujumbe wa maadhimisho ya Nane Nane kwa mwaka 2017. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Bw. Shaibu Ndemanga (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Simon Migangala (kulia).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kulia) akimkabidhi fulana na kofia Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (kushoto) zitakazotumika wakati wa kilele wa Maadhimisho ya Siku na Nane Nane kitaifa mjini Lindi.
Na Mwandishi wetu,
KATIKA kudhirisha umuhimu wa Siku ya Nane Nane Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeunga mkono kwa kutoa fulana na kofia zitakazovaliwa katika siku ya kilele cha maadhimisho hayo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Wageni Maalumu uliopo katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alisema kuwa TADB imeonesha mfano kwa taasisi nyingine nchi kwa kutambua umuhimu wa Nane Nane inayofanyika kitaifa mkoani humo.
“Tunaishukuru sana TADB kwa mchango huu ambao kwa hakika utang’arisha maadhimisho yetu,” alisema.
Bw. Zambi aliongeza kuwa mchango huo unachagiza kauli mbiu ya Maonesho hayo isemayo “Zalisha kwa tija mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati”.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa Benki ya Kilimo imeunga mkono Maonesho hayo ya Nane Nane kwa kutambua umuhimu wa kilimo na kutimiza malengo ya Benki hiyo katika kusaidia kilimo nchini.
“Mchango huu unasadifu malengo ya kuanzishwa kwa TADB ambayo yanajumuisha Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania; na Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema Bw. Assenga.
Maadhimisho ya maenesho hayo yatafikia kilele siku ya tarehe 08 ambapo Mgeni rasmi wa anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.

WAZIRI MAGHEMBE ASHUSHA TOZO ZA BARABARA KWA MITI YA MIKARATUSI IRINGA

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amepunguza bei ya miti aina mikaratusi kuanzia mwaka huu ambapo ada ya tozo za barabara imepunguzwa kutoka shilingi 35,000 hadi shilingi 17,800.

Waziri Maghembe amefikia hatua hiyo mara baada ya wadau kumuomba Waziri aweze kupunguza bei ya miti hiyo.Wakati huo huo Waziri Maghembe amepiga marufuku kwa wanavijiji waojaribu kumega eneo la msitu kwa ajili ya shughuli nyingine

"Hakuna kipande chochote cha ardhi katika shamba hili kitakachochukuliwa kwa ajili ya shughuli nje ya hii inayofanyika kwa sasa nasisitiza vijiji viendelee kupata fedha za mgawo wa miti ili watumie kwa shughuli za maendeleo." amesema Maghembe

Wadau wa Shamba la miti la Sao Hill wamempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Maghembe kwa utaratibu mzuri wa ugawaji wa malighafi ya miti kwa kuwa umesaidia kuwaondoa madalali waliokuwa wanapewa mgawo na kisha wao kuwauzia wenye viwanda kwa bei ya juu.

Waziri Maghembe amesema kuwa ugawaji wa malighafi ya miti kwa mwaka huu umefanywa kwenye wenye viwanda tu ili kuhakikisha wanakuwa na malighafi ya kutosha kwa ajili ya kuendeleza viwanda

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya tano ni ya viwanda hivyo wadau hao wasiishie kupasua mbao pekee wahakikishe wanatengeneza bidhaa kama vile samani katika viwanda vyao.Amesema lengo la Serikali siyo kuishia kugawa malighafi ya miti na kupasua mbao, bali ni kutengeneza viwanda vya mazao ya mbao.

Katika hatua nyingine, Waziri Maghembe amewaagiza wadau wanaotumisa misumeno aina ya Ding dong kuacha mara moja kwa ina ufanisi hafifu na zinapoteza kiasi kikubwa cha magogo badaala yake waanze kutumia za kisasa.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema kuwa utaratibu uliotumika mwaka huu wa ugawaji wa malighafi umekuwa mwarobaini wa kupunguza malalamiko kwa wadau ukilinganisha na miaka iliyopita Aidha, aliawapongeza wafanyabiashara na wadau wa shamaba hilo kwa kulipa kodi stahiki za Serikali.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Wadau wa Shamba la Miti wa Sao Hill katika kikao kilichofanyika jana mjini Mafinga Mkoani Iringa
Baadhi ya Wadau wa Shamba la Miti wa Sao Hill wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe katika mkutano uliofanyika mjini Mafinga mkoani Iringa

ROSE MMBAGA ASHINDA TUZO YA MWANAMKE MWENYE USHAWISHI

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Msichana wa kitanzania, Rose Mmbaga ameweza kushinda tuzo ya Mwanamke mwenye Ushawishi ‘Women in Events Hall of Fame’ ya nchini Marekani na kuwa ni Mwafrika pekee katika kusaidia vijana katika maswala ya masuala ya Mazingira.

Mmbaga ameshinda tuzo hiyo kutokana na uwezo wake wa ushawishi katika kazi za kijamii ambazo amezifanya nchi nzima.

Amesema kuwa Safari yake ilianza na kujitolea kwa takribani miaka mitatu baada ya kuona ajira zinasumbua, na alianza na VSO international kwenye mradi wa International Citizen Service alafu nikajiunga na Restless development katika mradi wa kijana tung’are kazini chini ya International Citizen Service programu kwa takribani miezi sita na tena nikaenda Raleigh Tanzania kwenye mradi wa Expedition.

“nilijenga shule kusaidia watoto yatima,mashirika yote nilishirikiana na vijana kutoka ndani na nje ya nchi na miradi ilifadhiliwa na DFID yani serikali ya wingereza.Haikua rahisi lakini leo hii naweza kuona matunda ya kujitolea katika jamii yangu.”amesema Rose.

Kupitia safari yangu leo hii nimeweza kupata tuzo ya kimataifa kutoka Association for women in events,Hall of fame kama “Woman of Influence”(Mwanamke mwenye ushawishi) ambayo walioniwezesha ni watu ambao wanafahamu kazi yangu na nilioshirikiana nao katika kazi zangu haswa vijana wa kitanzania na wengi wao ni wale waliojitolea

Amesema pongezi zinamwendea mwanaharakati wa kuwasaidia wanawake duniani Mandy Sanghera ameweza kuwa wa kwanza kuninominate jina langu kati ya wanawake wengi na leo hii ninamshukuru kwa kupitia yeye nimeweza kushinda.

JWTZ wapokea vifaa vya michezo kutoka NMB

$
0
0
   BENKI ya NMB leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) inayotarajia kushiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki itakayofanyika jijini Bujumbura - Burundi. Vifaa vilivyokabidhiwa leo ni pamoja na mipira kwaajili ya timu ya mpira wa miguu, mipira ya mchezo wa mikono (wasichana) na mipira mchezo wa kikapu kwa wanaume (Basket ball).

 Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa JWTZ - Kanali Richard Mwandike, Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB - Boma Raballa alisema vifaa vingine ni pamoja na mipira 10 ya mchezo wa volebo (Volleyball), jezi 42 za mpira wa miguu, seti mbili za jezi mpira wa kikapu (wasichana), seti mbili za jezi mpira wa basket na seti mbili za jezi mpira wa Volleyball.

 Vifaa vingine vilivyokabidhiwa ni pamoja na seti mbili za jezi za waamuzi kwa michezo ya Netball, Basketball, Volleyball na mabegi 30 ya wachezaji ambapo vyote kwa ujumla vina thamani ya shilingi milioni 10 za Kitanzania. Bw. Raballa alisema kuwa msaada huo umetokana na ushirikiano mzuri na wa muda mrefu kati ya benki ya NMB na jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) na ndiyo maana wakaona umuhimu wa kuendelea kuwashika Mkono kupitia msaada kwa timu za jeshi zinazoenda kushiriki mashindano ya majeshi ya jumuia ya afrika ya mashariki. 

 "...Hii si mara ya kwanza kusaidia katika mashindano haya, kwani nakumbuka hata mwaka jana tuliwasaidia baadhi ya vifaa vya michezo kushiriki katika mashindano haya. Tunaamini vifaa hivi mbali na kuendeleza ushirikiano wetu mzuri, vitakuwa chachu ya kufanya vizuri katika mashindano haya muhimu kwa jumuia ya Afrika ya Mashariki," alisema Raballa. 
Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB - Boma Raballa (kushoto) akimkabidhi vifaa mbalimbali vya michezo Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) - Kanali Richard Mwandike (kulia) leo jijini Dar es Salaam. 
Vifaa hivyo mbalimbali vya michezo zikiwemo jezi, mipira na vifaa vingine vyenye thamani ya shilingi milioni 10, vitatumiwa na wachezaji wa timu ya JWTZ wanaotarajia kusjiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Agosti 24, 2017.Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB - Boma Raballa (kushoto) akimkabidhi vifaa mbalimbali vya michezo Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) - Kanali Richard Mwandike (kulia) leo jijini Dar es Salaam. Vifaa hivyo mbalimbali vya michezo zikiwemo jezi, mipira na vifaa vingine vyenye thamani ya shilingi milioni 10, vitatumiwa na wachezaji wa timu ya JWTZ wanaotarajia kusjiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Agosti 24, 2017.Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) - Kanali Richard Mwandike (kulia) akimshukuru Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB - Boma Raballa (kushoto) mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo leo jijini Dar es Salaam vilivyotolewa na NMB kuwezesha timu ya JWTZ kushiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Agosti 24, 2017.Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB - Boma Raballa (kushoto) akimkabidhi vifaa mbalimbali vya michezo Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) - Kanali Richard Mwandike (kulia) leo jijini Dar es Salaam. Vifaa hivyo mbalimbali vya michezo zikiwemo jezi, mipira na vifaa vingine vyenye thamani ya shilingi milioni 10, vitatumiwa na wachezaji wa timu ya JWTZ wanaotarajia kusjiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Agosti 24, 2017.

  

Angalia Mwezi Ukipatwa Leo Jioni

KATIBU MKUU NYAMHANGA AAGIZA UJENZI WA MIZANI BARABARA YA DODOMA – BABATI (KM 263)

$
0
0
 Mhandisi Mshauri wa barabara ya Mayamaya – Mela (km 99.35), Eng. Leornado Licari, akitoa maelezo ya mradi wa barabara hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (wapili kushoto), alipofanya ukaguzi mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, amewaagiza Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma na Manyara kuhakikisha wanatafuta eneo la kujenga kituo cha mizani ili kudhibiti madereva wanaozidisha uzito katika barabara ya Dodoma- Babati (km 263), inayojengwa kwa kiwango cha lami.

Akizungumza katika eneo la Bonga, mkoani Manyara Eng. Nyamhanga, amesema kuwa barabara hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika baadae mwezi huu inahitaji uwepo wa mizani kwa haraka ili kudhibiti  magari yanayozidisha uzito na kuharibu barabara. 

"Hakikisheni mnatafuta eneo la kujenga mizani ndani ya miezi miwilli ambapo wakandarasi bado wapo hapa ili iwe rahisi kwenu kumtumia mmoja wa wakandarasi hawa kuweza kujenga kituo hiki haraka, uwepo wa mizani hii utasaidia kudhibiti magari makubwa yanayozidisha uzito", amesema Katibu Mkuu Nyamhanga.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, akikagua kingo za daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205 linalounganisha wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.

Aidha, Eng. Nyamhanga amewaagiza mameneja wote nchini kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu wote wanaopitisha mifugo katika barabara ili kudhibiti uharibifu wa barabara.

Amewataka  madereva wote nchini kuendesha magari yao kwa tahadhari na kuzingatia alama za barabarani ili kudhibiti ajali zinazoepukika.
Katibu Mkuu Nyamhanga ametoa wito kwa wananchi wanaoishi kando ya barabara hiyo kuhakikisha wanatumia fursa ya kukamilika kwa barabara hiyo kwa ajili ya kuleta maendeleo katika maeneo yao ili kukuza uchumi kwa familia zao na Taifa kwa ujumla.

Amemataka  mkandarasi wa sehemu ya barabara ya Mela - Bonga (km88.8)  kuhakikisha anakamilisha kazi zilizobaki kwa wakati na kwa viwango vilivyo kwenye mkataba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa kampuni ya CHICO anayejenga sehemu ya barabara ya Mayamaya – Mela (km 99.35), alipofanya ukaguzi mkoani Dodoma.

Katika hatua nyingine, Eng.Nyamhanga, ametembelea na kukagua barabara ya Mayamaya- Mela (km 99.35) kwa kiwango cha lami na daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205 na kuridhishwa na ujenzi wake na kumtaka mkandarasi wa mradi huo kukabidhi mradi huo ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAS Mbeya Afungua Mafunzo ya Mfumo Mpya wa Kuandaa Mipango na Bajeti katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa

$
0
0
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mariam A. Mtunguja akisisitiza jambo mbele ya watumishi wa umma kutoka mikoa ya Songwe, Iringa, Njombe na Mbeya alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina ya siku nane juu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Kisekta  (PlanRep)  leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID). Watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa hiyo
 Kiongozi wa wawezeshaji Bw. Frank Makua Charles akichokoza mada wakati wa semina katika akichokoza mada wakati siku ya kwanza ya semina ya siku nane kuhusu Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hii ya siku nane inaendeshwa kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID)ambapo imeshirikisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.
 Mwakilishi wa Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Makao Makuu Dar es Salaam Dkt. Gemini Mtei akielezea jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa semina ya siku nane juu ya Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID). Semina hii imewahusisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.
Mwakilishi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Bw. James Mtatifikolo akifafanua jambo wakati wa  hafla ya ufunguzi wa semina ya siku nane juu ya Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID). Semina hii imewahusisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.
 Baadhi ya washiriki wa semina ya siku nane kuhusu Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) wakifuatilia mada wakati wa ufunguzi wa semina hiyo leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inayoendeshwa kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya  Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID). Semina hii imewahusisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Wachumi, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama,  Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Radio Times Fm yazindua Msimu Mpya wa Mapinduzi ya Burudani

$
0
0
Kituo cha kurusha matangazo cha Radio Times Fm leo Agosti 07, 2017 kimezindua rasmi msimu wake mpya wa Mapinduzi ya Burudani na kutambulisha ratiba mpya ya vipindi na Logo mpya yenye muonekano wa rangi ya purple.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mapema hii leo, Msimamizi wa vipindi na uzalishaji wa Radio Times Fm Amani Missanah amesema kuelekea miaka 18 ya Times Fm Agosti 28 wameamua kubadili muonekano wa kituo hicho wenye mlengo wa kuwafikia watanzania wengi zaidi na kuwagusa kwa taarifa za ukweli na uhakika na burudani isiyo na kifani.

Amesema dhamira ya kubadili muonekano ni pamoja na kuendana na maudhui ya kituo hicho kwa kuwa wabunifu na watatuzi wa Matatizo ya kijamii kama ilivyo kawaida ya Times Fm kwa Kupitia Vipindi vyake vilivyoboreshwa zaidi. “Lengo letu la kubadili muonekano na kutumia rangi ya purple ni kuonesha Busara iliyonayo Times Fm kwa wasikilizaji ,Heshima, lakini pia Mamlaka.

(Ni rangi iliyotumiwa na matajiri wengi wakubwa wa kihistoria) lakini pia Wafalme, mfano Daudi hata pia Yusuph na hata madhabauni pia Inamaanisha utajiri” Miongoni mwa rangi zingine zilizoanza kutumika ni pamoja na rangi ya Orange inayohamasisha uchangamfu na kuonesha mtu ambaye yupo optimistic zaidi. Aidha amesema rangi Nyeupe Inamaanisha usafi, na kumaanisha Neutrality, pia ni rangi ihamasishayo Ubunifu ndani yake.

Akiongea kupitia kipindi cha Maisha Mseto kinachoongozwa na Stanslaus Lambart, Florah Matthew na Fredrick Mabula amevitaja vipindi hivyo vya wiki kuwa ni Maisha Mseto, Mitikisiko ya Pwani ,The PlayList ambayo kwa sasa itafanyika mchana kuanzia saa nane hadi saa kumi na mbili jioni, Wizara ya Michezo, Habari Xtra, Campus Vibes na Pillow Talk.

Upande wa vipindi vya wikiendi alisema ni ‘HABA NA HABA, Student Center, Dira Yetu,Deejays Battle ,Mita Mia,Request Zone,Afro Vibes,Gospel Hits ,Charts,Chipuka,Mambo ya Fedha,Bongo Dot Home,Old schools,Sunday Slowjam. “Times Fm hivi karibuni inatarajia kuanza kusikika katika mikoa mbali mbali ikiwemo mikoa ya Dodoma na Mbeya ,pia tunazo frequency za Mikoa mingine ambayo ni Tanga ,Morogoro,Iringa ,Songea ,Arusha Kilimanjaro na Mwanza ambapo tunataraji kuanza kusikika hivi punde .

Amewataka wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kufanya matangazo na Times Fm kwa punguzo kubwa la bei kwa wafanyabiashara ndogondogo na kubwa na kutoa fursa ya kutumia gari la kisasa kabisa la kurushia matangazo hapa nchini Tanzania OB-VAN .

Waziri Lukuvi Akabidhi hati zaidi ya 4000 Dar

$
0
0

Na Jonas Kamaleki-MAELEZO

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amekabidhi hatimiliki 88 kwa wakazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam kati ya 4333 ambazo ziko kwenye hatua za mwisho katika mradi wa urasimishaji wa makazi holela.

Akikabidhi hatimiliki hizo, Mhe. Lukuvi amesema hizi hati ni mtaji uliofufuliwa baada ya wakazi kukakaa na kuendeleza maeneo yasiyopimwa yaani mtaji mfu kwani hakuna mtu yeyote ambaye angewezakupata mkopo bila hati.

Mhe. Lukuvi amesema kuwa Serikali ya Aawamu ya Tano inayo dhamira ya dhati ya kurasimisha makazi nchi nzima ili kuongeza thamani ya ardhi au maeneo husika. Ardhi yenye hatimiliki thamani yake inaongezeka kwani inatambuliwa na taasisi za fedha ambazo ni rahisi kukuopesha wenye hati.

“Kwa hati hizi zilizotolewa takribani 4333 tukisema kila nyumba ikopeshwe kwa kiwango cha chini cha shilingi milioni 10, kwa siku ya leo Kimara inapata mtaji wa karibu bilioni 40.5,”alisema Mhe. Lukuvi.

Aliongeza kuwa maeneo yote ya miji ambayo hayajapimwa, yapimwe na halmashauri na manispaa zote nchini ili kuyaongezea thamani na kuondokana adha ya watu kujenga kwenye makazi holela.
 Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi  akizungumza leo na wananchi wa mtaa Lungule juu ya kudhibiti matapeli wa ardhi, na migogoro mbalimbali ya ardhi hapa nchini.
Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob akizungumza mbele ya Wananchi leo katika hafla ya kukabidhi hati 88  kwa wakazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi mtaa Lungule waliokabidhiwa hati wakiwa katika picha ya pamoja.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

NBS YAWATAKA WADAU WA TAKWIMU KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA UTOAJI TAKWIMU

$
0
0

Na Bushiri Matenda Na Agness Moshi - MAELEZO

Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS) imetoa rai kwa wadau wa Takwimu Nchini kufuata kanuni na taratibu za utoaji takwimu ili kuepusha sintofahamu baina yao, wapokeaji taarifa na Taasisi husika .

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa wakati akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo kufuatia taarifa zisizo sahihi zilizotolewa na Kampuni ya Utafiti ya Geopoll yenye ofisi ya Kanda ya Afrika, mjini Nairobi, Kenya kuhusiana Viwango na Idadi ya watazamaji wa vituo mbali mbali vya habari vinavyorushwa hapa nchini .

“Taarifa zozote zinazohusu utafiti ni lazima zihusishe wadau mbalimbali, na kwa kuzingatia vigezo vyote vinavyotakiwa na mamlaka iliyoidhinishwa kisheria kuhusiana na utoaji takwimu”, Dkt.Chuwa alivitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na uwazi na ukweli, uhusishwaji wa Wadau na kwa kuzingatia weledi.

Aidha, amefafanua kuwa ni vyema Taasisi yoyote inayotaka kukusanya taarifa mbalimbali za takwimu ni budi kushirikisha wahusika ili kuepusha mkanganyiko na upotoshwaji kama ilivyofanywa na Kampuni hiyo kutoka Nairobi, Kenya.

“Takwimu zinazotolewa bila kuzingatia taratibu zinazohitajika hazitatambulika na Serikali kwani utoaji wa Takwimu haufanywi kama unavyohesabu migomba shambani, hivyo ni lazima wahusika wafuate taratibu zote”, alifafanua Dkt.Chuwa.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015. Kwa mujibu wa Sheria hiyo, NBS imepewa mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji wa Takwimu rasmi kwa ajili ya matumizi ya Serikali na Wadau wa Takwimu.
Mkurugenzi mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Habari maelezo Jijini Dar es Salaam , kushoto Bw. Ephraim Kwisigabo Mkurugenzi Sensa na Takwimu za jamii.

MBUNGE KIBAHA VIJIJINI AWASAIDIA WANANCHI JIMBONI KWAKE

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha Vijijini 
MBUNGE wa jimbo la Kibaha Vijijini, mkoani Pwani  Mhe. Hamoud Jumaa (pichqni) , ametoa msaada wa sh.milioni 2.3 kwa mkazi wa kata ya Janga, Selemani Mgoto (43) ambaye alipata upofu kutokana na kudhurika na vidonge vya malaria vya 'fansidar' mwaka 2012.


Aidha mbunge huyo, amesema ataendelea kumshika mkono Mgoto kwa kumalizia ujenzi wa nyumba anayojenga. Jumaa pia ,anamjengea nyumba kada wa chama cha mapinduzi (CCM) ambaye aliwahi kukitumikia chama zaidi ya miaka 30, mzee Shabani Kifaru (80), mkazi wa kata ya Magindu.


Akizungumza wakati akikabidhi fedha hizo, Jumaa  alisema ataendelea kutatua changamoto za jimbo pamoja na kusaidia makundi maalum. Alieleza, ametoa fedha hizo kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa mtu huyo kuliko chakula ambacho angekula na kuisha.


Alisema licha ya Mgoto kuathirika macho yake lakini anaishi kwenye maisha ya kupanga hivyo nyumba anayojenga itamwezesha kuishi vizuri. Nae Mgoto ,alimshukuru Jumaa kwa msaada aliompatia na kumuomba asichoke kumshika mkono. Hata hivyo, aliwashukuru wadau wengine ambao wameweza kumsaidia tangu apate matatizo yake.

"Mbunge una watu wengi wa kuwasaidia lakini umeniona na mie, naahidi kuzitumia fedha hizi kwa matumizi lengwa ,nilianza ujenzi huu lakini ninekwama kumalizia "alisema Mgoto.

Vijana kutoka Mji wa Vallejo, California watembelea Ubalozi wetu Washington D.C.

$
0
0

Vijana sita wa Kimarekani kutoka Mji wa Vallejo, California,  (Sister City International) leo  wametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani jijini  Washington D.C. Mji wa Vallejo ni Mji Dada na Mji wa Bagamoyo. Lengo la ziara yao ni  kujua na kujifunza masuala mbalimbali kuhusu Tanzania, kwa kuwa wanatarajia kutembelea mji wa Bagamoyo mwaka 2019.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson M. Masilingi (kati) na afisa wa ubalozi Bw. Dismas Assenga (kulia) wakiwa na vijana  hao sita kutoka mji wa Vallejo, California

RAIS MHE.DKT. MAGUFULI AREJEA JIJINI DAR ES SALAAM NA KUHUTUBIA WANANCHI WA BUNJU B

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Bunju wakati akirejea jioni ya leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano katika mkoa wa  Tanga. 
 Baadhi ya wananchi wa eneo la Bunju wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza aliposimama eneo hilo kwa ajili ya kuwasalimia wakati akirejea jioni ya leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano katika mkoa wa  Tanga. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

LIVE: KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA KENYA

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 07.08.2017


MAGAZETI YA JUMANNE LEO AGOSTI 8,2017

BAADHI YA MABANDA KATIKA MAONESHO YA NANENANE MKOANI LINDI YAKITOA HUDUMA KWA WANANCHI.

$
0
0
 Afisa Rasilimali watu wa Kurugenzi ya Rasilimali Watu na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Peter Valerian akiwapa maelezo wananchi waliotembelea Banda la BoT  katika maonesho ya Nanenane kwenye  viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Afisa wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Tawi la Mtwara, Denis Malosha akitoa maelezo ya utoafautishaji Noti bandia na Noti halali  kwa wananchi waliotembelea banda la BoT katika maonesho ya Nanenane kwenye  viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Afisa wa BoT, akionesha noti chakavu ambazo wananchi hawapo (pichani) wamezipeleka katika maonesho ya Nanenane kwenye  viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Wananchi wakipata maelezo katika maeneo tofauti ndani ya banda la BoT katika  maonesho ya Nanenane kwenye  viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Afisa Uhusiano wa Tazara, Regina Tarimo akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea Banda la Tazara katika maonesho ya Nanenane kwenye  viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
Meneja wa Kitengo cha Hali ya Hewa Kilimo wa TMAA , Isack Yona akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la mamlaka ya hali hewa nchini TMAA, katika  maonesho ya Nanenane kwenye  viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

Spika Mstaafu Anna Makinda atembelea banda la Benki ya DCB katika maonyesho ya nane nane Dodoma

$
0
0
Spika Mstaafu Anna Makinda ameipongeza DCB Commercial Bank kwa huduma bora za kibenki inayotoa hasa huduma za mikopo kwa wajasirimali wadogo wadogo na kuwakwamua katika hali ya umasikini.

Makinda amewaasa DCB Commercial Bank kujikita zaidi kutoa huduma hii kwa  wajasiriamali wadogo wadogo vijijini ambao ndiyo wengi nchini ili kuboresha hali za maisha yao kwa kuwapatia mikopo.

Hayo aliyasema wakati alipotembelea banda la DCB Commercial bank katika maonesho ya nane nane kanda ya kati yanayoendelea mkoani Dodoma. Makinda aliongezea kuwa ili kuwezesha wajasiriamali wengi DCB Benki haina budi kupeleka huduma hii ya mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo wadogo vijijini ambako kuna uhitaji mkubwa wa huduma hii ya mikopo ya vikundi Sambamba na utoaji wa mikopo hii ya vikundi kwa wajasiriamali wadogo wadogo.

Makinda ameasa DCB kuwaunganisha wajasiriamali hawa na huduma ya bima ya afya kutoka NHIF na pia bima ya taifa ya Jamii ili wateja hawa au familia zao wanapougua wapate msaada wa matibabu kwa unafuu hivyo kuwafanya wawe na afya na kuweza kurejesha mikopo .
Spika Mstaafu Anna Makinda akikaribishwa na Mkuu wa Masoko wa benki ya kibiashara ya DCB Boyd Mwaisame katika banda lao katika Maonesho ya Nane nane yanaoendelea Mkoa wa Dodoma.
Spika Mstaafu Anna Makinda akisoma moja ya kipeperushi cha benki ya DCB
 katika banda lao katika Maonesho ya Nane nane yanaoendelea Mkoa wa Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Masoko wa benki ya kibiashara ya DCB Boyd Mwaisame

Wananchi wakipatiwa huduma katika banda la benki ya DCB katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mkoani Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

VETA KUSHIRIKIANA NA JKT KATIKA MAFUNZO YA UFUNDI STADI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Lindi.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo ameiomba Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kubuni mpango maalum wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wanaoingia katika mafunzo ya JKT ili wakitoka katika makambi waweze kupata fursa za ajira katika maeneo mbalimbali.

Meja Isamuhyo alitoa ombi hilo Jumatatu, Agosti 7, 2017 alipotembelea kwenye banda la VETA, katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Ngongo, mkoani Lindi.

Alisema vijana wanapoingia katika makambi ya JKT hupata mafunzo ya uzalendo na ukakamavu kwa kipindi cha takribani miezi mitatu na kisha kuingia katika  mafunzo ya stadi za maisha na stadi za kazi kwa kipindi kipatacho miezi 18.

Alifafanua kutokana na mgawanyiko huo wa mafunzo ya JKT, VETA kwa kushirikiana na jeshi hilo wanaweza kuweka mpango maalum wa kutumia kipindi cha miezi 18 ya mafunzo ya stadi za kazi na stadi za maisha kuandaa mafunzo ya ufundi stadi ili kuwapatia vijana ujuzi utakaowawezesha kuajirika baada ya kuhitimu JKT.

Alisema JKT wamekuwa wakitoa mafunzo ya ufundi stadi mbalimbali, lakini changamoto imekuwa ni kukidhi vigezo vya kutunuku vyeti vinavyotambulika na VETA, kwani kipindi cha miezi minane ni kifupi katika kukidhi matakwa ya mitaala ya VETA.
 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo akipata maelezo kutoka  Mtaalam wa Kutathimini mafunzo  wa VETA  Joyce Mwinuka  juu ya VETA inavyofanya kazi katika kuwajenga vijana katika mafunzo ya elimu ya ufundi stadi katika maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo akipata maelezo kutoka kwa Meneja uhusiano wa VETA, Sitta Peter wakati mkuu wa JKT alipotembelea maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo akipata maelezo wa tofari ambazo zinaokoa gharama kutokana mazingira ambayo kila mwananchi anaweza kumudu wakati mkuu wa JKT alipotembelea maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Shamba darasa la JKT ndani maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAARIFA KWA UMMA JUU YA UPATIKANAJI WA FEDHA SHILINGI MILIONI MIA MBILI KWA AJILI YA MAJI NA MIUNDOMBINU YA MAJI NDANI YA JIMBO LA NZEGA MJINI

$
0
0

Na Godfrey Robert Malema
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini  Mhe. Hussein Mohammed Bashe anapenda kuwataarifu umma ya kuwa tayari serikali imetoa fedha kiasi cha Shilingi Milioni Mia Mbili (Tzs 200,000,000) maalum kwa ajili ya kutatua matatizo au kero za maji na miundombinu ya maji ndani ya Jimbo la Nzega Mjini.
Kupatikana kwa fedha hizi ni matokeo ya Mhe. Hussein Bashe kumuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu wakati wa ziara ya kikazi ya Rais mkoani kwetu.
Ili kuhakikisha tunafikia malengo yaliyokusudiwa; Usimamizi wa fedha hizi hautafata taratibu za tenda ila utafuata utaratibu wa kuwa na timu ya pamoja itakayojumuisha Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi, Ofisi ya Mbunge, Mamlaka ya Maji, Madiwani wa Kata ya Nzega Mjini Magharibi, Nzega Mjini Mashariki na  Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa katika maeneo ambayo yatahusika na ukarabati huu mkubwa.

Aidha; Matumizi ya Fedha hizi yatajumuisha Usafishaji na Ukarabati wa Bwawa la Uchama;  Ukarabati wa Miundombinu ya Maji  ili kusaidia maji kuweza kufika maeneo ya mbali; Ujenzi wa Maghati Matano (5) kutoka Nyasa Mahakamani hadi Stendi Mpya; jambo hili litafanikisha ujenzi wa mtandao mpya wa maji wenye urefu wa zaidi ya mita 200 kupitia mtaa wa Uswilu.
Hivyo; Ofisi ya Mbunge inawataka madiwani wote kushirikiana na Wenyeviti wa serikali za Mitaa kuweza kubaini na kupendekeza maeneo sahihi ya ujenzi wa Maghati haya mapya.
Kipekee kabisa, Mheshimiwa Hussein Bashe anapenda kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwa namna anavyoendelea kushirikiana na wananchi wa Jimbo la Nzega Mjini katika kutatua kero mbalimbali ikiwemo kero na kilio cha muda mrefu juu ya Ukosefu wa Maji.

Na mpaka sasa tayari Rais anakua ametimiza ahadi yake ya kutupatia Tzs 400,000,000 ambazo nilimuomba nyakati tofauti ili kutatua changamoto kubwa za shida ya maji jimboni.
Kwa upande mwingine Mbunge anapenda kuwashukuru Waziri wa Maji Mhe. Gerson Lwenge na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhe. Prof. Kitila Mkumbo pamoja na watumishi wote wa Wizara hii kwa namna ambavyo wamekua wakishirikiana nasi katika kusaidia kupunguza matatizo ya maji ndani ya Jimbo la Nzega Mjini huku tukisubiria kukamilika kwa Mradi Mkubwa wa Maji wa Ziwa Victoria.
Mwisho, Ofisi ya Mbunge inapenda kusisitiza ya kuwa ni wajibu wetu wote kuhakikisha tunalinda vyanzo vyetu vya maji na kutoshiriki kwa namna yeyote katika kuharibu miundombinu ya maji ndani ya Jimbo la Nzega Mjini na mahali popote nchini ili kuvilinda na kuviendeleza vyanzo vilivyopo kwa matumizi endelevu ya kizazi kilichopo na vizazi vijavyo.


Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images