Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1847 | 1848 | (Page 1849) | 1850 | 1851 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Baadhi ya Wakandarasi nchini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upitaji wa magari makubwa bila ya kuwa na vipimo maalum, hali hiyo imekuwa ikiharibu miundombinu ya barabara,huku wakibainishwa kuwa wamekuwa wakitumia gharama kubwa ya kufanya marekebisho mbalimbali kabla ya kukabidhi barabara hizo kwa Serikali.

  Hayo yameelezwa leo na mmoja wakandarasi kutoka Kampuni ya Caberisa Co.Ltd Bernad Mgohamwende ambae anajenga barabara kwa kiwango cha changalawe yenye urefu wa kilomita 36, eneo la barabara ya mbauda ,Osunyai iko katika kiwango cha changarawe,barabara hiyo ipo katika hatua za mwisho kukabidhidhiwa katika wilaya ya Arusha,Mkoa wa Arusha.

  Mkanadarasi huyo amesema kuwa katika utekelezaji wa kujenga barabara hizo ,Serikali itaweka utaratibu wa kupima magari hayo ili kusaidia kutunza barabara hizo na wao za kutotumia gharama kubwa kuzirekebisha .

  Bila Serikali kuweka vipimo maalumu katika barabara zetu, italazimika kutoa pesa mara kwa mara kuwalipa wakandarasi kwa ajili ya kufanya marekebisho,jambo ambalo itazidi kuitia hasara Serikali na kuwa na matumizi mabaya ya pesa hizo.


  Picha ikimuonesha Mkandarasi kutoka Kampuni ya Caberisa Co.Ltd Bernad Mgohamwende, ambaye anajenga barabara kwa kiwango cha changarawe yenye urefu  wa kilomita 36, eneo la barabara ya mbauda ,Osunyai Mkoani Arusha iko katika hatua za mwisho kukabidhi (Picha na Pamela Mollel).


  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amefungua Mashindano ya Mbio za Baiskeli na Ngoma za Asili Mjini Bariadi(Simiyu Jambo Festival) ambayo yamehudhuriwa na Maelfu ya  Wananchi wa Mkoa wa Simiyu.

  Mashindano hayo ya mbio za baiskeli yamehusisha kilometa 200 wanaume, kilomita 80 wanawake ambapo pia walemavu waliweza kushindania katika umbali wa kilomita tano.

  Akizungumza baada ya kufungua mashindano hayo Dkt.Tulia pamoja na kuupongeza Mkoa wa Simiyu kuandaa mashindano hayo amesema, ipo michezo nchini haijapewa kipaumbele lakini ikitumiwa vizuri inaweza kutoa ajira ukiwemo mchezo wa mbio za baiskeli; ambapo ametoa wito kwa viongozi wa mikoa mingine pia kuwekeza katika michezo mbalimbali ili kuwasaidia wananchi kupata kipato.

  “Lililofanyika Simiyu ni jambo jema sasa watu watakuwa wanajua kuwa wakijifua vizuri kwenye baiskeli na ngoma za jadi wanakuja kushiriki mashindano ya Baiskeli Simiyu, nitoe wito kwa viongozi wengine kufikiria mambo mengine yanayoweza kuwasaidia wananchi katika maeneo yao kupata ajira na kujipatia kipato” alisema.

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema mkakati wa mkoa huo ni kurasimisha tamaduni zote za Mkoa wa Simiyu na kuhusianisha na shughuli za Utalii ndani ya mkoa huo. 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (wa pili kushoto) akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi (kulia) ni Mkurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products ambayo ni mdhamini, Mhe.Salum Khamis akimpongeza Mshindi huyo

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (mwenye bendera nyeupe kulia) akifungua mashindano ya Mbio za Baiskeli Mkoa wa Simiyu(Simiyu Jambo Festival) kwa kuruhusu washiri kuanza mashindano hayo Mjini Bariadi.

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (mwenye baiskeli wa pili kulia) akiwa na viongozi wa Mkoa na baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Simiyu na Viti Maalum kutoka nje ya Mkoa kwa ajili ya kufungua mashindano ya baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi.

  Mkurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products, Mhe.Salum Hamis ambaye ndio mdhamini wa mashindano ya baiskeli na ngoma za asili akimkabidhi Mshindi wa kwanza mbio za Kilometa 80 (wanawake) Raulensia Luzuba kutoka mkoani Mwanza zawadi ya shilingi laki tano taslimu.

  Rais wa Chama cha Baiskeli Taifa, Godfrey Mhagama akimkabidhi mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa 10 (walemavu) katika mashindano ya Baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) yaliyofanyika Mjini Bariadi Simiyu.

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza (wanaume) katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi kilometa 200, Hamisi Hussein kutoka Arusha

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa mbio za Kilometa 10 (walemavu) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi kutoka nje ya mkoa wa Simiyu, mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya baiskeli na Ngoma za Asili(Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.


  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Na Chalila Kibuda,GlobuyaLindi

  Katika kukabiliana na changamoto za madhara ya ajali za pikipiki yanayosababishwa na madereva kutovaa kofia ngumu (helmet), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imebuni teknolojia ya kukabiliana na hilo.

  Mwalimu wa fani ya elektroniki kutoka VETA Kipawa, AnethMganga, amebuni mfumo wa kielektroniki unaozuia pikipiki kuwaka mpaka dereva awe amevaa kofia ngumu (helmet).

  Akizungumza katika viwanja vya maonesho ya Nanenane Ngongo, mkoani Lindi, mwalimu Aneth amesema mfumo huo ukianza kutumika na madereva wa pikipiki utapunguza madhara endapo kunatokea ajali kwa kuwa bila ya kuvaa kofia ngumu pikipiki haiwezi kuwaka na hata ukiwa katika mwendo ikitokea ukavua kofiangumu pikipiki itazimika.

  Aidha, katika usalama barabarani inasaidia kuzuia wizi wa pikipiki kwani mwizi hatoweza kuiwasha bila kofiangumu ambayo imeunganishwa kieletroniki.

  Aneth amesema anaendelea kufanya utafiti nakuboresha zaidi ubunifu huo, lakini ameomba serikali na wadau mbalimbali kuunga mkono ili uweze kuenea, kukubalikana kutumika na waendesha pikipiki katika maeneo mbalimbali nchini.

  Mkuu wa wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo, akitembelea banda la VETA katika maonesho ya Kilimo 2017 yanayoendelea mkoani Lindi katika viwanja  vya Ngongo ambapo alipongeza VETA kwa kuweka fursa nyingi za mafunzo ya ujuzi kwa makundi mbalimbali ya wananchi. Aliahidi kushirikiana na VETA ilikuwa wezesha wananchi wilaya ni kwake kunufaika pia na fursa mbalimbali za mafunzo ya ufundi stadi. 
  Wanafunzi wa shule ya sekondari Medi ya mkoani Mtwara wakipata maelekezo juu ya aina ya mafunzo yanayotolewa katika vyuo vya ufundi Stadi walipotembelea banda la VETA katika Maonyesho ya kilimo ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
  .Mwalimu wa Elektroniki wa Veta Kipawa, Aneth Mganga akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la VETA Pikipiki inayoendeshwa ni lazima dereva awe amevaa kofiangumu.


  0 0
  0 0

  It has been reported that the number of data users in the country has increased from 3.4 to 5.8 million in a period of two years.

  The increase is the result of the increment in the number of new Tanzanians who have started using electronic devices such as mobile phones and computers with the intention of searching online for different information and constructive knowledge.

  Speaking about the increase, Vodacom Tanzania PLC Managing Director, Mr. Ian Ferrao said that during the years 2014 to 2016 internet and data usage, particularly through cell phones and computers, has increased from 3.8 to 5.4 million for Vodacom network users; and all of them being permanent customers.

  He said that based on these statistics it can be deduced that within a short period of time, data usage has increased from 37 to 44 percent of the total mobile users in 2016. He explained that the official Vodacom-Tanzania report points out that the largest data usage increase was during 2014 and 2015, which was from 37% to 43% in just one year.

  Mr. Ferrao said in an effort to increase the number of data users, Vodacom Tanzania will set a range of factors including affordable customer charges and faster internet speed than that of its competitors.

  "There are four main ways in which Vodacom Tanzania will operate to ensure that we remain the leading mobile network operator in providing the best and modern services to our customers."

  "Firstly, we will invest in our infrastructure to suit the needs of data users in Tanzania. Furthermore, we will ensure that our customers get data within a satisfactory speed basis, facilitate affordable customer charges and lastly, provide customer incentives to encourage more data usage", said Mr. Ferrao.

  In addition, Mr. Ferrao noted that in the early years of the commencement of mobile phones usage in the country, many cellular companies including Vodacom Tanzania were making a good profit out of multimedia calls and short messages. Respectively, Vodacom-Tanzania has now decided to focus all its attention on being a data technology leading company so as to increase the number of data users in the country.

  Mr. Ferrao said that up to date, the number of data users has grown in the country and Vodacom is prepared to take advantage of this opportunity.

  "In recent years, more Tanzanians have begun to use electronic devices such as mobile phones and computers for online information and knowledge search. At the moment, Vodacom Tanzania sees a great opportunity for growth in this area", concluded Mr. Ferrao.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Pizza Hut Afrika, Ewan Devenpot(Katikati) kwa pamoja wakishangilia mara baada ya kukata  utepe kufungua Mgahawa wa Pizza Hut Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Pizza Hut, Vikram Desai pamoja na Meneja masoko wa Pizza Hut Tanzania,Bahati Komba.
  Sehemu husika kwa wahusika watakaotembelea Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Amesema kuwa  ajira zilizopo ni katika viwanda vya mabox ambayo nao hutumia katika kuandaa Pizza pamoja na viwanda vya chill source, Tomato source ambapo kuna watu ambao wameajiliwa katika viwanda hivyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Pizza Hut, Vikram Desai na baadhi ya wateja wakionja pizza zilizoandaliwa ikiwa kunapizza za nyama, mbogamboga pamoja na uyoga.
   
  Pizza Hut inamilikiwa na kampuni ya Dough Works Ltd,sasa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 100 ambao ni watanzania hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Pizza Hut, Vikram Desai wakati wa uzinduzi wa  migahawa miwili iliyopo Mlimani City na Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.

  akizungumza katika uzinduzi wa migahawa hiyo amesema kuwa Mwaka huu mgahawa wa Pizza Hut ulitambulisha usambazaji bure wa chakula katika ofisi na majumbani na hivyo kuwarahisishia huduma wateja wake.


  Migahawa miwili ya Pizza hut ipo katika eneo la maduka la Mkuki, jengo la Peugeot na Shoppers Plaza Mikocheni inaendelea kuhudumia mamia ya wananchi kwa chakula cha mchana na usiku.

  Migahawa ya Pizza Hut ni ya kisasa ikiwa na sehemu ya watoto ya michezo mbalimbali, na sehemu za kukaa za ndani na nje. Pamoja na kuwa na chakula kitamu aina ya Pizza pia wametambulisha aina mbali mbali za bidhaa za kuku zenye ladha tofauti.

  Zaidi ya mpango huo wa kupanua biashara kwa migahawa miwili zaidi kabla ya mwisho wa mwaka pia tunaangalia uwezekano wa kufungua biashara katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Mwanza. 


  0 0

  MKAZI wa Dodoma nchini Tanzania, Innocent Nyalia, ameibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka kwa waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, katika droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam.

  Droo hiyo ilichezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, ambaye kwa pamoja alishuhudia kupatikana kwa mshindi huyo wa droo ya 29 ya Biko.

  Akizungumza katika droo hiyo, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alimpongeza mshindi huyo wa mjini Dodoma, Nyalia na kuwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa za mamilioni ya Biko.

  Alisema huu ni wakati wa kutajirika kwa kuvuna mamilioni ya Biko yanayoendelea kutolewa kwa wingi, ikiwa ni mwendelezo wa kuona wachezaji hao wanaotumia simu za M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa kwa kuingiza namba ya kampuni 505050 na kumbukumbu 2456 wananeemeka na Biko.
  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
  Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo imeyatupilia mbali maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na  Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji baada ya kukubaliana na mapingamizi yaliyowasilishwa na DPP.

  Maombi hayo yametupiliwa mbali na Jaji Isaya Arufani. Kabla ya kutupiliwa mbali, maombi hayo, Manji alisimama na kuieleza mahakama kukataa kuwakilishwa na Wakili Peter Kibatala kwa sababu za kisiasa. Amedai, alipopeleka maombi ya dhamana alimpa maelekezo wakili Joseph Tedayo lakini alishangaa kesi ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kisikilizwa maombi yake ya dhamana wakili Kibatala ndiyo alifika kumuwakilisha.

  Kutokana na hayo, Manji ameiomba Mahakama mawakili, Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na Seni Malimi ndio wawe wanamuwakilisha katika maombi hayo.
   Hivyo DPP akiwakilishwa na mawikili Paul Kadushi na Simon Wankyo walidai kuwa, wamewasilisha kiapo kinzani kupinga maombi hayo ya dhamana wakiwa na hoja tatu. Hoja hizo ni kuwa, Mahakama Kuu haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo ya dhamana na kwamba yanapaswa kusikilizwa na mahakama ya kifisadi kwa kuwa mshtakiwa anakabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi.

  Ameongeza kuwa vifungu vya kisheria vilivyotumika kuleta maombi hayo siyo sahihi na pia hati ya kiapo iliyoambatanishwa  kuunga mkono maombi hayo ina dosari kisheria ambazo haziwezi kurekebishika.
  Kadushi aliiomba mahakama kusikiliza kwanza mapingamizi ya DPP kabla ya kuanza kusikiliza maombi ya dhamana. Hata hivyo Wakili Mgongolwa akiwakilisha jopo la mawakili wa Manji walikubaliana na mapingamizi ya DPP kuwa ni kweli yana msingi na maombi ya dhamana yanadosari. Kufuatia kukiri huko, Kadushi aliiomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo ya dhamana.

  Akitoa uamuzi, Jaji Arufani amekubaliana na mleta Maombi (Manji) kuwa hawakilishwi na Kibatala. Pia amesema mahakama kuu haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo hivyo ameyatupilia mbali.
  Katika maombi hayo ya dhamana, Yusuf Manji anaiomba Mahakama Kuu itengue hati ya kunyimwa dhamana iliyowasilishwa na Mkurgenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kuwa ana matatizo ya kiafya akisumbuliwa na matatizo ya moyo.

  Kwa mujibu wa hati ya maombi hayo, Manji anadai kuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo  na kwamba ameambatanisha vyeti vya daktari katika maombi yake.

  Katika kesi ya msingi,  Manji na wenzake wanatuhumiwa kukutwa na mihuri mbalimbali ya JWTZ isilivyo halali vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 236.5.
  Mbali na Manji, washtakiwa wengine ni,  Ofisa Rasilimaliwatu Deogratias Kisinda (28), Mtunza Stoo, Abdallah Sangey (46) na Mtunza Stoo msaidizi, Thobias Fwele (43)
  Mfanyabiashara Yusuf Manji akiwa anatoka Mahakama kuu mara baada ya mahakama hiyo kutupilia mbali maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na mfanyabiashara huyo.  0 0

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeihirisha Kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange maarufu Kaburu hadi August 16 mwaka huu kwa sababu upelelezi haujakamilika.

  Kesi hiyo ilitajwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa na wakili wa serikali, Elia Athanas ambaye amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba ipangiwe tarehe nyingine.

  Hakimu Mwambapa alikubali maombi ya wakili wa Serikali Athanas na  aliahirsha kesi hiyo hadi August 16 mwaka huu.Kesi ya Kaburu na Aveva, Upelelezi bado haujakamilika

  Aveva na Kaburu wamerudishwa tena mahabusu mpaka kesi yao itakapotajwa tena.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo pamoja na Bodi ya Wakurugenzi Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Uongozi wa Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Nd,Omar Hassan Omar (katikati) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa kikao cha siku moja cha pamoja cha Wizara, Bodi ya Wakurugenzi Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Uongozi wa Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu kilichofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).Picha na Ikulu, Zanzibar.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirisha kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Pombe Magufuli inayomkabili mbunge wa Kawe, Halima Mdee hadi Septemba 12, kwa kuwa hakimu anayesikiliza kesi hiyo anaudhuru.

  Hata hivyo, kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Mshtakiwa Mdee  kupitia mawakili wake amewasilisha pingamizi la awali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

  Mawakili wa Mdee, wakiongozwa na Hekima Mwesigwa wamewasilisha pingamizi hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa baada ya wakili wa serikali Leonard Chalo kudai shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa.

  Mwesigwa amedai kuwa wanapingamizi mbili, kwanza hati ya mashtaka ina mapungufu, pia Mahakama hiyo haina mamlaka.

  Amedai kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka kwa sababu, Mkuu wa wilaya aliyetoa amri ya kukamatwa kwa Mdee ameshindwa kufuata matakwa ya kisheria.

  Hata hivyo, Hakimu Mwambapa hakujibu kitu chochote na ameiahirisha kesi     hiyo hadi September 12 mwaka huu.

  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi, Pwani.
  JESHI la Polisi Mkoani Pwani, linamshikilia mfanyabiashara, Rajabu Hitaji (30) mkazi wa Vigwaza, Bagamoyo anaedaiwa kuwasafirisha wahamiaji haramu 72 raia kutoka nchini Ethiopia.

  Aidha jeshi hilo linawashikilia pia wahamiaji haramu hao kwa kosa la kuingia nchini bila kibali .

  Akitolea ufafanuzi juu ya tukio hilo ,kamanda wa Polisi mkoani Pwani(ACP) Jonathan Shanna, alisema uchunguzi unaendelea na watafikishwa ofisi za uhamiaji kwa hatua nyingine stahiki. Alieleza ,mtuhumiwa Hitaji alikamatwa majira ya saa 3.30 asubuhi huko maeneo ya pori la ranchi ya Taifa Narco ,Vigwaza wilaya ya kipolisi Chalinze.

  "Kufuatia msako mkali ulioendeshwa na makachero wetu baada ya kupata taarifa juu ya uwepo wa raia walioingia nchini pasipo kufuata taratibu za uhamiaji na raia hao baada ya kugundua kuna gari la polisi linawafuatilia "

  "Waliingia kwenye hifadhi hiyo kwa lengo la kujificha lakini askari wetu waliweza kubaini mahali walipo kufuatia msako mkali uliokuwa ukiendeshwa katika ranchi hiyo " alisema kamanda Shanna .

  Alisema askari hao walifanikiwa kuwakamata kundi la kwanza la wahamiaji haramu 63 wakiwa mahali ambapo gari halifiki.

  Kamanda Shanna ,alieleza kwamba, licha ya kukamatwa kundi hilo askari waliendelea na msako na kufanikiwa kukamata kundi jingine la wahamiaji haramu Tisa, waliokuwa wakitafuta njia ya kutoroka katika ranchi ya taifa ya Narco .

  Wakati huo huo, MTU mmoja na watoto wawili wamefariki dunia baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kuvuka mto Ruvu kuzama.

  Mtumbwi huo walikuwa wakiutumia kutoka upande wa Vigwaza kwenda upande wa Mlandizi katika mto huo wilaya ya kipolisi Chalinze Mkoani Pwani.


  0 0

  MTU mmoja na watoto wawili wamefariki dunia baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kuvuka mto Ruvu  kuzama Mkoani Pwani. 

  Mtumbwi huo walikuwa wakiutumia kutoka upande wa Vigwaza kwenda upande wa Mlandizi katika mto huo wilaya ya kipolisi Chalinze Mkoani Pwani.

  Kamanda Shanna amesema, tukio hilo limetokea majira ya saa kumi alfariji usiku wa kuamkia Agosti 6 mwaka huu.

  Aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Sikuzani Mussa (41) ambae mwili wake bado haujapatikana na jitihada za kuutafuta zinaendelea.

  Kamanda Shanna, alisema watoto waliopoteza maisha kwenye tukio hilo ni Nusurat Haji mwenye miezi minne na Fesali Hamza mwenye mwaka mmoja.

  Aidha katika tukio hilo watu wawili waliweza kuokolewa wakiwa hai ambao ni Zuwena Ramadhani (29)na Tero Mziray (20).

  "Dereva wa mtumbwi huo haijajulikana alipo na inaaminika ya kwamba yeye hajafa maji.''

  Kamanda Shanna, alieleza chanzo cha mtumbwi huo kuzama maji bado kinachunguzwa na miili ya marehemu imeshafanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi .

  0 0  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Lindi mchana huu tayari kwa kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nane Nane itakayofanyika Kitaifa mkoani Lindi.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh.Nape Moses Nnauye ,mara baada ya kuwasili mkoani Lindi mchana huu tayari kwa kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nane Nane itakayofanyika Kitaifa mkoani Lindi.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama cha Mapinduzi (CCM),mara baada ya kuwasili mkoani Lindi mchana huu tayari kwa kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nane Nane itakayofanyika Kitaifa mkoani Lindi.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Kama ulipitwa na matukio ya wiki nzima yaliyojili mkoani Ruvuma kuanzia 7 July 31 hadi August 06, 2017 basi usipate tabu tumekusogezea matukio 7 ambayo ni ya wiki .

  0 0


  WATANZANIA wameshauriwa kutumia teknolojia za kisasa katika kada za kilimo,mifugo na uvuvi ili kujipatia ajira na kipato na hatimaye kukuza lengo la uchumi wa viwanda.

  Ushauri huo ulitolewa jana jijini Arusha na Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati Bw,Daniel Luther wakati akiongea na gazeti hili kwenye maonesho ya kilimo na mifugo Nane nane yenye kauli mbiu Zalisha kwa tija,mazao na bidhaa za kilimo,mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati ambapo kwa kanda ya Kaskazini yanafanyika mkoani Arusha.

  Luther alisema kuwa endapo watanzania wataamua kuwekeza nguvu zao katika teknolojia hizo ikiwemo ufugaji wa samaki wataweza kujiingizia kipato katika ngazi ya kaya kupitia samaki watakazozalisha.

  "Ufugaji wa samaki kisasa si lazima uwe na eneo kubwa hata eneo dogo nyumbani kwako unaweza ukafuga ama hata katika simtank,madyaba ama pipa ili mradi eneo hilo liwe na hewa pamoja na usafi wa mazingira ya maji ya kuhifadhia samaki wako.

  Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati Bw,Daniel Luther wakati akiongea na waandishi wa habari katika maonesho ya kilimo na mifugo Nane nane yenye kauli mbiu Zalisha kwa tija,mazao na bidhaa za kilimo,mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati ambapo kwa kanda ya Kaskazini yanafanyika mkoani Arusha.(Picha na Pamela Mollel)
  Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati Bw,Daniel Luther wakati akiongea na wananchi hili katika maonesho ya kilimo na mifugo Nane nane yenye kauli mbiu Zalisha kwa tija,mazao na bidhaa za kilimo,mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati ambapo kwa kanda ya Kaskazini yanafanyika mkoani Arusha.
  Wananchi wakiwa wanaangalia bwawa la samaki katika banda la halmashauri ya mji wa Babati katika maonyesho ya nane nane


  0 0

  Afisa Habari wa Bunge, Ndg. Patson Sobha (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maria de Mattias iliyopo kisasa Mjini Dodoma walipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea leo kwenye Viwanja vya Nzunguni, Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0

  Pichani ni eneo la stendi mpya na ya kisasa ya mabasi mjini Korogowe Mkoani Tanga, iliyozinduliwa rasmi na Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo. PICHA NA IKULU
  Sehemu ya Wananchi wa Korogwe wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye eneo la stendi hiyo, kumsikiliza Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kabla ya kuizindua rasmi leo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi cha Korogwe mjini mkoani Tanga.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi waliofika katika ufunguzi huo wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi cha Korogwe mjini mkoani Tanga.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo kabla ya kufungua rasmi Kituo hicho cha Kisasa cha Mabasi cha Korogwe mjini mkoani Tanga.
   Taaswira ya wananchi mbalimbali waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi cha Korogwe mjini mkoani Tanga.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mananchi mara baada ya kufungua Kituo cha Kisasa cha Mabasi cha Korogwe mjini mkoani Tanga.
   PICHA NA IKULU.


  0 0

   Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mariam A. Mtunguja akisisitiza jambo mbele ya watumishi wa umma kutoka mikoa ya Songwe, Iringa, Njombe na Mbeya alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina ya siku nane juu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Kisekta  (PlanRep)  leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID). Watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa hiyo.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mariam A. Mtunguja (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki washiriki wa semina ya siku nane juu ya Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) mara baada ya kufungua semina hiyo leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ambapo inahusisha watumishi wa umma kutoka kada za Maafisa Mipango,Wachumi, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu kutoka Halmashauri na Mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe.
  Picha zote na: Idara ya Habari – MAELEZO, Mbeya.

older | 1 | .... | 1847 | 1848 | (Page 1849) | 1850 | 1851 | .... | 3272 | newer