Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1845 | 1846 | (Page 1847) | 1848 | 1849 | .... | 3286 | newer

  0 0  Kazi zinazo fanyika chini ya Mradi huu ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa (9) ya kusambaza na kuhifadhi maji yenye ukubwa wa kuhifadhi lita milioni 3.0 hadi milioni 6.0, ujenzi wa vituo vinne (4) vya kusukuma maji, ununuzi na ufungaji wa Pampu kubwa za kusukuma maji 16, ununuzi wa transfoma na ufungaji njia za Umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji maji wa mabomba ya usambazaji maji mtaani yatakayokuwa na urefu wa jumla ya kilometa zipatazo 477.  

  Maeneo yatakayo nufaika na mradi huu ni pamoja na Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni, Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kitope, Ukuni, Kerenge, Buma, Mataya na ukanda maalum wa EPZA ambayo ni maeneo yanayo hudumiwa na mtambo wa Ruvu chini. Ambayo ni maeneo mengine yatakayo nufaika na mradi huu ni yale yaliyopo kati ya Mbezi luisi na kiluvya, ambayo ni Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Msakuzi, Makabe, Malamba mawili na Msigani. Maeneo haya huhudumiwa na mtambo wa ruvu juu ambao ulizinduliwa na mh,Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Juni 21,2017.

  Lengo la mradi huu ni pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wa kawaida , wenye viwanda na biashara katika eneo lote la mradi wanapata huduma bora za Maji hasa baada ya maji kuongezeka kufuatia kukamilika kwa upanuzi wa mitambo ya maji ya Ruvu juu na Ruvu chini. Lengo lengine ni kuweka mitandao ya maji katika maeneo mengine ambayo hayakuwa na mtandao rasmi wa maji, kwa kufanya hivi mradi utawezesha maji yagawanywe kwa urahisi na uwiano zaidi.

  Ili kudhibiti upotevu wa maji, mita maalum zitafungwa katika maeneo ya kupokea maji na katika matoleo ili kujuwa kiasi kamili cha maji kilicho ingia katika eneo husika na kiasi cha maji  moja kwa moja ofisi za (DAWASCO) ambapo vifaa maalum vitafungwa na itakuwa rahisi kujuwa ni wapi maji yanapotea na hivyo kuyadhibiti moja kwa moja.

  Mradi huu unatekelezwa kwa gharama ya dola za kimarekani Milioni 32,927,222,45 kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya India. 
  Mh.waziri Lwenge akiwa katika zoezi la kukaguwa miradi ya maji ya Dawasa katika eneo la Kibamba jijini Dar es salaam.


  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala siku ya jana alitembelea Kata ya Kitobo Wilayani Missenyi na  kuzindua  Daraja la Kyankoko lenye sehemu tatu zilizowekewa Kalavati ,mradi uliopewa jina la la Novati Rutegaruka Memorial Bridge ambalo ni jina la muasisi na mwanasiasa mkongwe ambaye aliangaingia eneo hilo katika kipindi cha Uhai wake.
   Muonekano wa Daraja la Kyankoko lililopewa jina la Novati Rutegaruka Memorial Bridge Daraja linalovikutanisha Vijiji vya Msibuka na Kayanga katika Kata ya Kitobo Wilayani Missenyi
   Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (pichani) akiongea na wananchi wa Kijiji cha Kashasha kata Kitobo  waliohudhuria katika mkutano wake wa hadhara,Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala ameweza kuchangia miradi ya maendeleo inayoendelea katika kata hiyo na pamoja na kuahidi kuzifanyia kazi kero mbalimbali kama Uhaba wa wauguzi katika Zahanati na vituo vya Afya,Utaratibu wa Bima ya Afya kwa Wazee na watu wenye Ulemavu kwa kuwapunguzia changamoto wanazokutana.


  0 0

  Afisa Habari (Itifaki) wa Bunge, Ndg. Patson Sobha (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Miyuji walipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea Mjini Dodoma.

  Afisa Habari (Itifaki) wa Bunge, Ndg. Patson Sobha akizungumza na wageni Mbali mbali waliotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wananchi wa Mbande, Kata ya Chamazi, Tarafa ya Mbagala, Wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam, wakati alipofanya ziara katika eneo hilo yenye lengo la kuimarisha ulinzi na usalama katika eneo hilo. Hata hivyo, Masauni aliamuru ujenzi wa Kituo cha Polisi Mbande ambao utajengwa kwa michango ya wananchi na Serikali uanze mara moja, na pia aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa kuwafichua askari polisi wanaohisiwa kushirikiana na wahalifu katika eneo hilo.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Mkazi wa Mbande, Mbagala, jijini Dar es Salaam, Muhidin Maftaa alipokua anamuuliza swali kuhusu hali ya ulinzi na usalama katika eneo hilo. Ambaye alifanya ziara katika eneo hilo yenye lengo la kuimarisha ulinzi na usalama, aliamuru ujenzi wa Kituo cha Polisi Mbande ambao utajengwa kwa michango ya wananchi na Serikali uanze mara moja, na pia aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa kuwafichua askari polisi wanaohisiwa kushirikiana na wahalifu katika eneo hilo.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Gilles Muroto,alipokuwa anajibu mswali mbalimbali ya wananchi wa Mtaa wa Magengeni Mbande, Mbagala, jijini Dar es Salaam. Masauni alifanya ziara katika eneo hilo yenye lengo la kuimarisha ulinzi na usalama na aliamuru ujenzi wa Kituo cha Polisi Mbande ambao utajengwa kwa michango ya wananchi na Serikali uanze mara moja, na pia aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa kuwafichua askari polisi wanaohisiwa kushirikiana na wahalifu katika eneo hilo.

  habari kamili BOFYA HAPA

  0 0

  --


   Ofisa kutoka Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa Tanzania ,Didi Nafisa akizungumza na Vijana wa Mtandao wa Vijana Temeke(TEYODEN), Juu ya Malengo ya Milenia kwa vijana na mambo yaliyopewa vipaumbele katika malengo hayo
   Katibu mkuu wa Mtandao wa Vijana Temeke(TEYODEN),Yusufu Kutegwa akizungumza juu ya namna Mtandao huo unavyofanya kazi kusaidia Vijana
   Baadhi ya Vijana walioshiriki Mkutano Huo wakisikiliza kinachozungumzwa kutoka kwa watoa mada
   Balozi wa Malengo ya Dunia kwa Vijana kutoka chuo cha Uhasibu Arusha ,Gloria Nassary akizungumza na Vijana wa Temeke juu ya Vipaumbele vitano vya Kibinadamu katika Malengo ya Milenia
    Balozi wa Malengo ya Dunia kwa Vijana kutoka chuo cha Mtakatifu Agustino ,Julius Kitingati akieleza namna Vijana wanavyoweza kufanikisha malengo hayo kwa Sera ya Viwanda hapa nchini
  Sehemu ya Viana walioshiriki katika mkutano huo ulioandaliwa na TEYODEN  Kwa kushirikiana na umoja wa Mataifa

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhandisi Ahmad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema jijini Dar es Salaam juu ya Tamasha la Usalama barabarani linalotaraji kufanyika Agosti 12 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kushirikisha makundi mbalimbali ya Wasanii watu maharufu na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhandisi Ahmad Masauni,akipokea jezi kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi na Mauzo ,Omary Mtiga NMB imetoa Vifaa Vyenye Thamani ya Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya Kufanikisha Tamasha la Usalama Barabarani Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhandisi Ahmad Masauni,akipokea jezi kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi na Mauzo ,Omary Mtiga NMB imetoa Vifaa Vyenye Thamani ya Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya Kufanikisha Tamasha la Usalama Barabarani Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhandisi Ahmad Masauni Akipokea Fulana kutoka kwa Meneja Masoko wa Azam Omary Kuwe.


  0 0  IMGL8670
  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba (katikati)akimsikiliza  Afisa Habari wa Bunge Ndg. Patson Sobha (kushoto) wakati alipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea  kwenye Viwanja vya Nzunguni, Mjini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Ndg. Deogratius Ndejembi
  IMGL8673
  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akiuliza swali baada kutembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nzunguni, Mjini Dodoma. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Ndg. Deogratius Ndejembi na kulia ni Afisa Habari wa Bunge Ndg. Patson Sobha.
  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akisalimiana na Katibu Msaidizi wa Bunge, Ndg. Bakari kishoma wakati alipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea  kwenye Viwanja vya Nzunguni, Mjini Dodoma.
  (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0  Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo ameagiza kukamatwa kwa wajumbe wa bodi ya Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula kufuatia kuchelewesha kwa makusudi malipo ya mkopo walioupata kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

  Akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na wanachama wa Skimu hiyo, Bw. Ihunyo alisema kuwa uzembe wa Bodi hiyo umepelekea kuchelewesha marejesho ya mkopo wa takribani shilingi milioni 790.

  Mkuu huyo wa wilaya aliongeza pia kitendo cha Bodi hiyo inarudisha nyuma juhudi za serikali katika kupambana na umaskini nchini.“Lengo la mikopo hiyo ni kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania, hivyo kuchelewesha mikopo hiyo kwa makusudi ni kurudisha nyuma juhudi hizi,” Bw. Ihunyo alisema.

  Bw. Ihunyo aliongeza kuwa kuchelewesha kurudisha mikopo hiyo kunakosesha wakulima wengine kuchelewa kupata fursa hizo za mikopo hiyo nafuu inayotolewa na TADB ambayo imelenga kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

  Akizungumza katika mkutano huo, Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Adam Kamanda alisema kuwa tangu wapatiwe mkopo huo, baadhi ya wakulima wa skimu hiyo wamekuwa wakichelewesha kwa makusudi kurejesha mkopo huo licha ya jitahada za kuwahimiza kurejesha mkopo huo.

  Bw. Kamanda alisema kuwa vitendo hivyo ni kwenda kinyume na malengo ya“Mheshimiwa Rais anahimiza watu kufanya kazi kwa bidii sasa vitendo hivi ni kukaidi maagizo hayo hivyo kupingana na dhana ya hapa kazi tu inayochagiza kufanya kazi kwa bidii,” alisema.

  Bw. Kamanda aliongeza kuwa Benki ya kilimo imejipanga kuhakikisha inatekeleza maelekezo ya serikali ya kuwawezesha wakulima nchini kwa kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika  kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.

  Mwakilishi huyo wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa TADB imedhamiria na kujizatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika  kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.

   “Tuna dira ya Kuwa benki ya mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.
  Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (aliyesimama) akizungumza katika mkutano wa pamoja na wanachama wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula,iliyopo katika kijiji cha Mkula wilaya ya Kilombero.
  DSC_0051
  Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (aliyesimama) akihimiza jambo wakati akizungumzia kukamatwa kwa wajumbe wa Bodi ya Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula ambao wamezembea kusimamia mkopo wa TADB.
  DSC_0052
  Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Adam Kamanda (kushoto) akiongea kwa uchungu kitendo cha wajumbe wa Bodi ya Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula ambao wamezembea kusimamia mkopo wa zaidi ya shilingi milioni 790 zilizotolewa TADB.
  DSC_0053
  Baadhi ya wanachama na wanakijiji wa kijiji cha Mkula wakifuatilia mazungumzo wakati wa kikao cha pamoja kati ya Mkuu wa Wilaya hiyo, wawakilishi wa Benki ya Kilimo na wanachama wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula.
  DSC_0057 DSC_0058
  Zoezi la kukamata wajumbe likiendelea.


  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Benny Mwaipaja-WFM, Arusha

  MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, amewataka wanafunzi 45 kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Ethiopia, wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia kilichoko mkoani Arusha, kusoma kwa bidii na maarifa ili waweze kuzisaidia nchi zao kuinua sekta ya viwanda kwa njia ya utafiti na ubunifu wa teknolojia mbalimbali

  Dkt. Weggoro ametoa rai hiyo alipotembelea Chuoni hapo ili kuangalia utekelezaji wa programu ya miaka mitano ya kuboresha masuala ya rasilimali watu inayofadhiliwa na Benki yake kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 8.2

  Alisema kuwa Benki yake imeamua kuwekeza fedha nyingi katika eneo la Sekta ya elimu ya juu katika nyanja ya ufundi ili kuwapata vijana wa kutosha watakaoziba pengo lililopo na kuweka misingi mizuri ya maendeleo ya baadae hasa katika matumizi ya teknolojia na sayansi.

   “Nimefurahi sana kuona wanafunzi wanasoma na wana ari kubwa na kwamba fedha tulizozitoa zinatumika vizuri, tunadhani hata baada ya mradi huu wa  miaka 5 kukamilika, Benki itaweza kusaidia zaidi ufadhili wa fedha na vifaa” Alisema Dkt. Weggoro.

  Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Prof. Joram Buza, ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB kwa ufadhili huo, hatua iliyoongeza udahili wa wanafunzi katika chuo hicho.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro akizungumza kuhusu umuhimu wa vijana wenye weledi wa kitaaluma katika kukuza uchumi, alipokutana na wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha (hawapo pichani) wanaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB)


  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (kulia) akiwa na Mkutano na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha Prof. Joram Buza, alipotembelea chuo hicho kuangalia mradi wa kuwafadhili wanafunzi unaotekelezwa na Benki yake.
   Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha wanaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (hayupo pichani) alipotembelea Chuo hicho, ambapo aliwasisitiza kusoma kwa bidii ili kuhimili ushindani katika soko la ajira.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa pongezi na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku Viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mbalimbali waliohudhuria shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono pamoja na mke wake Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakiagana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika uwanja wa ndege wa Tanga.
  Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimpa mkono Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza kuhutubia katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.
  Baadhi ya wananchi wakifurahia jambo wakati wa hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza jambo Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wakielekea kuweka jiwe hilo la msingi.


  0 0


  Na Mathias Canal, Lindi

  Pamoja na mazao mbalimbali yanayolimwa na wakulima nchini Tanzania lakini wametakiwa kujikita zaidi na kilimo cha mazao yanayostahimili ukame ikiwemo kuanzisha kilimo cha umwagiliaji hususani katika maeneo yaliyopo pembezoni mwa Bahari ya Hindi katika Mikoa ya Mtwara na Lindi.

  Kufanya hivyo ni kutumia vizuri rasilimali za nchi ikiwemo maji na maeneo oevu katika kilimo chenye tija jambo ambalo linatoa fursa kwa wakulima wadogo kuwa na kipato kikubwa na kutafsiri ipasavyo kipato cha nchi na mtu mmoja mmoja.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi idara kuu ya kilimo Ndg Twahir Nzallawahe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe akisoma na kupata maelezo mbalimbali kuhusu ufanisi katika Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe akisikiliza maelezo ya namna ya ufyatuaji matofali yanayotumika kujengea nyumba za NHC mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe (Kushoto) akisikiliz akwa makini maelezo kuhusu ufanyaji kazi katika banda la TAMISEMI mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi. Mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mhe Rukia Muwango.
  Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi idara kuu ya kilimo Ndg Twahir Nzallawahe akisikiliza maelezo mbalimbali katika banda la Nanyamba mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.


  0 0

  Na: Judith Mhina – MAELEZO

  Hakika historia imejirudia, mkoa wa Tanga ni kati ya mikoa mashuhuri nchini Tanzania kabla ya uhuru wa Tanganyika katika kupigania uhuru, kwa kuwa ni mkoa uliokuwa na wasomi wengi kuliko mikoa mingine wakati huo.

  Hii ilitokana na uwepo wa shule za wamisionari wa kanisa la Anglikana (UMCA) ambalo ni la kwanza kuingia katika Pwani ya Afrika Mashariki mwaka 1878 na waliojenga shule za Magila na Kiwanda Muheza, Korogwe misheni, Kideleko Handeni (Shule za Kati) na Saint Andrew Minaki Pwani (shule ya Sekondari).

  Hata baada ya uhuru chini ya Serikali ya Awamu ya Kwanza na ya Pili ya uongozi wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere na Rais Msataafu Ali Hassan Mwinyi, mkoa wa Tanga ulikuwa maarufu kutokana na uwepo wa viwanda vingi, njia za reli na Bandari yenye kina kirefu yenye uwezo wa kuingiza meli kubwa za mizigo za Kitaifa na Kimataifa.

  Viwanda ambavyo vilijengwa katika mkoa wa Tanga ni pamoja na vya chuma, mbolea, saruji, maziwa, kamba za katani na mazulia, amboni plastic, mbao, sabuni maarufu ya mbuni, gardenia, foma na mafuta ya nazi.

  Historia hii sasa inajirudia katika mkoa wa Tanga baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli, kupigania kwa nguvu zote Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda kuja nchini Tanzania ambalo litaishia katika kijiji cha Chongoleani.

  Wananchi wote wa Tanzania wana kila sababu ya kujivunia ujenzi wa bomba hilo la mafuta ambalo litawapatia ajira Watanzania hususan wananchi wa mkoa wa Tanga. Pongezi kubwa ziende kwa Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi zake za kuhakikisha kwamba Mradi huu unakuja Tanzania. Wananchi wa mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla wana kila sababu ya kulinda heshima ya nchi yetu kwa kuhakikisha kuwa kunakuwepo na ulinzi mkali wa Bomba hilo kila mahali lilikopita.

  Kurejea kwa mkoa wa tanga katika ramani ya Tanzania ya viwanda umedhihirishwa na Wananchi wa Chongoleani ambao siku ya uwekaji jiwe la msingi walikuwa wawakilishi wa Watanzania ambao hawakupata fursa ya kwenda Tanga kumshuhudia Mheshimiwa Rais na na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakifungua pazia la jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa Mradi huo.

  Kutokana na tukio hilo la uwekaji wa jiwe la msingi wana Chongoleani walitoa ya moyoni kwa kuonyesha furaha yao isiyo na kifani kupitia kwa Mwenyekiti wao wa kijiji Ndugu Mbwana Nondo wakisema; “Kwa moyo wa dhati kabisa tunamshukuru sana Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutujali Wananchi wake kwa kutuletea neema ya mradi huu wa bomba la mafuta”.

  Aidha, Mwenyekiti huyo aliongeza kwa kusema kwamba, katika maisha yetu Wananchi wa Chongoleani hatutaweza kumsahau Mheshimiwa Rais kwa mambo mengi anayowafanyia Watanzania na Taifa kwa ujumla na itakuwa ni kumbukumbu kwa kizazi kijacho.

  “Napenda kusisitiza kwamba tunamuahidi Rais, kuwa wote watakaopata fursa kwenye Mradi huu wa Bomba la Mafuta, watafanyakazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla”. Alihitimisha Bw Nondo.

  Naye Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Bibi Ummy Mwalimu, amewaomba wanawake wa Mkoa wa Tanga kuchangamkia fursa zinazojitokeza, kutokana na uwepo wa mradi wa bomba la mafuta.


  0 0  0 0  0 0

   Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya wanaounda kundi la Tanzania All Stars wakijiandaa kupanda jukwaani kutumbuiza kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
   Wasanii nyota wa filamu wa Bongo Movie wakiwa  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wamalize tofauti zao na kuweka maslahi ya nchi mbele wakati alipohutubia kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016.
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016.

  0 0
  0 0

  NA EVELYN MKOKOI – MWANZA 

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu w rais Muungano na mazingira amelipongeza jiji la mwanza kwa hatua iliyochukua ya kutunza mazingira kwa ujenzi wa Dampo na machinjio ya kisasa kwa lengo la kupunguza uharibifu na uchafuzi wa mazingira kutokana na utupaji taka ovyo.

  Aidha, amelipongeza jiji hilo kwa maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya dampo la kisasa kama mizani ya kupimia taka, ofisi na maabara ya kemikali katika dampo hilo uliopelekea jiji hilo kufuzu kupata ufadhili kupitia Bank ya dunia licha ya kutumia mapato ya ndani.”Nikiangalia naona mmewekeza kama zaidi ya milioni 700 ambayo mumewekeza kama manispaa ya Jiji la mwanza.” Alisema Mpina.

  Mpina aliongeza kwa kusema kuwa kwa jiji la mwanza kufanya hivyo ni hatua kubwa na kulitaka jiji hilo kuendelea na ari hiyo katika suala zima la hifadhi na utunzaji wa mazingira. Mpina pia aliitaka Manispaa hiyo kukamilisha kwa wakati hatua nyingine za ujenzi wa dampo hilo kama vile za Tathmini ya Athari kwa Mazingira na kulipa fidia kwa wananchi na kaya zilizobakia ili kukamilisha upanuzia wa dampo hilo, na kuepuka vipingamizi visivyo vya lazima.

  Katika hatua nyingine Mpina pia aliwapongeza wahisani kwa kuiamini serikali ya awamu ya tano katika mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika suala zima la hifadhi ya mazingira. “Naamini katika mradi huu unaokuja wa zaidi ya shilingi Bilioni 19.8 miundombinu ya hapa itakuwa ni mizuri na rafiki zaidi kwa mazingira, kikubwa zaidi ni kuwekeza nguvu zetu katika mradi huu na kuhakikisha kuwa unatekelezwa kama ulivyopangwa”. Alisema Mpina.

  Wakati huo huo Naibu Waziri Mpina alitembelea Machinjio ya kisasa ya jiji la Mwanza na kujionea ukarabati wa machinjio unahusisha utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mtambo wa kisasa wa kutibu majitaka yanayotoka katika machinjio hayo ambapo mtambo huo utazalisha pia biagas kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme na kuzalisha mbolea. Ukarabati huo unahusisha pia ujenzi wa chumba cha kisasa cha kuhifadhia nyama kitakachowezesha wafanyabiashara ya nyama kusafirisha nje ya nchi.

  Katika hali isiyo ya kawaida Naibu Waziri Mpina alitembelea kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Senrun Investment kilichopo eneo la Igoma na kusisitiza kiwanda hicho kiendelee kufungwa kutokana na kubainika kuendesha shughuli zake kinyume na Sheria kwa kutokuwa na vibali vya uchenjuaji dhahabu, cheti cha Tathmini ya athari kwa Mazingira na kibali cha matumizi ya kemikali kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali. 
   
  “Nasisitiza kwamba kiwanda hiki kiendelee kufungwa kama ambavyo NEMC wamekifunga na nawataka wamiliki kuwasilisha vibali husika ndani ya siku 7 na wasiendelee na uzalishaji mpaka watakapomaliza zoezi la kufanya tathmini ya athari kwa mazingira”. Awali kiwanda hicho kilifungwa na NEMC kufuatia malalamiko ya wananchi wa maeneo hayo kwa kutiririsha maji yenye kemikali, kutoa moshi mkali kutokana na uchomaji wa taka zenye sumu na kutokuwa na vibali muhimu vya kuruhusu uendeshaji wa shughuli za uchenjuaji dhahabu. 
  Karakana za kisasa zilizojengwa katika Dampo la jiji la Mwanza. 
  Mwenye Kofia Nyeupe Msimamizi wa Dampo la jiji la Mwanza (Site Manager) Bw. Desderius Pole akimuonyesha Naibu Waziri Mpina tokea mbali karakana za kisasa hazipo katika picha zilizojengwa katika Dampo la jiji hilo, kulia ni wana habari kazini. 
  Afisa Mazingira wa jiji la Mwanza wa pili kulia Bi Lidya Nyeme, akimuelezea Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na Ujumbe wake katika picha kuhusu machinjio ya kisasa ya Jiji la Mwanza iliyojengwa kwa ufadhili wa Bank ya Dunia kupitia Mradi wa hifadhi ya mazingira ya Ziwa Victoria (LVEMP) uliyopo chini ya Wizara ya Maji, Naibu Waziri Mpina yupo katika Ziara ya kikazi jijini Mwanza. 

  0 0
 • 08/06/17--04:44: Article 3
 • AgroForHelp Foundation ni taasisi inayojishughulisha na kusimamia mashamba kupitia mabwana shamba walionao, usaidizi katika solar water pumps, Irrigation systems na green house, hivyo kwa wale wakulima wapya na wa zamani wanaweza kuwatafuta AgroForHelp Foundation kwa msaada wa maswala mbalimbali ya kilimo. Wasiliana nao kwa kupitia 0715 569 203 au 0768 406 406.

  0 0

  Mwezeshaji kutoka Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney (kulia), akitoa mafunzo ya siku moja ya kilimo chenye tija kwa wakulima wa Mkoa wa Mtwara kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Ngongo mkoani Lindi jana.

  Na Dotto Mwaibale, Lindi

  HALMASHAURI ya Wilaya ya Newala mkoani Mtwara inakabiliwa na uhaba mkubwa wa maofisa ugani na mifugo jambo linalochangia kuporomoka kwa kilimo wilayani humo.

  Hayo yalielezwa na mkulima wa wilaya hiyo, Mohamed Ismail katika mafunzo ya siku moja kwa wakulima wa Mkoa wa Mtwara yenye lengo la kuwasaidia kulima kilimo chenye manufaa yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia kwa mwezeshaji kutoka Jukwaa la Bioteknolojia kwa maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk. Hamalord Mneney katika maonyesho ya kitaifa ya wakulima Nanenane yanayoendelea Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi jana.
  Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Philbert Nyinondi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA), akizungumza na wakulima hao.

  Alisema katika kata moja yenye vijiji sita ni ofisa ugani mmoja tu ndiye anayehudumia wakulima katika vijiji hivyo tena bila ya kuwa na usafiri wa uhakika hivyo kumfanya ashindwe kuwafikia wakulima kuwapa mafunzo na kujua changamoto walizonazo. Alisema kutokana na uhaba wa maofisa kilimo na mifugo imesababisha ofisa ugani kujikuta akifanya kazi mbili ya ugani na mifugo na ofisa mifugo naye akifanya kazi ya ugani na ambayo hakuisomea.

  Mkulima Shezili Mpangalika kutoka katika wilaya hiyo alisema kilimo cha kuhamahama kinachosababishwa na kuporomoka kwa bei ya zao la mbaazi kimechangia kuwepo kwa mimba za utotoni kwa wanafunzi na wavulana kuacha masomo kutokana na kutokuwepo kwa usimamizi wa wazazi na walezi wao wanaokimbia nyumba zao kwenda maeneo mengine kufanya kilimo chenye tija.
  Mkulima Lukia Hassan Nalamba kutoka Kata ya Nanyamba akizungumzia changamoto wanazokabiliana nazo kwenye mafunzo hayo.

  Alisema katika wilaya hiyo wakulima wengi wamekuwa wakikimbia kutokana na bei ya mbaazi kushuka kutoka shilingi 500 hadi kufikia 400 na hivyo kuhamua kwenda wilayani Kilwa kulima ufuta ambao bei yake ni kati ya shilingi 2000 hadi 2500.

  Wakulima hao walizitaja changamoto walizonazo ni mazao yao kushambuliwa na wadudu waharibifu, ukame, kukosekana kwa elimu ya kilimo,pembejeo, mvua kutonyesha kwa wakati na zao la mhogo kushambuliwa na ugonjwa wa batobato na michirizi kahawia na kuwa changamoto hizo zinalingana na wilaya zingine za mkoa wa Mtwara. Mwezeshaji kutoka Jukwaa la Bioteknolojia kwa maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk. Hamalord Mneney aliwataka wakulima hao kuacha kilimo cha mazoea na kufanya kilimo cha Kisayansi kutokana na hali ya sasa ya tabia nchi.

  "Wakulima mnapaswa kubadilika na kuacha kulima kilimo cha zamani hivi sasa hali imebadilika hivyo mnatakiwa kufanya kilimo cha Sayansi na Teknolojia chenye tija na kufuata maelekezo ya wataalamu na kuachana na kilimo cha zamani" alisema Dk. Mneney.
  Wakulima wakiwa kwenye mafunzo hayo.

  Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Philbert Nyinondi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA), aliwataka wakulima hao kujiongeza zaidi na kubadili matumizi ya simu zao kwa kuzitumia kutafuta masoko na kuwasiliana na wenzao kuelezana changamoto walizonazo kwenye kilimo badala ya kutumia kwa matumizi yasiyo na tija. Wakulima walionufaika na mafunzo hayo ni kutoka Wilaya za Mtwara mjini, Vijijini, Nanyamba, Tandahimba, Newala, Masasi na Nanyumbu.

  0 0

  Mkurugenzi na muanzilishi wa Taasisi ya Young Scientist Tanzania(YST), Gozibert Kamugisha akizungumza na Waandiishi wa Habari juu ya Maonesho ya Wanasayansi Chipukizi yanayotaraji kuanza Agosti 8 mpaka 9 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es salaam. kulia ni Mkurugenzi wa Bg Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Royal Dutch Shell, Marc den Hartag

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Maonesho ya elimu ya Sayansi kwa wanafunzi wa Sekondari maarufu kwa jina la 'Young Scientist' yanataraaji kuanza agosti 8 hadi 9 mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Young Scientist Tanzania(YST),  Dr Gozibert Kamugisha amesema onesho hili la aina yake na litaonyesha kazi za kisayansi na ugunduzi kutoka kwa wanafunzi wa Sekondari 200 na walimu 100 kutoka mikoa yote Tanzania.

  “kwa siku mbili za onesho wanasayansi Chipukizi wataonesha kazi zao katika Nyanja mbalimbali za Sayansi kama vile kemia, fizikia, hesabu, Bailojia, ekolojia, Sayansi ya Jamii na Teknonojia. hivyo kazi nyigi zitakazooneshwa zimejikita katika kutoa njia za kukabiliana na matatizo ya afya, Kilimo na usalama wa matatizo ya kijamii zaidi”Amesema Kamugisha.

  Amesema Onesho hilo limewezeshwa na udhamini endelevu wa BG Tanzaniaa ambayo ni kampuni tanzu ya Royal Dutch ShellPlc na wadhamini wengine. Ametaja kuwa Wanasayansi Chipukizi watakaonesha kazi nzuri watazawadiwa pesa Taslimu ,Vikombe ,Medali na Vifaa vya Maabara.

  Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shell Afrikaa ya Mashariki na Bg Tanzaniaa, Marc den Hartog amesema kuwa wao kama Shell wanaona fahari kubwa kuwa mdhamini wa mashindno hayo kwa kwa kufanya hivyo ndivyo wataweza kupata wanasayansi wa baadae ambao wataweza kusaidia katika uchumi wa Viwanda na sekta ya gesi na mafuta .
  Mkurugenzi wa Shell Afrika Mashariki na Bg Tanzania, Marc Den Hartog akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya namna kampuni yake inavyodhamini Maonesho hayo yenye manufa kwa kizazi cha kuwaandaa magwiji wa Sayansi nchini. 
  Muasisi na Mkurugenzi wa ushauri wa Masuaala ya Kisayansi, Joseph Clowry akizuungumza mafanikio ya tasisi hiyo ndani ya miaka sita tangu ianze kuendesha maonesho hayo.
  Waandishi wa habari wakiendelea na mkutano huo katika Hotel ya Golden Tulip iliyopo katikati ya jiji.

older | 1 | .... | 1845 | 1846 | (Page 1847) | 1848 | 1849 | .... | 3286 | newer