Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109610 articles
Browse latest View live

NMB yawezesha wakunga Muhimbili kutoa huduma za afya bure.

0
0
Afisa Muuguzi Mwandamizi, Gudila Mambacho (kushoto) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akichukua vipimo vya presha toka kwa mmoja wa wananchi (kulia) waliojitokeza kupata huduma za afya bure zinazotolewa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Mmoja wa maofisa kutoka Benki ya NMB (kushoto) akimuhudumia mwananchi aliyejitokeza kupata huduma za kibenki kwenye kongamano la Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo mbali na huduma hizo za kibenki toka NMB, wananchi walipata huduma mbalimbali za afya bure, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani. Muuguzi mwandamizi na afisa lishe kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dotto Msabila Kafulie (kushoto) akimuhudumia mmoja wa wananchi aliyejitokeza kupata huduma za afya bure zinazotolewa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.

RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA BODI YA KAMISHENI YA ARDHI IKULU.

0
0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira,Bodi ya Kamisheni ya Ardhi na Uongozi wa Kamisheni ya Ardhi katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira,Bodi ya Kamisheni ya Ardhi na Uongozi wa Kamisheni ya Ardhi katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira,Bodi ya Kamisheni ya Ardhi na Uongozi wa Kamisheni ya Ardhi katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji,(kuchoto) Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi.

SIHABA NKINGA AKUTANA NA MKURUGENZI MKAZI WA SHIRIKA LA ‘WORLD EDUCATION INITIATIVE’ OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto (Idara kuu Maendeleo ya Jamii) Bibi Sihaba Nkinga (wa pili kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la ‘World Education Initiative’ Bi Lilian Badi (hayupo pichani) walipofika kutambulisha programu ya ‘Waache Wasome’ katika Ofisi ya Wizara iliyoko UDOM Dodoma leo Agosti 04, 2017.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bibi Magreth Musai (katikati) akichangia hoja katika kikao kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto (Idara kuu Maendeleo ya Jamii) Bibi Sihaba Nkinga(kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la World Education Initiative Bi Lilian Badi( wa pili kushoto) walipofika kutambulisha programu ya ‘Waache Wasome’ katika Ofisi ya Wizara iliyoko UDOM Dodoma leo Agosti 04, 2017.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la World Education Initiative Bi Lilian Badi(katikati) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto (Idara kuu Maendeleo ya Jamii) Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani) walipofika kutambulisha programu ya ‘Waache Wasome’ katika Ofisi ya Wizara iliyoko UDOM Dodoma leo Agosti 04, 2017.Picha na Erasto Ching’oro WAMJW.

NDUGAI AKUTANA NA SPIKA WA BUNGE LA IRAN NA KUFANYA NAE MAZUNGUMZO

0
0
 Mhe. Spika Job Ndugai  leo amekutana na Spika wa Bunge  la Iran, Mhe. Dkt. Ali  Larijani na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuimarisha mahusiano ya kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Iran.

TASAF YASHIRIKI MAONYESHO YA NANE NANE KANDA YA KATI DODOMA.

0
0
Na Estom Sanga-TASAF 

Vikundi vya baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF kutoka mikoa ya Dodoma, Pwani Manyara na Singida vinashiriki kwenye maonyesho ya nane nane yaliyoanza mwanzoni mwa wiki hii mjini Dodoma. 

Vikundi hivyo vilivyoko kwenye banda la Ofisi ya Rais kwenye eneo la maonyesho la Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma, vinaonyesha bidhaa zilizotengenezwa na vikundi hivyo baada ya kuwezeshwa na TASAF ikiwa ni njia mojawapo ya kuinua shughuli za uzalishaji mali na kuongeza mapato ya walengwa wa Mpango huo wenye lengo la kusaidia jitihada za serikali za kuwapunguzia wananchi kero ya umasikini. 

Bidhaa zinazotengenezwa na vikundi hivyo na ambazo zimeletwa kwenye maonyesho hayo ni pamoja na sabuni na mafuta ya manukato ambavyo vimetengenezwa kwa kutumia mmea wa mwani ambao humea kwenye maeneo ya baharini. 

Bidhaa nyingine ambazo zimezalishwa na vikundi hivyo vya walengwa wa TASAF ni pamoja na asali,ubuyu,mafuta ya alizeti na mifuko bora ya kuhifadhia nafaka ambavyo vimetokana na kazi za mikono ya walengwa hao ikiwa ni maojawapo ya sharti la kuzifanya kuinua uchumi na kujiongezea kipato kwa njia ya vikundi. 

Walengwa hao wamepongeza hatua ya serikali kupitia TASAF kuwashirikisha kwenye maonyesho hayo kwani hatua hiyo inasaidia kutangaza shughuli za uzalishaji mali zinzofanywa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini ambao wanahitaji masoko ya bidhaa wanazozizalisha ili kukuza uchumi wao. 

 Baadhi ya maafisa wa TASAF wakitoa maelezo kwa wanafunzi waliotembelea banda la maonyesho la TASAF kwenye viwanja vya nane nane ,Nzuguni nje kidogo ya mji wa Doodoma.

 Mmoja wa walengwa wa TASAF kutoka kikundi cha Wakulima wa Mwani Msichoke cha Bagamoyo akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la TASAF. Kikundi hicho kimewezeshwa na TASAF na sasa kinatengeza sabuni na mafuta kutokana na zao la mwani kama njia ya kujiongezea kipato.

Mtaalam wa Mawasiliano wa TASAF Bi. Zuhura Mdungi akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea banda la maonyesho la TASAF lililoko kwenye jingo la Ofisi ya Rais kwenye eneo la Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 Mmoja wa maafisa wa TASAF, Bi. Grace Kibonde akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea banda la TASAF kwenye maonyesho ya nane nane  kwenye eneo la Nzuguni  nje kidogo ya mjini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Muhimbili Wajadili Mikakati ya Kuboresha Huduma za Afya

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji Baraza la Wafanyakazi ambacho kimefanyika leo katika hospitali hiyo. Kikao hicho kinajadili jinsi ya kuboresha huduma za afya zinazotolewa na MNH.
Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Museru.
Mkurugenzi wa Fedha na Mipango, Gerald Jeremia akieleza mikakati ya kuboresha huduma za afya katika kurugenzi ya upasuaji pamoja na huduma nyingine.
Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Fedha na Mipango leo.
Mshauri Mwelekezi katika Masuala ya Mawasiliano, Dk. Henry Mambo akieleza mkakati wa mawasiliano ambao umeandaliwa kwa ajili ya kufikia malengo ya kutoa huduma bora.

RC PAUL MAKONDA APOKEA VITANDA 150 NA MAGODORO 150 VYENYE THAMANI ZAIDI YA SHILINGI MILION 300

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amepokea Vitanda 150 na Magodoro 150 vyenye thamani zaidi ya shilingi Milion 300 kutoka kampuni ya mafuta ya Camel chini ya Kampuni tanzu za Amsons Group, iliyoamua kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa katika kuboresha sekta ya Afya.

Akizungumza baada ya kupokea Vitanda hivyo, Makonda amesema amedhamiria kuhakikisha changamoto zote zinazoikabili sekta ya Afya katika Mkoa wa Dar es Salaam zinamalizika ili kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya.

“Sitaacha kutafuta kwa ajili ya Wananchi wa Dar es salaam, nitabisha hodi kila panapostahili ili mradi Wananchi wangu wawe wanapata huduma za Afya katika mazingira mazuri, ili siku moja waone kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli, sisi tunataka Maendeleo na sio Siasa ndio maana hivi vitu vyote tunavyofanya vinatumiwa pia na wapinzani” Alisema Makonda.

Makonda amesema anatamani siku moja kila mama anaekwenda kujifungua alale kitanda kimoja mwenywe na sio kama ilivyo sasa ambapo wanatumia kitanda kimoja kinamama watatu hadi wanne.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa,Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kupokea  Vitanda 150 na Magodoro 150 vyenye thamani zaidi ya shilingi Milion 300 kutoka kwenye  kampuni ya mafuta ya Camel chini ya Kampuni tanzu za Amsons Group iliyomua kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa katika kuboresha sekta ya Afya. 
.Meneja Uendelezaji wa Biashara Kampuni ya Camel Oil,Suleiman Amour (kulia) akimkabidhi   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa,Paul Makonda Vitanda 150 na Magodoro 150 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Million 300 kutoka kwenye  kampuni ya mafuta ya Camel chini ya Kampuni tanzu za Amsons Group. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

TAARIFA KUHUSU UAMUZI WA SPIKA KWA WABUNGE WAWILI WA CUF WALIOFUKUZWA UANACHAMA


WIZARA YA AFYA MAENDELEO YAJAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO YA JAMII NCHINI KUJADILI SERA YA MAENDELEO YA WANAWAKE NA JINSIA MJINI DODOMA.

AfDB YAISAIDIA SERIKALI KUWAONDOLEA WAKAZI WA ARUSHA ADHA YA UMEME KUKATIKA MARA KWA MARA

0
0


Na Benny Mwaipaja, WFM-Arusha

WAKAZI wa Jiji la Arusha wameondokana na na adha ya umeme kukatika mara kwa mara baada ya kukamilika kwa mradi wa umeme katika Kituo cha kupoozea umeme cha Njiro kilichoko Mkoani Arusha chenye uwezo wa kuzalisha megawati 130.

Hali hiyo inatokana na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB kuwekeza kiasi cha Dola milioni 4.2, ukiwa ni mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili kuongeza uwezo wa Kituo hicho kuzalisha umeme unaotumika kwa ajili ya makazi ya watu, maeneo ya biashara na viwanda.

Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Usambazaji umeme cha Njiro Mhandisi Lembrice Mollel amesema mradi huo umesaidia kuongeza Megawati 130 za umeme ambao umekidhi mahitaji ya Jiji la Arusha linalo hitaji Megawati 60 hivyo kubakiwa na Umeme wa ziada kiasi cha Megawati 70.

Alisema kuwa tatizo la kukatika katika kwa umeme katika mji huo wa kitalii na kibiashara litakuwa historia na kwamba umeme unaozalishwa kituoni hapo unasafirishwa kwenye maeneo mengine yenye uhitaji ikiwemo mikoa ya Kilimanjaro na Tanga.


Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Kupoozea Umeme cha Njiro Mkoani Arusha, Mhandisi Lembrice Mollel, akitoa maelezo kuhusu mitambo ya Kituo hicho kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt Nyamajeje Weggoro (kulia) alipotembelea Kituo hicho kukagua mradi wa kusambaza umeme uliofadhiliwa na AfDB, uliogharimu Dola milioni 4.2, Jijini Arusha 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt Nyamajeje Weggoro (wa pili kulia) akipewa maelekezo ya namna mitambo ya usambazaji umeme katika Kituo cha Njiro Jijini Arusha inavyoendeshwa kwa mfumo wa Kidigitali. Mitambo hiyo imefadhiliwa na Benki ya AfDB ukiwa ni mkopo wenye masharti nafuu. 
Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Umeme cha Njiro Mkoani Arusha, Mhandisi Lembrice Mollel (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki Dkt Nyamajeje Weggoro (katikati) alopotembelea Kituo cha kusambaza umeme cha Njiro Jijini Arusha. Mitambo hiyo imefadhiliwa na Benki ya AfDB. Kushoto ni Meneja wa Mradi wa umeme wa AfDB Mhandisi Florence Gwang’ombe. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa Kituo cha Kupoozea Umeme cha Njiro, Mkoani Arusha, kuhusu usalama wa mitambo kutakapo tokea dharula. Mitambo hiyo imefadhiliwa na Benki ya AfDB, ikiwa ni mkopo wenye masharti nafuu.

ULAJI NYAMA ISIYO NA KIWANGO NI CHANZO CHA MAGONJWA.

0
0

Na: Agness Moshi – MAELEZO.

Ulaji wa nyama una faida lukuki kwa afya ya binadamu ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa virutubisho vya aina ya protini ambayo ni rahisi kutumika mwilini, madini mbalimbali (Calcium, Magnesium, Phosphorus, Zinc na Chuma); vitamini aina ya folic asidi, E, B na B12 ambayo inapatikana katika nyama pekee.

Nyama pia inasaidia katika ukuaji na kuongeza afya ya mlaji kutokana na uwezo mkubwa wa kujenga mwili, kukarabati seli za mwili zilizokufa, kuzalisha chembe hai mpya, kurekebisha kinga ya mwili, kuongeza damu na kuimarisha mifupa.

Hata hivyo faida zote hizo zinapatikana tu, kwa walaji wa nyama iliyo bora na yenye kiwango. Hivyo ni vizuri wananchi wakazingatia kanuni za ulaji wa nyama yenye kiwango ili kujiepusha na athari zinazoletwa na nyama isiyo na kiwango.

Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Bi.Suzana Kiango amesema kuwa nyama yenye kiwango na bora huanzia kwenye utunzwaji wa mifugo wenye kuzingatia kanuni za uzalishaji bora, unenepeshaji wa mifugo yenye umri mdogo kwa kuwalisha chakula mchanganyiko kwa muda usiopungua siku 90 kabla ya kuchinja.

Bi.Kiango amesema kuwa hatua nyingine ni katika uchinjaji ambapo inashauriwa ufanyike kwenye machinjio bora ambayo yanakidhi viwango vya usafi. Hii ni pamoja na kuwa na sakafu na kuta zinazosafishika, maji ya kutosha na sehemu za kuning’iniza wakati wa kuchuna na kupasua.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAHAKAMA YAIMARISHA HAKI ZA WATOTO KWA VITENDO

0
0
Na Lydia Churi-Mahakama

Mahakama ni moja kati ya Mihimili mitatu ya dola wenye jukumu la msingi la kutoa haki sawa kwa wote na kwa wakati. Mhimili huu hufanya kazi ya kutafsiri Sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwapatia wananchi haki. Kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano, Mahakama ya Tanzania imeendelea kusimamia haki za Watoto kama zilivyo haki nyingine wanazostahili kuzipata wananchi wa Tanzania.

UtekelezwajiwahakizaWatoto zilizoainishwakatika mikatabambalimbali yakikandana Kimataifa na kupewa nguvu ya kisheria kupitia Sheria ya Mtoto namba 21yamwaka2009,kunahitajiushirikianobainayaTaasisina wadau wa haki za watoto. Katika kulinda haki za watoto wa Tanzania, hivi karibuni, Mahakama ya Tanzania ilizindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) katika jiji la Mbeya na kufanya idadi ya Mahakama hizo kufikia mbili hapa nchini. Mahakama nyingine ya Watoto iko Kisutu jijini Dar es salaam.

Maendeleo Endelevu hupatikana kwakuzingatia misingi ya hakiza Watoto

Kwa kutambua umuhimu wa watoto kuwa ni uhai wa taifa lolote,Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) ilichukua hatua za makusudi kuhakikisha haki za kisheria za watoto zinalindwa kwa kujenga jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya. Jengo hili linakuwa ni la pili maalum kujengwa kwa shughuli za Mahakama ya watoto pekee kwa Tanzania bara. 

Akizindua jengo hilo hivi karibuni, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alisema endapo haki za Watoto zitadharauliwa kwa mapanayakesasa,basi azmayamaendeleo endelevu ya nchi hapo baadaye, itakuwa hatarini.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akikata utepe kuzindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) leo jijini Mbeya. Hii ni Mahakama ya Pili ya Watoto nchini Tanzania baada ya ile iliyoko Kisutu Jijini Dar es salaam. Mahakama hii imejengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF).
Mwakilishiwa UNICEF nchini, Stephanie Shanler akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Mahakama hiyo.
KaimuJajiMkuuwa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim JumaakifunguaPaziakuashiriauzinduziwa Mahakamaya Watoto (Juvenile Court) leojijiniMbeya. KatikatiniMwakilishiwa UNICEF nchini, Stephanie ShanlernakushotoniJajiKiongoziwaMahakamaKuuya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali.



RAIS MUSEVENI AWASILI JIJINI TANGA TAYARI KWA SHEREHE ZA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI HAPO KESHO

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga akiwa ameongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (haonekani pichani) na kupokewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tayari kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika Agosti 5 2017 katika eneo la Chongoleani.
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga akiwa ameongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kupokewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tayari kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika Agosti 5 2017 katika eneo la Chongoleani.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 04.08.2017

MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO AUG 5,2017


Idara yake ya Uhamiaji yawahakikishia Watanzania, kuwachukulia hatua raia wote wa kigeni wanaoingia nchini kinyume cha Sheria za Uhamiaji na nchi yetu

huduma ya fomu ya maombi ya pasipoti mtandaoni kuanzia Agosti 7, 2017

0
0
Idara ya Uhamiaji inapenda kuutangazia umma kuwa imezindua rasmi huduma ya fomu ya maombi ya pasipoti mtandaoni (Online Passport Application Form). Huduma hii inapatikana katika tovuti ya Idara kupitia link ifuatayo: https://www.immigration.go.tz/ppt_application/ na itaanza kutumika rasmi kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 07 Agosti, 2017. 

Kufuatia kuzinduliwa kwa huduma hii, waombaji wote wa pasipoti wanashauriwa kuzijaza fomu hizo mtandaoni, Kisha kuzichapisha (Printing) na kuziwasilisha katika Ofisi za Uhamiaji.

Hata hivyo, matumizi ya huduma hii yataenda sambamba na huduma inayotumiwa sasa ya fomu za maombi ya pasipoti mpaka pale itakapotangazwa vinginevyo. 

Utaratibu wa namna ya kujaza fomu hizo umeelekezwa katika fomu husika mtandaoni, na pia wateja wanaweza kupata ufafanuzi au maelezo zaidi kuhusu huduma hiyo kupitia anuani ya Idara ambayo ni  info@immigration.go.tz au katika Ofisi yoyote ya Uhamiaji iliyo karibu nao. 

Taarifa zaidi kuhusu huduma hii zitaendelea kutolewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Imetolewa na:

KITENGO CHA UHUSIANO,
MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI,
04 AGOSTI, 2017.

SHEREHE ZA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI BOMBA LA MAFUTA GHAFI KUTOKA HOIMA MPAKA CHONGOLEANI, TANGA ZAENDELEA HIVI SASA

0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri  Kaguta Museveni  wakiwasili katika viwanja vya Chongoleani, Mkoani Tanga tayari kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa  mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.



Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri  Kaguta Museveni  wakifurahi jambo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakiwa katika viwanja vya Chongoleani, Mkoani Tanga tayari kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa  mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri  Kaguta Museveni, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (wa tatu kushoto), Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) pamoja na viongozi wengine wakiwa wamesimama wakati wimbo wa taifa ukiimbwa.
Wananchi wakishangilia wakati Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri  Kaguta Museveni  wakiwasili katika viwanja vya Chongoleani, Mkoani Tanga tayari kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa  mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.

NEC YAPONGEZWA KWA USIMAMIZI NA MATUMIZI BORA YA RASILIMALI ZA SERIKALI

0
0
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani (Kulia) akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) alipotembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi eneo la kuhifadhia Mashine za BVR. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuendelea kusimamia matumizi bora ya rasilimali inazopewa na Serikali na kuzitaka taasisi nyingine za Serikali kuiga mfano huo.

Mhe. Muhagama ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora iliyoridhia Bunge lipitishe fedha kiasi cha shilingi bilioni 10 kuiwezesha Tume kufanya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini .

Akizungumza na watendaji na baadhi ya watumishi wa Tume amesema kuwa ameridhishwa na utendaji kazi wao na namna Tume ilivyojipanga kutekeleza jukumu la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuelekea uchaguzi ujao wa mwaka 2020 kwa kuwa na mpango Kazi, unaochambua na kubainisha mahitaji muhimu yanayotakiwa, lini na wapi ili kazi hiyo iweze kufanyika kwa umakini. 
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitazama moja ya Daftari la Wapiga Kura alipotembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani na Kushoto ni Afisa TEHAMA wa Tume Bi. Mwamvita Solo.

“ Naipongeza sana Tume kwa kuendelea kufanya vizuri , nimegundua kuwa imejipanga vizuri kutekeleza majukumu yake ambayo yameainishwa Katika Katiba,  kwa niaba ya Waziri Mkuu nimekuja hapa na timu ya watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora walioridhia Bunge lipitishe fedha shilingi Bilioni 10 ili kuiwezesha kufanya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura” Amesema.

Mhe. Mhagama ameeleza  kuwa kazi hiyo kazi ya utekelezaji wa maagizo hayo ya Bunge inazingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 5 kifungu kidogo cha 3 (a) ambacho kimeweka uanzishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini na Ibara ya 74 kifungu kidogo cha 6 (a) na (e) ambacho kinaipa Tume madaraka ya kuchukua jukumu la kuandikisha wapiga Kura nchini Tanzania.
Afisa TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Julius Kobelsiki akitoa ufafanuzi kuhusu Mashine ya kuandikisha Wapiga Kura ya BVR kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es salaam.

Aidha, ameongeza kuwa Sheria ya Uchaguzi kifungu cha 15 (3) kinaipa madaraka Tume ya Uchaguzi  kutengeneza mfumo na utaratibu wa  uandikishaji wa wapiga Kura nchini na uboreshaji wa daftari hilo mara mbili kati ya Uchaguzi mkuu mmoja na unaofuata.

“Tunaelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa hiyo ili tuzingatie takwa la Katiba na takwa la Sheria ya Uchaguzi ambayo inasimamiwa na Tume ni lazima sasa Serikali ione kwamba inaisaidia Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wote tunajua kuwa utendaji wake ni huru lakini Serikali tunaowajibu wa kuhakikisha kuwa Tume inafanya kazi yake vizuri” Amesisitiza.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ameipongeza uongozi wa Tume  kwa kuonyesha mfano katika kuondoa mazoea katika utendaji kazi ikiwemo utunzaji wa mali na rasilimali za Serikali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya watendaji na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika Ofisi za Tume jijini Dar es salaam. Kulia kwake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kulia). Picha na Aron Msigwa.

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuijengea uwezo Tume kwa kuipatia rasilimali na vitendea kazi inavyohitaji ili iweze kutimiza majukumu yake kwa wakati.

Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo amemshukuru viongozi hao kwa kuzitembelea ofisi za Tume kuangalia maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuishukuru Serikali kwa kutenga shilingi Bilioni 10 zitakazotumika kwa ajili ya uboreshaji huo.

 Amesisitiza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imejipanga kulitekeleza jukumu hilo kikamilifu na inaendelea kufanya maandalizi mbalimbali yakiwemo ya kuzipitia Mashine za BVR zitakazotumika kuandikisha wapiga Kura , kupitia mifumo Sheria na kanuni za Uboreshaji, kupitia vifaa vilivyopo ili kupunguza mzigo wa kununua vifaa vipya wakati wa zoezi hilo.

SHEREHE ZA NANENANE NI DARASA MUHIMU KWA WAKULIMA

0
0
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo (Kushoto) ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu akisikiliza kwa makini maelekezo ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu akiwasili katika banda la wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo (Kushoto) ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu akisikiliza kwa makini maelekezo kwa Mkurugenzi wa Farm Base Ltd Ndg Suleiman Msellem kuhusu Pembejeo za kilimo, na ushauri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi

Viewing all 109610 articles
Browse latest View live




Latest Images