Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA JUMANNE LEO AUG 1,2017


MWENYEKITI CHARLES MAKOGA : SHERIA MPYA KUTUMIKA KUKUZA MAPATO YA MJI WA MAFINGA

$
0
0

Na fredy Mgunda, Mafinga

Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoni Iringa inatarajia kukuza mapato katika mwaka Mpya wa 2017/2018 kutokana na kuanza kuzitumia sheria mpya za ukusanyaji mapato pamoja na kuvijua vyanzo vingine vya mapato ambavyo ndio vitasababisha kukuza uchumi wa halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa baraza la madiwani Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga alisema kuwa sheria mpya walizoletewa toka mwezi wa tano zinawapa nafasi ya kuanza kuzitumia wakati wa kukusanya mapato katika maeneo ambayo walikuwa hawakusanyi.

"Tulikuwa hatukusanyi mapato katika maeneo ya stand,sehemu za maegesho ya magari,sokoni na maeneo mengine kwa kuwa sheria zilikuwa bado si rafiki kwetu kwenda kukusanya mapato ila kwa mwaka unaoanza tutakusanya mapato na kukuza mapato kutoka asilimia 56 hadi kuvuka lengo la serikali la asilimia 80" alisema Makoga

Makoga aliwataka wananchi na viongozi kushiriana kukusanya mapato kulingana vyanzo ambavyo madiwani wameviolozesha kwa manufaa ya halmashauri ya Mafinga Mjini ambavyo vipo kisheria kutoka serikali kuu.

Jamani naombeni mchango wetu kufanikisha swala hili la kukusanya mapato ili tufikie lengo la serikali kwa kuwa mwaka huu hatufikia lengo hilo ni aibu kubwa kwa serikali hii ya awamu ya tank ambayo inaenda kwa kasi kubwa kwa kukuza uchumi wa nchi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga akizungumza wakati wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Mji wa Mafinga wakiwa katika baraza pamoja na wataalamu mbalimbali wa halmashauri hiyo.


NBC YASHEREHEA MIAKA 50 PAMOJA NA KUZINDUA KLABU YA BIASHARA JIJINI MWANZA.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella (katikati), akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi baada ya kuzindua Klabu ya Biashara mjini Mwanza hivi karibuni. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein. NBC imezindua Klabu ya Biashara iliyopewa jina la ‘NBC B-Club’ katika miji ya Kahama na Mwanza kwa kuandaa semina kwa wafanyabishara wajasiriamali.   NBC B-Club itasaida  huduma zisizo za kifedha kupitia mafunzo maalumu kwa kushirikiana  na wadau mbalimbali kuhusu mbinu za uendeshaji wa biashara na kuwajengea uwezo katika kuziendesha kwa ufanisi hivyo kukuza biashara hizo. 
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akihutubia wakati sherehe za uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara jijini Mwanza hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, aliyekuwa mgeni rasmi na Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Filbert Mponzi.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akihutubia wakati wa semina ya wafanyabiashara katika uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara ya NBC mjini Mwanza. Wengine kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi na Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Filbert Mponzi. 
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya mika 50 ya benki hiyo mjini Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati), akizungumza na ujumbe wa viongozi wa NBC waliofika ofisi kwake kumtembelea wakiongozwa na Dk. Kassim Hussein (kulia kwake) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theoblad Sabi (kushoto kwake). NBC ilizindua klabu za biashara katika miji ya Kahama na Mwanza pamoja na kusherehekea miaka 50 tokea ilipoanzishwa.  

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA MIRADI WILAYA YA MBEYA MJINI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Methadone Clinic ambao ni maalum kwa kuwahudumia na kuwapa ushauri nasaha waathirika wa madawa ya kulevya kwenye . hospitali ya Rufaa ya Mbeya Julai 31, 2017. Kushoto ni Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7118
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa  Salim Jessa  (wanne kushoto) ambaye ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Malumalu kilichopo Iyunga jijini Mbeya  wakati alipoembelea kiwanda hichi Julai 31, 2017.  Watatu kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7147
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa  Salim Jessa  (kulia) ambaye ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Malumalu kilichopo Iyunga jijini Mbeya  wakati alipoembelea kiwanda hicho Julai 31, 2017. Kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7364
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha vinywaji baridi  cha SBS- Pepsi kilichopo eneo la Iyunga jijini Mbeya, Julai 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7413
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wakazi wa Mbeya baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya  Ruanda Nzove jijini humo kuhutubia mkutano wa hadhara, Julai 31, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7422
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

KIPINDI CHA BBC DITA YA DUNIA

DC MNDEME AMPONGEZA MAVUNDE KWA KUTATUA KERO YA MAJI KWA WANANCHI WAKE

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Christine Mndeme leo amezindua mradi wa Maji katika kijiji cha Mhande,Kata ya Ngh’ong’hona ambao umefadhiliwa na Shirika shirika la wamishionari wa damu takatifu ya Yesu(CPPS) uliogharimu kiasi cha Sh.Milioni 35.

Mradi huu umetokana na maombi ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa Shirika la hilo kusaidia kutatua changamoto ya Maji katika kata hii ya Ngh’ongh’ona ambayo wananchi wake wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo kubwa la upatikanaji maji safi na salama.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mndeme amelishukuru shirika hilo la CPPS kwa ufadhili wa mradi huo na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa kuwa mstari wa mbele kutatua kero za wanachi wake hususani kero kubwa ya Maji katika kata ya Ngh’ongh’ona.

Amesema kutatuliwa kwa kero hiyo kumewatua kina mama ndoo kichwani kwa kuwa walikuwa wakienda kuchota maji umbali mrefu.

“Mwili unahitaji maji unapotafuta maji mbali roho inasononeka hata muda wa kusali unaukosa, tunashukuru sana shirika hili lakini wananchi tuna wajibu wa kuutunza mradi huu ambao ni wa thamani kubwa sana,”amesema

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akifurahi jambo na wafadhili wa mradi wa maji wa Mhande kutoka Canada. 
Wananchi wa Mhande wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Chritine Mndeme katika uzinduzi wa mradi wa maji wa kijiji hicho. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme pamoja na Father Fransis wakifungua bomba la maji kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji katika  kijiji cha Mhande. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akisalimiana na father Fransis .


MANISPAA YA KINONDONI YAKABIDHIWA SHULE YA SEKONDARI MAENDELEO

$
0
0


Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Benjamin Sitta akizungumza na watumishi wa serikali na wanafunzi mapema jana katika hafla ya kupokea msaada wa shule ya sekondari ya Maendeleo yenye thamani ya sh milioni 800 iliyojengwa na kampuni ya magari ya (KIA) ya Korea Kusini na Good Neighbors jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Good Neighbour ambao ndio wadhamini wa shule hiyo,Namun Heo akizungunza na watumishi wa serikali katika hafla ya kukabidhi majengo ya shule ya sekondari ya Maendeleo yenye thamani ya sh milioni 800 iliyojengwa na kampuni ya magari ya (KIA) ya Korea Kusini na Good Neighbors,jijini Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Benjamin Sitta (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Good Neighbour,Namun Heo (kulia) wakisani hati ya makabidhiano ya shule ya sekondari ya Maendeleo iliyojengwa na kampuni ya magari ya (KIA) ya Korea Kusini na Good Neighbors,mapema jana jijini Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Benjamin Sitta (wa kwanza kushoto) akiwa ameambata na watumishi wa serikali wakikagua moja ya majengo ya shule hiyo.

Muonekano wa shule ya sekondari ya Maendeleo yenye thamani ya sh milioni 800 iliyojengwa na kampuni ya magari ya (KIA) ya Korea Kusini na Good Neighbors jana jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

JAFO APONGEZA MSHIKAMANO WA VIONGOZI NA WATENDAJI RORYA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewapongeza viongozi na watendaji wa wilaya na halmashauri ya wilaya ya Rorya kwa mahusiano mazuri waliyonayo katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Jafo alitoa sifa hizo alipokuwa wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi na kuongea na watumishi .

Katika ziara hiyo, Jafo alifanikiwa kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, mabweni, maabara, na vyoo kwa sekondari ya Nyamtinga na Nyamunga ambapo majengo hayo yamebainika kujengwa kwa ubora wa kuridhisha. 

Ujenzi wa miundombinu hiyo imegharimu zaidi ya sh.milioni 500 kutoka serikali kuu kwa lengo la kuboresha elimu hapa nchini
Kwa upande wake,Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara, Agness Marwa amempongeza Naibu Waziri huyo kwa kufika wilayani Rorya na kwamba amekuwa Waziri pekee aliyefanikiwa kutembelea wilayani humo katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano. 


Mbunge huyo ameishukuru serikali kwa upendo wake wa kuisaidia wilaya hiyo miradi ya maendeleo. Naibu Waziri Jafo leo amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku sita ya kukagua miradi ya maendeleo na kuongea na watumishi kwa mkoa wa Kagera na Mara na anaendelea na ziara yake katika mikoa mingine.

.Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikata utepe na kuweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari Nyamtinga wilayani Rorya. 
Baadhi ya vyumba vya madarasa vilivyokaguliwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo. 
Mbunge wa Vitimaalum Agnes Marwa akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Rorya na kuwapongeza kwa ujenzi wa madarasa na mabweni. 

NEWS ALERT: KESI YA WEMA SEPETU KUSIKILIZWA MCHANA HUU MAHAKAMA YA KISUTU

$
0
0
 Msanii wa filamu nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, akitoka mahakamani baada ya kesi yake kuahirishwa hadi saa Sita na nusu mchana, ambapo mkemia atakuja kutoa ushahidi wake dhidi ya kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili yeye pamoja na wafanyakazi wake wawili.


IN LOVING MEMORY OF CATHERINE FLORENCE MWANGOTA

Dkt. Harrison Mwakyembe awaahidi BFT kuwatatulia kero ya eneo la Mafunzo

$
0
0
Na Benedict Liwenga-WHUSM.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaana Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewaahidi Shirikisho la Masumbwi Tanzania (BFT) kuwatatulia kero ya eneo la kufanyia mafunzo pamoja na ofisi ambalo limekuwa likiwakabili kwa muda mrefu zikiwemo na changamoto nyingine za Shirikisho hilo.

Mhe. Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Viongozi na wajumbe mbalimbali wa shirikisho hilo ikiwa ni sehemu ya kutambua utendaji kazi wao na changamoto zinazowakabili ili ziweze kutatuliwa.

Dkt. Mwakyembe amesema kwamba, kutokana na tatizo la ukosefu wa eneo rasmi la ofisi na sehemu ya kufanyia mafunzo, yeye atawasiliana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ili kuona namna gani wanaweza kupata eneo kwa ajili ya kulisaidia shirikisho hilo kwa ajili ya kujenga ofisi na eneo la kufanyia mazoezi.

Sambamba na hilo, ameupongeza uongozi wa shirikisho hilo kwa kazi wanazozifanya na kuwataka wazidi kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) hususani katika kupeana taarifa zinazohusu maendeleo ya mchezo wa masumbwi nchini.

“BFT jitahidini muwe na ushirikiano wa karibu na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na msifanye mambo yenu kimya kimya, muwasiliane kwa karibu na BMT kwani hii itasaidia Wizara kushughulikia kero zenu mbalimbali kuliko mkichelewa kutoa taarifa mapema”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha, amewahakikishia kuwa, yupo tayari kutafuta wafadhili ndani na nje ya nchi ili waweze kulisaidia shirikisho hilo kutatua kero za uhaba wa vifaa, rasilimali fedha pamoja na ukosefu wa mafunzo kwa makocha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo amelitaka shirikisho hilo kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali ikiwemo kujenga tabia ya ulipaji kodi, kuwaelimisha Wanamasumbwi kuachana na tabia chafu wanapokuwa michezoni pamoja na kuachana na kujihusisha na madawa ya kulevya.

Kwa upande wao Viongozi wanaounda shirikisho hilo pamoja na wajumbe kwa pamoja wamemuahidi Waziri Mwakyembe na Wizara kwa ujumla kuzingatia masuala mbalimbali ikiwemo kuboresha suala la mawasiliano kati ya Shirikisho na Wizara, kufuatilia suala la mikataba mbalimbali na uwajibikaji yakinifu.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akionyesha Jarida la Mpango Mkakati la Shirikisho la Masumbwi Tanzania (BFT) mara baada ya kufanya nao mazungumzo katika Ofisi za Wizara 01 Agosti, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa Iringa akabidhi Milioni 20 za Biko kwa mshindi wao

$
0
0




*Ally Issa Kumburu naye akabidhiwa Mil 10 zake Dar es Salaam

MKUU wa Mkoa Iringa, Amina Masenza, jana ameshiriki kumkabidhi mshindi wa Sh Milioni 20 wa mjini Iringa, Viane Kundi, ambaye aliibuka na ushindi wa fedha hizo katika droo ya 27 iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, RC Masenza alimpongeza mshindi huyo pamoja na kumtaka atumie fedha hizo kujikwamua kiuchumi kutokana na mamilioni hayo.

Alisema mchezo wa bahati nasibu ni moja ya sekta inayoweza kuinua uchumi wan chi endapo washindi watazitumia fedha zao kwa uangalifu, huku akiwahamasisha Watanzania, wakiwamo akina mama kucheza kwa wingi.

“Biko ni mchezo mzuri hata mimi nitaanza kucheza, hivyo naomba Watanzania wote tucheze Biko ili tuweze kuibuka na zawadi mbalimbali za Biko, ukizingatia kuwa pesa hizi zitakuwa mwangaza kwa washindi wote,” Alisema.


Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema Biko ni mchezo unaotoa ushindi kwa kiasi kikubwa kwa washindi wake kuzoa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja inayoingia kwenye simu ya mshindi dakika chache baada ya kushinda.

“Bahati nasibu yetu inachezwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema.


Mkuu wa Mkoa Iringa, Mheshimiwa Amina Masenza wa pili kutoka kulia akimkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wa Biko droo ya 27, Viane Kundi wa mjini Iringa aliyeibuka kidedea Jumapili iliyopita. Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles na kulia ni mtumishi wa NMB, Iringa,
Mshindi wa Biko wa Sh Milioni 20 Viane Kundi akifurahia fedha zake baada ya kukabidhiwa jana mjini Iringa katika benki ya NMB.



Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko kutoka mkoani Iringa, Viane Kundi akiwa na mume wake pamoja na mtoto wao wakifurahia donge nono la Biko baada ya kukabidhiwa katika benki ya NMB Mkoani Iringa.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

DKT. ALBINA CHUWA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU UNAOENDELEA MKOANI DODOMA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina  Chuwa (wa pili kulia) akizungumza na mmoja wa mafundi wanaojenga Jengo Jipya la Makao Makuu ya ofisi hiyo mkoani Dodoma wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi huo. Wa kwanza kushoto ni Mhandisi John Ainainyi Njau kutoka Benki ya Dunia - Tanzania.
 Muonekano wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu linalojengwa mkoani Dodoma.
 Baadhi ya mafundi wakiwa wanaendelea na kazi ya ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) linalojengwa mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa waandamizi  wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya ofisi hiyo mkoani Dodoma. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

Aliyeipaisha Tusiime kitaifa atamani PhD

$
0
0
MWANAFUNZI wa shule ya Sekondari ya Tusiime, Rashid Abdalah, aliyeshika nafasi ya tatu kitaifa kwa masomo ya biashara amesema nia yake ni kusoma hadi ngazi ya Shahada ya Uzamivu (PhD).

Akizungumza leo shuleni hapo Rashid amesema ndoto yake ya miaka mingi ni kuwa mkaguzi wa hesabu hivyo amenuia kusoma kwa bidii hadi afikie ngazi hiyo.

“Naamini nitafikia malengo yangu kwa kuwa najua siri ya kufika huko ni juhudi, kujitambua  na kuwasikiliza walimu, hakuna kingine zaidi ya kuwa makini na masomo na kuwa makini,” alisema Rashid ambaye alianzia kidato cha pili shuleni hapo mwaka 2012.

Amesema juhudi za walimu katika kufuatilia maendeleo ya wanafunzi na mazingira mazuri ya shule, ushirikiano mzuri na wanafunzi wenzake ni baadhi ya mambo ambayo yamekuwa chachu ya mafanikio yake.

Aidha amewaasa wanafunzi waliobaki shuleni hapo kujitambua wamefuata nini shuleni na kufuatilia kila wanachofundishwa na walimu wao ili mwisho wa siku wapate mafanikio kama yake.

“Kufaulu haiwezi kuwa muujiza ni juhudi tu na kusikiliza mafundisho na maelekezo ya walimu, lazima mtambue kuwa walimu wanataka mfaulu hivyo mkiwasikiliza na kuwafuata mtafaulu kwa viwango vya juu sana,” amesema Rashid alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa kidato cha tano shuleni hapo.

Mkuu wa shule hiyo, Emil Rugambwa, amesema mafanikio ya shule hiyo kwenye matokeo ya kidato cha sita ni mwendelezo wa mafanikio kwenye matokeo ya kitaifa ambayo shule imekuwa ikiyapata kuanzia yale ya darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili na cha nne.

Kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka huu, Tusiime imefanikiwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) hivi karibuni kwa kufaulisha wanafunzi wote 518.

Mwanafunzi bora nafasi ya tatu kitaifa katika masomo ya biashara wa shule ya Tusiime, Rashid  Abdalah aliyevaa flana, akifurahia na kupongezwa na wanafunzi wa kidato cha tano wa shule hiyo alipokwenda kuwatembelea na kuwadokeza siri ya mafanikio yake.

SERIKALI, WADAU KUANDAA RIPOTI YA KWANZA YA KITAIFA YA UTEKELEZAJI WA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU NCHINI

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza imeanza maandalizi ya ripoti ya utekelezaji wa haki za watu wenye ulemavu tangu Tanzania kuridhiria Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye ulemavu mwaka 2009.

Katika kufanikisha suala hili, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeandaa kikao kazi kinachoshirikisha wadau wa haki za watu wenye ulemavu nchini ili kushirikiana katika maandalizi ya rasimu ya awali ya ripoti ambayo itajadiliwa,kuboreshwa na hatimaye kuwasilishwa katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ikiwa ni hatua stahiki katika utekelezaji wa Mkataba wa Haki za watu wenye Ulemavu.

Kikao kazi hiki kinafanyika Mkoani Morogoro kuanzia leo tarehe 31 Julai 2017 mpaka tarehe 2 Agosti 2017 kwa lengo mahususi la kua na uelewa wa pamoja wa mfumo wa uandaaji ripoti za haki za watu wenye ulemavu wa Umoja wa Mataifa,kujadili na kutathmini utekelezaji wa Sheria ya Watu wenye Ulemavu,kutoa elimu kwa wadau kuhusu usimamizi na ulinzi wa haki za watu wenye ulemavu na kuandaa rasimu ya awali ya haki za watu wenye ulemavu.

Akifungua kikao kazi hicho,Ndugu Erick Shitindi , Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Vijana,Kazi,Ajira na Watu wenye Ulemavu ameeleza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 35 sehemu ya i na ii, ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu, kila nchi inapaswa kuwasilisha ripoti ya kitaifa miaka miwili mara baada ya kuridhia mkataba husika jambo ambalo Tanzania haijwahi kulitekeleza kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha kwa ajili ya maandalizi ya ripoti hiyo.

“Kwa mantiki hiyo,maandalizi ya ripoti hii yamekuja wakati muafaka na itaifanya Tanzania kuingia katika historia ya kutekeleza mikataba mbalimbali ya haki za binadamu ikiwemo haki za watu wenye ulemavu na kwa ujumla nchi ilishaanza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kutunga Sheria ya watu wenye ulemavu (The Persons with Disabilities Act,2010)”.anasistiza Katibu Mkuu Shitindi.


MAONYESHO YA WAZI YA FILAMU FUPI

HOSPITALI ZOTE ZA MIKOA ZIJENGE VITUO VYA METHADONE-MAJALIWA

$
0
0

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amegiza hospitali zote za mikoa nchini kujenga vituo vya kutolea huduma ya Methadone kwa ajili ya kuwahudumia waathirika wa dawa za kulevya.

Alitoa agizo hilo jana (Jumatatu, Julai 31, 2017) alipozindua kituo cha kuhudumia waathirika wa dawa za kulevya katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, ambapo alisema Serikali inaendelea na mpango wake wa kudhibiti uingizwaji wa dawa hizo.

Kituo hicho kinatarajiwa kuhudumia watumiaji wa dawa za kulevya katika mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini, ambayo ni Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya.

Waziri Mkuu alisema vituo vya kuhudumia waathirika wa dawa za kulevya ni msaada mkubwa kwa vijana kwa kuwa mbali na kupewa dawa pia watafundishwa stadi za maisha ili wanapomaliza matibabu waweze kushiri katika shughuli za maendeleo ikiwemo kujiajiri.

Hata hivyo aliwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuwafichua wazalishaji, watumiaji na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kwa sababu ni watu wanaoishi nao katika jamii.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Rodgers Sianga alisema licha ya matumizi ya dawa za kulevya kuathiri mfumo wa fahamu pia watumiaji wako katika hatari ya kuugua homa ya ini.

Alisema vituo hivyo licha ya kutoa dawa ya methadone pia waathirika wa dawa za kulevya ambao watagundulika kuwa na maradhi mengine kama ukimwi, kifua kikuu, matatizo ya kisaikolojia pamoja na homa ya ini pia watatibiwa katika vituo hivyo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt.Godlove Mbwanji alisema matumizi ya dawa za kulevya yamechangia ongezeko la wagonjwa wa akili mkoani Mbeya, ambapo mwaka jana  pekee walibainika wagonjwa 486.

JESHI LA ZIMAMOTO LAZINDUA KAMPENI YA NAMBA YA DHARURA 114 KUKABILIANA NA MAOKOZI YA MAISHA NA MALI

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye, akikabidhiwa kipeperushi na Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na kuzuia Uhalifu, ajali (UAC), Elliot Andrew(kushoto), wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Namba ya Dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine. Kulia ni Naibu Kamishna Rasilimali Watu wa Jeshi hilo, Billy Mwakatage. Uzinduzi huo umefanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye, akionyesha kipeperushi wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Namba ya Dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine. Wengine ni Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na kuzuia Uhalifu, ajali S(UAC), Elliot Andrew na Naibu Kamishna Rasilimali Watu wa Jeshi wa jeshi hilo, Billy Mwakatage(kulia).Uzinduzi huo umefanyika leo Makao Makuu ya Jeshi,jijini Dar es Salaam.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Namba ya Dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine. Wengine ni Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na kuzuia Uhalifu, ajali (UAC), Elliot Andrew na Naibu Kamishna Rasilimali Watu wa Jeshi hilo, Billy Mwakatage (kulia). Uzinduzi huo umefanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.


WATUMISHI HOUSING WAPELEKA MRADI WA NYUMBA 500 MKOANI DODOMA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KATIKA juhudi za kuunga mkono uamuzi wa serikali wa kuhamishia shughuli za serikali katika Mkoa wa Dodoma, Kampuni ya Watumishi Housing imepanga kuwajengea watumishi nyumba bora na za kisasa Mkoani humo.

Kampuni hiyo yenye dhamana ya uwekezaji katika nyumba ikiwa ni mpango wa taifa wa makazi kwa watumishi, imeamua kuwekeza katika Mkoa wa Dodoma na wameshapata eneo la Njedengwa lenye ukubwa wa  hekari 55 likiwa limeshapimwa tayari kwa ujenzi wa nyumba 500.

Akielezea mikakati hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Fredy Msemwa amesema kuwa katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba hizo zitajengwa nyumba 159 na zitakuwa kwa ajili ya watumishi watakaokuwa wamehamia Mkoani Dodoma na wale wanaoishi haoo.

Msemwa amesema, eneo la Njedengwa ni eneo ambalo limeendelezwa tayari likiwa lina huduma zote za kijamii ikiwemo barabara ya lami, maji, umeme na miundo mbinu mingine ambayo inalifanya kuwa eneo bora zaidi kwa makazi ya watumishi na yatai ujenzi umeshaanza na utakamilika baada ya miezi nane (8) na zitakuwa katika mfumo wa aina mbili zile zilizoisha kabisa na zitakazokuwa zimeisha kwa asilimia 80.

Nyumba hizo zitakuwa na mahitaji ya kutosha kabisa kwa watumishi wa umma wa kipato tofauti na utapatikana kwa njia ya mkopo endelevu kupitia benki washirika huku nyumba zilizokamilika kabisa zitauzwa kwa shilingi milioni 56 na zile zilizokamilika kwa asilimia 80 zitakuwa kwa milioni 46 zote zikiwa pamoja na VAT.

Mbali na hilo, Msemwa amesema wamepokea msaada wa vifaa vya upimaji wa viwanja na miji kutoka benki ya Dunia kwahiyo itarahisisha katika upimaji wa viwanja na pia kuanza kutoa huduma zote za makazi kuanzia uuzaji wa viwanja vilivyopimwa pamoja na nyumba zilizokamilika na huduma hii itaanzia mkoani Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Fredy Msemwa  akielezea namba walivyojizatiti katika kuiunga mkono serikali uamuzi wa kuhamishia shughuli za serikali katika Mkoa wa Dodoma ikiwa imepanga kuwajengea watumishi nyumba bora na za kisasa Mkoani humo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Watumishi Housing Raphael Mwabuponde akiwaelezea waandishi wa habari namna ya watumishi kupata nyumba hizo zitakazojengwa katika Mkoa wa Dodoma.

WANAOVAMIA MAENEO, UJENZI HOLELA MANISPAA YA DODOMA SIKU ZAO ZINAHESABIKA

$
0
0
 MKURUGENZI wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi ametoa wito kwa wakazi wa Manispaa hiyo kuacha mara moja uvamizi wa maeneo ya wazi na yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi za misitu ambapo watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha amewataka wanaojenga nyumba za makazi au za biashara katika maeneo yasiyo rasmi na ambayo hayakupimwa kusitisha shughuli za ujenzi na kubomoa majengo hayo kwa hiyari yao vinginevyo Halmashauri ya Manispaa itayabomoa.

Alisema hayo jana wakati akizungumza wa wamiliki wa nyumba za kupanga na Maofisa Watendaji wa Kata wa Manispaa ya Dodoma katika ukumbi wa Dodoma Sekondari, ambapo alisema kujenga katika maeneo yasiyopimwa ni kinyume na sheria na Manispaa ya Dodoma imejipanga kusimamia hilo kikamilifu.

Alisema Manispaa ya Dodoma imejipanga kuanza upimaji wa viwanja kwa kasi ili kuwawezesha wananchi  hususan wakazi wa Dodoma kujenga kwa kuzingatia sheria za Mipango Miji na kwamba upimaji huo utaenda sambamba na utoaji wa vibali vya ujenzi katika kipindi kisichozi siku saba kwa mmiliki wa kiwanja.

Kwa upande wa wamiliki wa nyumba za kupanga, aliwataka kuungana na kuwa na umoja na uongozi wao ili kuepukana na madalali ambao baadhi yao sio waaminifu, huku akiwapa changamoto ya kujenga nyumba zaidi za makazi na kuziimarisha zilizopo huku akiwajulisha kuwa, hivi karibuni watumishi  wa Serikali zaidi ya 2,000 wanatarajiwa kuhamia Mjini Dodoma ikiwa ni awamu ya pili ya Serikali kuhamia Dodoma hivyo mahitaji ya nyumba za kuishi yatakuwa makubwa.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akizungumza na wamiliki wa nyumba za kupanga Manispaa ya Dodoma (hawapo pichani) wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau hao na Mkurugenzi huyo jana Katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma. 

Baadhi ya wamiliki wa nyumba za kupanga katika Manispaa ya Dodoma wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (hayupo pichani) wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau hao na Mkurugenzi huyo jana Katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma.  PICHA NA RAMDHANI JUMA.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>