Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1833 | 1834 | (Page 1835) | 1836 | 1837 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Spika wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ametembelea Kiwanja cha Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria ambapo kinakusudiwa kujengwa ofisi za Ubalozi mjini Abuja. Anaemuonesha ni Mhe Elias Mwandobo, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini humo.Mwingine pichani ni Katibu wa Spika,Ndg.Saidi Yakubu.
  Spika wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwa kwenye  Kiwanja ambacho kinakusudiwa kujengwa Ofisi za Ubalozi mjini Abuja. Kushoto ni  Mhe Elias Mwandobo,Kaimu Balozi wa Tanzania nchini humo.

  0 0

  Katika kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kuleta maendeleo kwa wananchi kampuni ya magari ya Mantrack Tanzania jana imeendesha warsha fupi yenye lengo la kutambulisha vifaa na teknolojia mpya itakayoongeza ufanisi wa kazi hasa katika sekta ya ujenzi.

  Akizungumza na waandishi wa habari, mwakilishi wa kampuni ya Mantrack Tanzania alisema kuwa wameleta vifaa vipya vitakavyoendana na kasi ya maendeleo ya Serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha Tanzania mpya inajengwa na uchumi bora na yenye miundombinu bora.

  “Vifaa hivi ni imara na vinatumia teknolojia mpya na ya kisasa inayosaidia utendakaji wa shughuli za ujenzi kuwa rahisi. Tumeamua kuja na kasi ya serikali mpya ya kutenda vitu kwa urahisi na kwa ufanisi wa hali ya juu”.

  Tuna wakaribisha wadau wa ujenzi wafike kujionea wenye tunachosema. Alisema. Warsha hiyo imefanyika katika karakana ya Mantrack Tanzania iliyopo karibu na jengo la Quality Plaza barabara ya Nyerere na ilihudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka makampuni mbalimbali ya ujenzi hapa nchini waliofika kushuhudia vifaa hivyo vinavyofanya kazi.
  Mwakilishi wa ManTrack Tanzania akitoa maelezo mbalimbali kwa wadau juu ya teknolojia mpya na bidhaa zao mbalimbali.

  0 0


  0 0


  Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Mkoani Songwe, Haji Mnasi akiwa darasani kufundisha wanafunzi huku wanafunzi wakiwa makini kusikiliza nini wanachofundishwa na Mkurugenzi hiyo.
  Na Fredy Mgunda,Ileje

  Katika hali isiyozoeleke kwa watumishi wengi wa Idara ya Elimu wilayani Ileje mkoani Songwe kwa Mkurugenzi Mtedaji wa Halmsahauri ya wilaya hiyo kwa kuingia kwenye baadhi ya shule za msingi na kufundisha.

  Mkurugenzi huyo Ndugu Haji Mnasi ambaye kitaaluma ni mwalimu aliamua kufanya hivyo katika ziara ya kushtukiza aliyoifanya kweye shule za Nyerere,Rungwa na Itumba zilizopo katika kata za Itumba na Isongole Tarafa ya Bulambya.

  Akiwa katika shule ya Msingi Nyerere aliweza kufundisha masomo ya Kiiingeriza,Hisabati na Kiswahili, pia aliweza kupima uelewa wa wanafunzi pamoja na kutoa maswali machache ya kuandika.

  Ziara hiyo iliweza pia kumfikisha katika Shule ya Msingi Rungwa ambapo aliweza kuzungumza na walimu akiwapa moyo katika kuwapatia elimu bora wanafunzi akiwapa moyo wa utendaji kazi akiwataka kuzingatia maagizo mbalimbali ya serikali.

  Pia Mkurugenzi huyo,aliyekuwa amefuatana na mmoja wa viongozi wa Idara ya Elimu Msingi akiwa Rungwa aliweza kuzungumza na mafundi waliokuwa wakiendelea na ujenzi ambapo aliwataka kumaliza kazi kwa wakati wakifuata viwango vinavyotakiwa.

  Ziara yake kwa siku hiyo ilishia katika shule ya Msingi Isongole ambako alipata fursaa kufuwatathimini wanafunzi wa Darasa la Saba ambao walikuwa wametoka kumalizia mtihani wa Moko ya Wilaya.

  Mara baada ya kumalizia ufundishaji kwa masomo ya Hisabati,Kiswahili na Kiingereza Mkurugenzi huyo aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa jinsi walivyowaanda wanafunzi wao ambao wanatarajiwa kufanya Mtihani wa Taifa siku chache zijazo.

  Walimu kwa upande wao walimpongeza mwajiri wao kwa kuweza kutembelea shule yao na kuzungumza nao wakisema hali hiyo imewapaa ari ya kufanya kazi wakishauri ziara hiyo iendelee na kwa shule zingine

  Mwalimu Denis Umbo alisema kuwa ,kitendo cha mwajili wao kuingia darasani hakijawatia moyo wa kufanya kazi tu bali ameitendea haki taaluma yake na kujionea hali halisi ilivyo mashuleni badala ya kusubiri taarifa za mezani.

  Si hayo tu yaliyojili katika shule hiyo pia Mkurugenzi alibahatika kuzungumza na wananchi waliokuwa kwenye mkutano ambao pamoja na mambo mengine walitarajia kujadili masuala mbalimbali ya shule likiwemo la chakula cha mchana kwa wanafunzi na taaluma.

  Mnasi aliwataka wazazi hao kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano juu ya utoaji elimu bure kwa watoto wote hapa nchini.

  0 0

  Taasisi ya Fikra ya Jijini Dar es salaam, ambayo imeamua kujikita katika kuwahamasisha vijana hasa wanaosoma shule za msingi, sekondari na wanafunzi wa vyuo, ikiwa na lengo kuongea nao kuhuhsu changamoto zinazowakabili na kuweza kutambua vipaji vyao, imefanya ziara katika Sekondari Shungibweni ambayo ni ya wasichana iliopo Mkuranga, mkoani Pwani. 

  Taasisi hiyo ambayo imezinduliwa hivi karibuni, ilitembelea shule hiyo na kufanya Uzinduzi wake rasmi na baadae kutoa mafunzo mbalimbali kwa wanafuunzi wa shule hiyo.

  Ujumbe wa taasisi hiyo ulijumuisha waanzilishi wote wa taasisi hiyo ambao ni
  Tarqi Mikidadi Mressa, Kassim Suleman Mketema, Maguli Meja Kapalata, Kennedy Alphonse Mlawa na Ally Mchume. Wanafunzi wa shule hiyo walifurahia ujio huo wa Fikra Foundation katika shule yao.
  Sehemu ya Wanafunzi wa shule hiyo wakifatilia kwa makini mafunzo waliyokuwa wakitariwa kutoka kwa ujumbe wa Taasisi ya Fikra.
  Picha ya pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo.
  Mafunzo yakiendelea.

  0 0

  Shirika la MajiSafi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia wateja wake wote wa jiji la Dar-es-salaam, pamoja na Mji wa Kibaha Mkoani Pwani kuwa mtambo wa uzalishaji Maji wa Ruvu Juu utazimwa kwa wastani wa Saa 8, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni, siku ya Jumatatu tarehe 31/07/2017.

  Sababu ya kuzimwa kwa Mtambo : Kumruhusu Mkandarasi (WABAG), kukamilisha Mfumo wa umeme katika mtambo mpya wa uzalishaji Maji wa Ruvu Juu uliopo Mlandizi mkoani Pwani.

  Maeneo yatakayoathirika na Kuzimwa Kwa Mtambo huu:

  Mlandizi Mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Disunyara, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misugusugu, Tanita, Kibondeni, Kwa Mathias, Nyumbu, Msangani, Kwa Mbonde, Picha Ya Ndege, Sofu, Lulanzi, Gogoni, Kibamba, Kibamba Njia Panda Shule Kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba Hospitali, Kwa Mkinga, Luguruni, Kimara, Ubungo, na baadhi ya maeneo ya Tabata.

  Toa taarifa Dawasco kupitia vituo vya wateja  Dawasco kimara 0743-451865, Dawasco Tabata 0743-451867, Dawasco Kibaha 0743-451875.

  Dawasco inawaomba wateja kutunza Maji ya kutosha pindi Mtambo utakapokamilika
  Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi: Kituo cha huduma Kwa wateja 0800110064 (BURE) au Tembelea: www.dawasco.go.tz

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania wanaofanya kazi katika viwanda mbalimbali nchini kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu. Amesema Tanzania imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda hivyo ni vema watakaopata fursa ya ajira katika viwanda hivyo kuwa waadilifu.

  Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 30, 2017) wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha gesi cha Ikama kilichoko wilayani Rungwe. Waziri Mkuu amesema wakati Serikali ikiendelea kuwakaribisha wawekezaji nchini, wananchi walioajiriwa kwenye maeneo hayo wawe waaminifu.

  “Mnatakiwa muwe waaminifu, msibebe kitu chochote ndani ya kiwanda bila ya ridhaa ya wamiliki kwa kuwa mtaonyesha taswira mbaya kwa wawekezaji.”

  Amesema uaminifu wao ndio utawezesha Watanzania wengi kupata ajira kwenye viwanda hivyo ambavyo vimejengwa  katika maeneo yao. Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na kampuni ya TOL Gases, Mhandisi  Harold Temu alisema kiwanda kinauwezo wa kuzalisha tani 46 kwa siku.

  Alisema gesi inayozalishwa kiwandani hapo ni ya Carbon Dioxide ambayo inauzwa nchini na nchi jirani za Zambia, Malawi, Zimbabwe na Congo. Mhandisi Temu alisema wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda vya kutengenezea soda, bia na pia hutumika katika kuhifadhia chakula na kwenye vifaa vya kuzimia moto.

  Mapema Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kuchakata majani ya chai cha Katumba, ambapo alisema Serikali inaimarisha Ushirika wa zao hili ili wakulima waweze kupata tija.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Riziki Pembe Juma ameviasa vyuo vikuu nchini vizalishe wataalam ambao watakuwa msaada kwa taifa.

  Waziri huyo ameyasema hayo wakati akifunga maonesho ya vyuo vikuu nchini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inasisitiza viwanda hivyo lazima vyuo vijenge dhana hiyo kwa kuzalisha wataalam wataofanya viwanda hivyo viwepo kutokana na ujuzi walionao.

  Waziri Riziki ametaka vyuo vikuu kutokana na maonesho kuwa na mitazamo mipya ya kuwa na mitaala ambayo itazalisha wataalam wenye uwezo katika soko la ajira na hata kujiajiri.

  Amesema kuwa serikali inaangalia vyuo vikuu vinavyofanya kazi ikiwa ni pamoja na kuangalia utafiti kwa ajili ya maendeleo ya taifa  pamoja na watu wote.

  Nae Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Eleuther Mwageni amesema kuwa maonesho yajayo wataboresha na kuangalia uwezekano wa kuongeza siku kutokana na maoni ya wadau wa vyuo vikuu.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Riziki Pembe Juma akizungumza wakati wa kufunga maonesho ya vyuo vikuu nchini katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Eleuther Mwageni akizungumza wakati maonesho ya vyuo vikuu nchini katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewataka wananchi wa wilaya ya Ukerewe kutunza miradi ya Maji kwa kuwa serikali inaigharamia kwa fedha nyingi.

  Jafo aliyasema hayo alipotembelea mradi mkubwa wa maji wa Kazilamkanda ambao utahudumia vijiji vipatavyo 13 wilayani humo.

  Amesema serikali inafanya jitihada za kuwatatulia wananchi wake kero mbalimbali ikiwemo ya upatikanaji wa huduma ya maji, hivyo ni vyema wakatunza miundombinu ya miradi hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

  Akikagua mradi huo, Jafo alimpongeza Mkandarasi aliye jenga chanzo na tanki la kuhifadhia maji la lita 680,000 ambaye ni Lutare Make Enginnering Ltd kwa kazi nzuri.

  Amesisitiza kukamilishwa kwa usambazaji wa Maji katika vijiji vyote 13 kabla  ya Disemba 30 mwaka huu.

  Naibu Waziri huyo amesisitiza kulazwa mabomba yaliyo na ubora ili kuepusha kupasuka kwa mabomba endapo mabomba hayo yatakuwa hayana viwango na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi na halmashauri baada ya kukabidhiwa mradi husika.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Rutala wilayani Ukerewe mkoani Mwanza juu ya utunzaji wa miradi ya maji.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akipata taarifa kuhusu miradi ya maji wilayani Ukerewe.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akifanya ukaguzi wa tenki la maji.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akifanya ukaguzi wa mashine za kusukumia maji.

  0 0
 • 07/30/17--10:22: TAARIFA KWA UMMA


 • 0 0

   Jengo la Uwanja wa Ndege wa Pemba kwa abiria wanaosafiri na kuwasili kisiwani humo.
   Chai Maharage ikiwa levo siti
   Barabara kuu katika eneo la Chakechake.  0 0  *Issa naye achota Mil 10 zake.

  Na Mwandishi Wetu, Dar es SalaamBAHATI Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ imezidi kushika kasi baada ya droo yake ya 27 kutua kwa Viane Kundi wa mjini Iringa, nchini Tanzania aliyevuna jumla ya Sh Milioni 20, huku Ally Issa Kumburu mkazi wa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam naye akivuna Sh Milioni 10 za Tamasha la Komaa Concert, lililofanyika jana na kudhaminiwa kwa kiasi kikubwa na Biko.

  Droo zote mbili zilichezeshwa leo jijini Dar es Salaam kwa kuendeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, ambapo ni matokeo ya kutopatikana kwa mshindi wa tamasha la Komaa Concert, lililofanyika juzi katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza katika droo hiyo ya 27, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kupatikana kwa washindi hao ni sehemu ya kuendelea kugawa fedha kwa kwa wote wanaoshinda katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, akiwamo Kumburu wa Komaa Concert, mkazi wa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam na Viane aliyejinyakulia Sh Milioni 20 akitokea mkoani Iringa.  Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, kushoto akiandika dondoo katika droo ya Komaa Concert iliyorudiwa leo asubuhi baada ya jana kutopaatikana mshindi katika Tamasha la Komaa lililoandaliwa na EFM Radio na kudhaminiwa na Bahati Nasibu ya Biko Tanzania. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.
  Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, kushoto akiandika dondoo katika droo ya 27 ya Biko ambapo Viane Kundi wa Iringa, alitangazwa mshindi na kuzoa Sh Milioni 20 za Biko. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paulo Makonda, akizungumza na wadau wa muziki waliofurika katika Tamasha la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio kwa udhamini mkubwa wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku'. Katika Tamasha hilo lililokwenda na kumpata mshindi wa Sh Milioni 10 limempata Ally Issa Kumburu wa Mwananyamala, aliyepatikana katika droo iliyochezeshwa leo baada ya ndani ya tamasha kutopokea simu kutokana na wingi wa watu na kelele za uwanjani Tanganyika Packers, Kawe. Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa EFM Radio, Denis Busurwa (Sebo). Picha na Mpigapicha Wetu.  0 0

  *Aagiza kuimarishwa kwa ukaguzi wa watu, magari na mizigo mipakani

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania siyo lango la kupitishia dawa za kulevya kwenda nchi za nje hivyo ameagiza ulinzi uimarishwe katika mipaka yote.

  Amesema kunatabia ya baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kutumia Tanzania kama njia ya kupitisha dawa za kulevya kwa ajili ya kupeleka nchi za Afrika ya Kusini, Malawi na Zambia.

  Alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Julai 29, 2017) alipozungumza na watumishi wa kituo cha forodha cha Kasumulu kilicho katika mpaka wa Tanzania na Malawi wilayani Kyela.

  Waziri Mkuu alisema ili kuhakikisha jambo hilo linadhibitiwa ni vema ukaguzi wa watu wanaopita kwenye maeneo hayo pamoja na mizigo ukaimarishwa.“Endeleeni kufanya upekuzi wa kina wa magari, watu na mizigo yote yote katika mipaka yetu. Tanzania siyo lango la kupitishia dawa za kulevya na Serikali haitakubaliana na jambo hilo.”

  Pia aliwataka viongozi hao kuhakikisha biashara zote za magendo zinazifanyika mipakani, zikiwemo za kubadilisha fedha zinadhibitiwa kwa kuwa zinaikosesha Serikali mapato.

  Alisema ni vema yakawepo maduka ya kubadilishia fedha katika maeneo hayo ili kudhibiti biashara hiyo ambayo kwa sasa inafanywa kimagendo huku Serikali ikikosa kodi.“Biashara za magendo zidhibitiwe katika maeneo haya na yaanzishwe maduka ya kubadilishia fedha ili biashara hiyo ifanyike kihalali. Pia imarisheni vyanzo vya mapato.”

  Pia Waziri Mkuu aliwataka Maofisa wa Uhamiaji katika mikoa hiyo ya mipakani kuhakikisha wanadhibiti uingiaji holela wa raia wa kigeni kwa lengo la kuimarisha ulinzi nchini.

  Waziri Mkuu alisema katika baadhi ya maeneo kwa sasa zimeanza kuonekana silaha ambazo hapo awali hazikuwepo na ndizo zinazosadikiwa kutumika katika matukio ya kihalifu.Awali, Bw. Taniel Magwaza ambaye ni Afisa Mfawidhi wa Uhamiaji alisema watahakikisha wanafanya kazi kwa weledi katika kupambana na biashara za magendo kwenye mpaka huo.

  Alisema mbali na kupambana na biashara za magendo pia watadhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu kwa kushirikiana na watumishi idara zote waliopo katika mpaka huo wa Kasumulu.Bw. Magwaza alisema katika doria zilizofanywa mwaka 2016/2017 jumla ya wahamiaji haramu 87 walikamatwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

  Alisema wahamiaji hao walitokea nchi za Malawi (30), Ethiopia (47), Burundi (6) Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) (4), ambapo baadhi walirudishwa makwao na wengine walifungwa katika Gereza la mkoa wa Mbeya.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI, JULAI 30, 2017

  0 0  Na Jeshi la Polisi Nchini

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, amemaliza ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na mkoa wa Singida, huku akiacha morali kwa watendaji wa Jeshi hilo hatua ambayo italiwezesha ieshi hilo kufanyakazi zake kwa weledi katika kukabiliana na matishio ya uhalifu na wahalifu.

  IGP Sirro, amefanya ziara hiyo ikiwa ni mkakati wake aliojiwekea tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi hilo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa ili kujua namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi.

  Katika mazungumzo yake IGP Sirro, amewataka askari na maofisa kutimiza wajibu wao kwa kutenda haki na bila uwoga wala kumuonea mtu muhali jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu katika jamii.

  Hata hivyo, katika mabaraza ya kuzungumza na askari na maofisa baadhi ya hoja kadhaa ziliibuliwa kwa baadhi ya askari waliopata nafasi ya kutoa mawazo yao, ambapo IGP Sirro aliahidi kuzishughulikia mapema ili kuzidisha morari katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

  Aidha, katika ziara yake IGP Sirro, alipata fursa ya kukutanana Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama ya mkoa huku masuala kadhaa ya kiusalama na mbinu na mikakati ikijadiliwa katika kamati hizo na kuahidi kutoa ushirikiano utakaowezesha kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiuhalifu.

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi wa  Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Singida, wakati alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi. 

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo na kuwataka wafanyekazi kwa kutenda haki na kusimamia misingi ya sheria na taratibu, IGP Sirro yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi. 
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na kikosi cha Polisi wanawake baada ya kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili mkoani Singida, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi. 

  0 0

  Na Hamza Temba - WMU - Muheza, Tanga
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga kukutana na wakulima 879 wa vijiji vitano katika Tarafa ya Amani Wilayani humo kwa ajili kufanya uhakiki wa malipo ya fidia ya mazao waliyolipwa na Serikali ili kupisha eneo la hifadhi ya msitu wa Derema.
  Mhandisi Makani ametoa agizo hilo  katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Msasa IBC, Tarafa ya Amani, Wilayani Muheza kufuatia malalamiko ya wananchi hao kupunjwa malipo yao wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 15 baina Serikali na wananchi wa vijiji hivyo vya Kisiwani, Kwemdim, Msasa IBC, Antakae na Kambi.
  Akisoma risala ya wakulima hao mbele ya Naibu Waziri Makani, Mwenyekiti wa Kamati ya wakulima hao, Mohammed Rama Shesha alidai kuwa jumla ya wakulima 1,128 wa vijiji hivyo wanailalamikia Serikali kwa kuwalipa viwango pungufu vya malipo ya fidia ya mazao yao tofauti na viwango vilivyolipwa na Serikali mwaka 2002 kupitia mradi wa FINIDA. Aidha, alidai kuwa kuna baadhi ya mazao pia hayakulipiwa kabisa fidia hizo.
  Akizungumzia viwango vya fidia hizo Shesha alisema wananchi walilipwa Shilingi 28,800 kwa mche mmoja wa iliki na Shilingi 11,000 kwa mche mmoja wa mgomba. Alidai viwango hivyo vilibadilika kuanzia mwaka 2005 ambapo walilipwa Shilingi 3,315 kwa kila mche mmoja badala ya Shilingi 5,100 kama ilivyoainishwa kwenye viwango vya Serikali hivyo akaomba walipwe kiasi kilichobakia cha shilingi 1,785.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msasa IBC wilaya ya Muheza mkoani Tanga jana wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili kutatua mgogoro wa hifadhi ya msitu wa Derema. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanaisha Tumbo. 
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati), akimuonesha mwenyekiti wa kamati ya wakulima wa vijiji vitano vya tarafa ya Amani, Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mohammed Ramadhani Shesha viwango halali vya serikali vya kulipia fidia za mazao kwa wananchi waliondolewa katika eneo la hifadhi ya msitu wa Derema wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana kwa ajili ya kutatua migogoro wa hifadhi hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanaisha Tumbo.  
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msasa IBC wilaya ya Muheza mkoani Tanga jana wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili kutatua mgogoro wa hifadhi ya msitu wa Derema.
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani, (wa tatu kushoto), akiangalia eneo la Msitu wa hifadhi ya Derema na viongozi wa wilaya ya Muheza Muheza wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana kwa ajili ya kutatua mgogoro wa hifadhi hiyo. 

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  VIONGOZI WAPYA WALIOCHAGULIWA KUONGOZA JUMUIYA YA WATANZANIA READING - BERKSHIRE NI KAMA IFUATAVYO:

  MWENYEKITI NI NDUGU JOE J.E WARIOBA, MAKAMU MWENYEKITI  NI Bi. LAURA BANDUKA, KATIBU MKUU NI  Bi. Raya Walker, NAIBU KATIBU {KAIMU}, Bw.   Peter Owino, MTUNZA HAZINA ni  Bi. FLORA DICKSON, wakati MTUNZA HAZINA MSAIDIZI ni   Ndugu Elijah Mwamunyange.

  WAJUMBE SITA NI Peter Owino, MOHAMMED Upete, Paul Onyango, Geofrey Mumu, Evelyne Furzei na Dorine White, wakati Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu (AUDITOR) ni Eliud Mwijarubi. 
  Pia kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania Diaspora Community United Kingdom of Great Britain &  kila jumuiya za matawi zinatakiwa kuchagua wawakilishi wawili (2) katika Baraza (The Council) la Tanzania Diaspora UK. Wajumbe watachaguliwa hapo baadae.
  Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza sana katika hatua hio kubwa na ya muhimu katika ujenzi wa Umoja wa Watanzania UK
  Asanteni sana

  Uongozi: TA READING -  BERKSHIRE*Kwa kushirikiana na

  Tanzania Diaspora Community/Association - United Kingdom of Great Britain & Northern Ireland
   Makamu na Kaimu Mwenyekiti Mstaafu Ndugu Hussein Chang'a akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa TA Reading- Berkshire aliyechaguliwa Ndugu Joe J.E Warioba. Kushoto ni Katibu mpya Bi Raya Walker na kulia ni Makamu mwenyekiti mpya Bi. Laura Noel
   
  Mtunza Hazina Bi. Flora Dickson akimkabidhi ripoti ya Fedha na Akaunti ya Jumuiya Mwenyekiti Mpya wa TA READING BERKSHIRE Ndugu Joe J.E Warioba
   Wanakamati na Viongozi wa wapya wa Jumuiya
   Viongozi wa TZUK na TA READING BERKSHIRE
  Baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Uchaguzi TA READING- BERKSHIRE na Uongozi wa TZUK. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

   Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na viongozi na mashabiki wakati alipowasili uwanja wa Kinesi Ubungo jijini Dar es salaam  kuangalia kuangalia mtanange wa Ndondo Cup kati ya timu ya Stim Tosha na Keko Furniture. Katika Mechi hiyo Keko wameshinda kwa penati 4-2 baada ya kutoka Sare ya magoli 1-1 katika muda wa kawaida.
    Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na viongozi na mashabiki wakati alipowasili uwanja wa Kinesi Ubungo jijini Dar es salaam  kuangalia kuangalia mtanange wa Ndondo Cup kati ya timu ya Stim Tosha na Keko Furniture. Katika Mechi hiyo Keko wameshinda kwa penati 4-2 baada ya kutoka Sare ya magoli 1-1 katika muda wa kawaida.
   Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akihojiwa na Azam TV katika  uwanja wa Kinesi Ubungo jijini Dar es salaam  alipofika kuangalia kuangalia mtanange wa Ndondo Cup kati ya timu ya Stim Tosha na Keko Furniture. Katika Mechi hiyo Keko wameshinda kwa penati 4-2 baada ya kutoka Sare ya magoli 1-1 katika muda wa kawaida.

  0 0
  0 0

  Kumekuwepo na upotoshaji wa mafunzo ya utarajali (Internship programme) bila malipo yaani fedha za kujikimu wakati wa mafunzo hayo kwa baadhi ya wanaotarajia kuanza mafunzo kwa vitendo mapema mwaka huu.

  Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inapenda kuwajulisha kwamba kwa sasa hakuna ‘intern’ aliyepangiwa kuanza mafunzo hayo kwani tunasubiri watoke waliopo kwenye mafunzo.

  Barua iliyodukuliwa na kusambaa kwa lengo la kupotosha wataraji hao ilikuwa ni kwa ajili ya wataraji (intern) kutoka nje ya nchi ambao kwa sheria hawalipiwi na Serikali ya Tanzania.

  Aidha wapo ‘intern’ wawili ambao wanasoma nchini China na mwingine Algeria masomo yao yalihitaji mafunzo kwa vitendo kabla ya kumaliza na kwa kuwa ilikua lazima warudi vyuoni mwezi Oktoba waliomba kufanya mafunzo hayo  kwa kujigharimia  pamoja na kuwa ni watanzania na wazazi wao walikuwa wameridhia hilo kwa maandishi ili warudi  mapema kumalizia program yao ya udaktari.

  Hivyo ni watanzania wawili tu wameshapata barua yenye kuwataka  kujilipia kwa mazingira hayo hakuna wengine waliyepewa barua ya kuruhusiwa kwenda mafunzo ya utarajali (internship) bila malipo.

  Imetolewa na; 
  Nsachris Mwamwaja

  Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikali-Afya


  30/7/2017


  0 0older | 1 | .... | 1833 | 1834 | (Page 1835) | 1836 | 1837 | .... | 3348 | newer