Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1832 | 1833 | (Page 1834) | 1835 | 1836 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Benny Mwaipaja, WFM
  Wizara ya Fedha na Mipango imetiliana saini na Kampuni ya ujenzi wa barabara ya Reynolds kandarasi ya ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara mkoani Morogoro, yenye urefu wa kilometa 67 kwa kiwango cha lami utakaojengwa kwa shilingi bilioni 101, kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya, Marekani na Uingereza. 


  Mkataba huo umesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shaaban kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Bw. Dan Yzhak Shahn, Bw. Benjamin Arbit ambaye ni Mkandarasi kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Reynolds. 


  Kiasi hicho cha fedha ni sawa na Euro milioni 40.4 ambapo Euro milioni 29.6 zimetolewa kwa ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Shirika la Misaada la Uingereza-UK-AID, huku kiasi kinachobaki cha Euro milioni 10.8 kikitolewa na Shirika la Misaada la watu wa Marekani- USAID. 


  Akizungumza mara baada ya kutiwa saini kwa kandarasi hiyo, Bi. Amina Khamis Shaaban, amesema ujenzi wa barabara hiyo utakaohusisha pia ujenzi wa daraja katika Mto Ruaha Mkuu, utasaidia wakulima wadogo kupitia Program ya Uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania-SAGCOT, walioko katika Bonde la Mto Kilombero, kuyafikia masoko ya uhakika ya mazao yao.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia) na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Reynolds, Bw. Dan Yzhak Shahn (kushoto) wakisaini mkataba wa Sh. Bilioni 101 kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Kidatu- Ifakara yenye urefu wa Kilometa 66.9, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kulia) na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Reynolds, Bw. Dan Yzhak Shahn (kushoto) wakibadilishana mkataba wa Sh. bilioni 101 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kidatu – Ifakara yenye urefu wa Kilometa 66.9, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto) akizungumza kuhusu umuhimu wa barabara ya Kidatu – Ifakara kwa kiwango cha lami kwa maendeleo ya Kilimo baada ya kutiliana saini mkandarasi atakayejenga barabara hiyo, hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. 
  Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, Roeland van de Geer akizungumza kwa niaba ya EU, UK-AID na USAID, kuhusu mpango wao wa kuendelea kuisaidia Tanzania katika ujenzi wa miundombinu baada ya kuwekwa saini mkataba wa Sh. bilioni 101 kwa ajili ya Ujenzi wa barabara ya Kidatu – Ifakara, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban. 
  Baadhi ya wajumbe waliohudhuria hafla ya kuwekwa saini mkataba wa Sh. bilioni 101 kwa ajili ya Ujenzi wa barabara ya Kidatu – Ifakara wakifuatilia nyaraka za mkataba huo kabla ya kusainiwa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM) 

  0 0


  0 0

  Sheikh Shariff Majini kutoka kituo cha Dua na Maombi Mabibo Jijini Dar es salaam Ijumaa amefanya Dua maalum kwa wakaazi wa Temeke na maeneo ya jirani katika uwanja wa Mwembe Yanga.
   Dua hiyo  ambayo imefunguliwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Musa itakuwa kwa siku tatu kuanzia Ijumaa tarehe 28-07-2017 mpaka Jumapili tarehe 30-07-2017 ambapo itafungwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda. 
   Dua ya Sheikh Shariff  pamoja na kuliombea Taifa letu pamoja viongozi wake makini lakini pia ni maalum kwa wakazi wa Temeke ambao mara nyingi wamekuwa wakimpigia simu Sheikh mara kwa mara ili aende kufanya mkutano wa Dua kwa ajili ya utatuzi wa matatizo yao mbalimbali yakiwemo Majini na wachawi mbalimbali wanaowasumbua. 
   Dua za Sheikh huwa zinaanza mchana saa nane na kumalizika saa kumi na mbili jioni.
  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa akizungumza kwenye Dua hiyo iliyoendeshwa na Sheikh Shariff Majini kutoka kituo cha Dua na Maombi Mabibo Jijini Dar es salaam
  Sheikh Shariff Majini kutoka kituo cha Dua na Maombi Mabibo Jijini Dar es salaam akiongea
  Sheikh Shariff Majini kutoka kituo cha Dua na Maombi Mabibo Jijini Dar es salaam akimshukuru Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa
  Sehemu ya umati wa kinamama wa Temeke na maeneo ya jirani waliohudhuria dua hiyo

  0 0


  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani anawaalika wananchi katika halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania.

  Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Agosti 5, 2017 eneo la Chongoleani jijini Tanga ambapo utahudhuriwa na waasisi wa mradi huo mkubwa - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

  0 0
  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhiwa ripoti ya wezi wa magari pamoja na vifaa vya magari vya wizi na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam DCP Lucas Mkondya ikiwa ni wiki mbili toka mkuu huyo aliagize jeshi hilo kuchukua hatua baada ya matukio ya namna hiyo kushamiri ndani ya mkoa huo. 
   Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi hii wakiwa ndani ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kamanda Mkondya alisema katika operesheni hiyo kali jumla ya wahumiwa 73 wamekamatwa na kupekuliwa na kukutwa na vifaa mbalimbali vya magari ikiwemo side mirrors, taa za magari, power windows, radio, injector pumps, starters na seat cover. 
   “Tarehe 19 mwezi wa saba mweshimiwa RC Makonda ulitoa maagizo kwa jeshi la polisi kwamba unatupatia siku saba kuhakikisha tunasambaratisha mtandao wa wezi wa vifaa vya magari pamoja na magari baada na sisi tumelitekeleza hilo tayari kuna watu 73 tunawashikilia
  "Kinondani wamekamatwa watuhumiwa 29, Ilala wamekamatwa wahutumiwa 33 na mkoa wa kipolisi Temeke wamekamatwa wahumiwa 11,” alisema.
  Alieleza kuwa  jumla ya power windows zilizokamatwa ni 40, Radio 12, Taa za magari aina mbalimbali 105, side mirrors 92, vitasa vya magari 109, wiper switch 7, Tampa 4, left pump3, Air cleaner 1, Booster 3, show grill 6, machine za kupandisha vioo 1 na tyre used 2. 
   Pia alisema katika mahojiano na wahutumiwa wote waliokamatwa wapo walioshindwa kuvitolea maelezo vifaa hivyo ni namna gani na wapi wamevipata, na wote  wanaendelea na mahojiano na uchunguzi bado unaendelea ili kubaini mtandao wote unaojihusisha na wizi huo wa vifaa vya magari ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahamani kwa hatua zaidi. 
   Kwa upande wa RC Makonda alisema yeye anataka kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa salama ili kutimiza gamma ya Rais John Magufuli katika kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi wake.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wanahabari leo wakati akikabidhiwa ripoti ya wezi wa vifaa vya magari.
   Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam DCP Lucas Mkondya akizungumza na wanahabari juu ya watuhumiwa 73 ambao wamekamatwa na kupekuliwa na kukutwa na vifaa mbalimbali vya magari
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akikagua vifaa vya magari vinavyosadikiwa kuwa ni vya wizi leo jijini Dar es Salaam.
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akikagua vifaa vya magari vinavyosadikiwa kuwa ni vya wizi leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya vifaa vya magari vinavyosadikiwa kuwa ni vya wizi vilivyooneshwa na jeshi la polisi leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivalishwa skafu na vija wa CCM, Green Guard bade ya kuwasili kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kuanza ziara wilayani humo leo Julai 29, 2017. Kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla
     Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Mbeya
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mbeya baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Mbeya 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi "Sugu" baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Mbeya
  Baadhi ya watumishi wa umma wa wilaya ya Kyela wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza naokwenye ukumbi wa Halmahauri ya wilaya ya Kyela akiwa ktik ziara ya mkoa wa Mbeya leo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma wa  wilaya ya Kyela  baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla (kushoto) kwenye ukumbi wa Halmashuri ya Wilaya ya Kyela leo Julai 29, 2017. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu

  0 0  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili wateja wa Benki nyingi hapa nchini ni msongamano wa wateja pamoja na ucheleweshaji huduma na kuitaka Benki ya CRDB kuwa na mikakati katika kupambana na kadhia hiyo. 
  Dk. Shein aliyasema hayo leo huko Chake Chake Pemba, katika sherehe ya ufunguzi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB likiwa Tawi la 280 ndani ya mtandao wa benki hiyo kutoka matawi 19 iliyokuwa nayo mara tu baada ya kuanzishwa mnamo mwaka 1996. 
  Katika hotuba yake, Dk. Shein alisema kuwa wananchi wanaeleza kwamba, miongoni mwa changamoto zinazosababisha msongamano ni kuwa benki za hapa nchini bado haziendani na kasi ya mabadiliko yanayotokea katika sekta ya fedha. 
  Alieleza kuwa katika Siku ya Sherehe za Maadhimisho ya Mei Mosi, mwaka huu yaliyofanyika katika viwanja vya Mahonda, Unguja, Wafanyakazi walipendekeza kuwa Serikali ikae na uongozi wa benki mbali mbali ili ione namna ya kupunguza kero hii kubwa ya msongamano na kuchelewa kutolewa huduma, hasa ifikapo mwisho wa mwezi. 
  “Leo nimeona ni busara nikuleteeni mawazo hayo ya wafanyakazi, ambao pia, ni baadhi ya wateja wa benki zenu. Wahenga wanasema ‘Mjumbe hauawi’ ndio maana na mimi nimeufikisha ujumbe kama nilivyoambiwa”, alisema Dk. Shen. 
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein (katikati)  akikata utepe kuzindua Tawi la Benki ya RCDB katika Mji wa Chake chake Pemba leo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla,akifuatatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB  Bw.Ally Hussein Laay na kulia ni  Mkugenzi Mtendaji wa CRDB Dkt. Charles Kimei
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein (kulia) akipeana mkono wa shukurani  na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB  Bw.Ally Hussein Laay  mara baada ya  kuzindua Tawi la Benki ya RCDB katika Mji wa Chake chake Pemba leo
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein (katikati)  akitia saini kitabu cha wageni alipotembelea katika Ofisi za Benki ya RCDB baada ya kiuzindua rasmi leo (kulia) Meneja wa Tawi la CRDB Chake chake Pemba Nd,Hamadi Abubakar na (kushoto) Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira poia akiwa kaimu Waziri wa Fedha na Mipango Salama Aboud Twalib
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein na Meneja wa Tawi la CRDB Chake chake Pemba Nd,Hamadi Abubakar (katikati) pamoja na Viongozi wengine na Wafanyakazi wa Benki hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa  Tawi la Benki ya RCDB katika Mji wa Chake chake Pemba uliofanyika leo. Picha na Ikulu. 

  0 0

  NA EVELYN MKOKOI –MASWA 

  Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amewapongeza viongozi wa mikoa wilaya na halmashauri nchini waliotekeleza kwa kiwango cha kuridhisha agizo la kusimamia utekelezaji wa siku ya kitaifa ya kufanya usafi na kuhakikisha usafi wa mazingira katika maeneo yao unaimarishwa.

  Mpina ameyasema hayo leo Wilayani Maswa alipokuwa akishiriki zoezi la kufanya usafi kitaifa na kuongeza kuwa majina ya viongozi hao pamoja na wale ambao wamezembea kutekeleza agizo hilo yatafikishwa kwa Mhe. Rais na Mhe. Makamu kwa hatua za kiutendaji.

  “Hatuwezi kufikia mapinduzi ya uchumi wa viwanda kama taifa litaendelea kuwa chafu kwani tutaendelea kupoteza nguvu kazi nyingi kutokana na maradhi yanayosababishwa na uchafu, hivyo viongozi wa mikoa na wilaya wana jukumu kubwa la kusimamia usafi wa mazingira.” Alisisitiza Mpina.

  Naibu Waziri Mpina aliongeza kwa kusema kuwa serikali imeona kuwa usafi ndio afya na usafi ndio maisha na ndio maana Serikali imeitenga siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa ni siku maalum kwa ajili ya usafi wa Mazingira. 

  Akiwa ziarani wilayani Maswa Mhe. Mpina alibaini changamoto mbalimbali za kimazingira zinazoikumba wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo katika soko la Maswa, mazingira yasiyoridhisha ya kufanyia biashara sokoni na ukosefu wa maji katika machinjio ya wilaya, ambapo aliekeza uongozi wa Halmashauri kuhakikisha ndani ya miezi mitatu changamoto ya upungufu wa matundu ya choo iwe imefanyiwa kazi, kuwepo kwa mabanda ya kisasa ya kufanyia biashara katika soko hilo na kuhakikisha kunakuwepo na maji ya kutosha wakati wote katika machinjio.

  Kwa Upande wake kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Bw. Vivian Christopher, alieleza kuwa Halmashauri yake imetenga fedha kwa ajili ya kushughulikia changamoto hizo katika Bajeti wilaya kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
  Pichani Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Akizungumza na Baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya Wilaya wa Maswa (hawapo katika picha)  leo baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kindoni Mhe Ally Hapi leo ametangaza msimamo wa serikali ya wilaya ya Kinondoni kuwa wananchi wa Kunduchi Mecco na mji mpya Kata ya Kunduchi waliokuwa na hofu ya kuondolewa kuwa hawataondolewa na kwamba badala yake makazi yao yatapimiwa viwanja na watamilikishwa rasmi. 

  Uamuzi huo umekuja baada ya mvutano wa miaka mingi baina ya manispaa ya Kinondoni na wananchi hao waliovamia eneo hilo ambalo awali lilitengwa kwa ajili ya machimbo ya kokoto. Katika mvutano huo ulioibua kesi mbili zilizoendeshwa kwa muda mrefu na hatimaye manispaa kushinda kesi hizo, uamuzi umefikiwa kuwa Manispaa ya Kinondoni haitawavunjia na kuwaondoa wananchi hao wapatao zaidi ya 3000 waliojenga eneo hilo.
   Badala yake eneo hilo litapimwa ili kupanga vema mji na kuruhusu maeneo ya huduma za msingi za jamii kama barabara, shule, afya na zahanati kutengewa maeneo.
  DC Hapi ameagiza wananchi wa eneo hilo kuendelea kukaa maeneo hayo baada ya leseni ya uchimbaji kokoto eneo hilo kufutwa kutokana na uharibifu wa miundombinu.
  "Hatuwezi kuhatarisha maisha ya wananchi 3000, tutawapeleka wapi, kwani wao siyo wanakinondoni, kwani wao siyo watanzania" Alisema DC Hapi.
  DC Hapi ametoa maagizo kwa watendaji kuhakikisha kuwa wananchi hao wanamilikishwa maeneo hayo kwao kufuata taratibu na sheria ambapo itabidi maeneo hayo yapimwe na wananchi hao wawe wavumilivu maana kuna baadhi ya maeneo yatatengwa kwa huduma za kijamii, ikiwemo vituo vya Afya, Polisi na barabara.
  Hata hivyo DC Hapi amewatoa hofu wananchi wa maeneo hayo kuhusu kulipia gharama za upimaji wa ardhi ambazo itabidi wachangie, huku akieleza kuwa wataiandikia barua mamlaka ya chuo cha Ardhi ili waweze kutoa baadhi ya wanafunzi ambao watafanya upimaji katika eneo hilo bure na kuwaondolea wananchi gharama za ziada.
  Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta amesisitiza kuwa serikali itakuwa bega kwa bega na wananchi wanyonge kuhakikisha haki yao haipotei, huku Diwani wa Kata hiyo akihimiza ushirikiano katika shughuli za maendeleo kwani maendeleo hayana chama, hvyo ni vyema kuondoa itikadi.
   
  Mkuu wa Wilaya ya Kindoni Mhe Ally Hapi akishangiliwa na wananchi mara  baada ya kuzungumza nao na kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa ardhi katika eneo la Kunduchi Mecco na mji mpya Kata ya Kunduchi ambao hapo mwanza ilidaiwa na Manispaa ya Kinondoni kuwa wamevamia kwakuwa eneo hilo lilikuwa limepangwa kwa ajili ya Machimbo ya Kokoto. 


  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma dkt.Bilinith Mahenge atoa agizo kwa wiazara ya maliasili mkoa wa Ruvuma kuwachukilia hatua mara moja wale wote wanaohusika na ukataji miti ovyo na uchomaji mkaa ,rai hiyo ameitoa baada ya kukamata gari lilo beba mbao 400 zilizokuwa zinasafirishwa kunyume na sheria .HABARI KAMILI HII HAPA.

  0 0

  Balozi wa mchezo wa mpira wa kikapu nchini, Jokate Mwegelo ametoa rai kwa wasichana na wazazi kuwaruhusu watoto wa kike kushiriki katika michezo mbalimbali ili kukuza vipaji na kujiingizia kipato.

  Jokate alitoa rai hiyo wakati wa kukabidhi bendera kwa mchezaji chipukizi wa mpira wa kikapu nchini, Jesca Julius Ngaise ambaye anaondoka leo kwenda nchini Afrika Kusini kushiriki katika mafunzo ya juu mchezo huo yatakayoendeshwa na makocha wa kimataifa wa ligi ya NBA ya Marekani.

  Amesema kuwa Jesca ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Juhudi ya Ukonga, amepata nafasi hiyo baada ya kuchaguliwa na jopo la makocha na kuweka historia ya kuwa msichana wa kwanza wa Tanzania kuhudhuria mafunzo hayo.

  “Hii ni faraja kwa Tanzania, makocha wa kimataifa wameona kipaji cha Jesca ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya wasichana ya wachezaji wa chini ya miaka 16, ameiwezesha Tanzania kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Afrika Mashariki nchini Kenya, sasa tunampa bendera na kuiwakilisha nchi katika kozi hiyo, ni sifa kubwa kwake na kwa Taifa,”
  Balozi wa mchezo wa mpira wa kikapu nchini, Jokate Mwegelo akikabidhi bendera ya Taifa kwa mchezaji Chipukizi, Jesca Ngaise (katikati) wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye kituo cha michezo za Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park. Anayeshuhudia zoezi hilo ni Kocha maarufu wa mpira wa kikapu Tanzania, Bahati Mgunda.
  Balozi wa mchezo wa mpira wa kikapu, Jokate katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji chipukizi wa mpira wa kikapu kwenye viwanja vya JMK Park.
  Baba Mzazji wa Jesca, Julius Ngaise akizungumza
  0 0


  TIMU ya Vijana wa Simba chini ya umri wa miaka 20, jana walishinda kuungana na wenzao wa Yanga katika fainali ya Mechi za Hisani kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI baada ya kufungwa na Tanzania Prisons kwa mikwaju ya penati 6-5 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu wa Sokoine jijini Mbeya.

  Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoka uwanjani bila kupata bao, huku timu zote zikicheza kwa taadhari na kufanya mashambulizi ya kushitukiza.

  Katika mchezo huo Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 69 kupitia kwa mshambuliaji wake, Dadi Mbarouk, baada ya kuwatoka mabeki wa Tanzania Prisons Aron Kalambo, aliyekuwa ametoka golini akijaribu kuwahi kumzuia na  kupishana na mpira uliotinga wavuni.
  Bao la kusawazisha la Tanzania Prisons, lilifungwa na Kassim Hamis, kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 79, baada ya mchezaji wa Simba U20, kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na kufanya dakika 90 kumalizika timu hizo zikiwa sare kwa kufungana 1-1.

  Baada ya sare hiyo timu hizo zilikwenda katika hatua ya matuta, ambapo zilipigwa jumla ya penati 8, na Tanzania Prisonswakikosa 2 na kupata penati 6 na Simba wakikosa 3 na kupata penati 5.

  Simba wameungana na wenzao Mbeya City Kikosi cha kwanza ambao walitolewa na Kikosi cha Yanga U20 kwa kukubali kichapo cha mabao 3-0 katika mechi hizo za Hisani zilizoandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS, na kushirikisha jumla ya timu Nne za Yanga U20 na Simba U20 kutoka jijini Dar es Salaam, Mbeya City na Tanzania Prisons vikosi vya kwanza Ligi Kuu Bara.
   Beki wa Simba U20, Jacob Jalala (kulia) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Mohamed Rashid, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
  Beki wa Tanzania Prisons, Michael Ismail (kushoto) akijaribu kumpita mchezaji wa Simba U20, Rashid Juma, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1.
   Beki wa Simba U20, Abdallah Rashid (kulia) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Kassim Hamis, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka  dakika 90 kwa sare ya 1-1.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, amewataka manahodha na mabaharia wa meli ya MV. Liemba kufanyakazi kwa ubunifu na uadilifu ili kuiwezesha meli hiyo kujiendesha kibiashara.

  Akizungumza na wafanyakazi wa meli hiyo Prof. Mbarawa, ameelezea kuridhishwa na mabadiliko yanayoendelea katika meli hiyo na kuwataka wasibweteke bali waongeze ubunifu.“Hakikisheni mnatoa huduma bora kwa wateja wenu na kupata faida ili serikali na wadau wengine wawaamini na kutumia huduma yenu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

  Waziri Prof. Mbarawa ameitaka meli hiyo kuongeza safari zake kutoka awamu tatu hadi kumi kwa mwezi ili kuhuisha huduma za usafiri na uchukuzi katika Ziwa Tanganyika. 

  Prof. Mbarawa ambaye yuko katika ziara ya ukaguzi wa miundombinu mkoani Kigoma amepata fursa ya kukagua utendaji wa meli ya MV. Liemba, kupata chakula cha pamoja na wafanyakazi wake katika meli hiyo na hatimae kutoa maelekezo kwa manahodha na mabaharia wa meli hiyo kongwe hapa nchini.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata chakula na manahodha na mabaharia wa meli ya MV Liemba inayofanya safari katika Ziwa Tanganyika.
  Muonekano wa meli kongwe ya MV. Liemba ikiwa imetia nanga katika bandari ya Kigoma, meli hiyo imeatkiwa kuongeza safari zake kutoka awamu tatu hadi kumi kwa mwezi.

  0 0


  *Ameonya zisitumike kuvushia wahamiaji haramu na dawa za kulevya

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua meli mbili za mizigo za Mv Njombe na Mv Ruvuma zitakazotumika katika kusafirishia mizigo kwenye ziwa Nyasa na kuonya kwamba zisitumike kama eneo la kuvushia wahamiaji haramu na dawa za kulevya.

  Amesema kukamilika kwa ujenzi wa meli hizo zilizogharimu sh. bilioni 11.253 ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Magufuli alizozitoa katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 kwa lengo la kutatua changamoto ya usafiri wa abiria na mizigo katika ziwa Nyasa.

  Amesema ni jambo la faraja na la kujivunia kwa Serikali na wananchi kwa pamoja kushuhudia meli zilizotengenezwa na Mtanzania, zikiwa zimekamilika tayari kwa kuanza kazi ya kuwahudumia wananchi, ambapo awali suala hilo lilikuwa likifanywa na raia wa kigeni.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa . Uzinduzi huo ulifanyika kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited. Wapili kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu na Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya moja kati ya meli mbili alizozizindua kwenye badari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa na zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chumba cha kulala cha mabaharia wa moja kati ya meli mbili alizozizindua kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali na zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika chumba cha mitambo ya moja ya meli mbili alizozizindua katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29,  2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali na kujengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika chumba cha nahodha wa moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa, baada ya kuzindua meli hizo kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017.Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa na serikali na kujengwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Limited ikiondoka kwenye gati la bandari Kiwira wialyani Kyela baada ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Julai 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Baadhi ya wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa. 


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo katika Mji wa Chake chake, kisiwani Pemba, Julai 29, 2017. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha na Mipando wa Zanzibar, Salama Aboud Talib na kulia ni Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein akifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo katika Mji wa Chake chake, kisiwani Pemba, Julai 29, 2017. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein (katikati) akihutubia katika hafya ya ufunguzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo katika Mji wa Chake chake, kisiwani Pemba, Julai 29, 2017. Kulia ni Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha na Mipando wa Zanzibar, Salama Aboud Talib, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay (wa pili kushoto) pamoja na Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei.
  Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akizungumza katika hafla hiyo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein akisikiliza jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay, wakati wa hafya ya ufunguzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo katika Mji wa Chake chake, kisiwani Pemba, Julai 29, 2017.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein (katikati), Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha na Mipando wa Zanzibar, Salama Aboud Talib (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla (kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay (kushoto) pamoja na Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (aliyeketi nyuma) wakiwa katika picha ya pamoja katika madawati na baadhi ya wanafunzi wa skuli ya msingi Madunghe ya Chakecaheke kisiwani Pemba. Madawati hayo yametolea na Benki ya CRDB kwa shule hiyo. 


  0 0
  0 0
 • 07/30/17--00:16: TAMKO TOKA IDARA YA UHAMIAJI
 • Idara ya Uhamiaji   imesema jukumu la Udhibiti  wa Uingiaji na Utokaji  wa raia  wa kigeni nchini, linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji  Sura ya 54 (Rejeo la 2016) na wala  haiwalengi  wafanyakazi  wa  Kampuni ya Madini ya Acacia  peke yake.


  Ni hitajio la kisheria  kwa kila raia wa kigeni  anayeingia na kutoka nchini  kukaguliwa  ili kujiridhisha  iwapo  hakuna  dosari zozote za Uhamiaji, Ulinzi na Usalama.


  Sheria ya Uhamiaji inaitaka Idara ya Uhamiaji  kumhoji  mtu yeyote awe raia wa Tanzania au kigeni  bila kujali anafanya  kazi  kwenye Kampuni au Shirika  gani, pale  inapotaka kujiridhisha  juu ya  uhalali  wa ukaazi wake hapa nchini na ikijiridhisha kuwa mtu huyu  hana dosari zozote inamwachia huru kama ilivyofanyika  kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Madini ya Acacia  waliohojiwa  na kuruhusiwa kuendelea na safari yao hivi karibuni.


  Idara ya Uhamiaji  inapenda kuuarifu Umma kuwa hakuna sababu zozote  nje ya matakwa ya  Sheria  ya Uhamiaji zinazopelekea  Idara ya Uhamiaji   kuweka kizuizi  cha kuja au kutoka kwa wafanyakazi wa kigeni wa Acacia.


  Tunapenda kuujulisha Umma kuwa  ni muhimu  kwa watanzania na raia wa kigeni wanaokusudia kuingia na kutoka nchini kuhakikisha wanafuata  Sheria za Uhamiaji  ili  kutimiza hitajio la kisheria.


  Imetolewa na

  Ally M. Mtanda

  Msemaji wa Idara ya Uhamiaji


  29 Julai 2017


older | 1 | .... | 1832 | 1833 | (Page 1834) | 1835 | 1836 | .... | 3272 | newer