Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 120100 articles
Browse latest View live

JAFO AFURAHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI IHUNGO.

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa shule ya wavulana ya kidato cha tano na sita ya Ihungo ambayo majengo yake yalibomoka kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka Jana.

Kutokana na kubomoka kwa majengo hayo, Serikali iliamua kuijenga upya kwa kutumia wakala wa majengo Tanzania (TBA). Akiwa katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali mkoani Kagera, Jafo alitembelea shuleni hapo kukagua ujenzi wake.

Naibu Waziri Jafo aliwapongeza wakandarasi kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya ambapo kazi hiyo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Agosti. Akizungumza na wananchi waliokuwepo katika eneo hilo, Jafo alisema serikali imeamua kuijenga sekondari hiyo kisasa zaidi. Alisema sekondari hiyo inatarajiwa kuwa sekondari ya mfano ndani ya Tanzania kwa kuwa na majengo ya kisasa zaidi kuliko sekondari zote hapa nchini.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akifanya ukaguzi wa miundombinu inayojengwa katika Shule ya Sekondari Ihungo. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika ukaguzi wa ujenzi wa madarasa na mabweni katika Shule ya Sekondari Ihungo. 
Jengo la bweni linalojengwa katika shule ya Sekondari Ihungo. 



MAANDALIZI MKUTANO WA MAWAZIRI TANZANIA NA UGANDA: Ujumbe wa Tanzania wakagua maeneo itakapotekelezwa miradi ya umeme ya ushirikiano

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa tatu kutoka kulia) akimweleza jambo Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis Maze (wa kwanza kutoka kulia), wakati walipokuwa wakikagua eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 14 kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda, unaojulikana kama Murongo-Kikagati. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgavano. Wengine pichani ni Maofisa mbalimbali kutoka TANESCO, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wizara ya Ardhi.
 Meneja wa Sheria anayeshughulikia Mikataba, kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mwesiga Mwesigwa (wa pili kutoka kushoto), akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa kwanza kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgavano (katikati) wakati walipokuwa wakikagua eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 14 kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda, unaojulikana kama Murongo-Kikagati. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Uwekezaji kutoka TANESCO, Rwebangi Luteganya na wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mikataba kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Evelyni Makala.
 Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wa Mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis Maze (kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) na Balozi wa Tanzania nchini Uganda (wa pili kutoka kulia), wakati walipokuwa wakikagua eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 35 wa Nsongezi kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda. Wengine kutoka kushoto ni Meneja wa Uwekezaji kutoka TANESCO, Rwebangi Luteganya, Mkurugenzi wa Mikataba kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Evelyni Makala na Meneja wa Sheria anayeshughulikia Mikataba, kutoka TANESCO, Mwesiga Mwesigwa.
 Sehemu ya Mto Kagera, unavyoonekana katika eneo la Nsongezi, mpakani mwa Tanzania na Uganda. Maji ya Mto huo yatatumika kuzalisha umeme wa megawati 35 kwa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili kwa manufaa ya wananchi wake. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

PROF. MAGHEMBE ATAMBUA MCHANGO WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA VITA DHIDI YA UJANGILI NCHINI

$
0
0
NA HAMZA TEMBA - WMU

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amevipongeza vyombo vya habari nchini kwa mchango wake katika vita dhidi ya ujangili huku akitoa rai kwa vyombo hivyo kuongeza bidii katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa uhifadhi endelevu wa maliasili za taifa kwa faida ya jamii iliyopo na vizazi vijavyo.

Prof. Maghembe ametoa pongezi na rai hiyo leo wakati akifungua mkutano wa sita wa mwaka wa wahariri na wanahabari waandamizi wa vyombo vyote vya habari nchini ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) jijini Tanga huku kaulimbiu ya mkutano huo ikiwa UTALII WA TANZANIA YA UCHUMI WA VIWANDA.

"Ujangili bado upo, Majangili tumepambana nao kweli kweli, na ninyi wanahabari mmetusaidia sana katika kuhabarisha jamii juu ya matukio ya kukamatwa kwao na hukumu wanazozipata, jambo ambalo limesaidia kujenga uoga kwa watu kushiriki katika vitendo hivyo", alisema Maghembe.
Alisema hofu hiyo pamoja na jitihada za Serikali za kupambana na ujangili imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya ujangili nchini hasa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ambapo mizoga ya tembo inayotokana na ujangili imeonekana kupungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha ni miaka iliyopita.

Akizungumzia changamoto ya mifugo kwenye maeneo ya hifadhi nchini amesema sheria za uhifadhi zinakataza watu kuingiza mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa kisheria, hivyo ni wajibu kwa wanahabari kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutii sheria hizo.  "Ni vema wanahabari wakatumia kalamu zao vizuri kuelimisha jamii juu ya athari za muingiliano wa binadamu, mifugo na wanyamapori".

Alisema wanyamapori wanabeba virusi vya magonjwa mbalimbali ikiwemo homa ya bonde la ufa, ndigana, kifua kikuu, homa za vipindi (brucolosis) na kimeta, Magonjwa ambayo yanaweza pia kuambukiza mifugo na binaadamu wanaoishi karibu na wanyamapori. Alisema kuwa endapo muingiliano huo utaendelea kuwepo kwa muda mrefu unaweza kusababisha mlipuko mkubwa wa magonjwa hayo kwa binaadamu na mifugo hivyo kusababisha vifo vingi kwa wakati mmoja.

Prof. Maghembe alisema kumekuwepo na kisingizio cha kumega maeneo ya hifadhi nchini kwa ajili ya matumizi ya kawaida kutokana na ongezeko la wananchi jambo ambalo sio sahihi na kwamba njia pekee na salama ni kubadili mfumo wa matumizi ya rasilimali zilizopo ikiwepo ya ardhi kwa kutumia sayansi na teknolojia na kuweka matumizi bora ya ardhi kwa kulenga matokeo chanya.

BARAZA LA MADIWANI KISHAPU MKOANI SHINYANGA WAPONGEZWA KWA HATUA YA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO KWA UFANISI PAMOJA NA CHANGAMOTO ZA UHABA WA FEDHA

$
0
0
Na Robert Hokororo

Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imepongezwa kwa hatua yake ya utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ufanisi pamoja na changamoto za uhaba wa fedha.

Pongezi hizo zimetolewa leo na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Boniphace Butondo wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi kupokea taarifa za kata kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka.Butondo alisema miradi hiyo imetekelezwa kwa kiwango kizuri pamoja na changamoto ya uhaba wa fedha iliyoikabili halmashauri hiyo kwa kipindi hicho.

Alisema ushirikianoa baina ya madiwani na wataalamu kutoka halmashauri hiyo ndiyo siri ya mafanikio hayo ambayo ni tija kwa wananchi wanaowahudumia.Aidha, aliwapongeza wataalamu hao kutoka idara mbalimbali kwa kuwa na usimamizi mzuri ikiwemo wa fedha na maeneo ambayo miradi hiyo inatekelezwa na kuwataka waendelee kushikamana.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani la kupokea na kujadili tarifa za kata za robo ya nne ya mwaka. Wengine pichani kushoto ni Makamu mwenyekiti wa halmashauri, Edward Shigela na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Stephen Magoiga.

Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza wakati wa kikao hicho. Wengine pichani kuanzia kushoto ni Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese, Makamu mwenyekiti wa halmshauri, Edward Shigela na Mwenyekiti Boniphace Butondo.

Madiwani na wataalamu kutoka halmashauri hiyo wakifuatilia kikao hicho cha kupokea na kujadili tarifa za maendeleo ya kata.

KLABU YA MAJIMAJI YAJA NA MIKAKTI MIPYA YA MSIMU HUU WA LIGI.

$
0
0
Mwenyekiti wa majimaji ambaye amechaguliwa hivi karibu bwana steven Ngonyani amesema msimu huu mpaya wa ligi kuu TANZANIA bara lazima klabu hiyo ichukue ubigwa.NGONYANI AMESEMA jana mara baada ya kuchaguliwa kwa asilimia 93.5 na anachukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi na mtangulizi wake HAMPHREY MILANZI aliyemaliza muda wake huku wajumbe 6 wamechaguliwa isipokuwa makamu mwenyekiti ameshindwa kupatikana sababu ya kukosa vigezo.HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.  

TIMU YA RIADHA CHINI YA MIAKA 17 YAREJEA NCHINI NA MEDALI YA SHABA

$
0
0
Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Timu ya riadha ya vijana chini ya miaka 17 imeleta heshima kubwa kwa nchi yetu baada ya kurejea na medali ya shaba aliyoshinda kijana Francis Damasi katika  mbio za mita 3000 kwenye mashindano ya  Jumiya ya Madola yaliyomalizika hivi  karibuni huko nchini India.
Medali ya shaba katika mahindano ya riadha  iliyoletwa na kijana Francis imerejea tena baada ya miaka 19 tangu Tanzania ilivoshinda medali hiyo mwaka 2008 katika michezo hiyo.
Timu hiyo iliyorejea nchini leo imepokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo  ameeleza kufurahishwa na matokeo hayo mazuri waliyopata wanariadha hao ambao wameitangaza vyema Tanzania.
“Vijana mmefanya vizuri sana katika mashindano haya Serikali tunawapongeza sana  kwa kuitangaza nchi yetu lakini pia kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu katika mashindano haya nawaahidi kuendelea kushirikiana na uongozi na wadau wa riadha nchini ili tufike mbali zaidi” Alisema Prof. Elisante Ole Gabriel.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa chama cha riadha nchini Bw. Filbert Bayi  amesema kuwa mchezo wa riadha kwa sasa ni mchezo ambao umeitangaza Tanzania kwa kiasi kikubwa kutokana na kushiriki  mashindano mengi ya Kimataifa hivyo ni vyema wadau wakajitokeza kwa wingi kuwekeza katika mchezo huo ambao umeendelea kuletea heshima Taifa.
“Riadha imeitangaza Tanzania na itaendelea kuitangaza hivyo wadau wanapaswa kuona fursa hii na kuwekeza katika mchezo huu ili ufike mbali,kila mtu katika eneo lake aone fursa hii na aitumie kwa manufaa ya kizazi hiki na kitakachokuja” Alisema Bw. Bayi.
Naye Kijana Francis Damian aliyepata medali hiyo baada kushinda mbio za mita 3000 ameeleza kufurahishwa na ushindi huo kwani alijiandaa na alizingatia maelekezo ya walimu wake yaliyompelekea kupata ushindi huo na ameshauri vijana kama yeye kuthubutu na kuamini kuwa wanaweza kwani mchezo huo ni mzuri na una mafanikio makubwa.

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akimpongeza mwanariadha Francis Damas leo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa kupata ushindi wa medali ya shaba baada ya kushinda mbio za mita 3000 katika mashindano ya Jumuiya ya madola chini ya miaka 17 yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini Bahamas
 Katibu Mkuu chama cha Riadha nchini Bw. Filbert Bayi (aliyesimama) akizungumza  na wanariadha na wadau wa mchezo huo mara baada ya timu ya riadha ya vijana chini ya miaka 17 kurejea nchini na medali ya shaba katika mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyoalizika hivi karibuni huko Bahamas.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea Bendera ya Tanzania kutoka kwa  mwanariadha  Regina Mpigachai mara baada ya kurejea nchini na ushindi wa medali ya shaba katika mashindano ya Jumuiya ya madola chini ya miaka 17 yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini Bahamas.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi msaidizi wa maendeleo ya michezo wa Wizara hiyo Bw. Alex Nkenyenge.
Mkuu wa Msafara na mwalimu wa wanariadha Bibi Mwinga Mwanjala akitoa neno la shukrani  mara baada ya kurejea nchini na  ushindi wa medali ya shaba katika mashindano ya Jumuiya ya madola chini ya miaka 17 yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini Bahamas.

DC Babati awataka wakulima kuunga mkono jitihada za watafiti wa mbegu

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi akizungumza na wakulima na watafiti wa Mradi wa utafiti mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame na magonjwa (WEMA), katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati. Mratibu wa Mradi wa WEMA, na Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti Ilonga, Dk. Justin Ringo (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi (kulia) juu ya shamba la majaribio ya mbegu chotara za mahindi zinazostahimili magonjwa na ukame (WEMA), katika moja ya shamba la utafiti shirikishi lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati walipotembelea. Mtafiti wa Mradi wa WEMA, Ismail Ngolinda (kulia) akimtembeza mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi (kushoto) ndani ya shamba la majaribio katika moja ya shamba la utafiti shirikishi lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati walipotembelea.

SIMU TV: YALIYOJIRI KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI

$
0
0
 Tazama makala maalum inayoelezea suala la ukusanyaji kodi katika maeneo ya mipaka ya nchi ya Tanzania kwa ajili ya kuleta maendeleo chini; https://youtu.be/oxQL_wQ6SUY

Madiwani watatu CHADEMA halmashauri ya  wilaya ya Hai mkoa Kilimanjaro wamejiuzuru nafasi zao na kujiunga na CCM; https://youtu.be/IvUWc32ug-Y

Watu watano wameuawa kwa kuchomwa moto wilayani Nzenga mkoani Tabora kwa tuhuma za imanai ya kishirikiana; https://youtu.be/xZbxBi8v0k0

Mkuu wa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ameiagiza serikali ya kijiji cha Segeri kurudisha ardhi ya mwananchi aliyedhulumiwa na kiongozi wa serikali; https://youtu.be/qhRJ-JxSjBg

Mkuu wa mkoa wa Mbeya ametoa siku 20 kwa maafisa ardhi wa Mbeya kumaliza migogoro yote ya ardhi kabla ya kuchukuliwa hatua kali; https://youtu.be/Wyz6s5x1jYg

Baraza la madiwani halmashauri ya Mpanda wametoa kauli ya kutaka fedha za jimbo zirejeshwe kutokana na miradi mingi kusimama kwa muda mrefu; https://youtu.be/KSSi0QoxC9Y

Viongozi vyama vya ushirika mkoani Arusha wametakiwa kutatua changamoto zinazovikabili vyama vya ushirika mkoani humo; https://youtu.be/G2hLqpyB2DQ

Fuatilia mazunguzmo kuhusu nafasi ya kilimo kwa maendeleo ya uchumi wan chi na kipi kifanye kuboresha kilimo nchini Tanzania; https://youtu.be/Gy3YNZi8H7k

Kampeni ya Rais Magufuli ya kumtua mwanamke ndoo kichwani  imeanza kutekelezwa jijini Mwanza kwa mbunge wa Kwimba kuchimba visima 11. https://youtu.be/_nnxol7tWJg

Wananchi manispaa ya Songea wameamua kujenga zahanati ili kuondokana na kutembea umbali mrefu kwenda kupata huduma za afya; https://youtu.be/I_IMojm3ydQ

Bohari ya dawa nchini MSD imesema uanzishwaji wa maduka ya dawa umeleta mafanikio makubwa katika upatikanaji wa dawa kwa wananchi; https://youtu.be/JwZZSutNBHM

Wana-Diaspora wa Kitanzania waishio nchini Ufaransa waibuka na "Ndoto"

$
0
0
Filamu ya Ndoto imechezwa na wana-Diaspora wa Kitanzania waishio nchini Ufaransa. Lengo kubwa la filamu hii ni kuelimisha jamii kwa ujumla katika suala zima la watoto na vijana wenye magonjwa hadimu. 
Filamu hii ambayo inatoka kwa Maüa Association ikishirikiana na Mr Bodmas Studios inatarajiwa kuachiwa hivi karibuni.


DKT. PHILIP MPANGO ABAINI BAADHI YA WAFANYABIASHARA DODOMA HAWATUMII IPASAVYO EFDs

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua mashine ya EFD na risiti ya kieletroniki aliyopewa baada ya kununua bidhaa kwenye moja ya maduka mjini Dodoma, alipofanya ziara ya kushitukiza kukagua kama wafanyabiashara wa mji huo wanatumia ipasavyo mashine hizo.
Kiongozi wa Timu Maalumu ya Ukaguzi wa Mashine za EFD’s kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Dodoma, Bw. Godfrey Patrick (wa pili kushoto) akifafanua jambo wakati wa ziara ya kushitukiza iliyofanywa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), kwenye maduka mjini Dodoma.
Mfanyabiashara wa duka la rejareja mjini Dodoma, Bw. Donald Chami, akimwonesha mashine ya kieletroniki ambayo imeharibika, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), baada ya kufanyaziara ya kushitukiza kwenye duka lake na kubaini kuwa hatoi risiti za kielektroniki kwa wateja wake.

MAGAZETI YA IJUMAA LEO JULAI 28,2017

VIDEO: NAIBU WAZIRI WA AFYA AMPONGEZA KATIBU MKUU SIHABA NKINGA KWA UBORESHAJI WA MAKAZI YA WAZEE NCHINI

SHUGHULI MBALIMBALI ZA UVUVI WA SAMAKI PWANI YA TANGA MAPEMA LEO.

$
0
0
 Wachuuzi wa Samaki  wakiwa wanaelekea ndani ya Maji kwa ajili ya kununua Samaki maarufu kwa jina la Uono, ambao unapendwa sana katika mji wa Tanga kwa ajili ya kulia Ugali na kutafuna wakati wa chai asubuhi
 Wachuuzi wa Samaki wakichangamkia Samaki katika moja ya jahazi lililoingia na mzigo kutoka  katika kina kirefu mara baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu
 Mchuuzi wa Samaki akingia katika maji kwa ajili ya kununua Samaki katika Majahazi yaliyofika katika ufukwe wa Sahare
 Wavuvi wakiondoka kwenda kuvua mapema leo Asubuhi katika pwani ya Jiji la Tanga
 Mkazi wa Jiji la Tanga akichagua Samaki kutoka wauzaji wa soko la Sahare jijini Tanga.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

IGP SIRRO AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI SHINYANGA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na askari wa Jeshi hilo wakati alipofanya ziara ya kikazi katika mkoa wa Shinyanga, IGP Sirro, amewataka askari kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia wananchi kwa kutenda haki na kuzingatia sheria na taratibu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Simon Haule (aliyesimama), akitoa hotuba mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, ambaye yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga, waliojitokeza barabarani msafara wake wakati akitoka kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo, IGP Sirro, amewataka wananchi hao kuendelea kuitunza amani na kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwavichua wahalifu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kulia), akimsikiliza kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Wilbroad Mutafungwa, aliyekutananae wakati akiwa safarini kuelekea mkoa wa Singida kwa ajili ya muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kujitambulisha na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Polisi.

HIZI NDIZO SABABU KWANINI BAADHI YA VIVUTIO VYA UTALII HATUVITANGAZI -TANAPA

$
0
0
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa akifafanua mambo mbalimbali ukiwemo moja ya mjadala kuwa ni kwanini Tanzania ina vivutio vingi lakini havitangazwi,Mkurugenzi huyo ameyazungumza mapema leo kwenye Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.  

NIC YATOA ELIMU YA BIMA KWENYE MAONYESHO YA 12 YA TCU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, wakipewa maelezo na Afisa Mwanadamizi wa Shirikala Bima la Taifa(NIC) Konjeta Mwaipopo juu ya namna ya kujiunga na huduma za bima wakati walipotemblea banda la Shirika hilo, kwenye maonesho ya 12 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkazi wa Dar es Salaam, ambaye ni mjasiriamali Manoko Marikishua (kushoto) akipewa maelezo na Afisa Bima wa shirika la Bima la Taifa (NIC)) juu ya bima ya mazao wakati alipofika kwenye banda la Shirika hilo, kwenye maonesho ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam,wakipata maelezo juu ya huduma za bima toka kwa Afisa Bima wa Shirikala Bima la Taifa (NIC)) wakati walipofika kwenye banda la Shirika hilo, kwenye maonesho ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

TIMU YA RIADHA CHINI YA MIAKA 17 YAREJEA NCHINI NA MEDALI YA SHABA.

$
0
0
Na Shamimu Nyaki –WHUSM.

Timu ya riadha ya vijana chini ya miaka 17 imeleta heshima kubwa kwa nchi yetu baada ya kurejea na medali ya shaba aliyoshinda kijana Francis Damasi katika  mbio za mita 3000 kwenye mashindano ya  Jumiya ya Madola yaliyomalizika hivi  karibuni huko nchini India.

Timu hiyo iliyorejea nchini leo imepokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo  ameeleza kufurahishwa na matokeo hayo mazuri waliyopata wanariadha hao ambao wameitangaza vyema Tanzania.

“Vijana mmefanya vizuri sana katika mashindano haya Serikali tunawapongeza sana  kwa kuitangaza nchi yetu lakini pia kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu katika mashindano haya nawaahidi kuendelea kushirikiana na uongozi na wadau wa riadha nchini ili tufike mbali zaidi” Alisema Prof. Elisante Ole Gabriel.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa chama cha riadha nchini Bw. Filbert Bayi  amesema kuwa mchezo wa riadha kwa sasa ni mchezo ambao umeitangaza Tanzania kwa kiasi kikubwa kutokana na kushiriki  mashindano mengi ya Kimataifa hivyo ni vyema wadau wakajitokeza kwa wingi kuwekeza katika mchezo huo ambao umeendelea kuletea heshima Taifa.

“Riadha imeitangaza Tanzania na itaendelea kuitangaza hivyo wadau wanapaswa kuona fursa hii na kuwekeza katika mchezo huu ili ufike mbali,kila mtu katika eneo lake aone fursa hii na aitumie kwa manufaa ya kizazi hiki na kitakachokuja” Alisema Bw. Bayi.

Naye Kijana Francis Damian aliyepata medali hiyo baada kushinda mbio za mita 3000 ameeleza kufurahishwa na ushindi huo kwani alijiandaa na alizingatia maelekezo ya walimu wake yaliyompelekea kupata ushindi huo na ameshauri vijana kama yeye kuthubutu na kuamini kuwa wanaweza kwani mchezo huo ni mzuri na una mafanikio makubwa.

Medali ya shaba katika mahindano ya riadha  iliyoletwa na kijana Francis imerejea tena baada ya miaka 19 tangu Tanzania ilivoshinda medali hiyo mwaka 2008.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akimpongeza mwanariadha Francis Damas leo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa kupata ushindi wa medali ya shaba baada ya kushinda mbio za mita 3000 katika mashindano ya Jumuiya ya madola chini ya miaka 17 yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini India.
  Katibu Mkuu chama cha Riadha nchini Bw. Filbert Bayi (aliyesimama) akizungumza  na wanariadha na wadau wa mchezo huo mara baada ya timu ya riadha ya vijana chini ya miaka 17 kurejea nchini na medali ya shaba katika mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyoalizika hivi karibuni huko  chini India.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea Bendera ya Tanzania kutoka kwa  mwanariadha  Regina Mpigachai mara baada ya kurejea nchini na ushindi wa medali ya shaba katika mashindano ya Jumuiya ya madola chini ya miaka 17 yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini India.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi msaidizi wa maendeleo ya michezo wa Wizara hiyo Bw. Alex Nkenyenge.


Mkuu wa Msafara na mwalimu wa wanariadha Bibi Mwinga Mwanjala akitoa neno la shukrani  mara baada ya kurejea nchini na  ushindi wa medali ya shaba katika mashindano ya Jumuiya ya madola chini ya miaka 17 yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini India.

SIMIYU KUNUFAIKA NA MRADI MKUBWA WA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KWA UFADHILI WA MFUKO WA MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0

Na Lulu Mussa, Dodoma.

Serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (Green Climate Fund) imepata fedha za kutekeleza mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Mkoa wa Simiyu ambapo fedha za Mradi huo zitapitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW).

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora wakati wa kikao kazi kilichojumuisha wadau wanaohusika na utekelezaji wa Mradi wa maji wa Simiyu, mradi unaofadhiliwa na Mfuko wa mabadiliko ya tabianchi ambapo imebainika kuwa utekelezaji wake utaanza mara moja.

Aidha, Prof. Kamuzora amesema kuwa fedha hizo zinapitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani kutokana na sababu kwamba Serikali ya Ujerumani imekua ikifadhili miradi mbalimbali ya maji hapa nchini. “Ili kupata fedha kutoka katika mfuko huu ni lazima zipite kwenye taasisi ambayo imethibitishwa “accredited entity”alisisitiza Profesa Kamuzora.

Prof. Kamuzora amesema kuwa huu ni mradi mkubwa sana na wenye manufaa kwa wakazi wa Simiyu ambapo Mfuko wa Mabadiliko ya tabianchi umetoa kiasi cha 102,700,000 EURO, Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) itachangia 25,900,000 EURO na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itagharamia kiasi cha 13,100,000 EURO. Vilevile jamii inayozunguka mradi itachangia kiasi cha 1,500,000EURO, hivyo mradi wote unatarajiwa kugharimu kiasi cha EURO 143,000,000 na utatekelezwa ndani ya kipindi cha miaka mitano.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora akifungua mkutano wa wadau wa Utekelezaji wa Mradi wa Maji Simuyu. Mradi huo mkubwa uko katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kutekelezwa. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Eng. Emmanuel Kalobelo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Eng. Emmanuel Kalobelo akifunga kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora.

Katibu Mkuu Prof. Faustin Kamuzora (watatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi wanaohusika na utekelezaji wa Mradi wa maji wa Simiyu mara baada ya ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MAKAMBA ATOA RAI KWA WAANDAAJI WA MICHUANO YA NDONDO CUP

$
0
0
Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Janury Makamba jana akiwa mgeni wa heshima kwenye mchezo wa robo fainali ya kwanza ya michuano ya Ndondo Cup 2017 kwenye uwanja wa Kinesi-Sinza.

Wakati akitoa neno baada ya mchezo kati ya Vijana Rangers vs Kibada One, Makamba amezungumzia changamoto nne ambazo zinatakiwa kutatuliwa ili kupiga hatua kwenye soka la Tanzania.

“Changamoto kubwa ni kuendeleza mashindano haya lakini kuendeleza soka la Tanzania, mpira unahitaji vitu vinne ili ufanikiwe. Kwanza unahitaji vipaji ambavyo vipo, pili miundo mbinu ya mchezo wenyewe kama viwanja, academies na kadhalika, tatu tunahitaji mifumo ya kuvumbua na kuendeleza vipaji lakini naamini mashindano haya yanatoa fursa hiyo ya kuvumbua na kuviendeleza halafu tunahitaji utawala ‘sports management’,”

“Nimeshuhudia mpira mzuri sana ambao ulikuwa na ushindani mzuri na nguvu sawa ndio maana mshindi amepatikana kwa penati. Kubwa zaidi nimeshuhudia mwamko mkubwa sana lakini tunaona mafanikio makubwa kwenye mashindano haya ya Ndondo Cup na wote waliohudhuria hapa wamepata burudani.”

Makamba amesema amefurahi kuwa karibu na wananchi alipokwenda kushuhudia mechi ya Ndondo tofauti na anapokwenda kwenye mechi nyingine ambazo ni rasmi sana ambapo huwa na itifaki kubwa.
Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Janury Makamba akiwa katika picha ya pamoja na Mratibu wa michuano hiyo (katikati) Shafii Dauda na Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam Almas Kisongo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA MKUU WA MAJESHI WA INDIA NA KUFANYA MAZUNGUMZO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano na Serikali ya India katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya ulinzi.

Ametoa kauli leo (Ijumaa, Julai 28 , 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi wa India, Bw. Admiral Sunil Lanba jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Tanzania na India ni nchini ambazo zina uhusiano mzuri na wa muda mrefu, ambapo ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha. “Ushirikiano wa Tanzania na India ni wa kihistoria, hivyo tutauendeleza na kuudumisha. India tunashrikiana nao katika sekta za uchumi, afya, elimu na ulinzi.”

Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya India kwa ufadhili walioutoa kwa Tanzania  katika kuimarisha miradi ya maji kwenye mikoa mbalimbali nchini.Pia Waziri Mkuu amewakaribisha raia wa India kuja kutembelea maeneo ya  utalii nchini ukiwemo mlima wa Kilimanjaro, mbuga za wanyama na visiwa vya Zanzibar.

Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi wa India, Bw. Lanba ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano inaoutoa kwa Serikali ya India hususan katika masuala ya ulinzi.

Amesema wamefanya kikao na Mkuu wa Majeshi nchini Generali Venance Mabeyo ambapo katika mazungumzo yao wameweka mikakati ya kushirikiana katika kuimarisha ulinzi hususan maeneo ya mipakani pamoja na masuala ya mafunzo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral  Sunil Lanba Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kulia ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venance Mabeyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India , Admiral Sunil Lanba  (kulia kwake) pamoja na ujumbe wake, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venace Mabeyo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa Majeshi wa India Admiral Sunil Lanba  (wapili Kushoto) na Mkuu wa Majeshi nchini, Jeneral Venance Mabeyo (kushoto) baada ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa Majeshi wa India Admiral Sunil Lanba  (kulia kwake ) na Mkuu wa Majeshi nchini, Jeneral Venance mabeyo (kushoto kwake ) baada ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo  na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral  Sunil Lanba (kulia) baada ya mazungumzo yao Ofisini kwa  Waziri Mkuu  jijini Dar es salaam Julai 28, 2017 . Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi Nchini, Jeneral Venance Mabeyo na kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.v
Viewing all 120100 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>