Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1818 | 1819 | (Page 1820) | 1821 | 1822 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na Tamimu Adam - Jeshi la Polisi. 

  Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika Kanda maalumu ya kipolisi Rufiji ambapo mmoja kati ya watu hao ametambulika kwa jina la Abdallah Ally Ngande Makeo ambaye alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa muda mrefu kutokana na kushiriki kwake katika matukio ya mauaji maeneo ya Ikwiriri, Kibiti pamoja na uvamizi wa kituo cha Polisi Ikwiriri. 
  Akielezea tukio hilo, Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 19, julai, 2017 saa mbili usiku katika eneo la Utende kata ya Ikwiriri, wilaya Rufiji kanda maalum ya Polisi Rufiji. 
  “ Askari Polisi wa doria waliwatilia mashaka watu wanaokadiliwa kuwa watano ambapo walianza kuwafutilia ndipo walianza kukimbia huku wakiwashambulia askari kwa risasi, askari nao kwa ujasiri walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi wahalifu wawili miongonio mwao ambao baadaye walifariki wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya muhimbili kutokana na kuvuja damu iliyosababisishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata” alisema Sabas. 
  Aliongeza kuwa katika eneo hilo la tukio ilipatikana silaha moja aina ya rifle 375 ambayo ilikutwa imekatwa kitako na mtutu ikiwa na risasi mbili (2). Aidha, Miili ya marehemu wote wamehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Taifa ya muhimbili. 
  Kamanda sabas ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa wahalifu wengine waliosalia na kwamba opereheni hiyo ya kuwasaka wahalifu katika Kanda hiyo ya kipolisi Rufiji ni endelevu na hakuna atakaye baki. 
  Mkuu wa Operesheni Maalun za Jeshi la Polisi, Naibu kamishina wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas akiwa katika eneo la tukio akizungumzia namna Jeshi la Polisi lilivyofanikiwa kuuawa watu wawili awanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu wanaojihusisha na mauaji watu katika Ikwiriri na kibiti. (Kushoto kwake ) ni Kamanda wa Kanda maalum ya Kipolisi Rufiji, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Onesmo Lyanga akiwa ameshika silaha aina ya Rifle 375 iliyokutwa katika eneo la tukio. Picha na Tamimu Adam.

  0 0

  Na Tamimu Adam - Jeshi la Polisi

  Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua watu wawili  wanaosadikiwa kuwa  ni miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika  Kanda maalumu ya  kipolisi Rufiji ambapo  mmoja  kati ya watu hao  ametambulika  kwa jina la Abdallah Ally Ngande Makeo ambaye alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa muda mrefu kutokana na kushiriki  kwake katika matukio ya  mauaji maeneo ya Ikwiriri, Kibiti pamoja na uvamizi wa kituo cha Polisi Ikwiriri.

  Akielezea tukio hilo,  Mkuu wa Operesheni Maalum  za Jeshi la Polisi,  Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 19, julai, 2017 saa mbili usiku katika eneo la  Utende kata ya Ikwiriri,  wilaya Rufiji kanda maalum  ya Polisi  Rufiji.


   “Askari  Polisi  wa doria  waliwatilia mashaka watu wanaokadiliwa kuwa watano ambapo walipoanza kuwafutilia ndipo walianza kukimbia huku wakiwashambulia  askari kwa risasi. Askari nao kwa ujasiri walijibu   mashambulizi na kufanikiwa  kuwajeruhi  wahalifu wawili miongonio mwao ambao baadaye  walifariki  wakipelekwa Hospitali  ya Taifa ya muhimbili kutokana na kuvuja damu iliyosababisishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata” alisema Sabas.

  Aliongeza kuwa  katika eneo  hilo la tukio ilipatikana silaha moja aina ya rifle 375 ambayo  ilikutwa imekatwa kitako na mtutu ikiwa na risasi mbili (2).  Aidha, Miili ya marehemu wote wamehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Taifa ya muhimbili.

   Kamanda sabas ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa wahalifu wengine waliosalia na kwamba  opereheni hiyo ya kuwasaka wahalifu katika Kanda hiyo ya kipolisi Rufiji  ni endelevu  na hakuna atakayebaki.

  0 0
  0 0

  NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
  UONGOZI mpya wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), umekabidhiwa rasmi usukani wa kuongoza taasisi hiyo muhimu katika mawasiloiano ya serikali nchini.
  Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jijini Dar es Salaam, Julai 20, 2017 ambapo Mwenyekiti wa TAGCO aliyemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy, alimkabidhi “nyenzo” za kufanyia kazi Katibu Mkuu mpya wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi, ambapo shughuli hiyo ilishuhudiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO anayeshuhulikia Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus, Mweka Hazina wa chama  hicho aliyemaliza muda wake, Bw. Peter Malinzi, Mweka Hazina Msaidizi Mteule, Bw.Gerald Chami.
  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekliti aliyemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy alisema, “tunawakabidhi TAGCO, hiki ni chombo muhimu sana kwa mawasiliano ya serikali, hivyo hakikisheni mnakiongoza vyema ili maelengo kusudiwa yafikiwe,”.alisema Bw. Mungy.
  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi alisema, “Tunashukuru kwa kukabidhiwa usukani wa TAGCO, tunajua hiki chombo ni muhimu sana katika kuhakikisha wananchi wanapatiwa taarifa sahihi za shughuli za Serikali yao inazofanya, tutatekeleza majukumu yetu kwa umakini na uaminifu mkubwa, tunaomba ushirikiano kutoka kwa uongozi uliopita na wanachama wote wa TAGCO na watendaji wote serikalini,”. Alisema Bw. Njaidi wakati akitoa neon la shukrani.
  Viongozi wengine wapya wa TAGCO ni Bw. Pascal Shelutete (Mwenyekiti), Bi. Sarah Kibonde Msika (Makamu Mwenyekiti), Bi. Tabu Shaibu (Mweka Hazina), Bi. Gaudensia Simwanza (Katibu Msaidizi), Bw. Owen Mwandubya (Katibu Mwenezi) na Bw. Mpokigwa Mwakasipo (Katibu Mwenezi Msaidizi).
  TAGCO nichama kinachowa kutanisha pamoja Maafisa Mawasiliano wa Taasisi mbambali za umma, serikali na Halmashauri zote hapa nchini, lengo likiwa ni kupena ujuzi na uwezo wa kuhakikisha taarifa za serikali zinawafikia wananchi kwa usahihi na kwa wakati.
   
  Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), ambaye amemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy, (wapili kulia), akimkabidhi nyaraka za chama, Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, Bw. Abdul Njaidi. (wapili kushoto), ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi majukumu ya kiuongozi jijini Dar es Salaam Julai 20, 2017. Wengine pichani walioshuhudia hafla hiyo ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO anayeshughulikia Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus, (watatu kushoto), Bw. Gerald Chami, (wakwanza kushoto), ambaye ni Mweka Hazina Msaidizi na Bw.Peter Malinzi, (kulia), Mweka Hazina aliyemaliza muda wake.

  Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), ambaye amemaliza muda wake Bw. Innocent Mungy, (wapili kulia), akishuhudia wakati  Katibu Mkuu mpya wa chama hicho Bw. Abdul Njaidi. akisaini  nyaraka za makabidhiano.

  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto) akizungumza na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi (SACP) Augusine Ollomi, muda mfupi alipowasili. IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari pamoja na kujua chamgamoto wanazokutana nazo wakati wakitekeleza majukumu yao
   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya askari wa kikosi maalum kinachofanya doria za kupambana na wahalifu aliokutana nao katika eneo la Nyakanazi mkoani Kagera, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari pamoja na kujua chamgamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (Mb), akitafakari jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro walipokutana katika viwanja vya Lemela wilayani Ngara mkoa wa Kagera, wakisubiri kuwasili kwa Rais Dkt. John Magufuli na Rais Pierre Nkurunziza wa Jamhuri ya Burundi. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi.


  0 0

   Mgeni rasmi Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete (meza kuu kulia juu) akimshangilia shabiki mkubwa  wa timu ya Kauzu Fc ya Tandika  Chief Kauzu wakati akiingia katika uwanja wa Kinesi eneo la Ubungo jijini Dar es salaam kabla ya mchezo wa Mashindano ya Mpira wa Miguu ya SportsXtra Ndondo Cup yanayoandaliwa na Clouds FM na AzamTv,  baina ya Kauzu FC na Stim Tosha ambayo iliibuka mshindi kwa njia ya penati 4-2 baada ya kutoka sare ya 1-1.
   Mgeni rasmi Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiongea jambo na Chief Kauzu wa Timu ya Kauzu Fc ya Tandika
   Mgeni rasmi Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa meza kuu na viongozi wengine wa michuano hiyo
   Mgeni rasmi Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akigawa zawadi kwa kiongozi wa timu ya Kauzu FC. Kushoto ni Mbunge wa Ubungo Mhe. Saeed Kubenea
  Mgeni rasmi Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akigawa zawadi  kwa viongozi wa timu ya StimTosha ya Mabibo ambao ndiyo walioibuka na Ushindi wa Magoli 4-2 kwa njia ya Penalti baada ya kumaliza mchezo kwa sare ya 1-1

  0 0
  0 0


  0 0

  Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu amekamatwa leo, Alhamisi, Julai 20 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akielekea Kigali, Rwanda kwenye Mkutano wa Marais wa Vyama vya Mawakili Afrika Mashariki.
  Kamanda wa polisi viwanja vya ndege, Martin Ortieno amesema kwamba ni kweli wamemkamata Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema na kwamba amepelekwa makao makuu ya Polisi kwa ma.
  Hata hivyo, kamanda huyo hakutaja sababu za kukamatwa kwa mwanasheria huyo.
  Nae Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amekiri kuwa mwanasheria huyo amekamatwa jioni hii. Mrema amesema Lissu amekamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni maofisa wa polisi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

  0 0
 • 07/21/17--03:25: UNYAMA WA MBWA MWITU


 • 0 0

  Wataalam wa Usafiri wa Anga  nchini wamekutana katika semina ya siku tatu ya kuwajengea uwezo kuhusu namna bora ya kushughulikia malalamiko na kero za watumiaji wa usafiri wa anga nchini katika semina iliyofanyika mjini Morogoro kuanzia  Julai 20, 2017. 

  Semina hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)  nchini imewakutanisha wajumbe wa kitengo cha Kushughulikia Malalamiko ya Watumiaji wa Usafiri wa Anga cha TCAA(TCAA-CCU), Watendaji wa Baraza la Watumiaji wa Usafiri wa Anga(TCAA-CCC), wanasheria wa Mamlaka na maafisa  kutoka idara ya udhibiti masuala ya Kiuchumi ya TCAA ambayo inajukumu la kulinda maslahi ya watumiaji wa usafiri  wa anga .

  Miongoni mwa mada zilizotolewa kwenye semina hiyo ni pamoja na  wajibu wa  kampuni za ndege kwa abiria, iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa  TCAA, Hamza S. Johari, majukumu ya kitengo cha kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa usafiri wa anga na  nyezo za kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa usafiri wa anga.

  Semina hii ni sehemu ya mkakati wa usafiri wa anga wa kuboresha huduma zinazotolewa kwa watumiaji wa usafiri wa anga na kukuza sekta ya usafiri wa anga Tanzania
   Mkurugenzi  Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari, akitoa mada kuhusu wajibu wa Mashirika ya Ndege kwa Abiria Kwa Washiriki wa Semina ya Siku Tatu Kuhusu Namna ya Kushughulikia Malalamiko ya Watumiaji wa Usafiri wa Anga Nchini Iliyofanyika Morogoro, Kuanzia Julai 20, 2017. 
   Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza S. Johari(Kulia) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kudhibiti Masuala ya Kiuchumi, Dan Malanga wakifuatilia mada kwenye semina kuhusu namna ya kushughulikia Malalamiko ya Watumiaji wa Usafiri wa Anga iliyofanyika Morogoro Mwezi July 20, 2017.
   Washiriki wa Semina kuhusu namna ya kushughulikia malalamiko ya matumiaji wa Usafiri wa Anga wakifuatilia mada ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza S. Johari.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Watumiaji wa Usafiri wa Anga(TCAA-CCC) Elias Mwashiuya, akiwasilisha mada kwa Washiriki wa Semina ya Siku Tatu kuhusu namna ya kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa Usafiri wa Anga iliyofanyika Morogoro Julai 20, 2017.


  0 0

  Kwa niaba ya Manispaa ya Kigoma Ujiji naomba kuchukua fursa hii kuushukuru Ubalozi wa China nchini, Balozi pamoja na Timu ya Wawekezaji kutoka China waliokuwa wageni wetu hapa Ujiji kwa muda wa siku 3. 

  Ujio wao ni jambo lenye faraja kwetu kwamba juhudi zetu za kuainisha fursa za uwekezaji hapa  Kigoma (kupitia mwongozo wa Uwekezaji Kigoma Ujiji - Kigoma Ujiji Investor's Guide) zimeanza kuzaa matunda na kuvutia uwekezaji kutoka maeneo mbalimbali duniani.

  Ziara ya Balozi Lu Youqing na timu yake imewezesha makubaliano kwenye maeneo matano (5) ya uwekezaji:

  1. Ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata Samaki na mazao ya Samaki katika mji wa Katonga, Kata ya Bangwe.

  2. Ujenzi wa Kituo cha Biashara Ujiji (Ujiji City - The Great Lakes Trade and Logistics Center) katika kata ya Kitongoni na Kasimbu.
  3. Uwekezaji Wa Kiwanda cha kusindika mazao ya michikichi.
  4. Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Vijana eneo la Mwanga Community Center.
  5. Ukarabati wa Soko la Ujiji na jengo la watumwa na ujenzi wa barabara ya watumwa ili kukuza Utalii na Ujenzi Mwalo wa Katonga.

  Ziara ilikuwa ya mafanikio makubwa sana, ikitufikisha hata katika maeneo ambayo ni nadra mabalozi kufika (kama pichani tukivuka mto Luiche), ninaamini kuwa wananchi wa Kigoma watafanikiwa na miradi hii inayotokana na mahusiano mazuri kati ya nchi yetu na Jamhuri ya watu wa China. 

  Ni dhamira yetu kuhakikisha tunautumia muda wa dhamana yetu tuliyopewa na wananchi kushirikiana nao kuleta maendeleo na kuipeleka mbele Kigoma Ujiji.

  Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
  Mbunge, Kigoma Mjini - ACT Wazalendo 
  Kigoma 

  0 0  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mwanachuo wa Chuo cha DIT, Grolia Shoo kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba zinazojengwa na Shirika la Taifa la Nyumba katika eneo la Chitete wialyani Momba Julai 21, 2017. Gloria anafanya kazi kwa muda akijifunza katika shirika hilo. Kushoto kwake ni mkewe Mary na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, NHC, Blandina Nyoni. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la ujenzi wa nyumba 20 za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba katika eneo la Chitete akiwa katika ziara ya mkoa wa Songwe Julai 21, 2017. Wapili kulia ni mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linalojenga nyumba hizo, Blandina Nyoni. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mwenyekiti wa CHADEMA wa kata ya Kangwa wilayani Songwe ,Keneth Nzowa ambaye pamoja na wenzake walitangaza kukihama Chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa michezo wa Mkwajuni wilayani Songwe Julai 20, 2017.
  Wananchi wa Songwe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadahara katika uwanja wa michezo wa Songwe Julai 20, 2017.(picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Chief Mwibongo wa Ivungu baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa michezo wa Mkwajuni wilayani Songwe Julai 20, 2017.

  0 0


  Tunapenda kutoa taarifa kwa Ndugu, Jamaa, Marafiki, Familia na wote  tuliopatwa na msiba huu wa marehemu Professor  Henslay William Kabisama uliyotokea huko Ontario, California, Marekani. 


  Mwili wa mpendwa wetu Prof Henslay Kabisama utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Ijumaa Julai 21, 2017 saa tisa mchana. Tunaombeleza nyumbani kwa marehemu Ursino  Victoria nyuma ya Ofisi za Halotel.  
  Mazishi yatafanyika kesho Jumamosi Julai 22, 2017 yakitanguliwa na Ibada ambayo itafanyika  katika kanisa la   St Alban Upanga saa saba kamili mchana. Baada ya hapo tutaelekea  makaburi ya Kinondoni kwa mazishi. 

  Bwana alitoa na bwana ametwaa
  Jina la Bwana libarikiwe
  AMEN.

  0 0

  Nteghenjwa Hosseah, Kibakwe.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote Nchini kuandaa mazingira rafiki kwa watumishi wapya wanaopangiwa katika Halmashauri zao.

  Simbachawene ameyasema hayo ikiwa ni wiki moja tangu kutangaza ajira mpya za Walimu wa Masomo ya Hisabati na Sayansi wapatao 3,081 wa ngazi ya Shahada na Stashahada ambao wamepangiwa kwenye Halmashauri mbalimbali Nchini.

  Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msangambuya wakati wa Ziara yake ya Kikazi Wilayani Mpwapwa katika Jimbo la Kibakwe Mhe. Simbachawene amesema watumishi wengi wapya wanakatishwa tamaa na mazingira mabovu wanayoyakuta katika Halmashauri zao na hali hiyo huwatia hofu ya kuendelea kukaa katika maeneo hao.

  Unakuta mtumishi anafika Halmashauri malipo yake hayajaandaliwa zaidi ya mwezi mzima, kisha anapangiwa kwenye Kata mbayo hata hajawahi kuifahamu hapo awali na hapewi hata maelekezo ya ziada ya namna ya kufika katika Kituo chake na unakuta wenyeji wake katika Kata na Shule hawana taarifa za ujio wa mtumishi huyo hivyo mtumishi anahangaika mpaka anakosa ari ya kufanya kazi katika kituo chake kipya alisema Simbachawene.

  “Ninahitaji Kila Halmashauri kuandaa Malipo stahiki kwa ajili ya walimu wanaoendelea kuripoti hivi sasa katika maeneo mbalimbali, Usafiri wa kuwapeleka katika vituo vyao vya Kazi, mapokezi stahiki kwa uongozi wa Kata pamoja Shule sambamba na kuhakikisha anapata makazi bora ya kuishi katika eneo lake jipya la Kazi”.

  Sitaelewa Halmashauri ambayo itashindwa kuzingatia maagizo haya kwa namna yeyeote ile na ntaendelea kufuatilia mazingira ya mapokezi ya watumishi hawa, sitaki mtumishi yeyote ashindwe kufanya kazi yake kwa ufanisi kwa sababu ya mazingira magumu anayokutana nayo wakati wa kuripoti kazini, Aliongeza.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene (kwanza Kulia) akisalimiana na Wakina Mama wa Kijiji cha Msangambuye wakati wa Ziara yake Wilayani Mpwapwa katika Jimbo la Kibakwe.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene(mbele) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msangambue, Kata ya Mtera Tarafa ya Rudi wakati wa Ziara yake Katika Jimbo la Kibakwe.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene(mbele) akitoa maelekezo kwa Wazee wa Kijiji cha Msangambuye wakati wa Ziara ya Kikazi Jimboni Kibwakwe.


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano - Sekta ya Mawasiliano, Injinia Angelina Madete amesema uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ufundi (ICoT), utasaidia kupunguza pengo lililopo sasa baina ya wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo hapa nchini.

  Akifungua warsha ya wataalam washauri na wadau wa Taasisi ya Teknolojia ya Ufundi Jijini Dar es salaam leo, Mhandisi Madete amewataka wataalam hao kufanya uchambuzi wa kina ili kuwezesha taasisi hiyo mpya kukidhi mahitaji ya mafundi sanifu na mchundo na hivyo kukidhi uwiano wa kimataifa unaotaka mhandisi mmoja, fundi sanifu watano na mafundi mchundo 25.

  “Tunataka kuwa nchi ya viwanda vya kati ifikapo mwaka 2025, hivyo ni lazima tuwe na wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo wa kutosha watakaofanyakazi kwa weledi na kumudu ushindani katika soko la ajira”, amebainisha Injinia Madete.

  Mhandisi Madete amesema kuwa pengo la wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo limeongezeka kutokana na vyuo vingi vya kati kutoa shahada hivyo uwepo wa ICoT utakabiliana na kumaliza changamoto hiyo.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Sekta ya Mawasiliano Mhandisi Angelina Madete akisisitiza jambo alipokuwa akifungua warsha kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya ECOM Research Group Ltd, Profesa Godwin Daniel Mjema akifafanua jambo mbele ya wadau wa sekta ya ujenzi wakati wa warsha kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya ECOM Research Group Ltd, Profesa Godwin Daniel Mjema akifafanua jambo mbele ya wadau wa sekta ya ujenzi wakati wa warsha kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.


  0 0

  Mrakibu wa Polisi Mkoani Tanga (SP),Bahati Ngoli akifungua mafunzo ya jinsi ya kushughulika na watoto walio katika ukinzani na Sheria leo ulioandaliwa na chama cha wanasheria wanawake Tanzania (Tawla) Mkoani Tanga kwenye ukumbi wa Hotel ya Nyumbani mjini Tanga 
  Mratibu wa Chama cha Wanasheria wanawake Tanzania Mkoani Tanga (Tawla) Latifa Ayoub akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo leo 
  Juma Abdallah kutoka Tawla Mkoani wa Tanga akitoa mada kuhusu wajibu wa familia na jamii kuzuia uhalifu wa watoto 
  Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria wanawake Tanzania Mkoani Tanga,Adolphina Mbekinga akizungumza wakati akiwasilisha mada ya mfumo wa haki jinai kwa watoto Tanzania na Taratibu zake.


  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi (kushoto)  akikabidhi kifaa kinachotumika kutambua gesi zinazoharibu na zisizoharibu  tabaka la ozoni (Refrigerant Identifier)  kwa Mkufunzi wa Chuo cha Ufundi stadi (VETA) Bwana Daudi Kadinda wakati wa makabidhiano Ofisini kwa Mkurugenzi huyo.

   Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi (kushoto) akikabidhi kifaa kinachotumika kutambua gesi zinazoharibu na zisizo haribu tabaka la ozoni(Refrigerant Identifier ) kwa Afisa toka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bwana Arnold Mato, wakati wa makabidhiano Ofisini kwa Mkurugenzi huyo.

   Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akipeana mkono na Wataalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  na Chuo cha ufundi Stadi VETA-Chang'ombe mara baada ya kuwakabidhi vifaa vya vinavyotumika kutambua gesi zinazoharibu na zisizoharibu  tabaka la ozoni.

   Pichani kifaa kinachotumika kutambua gesi zinazoharibu na zisizo haribu tabaka la ozoni(Refrigerant Identifier ) kinavyoonekana kwa ndani.

  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais  Bibi Magdalena Mtenga akijadiliana jambo na Wawakilishi toka TBS na VETA-Chang'ombe mara baada ya makabidhiano hayo.


  0 0  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Israel nchini anayemaliza muda wake Mhe. Yahel Vilan.

  Balozi huyo alikutana na Makamu wa Rais na kumuaga rasmi kwani muda wake wa kutumikia nchini ulikuwa umemalizika. akamu wa Rais alisema anafurahi kuona Idadi kubwa ya Watalii kutoka Israel wanaokuja Tanzania .

  “Tunawakaribisha sana Tanzania ,waje kwa wingi wao, tunawakaribisha kwa mikono miwili” na alimuhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili.

  Kwa upande wake Balozi Yahel alisema watalii kutoka nchini Israel wameongezeka kutokana na kuvutiwa na mazingira mazuri , amani na utulivu wa nchi.

  Balozi Yahel alisema atakuwa mjumbe wa kuitangaza Tanzania popote duniani .
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Israel nchini Mhe. Yahel Vilan (kushoto) ambaye muda wake wa kutumikia umemalizika na alifika kumuaga Mhe. Makamu wa Rais kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuaga .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Israel nchini Mhe. Yahel Vilan (kushoto) ambaye muda wake wa kutumikia umemalizika na alifika kumuaga Mhe. Makamu wa Rais kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuaga .
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Israel nchini Mhe. Yahel Vilan (kushoto)ambaye muda wake wa kutumikia umemalizika na alifika kumuaga Mhe. Makamu wa Rais kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuaga . 

older | 1 | .... | 1818 | 1819 | (Page 1820) | 1821 | 1822 | .... | 3286 | newer