Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1817 | 1818 | (Page 1819) | 1820 | 1821 | .... | 3286 | newer

  0 0

  MBUNGE wa Dodoma mjini Anthony Mavunde ameendelea kutatua kero katika sekta ya Afya jimboni humo ambapo leo amezindua matumizi ya mfumo wa Biometrics na kamera za CCTV katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,kufuatia hali hiyo wagonjwa wengi waliokuwepo hospital hapo walionekana wenye furaha na kuunga mkono jitihada za mbunge wao katika kusaidia kuboresha huduma za Afya katika hospital hiyo.

  Akizungumza katika uzinduzi wa matumizi ya vifaa hivyo, Mavunde amesema ufungaji wa mifumo hiyo ni miongoni mwa jitihada zake za kuhakikisha huduma za afya katika jimbo hilo zinatolewa ipasavyo.

  Mavunde ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana amesema mfumo huo umefungwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma na amelazimika kufunga vifaa hivyo kutokana na malalamiko ya muda mrefu ya wagonjwa kuwa wamekuwa wakitolewa lugha chafu na wauguzi.

  Amesema pamoja na kamera hizo, pia umefungwa mfumo wa Biometrics(uchukuaji alama za dole gumba) ili kudhibiti watumishi ambao wamekuwa wakiondoka kabla ya muda na kuchelewa kuingia kazini.

  “Kamera hizi zinarekodi sauti na kuchukua video ili kuondokana na malalamiko yaliyotolewa na wananchi na itakuwa ni rahisi kumbaini mtu atakayelalamikiwa na mgonjwa,”amesema Mavunde
  Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde,akizungumza na wafanyakazi wa Hospital ya Mkoa wa Dodoma hii leo.
  Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde,akizungumza na wafanyakazi wa Hospital ya Mkoa wa Dodoma hii leo,wakati wa uzinduzi mfumo wa Biometrics na kamera za CCTV katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo.
  Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde,akibonyeza kitufe wakati wa kuzindua matumizi ya mfumo wa Biometrics na kamera za CCTV katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

  0 0

  Mwanamuziki nguli na mpiga Saxophone maarufu na aliyekuwa rais wa bendi ya Super Kamanyola yenye maskani yake jijini Mwanza, Munuka Roy maarufu "Bwana Kitoko" amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili likokuwa amelazwa kwa matibabu.
  Mwanamuziki Roy ambaye alikuwa pia ni mwalimu wa muziki, mtunzi na mpuliza saxophone mahiri, alitamba zaidi na iliyokuwa bendi maarafu hapa nchini ya Orchestra Maquis Du Zaire na baadae Maquis Original. 
  Mungu Aiweke Roho yake mahala pema peponi.
  -AMIN

  0 0

  Pichani ni Jenerali Mirisho Hagai Sarakikya (kati) akiwa na wanariadha mabingwa wa dunia wa zamani, Filbert Bayi (kushoto) na Juma Ikangaa.  Hawa ni watu watatu ambao mjina yao yanastahili kuandikwa kwa wino wa dhahabu katika vitabu vya kumbukumbu  ya historia ya riadha na michezo nchini Tanzania. Hilo halina ubishi...
  Tukianza na Jenerali Sarakikya, yeye ndiye alikuwa Mkuu wa Majeshi wa kwanza mara tu bada ya Tanganyika kupata uhuru mwaka 1964 na akatumikia wadhifa huo kwa miaka kumi yaani toka hiyo 1964 hadi alipostaafu mwaka 1974. Wakati anapata cheo kuwa CDF Jenerali Sarakiya pia alikuwa ndiye mwenyekiti wa chama cha riadha cha Tanzania (TAA) kuanzia mwaka 1962 hadi mwaka 1972.
  Ikiwa hiyo haitoshi mara baada ya kustaafu jeshini mwaka huo huo wa 1974, Mwalimu Nyerere alimteua Jenerali  Sarakikya kuwa Waziri wa Michezo, Vijana na Utamaduni.
  Ukiangalia katikati ya mistari utamaizi kwamba historia ya mafanikio ya riadha na michezo kwa ujumla nchini Tanzania yalikuwa katika miaka hiyo ambayo Jenerali Sarakikya alikuwa mwenyekiti wa TAA, Mkuu wa Majeshi na baadaye Waziri wa michezo, vijana na utamaduni.
  Huo ndio wakati wanariadha Filbert Bayi, Juma Ikangaa, Suleiman Nyambui, Gidamis Shaganga, Mwinga Mwanjala, Nzaeli Kyomo na wengi wengine walikuwa wanang’ara kwenye medani za kimataifa.
  Kwa hiyo picha hii ni kubwa na yenye historia nzito kwa kadri mafanikio katika michezo kwa nchi hii yanahusika.
  Wote watatu ni wanajeshi wastaafu, kwani Filbert Bayi  baada ya ushindi wake alipandishwa cheo hadi kuwa Luteni, na baada ya kuhudhuria mafunzo ya afisa kadet huko Monduli mwaka 1977 alipanda kuwa Kepteni. Hadi anastaafu mwaka 2001 alikuwa na cheo cha Meja kitengo cha ufundi wa ndege jeshini.

  Kwa upande wa Ikangaa, yeye alikuwa Mkurugenzi wa michezo makao makuu ya jeshi hadi alipostaafu kwa mujibu wa sheria akiwa na cheo cha Kanali. 
  Filbert Bayi Sanka ni mwanariadha aliyeiandikia Tanzania historia isiyoweza kusahaulika. Filbert Bayi ndie mwanariadha wa Pili ambae anakamilisha medali ya pili ya Tanzania kwenye Mashindano ya Olympic.
  Tanzania Imewahi kupata Medali mbili tu katika Mashindano ya Olympic mpaka sasa. Filbert Bayi alipata Medali ya Silver katika mbio za mita 3000 katika mashindano ya Olympic yaliyofanyika mwaka 1980 MOSCOW Mwaka 1978(mita 1500) na Mwaka 1973 (mita 1500) katika mashindano ya All African Games Fibert Bayi alishinda Medali za Dhahabu kwa kuibuka namba moja katika mashindano yote 2.
  Ushindi huu ulitengeneza historia kubwa Tanzania. Mwaka 1974 katika mashindano ya Commonwealth Games yaliyofanyika Christchurch “New Zealand” Filbert Bayi aliweka rekodi ya kukimbia mita 1500 kwa dakika 3 na sekunde 32.2 mbele ya mwanariadha kutoka New Zealand John Walker na Mkenya Ben Jipcho, hivyo kuiwezesha Tanzania kupata medali ya Dhahabu katika mashindano hayo. Video ya chini inakupa maajabu aliyofanya Juma Ikangaa. 

  0 0

  Watanzania wametakiwa kutumia fursa zinazoendelea kuwekwa na serikali ya awamu ya tano kujikita katika ujasiriamali na kuanzisha viwanda kwa ajili ya kujenga uchumi viwanda ili kufikia uchumi kati na kuboresha ustawi wa jamii hapa nchini

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,Profesa Adolf Mkenda alisema hayo wakati wa mkutano wa wadau uliokuwa ukijadili rasimu ya mapendekezo ya kuwa na mkakati wa kitaifa kuendeleza ujasiriamali hapa nchini, kuwa wakati wa watanzania kujikita katika ujasiriamali na kuwekeza katika viwanda umewadia.

  “Wakati wa watanzania kuanzisha viwanda kuzalisha bidhaa zinazotokana na mali ghafi za hapa nchini umewadia,” na hakuna wakati mzuri zaidi kuliko kipindi hiki ambacho serikali imweka kipaumbele zaidi katika hili, aliongeza kusema Profesa Mkenda.

  Mkakati huo wa kitaifa wa kuendeleza ujasiriamali umeandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali likiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa Linalojihusisha na Maendeleo ya Biashara (UNCTAD).
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,Profesa Adolf Mkenda (katikati) akifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na Mwezeshaji, Dkt Donath Olomi hayupo pichani wakati wa mkutano wa wadau uliokuwa ukijadili rasimu ya mapendekezo ya kuwa na mkakati wa kitaifa kuendeleza ujasiriamali hapa nchini, wapili kushoto Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa, kushoto ni Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Linalojihusisha na Maendeleo ya Biashara (UNCTAD),Bw. Lorenzo Tosini, wa pili kuli ni Mkurugenzi Msaidizi Mazingira ya Biashara Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Christopher Mramba na kulia ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa baraza hilo, Bi. Anna Dominick.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,Profesa Adolf Mkenda (katikati) akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa, wakati wa mkutano wa wadau uliokuwa ukijadili rasimu ya mapendekezo ya kuwa na mkakati wa kitaifa kuendeleza ujasiriamali hapa nchini, na kulia ni Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Linalojihusisha na Maendeleo ya Biashara (UNCTAD),Bw. Lorenzo Tosini.


  Wadau kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika makundi wakati wa mkutano uliokuwa ukijadili rasimu ya mapendekezo ya kuwa na mkakati wa kitaifa wa kuendeleza ujasiriamali hapa nchini, aliyesimama ni mwezeshaji wa mkutano huo, Dkt. Donath Olomi.


  0 0  Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwasalimia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara 20 Julai 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya Rais wa Burundi kuwahutubia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara 20 Julai 2017.
  Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017.
  Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwapungia wananchi alipowasili katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017
  Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akikagua graride la lililoandaliwa na jeshi la ulinzi la Tanzania JWTZ katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na ujumbe wake katika mazungumzo maalum ya kiserikali na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza na ujumbe wake Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza pamoja na mama Janeth Magufuli katika Maongezi.

  0 0


  Na Lilian Lundo - MAELEZO.
  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ( TCU) umeutangazia Umma kuwa kuanzia Julai 22 mwaka huu vyuo vyote vya elimu ya juu hapa nchini vitaanza kupokea maombi ya udahili kwa mwaka wa masomo  2017/2018.

  Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Prof. Eleuther Mwageni (pichani) ameyasema hayo leo, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya kuanza rasmi udahili kwa mwaka 2017/2018.
  Prof. Mwageni amesema kuwa waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao  kwenye vyuo husika na siyo tena TCU kama ilivyokuwa kwa mwaka jana na miaka mingine ya nyuma.
  Aidha amesema kuwa waombaji wahakikishe wanaomba programu za masomo ambazo zimeidhinishwa na kutambuliwa na TCU na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).
  "Tunavikumbusha vyuo kutangaza programu ambazo zimeidhinishwa na kutambuliwa na TCU na NACTE, ikiwa chuo kitatangaza programu ambazo  hazitambuliki na Tume, basi chuo husika kitachukuliwa hatua," amesema Prof. Mwageni.
  Ameendelea kwa kusema kuwa, orodha ya programu hizo inapatikana katika tovuti ya TCU ( www.tcu.go.tz) ambapo programu hizo zimegawanywa katika makundi mawili yaani Kidato cha Sita na Diploma.
  Vile vile, Prof. Mwageni amewataka waombaji watakao chaguliwa kwa zaidi ya chuo kimoja, kuthibitisha kwa wakati chuo watakachokwenda ili kutoa nafasi kwa waombaji wengine.
  Waombaji wamehimizwa kusoma kwa makini mwongozo wa udahili kwa mwaka 2017/18 ambao unapatikana kwenye tovuti ya Tume.  
  Aidha Tume inawakaribisha wadau wote kushiriki maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yatakayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam kuanzia Jula 26 hadi 29 mwaka huu ambapo zaidi ya vyuo 80 vinatarajiwa kuwepo katika maonesho hayo.

  0 0

  Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu amekamatwa leo, Alhamisi, Julai 20 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akielekea Kigali, Rwanda kwenye Mkutano wa Marais wa Vyama vya Mawakili Afrika Mashariki.
  Kamanda wa polisi viwanja vya ndege, Martin Ortieno amesema kwamba ni kweli wamemkamata Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema na kwamba amepelekwa makao makuu ya Polisi kwa ma.
  Hata hivyo, kamanda huyo hakutaja sababu za kukamatwa kwa mwanasheria huyo.
  Nae Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amekiri kuwa mwanasheria huyo amekamatwa jioni hii. Mrema amesema Lissu amekamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni maofisa wa polisi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

  0 0

  Na Ali O. Ali 
  Kampuni ya Rafiki Network itafanya Tamasha la Michezo na Utamaduni linalojulikana kama “ Pemba Weekend Bonanza” litakalofanyika kisiwani Pemba kuanzia tarehe 28 hadi 30 Julai mwaka 2017. 
  Taarifa ya kampuni hiyo imesema kwamba tamasha hilo litajumuisha matukio mbali mbali kama vile mchezo wa ng’ombe, resi za baiskeli, mashindano ya kuogelea na resi za ngalawa,  na kwamba miongoni mwa matukio, imeelezwa kwamba mchezo wa ng’ombe ambao utafanyika siku ya Ijumaa tarehe 28 Julai, 2017, majira ya alasiri katika viwanja vya skuli ya Chwale, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba. 
   Aidha, taarifa hiyo imebainisha kwamba resi za baiskeli ambazo zitafanyika kwa mizunguko miwili tafauti zitakuwa siku ya Jumamosi tarehe 29 na Jumapili tarehe 30 Julai katika maeneo na taratibu tofauti.
  Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Siku ya Jumamosi, tarehe 29 Julai, kutakuwa na resi za baiskeli hatua ya mchujo, zitakazofanyika kwa kujumuisha makundi matatu yanayokimbia kwa kupitia barabara tatu tafauti kiswani Pemba. 
  Fainali za resi za baisikeli zitaanzia Uwanja wa Gombani hadi Vumawimbi, Makangale Pemba majira ya saa 1 kamili asubuhi. 
  Taarifa imethibitisha kuwa kutakuwa na mashindano ya kuogelea baharini yatakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 30 Julai 2017 katika fukwe za Vumamwimbi. Shindano hili litawashirikisha waogeleaji mbalimbali nchini ambapo washiriki wapatao 100 watachuana katika mpambano huu. Vile vile taarifa hiyo imesema kwamba kutakuwa na resi za ngalawa zitakazofanyika tarehe 30 Julai, 2017, pia katika fukwe za Vumawimbi Pemba. Shindano litashirikisha ngalawa takribani 20 kutoka maeneno mbali mbali Kiswaini Pemba kama vile Tumbe, Kiuyu, Msuka, Shumba Mjini, Mwambe na Mnarani. Kwa mujibu wa taarifa hiyo Tamasha hili limedhaminiwa na ZURA (Zanzibar Utility Regulatory Authority) na litarushwa hewani na kituo cha Televisheni cha AZAM ambao ni washirika wenza (Partners) wa Kampuni ya Rafiki Network.

  0 0


  0 0


  0 0


  0 0


  0 0

  Shule ya sekondari LONDONI iliyopo katika manispaa ya SONGEA mkoani RUVUMA, ni kati ya shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2017 ambapo kwa mwaka 2017 imeshika nafasi ya kwanza katika manispaa ya SONGEA huku kimkoa imeshika nafasi ya nne.
  HABRI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

  0 0

  Katika Sherehe za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika katika Uwanja wa Parking wilayani Nzega mkoani Tabora; Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Mohammed Bashe amekabidhi hundi ya Shilingi za Kitanzania Milioni Tatu na Laki Tisa (Tzs 3,900,000) kwa ajili ya kuwezesha vikundi mbalimbali vya wajasiriamali vilivyojitokeza kwenye sherehe hizo kuweza kumudu gharama za uendeshaji wa ofisi zao.
  Hundi hiyo ilikabidhiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Bw. Amour Hamad Amour ambaye hakusita kusifia juhudi za Mheshimiwa mbunge kila mahali alipotembelea miradi ya maendeleo na huduma za jamii iliyokuwa anatekelezwa na Mhe. Hussein Bashe jimboni kwake na ndani ya Halmashauri ya Mji wa Nzega.
  Bw. Amour H. Amour anasema.... "Tumetembea maeneo mengi, majimboni na wilayani, tumezunguka tukiukimbiza Mwenge kila mahali; wabunge wamejitokeza kushiriki zoezi hili lakini Mhe. Bashe amekua nasi bega kwa bega na ushirikiano wake umekua ni mkubwa sana. Haitoshi mambo anayoyafanya kwa wananchi wake ni mambo makubwa, ya kuigwa na kuungwa mkono"
  Kwa upande waje Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe. Godfrey Ngupula alisema...."Kiongozi wa mbio za Mwenge, kuna msemo usemao msifie mtu angali yupo hai; nami leo nasema Mhe. Bashe anafanya kazi kubwa sana. Hapa tulipo tayari Mhe. Bashe amewapa ufadhili na amewalipia ada wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kidato cha Tano kwenye shule mbalimbali za serikali nchini, haitoshi bado anapambana kuhakikisha elimu ndani ya Jimbo la Nzega Mjini inakua na ufaulu unaongezeka"
   Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Bw. Amour Hamad Amour akikabidhi  mfano wa hundi ya Shilingi za Kitanzania Milioni Tatu na Laki Tisa (Tzs 3,900,000) kwa ajili ya kuwezesha vikundi mbalimbali vya wajasiriamali.

  0 0

  Mpango mpya unaohamasishwa na wadau wa sekta ya kilimo hatimaye utawapa wakulima wadogo nchini kote fursa ya kupata masoko ya uhakika na endelevu kwa kuepuka madalali wa mazao yao.

  Akizungumza na waandishi wa habari kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Farm Africa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkazi wa Tanzania wa Farm Africa,  Steve Ball alisema kuwa warsha hiyo ililenga kuwafudisha wakulima namna bora kuingia kwenye mfumo rasmi wa biashara ya nafaka.

  Alisema kuwa jukwaa hilo la wadau kwenye sekta hiyo linaunganisha biashara nzima ya nafaka kutoka kwenye shamba hadi sokoni  na inashirikisha mkusanyiko wa programu zinazoruhusu watumiaji kusimamia hesabu, mazao ya biashara, soko endelevu na kupata mikopo kutoa kwenye taasisi za fedha.

  "Tuko hapa kuzungumza juu ya njia bora ya kuwasaidia wakulima wadogo ili kuepuka madalali wakati wa kutafuta masoko ya mazao yao na ili waweze kupata kwa bei bora zaidi baada ya kupata taarifa sahihi na kwa wakati muafaka juu ya mwenendo wa soko,” alisema.

  Aliongeza pia kwamba wadau katika sekta hiyo wana matumaini kwamba wakulima watakusanya nguvu kwa pamoja na kutengeneza maghala yao ya kuhifadhi mazao yao na kuuza kwa pamoja ili kupata bei nzri zaidi.

  Alibainisha kuwa kwa njia ya G-Soko, wakulima wanaweza kuunganisha mavuno yao kupitia ghala lao na kuthibitishwa na kupata huduma za kifedha kwa kutumia nafaka zao kama dhamana. Jukwaa pia hutoa programu ya malipo ya huduma na ukusanyaji wa data wa wakulima.


  Mkurugenzi Mkazi wa Farm Africa, Steve Ball akizungumza kuhusu umuhimu wa wakulima kupata taarifa za uhakika kuhusu mwenendo wa masoko, wakati wa warsha ya wadau wa mazao ya nafaka iliyofanyika  jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (The Foundation for Civil Society- FCS), Bw. Francis Kiwanga akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa katika Kongamano la siku moja la kuwahamasisha vijana kuchangamkia fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kongamano hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza tarehe 19 Julai 2017. 
  Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Mary Onesmo Tesha ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella akisoma hotuba ya ufunguzi kwenye kongmano la kuwhamasisha vijana kufanya biashara za kuvuka mipaka ya nchi za EAC. Mhe. Tesha aliwasihi vijana waondoe hofu na wajiunge katika vikundi ili waweza kufanya biashara kwa urahisi. Aliahidi kutoa milioni moja kwa kikundi kilichoundwa hapohapo kwa uratibu wa Mwkilishi wa Cloud Media, Bw. Samsonight Odera 
  Bi. Tesha akiendelea na hotuba yake. 
  Mchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw, Justin Kisoka akiwaeleza vijana wa Mwanza waliofurika kwenye ukumbi wa Rock City Mall sheria, kanuni na taratibu za kufuata kwa yeyote anayetaka kuanza biashara ya kuvuka mipaka ya nchi za EAC. 
  Mtaalamu wa Msauala ya EAC, Bw. Abel Maganya akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya EAC ikiwemo namna ya kupata cheti cha uasili na hati za kusafiria. 
  Mbinu mbalimbali zilitumika kufikisha ujumbe wa umuhimu wa kufanya biashara katika nchi za EAC. Hapa vijana wa Vipaji Foundation wakionesha kwa kutumia igizo baaadhi ya bidhaa zinazoweza kuuzwa katika nchi za EAC. 


  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Ushiriki watanzania katika  uwekezaji  wa katika  sekta ya madini na kilimo ni mdogo kutokana na mifumo  iliyopo na kufanya nchi kwa wazawa kushindwa kunufaika.

  Akizungumza katika mdahalo  ulioandaliwa na Taasisi  Isiyo ya Kiserikali inayojighulisha na Utafiti  wa Kisera  kwa ajili ya Kukuza Sayansi , Teknolojia  na Ubunifu (Stipro), Kaimu  Mkurugenzi Idara ya Ushiriki Watanzania katika sekta ya Uwekezaji wa  Baraza la  Taifa uwezeshaji wananchi Kiuchumu (TNBC) , Esther  Mmbaga amesema kuwa baraza limeunda kitu cha kuweza kufatilia mikataba na sera  namna ya wazawa  wanavyoshiriki katika uwekezaji.

  Amesema  ushiriki watanzania katika uwekezaji kuanzia ajira na hata bidhaa zinazozalishwa nchini  hazitumiki kwa wawekezaji kutokana na madai kuwa hazina ubora.

  Mmbaga amesema kutokana na ukosekanaji wa ushiriki Baraza litaweka utaratibu kwa kila kinachofanyika  nchini chi ya uwekezaji watanzania waweze kushiriki au kufanya ubia kwa teknolojia kuandaa utaalam wa uzalishaji wa taaluma.

  Amesema kuwa tafiti hizo ndizo zinafanya baraza kufanyia  kazi katika kuangalia wazawa wanavyonufaika na  uwekezaji unaofanywa nchini.

  Nae  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi  Isiyo ya Kiserikali inayojighulisha na Utafiti  wa Kisera  kwa ajili ya Kukuza Sayansi , Teknolojia  na Ubunifu (Stipro) Bitrina Diyamett  amesekuwa utafiti  huo ulijikita  kuangalia uwekezaji  kwa kiasi gani watanzania wanashiriki.

  Amesema watu wanafanya uwekezaji  nchini  lakini hawanunui bidhaa za ndani  na kuonekana  watanzania sio  sehemu ya uwekezaji hali ambayo inahitaji kuangalia sera  pamoja na mikataba.
  Kaimu  Mkurugenzi Idara ya Ushiriki Watanzania katika sekta ya Uwekezaji wa  Baraza la  Taifa uwezeshaji wananchi Kiuchumu (TNBC) , Esther  Mmbaga akizungumza  katika ufunguzi wa mdahalo uliojikita  kuangalia uwekezaji  kwa kiasi gani watanzania  wanashiriki atika masuala ya uwekezaji kwenye mkutano uliofanyika  katika ukumbi wa Costech jana jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi  Isiyo ya Kiserikali inayojighulisha na Utafiti  wa Kisera  kwa ajili ya Kukuza Sayansi , Teknolojia  na Ubunifu (Stipro) Bitrina Diyamett  akizungumza juu utafiti wao waliofanya kupitia taasisi  hiyo katika kuangalia watanzania kunufaika katika masuala ya uwekezaji .
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe , Profesa Honest Ngowi akizungumza juu masuala ya uwekezaji na utafiti uliofanywa na Taasisi ya Stipro jana  jijini  Dar es Salaam.

  Sehemu ya wadau katika wa mdahalo uliojikita  kuangalia uwekezaji  kwa kiasi gani watanzania  wanashiriki uliofanyika  katika ukumbi wa Costech  jana jijini Dar es Salaam.

  0 0
 • 07/20/17--22:30: Kumbukumbu

 • Marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo
  Kuzaliwa 11/03/1973 - Kufariki 21/07/2016


  Zimepita saa, siku, miezi na hatimaye leo mwaka mmoja umetimia tangu ututoke ghafla kunako Alhamisi, tarehe 21 Julai  2016.
  Tunakukumbuka kwa upendo, ucheshi, ukarimu na moyo wako wa kusaidia wahitaji. Tumejifunza mengi kutokana na maisha yako na tutaendelea kukuenzi kwa yale mema na mazuri uliyotenda hapa duniani.
  Unakumbukwa sana na mama yako mzazi Amina Mtaturu, mke wako mpenzi Naiz Mavura, watoto wako wapendwa Nassa na mdogo wake Nolan-Idrissa; kaka na dada zako, wakwe zako, shemeji zako pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zako lukuki.
  Tunamshukuru Mungu ambaye anaendelea kutupa nguvu ya kuishi pasi na uwepo wako--ni mmoja wa neema na miujiza yake Allah. Tunaendelea kukuombea dua ili Mungu aendelee kukupumzisha kwa amani huku ukitusubiri katika Ufalme wake wa milele.

  Inna Lillah wa Inna Illayh Raj'un
  "Sisi ni wa Mwenyezi mungu na kwake Tutarejea"

  0 0

  Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kulea wazee cha Kolandoto Bi Sophia Kang’ombe jinsi ya kuwasha Jiko la Gesi lililopo katika kituo hicho ikiwa ni moja ya mradi wa majiko ya Gesi katika Makazi ya kulea wazee nchini wa pili kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt Rashid Mfaume.
  Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(Kushoto) akiangalia moja ya jiko linalotumia Nishati ya Gesi linalowaka wakati alipotembele kukagua maendeleo ya mradi huo hivi karibuni.
  Muonekano wa Majiko yanayotumia Nishati ya Gesi yatakayotumiwa kuhudumia katika makazi ya kulea wazee ya Kolandoto na makazi mengine ya kulea wazee nchini.


  0 0  Elias Banyenza nduo jina alilopewa na wazazi wake, lakini unafahamika na wengi kwa jina la Banye. Anapenda kuimba na RnB ndio muziki ana unaoupenda zaidi. Banye alianza kuimba akiwa Sunday Schools na Talent Shows lakini alivutiwa zaidi na Mwanamziki Tyrese tangu alipomuona mara ya kwanza kwenye Tangazo la Coca-Cola la mwaka 1986 na kujaribu kumfuatisha jinsi alivyoimba kila mara lile Tangazo lilipopita. 
  Watu wengi wakimuona kwa mara ya kwanza huwa wanahisi kama waliwahi kumuona sehemu nahisi hii ni kwasababu waliwahi kuomuona kwenye sehemu zifuatazo:- Mwaka 2014/2015 alikuwa miongoni mwa wawashiriki 6 (Damian Soul,Grace Matata,Eli Daddy, Rogers Lucas, Myra) waliowakilisha Tanzania kwenye shindano la kuimba la Maisha Superstar nchini Kenya, kipindi hicho cha Tv kilirushwa na Maisha Magic ambapo walienda kushindana na washiriki wengine 12 kutoka nchi tofauti tofauti za Africa Mashariki, walisimamiwa na Shaa, AY(Tanzania), Jose Chameleon, Maurice Kirya (Uganda),Nameless, King Kaka(Kenya) na Music Director alikuwa Eric Wanaina. 
  Mwaka 2015/2016, alikuwa kati ya washiriki 5 (Nandy, Jeff, Kechu na Zouccu) waliochagulia kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano makubwa zaidi ya Karaoke kuwahi kutokea Africa, Tecno Own The Stage Lagos nchini Nigeria, kipindi hicho kilirushwa na Africa Magic Showcase ambapo pia alishindana na waimbaji wengine 14 kutoka sehemu mbalimbali za bara la Afrika. Kwenye shindano hili walikuwa chini ya usimamizi wa Yemi Alade, MI, ID Cabasa (Nigeria), Bien Soul/Saut Sol, Anto Neosoul(Kenya) and AY (Tanzania) 
  Ndoto yake kubwa alitamani atoke kimuziki kupitia Mashindano ya kuimba, lakini hakuweza kufanya vizuri huko kwa sababu alikuwa anafanya multitasking…ikiwemo Shule,Kazi na Muziki kwa wakati mmoja hivyo kumpelekea kufanya maandalizi ya zima moto.
  Ukiachana na Muziki Banye amesoma Masters of Business Administration in Marketing na Bachelor in Mass Communication na kaspecilize kwenye Public Relations and Marketing. Na sasa kaamua kuingia studio na wimbo wake wa kwanza ni huo Brown Colour.

older | 1 | .... | 1817 | 1818 | (Page 1819) | 1820 | 1821 | .... | 3286 | newer