Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI AMUUNGA MKONO MLEMAVU ARON MICHAEL

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo  Mlemavu aitwaye Aron Michael Kipalilo ambaye ni mkazi wa kibondo mwenye ujuzi/fundi wa kushona nguo. Amekutana na Rais Magufuli na ameomba amshonee Kaunda Suti.Rais Dkt Magufuli yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya siku tatu ya kikazi
Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo na  mmoja wa Walemavu aitwaye Aron Michael Kipalilo ambaye ni mkazi wa kibondo mwenye ujuzi/fundi wa kushona nguo. Mlemavu huyo amekutana na Rais Dkt Magufuli amshonee Kaunda Suti.

Ujumbe Ubalozi wa Israel Watembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili Leo

$
0
0
 Ujumbe kutoka Ubalozi wa Israel nchini Kenya umetembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo. Maestro Nir Brand akipiga kinanda ili kuwaburudisha watoto wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni Ofisa Uhusiano kutoka ubalozi huo, Angela Mogusu.  
 Watoto wanaotibiwa katika hospitali hiyo wakisikiliza moja wa wimbo uliokuwa ikiimbwa na Brand leo kwenye Jengo la watoto.
 Watoto wakicheza na Daktari Bingwa wa Watoto, Rehema Laiti leo.
  Ilala Brand akipiga makofi ikiwa ni sehemu ya kuungana wagonjwa leo.



 Dk. Shlomi Cohen akishiriki katika shughuli ya kuimba na kucheza na watoto hao leo.

DKT. MPANGO ATANGAZA MAPATO KODI YA MAJENGO SHILINGI BILIONI 32.5.

$
0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Sh bilioni 32.5 ya kodi ya majengo, kwa mwaka wa fedha 2016/17 kutoka katika Majiji, Miji na Manispaa 30 nchini.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) amewaambia waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kwamba makusanyo hayo ni sawa na asilimia 56 ya lengo lililowekwa Mwaka wa Fedha uliopita la kukusanya shilingi bilioni 58.

Alisema kuwa hatua niyo ni mafanikio makubwa tangu TRA ipewe jukumu la kukusanya kodi hiyo ambapo mwaka wa fedha 2015/2016 katika maeneo hayo, Halmashauri zilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 28.3 wakati TRA imekusanya kiasi hicho cha shilingi bilioni 32.5 tangu ianze kukusanya kodi hiyo mwezi Oktoba mwaka wa fedha 2016/2017.

“Mpaka kufikia tarehe 15 Julai mwaka huu TRA imekusanya sh. bil 32.5 kipindi ambacho ni kifupi, na kwamba mapato hayo yanatarajiwa kuongezeka kutokana na mwitio mkubwa wa wananchi kulipa kodi ya majengo”Alisema Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango aliwapongeza wananchi kwa mwitio wao mkubwa wa kulipa kodi ya majengo na kwamba wameonesha uzalendo wa kweli na ndio maana Serikali imeamua kuongeza muda wa kulipa kodi hiyo bila adhabu hadi Julai 30 mwaka huu, hali anayoamini itapandisha zaidi mapato hayo.

Katika hatua nyingine Dkt, Philip Mpango aliwapongeza wamiliki wa vituo vya mafuta waliotii maagizo ya Serikali, kwa kufunga mashine stahiki za EFDs, akitolea mfano vituo vya PUMA na TOTAL ambavyo vimefunga mashine hizo kwenye pampu zao zote.

Aliwaonya wamiliki wote wa vituo vya mafuta ambao hawatafunga mashine hizo za EFDs ndani ya siku 14 kama agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli linavyoelekeza na kwamba yeye kama Waziri mwenye dhamana atahakikisha analisimamia kikamilifu na kwamba baada ya muda huo mtu asijekuilaumu Serikali baada ya kuanza kuchukua hatua kali za kisheria.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akivipongeza Vituo vya Mafuta vya Puma na Total kwa kuonesha mfano wa kufunga mashine za EFDs katika Pampu zote za mafuta kwenye vituo vyao, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.(Picha: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwaomba wananchi kulipa kodi ya Majengo mapema kwa mwaka wa Fedha 2017/18 ili kuepuka usumbufu wa msongamano, alipofanya Mkutano na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akitoa agizo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha kuwa mashine za kutolea risiti za kielektroniki (EFDs) zinatumika ipasavyo na kutengenezwa mara moja zinapoharibika na kwamba zisipotengenezwa ndani ya saa 48 zifungwe na wamiliki wake watozwe faini, alipozungumza na wanahabari, Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wakiwa katika Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) ambapo Waziri huyo aliwashukuru wananchi kwa kulipa kodi ya Majengo kiasi cha Sh. Bilioni 32.5 kufikia Julai 15, 2017, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam.

RAIS MAGUFULI AZINDUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO NA KUHUTUBIA WANANCHI KWENYE MIKUTANO MBALIMBALI YA HADHARA

$
0
0
 Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  pamoja na viongozi mbalimbali wakifungua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi la ufunguzi wa Barabara  ya Kibondo -Nyakanazi kiwango cha lami.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  pamoja na viongozi mbalimbali serikali wakikata Utepe  kuashiria kuweka jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Ujenzi wa  Barabara  ya Kibondo -Nyakanazi 
Baaadhi ya Viongozi wa vyama vya siasa na wananchi wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma wakisikiliza Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Uzinduzi wa  Ujenzi  wa Barabara  ya Kibondo -Nyakanazi.
 Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na kijana mwenye ulemavu amabye ni fundi wa kushona nguo ndugu Aron Michael Kapililo mkazi wa Kibondo ambaye alisimiana na Rais Magufuli 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwapungia mikono mamia ya wakazi wa Kasulu, Mkoani Kigoma.
Mamia ya wakazi wa Kasulu Mkoani Kigoma waliojitokeza kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 63 Kidawe - Kasulu.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge Kigoma Mjini Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe mara baada ya kuzindua  ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 63 Kidawe - Kasulu
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliokuwa wamefurika njiani mara baada ya  Uzinduzi wa  ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 63 Kidawe - Kasulu Mkoani Kigoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 21.07.2017

MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO JULAI 22,2017

Marianus: Mchezo wa Biko utakuza uchumi wa Watanzania wengi

$
0
0
MJASIRIAMALI mdogo mkazi wa Chanika, jijini Dar es Salaam, Enos Marianus, amesema bahati nasibu ya Biko inayaoendelea kuchanja mbuga nchini Tanzania, utakuza uchumi wa washiriki na Watanzania kwa ujumla, akiwamo yeye ambapo ana mpango wa kuendeleza biashara zake..

Hayo yamesemwa na mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko, Marianus wakaati anakabidhiwa fedha zake katika makabidhiano yaaliyofanyika jana katika benki ya NMB, Posta, jijini Dar es Salaam.

Marianus alisema ukosefu wa ajira unasababisha watu wengi watamani kuingia kwenye ujasiriamali, hivyo uwapo wa mchezo wa Biko utapunguza changamoto hiyo, hivyo ni jambo la msingi la kuhakikisha kuwa kila mtu anacheza Biko ili ashinde mamilioni ya Biko.

“Nashukuru leo kwa kukabidhiwa fedha zangu Sh Milioni 20 kutoka kwa watu wa Biko, hivyo ninaamini kabisa mchezo huu utakuza uchumi wetu hususan sisi wajasiriamali wadogo ambao fedha hizi zitaingia kwenye kupanua wigo wa biashara zetu kwa namna moja ama nyingine,” Alisema.

Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema ushindi wa Biko ni rahisi husuan kwa wale wanaocheza mara nyingi kwa kufanyaa miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel kuanzia Sh 1,000 na kuendelea ambapo namba yao ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.

“Sh 1,000 ya Biko inayochezwa inampa mtu ushindi wa papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni Moja inayolipwa papo hapo kwenye simu iliyotumika kuchezea Biko pamoja na zawadi nono ya Sh Milioni 20 inayotoka Jumatano na Jumapili,” Alisema Melles.

Zaidi ya Sh Bilioni moja tayari zimelipwa kwa washindi wa Biko kwa kipindi cha mwezi Mei na Juni pekee, ikiwa ni mwendelezo wa kutoa mamilioni ya fedha kwa washindi wake wanaocheza Biko tangu kuanzishwa kwa mchezo huo hapa nchini.
 Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heave wa pili kutoka kulia akimkabidhi fedha zake mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko, Enos Marianus mwenye shati jeupe, jana jijini Dar es Salaam, katika benki ya NMB. Wa kwanza kulia ni Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko Tanzania, Hassan Melles.
 Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko Tanzania, Hassan Melles wa pili kutoka kulia akimkabidhi fedha zake mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko, Enos Marianus mwenye shati jeupe, jana jijini Dar es Salaam, katika benki ya NMB. Wa kwanza kulia ni Goodhope Heaven, Meneja Masoko wa Biko Tanzania.
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko droo ya 24, Enos Marianus kulia aakiwa na furaha tele baada ya kukabidhiwa fedha zake jana katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam, siku moja baada yaa kutangazwa mshindi wa bahati nasibu ya Biko. Kushoto kwake ni mkewe Bi Kisa Kasito aliyemsindikiza katika kukabidhiwa fedha zake.

KWA SIMU TOKA LONDON- Mitaani na muziki wa Kizungu

$
0
0
IJUE PIANO – NA MANUFAA YAKE

Na Freddy Macha 
Piano (au kinanda)  ni chombo mahsusi cha  Wazungu. Kitaaluma muziki maana yake ni vitu vitatu : melodi (unayoisikia bila hata kujua maneno na kuipigia uluzi), ridhimu (mapigo), na mpangilio wa sauti (“harmony”). Kipengele cha tatu ndiyo kigumu zaidi....
Kati ya vyombo muhimu  vya kitengo cha utunzi na upangaji (“harmony”) wa muziki ni Piano na Gitaa.

Ila Piano inaongoza Uzunguni.

 Ndiyo maana kila utakapokwenda,  makanisani, mabaa, mashuleni, majumbani na hata vituo vya usafiri hukosi Piano. Kihistoria, watunzi mashuhuri wa muziki ulimwenguni wametumia Piano kupanga vibao vyao vilivyofahamika na kupendwa miaka mingi  zaidi.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA

WAJASIRIAMALI WAKIWA KAZINI

$
0
0

 .Kamera imenasa wakazi wa jiji Dar es Salaam wajasiliamali maarufu kama machinga wakiandaa biashara zao leo katika soko la Karume Ilala.
Machinga akisafisha viatu ili kwa kuingiza sokoni katika soko la Karume Ilala jijini Dar es Salaam.
Watembea kwa miguu wakikwepa shimo lililopo katika barabara ya Kilwa jijini Dar s Salaam.

Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

KOMBE LA MATAIFA AFRIKA SASA KUFANYIKA JUNI NA JULAI 2019 NCHINI CAMEROON

$
0
0

Shirikisho la soka barani Afrika  (CAF) limethibitisha.kuwa Kombe la mataifa bingwa Afrika 2019 litafanyika mwezi Juni na Julai 2019.

Mchuano huo huwa unafanyika mnamo mwezi Januari na Februari na kusababisha migogro na vilabu vya Ulaya ambavyo hulazimika kuwatoa wachezaji katikati ya msimu.
Kinyang'anyiro hicho cha 2019 kitakachoandaliwa Cameroon kitashirikisha timu 24 badala ya 16. Mabadiliko hayo yalitiwa sahihi na kamati kuu ya CAF katika mkutano uliofanyika mji mkuu wa Rabat.
Michuano hiyo imekuwa ikishirikisha timu 16 tangu 1996. Upanuzi wa mechi hizo unaweza kusababisha matatizo kwa Cameroon ambayo itaanda fainali ijayo, huku waziri wa michezo wa taifa hilo la Afrika ya kati akilazimika kukataa ripoti kwamba maandalizi yalikuwa nyuma.
Mashindano hayo yataendelea kila baada ya miaka miwili barani Afrika. Caf ilikuwa inapanga iwapo itaruhusu mataifa kutoka mabara mengine kushiriki ama hata kuandaa mchuano huo.
Tangazo hilo linajiri kufuatia mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na rais wa Caf Ahmad kuzungumzia hali ya soka barani Afrika.

NDOTO ZA ZANZIBAR KUSHIRIKI MICHUANO YA CAF ZAFUTIKA, YAVULIWA UANACHAMA

$
0
0


Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limefanya maamuzi ya kuwavua uanachama chama cha soka cha Zanzibar ikiwa ni miezi minne toka  kipewe uanachama na CAF kutoka kwa Rais aliyepita Issa Hayatou.

Rais wa CAF Ahmad Ahmad (pichani)  amesema Zanzibar walipewa uanachama kimakosa na kama sheria zingepitiwa vizuri wasingepewa uanachama. 
“Walipewa uanachama bila kupitia vizuri kanuni ambazo ziko wazi na zinaeleza kila kitu, kama kanuni na sheria zingepitiwa kiufasaha wasingepewa uanachama”, alisema.

Sababu kubwa ambayo CAF wameivua uanachama Zanzibar ni kutokana na kisiwa hicho kuwa ndani ya Tanzania ambao nao ni wanachama wa CAF.

“Jina la nchi linatokana na jina linaloandikwa katika umoja wa mataifa UN na Zanzibar katika umoja huo inafahamika ipo ndani ya nchi iitwayo Tanzania ambao ni wanachama wa CAF” alisema Ahmad.

Hilo ni pigo kubwa kwa Wazanzibari kwani wakati huu walikuwa wakipambana kupata uanachama wa FIFA ambao wameukosa na wa CAF nao pia wamekosa.
Kwa maana hiyo ndoto ya kisiwa cha Zanzibar kushiriki michuano ya CAF kama mwanachama zimekufa rasmi na sasa watakuwa wakishiriki michuano hiyo kama Tanzania (Zanzibar na Tanzania bara).

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA TUNDUMA

$
0
0
PMO_4468
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza ujumbe kutoka kwa Chifu Jubeki Chimpansya wa  Momba baada ya kusimikwa na wazee wa mila kuwa Chifu Simpanji katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye Uwanja wa Shule ya Misngi ya Mwaka katika mji mdogo wa Tunduma mkoani Songwe Julai 21, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_4522
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipokagua eneo la ujenzi wa jengo la pamoja la forodha kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia  katika mji mdogo wa Tunduma. Alikuwa  katika ziara ya mkoa wa Songwe Julai 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_4586
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  (kushoto kwake) wakitazama gari lililotengenezwa na  Adam Zachariah Kinyekie wakati alipowasili kwenye uwanja 
PMO_4669
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Shule ya Misingi ya Mwaka katika mji mdogo wa  Tunduma.  Alikuwa  katika ziara ya mkoa wa Songwe Julai 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_4707
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  Dickson Mwandambila ambaye ni mlemavu baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye  Uwanja wa Shule ya Msingi ya Mwaka katika mji mdogo wa Tunduma.  Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Songwe Julai 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PMO_4358
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  wa Ujenzi wa banio na mfereji wa maji wakati alipotembelea mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa Makamba wilayani Momba Julai 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUMBUKUMBU

$
0
0
Ni miaka miwili sasa imepita tangu ututoke mpendwa wetu Abel Charles Yanga. 
Familia, ndugu, jamaa na marafiki bado tunakukumbuka sana kwa kuwa ulitugusa katika maisha yetu kwa namna ya kipekee sana.
Hakika pengo lako halitazibika kamwe. Sisi tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi.
Tunazidi kukuombea upumzike kwa amani

BARABARA YA SARANGA-KING'ONG'O KUKARABATIWA KWA DHARULA

$
0
0

Dereva wa pikipiki akikwepa shimo katika barabra ya Saranga, King'ong'o jijini Dar es Salaam.

Halmashauri ya manispaa ya Ubungo, kupitia ziara ya kamati ya fedha iliyokuwa ikiongozwa na Mstahiki Meya, Boniface Jacob walifika kujionea hali ya uharibifu wa barabara hasa maeneo ya Kwandevu kuelekea King'ong'o kata ya Saranga.
Nakuhaidi kuishughulikia kwa dharula maeneo mawili 




yaliyoonekana kuharibika sana na kisababisha uharibifu wa magari, foleni na kuhatarisha Maisha ya watembea kwa miguu.

Matengenezo ya dharula yataanza hivi karibuni chini ya Mhandisi wa Halamshauri ya Ubungo huku Manispaa ikiendelea kufuatilia kuingiziwa fedha za barabara hiyo kutoka Manispaa ya kinondoni kwenye akaunti ya pamoja iliyofungwa na Bodi ya barabar ambapo zilitengewa kiasi cha shillingi Millioni 400 kuweka zege maeneo yote ya miteremko na vilima vya Matosa mpaka kimara kupitia King'ong'o.



Mstahiki Meya wa Ubungo Boniface Jacob akiwa ameongozana na kamati ya fedha wakikangua barabara ya Saranga, King'ong'o ambazo zipo kwenye Matengenezo ya dharura, jijini Dar es Salaam.

IMETOLEWA Na OFISI YA MSTAHIKI MEYA HALMASHAURI YA MANISPAA UBUNGO.

WAZIRI LUKUVI AONYA MAAFISA ARDHI WASIO WAADILIFU

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amewaonya maafisa ardhi na maafisa mipango miji wasio waadilifu na kusababisha kero za migogoro ya ardhi nchini. 

Waziri Lukuvi aliyasema hayo leo katika ukumbi wa shule ya sekondari Lugalo mjini Iringa wakati wa Uzinduzi wa Master Plan ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Amesema mchezo huo wa ufisadi ambao umekuwa ukitumiwa miaka yote na maofisa ardhi nchini ameubaini na kuwataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutokubaliana na ramani za maeneo mapya zinazoletwa na wataalam hao bila ya wao kufika maeneo husika na kuoneshwa maeneo hayo ili kujiridhisha.

Waziri Lukuvi amefichua kuwa ufisadi unaofanywa na maafisa ardhi nchini kwa kupima viwanja hewa kwa ajili ya maslahi yao na kusema kuwa mbinu ambayo wamekuwa wakiitumia kuiibia serikali amekwisha ibaini na hata kubali kuona mbinu hiyo inapewa nafasi katika serikali hii ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli .

Maafisa ardhi wakishirikiana na maafisa mipango miji pamoja na wapima wamekuwa wakitajirika sana kwenye idara zao na wanatakata kwa ujanjaujanja na ufisadi wanaoufanya kwa kutengeneza ramani zinazoonesha maeneo mazuri na muhimu katika miji kwamba hayafai kutumika, kumbe wameyauza maeneo hayo kwa mlango wa nyuma na kwa bei za juu.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwaonya maafisa ardhi na maafisa mipango miji wasio waadilifu na kusababisha kero za migogoro ya ardhi nchini wakati wa uzinduzi Master Plan ya mji wa Iringa. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkabidhi kitabu cha Master Plan ya mji wa Iringa Meya wa Halmashauri ya Iringa Alex Kimbe. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiteta jambo na Meya wa Halmashauri ya Iringa Alex Kimbe na Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akipongezwa na Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa mara baada ya Uzinduzi wa Master Plan ya mji wa Iringa. 


Bachelor Admission Applications for the Year 2017-2018

BALOZI WA ISRAEL NCHINI MHE. YAHEL VILAN AWAAGA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE WA KUFANYA KAZI HAPA NCHINI

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimshukuru Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan (kulia) kutokana na nchi yake kuisaidia Taasisi hiyo kuwapatia mafunzo madaktari, wauguzi na kutoa matibabu kwa watoto. Katikati ni Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo Sulende Kubhoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan wakati alipotembelea Taasisi hiyo jana kuwaaga wafanyakazi baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini. Israel imekuwa ikiisadia JKCI kwa kutoa mafunzo kwa madaktari, wauguzi na matibabu kwa watoto.
Mwanamuziki kutoka nchini Israel Maestro Nir Brand akiwaimbia wimbo watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati balozi wa nchi hiyo Mhe. Yahel Vilan alipotembelea Taasisi hiyo kuwaaga wafanyakazi baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini. 
Baadhi ya watoto wanaotiba katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Balozi wa Israel nchini ambaye makazi yake yapo Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan alipokuwa akiwaaga wakati wa ziara yake aliyoifanya jana katika Taasisi hiyo. Serikali ya Israel kupitia Taasisi ya Save Child Heart (SACH) imegharamia matibabu ya watoto 40 tangu Novemba 2015 hadi sasa ambao walitibiwa nchini humo. 

WAZIRI MKUU ATOA MIEZI MITATU WALIOJENGA NDANI YA MPAKA WA TANZANIA NA ZAMBIA KUBOMOA NYUMBA ZAO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa miezi mitatu kwa wananchi wote waliojenga ndani ya eneo la mpaka wa Tanzania na Zambia kubomoa nyumba zao .

Pia ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuanza kuweka alama za X katika nyumba 252 zilizojengwa ndani ya mpaka huo ili wahusika wazibomoe.

Agizo hilo amelitoa leo jioni (Ijumaa, Julai 21, 2017) alipotembelea eneo la ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha (OSBP) katika mpaka wa Tanzania na Zambia, ambacho kinajengwa na Serikali ya Tanzania na kitagharimu sh. bilioni 12.

“Kuna watu wamejenga ndani ya mpaka wa Tanzania na Zambia na kuendesha biashara zao jambo ambalo ni kinyume cha sheria na linazikosesha Serikali mapato.”Kufuatia hatua hiyo Waziri Mkuu ametoa muda wa miezi mitatu kwa watu wote waliojenga kuanzia umbali wa mita 50 kutoka Tanzania na mita 50 kutoka Zambia kuzibomoa nyumba hizo kwa hiari.

“Hatuna msamaha kwa watu waliojenga katika eneo hili kwa sababu wamesababisha tupoteze kodi nyingi, hivyo baada ya kumalizika muda huo mamlaka husika zibomoe nyumba zote zitakazosalia.”

Awali Waziri Mkuu alikutana na Mkuu wa wilaya ya Nakonde nchini Zambia, Bw. Field Simwinga ambaye alisema wamekubaliana na utekelezaji wa agizo hilo kwa kuwa jambo hilo linaathiri shughuli za mipakani kwa pande zote mbili.

Bw. Simwinga alisema tayari wameshaanza kuwaeleza wananchi wao waliojenga ndani ya mpaka huo kuanza kuondoka, ambapo Waziri Mkuu amesema wanataka eneo hilo liwe wazi ili iwe rahisi kuutazama mpaka huo kwa umakini.

Mkuu huyo wa wilaya ya Nakonde alisema utekelezaji wa jambo utafanikiwa kwa urahisi kutokana na ushirikiano wa Serikali za Tanzania na Zambia.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JULAI 21, 2017



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipokagua eneo la ujenzi wa jengo la pamoja la forodha kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia katika mji mdogo wa Tunduma. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Songwe Julai 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Dk. Kigwangalla afanya ziara mikoa ya Rukwa, Katavi na Tabora

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla ameendelea na ziara yake ya kikazi ya kukagua huduma za Afya ‘Imarisha Afya’ katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali mbalimbali kwenye mikoa ya Rukwa, Katavi pamoja na Tabora. 

Akiwa katika mkoa wa Rukwa, Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea Hospitali ya Sumbawanga ambayp ni ya Mkoa wa Rukwa na kujionea mambo mbalimbali huku akiwapongeza kwa namna walivyoboresha huduma zao ikiwemo ile ya Maabara, Chumba cha upasuaji na huduma zingine ambapo aliwaagiza kuhakikisha wanakuwa na hakiba ya kutosha ya damu salama kwa ajili ya dharura kwa wagonjwa wa ukanda huo. 

 Mbali na Hospitali ya Mkoa wa Rukwa, pia aliweza kutembelea kituo ca Laela ambapo pia mbali ya kujionea utendaji kazi wa kituo hicho alipongeza juhudi za Mbunge wa jimbo la Kwera, Mh. Ignas Alloyce Malocha kwa kushirikiana na wananchi wake katika masuala ya huduma za Afya. 

Ziara hiyo katika mkoa wa Rukwa, aliweza kumalizia katika Kituo cha Afya Wampembe kilichopo Wilayani Nkasi ambapo alijionea shughuli mbalimbali ikiwemo huduma za Upasuaji hata hivyo aliutaka uongozi wa kituo hicho ambacho kipo mwambao wa Ziwa Tanganyika kuhakikisha wanakamilisha mifum ya maji safi na salama ndani ya kituo pamoja na kuboresha huduma za Maabara na usafi kwa ajumla. 
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua Maabara ya Mkoa wa Rukwa
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akikaguachumba cha upasuaji Hospitali ya Mkoa wa Rukwa
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akielekea kukagua Maabara ya Kituo cha Afya Laela Mkoa wa Rukwa
Jengo linaloendelea kujengwa kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Uyui.

Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo leo asherehekea miaka 25 kama kiongozi wa Kiroho jimbo Kuu la Dar es salaam

$
0
0
Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi leo muda mfupi kabla ya kuanza kwa sherehe kutimiza miaka 25 kama kiongozi wa Kiroho katika kanisa la Katoliki jimbo Kuu la Dar es salaam katika kanisa la St. Joseph.
Muadhama Polycarp Kardinali Pengo ni kardinali wa pili kutoka Tanzania, akiwa kateuliwa mara baada ya kifo cha Muadhama Laurean Rugambwa, aliyekuwa kardinali wa kwanza kutoka kusini kwa Sahara. 
Alizaliwa kijiji cha Mwazye, mkoani wa Rukwa, tarehe 5 Agosti 1944. Baada ya masomo ya ngazi mbalimbali, alipewa upadrisho mwaka 1971 na askofu Charles Msakila wa Jimbo Katoliki la Sumbawanga, akasoma teolojia ya maadili huko Roma, Italia, akijitwalia digrii ya udaktari mwaka 1977. Kisha kufundisha somo hilo kwa muda mfupi kwenye seminari kuu ya Kipalapala (mkoa wa Tabora), baadaye 
alichaguliwa kuwa gombera wa seminari kuu ya Segerea hadi mwaka 1983. 
Aliteuliwa askofu wa Nachingwea tarehe 11 Novemba 1983, akapewa daraja takatifu hiyo na Papa Yohane Paulo II tarehe 6 Januari 1984. 
Tarehe 17 Oktoba 1986 alihamishiwa jimbo jipya la Tunduru-Masasi. Tarehe 22 Januari 1990 alifanywa askofu mwandamizi wa Dar-es-Salaam na mwaka 1992, ambapo Kardinali Laurean Rugambwa alipojiuzulu, akawa askofu mkuu.
Muadhama Polycarp Kardinali Pengo  aliteuliwa na Papa Yohane Paulo II kuwa kardinali tarehe 21 Februari 1998, akikabidhiwa parokia ya Nostra Signora de La Salette mjini Roma. 
Pamoja na majukumu mbalimbali katika idara za Papa, tangu mwaka 2007 hadi 2013 alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki ya Afrika na Madagaska.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images